Thursday, November 22, 2012


ASHANTI NOMA YATEMBEZA BAKORA KUMI KWA MORO UNITED

TIMU ya Ashanti United jana iliivurumisha bila huruma Moro United mabao 10-1 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulionekana dhahiri kuwa wa upande mmoja kutokana na wachezaji mahiri wa Moro United kutokuwepo, Ashanti walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza mabao 5-1.

Moro ambayo mlinda mlango wake alikuwa bonge la mtu alikuwa akijigararagaza kila wakati kwa madai akaumia.

Mabao ya Ashanti yalifungwa na  Lambele Jerome alifunga mabao sita dakika ya 35, 52, 71, 76, 81 na 89, Shabani Hatibu alifunga matatu dakika ya nane, 11 na 37, na Raju Mahmoud dakika ya 16.

Bao la Moro United lilifungwa kwa njia ya penalti  na Twahir Kiparamoto dakika ya 21.

Kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani Green Warriors na Polisi Dar es Salaam zilitoka sare ya kufungana bao 2-2.

Mabao ya Green Worriors yalifungwa na Said Asaa dakika ya 80  Edward Kheri dakika ya 89.



Mil.300/ KUNUNUA WACHEZAJI HAWA !!!!

Washambuliaji Emmanuel Okwi na Mrisho Ngasa wa Simba pamoja na beki wa kimataifa Mbuyu Twite wa Yanga wanatakiwa kwa dau la jumla la Sh. Milioni 300 ili wazihame timu zao wakati dirisha la usajili wa dirisha dogo litakapofunguliwa rasmi, imefahamika.

Taarifa zilizothibitishwa jana, zimetaja mchanganuo wa ofa iliyotolewa kwa nyota hao kuwa ni dola za Marekani 50,000 kwa ajili ya kumtwaa Okwi, dola 40,000 za kumsajili Ngassa na beki wa kimataifa wa Rwanda, Mbuyu Twite ametengewa dau la dola 100,000; hivyo jumla ya fedha zote kufikia dola 190,000 (Sh. Milioni 300).

 Mkurugenzi wa klabu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Rahim Kangezi, amesema kuwa uongozi wa klabu yake ndiyo unaowataka wachezaji hao na tayari wameshaanza mawasiliano kwa kuziandikia barua klabu za Simba na Yanga kwa nia ya kujaribu kufanya nao biashara, lakini hadi sasa bado hawajajibiwa.

Kangezi amesema kuwa klabu yao ambayo iko katika nafasi ya pili kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi, iko tayari  kutoa fedha hizo ili kuwatwaa nyota hao kwa vile wanajua kuwa watawasaidia kutimiza malengo yao.

"Tayari tumeshampa barua Kaburu (Geofrey- Makamu Mwenyekiti wa Simba) ila wanaonekana hawataki kutupa ushirikiano… kuna wadau tumewapata ambao ndiyo wanatoa fedha hizo," alisema Kangezi, ambaye ndiye alifanikisha usajili wa kiungo Nizar Khalfan kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada kabla hajahamia Philadephia Union na baadaye kurejea nchini kuichezea Yanga.

Kangezi aliongeza kwamba wadau wao ambao ndiyo wanaoisaidia Lyon wanataka kuona timu hiyo inaendelea kushiriki kwenye ligi ya Bara na ndiyo maana wameahidi kuisaidia fedha za kusajili wachezaji zaidi watakaowaongezea nguvu kikosini na kutimiza lengo la kuibakiza timu yao ligi kuu.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako, aliliambia K-SPORT  kwamba hawako tayari kumuuza mchezaji wao yeyote ikiwa wanunuzi hawajafikia vigezo vyao, ikiwa ni pamoja na kutanguliza ofa ya maana ya walau dola za Marekani 200,000 (Sh. Milioni 315).

Afisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga na katibu mkuu wake wake, Evodius Mtawala hawakupatikana  kuzungumzia suala hilo huku Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akishindwa kulielezea baada ya kusema kuwa yeye na viongozi wengine wa klabu yake wako katika kikao cha kamati ya utendaji.

