Thursday, January 3, 2013

YANGA KUCHEZA NA TIMU YA DARAJA LA PILI UJERUMANI KESHO


Yanga mazoezini Uturuki jana
KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam, kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na Arminia Bielefeld ya Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya, Uturuki.
Yanga ambayo imeweka kambi ya mafunzo mjini Antalya, itatumia mchezo huo kama fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani ambayo pia imekuja kuweka kambi ya mafunzo kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Pili Ujerumani.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo ina wachezaji wa kiwango cha kimataifa, hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
“Unajua tuna siku sita tangu tufike hapa (Antalya Uturuki) na tumeshafanya mazoezi kwa siku nne, hivyo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu,” alisema Brandts.
Arminia Bielefeld  imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na timu ya Yanga ambao ni mabingwa mara 23 Tanzania Bara.
Jana asubuhi Yanga imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna majeruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.

BABBI KUKIMBIA BENCHI AZAM, HUENDA AKAREJEA MTIBWA


Abdi Kassim
ABDI Kassim Sadallah ‘Babbi’ au Ballack wa Unguja yuko mbioni kuihama klabu ya Azam FC na kurejea na Mtibwa Sugar ya Morogoro, kutokana na kushindwa kuvumilia kuwekwa benchi chini ya kocha Muingereza, Stewart Hall.
  Babbi tayari yupo kwenye mazungumzo na Mtibwa Sugar, klabu yake ya kwanza kuchezea Tanzania Bara, ambayo imeonyesha nia ya kumpokea tena.
Babbi amekuwa akilalamika kwa watu wake wa karibu kwamba, wakati wa kocha Mserbia Boris Bunjak alikuwa anapangwa Azam na kufanya vizuri kiasi cha kuisaidia sana timu, lakini baada ya kurejea Stewart amekuwa mtu wa benchi.
Babbi amekuwa akisema Azam ilipokuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwezi uliopita kwenye Kombe la Hisani, alipangwa katika mechi mbili za mwanzo ambazo Stewart alibaki Kenya kwa kukosa viza ya kuingia Kinshasa.
Amekuwa akilalamika kwamba pamoja na kucheza vizuri katika mechi hizo, maisha yalibadilika ghafla baada ya Stewart kutua Kinshasa, kwani kuanzia hapo hakumbuki kama alivaa tena hata jezi ya Azam hadi mashindano yanaisha.
Habari zaidi zinasema, tayari Babbi amekwishawaeleza nia yake ya kuondoka baadhi ya viongozi wa Azam, ambao wameonekana kukosa namna ya kumzuia, kwa sababu nao wanaona ana sababu ya kufikia uamuzi huo, kunusuru kiwango chake.   
Azam ipo visiwani hapa kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi, lakini katika mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union alikuwa sehemu ya watazamaji jukwaani.

STEWART AKIRI SELEMBE NOMA, LAKINI ASEMA HANA NAFASI AZAM


Selemba katika mechi ya jana, cheki kitu alichomfanya Khamis Mcha 'Vialli'
KOCHA wa Azam FC ya Dar es Salaam, Muingereza Stewart Hall amesifia kiwango cha kiungo wa zamani wa timu yake, Suleiman Kassim ‘Selembe’ ambaye kwa sasa anachezea Coastal Union ya Tanga kwamba kimepanda.
Pamoja na kusifia kiwango cha mchezaji huyo, Hall amesema kiungo hana nafasi Azam, kwa kuwa sasa ina wachezaji bora zaidi yake kama Kipre Herman Tchetche kutoka Ivory Coast na Brian Umony kutoka Uganda.
“Kweli ameimarika tofauti na alivyokuwa Azam, lakini sijutii kwa sababu kikosini nina wachezaji wazuri kama Kipre Tchetche na Umony, nitamkumbuka Selembe?”alisema.
Azam FC na Coastal Union jana zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Coastal leo ndio waliotawala mchezo na kupoteza nafasi kama tatu za wazi za kufunga mabao, kutokana na umakini mdogo kila walipopata nafasi hizo.
Azam walipata nafasi moja nzuri kipindi cha pili, lakini walinzi wa Coastal walisimama imara na kuondosha kwenye hatari jaribio hilo.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar, Humphrey Mieno, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche/Brian Umony dk 24 na Hamisi Mcha ‘Vialli’/Seif Abdallah dk 66. 
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Hussein Twaha dk 50, Jerry Santo, Mohamed Mtindi, Soud Othman/Razack Khalfan dk90 na Danny Lyanga/Joseph Mahundi dk 90. 
Katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Miembeni iliitandika mabao 4-1 Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa mao Dze Tung.
Mabao ya Miembeni yalitiwa kimiani Adeyum Saleh Ahmed dakika ya 41 na 72, Mohamed Hamdani na Rashid Roshwa dakiaka ya 74, wakati la Mtibwa la kufutia machozi lilifungwa na Juma Mpakala dakika ya 10.

