Sunday, January 20, 2013

MCHAKATO TIKETI ZA ELEKTRONIKI WAFIKIA ASILIMIA 80



Mashabiki Uwanja wa Taifa 

UJENZI wa vifaa (turnstiles) vitakavyotumika kwa ajili ya tiketi za elektroniki kwenye viwanja saba kati ya nane vitakavyotumia mfumo huo umekamilika kwa asilimia 80.
Viwanja hivyo ni Chamazi (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Sokoine (Mbeya), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), na Mkwakwani (Tanga).
Wakati Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tayari una turnstiles, Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza bado haujaruhusu ufungaji wa vifaa ukisubiri idhini kutoka kwa wamiliki wake (CCM Makao Makuu).
Vifaa vitakavyotumika kusoma tiketi za elektroniki katika viwanja hivyo vinatarajiwa kuwa vimefungwa kufikia Februari 20 mwaka huu.
Hakutakuwa na matumizi ya fedha taslimu mara baada ya mradi huo wa tiketi la elektroniki kuanza, kwani tiketi zitakuwa zikinunuliwa kwa kadi maalumu (smart card) katika vituo mbalimbali vitakavyotangazwa baadaye.
Benki ya CRDB ndiyo iliyoingia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutengeneza tiketi za elektroniki baada ya kuibuka mshindi kwenye tenda.

No comments:

Post a Comment