Katika hatua nyingine, Kangezi alisema kuwa licha ya kutokuwapo na muafaka kati yao na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), bado wadhamini wao (Zantel) wanaendelea kuwapa fedha na wiki ijayo wachezaji wataanza mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi.

RAGE AMREJESHA HANSPOPPE KAMATI YA USAJILI

SIKU chache baada ya kamati ya utendaji ya klabu ya Simba kutangza kuzivunja kamati zake ndogondogo, mwenmyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage ameanza kuteua wajumbe wa kamati mbalimbali am,bapo ameanza na ya Usajili  ambapo amemrejeshea madaraka yake mwenyekiti wa awali, Zacharia Hanspoppe.
Rage ambayea aliamua kuzivunja kamati hizo kutokana na kutokuwa na mchango wowote katika timu hiyo ambayo iliishia kushika nafasi ya tatu katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodaco, amesema kwamba ameamua kumrejesha Hansopppe katika nafasi yake kutokana na kutoa mchango mkubwa katika zoezi la usajili na hasa kutumia fedha zake katika kusajili.
Amesema katika kamati hiyo, Rage atashirikiana na Azim Dewji, Mbunge wa Korogwe Steven Ngonyani maarufu kama 'Prof. Maji Marefu', Muhsin Ruhwey, Sued Nkwabi na wengineo atakaowatangaza baadaye.
Rage ameongeza kuwa hivi karibuni atatatangaza wajumbe wa kamati nyingine baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwateua.
Awali kulikuwa na kamati za Ufundi iliyokuwa chini ya Ibrahim Masoud 'Maestro', Kamati ya Nidhamu iliyokuwa chini Jamal Rwambow, Kamati ya Fedha iliyokuwa chini ya Geofrey Nyange 'Kaburu' na Kamati ya Mashindabno iliyokuwa chini ya Joseph Itang'are 'Mzee Kinesi

  

SUNZU KUENDELEA KUOGELEA KWENYE FWEZA MSIMBAZI

Feliux Sunzu akitibiwa

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. ataongezewa mkataba baada ya kumaliza mkataba wake wa awali mwishoni mwa msimu katika klabu ya bingwa Tanzania Bara, Simba SC.
Kiongozi mmoja wa Simba amesema jana kwamba klabu hiyo imeridhika na huduma ya mchezaji huyo mrefu na inahitaji kuendelea naye.  
Kumekuwa na mawazo tofauti ndani ya Simba SC kuhusu Sunzu, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Tanzania, Sh Milioni 5, kwamba hachezi kwa kiwango cha fedha anazolipwa.
Lakini wengine wanaamini Sunzu anawajibika vizuri na anastahili kwa fedha anayolipwa. Pamoja na hayo, hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo kwa sasa, inatia shaka kama itaweza kuurudia mkataba ule ule wa Sunzu.
Hata hivyo, habari zaidi zinasema kwamba Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameamua kumaliza suala la Sunzu kwa kumsainisha mkataba mpya hivi karibuni.
Baada ya kumaliza mkataba wa awali, Simba ili kuendelea kuishi na Sunzu, inakadiriwa kumpa fedha ya dau la usajili, ambalo kwa mwaka haliwezi kuwa chini ya dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. Milioni 20 za Tanzania) na kukubaliana kuhusu mshahara uwe ule ule au mpya.
Kulingana zengwe lililotawala juu ya dola za Kimarekani 3,500 anazolipwa Sunzu kuna uwezekano Simba ikataka kuuteremsha mshahara huo, lakini habari zilizopatikana jana zimesema kwamba Sunzu ataendelea kulipwa mshahara ule ule katika mkataba wake mpya.
Kumalizika kwa mkataba wa Sunzu ni mtihani mwingine kwa Simba, ambayo kwa sasa inakabiliwa na kasheshe la kuingia mkataba mpya na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi ambaye yuko vizuri kisoka na anatolewa macho na Azam na Yanga.
Na suala la usajili linaonekana kuwa zito kwa wakati huu, kwa sababu Kamati ya Utendaji ya Simba SC wiki hii imevunja Kamati zote ndogondogo, ikiwemo Kamati ya Usajili, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Zacharia Hans Poppe.   
Hata hivyo, inadaiwa vibopa wa Kamati ya Usajili, akiwemo Hans Poppe watarejeshewa majukumu hayo. 
 

WATANO KUGOMBEA TUZO YA BBC AFRICAN PLAYER OF THE YEAR.

MAJINA matano ya wachezaji watakaogombea tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika mwaka huu ambayo inatolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC yametangazwa rasmi. Majina ya wachezaji hao ni pamoja na Yaya Toure ambaye anaingia katika orodha hiyo kwa mara ya pili mfululizo akiungana na nyota mwenzake kutoka Ivory Coast, Didier Drogba, Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda kutoka Morocco na nahodha wa Zambia Christopher Katongo. Mshindi wa tuzo hiyo ataamuliwa na mashabiki wa soka barani Afrika Afrika ambao wanatapa nafasi ya kupiga kura mpaka Alhamisi Desemba 13 mwaka huu ya kuchagua mchezaji wanayedhani amefanya vizuri. Wachezaji hao wamechaguliwa kugombea tuzo hiyo kutokana na kufanya vizuri kwa mwaka huu katika vilabu na timu zao za taifa ambapo mshindi anatarajiwa kutangazwa Jumatatu Desemba 17 mwaka huu.

DI MATTEO AELEZA MAPENZI ALIYONAYO KWA CHELSEA PAMOJA NA KUTIMULIWA.

ROBERTO Di Matteo amezungumzia mapenzi yake ya dhati aliyonayo kwa klabu ya Chelsea pamoja na kutimuliwa kuinoa timu hiyo baada ya kukabidhiwa miezi nane iliyopita. Kocha huyo alifanikiwa kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA baada ya kushika nafasi kwa muda baada ya aliyekuwa kocha wa timu Adres Villas Boas kutimuliwa ingawa baadae alipewa mkataba wa miaka miwili. Akihojiwa mara baada ya taarifa za kutimuliwa kutolewa Di Matteo amesema kuwa anajivunia mafanikio aliyopata katika kipindi kifupi alichokuwa meneja wa klabu hiyo ambayo amekuwa na mapenzi nayo kwa kipindi kirefu. Di Matteo alijiunga na Chelsea kama mchezaji mwaka 1996 na kufunga mabao 26 katika michezo 175 aliyocheza kabla ya kuamua kutundika daruga kwasababu ya kuwa majeruhi akiwa na umri wa miaka 31. Aliyewahi kuwa meneja wa Liverpool, Rafael Banitez ndio ameteuliwa kuchukua nafasi ya Di Matteo mpaka msimu huu utakapomalizika.

CHELSEA YAPANGA KUMREJESHA DROGBA STAMFORD BRIDGE.

KLABU ya Chelsea iko katika mazungumzo ambayo kuna uwezekano wa kuona mshambuliaji wake wa zamani Didier Drogba akirejea Stamford Bridge akitokea klabu ya Shanghai Shenhua ya China kwa mkopo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 34 anataka kujiweka fiti kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2013 katika kipindi hiki ambacho msimu wa ligi nchini china umemalizika. Drogba ameliomba Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kumpa ruhusa ya kuhama kabla ya kipindi cha usajili cha dirisha dogo Januari mwakani ombi ambalo shirikisho hilo limedai inalishughulikia. Chelsea katika kipindi cha karibuni imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mshambuliaji kutokana na Fernando Torres kushuka kiwango huku Daniel Sturridge kuwa majeruhi. Drogba ambaye pia amehusishwa na tetesi za kwenda Liverpool, alikaa katika klabu Chelsea kipindi cha miaka nane baada ya kusajiliwa akitokea Olympique Marseille ya Ufaransa mwaka 2004.

