Sunday, January 20, 2013

KATIKA ULINGO WA NDONDIIIII SHAURI, NJECHELE KUWANIA UBINGWA WA MABARA KESHO



Bondia wa ngumi za kulipwa na bingwa wa IBF  INTERCONTINETAL Ramadhani shauri anategemea kupanda ulingoni kesho kuzipiga na Said njechele wa iringa katika pambano la kirafiki la raundi nane katika ukumbi wa  D.I.D Hall uliopo mabibo mwasho.

Mratibu  wa pambano hilo Charles Christopher mzazi  ameeleza kuwa maaandalizi ya pambano yapo kamili na mabondia wote wapo katika hali nzuri ya ushindani  na wamepima wapo sawa kabisa kwa kuzipiga. Ambapo pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi na mabondia watakaosindikiza  pia wamepima chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim kamwe na docta john wapo sawa kwa kupambana.

Mabondia watakaocheza utangulizi ni kama ifuatavyo HAMIS MOHAMED na  HARUNA MNYALUKOLO, PENDEZA SHOMARI atazipiga na MARTIN RICHARD, MBARUKU NASORO na KARIMU RESPECT, DOTO MUSTAFA atakabiliana na SHOMARI MIURUNDI, huku ISSA OMAR akizipiga na  JUMA J KASHNDE.

Katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe  ama bigright amethibisha kuwa kanuni na taratibu za ngumi za kulipwa zimefuatwa  na mabondia wapo katika hali nzuri ya kupigana hiyo siku ya jumapili katika ukumbi wa DID HALL mabibo mwisho kati ya bingwa wa IBF INTERCONTINENTAL RAMADHANI SHAURI  na  SAID  NJECHELE

MSHAMBULIAJI WA ZAMANI W ATIMU YA TAIFA ALIYEING'ARISHA STARS DHIDI YA SENEGAL MWAIKIMBA AITAKATISHA AZAM NAIROBI, YAIPIGA SOFAPAKA KWAO


Shujaa wa Azam leo, Mwaikimba

BAO pekee la Gaudence Exavery Mwaikimba kwa penalti dakika ya 58, jioni hii limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Sofapaka ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Huo ni ushindi wa kwanza wa Azam katika ziara yake ya wiki moja nchini Kenya, baada ya jana kufungwa 2-1 na AFC Leopard kwenye Uwanja huo huo wa Nyayo.
Penalti hiyo, ilitolewa baada ya beki mmoja wa Sofapaka, kuunawa mpira uliopigwa na kiungo Mkenya, Humphrey Mieno.
Akiuzungumzia ushindi huo, Kocha wa Azam Muingereza Stewart Hall alisema hii inamaanisha timu yake sasa imeimarika kiasi cha kutosha na ndiyo maana inashinda mechi hata nje ya nchi.
Pamoja na kufungwa jana na Leopard, Azam watajilaumu wenyewe, kwani walipoteza penalti mbili kupitia kwa Joackins Atudo na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Mabao ya Leopard katika mchezo wa jana, yalifungwa na Paul Were na Mike Barasa, wakati la Azam lilifungwa na Sammih Hajji Nuhu kwa penalti.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Salum, Himid Mao/Malika Ndeule, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika/Luckson Kakolaki, Joackins Atudo, Kipre Balou/Abdulhalim Humud, Seif Abdallah, Salum Abubakar, Brian Umony/Jabir Aziz, Humphrey Mieno/Gaudence Mwaikimba na Khamis Mcha/Uhuru Suleiman.
Azam itashuka dimbani Jumanne, kucheza mechi ya mwisho na timu ya Benki ya Biashara ya Kenya, KCB kwenye Uwanja wa City na Jumatano watapanda basi lao kuvuka boda la Namanga kurejea nyumbani Dar es Salaam.

DJIBRIL CISSE ASAINI AL GHARAFA


Football | International

Djibril Cisse © Action Images

Cisse joins Al Gharafa


Much-travelled former France international striker Djibril Cisse joined Qatari outfit Al Gharafa on loan on Sunday from English Premier League strugglers QPR.
The 31-year-old, capped 41 times, has joined the ambitious Qatari side until the end of the season and is their second signing inside a week after they snapped up Brazilian striker Nene from Paris Saint Germain.
Cisse, who has has also played for Liverpool, Lazio and Panathinaikos, among others, has featured in 21 games for QPR this season, scoring four goals.
However, he has dropped down the pecking order at QPR now they have signed his fellow French international Loic Remy from Marseille

CHELSEA WAKATA NGEMBE YA KUTOSHINDA NYUMBANI KWA MECHI SITA BAADA YA KUITANDIKA ARSENAL 2-1 STAMFORD BRIDGE WAJIBANZA NAFASI YA 3 NYUMA YA POINTI 6 DHIDI YA MAN CITY


Chelsea celebrate a goal against Arsenal
>>CHELSEA 2 ARSENAL 1
Chelsea walipata Bao 2 za haraka na kuizuia Arsenal wasirudishe katika Mechi ya BPL, Barclays Premier League, iliyochezwa leo Stamford Bridge na kuwapa ushindi wao wa kwanza wa nyumbani katika Mechi 4 za 2013 na kuwafanya wajizatiti nafasi ya 3 wakiwa Pointi 6 nyuma ya Man City na Pointi 10 nyuma ya Vinara Man United.

MAGOLI:
Chelsea 2
-Mata Dakika ya 6
-Lampard 16 (Penati)
Arsenal 1
-Walcott Dakika ya 58

Juan Mata ndie alieipa Chelsea Bao la Kwanza na Kipa Wojciech Szczesny kumwangusha Ramires na Refa Martin Atkinson kutoa Penati iliyofungwa na Frank Lampard.
Kipindi cha Pili Arsenal walizinduka na kubadilika na Theo Walcott kuwapa Bao lao moja lililowafanye wachangamke kutafuta sare ambayo, hata hivyo, hawakuipata.

MSIMAMO-Timu zaJuu:
1 Man United Mechi 22 Pointi 55
2 Man City  Mechi 23 Pointi 51
3 Chelsea  Mechi 23 Pointi 45
4 Tottenham  Mechi 22 Pointi 40
5 Everton  Mechi 22 Pointi 37
6 Arsenal  Mechi 22 Pointi 34
7 Liverpool  Mechi 23 Pointi 34
8 West Brom Mechi 23 Pointi 34
9 Swansea  Mechi 23 Pointi 33
10 Stoke Mechi 23 Pointi 29

Kipigo hiki kimewaacha Arsenal wabakie nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 34 huku juu yao wapo Everton wenye Pointi 37.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Cahill, Ivanovic, Cole, Ramires, Lampard, Oscar, Hazard, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Ferreira, Marin, Terry, Ba, Bertrand, Ake.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs, Coquelin, Diaby, Walcott, Wilshere, Cazorla, Giroud
Akiba: Mannone, Koscielny, Andre Santos, Ramsey, Arshavin, Jenkinson, Frimpong.
Refa: Martin Atkinson

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumapili Januari 20
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United
Jumatatu Januari 21
[SAA 5 Usiku]
Southampton v Everton


Possession40%60%90minsChelseaArsenal

YANGA YAENDESHA MKUTANO MKUU WAKE KISASA!!

>>CLOUDS TV YAPEPERUSHA MKUTANO LAIVU!!
>>YATOA VYETI, FEDHA, PIKIPIKI KWA BAADHI YA WANACHAMA KWA UTUMISHI ULIOTUKUKA!!
>>UWANJA WAO WA WATAZAMAJI 40,000 KUANZA KUJENGWA MEI!!
YANGA_MKUTANO_MKUUKLABU KONGWE NCHINI, Yanga, leo chini ya Mwenyekiti wake Yusuf Manji wamefanya Mkutano Mkuu kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam huku ukihudhuriwa na Wanachama 1440 na kuweka Historia kwa kuendeshwa kisasa kabisa na kwa utulivu mkubwa na pia kuonyeshwa moja kwa moja kupitia Kituo cha TV cha Clouds.
Mara baada ya Mwenyekiti Manji kuufungua Mkutano huo, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, na Mzee Ibrahim Akilimali waliongoza Sala fupi huku Sanga akiongoza ile ya Madhehebu ya Kikristo na Mzee Akilimali ile ya Kiislam.
Miongoni mwa mambo yaliyoamuliwa kwenye Mkutano huo ni kuongeza muda wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mama Fatma Karume na Francis Kifukwe, na pia kuteua Wajumbe wapya wa Bodi hiyo ambao ni Captain George Mkuchika na Balozi Ameir Mpumbwe.YANGA_MJENGO
Miongoni mwa mambo makubwa yaliyotajwa Mkutanoni ni kuhusu Ujenzi wa Uwanja utakaochukua Watazamaji 40,000 na kugharimu Shilingi Bilioni 32 huku Wanachama wakionyeshwa Michoro yake na pia kujulishwa Ujenzi wake unatarajiwa Kuanza Mwezi Mei chini ya Kampuni ya Ujenzi ya BCCG iliyojenga Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Pia, Mkutano huo uliwatimua Uanachama Mwesigwa Selestine, Lousi Sendeu na Godwin Muganyizi kwa kosa la kufungua Kesi za Madai dhidi ya Yanga.
Pia Uongozi wa Yanga ulitoa Vyeti vya Utambuzi kwa baadhi ya Wanachama na Wachezaji/Viongozi kwa mchango wao katika Klabu ya Yanga..
Waliotunukiwa ni:
1.Abdallah Bin Kleb-Kongozi kwa kujitolea sana katika kuhakikisha Timu inafanya vizuri na kushinda michezo inayoikabili
2.Shadrack Nsajigwa-Mchezaji aliyechezea Yanga kwa muda mrefu ambae alipewa Barua na Fedha Shilingi 1,000,000/=.
3.Mahmoud Momar-Mfanyakazi Mtunza Vifaa wa siku nyingi katika Benchi la Ufundi (Barua na Fedha taslimu Sh. 1,000,000/=)
4.Stephen Samuel-Mwanachama Bora na mwenye uchungu na Yanga (Barua na zawadi ya Pikipiki mpya)
5.Hayati Isamail Rashid-Mwanachama aliyesaidia kupatikana kwa muafaka (Barua).

