Thursday, October 4, 2012

AARON RAMSEY KAMA KAWAIDA YAKE ANAPOFUNGA: JANA KATIA KAMBANI LEO WAZIRI MKUU WA SYRIA AFARIKI

*Mkosi wa Aaron Ramsey *

Kila mara mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey anapofunga goli, mtu anakufa siku inayofuata.

May 1, 2011 = Ramsey alifunga bao dhidi ya Man Utd.
OSAMA BIN LADEN akafa siku inayofuata

Oct 2, 2011 = Ramsey alifunga dhidi Spurs
STEVE JOBS muasisi na mmiliki wa kampuni ya Apple akafa siku iliyofuata.

Oct 19, 2011 = Ramsey akafunga dhidi ya Olympic Marsellie
MUNMMAR GADDAFI akafa siku iliyofauta.

Feb 11, 2012 = Ramsey akatia kambani dhidi Sunderland
WHITNEY HOUSTON akafariki siku iliyofuata.

Aug 4, 2012 = Ramsey akafunga dhidi ya South Korea
KIRK URSO akavuta siku ya pili yake.

Oct 3, 2012(Jana) = Ramsey alifunga dhidi ya Olympiakios
Waziri mkuu wa Syria amethibitishwa kuaga dunia leo hii.

MWINYI KAZIMOTO YUKO FITI 100%, ILIKUWA MISULI TU, SIMBA HAINA MAJERUHI, YACHEZA MECHI KINESI LEO

Mwinyi Kazimoto

KIUNGO Mwinyi Kazimoto Mwitula yupo fiti kabisa kuendelea kuitumikia Simba SC katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, licha ya jana kuumia katika mchezo dhidi ya wapinzani wa jadi, Yanga.
 
Daktari wa Simba SC, Cossmas Kapinga amesema  mida hii kwamba wachezaji wote wa Simba wapo fiti, bali kuna wachache wanaokabiliwa na uchovu wa kawaida wa mechi.
 
“Kazimoto ni misuli tu ilimshika jana, yuko fiti kabisa, hana maumivu, kwa kifupi sina majeruhi,”alisema Kapinga.
 
Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba wachezaji ambao hawakucheza mechi ya jana, leo watacheza mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Kinesi jioni.
 
“Kuna utaratibu ambao tunao ili kutunza viwango vya wachezaji wetu, siku moja baada ya mechi ya Ligi, wachezaji wote ambao hawakucheza, wanacheza mechi ya kirafiki, sasa leo pia kuna mechi hiyo jioni Uwanja wa Kinesi,”alisema Kamwaga.  
 
Simba jana ilishindwa kuendeleza ubabe wake kwa Yanga, baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wapinzani wao hao wa jadi, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuanzia saa 1:02 usiku.
 
Yanga ambao walimaliza mechi hiyo wakiwa pungufu baada ya Simon Msuva kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 77 kwa kumrudishia rafu Juma Nyosso, ndio waliohaha kusawazisha bao, baada ya kutanguliwa kwa bao la mapema la kiungo Amri Kiemba.  
 
Hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na kiungo Amri Kiemba dakika ya pili.
 
Simba walicheza vizuri kipindi chote cha kwanza wakigongeana pasi za uhakika na kuwazidi kasi uwanjani wapinzani wao, wakati Yanga pamoja na kuzinduka baada ya kufungwa bao, lakini makosa yalikuwa mengi.
 
Pasi zao zilikuwa nyingi hazifiki, walikuwa wanapokonyeka mipira kirahisi, wanazidiwa nguvu na wapinzani wao katika kugombea mipira na hata mashambulizi yao hayakuwa ya mpangilio, zaidi ya kuonekana kubahatisha zaidi.
 
Katika kubahatisha huko, Mbuyu Twite alifumua shuti zuri dakika ya 38 kutoka wingi ya kulia, ambalo lilitoka nje sentimita chache.    
 
Kabla hata ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika, kocha Mholanzi Ernie Brandts alimtoa Hamisi Kiiza na kumuingiza Frank Domayo ili kuimarisha safu ya kiungo, ambayo ilionekana kuzidiwa na Simba inayofundishwa na Mserbia, Milovan Cirkovick.
 
Kipindi cha pili, Yanga walianza na mabadiliko, kocha Ernie Brandts akimtoa kiungo Nizar Khalfan na kumuingiza mshambuliaji Didier Kavumbangu, ambaye alikwenda kuongeza nguvu ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
 
Angalau, kipindi cha pili Yanga walionekana kucheza vizuri na kupeleka mashambulizi yenye uhai langoni mwa Simba, ingawa safu imara ya ulinzi ya Wekundu wa Msimbazi ilikuwa kikwazo.
 
Katika dakika ya 63, beki Paul Ngalema aliunawa mpira katika harakati za kuokoa na refa Mathew Akrama akaamuru penalti, ambayo ilikwamisha kimiani kiufundi na Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
 
Katika dakika ya 77 Mathew Amkrama alimtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Simon Msuva, baada ya kumkita Juma Nyosso, aliyemkanyaga ‘kwa bahati mbaya’. 
 
Msuva alichezewa rafu na Nyosso na tayari refa alikwishapuliza filimbi na kumpa kadi ya njano beki huyo wa Simba, lakini kiungo huyo wa Yanga akaponzwa na hasira za kitoto.
 
Pamoja na Yanga kubaki pungufu, waliendelea kucheza vema na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili. Refa Akrama alishindwa kuumudu mchezo na maamuzi yake mengi yalikuwa chungu kwa Yanga, mfano Haruna Moshi ‘Boban’ alipomchezea rafu mbaya beki Kevin Yondan hadi akashindwa kuendelea na mchezo, na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Abdul alimpoza kwa kadi ya njano.
 
Hakumchukulia hatua yoyote kipa Juma Kaseja aliyeonekana kupoteza muda tangu mwanzo, na alimpa onyo tu zaidi ya mara tatu.
 
Alipingia Abdul alikwenda kucheza beki ya kulia na Mbuyu Twite akahamia katikati kucheza na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
 
Baada ya mchezo huo, kocha wa Simba, Milovan alisema kwamba ulikuwa mchezo mzuri na Yanga walicheza vizuri, lakini timu yake ilicheza vizuri na anajivunia. Alisema Yanga imeimarika tofauti na ilivyokuwa awali na kwamba hizo ni dalili Ligi Kuu msimu huu itakuwa ngumu.
 
Kwa upande wake, kocha wa Yanga, mwanzoni hawakucheza vizuri, lakini baadaye walitulia na kucheza vizuri. “Hii ni mechi ya kweli ya upinzani, unaweza kuona rafu na kadi nyingi,”alisema Brandts.
 
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 13, ndani ya mechi tano na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, wakati Yanga imefikisha pointi nane na kubaki nafasi ya tano, kwani Coastal Union imetoa sare ya 2-2 na JKT Oljoro mjini Arusha na kufikisha pointi tisa.   
 
SIMBA: Juma Kaseja, Nassor Chollo, Paul Ngalema, Juma Nyosso, Shomary Kapombe, Jonas Mkude/Haruna Moshi, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Edward Christopher/Daniel Akuffo na Mrisho Ngassa.
 
YANGA: Yaw Berko, Mbuyu Twite, Stefano Mwasyika, Nadir Cannavaro, Kevin Yondan/Juma Abdul, Athumani Iddi, Simon  Msuva, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza/Frank Domayo na Nizar Khalfan/Didier Kavumbangu.

MATUKIO MBALIMBALI SIMBA NA YANGA JANA TAIFA NDANI NA NJE YA UWANJA

Ally Mustafa 'Barthez' akisalimiana na Amri Kiemba baada ya mechi

Barthez na Chollo

Waghana; Yaw Berko na Daniel Akuffo wa Simba

Barthez na Kaseja

Kocha wa Yanga, Ernie Brandts

Simba wanapsaha

Yanga wanapasha

Msafiri Mgoyi kazini

Mashabiki wa Simba

Kiemba akipongezwa kwa bao la kuongoza

Simba wakishangilia bao la kutangulia

Bahanuzi anaweka mpira gambani mbele ya Kapombe, Paul Ngalema akiwa tayari kusaidia

Hapa Bahanuzi alimuumiza Kapombe, anatibiwa huku wachezaji wa Simba wakimlalamikia refa Akrama 

Hesabu za Kapombe kwenye mpira...kubali, kataa, dogo bonge la beki

Kapombe anamdhibiti Bahanuzi

Haruna anatafuta maarifa ya kumtoka Jonas Mkude

Cannavaro chupuchupu afunge kwa kichwa hapa

Paul Ngalema akimdhibiti Kiiza Diego

Niyonzima akimsema ovyo Nyosso baada ya kufanyiwa 'undavaku'

Nizar Khalfan kulia na Mrisho Ngassa kushoto

Mrisho anamkaba Mwasyika

Mashabiki wa Simba

Chollo anamdhibiti Bahanuzi

Kavumbangu anawashughulisha mabeki wa Simba..ameenda hewani kutoa pasi ya kichwa kwa Bahanuzi
Iddi Moshi akiingia na mwanawe Amran

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga katikati

Kocha Mkuu wa taifa Stars, Kim Poulsen kulia, katikati kocha wa timu za vijana, Jacob Michelsen na mpenzi wake kushoto 

Makamu Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Isaac Shekiondo

Wadau

Alex Mgongolwa kushoto akiwa na Mohamed Bhinda
Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' kulia akiwa na beki na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo
Alikuwa anaangalia mpira nyuma ya lango la Simba
Simba wanaingia

Friends Of Simba 'wanakaba'

Friends Of Simba 
Yanga wanapasha
Vigogo wa Simba

BOBAN AOMBA RADHI KWA RAFU YA YONDAN

Ilikuwa bahati mbaya, kijana ameomba radhi

KIUNGO wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ amewaomba radhi wapenzi wa soka Tanzania kwa kitendo chake cha kumchezea rafu mbaya mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kevin Yonda jana. 
 
Akizungumza  leo, Boban alisema kwamba wengi wanaweza kudhani alikusudia, lakini ukweli hadi anafika kwa Yondan hakuwa na dhamira ile. 
 
“Nia yangu ilikuwa kuukita mpira, lakini Yondan naye fundi, akautuliza ukahama, na mimi wakati huo nishauinua mguu wangu ndio unatua sasa, ukatua kwenye mguu wake.
 
Binafsi iliniumiza sana na kama utaona kuanzia pale sikucheza vizuri kabisa, sikuwa na raha kabisa. 
 
Yondan ni rafiki yangu sana, nimempokea Simba, nimeondoka nimemuacha, nimerudi, amenipokea, tumeishi vizuri, kwa kweli inaniumiza sana,”alisema Boban.
Aidha, Boban alisema kwamba atakwenda kumjulia hali Yondan na kumuomba msamaha. “Nawaomba msamaha zaidi mashabiki wa Yanga, mimi ni binadamu, wanisamahe,”alisema Boban.    
 
Yondan atakuwa nje kwa wiki mbili, kutokana na kuumizwa na kiungo huyo wa Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Daktari wa Yanga, Sufiani Juma amesema kwamba beki huyo tegemeo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, tangu jana alikuwa anasikia maumivu makali na baada ya kufanyiwa vipimo katika Kitengo cha Mifupa cha Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili (MOI), imeelezwa anatakiwa kupumzika wiki mbili.
 
Lakini Yondan pia anaweza kukaa nje ya Uwanja kwa zaidi ya muda, huo kwani majibu hayo yanatokana na uchunguzi wa awali.
 
Yondan aliumizwa jana wakati Yanga ikitoka nyuma na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wapinzani wao wa jadi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuanzia saa 1:02 usiku.
 
Yanga ambao walimaliza mechi hiyo wakiwa pungufu baada ya Simon Msuva kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 77 kwa kumrudishia rafu Juma Nyosso, ndio waliohaha kusawazisha bao, baada ya kutanguliwa kwa bao la mapema la kiungo Amri Kiemba.  
 
Hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na kiungo Amri Kiemba dakika ya pili, wakati Yanga ilisawazisha dakika ya 63, baada ya beki Paul Ngalema kuunawa mpira katika harakati za kuokoa na refa Mathew Akrama akaamuru penalti, ambayo ilikwamisha kimiani kiufundi na Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
 
Katika dakika ya 77 Mathew Amkrama alimtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja Simon Msuva, baada ya kumkita Juma Nyosso, aliyemkanyaga ‘kwa bahati mbaya’. Msuva alichezewa rafu na Nyosso na tayari refa alikwishapuliza filimbi na kumpa kadi ya njano beki huyo wa Simba, lakini kiungo huyo wa Yanga akaponzwa na hasira za kitoto.

SIMBA, YANGA YAINGIZA MILIONI 400 KASORO KIDOGO, KLABU ZAPEWA KARIBU NUSU YA MAPATO YOTE

Juma Kaseja akidaka katika mechi ya jana

MECHI ya watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.
 
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo amesema mida hii kwamba, watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.
 
Amesema mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
 
Amesema umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.
 
Wakati huo huo, Wambura amesema mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.
 
Amesema mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2

SIMBA B MABINGWA WA KOMBE LA BANC ABC CHUPUCHUPU KWA YANGA B TAIFA

Yanga B imeshindwa kuwatilia baraka kaka zao, kuelekea mchezo wa jioni, baada ya kuwaruhusu mabingwa wa Kombe la BancABC Sup8R, Simba B, inayofundishwa na Suleiman Matola, akisaidiwa na Amri Said kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2. Mabao ya Yanga B inayofundishwa na kocha wake, Salvatory Edward akisaidiwa na Abubakar Salum yamefungwa na Kelvin Nkini kipindei cha kwanza na Notikel Masasi kipindi cha pili, wakati ya Simba yalifungwa na dakika za lala salama. 

BAHANUZI AIOKOA YANGA PUNGUFU KULALA KWA SIMBA

DAKIKA 90

Bahanuzi anafunga penalti

Refa Mathwe Akrama aliyeshika mpira na wasaidizi wake baada ya mechi

Ngassa akiomba dua

Akrama akitoa kadi nyekundu

Bahanuzi akishangilia baada ya kufunga lla kusawazisha

Bahanuzi akipongezwa

Kaseja akiokoa moja ya hatari

Berko

Boban naAkuffo wakimpongeza Kiemba

11 wa Yanga walioanza

11 wa Simba walioanza

YANGA imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wapinzani wao wa jadi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuanzia saa 1:02 usiku.