WENGER SASA ATAKA KUONGOZA KUNDI.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amepanga kutumia kikosi chake cha kwanza katika mchezo wa mwisho wa kundi B wa Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na timu yake kufuzu hatua ya timu 16 bora. Arsenal ilifanikiwa kutinga katika hatua hiyo baada ya kuifunga Montpellier ya Ufaransa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika jana lakini wanatarajia kusafiri kuifuata Olympiakos Desemba 4 katika mchezo wa mwisho huku wakiwa katika nafasi ya pili mbele ya Schalke 04 ambao wanaongoza kundi hilo. Wenger amesema kuwa amepanga kutumia kikosi chake kamili katika mchezo huyo ili kujaribu kushinda na kumaliza wakiwa vinara wa kundi hilo kitu ambacho kitakuwa muhimu. Kama wakimaliza vinara katika kundi lao watapangiwa timu ambazo zimeshika nafasi ya pili katika makundi mengine na kama wakishindwa kufanya hivyo na kumaliza katika nafasi ya pili watapangiwa kucheza na washindi wa makundi mengine katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.

 

Benitez atua Stamford Bridge, Mashabiki hawamfurahii!!

Uteuzi wa Bosi wa zamani wa Liverpool, Rafael Benitez, kuwa Meneja wa muda wa Chelsea hadi mwishoni mwa Msimu ili kumbadili Roberto Di Matteo alietimuliwa, kumepokelewa kwa masikitiko na baadhi ya Mashabiki wa Klabu hiyo ambao hawakupendezwa na uteuzi huo.
Benitez, Miaka 52, anakuwa ni Meneja wa 9 kwa Chelsea tangu Mmiliki Roman Abramovich aitwae Klabu hiyo Mwaka 2003.
++++++++++++++++++++++++++++++
HIMAYA ya ROMAN ABRAMOVICH=MAMENEJA:
-Claudio Ranieri: Septemba 2000-Mei 2004
-Jose Mourinho: Juni 2004-Septemba 2007
-Avram Grant: Septemba 2007-Mei 2008
-Luiz Felipe Scolari: Julai 2008-Februari 2009
-Guus Hiddink: Februari 2009-Mei 2009
-Carlo Ancelotti: Juni 2009-Mei 2011
-Andre Villas-Boas: Juni 2011-Machi 2012
-Roberto di Matteo: Machi 2012-Novemba 2012
++++++++++++++++++++++++++++++
Benitez jalijiunga na Liverpool kutoka Valencia Mwaka 2004 na akatwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2005, kuifikisha Fainali ya Mashindano hayo Mwaka 2007, na kisha kuondoka Anfield Mwaka 2010 na kujiunga na Inter Milan ambako alidumu Miezi 6 tu na kutimuliwa na tangu wakati huo hajafundisha tena Timu yeyote.
Lakini uteuzi huu wa Benitez umepokewa vibaya kwa baadhi ya Wadau wa Chelsea, mmojawapo akiwa Kiungo wao wa zamani, Nigel Spackman, ambae amesema Meneja huyo hatapendwa hapo Stamford Bridge.
++++++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO za BENITEZ:
1960: Alizaliwa Madrid, 4 Aprili
1986: Ajiunga na Real Madrid kama mmoja wa Makocha
1995: Awa Kocha wa Valladolid na kutimuliwa baada ya Mechi 23
1996: Atua Osasuna na kuondolewa baada Mechi 9
1997: Aipandisha Daraja toka Segunda Division Klabu ya Extremadura
2000: Aipandisha Daraja toka Segunda Division Klabu ya Tenerife
2001: Atua Valencia, atwaa Ubingwa La Liga, Taji la kwanza baada Miaka 31
2004: Atwaa Kombe la Ligi na Uefa Cup akiwa na Valencia
Juni 2004: Asaini Mkataba wa Miaka 5 na Liverpool
2005: Atwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI na Liverpool
Juni 2010: Awa Meneja mpya Inter Milan
Desemba 2010: Atimuliwa Inter baada kutwaa Kombe la FIFA Klabu Bingwa Duniani.
++++++++++++++++++++++++++++++++
BENITEZMapema, kabla uteuzi wa Benitez haujathibitishwa, kulipokuwa na minong’ono tu, Msemaji wa Kundi la Jarida la Mashabiki wa Chelsea, David Johnstone, alitamka: “Rafa Benitez si Meneja wa Chelsea. Baadhi ya Watu huzaliwa kuichezea au kuongoza  Klabu fulani na kwetu sisi Benitez si tunaemtaka!”
Aliongeza: “Alipokuwa Liverpool na Jose Mourinho akiwa Meneja wa Chelsea kulikuwa na bifu kati yao. Benitez aliiponda Chelsea, alikuwa ni Mtu mbaya kwetu na sifa aliyojizolea ni kuwa mambo yakipinda basi si kosa lake ni la wengine!”
Lakini Kiungo wa zamani wa Liverpool na Germany, Dietmar Hamann, ambae alikuwemo kwenye Kikosi cha Liverpool kilichokuwa chini ya Benitez na kutwaa Ubingwa wa Ulaya, anaamini Benitez atainyoosha vyema Chelsea na watatwaa Mataji.
Taarifa za kutoka ndani ya Chelsea zimedokeza kuwa uteuzi  wa Benitez na kupewa Makataba hadi mwisho wa Msimu unatekeleza lengo la Abramovich la kumtaka Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, ambae amejipa mwenyewe likizo toka kwenye Soka hadi Mwakani, aende na kuwa Meneja wa Chelsea kuanzia Msimu ujao.
Wakati huo huo, Kocha alietimuliwa Roberto Di Matteo, ambae akiwa Meneja wa muda aliiwezesha Chelsea kuwa Klabu Bingwa ya Ulaya na kutwaa FA Cup, na baada ya hapo kupewa Mkataba wa kudumu kuanzia Mwezi Juni, amezungumza kuwa hana kinyongo na kufukuzwa kwake na atabaki akiipenda Chelsea.
 

MAN CITY yaaga UEFA CHAMPIONZ LIGI, Arsenal wapeta!


>> PSG, SCHALKE, ARSENAL, AC MILAN, DORTMUND, REAL, ZASONGA!
>>ZAUNGANA na MAN UNITED, MALAGA, PORTO, BARCA, SHAKHTAR, BAYERN, VALENCIA!!
MANCINI_n_MICAHMATOKEO:
Jumatano Novemba 21
FC Porto 3 GNK Dinamo 0
FC Dynamo Kyiv 0 Paris Saint Germain 2
Arsenal 2 Montpellier 0
FC Schalke 1 Olympiacos 0
FC Zenit St. Petersburg 2 Málaga 2
Anderlecht 1 AC Milan 3
Ajax 1 Borussia Dortmund 4
Manchester City 1 Real Madrid 1
++++++++++++++++++++++++++++++++
Mabingwa wa England, Manchester City, wakiwa kwao Uwanja wa Etihad, wameaga rasmi Mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA CHAMPIONZ LIGI, baada ya kutoka sare 1-1 na Real Madrid katika Mechi ya Kundi D ambalo Borussia Dortmund, walioinyuka Ajax 4-1, wanafuzu pamoja na Real na kuwaacha Man City kusaka nafasi ya kucheza EUROPA LIGI ikiwa watawapiku Ajax katika Mechi za mwisho za Kundi hili.
++++++++++++++++++++++++++++++++
KUNDI D
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 5]
1 Borussia Dortmund Pointi 11
2 Real Madrid 8
3 Ajax 4
4 Man City 3
++++++++++++++++++++++++++++++++
Bao za leo zilifungwa na Karim Benzema kwa Real katika Kipindi cha Kwanza na Man City wakarudisha kwa Penati ya Aguero Kipindi cha Pili.
VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Maicon, Kolarov, Nasri, Toure, Silva, Dzeko, Aguero
Akiba: Pantilimon, Lescott, Milner, Sinclair, Javi Garcia, Barry, Tevez.
Real Madrid: Casillas, Arbeloa, Sergio Ramos, Pepe, Fabio Coentrao, Khedira, Alonso, Di Maria, Modric, Ronaldo, Benzema
Akiba: Adan, Varane, Kaka, Ozil, Albiol, Callejon, Nacho.
Refa: Gianluca Rocchi (Italy)
+++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI:
Jumanne Desemba 4
GNK Dinamo v FC Dynamo Kyiv
Paris SaintvGermain FC v FC Porto
Montpellier Hérault SC v FC Schalke 04
Olympiacos FC v Arsenal FC
Málaga CF v RSC Anderlecht
AC Milan v FC Zenit St. Petersburg
Borussia Dortmund v Manchester City FC
Real Madrid CF v AFC Ajax
Jumatano Desemba 5
FC Shakhtar Donetsk v Juventus
Chelsea FC v FC Nordsjælland
LOSC Lille v Valencia CF
FC Bayern München v FC BATE Borisov
FC Barcelona v SL Benfica
Celtic FC v FC Spartak Moskva
Manchester United FC v CFR 1907 Cluj
SC Braga v Galatasaray A.S.
 

UEFA yamshitaki Adriano kwa kupuuza ‘HAKI MCHEZONI!’ na kufunga BAO!!


LUIZ_ADRIANO>>GOLI la ADRIANO kwa SHAKHTAR lazua utata wa KIHISTORIA!
Fowadi wa Shakhtar Donetsk Luiz Adriano ambae jana alifunga Bao la kwanza na la kusawazisha ambalo liliibeba Timu yake iwatandike Nordsjaelland Bao 5-2 amefunguliwa Mashitaka na UEFA kwa ‘Kuvunja Nguzo za Mchezo wa Haki’ kitu ambacho kimeshangaza mno Wadau mbalimbali wa Soka Duniani.
Bao la Adriano lilifungwa baada ya Mchezaji wa Nordsjaelland kuumia na Refa kusimamisha Gemu na ilipoanza tena, Willian wa Shakhtar alipiga mpira mbele kumrudishia Kipa wa Nordsjaelland, kama misingi ya ‘HAKI MCHEZONI!’ inavyotaka, lakini Luiz Adriano akaunasa mpira huo, akamzunguka Kipa na kufunga Bao ambalo, KISHERIA, ni la HAKI.
Wakati huo Shakhtar walikuwa nyuma kwa Bao 1-0.
Kitendo hiki cha UEFA kumshitaki Adriano kimezua mjadala mkali huku Wadau wengi wakidai, hamna Sheria inayolinda Mchezaji asifunge Bao kiaina hiyo na kumshitaki Adriano ni kuleta utata kwenye Soka kwani hamna Sheria yeyote iliyovunjwa.
Mwenyewe Adriano amesema kuwa alishitukia mpira uko miguuni mwake na yeye kwa vile ni Straika alifunga Bao.
Mechi hiyo ilikuwa ni ya Kundi E la UEFA CHAMPIONZ LIGI.
++++++++++++++++++++++++++++++++
[MSIMAMO=Kila Timu imecheza Mechi 5]
KUNDI E
FC Nordsjælland 2 FC Shakhtar Donetsk 5
Juventus 3 Chelsea FC 0
MSIMAMO:
1 Shakhtar Donetsk Pointi 10
2 Juventus 9
3 Chelsea 7
4 Nordsjaelland 1 [NJE]
++++++++++++++++++++++++++++++++
 

Drogba aomba Kibali FIFA kuhama kwa Mkopo!


>>NJIANI kutua CHELSEA???
CHELSEA_ULAYA_2012AStraika wa zamani wa Chelsea Didier Drogba ameomba Kibali maalum kutoka FIFA ili aruhusiwe kuhama Klabu yake ya China, Shanghai Shenhua, na kwenda Klabu nyingine kwa Mkopo wakati huu ambapo Msimu wa Soka huko China umemalizika.
Imegusiwa kuwa nia ya Drogba, mwenye Miaka 34, ni kujiweka fiti wakati huu ili kujitayarisha kuichezea Nchi yake Ivory Coast kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 19 na kumalizika Februari 10, Mwaka 2013 na upo uvumi mkubwa atarudi Chelsea.
Kipindi cha Uhamisho kwa Wachezaji kimefungwa na kitafunguliwa rasmi hapo Januari Mosi lakini Drogba amewasilisha maombi ili apewe Kibali maalum.
++++++++++++++++++++++++
REKODI ya DROGBA na CHELSEA:
-MECHI ya KWANZA: Dhidi ya Manchester United, 15 Agosti 2004.
-GOLI la KWANZA: Dhidi ya Crystal Palace, 24 Agosti, 2004.
-MECHI: 342.
-MAGOLI: 157.
-MATAJI: LIGI KUU: 2004-05, 2005-06, 2009-10. FA Cup: 2006-07, 2008-09. 2009-10, 2011-12. KOMBE la LIGI: 2004-05, 2006-07. UAFA CHAMPIONZ LIGI: 2011-12.
-UFUNGAJI BORA LIGI KUU: 2007, 2010.
++++++++++++++++++++++++
Maombi haya ya Drogba yamethibitishwa kupokelewa na FIFA lakini hadi sasa haijulikani ni Klabu ipi atatua ingawa pia amehusishwa na Marseille Klabu ambayo aliihama Mwaka 2004 kujiunga na Chelsea.
Mechi ya mwisho Drogba kuichezea Chelsea ni Mwezi Mei kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo alifunga Penati iliyowapa Chelsea Ubingwa.
Akiwa na Shanghai Shenhua, Drogba amefunga Bao 8 katika Mechi 11.
 

USIKU wa EUROPA: Klabu zawania kuingia Mtoano toka Makundi!


>>WASHASONGA: Inter Milan, Rubin Kazan, Lyon, Bayer Leverkusen, Kharkiv & Hannover!
>>SPURS, NEWCASTLE & LIVERPOOL BADO KUJIJUA!!
EUROPA_LIGI_CUPTayari Timu 6 zishanyakua nafasi kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 na MECHI DEI 5, mzunguko wa 5 wa Mechi za Makundi, utafanyika Alhamisi Novemba 22 na Timu kadhaa zina nafasi kusonga kugombea nafasi zikibakiza Mechi moja mkononi.
Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI itaundwa na Timu 24 toka hatua ya Makundi ya EUROPA LIGI ambapo Timu mbili za juu toka kila Kundi zitafuzu na kujumuishwa na Timu 8 zitakazomaliza nafasi ya 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kufanya jumla ya Timu 32 ambazo zitafanyiwa Droo kupanga Mechi 16 za Mtoano zitakazochezwa kwa mtindo wa Nyumbani na Ugenini.
Kwenye Kundi A, Timu zote 4 zina nafasi ya kuendelea ingawa ushindi kwa FC Anzi Makhachkala, walio nyumbani wakicheza na Udinese, na Liverpool FC dhidi ya BSC Young Boys Uwanjani Anfield, utazifanya Timu hizo za nyumbani kusonga mbele.
Kundi B linaeleweka kwani Mabingwa watetezi Atletico Madrid na FC Viktoria Plzeň wanahitaji sare tu il wafuzu.
Kundi C, Fenerbahce wanahitaji sare tu wakicheza ugenini na Olympic Marseille ili wasonge mbele ingawa ushindi kwa Marseille na ule wa VfL Borussia Mönchengladbach, ambao wako nyumbani kucheza na Limassol ambao wameshaaga Mashindano, utalifanya Timu 3 za Kundi hili kujua hatima yao kwenye Mechi za mwisho.
Ikiwa Newcastle wataifunga Maritimo basi wataendelea toka Kundi D pamoja na Bordeaux ambao watapita wakishinda ugenini watakapocheza na Club Brugge.
Katika Kundi E, FC Steaua Bucureşti wanachungulia mafanikio na wanaweza kufuzu hata wakifungwa na Stuttgart ikiwa FC Copenhagen watashindwa kuifunga Molde.
Toka Kundi F, PSV Eindhoven wanajua ni lazima waifunge FC Dnipro Dniproptrovsk ili wajiweke hai kufuzu lakini FC Dnipro Dniproptrovsk wao wakipata ushindi wamesonga.
Kimbembe kipo Kundi G ambapo Timu zote 4 zinaweza kufuzu ingawa njia ni nyeupe kwa Genk ambao wakiifunga Videoton watafuzu.
Kundi H Timu mbili, Inter Milan na Rubin Kazan, tayari zimeshasonga mbele.
Katika Kundi I, ambalo Lyon wameshafuzu, sare katika Mechi ya Sparta Prague na Lyon itawatupa nje Athletic Bilbao na Hapoel Shmona.
Lazio watatwaa nafasi ya kwanza toka Kundi J ikiwa wataifunga Tottenham lakini Tottenham wanaweza kufuzu wakishinda na kisha Maribor wafungwe na Panthinaikos.
Levante watasonga toka Kundi L wakiifunga Helsingborgs IF.