KIGGI MAISHA MAGUMU SIMBA SC


KIGGI Makassy hafurahii maisha Simba SC na lolote linaweza kutokea juu yake wakati wowote.
Kiungo huyo aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu kutoka mahasimu Yanga, amekutana na kile amabcho alikimbia timu yake ya zamani, benchi mfululizo.
Katika mchezo wa juzi wa Kombe la Mapinduzi visiwani hapa, Kiggi alionyesha dhahiri kuchukizwa na kitendo cha kutolewa dakika ya 27 nafasi yake ikichukuliwa na Edward Christopher.
Akitoka kupiga maridadi iliyounganishwa nyavuni na Haruna Chanongo, Kiggi aliitwa benchi kumpisha Edward na alionekana kutoka kwa huzuni na alipofika benchi alikataa hata kupokea chupa ya maji aliyopewa.
Habari zaidi zinasema, tayari Kiggi amekwishaanza mishemishe za kusaka timu nyingine ya kwenda kuchezea baada ya kuona yupo katika wakati mgumu Simba SC.   
Simba SC leo inashuka tena dimbani kumenyana Tusker ya Kenya katika mchezo wa pili wa Kundi A, baada ya kushinda 4-2 dhidi ya Jamhuri ya Pemba juzi. Je, Kiggi atapangwa? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