CHEKI MARIA SHARAPOVA ALIVYOMWANGAMIZA MWANADADA Kirsten Flipkens KATIKA TENISI HIYO JANA

AFCON 2013: South Africa 0 Cape Verde Islands 0


AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZE>>UBINGWA MATAIFA YA AFRIKA WAANZA HUKO BONDENI!!
>>BAADAE LEO: ANGOLA v MOROCCO!
WENYEJI wa Mashindano, South Africa, maarufu kama Bafana Bafana, leo wamefungua rasmi Mashindano ya CAF ya kusaka Taifa Bingwa Barani Afrika, AFCON 2013 kwa kutoka sare ya kuvunja moyo kwao dhidi ya ‘Taifa Dogo’ Visiwa vya Cape Verde katika Mechi ya Kundi A iliyochezwa Uwanja wa Soccer City huko Soweto Jijini Johannesburg.
+++++++++++++
KUNDI A:
-South Africa
-Cape Verde
-Morocco
-Angola
+++++++++++++AFCON_2013_LOGO
Bafana Bafana walikuwa na wakati mgumu dhidi ya Cape Verde ambao nusura Straika wao Platini awape Bao lakini akapiga Shuti lake nje.
Baadae leo, kuanzia Saa 4 Usiku, Bongo Taimu, Angola na Morocco zitacheza Uwanja wa Moses Mabhida huko Mjini Durban katika Mechi ya pili ya Kundi A.
VIKOSI:
South Africa: Khune; Ngcongca, Khumalo, Sangweni, Matlaba; Dikgacoi, Letsholonyane, Phala, Tshabalala; Majoro, Parker
Akiba: Sandilands, Nthethe, Gaxa, Masilela, Chabangu, Mphela, Serero, Furman, Mahlangu, Manyisa, Meyiwa, Rantie.
Cape Verde Islands: Vozinha; Carlitos, Fernando Varela, Nando, Nivaldo; Babanco, Soares, Platini, Toni Varela; Heldon, Mendes
Akiba: Fredson Tavares, Rilly, Pecks, Guy Ramos, Lima, Gege, David Silva, Rony, Stenio, Ramilton Rosarip, Julio Tavares, Djaniny.
Refa: Djamel Haimoudi (Algeria)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
[SAA za BONGO]
Jumamosi Januari 19
South Africa 0 Cape Verde Islands 0
Angola v Morocco [Moses Mabhida Stadium, Durban Saa 4 Usiku]
Jumapili Januari 20
Ghana v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mali v Niger Nelson [Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatatu Januari 21
Zambia v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Nigeria v Burkina Faso [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumanne Januari 22
Ivory Coast v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Tunisia v Algeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatano Januari 23
South Africa v Angola [Moses Mabhida Stadium Saa 12 Jioni]
Morocco v Cape Verde Islands [Moses Mabhida Stadium Saa 3 Usiku]
Alhamisi Januari 24
Ghana v Mali [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Niger v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast v Tunisia [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Algeria v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumapili Januari 27
Morocco v South Africa [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Cape Verde Islands v Angola [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatatu Januari 28
Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumanne Januari 29
Ethiopia v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Burkina Faso v Zambia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatano Januari 30
Algeria v Ivory Coast [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Togo v Tunisia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]

LA LIGA: BARCA WAONJA KICHAPO CHA KWANZA MSIMU HUU!!


>>WAONGOZA 2-0 NDANI YA DAKIKA 25, WAPIGWA 3-2 DAKIKA 90!!
LIONEL_MESSI-HUZUNIREAL SOCIEDAD walitoka nyuma kwa Bao 2-0 ndani ya Dakika 25 na kuwatwanga Vinara wa La Liga Barcelona Bao 3-2 na kuwashushia kipigo chao cha kwanza Msimu huu kwenye Ligi hiyo.
Bao za Lionel Messi na Pedro ziliwapa Barca uongozi wa Bao 2-0 lakini Gonzalo Castro akaifungia Real Sociedad Bao moja kabla Haftaimu.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Real Sociedad 3
-Castro Dakika ya 41 & 63
-Imanol Agirretxe 91
Barcelona 2
-Lionel Messi Dakika ya 7
-Pedro Rodriguez 25
KADI:
-Gerard Pique [Barcelona] 33 & 56

Beki wa Barca Gerard Pique alitolewa nje katika Dakika ya 56 baada ya kulambwa Kadi za Njano mbili na Castro akaisawazishia Real Sociedad kabla Imanol Agirretxe kupiga Bao la 3 na la ushindi katika Dakika ya 91.
RATIBA:
Jumapili Januari 20
Osasuna v Deportivo la Coruna
Valladolid v Zaragoza
Atletico Madrid v Levante
Valencia v Real Madrid
Jumatatu Januari 21
Real Betis v Athletic Bilbao

BPL: WEST BROM 2 ASTON VILLA 2


 
BPL_LOGOPeter Odemwingie, Mchezaji ambae alitemwa na Nigeria kuwemo kwenye Kikosi cha Nchi hiyo kwenye AFCON 2013, leo ameiokoa Klabu yake West Bromwich Albion baada ya kufunga Bao la kusawazisha katika Dakika ya 83 walipotoka nyuma kwa Bao 2-0 na kutoka sare 2-2 na Aston Villa katika Mechi ya BPL, Barclays Premier League.