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
KUNDI A
1 FC Anzhi Pointi 7
2 Liverpool 6
3 Young Boys 6
4 Udinese 4
KUNDI B
1 Viktoria Plzen Pointi 9
2 Atletico Madrid 9
3 Academica Coimbra 4
4 Hapoel Tel Aviv 1
KUNDI C
1 Fenerbahce Pointi 10
2 Olympic Marseille 5
3 Borussia Monchengladbach 5
4 Limassol 1
KUNDI D
1 Newcastle Pointi 8
2 Bordeaux 7
3 Club Brugge 4
4 Maritimo 2
KUNDI E
1 Steau Bucharest Pointi 10
2 Stuttgart 5
3 FC Copenhagen 4
4 Molde 3
KUNDI F
1 FC Dnipro Pointi 9
2 Napoli 6
3 PSV 4
4 AIK Solna 4
KUNDI G
1 Genk Pointi 8
2 Videoton 6
3 FC Basel 6
3 Sporting Lisbon 2
KUNDI H
1 Inter Milan Pointi 10 [IMEFUZU]
2 FC Rubin Kazan 10 [IMEFUZU]
3 Neftchi Baku 1
4 FK Partizan 1
KUNDI 1
1 Lyon Pointi 12 [IMEFUZU]
2 Sparta Prague 7
3 Hapoel 1
4 Athletic Bilbao 1
KUNDI J
1 Lazio Pointi 8
2 Tottenham 6
3 Maribor 4
4 Panathinaikos 2
KUNDI K
1 Bayer Leverkusen Pointi 10 [IMEFUZU]
2 Metalist Kharkiv 10 [IMEFUZU]
3 Rosenborg 3
4 Rapid Wien 0
KUNDI L
1 Hannover Pointi 10 [IMEFUZU]
2 Levante 7
3 FC Twente 3
4 Helsingborgs 1
RATIBA:
Alhamisi, Novemba 22
[SAA za BONGO]
20:00 FC Anzhi – Russia v Udinese - Italy
20:00 Neftchi Baku – Azerbaijan v FK Partizan - Serbia
20:00 FC Rubin Kazan – Russia v Internazionale - Italy
21:00 SS Lazio – Italy v Tottenham Hotspur - England
21:00 Hannover 96 – Germany v FC Twente Enschede - Netherlands
21:00 FC Basel 1893 – Switzerland v Sporting Lisbon - Portugal
21:00 Helsingborgs IF – Sweden v Levante - Spain
21:00 Videoton Szekesfehervar – Hungary v KRC Genk - Belgium
21:00 AC Sparta Prague - Czech Republic v Olympique Lyonnais - France
21:00 Rosenborg BK – Norway v SK Rapid Wien - Austria
21:00 Panathinaikos – Greece v NK Maribor - Slovenia
21:00 FC Metalist Kharkiv – Ukraine v Bayer 04 Leverkusen - Germany
21:00 Hapoel Ironi Kiryat Shmona – Israel v Athletic de Bilbao - Spain
23:05 Liverpool - England v BSC Young Boys - Switzerland
23:05 Newcastle United FC – England v Maritimo - Portugal
23:05 PSV Eindhoven – Netherlands v FC Dnipro Dnipropetrovsk - Ukraine
23:05 Atletico de Madrid – Spain v Hapoel Tel-Aviv FC - Israel
23:05 Borussia Mönchengladbach – Germany v AEL Limassol - Cyprus
23:05 Olympique de Marseille – France v Fenerbahçe - Turkey
23:05 Club Brugge KV – Belgium v FC Girondins de Bordeaux - France
23:05 AIK Solna - Sweden v Napoli - Italy        Råsunda Stadion
23:05 FC Steaua Bucuresti – Romania v  VfB Stuttgart - Germany
23:05 Molde FK - Norway  v FC Kobenhavn - Denmark
23:05 Academica Coimbra – Portugal v FC Viktoria Plzen - Czech Republic