RIDHIWANI, AZZAN WAMLILIA SAJUKI




  Msanii mkongwe katika tasnia ya muziki wa Dansi na Rhumba Kikumba Mwanza Mpango almaarufu kama King Kiki akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar leo.
Mzee King Kiki akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka (katikati) nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini Dar leo. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce Fisso
Wasanii mbalimbali na wakiendelea kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam. Pichani ni Msanii wa muziki Dokii (kushoto) sambamba na Mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa Mwisho Mwampamba na wasanii wengine.
Mchekeshaji maarufu wa The comedy Masanja Mkandamizi akijifuta jasho kwa mbali akielekea msibani nyumbani kwa Marehemu Sajuki. Masanja alikuwa ni mmoja wa wahamishaji katika kuchangia pesa za matibabu ya marehemu Sajuki kwenda nchini India kupitia kipindi cha Luninga cha The Comedy kinachorushwa na Televisheni ya TBC.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye huzuni kutafakari kifo cha Sajuki.
VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWASILI: Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la  Kinondoni Mh.Iddi Azzan wakipokelewa na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba na wasanii wengine wa filamu baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani msiba huo.
Mkuu wa Itifaki Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimuongoza Mh.Makongoro Mahanga sehemu maalum kwa ajili ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitia saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki.
Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan naye aliangusha saini kwenye kitabu hicho.
Mzee King Kiki akizungumza jambo na Waheshimiwa Wabunge kwenye msiba wa Sajuki Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo.
Waheshimiwa wakielekea nyumba ya jirani walikokusanyika baadhi ya waombolezaji na wasanii wa filamu nchini kwa ajili ya kuzungumza machache na kutoa Ubani.
Katibu wa Fedha msibani hapo mchekeshaji maarufu Steve Nyerere akiwakaribisha waheshimiwa wabunge kuzungumza na hadhira ya waombolezaji (hawapo pichani).
Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga akitoa salamu zake  za rambimbi na kuahidi kuchangia shilingi 200,000/= kwa ajili ya kufanikisha shughuli za mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Sajuki atakayezikwa Kesho Ijumaa katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzani akielezea kwa majonzi alivyopokea taarifa za msiba wa Sajuki na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na Wastara panapomajaliwa ya Mola katika malezi ya mtoto aliyeachwa na marehemu na kuwaasa wadau, ndugu, jamaa na marafiki kumsaidia Wastara kutokana na hali yake na amechangia kiasi cha Shilingi 500,ooo/= kufanikisha shughuli za mazishi ya marehemu Sajuki.
Pichani Juu na Chini ni Umati wa waombolezaji ukisikiliza nasaha za waheshimiwa Wabunge (hawapo pichani) walipofika nyumbani kwa marehemu Sajuki kuhani msiba huo.
Kazi ya kuosha vyombo si kina Dada tu, hata kina Kaka wanaweza pia....Pichani ni baadhi ya Watangazaji wa Clouds Radio wakiongozwa na Dina Marios kushiriki kuosha vyombo vilivyotumika katika msiba huo huku wakisaidiana na waombolezaji wengine.
Mganga wa Jadi anayefahamika kwa jina la Dokta Manyaunyau (kushoto) sambamba na Msanii wa filamu nchini Cloud wakisikiliza mawaidha ya waheshimiwa wabunge (hawapo pichani).
Mkuu wa Itifaki msibani hapo Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimpokea  Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete alipowasili nyumbani kwa marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa pole baada ya kusaili kwa baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Sajuki msibani hapo.
Bw. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko nyumbani kwa marehemu Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki leo.
Bw. Ridhiwani Kikwete akimpa maneno ya faraja Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko.
Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa mkono wa pole kwa mke wa marehemu Sajuki Bi. Wastara (mwenye buibui).
Bw. Ridhiwani Kikwete akimfariji mama mzazi wa Marehemu Sajuki alipofika nyumbani hapo kuhani msiba huo.
Katibu wa fedha msibani hapo Steve Nyerere akitetea jambo na Bw. Ridhiwani Kikwete.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Bw. Ridhiwani Kikwete kuzungumza machache na waombolezaji.
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akizungumzia marehemu Sajuki na kuwataka wanawake kuiga mfano wa Maisha ya Sajuki na Wastara jinsi walivyokuwa wakiishi na Upendo mpaka Umauti ulipomkuta marehemu Sajuki na kuwasisitiza kuenzi yale yote mema aliyokuwa akifanya kipindi cha uhai wake na kuwamasisha Umoja na Mshikamano baina yao.
Bw. Ridhiwani Kikwete naye alichangia Shilingi 500,000/=  kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu Sajuki anayetarajiwa kuzikwa Kesho Ijumaa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani).
Marehemu Sajuki alikuwa kipenzi cha watoto na wakubwa pia. Pichani ni Umati wa watoto wanaokaa jirani na Nyumba ya Marehemu Sajuki wakiwa wamekusanyika huku wakionyesha majonzi na simanzi tele

WANACHAMA SIMBA NA YANGA WAHIMIZWA KULIPIA ADA ZAO KUTUMIA M-PESA



Taarifa kwa vyombo vya habari
Wanachama Yanga, Simba waaswa kulipia ada  kupitia M-pesa.
Dar es Salaam (3 January 2013) –Kutokana na kukua kwa kasi kwa maendeleo ya teknolojia katika sekta ya soka nchini –klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara zimeaswa kuwahamasisha wanachama wa klabu hizo kulipia ada ya uanachama kupitia huduma ya M -Pesa.
Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, alisema kuwa hali hiyo itasaidia kuepusha ubebaji wa fedha taslimu mbali na hivyo, pia zoezi hilo liitapunguza upotevu wa muda wa wanachama kutoka sehemu moja hadi nyingine na kwenda klabuni kulipia ada ya uanachama.
“Iwapo vilabu vya soka nchini vitawaahamasisha wanachama wake kutumia huduma ya M-Pesa  kulipia ada ya uanachama wataweza kuoka muda wa kwenda klabuni, wataokoa gharama na pia kutakuwa na usalama wa fedha zao,” Bw. Twissa alisema.
Aidha, Bw. Twissa aliongeza kuwa kutokana na utumiaji wa malipo kwa huduma ya M-Pesa –mapato ya vilabu pia yatakuwa salama.
Hivi karibuni mhasibu wa klabu ya soka ya Simba, alivamiwa na kuporwa fedha za mapato ya klabu hiyo zilizotokana na mgawo wao wa mechi ya kirafiki kati ya klabu hiyo na klabu ya Tusker ya Kenya.
Bw. Twissa, anaamini kuwa kwa kuanzishwa kwa huduma hiyo ya ulipaji wa ada ya uanachama kwa vilabu kwa kupitia huduma ya M-Pesa itasadia kuchochea ongezeko la idadi ya wanachama kwenye vilabu hivyo pamoja na uhai wa wanachama hao.
“Huduma hii ya M-Pesa nina imani itakapoanza itasaidia kuongeza idadi ya wanachama wapya kwenye vilabu na hata kuongeza mapato ya vilabu. Kuna wanachama wengine ambao wanashughuli nyingi ambapo kwao kupata ule muda wa kufanya mambo kama hayo ni nadra sana lakini pia kuna wengine wao wanapata uvivu wa kwenda kulipia ada hiyo,” alisema.
Huduma ya M-Pesa nchini imekuwa ikikuawa kwa kasi ambapo imeweza kurahisisha maisha ya wananchi kwa ujumla kwa kupata mahitaji ya kila siku ya binadamu. Hivi karibuni, Vodacom Tanzania imeingia mikataba na Shoppers Supermarket kwenye maeneo ya Msasani na Masaki.