MAGOLI:
West Brom 2
-Brunt Dakika ya 49
-Odemwingie 83
Aston Villa 2
-Benteke Dakika ya 12
-Agbonlahor 31

Aston Villa, wakicheza ugenini katika Dabi ya Miji ya Kati ya England, walitangulia 2-0 kwa Bao za Christian Benteke na Gabriel Agbonlahor.
Lakini Kipindi cha Pili Chris Brunt alifunga Bao la Kwanza na Odemwingie kusawazisha.
VIKOSI:
West Brom: Foster, Jones, McAuley, Olsson, Ridgewell, Morrison, Dorrans, Yacob, Brunt, Lukaku, Odemwingie
Akiba: Myhill, Popov, Rosenberg, Thomas, Thorne, Dawson, Tamas.
Aston Villa: Guzan, Vlaar, Clark, Baker, Lowton, Westwood, Delph, N'Zogbia, Bennett, Agbonlahor, Benteke
Akiba: Marshall, Ireland, Bent, Holman, Bowery, Bannan, Lichaj.
Refa: Lee Probert

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United
Jumatatu Januari 21
[SAA 5 Usiku]
Southampton v Everton

AUSTRALIA OPEN: SHARAPOVA, FERRER WATINGA ROBO FAINALI.


MWANADADA nyota katika mchezo wa tenisi, Maria Sharapova amefanikiwa kutinga kirahisi hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya Australia baada ya kufanikiwa kumfunga Kirsten Flipkens wa Ubelgiji kwa 6-1 6-0. Sharapova amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu katika michuano hiyo na kuweka rekodi ya kushinda michezo miwili bila kupoteza alama katika michezo miwili ya kwanza kabla ya kumuondosha bingwa mara saba wa mataji ya Grand Slam Venus Williams katika mzunguko wa tatu. Sharapova sasa atakutana na Mrusi mwenzake Ekaterina Makarova baada ya mwanadada huyo kufanikiwa kumg’oa Angelique Kerber kwa 7-5 6-4 katika mzunguko wa nne wa michuano hiyo. Kwa upande wanaume David Ferrer anayeshika namba nne katika orodha za ubora duniani alifanikiwa kutumia udhaifu wa Kei Nishikori wa Japan alieumia mguu na kufanikiwa kumsambaratisha na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Nishikori aliingia katika mchezo huo akiwa na matatizo katika mguu wake wa kushoto na katika seti ya pili alijitonesha mguu wake huo na kumpa nafasi Ferrer kumuadhibu kwa 6-2 6-1 6-4 ambapo sasa atakutana na aidha Janko Tipsarevic wa Serbia au Mhispania mwenzake Nicolas Almagro katika robo fainali.

LIVERPOOL INAHITAJI KUONGEZA WACHEZAJI WAWILI AU WATATU ILI IWE MOTO - GERRARD.


KIUNGO nyota wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard anaamini kuwa timu hiyo inaweza kucheza na timu yoyote chini ya meneja mpya Brandan Rogders lakini inahitaji kuongeza wachezaji wawili au watatu ili kusaidia kuongeza nguvu. Liverpool jana wakicheza kwa kiwango bora iliifunga Norwich mabao 5-0 katika Uwanja wa Anfield huku Daniel Sturridge aliyesajiliwa kwa paundi milioni 12 kutoka Chelsea akifunga bao lake la tatu katika michezo mitatu toka atue hapo. Lakini pamoja na ushindi huo mnono Gerrard anaamini kuwa bado wanahitaji wachezaji wawili au watatu wakubwa ili waweze kufukuzia mataji. Liverpool inakabiliwa na mchezo mgumu wa ligi dhidi ya Arsenal katika Uwanja wa Emirates mwishoni mwa wiki ijayo baada ya kucheza mchezo wao wa mzunguko wa nne wa Kombe la FA huko Oldham.

PETERHANSEL, DESPRES WATAMBA MBIO ZA DAKAR RALLY.


DEREVA nyota wa mashindano ya Dakar Rally, Stephane Peterhansel amefanikiwa kushinda taji la tano la mashindano hayo na kuweka rekodi kuwa dereva wa kwanza kufanya hivyo, wakati Mfaransa mwenzake Cyril Despres naye alishinda taji la tano kwa upande wa mbio za pikipiki. Peterhensel ambaye ameshinda mbio za magari za Dakar mwaka 2004, 2005, 2007, 2012 na mwaka huu, na pia kuwa bingwa katika mbio za pikipiki mara sita na kuvunja rekodi ya Ari Vatanen aliyewahi kushinda mbio hizo mara nne. 
Akihojiwa mara baada ya ushindi huo Peterhensel alidai kuwa hiyo ni siku muhimu kwake kwa kuweka rekodi hiyo na kushukuru kwakuwa ni mara ya kwanza anamaliza mbio za zilizochukua siku 15 bila kupata matatizo yoyote katika gari lake. Wapinzani wakubwa wa Peterhensel kwenye mbio hizo Carlos Sainz na Nasser al-Attiyah walijitoa mapema baada ya magari kupata matatizo ya kiufundi.

BAFANA BAFANA YABANWA MBAVU NA CAPE VERDE JANA KULE SOUTH AFRIKA KWA MADIBA


HALI ya baridi kali, mvua, soka lisilovutia na uhaba wa mabao ndio mambo yaliyoonekana kuchukua nafasi katika ufunguzi wa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon inayofanyika nchini Afrika Kusini jana. Michuano ya 29 inayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kuanzia mwaka 1957 ilishuhudia michezo miwili kuisha ya kundi A kumalizika huku hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Wenyeji wa michuano hiyo Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana walishindwa kuwapa raha mashabiki wao wapatao 85,000 waliojitokeza katika Uwanja wa Soccer City jijini Johannesburg pale alipong’ang’aniwa na timu ngeni katika mashindano hayo ya Cape Verde. Baada ya mchezo ulifuatiwa na mchezo mwingine katika huohuo kati ya Morocco na Angola lakini mpaka dakika tisini zinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Michuano hiyo inaendelea tena baadae leo kwa michezo miwili ya kundi B ambapo katika mchezo wa kwanza Ghana itacheza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC ukifuatiwa na mchezo kati ya Mali na Niger katika Uwanja wa Nelson Mandela Bay jijini Port Elizabeth.

AFCON 2013: UHABA WA MABAO WATAWALA MECHI ZA UFUNGUZI.


HALI ya baridi kali, mvua, soka lisilovutia na uhaba wa mabao ndio mambo yaliyoonekana kuchukua nafasi katika ufunguzi wa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon inayofanyika nchini Afrika Kusini jana. Michuano ya 29 inayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kuanzia mwaka 1957 ilishuhudia michezo miwili kuisha ya kundi A kumalizika huku hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Wenyeji wa michuano hiyo Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana walishindwa kuwapa raha mashabiki wao wapatao 85,000 waliojitokeza katika Uwanja wa Soccer City jijini Johannesburg pale alipong’ang’aniwa na timu ngeni katika mashindano hayo ya Cape Verde. Baada ya mchezo ulifuatiwa na mchezo mwingine katika huohuo kati ya Morocco na Angola lakini mpaka dakika tisini zinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Michuano hiyo inaendelea tena baadae leo kwa michezo miwili ya kundi B ambapo katika mchezo wa kwanza Ghana itacheza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC ukifuatiwa na mchezo kati ya Mali na Niger katika Uwanja wa Nelson Mandela Bay jijini Port Elizabeth.

STEWART AJIVUNIA KIWANGO AZAM LICHA YA KIPIGO KENYA JANA


Azam katika mechi ya jana
LICHA ya kupoteza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya AFC Leopard jana, kocha wa Azam FC Stewart Hall amesema timu yake imecheza vizuri na kufungwa ni sehemu ya mchezo.
Stewart alisema haikuwa bahati kwao kwa kuwa walipata nafasi nyingi za wazi umaliziaji ukawa tatizo, pia na penati mbili walizopata wachezaji wake walikosa na kuipa ushindi timu hiyo iliyokuwa na mashabiki wengi uwanjani hapo.
“Timu inayocheza vizuri ni ile inayotengeneza nafasi na kucheza mpira mzuri, tulicheza vizuri nafurahi kuona wachezaji wanajituma, kukosa penati na nafasi za wazi ni matatizo yanaweza kuzibika” alisema Stewart.
Aliongeza kuwa kupitia mechi hizi zote watakuwa na wakati mzuri wa kurekebisha makosa yanayotokea kabla ya kuanza kwa mechi za ligi.
Katika mchezo huo AFC Leopards walikuwa wa kwanza kupata magoli yalifungwa katika dk ya 14 na Paul Were na dk 54 Mike Baraza aliifungia timu hiyo goli la pili kufuatia kosa la beki wa Azam FC, kumruhusu akapiga shuti likaenda moja kwa moja wavuni.
Azam FC walipata penati tatu katika dk 19, Jockins Atudo alikosa baada ya kupiga mkwaju uliotoka nje, dk 65 Khamis Mcha nae alikosa penati baada ya kugonga mwamba na kurudi ndani ikaokolewa na mabeki wa AFC.
Goli la Azam FC lilipatikana kupitia kwa mkwaju wa penati iliyopigwa na Samih Haji Nuhu baada ya beki wa AFC Erick Masika kumwangusha Humprey Mieno kwenye eneo la hatari.
Kipindi cha pili Kocha Stewart alifanya mabadiliko walitoka, Luckson Kakolaki, Salum Abubakar, Abdulhalim Humud, Uhuru Seleman, Jabir Aziz na Gaudence Mwaikimba nafasi zao zikachukuliwa na David Mwantika, Michael Bolou,Humphrey Mieno, Ibrahim Mwaipopo, Brian Umony na Abdi Kassim, mabadiliko hayo yaliimarisha kikosi hicho muda wote wa mchezo.
Baada ya mchezo huo kocha wa AFC, Tom Olaba alisema kupata ushindi kwa kuifunga timu bora ni mafanikio kwake na kuonyesha ukomavu kwa wachezaji wake.

WAANDAAJI WA MSHINDANO YA MARATHON WAMETANGAZA KUWA KILI MARATHON MACHI 3 MOSHI



Washiriki wa Kili Marathon mwaka jana
WAANDAAJI wa Kilimanjaro Marathon 2013 wametangaza kwamba maandalizi kwa ajili ya mashindano ya mwaka huu yanaendelea vizuri na mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuwa na msisimko wa aina yake. Mbio hizo zimepangwa kufanyika tarehe 3 Machi 2013 mjini Moshi.
John Addison Mkurugenzi Mtendaji wa Wild Frontiers, waandaaji wa tukio hilo alisema kwamba usajili wa washiriki utafanyika mjini Arusha tarehe 28 Februari katika hotel ya New Arusha, na tarehe 1 na 2 Machi usajili utafanyika Hoteli ya  Keys Moshi. Hakuna mtu ataruhusiwa kujisajili siku ya mashindano.
Usajili wa mtandao tayari upo wazi na washiriki wanaweza kuanza kujiandikisha kwenye mtandao kupitia tovuti ya www.kilimanjaromarathon.com.
Alisema, Kilimanjaro Premium Lager Marathon ya km 42, Nusu Marathoni ya km 21, na GAPCO Nusu Marathoni kwa walemavu ztaanzia uwanja wa MUCCoBs, wakati Vodacom  Fun Run ya km 5 itaanzia mashariki mwa geti la uwanja wa MUCCoBs kwa upande wa barabara ya Uru na kumalizika ndani ya uwanja.
Kilimanjaro Premium lager Marathon ya km 42 itaanza saa 12:30 asubuhi, na kufuatiwa na Km 21 Nusu Marathon kwa walemavu saa 12:45 Asubuhi na Km 21 Nusu Marathon itaanza saa 01:00 asubuhi wakati Vodacom Fun Run ya Km 5 inategemea kuanza 01:30 Asubuhi.“Kilimanjaro Marathon 2013 itapata usimamizi wa wataalamu wa riadha pamoja na wataalamu wa masuala ya muda (time-keeping) navilevile kutakuwepo vituo mbalimbali vya kunywa maji na viburudisho.
Addison aliongeza kuwa Kilimanjaro Marathon ni tukio ambalo limeendelea kuongeza  hadhi ya Tanzania kimataifa kila mwaka; na imesaidia kutambua na kutoa fursa kwa wanariadha wa ndani kukua zaidi, kukuza utalii wa Tanzania na watu kupata nafasi ya kufurahi zaidi.
Alisema mbio hizo zitakuwa na viwango vya kimataifa na kusimamiwa na Kilimanjaro Marathon Club, Athletics Tanzania na Kilimanjaro Amateur Athletics Association. Ili kuhakikisha usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara za ndani na nje ya mji wa Moshi zitafungwa kuanzia saa 12:15 asubuhi hadi 03:30 asubuhi tarehe 3, Machi 2013 ili kuruhusu wakimbiaji kupita salama.
Tanzania Breweries Limited na bidhaa yao ya Kilimanjaro Premium Lager ni wadhamini wakuu wa Kilimanjaro Marathon na shughuli zingine za burudani baada ya riadha, na wamekuwa wadhamini wa tukio hili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003, juhudi zao katika masoko na matangazo imekuwa mchango mkubwa katika kukuza mbio hizi.
Executive Solutions ni waratibu wa tukio hilo wakati wadhamini wengine ni Vodacom Tanzania (Km 5 Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon kwa Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Tanzanite One, New Arusha Hotel, na Kilimanjaro Water.

MCHAKATO TIKETI ZA ELEKTRONIKI WAFIKIA ASILIMIA 80



Mashabiki Uwanja wa Taifa 

UJENZI wa vifaa (turnstiles) vitakavyotumika kwa ajili ya tiketi za elektroniki kwenye viwanja saba kati ya nane vitakavyotumia mfumo huo umekamilika kwa asilimia 80.
Viwanja hivyo ni Chamazi (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Sokoine (Mbeya), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), na Mkwakwani (Tanga).
Wakati Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari una turnstiles, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza bado haujaruhusu ufungaji wa vifaa ukisubiri idhini kutoka kwa wamiliki wake (CCM Makao Makuu).
Vifaa vitakavyotumika kusoma tiketi za elektroniki katika viwanja hivyo vinatarajiwa kuwa vimefungwa kufikia Februari 20 mwaka huu.
Hakutakuwa na matumizi ya fedha taslimu mara baada ya mradi huo wa tiketi la elektroniki kuanza, kwani tiketi zitakuwa zikinunuliwa kwa kadi maalumu (smart card) katika vituo mbalimbali vitakavyotangazwa baadaye.
Benki ya CRDB ndiyo iliyoingia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutengeneza tiketi za elektroniki baada ya kuibuka mshindi kwenye tenda.

MAREFA WA KENYA KUICHEZESHA AZAM KATIKA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA


Wachezaji wa Azam mazoezini

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka Kenya kuchezesha mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini itakayofanyika jijini Dar es Salaam kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.
Mwamuzi wa kati atakuwa Davies Omweno na atasaidiziwa na mwamuzi msaidizi namba moja Peter Keireini, mwamuzi msaidizi namba mbili Gilbert Cheruiyot wakati mwamuzi wa mezani Anthony Ogwayo.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Hassan Mohamed Mohamud kutoka Somalia. Waamuzi wa mechi ya marudiano itakayochezwa jijini Juba watatoka Rwanda wakiongozwa na Gervais Munyanziza.
Wakati huo huo: Waamuzi wa Tanzania wakiongozwa na Israel Mujuni wameteuliwa kuchezesha pambano la awali la raundi ya kwanza kuwania Kombe la Shirikisho kati ya UFC Haut Nkam ya Cameroon na US Bougouni ya Mali.
Kwa uteuzi huo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Mujuni na wenzake Ali Kinduli, Samuel Mpenzu na Waziri Sheha watachezesha mechi hiyo itakayofanyika kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.
Pierre Alain Mouguengui kutoka Gabon ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo. UFC Haut Nkam na US Bougouni zitarudiana wiki mbili baadaye nchini Mali.

GUARDIOLA ATAKA KUFANYA BALAA, ATANGAZA KUWASAJILI SUAREZ NA FALCAO




Wanted man: Luis Suarez is on Pep Guardiola's radar

Pep Guardiola is set to deliver another blow to the Premier League by making Luis Suarez and Radamel Falcao his top Bayern Munich targets.
Former Barcelona boss Guardiola last week agreed to take over as Bayern manager in July and will spend the next five months drawing up an action plan.
That will include signing a new world-class forward, with Suarez and Falcao two players Guardiola is ­particularly keen on.
Bayern would be unlikely to pay out for both players, with Suarez valued at £40m and Falcao’s Atletico Madrid ­release clause set at ­£46m, so Guardiola will have to decide on his favourite.
News of Guardiola’s interest will worry both Liverpool, who are desperate to keep hold of star man Suarez, and Chelsea, who have been ­chasing Falcao’s signature.
Suarez’s agent is Guardiola’s brother Pere and that has been a cause of concern to some Anfield insiders ever since Pep left Barca.
Uruguay star ­Suarez signed a new Liverpool contract last summer and has consistently reiterated his love for the club and fans.


David Ramos
But just last week ex-Liverpool ­director of football Damien ­Comolli warned that Suarez could be driven out by the constant controversy ­surrounding his actions.
That was before Suarez ­created a new storm by ­admitting to diving against Stoke and claiming ­Manchester United control the English media.
Liverpool boss Brendan Rodgers described the Suarez admission of diving ­“unacceptable”and promised the 25-year-old would be dealt with by the club.
Guardiola’s decision to snub Chelsea for Bayern was a major blow for owner Roman Abramovich and missing out on Falcao to the Spaniard would rub salt in the wounds.
Speaking last year about ­Falcao, Guardiola said: “He’s a sensational player — the best ­striker inside the box.”



Neymar is another option, but Barca are confident of landing the Brazilian.
Meanwhile, ­Guardiola has kept alive his dream of eventually managing ­Manchester United by
taking the Bayern job.
Sources who have worked with the Spaniard, ­maintain he would ideally like to ­manage at Old ­Trafford when he does move to the ­Premier League.

TIMU YA MAAFANDE WA POLISI TABORA YAWAPIGISHA KWATA KOMBAIN YA WILAYA 2-1 ALLY HASSAN MWINYI JANA>>>>>WAKATI HUO HUO TIMU YA KAGERA SUGAR INATARAJIA KUWASILI MKOANI TABORA TAYARI KWA MCHEZO W AKESHO DHIDI YA RHINO&NA JUMANNE DHIDI YA POLISI TABORA


 

 Timu ya maafande wa mkoani tabora polisi tabora jana ilitoka nyuma ya bao 1-0 na kuibuka na ushindi w amabao 2-1 katika mchezo w akirafiki uluochezwa katika dimba la ALLY HASSAN MWINYI  kuanzia majira ya saa 4;30 za jioni.

Bao la kuongoza kwa timu ya kombaini wilaya lilifungw ana nahodha wa timu hiyo GOFREY MAGASO akiunganisha krosi ya kona iliyochongwa toka upande wa mashariki na winga ABDALAHA JUMA.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza timu ya kombaini wilaya ilienda kifua mbele kwa bao 1-0 lililofungwa mnamo dakika ya 33.
Kipindi cha pili kocha wa polisi tabora ambaye amesainishwa mkata akitokea dar es salaam alifanya mabadiliko katika timu yake ndipo alipopata mafanikipo mnamo dakika ya 67 ya kipindi cha pili baaada ya mshambuliaji wake IDDY KIBWANA kuachia shuti kali lililoenda moja klwa moja wavuni.

Naye IBRAHIM MUSSA liunganisha krosi nzuri iliyochongwa na iddy kibwana na kuiandikia polisi bao la 2 na la ushindi kwao.hadi dakika 90 za mchezo polisi tabora walitoka kifua mbele kwa goli 2-1 na kuonesha matumaini kwa mashabiki w amkoani tabora.

Na kuelekea katika duru la pili la michuano ya ligi daraja la kwanza timu ya polisi tabora imesajili wachezaji watano kutoka timu mbali mbali hapa tanzania wachezaji hao ni DANIEL KINDU na JEREMIA wote kutoka timu ya Samaria,JAPHARI kutoka katika timu ya A.F.C Arusha ,AMOS AMBAN kutoka timu ya polisi dodoma na RAYGAN MBUTA kutoka timu ya polisi dodoma naye kw amkopo.
Wachezaji wa zamani watimu hiyo ni JOHN MTULI,JAMAI JUMANNE,JOSEPHY KILINDI,ERNEST NKANDI,HUSSEIN ABDALAH,RAMADHAN SEMWA,IDDY KIBWANA,ATHUMAIN MPONDELA,HUSSEIN ABDALAH,MUSSA BOAZ,DAVID JOSEPHY,KAIZAR KILOWOKO,ABDUL  AZIZ,IBRAHIM MUSSA,SAMUEL KILINDI na RAMADHAN FIRSTEEN

WAKATI HUO HUO timu ya Kagera sugar ya manungu turiani BUKOBA inatarajia kuwasili leo kuanzia majira ya saa mbili kamili za uskiku ikitoka Bukoba tayari kwa michezo yake ya kirafiki siku ya jumatatu kesho na jumanne.

Kesho jumatatu inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya jeshi la wananchi tanzania RHINO RANGERS mchezo w akirafiki utakaofanyika katika dimba la ALLY HASSAN MWINYI kuanzia majira ya saa kumi na nusu za jioni na kesho kutwa jumanne itacheza na wapiga kwata wa hapa mkoani tabora POLISI TABORA katika dimba hilo hilo la ALLY HASSAN MWINYI.

Pia siku hiyo ya jumanne nayo timu ya wnaakisha mapanda ya mwanza TOTO AFRICAN inatarajia kushuka dimbani hapa mkoani tabora na timu ya RHINO RANGERS mchezo wa kujipima nguvu kuelekea katika duru la pili la vodacom bara na ligi daraja la kwanza FDL ambayo inatarajia kutimua vumbi siku ya jumamosi ya Januari 26 kati  VPL ni kati ya African Lyon v Simba [National Stadium, Dar es Salaam]Mtibwa Sugar v Polisi Morogoro [Manungu, Morogoro] Coastal Union v Mgambo JKT [Mkwakwani, Tanga] Ruvu Shootings v JKT Ruvu [Mabatini, Pwani]  Azam v Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]  JKT Oljoro v Toto Africans [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Na  Januari 27Yanga v Tanzania Prisons [National Stadium, Dar es Salaam]

PICHA MBALI MBALI ZA TIMU YA POLISI TABORA NA KOMBAINI WILAYA HIYO JANA


TIMU YA KOMBAINI YA WILAYA MKOA W ATABORA WAKIWA TAYARI KWA MECHI DHIDI YA WAPIGA KWATA WA HAPA MKOANI TABORA [POLISI TABORA SIKU YA JANA KATIKA DIMBA LA ALLY HASSAN MWINYI
 
TIMU YA MAAFANDE W APOLISI TABORA WENYE NYEKUNDU TAYARI KW AGEMU LA JANA DHIDI YA TIMU YA KOMBAINI YA WILAYA


HAPA KIROHO KINADUNDA KWA WACHEZAJI TAYARI KW AGAME HAPA WANAPEANA MIKONO FAIR PLAY
 
KAMA UWANJA WA KIMATAIFA VILE ALLY HASAAN MWINYI INAVYOONEKANA KWA SASA
 
GOLIKIPA WA KOMBAINI WILAYA HUYO TAYARI KWA MCHEZO AKIWAPA MKONO WACHEZAJI WA POLISI TABORA HIYO JANA

BENCHI LA KOMBAINI WAKIFUATILIA MCHEZO WA JANA KATIKA DIMBA LA ALLY HASSANI MWINYI
 
JUKWAA KUU LINAVYOONEKANA KKWA NYUMA YA WACHEZAJI W AKOMBAINI YA WILAYA

 
HAPA KOCHA WA POLISI TABORA MWINYIMAJI TAMBAZA AKIWAPA MAELEZO WACHEZAJI WAKE BAADA YA MAPUMZIKO KWENDA WAKIWA NYUMA KW ABAO 1-0 DHIDI YA KOMBAINI WILAYA