AZAM, COASTAL HAKUNA MBABE MAPINDUZI


Beki wa Coastal Union akiupitia mpira kwenye miguu ya mshambuliaji wa Azam, Seif Abdallah usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi. timu hizo zilitoka 0-0.

AZAM FC na Coastal Union ya Tanga zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa.
Coastal leo ndio waliotawala mchezo na kupoteza nafasi kama tatu za wazi za kufunga mabao, kutokana na umakini mdogo kila walipopata nafasi hizo.
Azam walipata nafasi moja nzuri kipindi cha pili, lakini walinzi wa Coastal walisimama imara na kuondosha kwenye hatari jaribio hilo.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar, Humphrey Mieno, Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche/Brian Umony dk 24 na Hamisi Mcha ‘Vialli’/Seif Abdallah dk 66. 
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Hussein Twaha dk 50, Jerry Santo, Mohamed Mtindi, Soud Othman/Razack Khalfan dk90 na Danny Lyanga/Joseph Mahundi dk 90. 
Katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, Miembeni iliitandika mabao 4-1 Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa mao Dze Tung.
Mabao ya Miembeni yalitiwa kimiani Adeyum Saleh Ahmed dakika ya 41 na 72, Mohamed Hamdani na Rashid Roshwa dakiaka ya 74, wakati la Mtibwa la kufutia machozi lilifungwa na Juma Mpakala dakika ya 10. 


Kiungo wa Coastal Union ya Tanga, Jerry Santo akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Azam FC ya Dar es Salaam, Salum Abubakar katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku huu. Timu hizo zilitoka 0-0.

Hatari langoni mwa Coastal

Suleiman Kassim 'Selembe' akimuacha chini Khamis Mcha 'Vialli'

Kipre Balou akiuwahi mpira mrefi dhidi ya Jerry Santo wa Coastal

Himid Mao wa Azam na Mohamed Mtindi wa Coastal Union wakigombea mpira

Himid Mao na Salum Abubakar wakishirikiana kumpokonya mpira mchezaji wa Coastal

Suleiman Kassim 'Selembe' akimtoka kiungo wa Azam, Khamis Mcha 'Vialli'

Juma Mpongo amedaka mbele ya mshambuliaji wa Azam, Gaudence Mwaikimba 

Brian Umony wa Azam akiwa amemuangukia mchezaji wa Coastal

Hamisi Shengo wa Coastal Union, akitafuta mbinu za kumtoka Humphrey Mieno wa Coastal Union 

Hamisi Shengo wa Coastal Union, akitafuta mbinu za kumpokonya mpira Humphrey Mieno wa Azam 


Kikosi cha Azam leo

Manahodha Jerry Santo wa Coastal Union na Himid Mao wa Azam FC kulia

Kikosi cha Coastal Union leo

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Bihindi Hamad Khamis akisalimiana na kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar kabla ya mechi ya Kundi B ya Kombe la Mapinduzi kati yao na Coastal Union kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Rais wa ZFA, Aman Ibrahim Makungu akisalimiana na beki wa Azam FC, Joackins Atudo kabla ya mechi ya Kundi B ya Kombe la Mapinduzi kati yao na Coastal Union kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar