Friday, January 11, 2013

KATIKA NDONDOO MICHEZO BARANI ULAYA NI KUHUSIANA NA JOHN TERRY JT ANATARAJIA KURUDI MZIGONI BAADA YA KUPONA GOTI

John Terry

Nahodha wa chelsea  John Terry  anatarajia kurudi mzigoni katika mechi ya 21 ya ligi nchini England baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani  miezi 2 akijiuguza mguu wake  alioumia goti siku ya mchezo dhidi ya liverpool .Mchezo ambao alilazimika kucheza dakika 45 za kipindi cha kwanza na kutolewa nje alipoumia.Terry 32 anatarajia kuwepo katika mchezo wa kesho dhidi ya stoke city ,,,,amesema kocha mkuu wa timu hiyo Rafael Benitez, 

 THEO WALCOT ANAWEZA KUSAINI MKATABA MPYA

Theo Walcott

Boss wa Arsenal  Arsene Wenger  anaamini mshambuliaji wake raia wa englands Theo Walcott  atasaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo ndani ya tarehe hizi za mwezi  31 January.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka  23 ameshabakisha miezi 6 amalize mkataba wake na anaweza kuondoka bure kama hatasaini mkataba mwingine.

MFUNGAJI BORA WA ARSENAL MPAKA SASA

Premier League League Cup Europe Total
Theo Walcott 8 5 1 14
Olivier Giroud 6 2 1 9
Lukas Podolski 6 0 3 9
Santi Cazorla 7 0 0 7
Gervinho 3 0 2 5

ROONEY ANAWEZA KURUDI DIMBANI KATIKA KOMBE LA FA CUP


 
Wayne Rooney  anaweza akawa fiti kuichezea klabu yake ya r Manchester United's katika kombe la  FA Cup  dhidi ya klabu ya  West Ham siku ya jumatano hayo yamesemwa na kocha mkuu wa klabu hiyo    Sir Alex Ferguson.Rooney aliumia siku ya boxing day ya tarehe 26 dec 2012 katika mchezo dhidi ya Newcastle.


 

Fabricio Coloccini ATAKA ARUDI NCHINI ARGENTINA


Newcastle captain Fabricio Coloccini
Newcastle United captain Fabricio Coloccini amesema na kuiambia klabu yake kuwa anataka mwezi huu ndani yake apewe ruhusa ya kuhamia nchini Argentina.Mchezaji huyo wa miaka 30 amesema hafurahii na maisha ya nchini England na katika klabu yake hiyo.


Nahodha huyo wa newcastle alisajiliw akutoka klabu ya
Deportivo kwa  £10.3m in 2008  na alisaini miaka 4 kuitumikia newcastle

Van Persie mchezaji bora wa mwezi disemba wa Premier League na Shakhtar yaizidi kete Chelsea yamsajili Taison wa Metalist..

MESSI NDIYE GOLDENBALLS MPYA BAADA YA KUMSHINDA DAVID BECKHAM SASA KUVAA VIATU MAALUM KUTOKA ADIDA DHIDI YA MALAGA KUSHEHEREKEA MAFANIKIO YAKE.

Lionel Messi shows off his four Ballon D'Or trophies


Boot-iful: The specially-designed Adidas F50s Messi will wear against Malaga on Sunday
`Boot-iful: The specially-designed Adidas F50s Messi will wear against Malaga on Sunday
Viatu maalum ambavyo vimetengenezwa na kampuni ya Adidas aina ya F50s ambavyo Messi atavaa katika mchezo dhidi ya Malaga jumapili.

Baada ya kumshinda David Beckham kwa tuzo za mipira ya dhahabu Lionel Mess atakuwa akivaa viatu maalum kusherekea mafanikio yake. 

Kwa miaka mingi David Beckham ndiye mchezaji aliyekuwa amekusanya tuzo nyingi zaidi kuliko mchezaji yoyote duniani lakini sasa amejitokeza mshindani mpya Messi.

 Golden Balls! Lionel Messi poses with his four Ballon D'Or trophies after winning the World Player accolade for a fourth straight year this week
Golden Balls! Lionel Messi akiwa pamoja na tuzo zake nne za Ballon D'Or 

Lionel Messi shows off his four Ballon D'Or trophies



Boot-iful: The specially-designed Adidas F50s Messi will wear against Malaga on Sunday
Viatu maalum ambavyo vimetengenezwa na kampuni ya Adidas aina ya F50s ambavyo Messi atavaa katika mchezo dhidi ya Malaga jumapili.

TFF YAAHIDI KUWASAFIRISHA WACHEZAJI 6 WA SIMBA AMBAO WAPO TIMU YA TAIFA WAKATI JANA ILIONDOKA NA WACHEZAJI WANANE KWENDA OMAN ,,JE HUU NI MFUMO GANI KW ATIMU ZETU HIZI KONGWE?????


Wachezaji sita wa klabu ya simba walioko katika kambi ya timu ya taifa Kili taifa Stars ambayo inajiandaa na mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Ethiopia mjini Addis Ababa watasafirishwa na shirikisho la soka nchini TFF kuelekea Oman kuungana na wenzao ambao wanatarajiwa kuanza kambi yao ya wiki mbili nchini humo.
 Akiongea na waandishi wa habari afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Bonface Wambura amesema shirikisho lake litagharamia usafiri wa wachezaji hao kuelekea Oman mara baada ya mchezo wa Stars dhidi ya Ethiopia na kwamba hayo ni makubaliano baina ya pande mbili hizo.

Wambura amesema kimsingi TFF inatambua safari ya Simba kuelekea nchini Oman kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya timu yao kwa ajili ya mashindano mbalimbali ikiwemo ligi kuu ya soka Tanzania bara pamoja na klabu bingwa Afrika hivyo wamekubaliana kuwasafirisha wachezaji hao kuelekea Oman.

Amesema ingawa kambi ya timu ya taifa itakuwa ikiendelea jijini Dar es Salaam mara baada ya mchezo wa Kili taifa stars na Ethiopia, bado TFF italazimika kuyaheshimu makubaliana hayo.

Amesema kama walivyofanya kwa wachezaji wa Yanga ambao TFF iliwatumia tiketi wachezaji Kelvin Yondan na Frank Domayo, ndivyo watakavyofanya kwa wachezaji wa Simba mara baada ya mchezo huo na kwamba wachezaji hao hawatarejea Dar es Salaam wataelekea moja kwa moja Oman kuungana na kambi ya timu yao ya Simba ambayo inatarajia kuanza hapo kesho.
Baadhi ya wachezaji wa Simba waliko katika kikosi cha Stars kutoka kushoto ni Amir Maftaha, Mwinyi Kazimoto na Amri Kiemba.
 Wachezaji wa Simba walio katika kikosi cha timu ya taifa ni pamoja na nahodha Juma Kaseja, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Amir Maftaha, Shomari Kapombe na Mwinyi Kazimoto. 
Simba inatarajia kuelekea nchini Oman hii leo kwa maandalizi ya ligi kuu ya soka Tanzania bara pamoja na mchezo wa mzunguko wa kwanza wa michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Recreative de Libobo ya Angola ambao kwa mujibu wa ratiba ya shirikisho la soka barani Afrika mchezo huo utachezwa kati ya Februari 17 na 19.WAKATI HUO HUO
 
Jumla ya wachezaji 8 wa timu ya Simba jana waliondoka iliondoka nchini kwenda kuweka kambi Oman kwa ajili ya mandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara huku wachezaji wake watatu wakishindwa kuondoka kutokana na kukosa visa.

Wachezaji walikosa visa ni Paul Ngalema, Abdallah Juma na Keita, hivyo watawasubiri waondoke januari 13 mwaka huu na wenzao waliobaki na timu Zanzibar.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Bara wameondoka saa tisa ikiwa na wachezaji nane na benchi la ufundi lenye watu wanne.

Waliondoka ni kocha mkuu Mfanransa Leiwing, Kocha msaidizi Basena, Daktari wa timu Cosmas Kapinga na Mtunza vifaa, Kessy.

Wachezaji waliondoka ni mlinda mlango Dhaira, Felex Sunzu, Kigi Makasy, Nassor Masoud "Cholo", Shamte Ally, Ramadhan Chombo na Salum Kinje. 


CHELSEA KWANUKA MASHABIKI CHELSEA KUGOMEA MECHI KUMPINGA BENITEZ??

BENITEZ-CHELSEABAADHI ya MASHABIKI wa Chelsea wameamua kugomea Mechi za Klabu hiyo hadi Meneja wao, Rafael Benitez, atakapoondolewa.
Mara baada ya kupigwa 2-0 na Swansea City Uwanjani Stamford Bridge Jumatano Usiku katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP, hasira zilipamba moto miongoni mwa Mashabiki na Kiongozi wa Kundi rasmi la Mashabiki wa Chelsea, Chelsea Supporters’ Group, aitwae Trizia Fiorellino, alitamka: “Tupo kwenye hali ya machafuko na ipo hatari Klabu itapoteza Roho yake. Najua wapo Mashabiki wasiotaka kuiangalia Chelsea hadi Benitez aondoke. Na kwa uzoefu wangu Mashabiki wanaosusa kuitazama Klabu hawarudi tena!”
Mara baada ya kipigo cha Swansea, Mashabiki walimshushia matusi Mwenyekiti wa Chelsea, Bruce Buck, huku wakiimba na kutaja Majina ya Mameneja waliopita wa Chelsea, Jose Mourinho na Roberto Di Matteo.
Fiorellino alisema: ‘Kuzomewa kwa Bruce Buck kuliungwa mkono na kila mmoja. Tunashukuru kwa yote anayofanya Roman Abramovich kwa Klabu hii lakini kumleta Benitez si sawa kwa Chelsea. Ameletwa ili ‘kumfufua’ Fernando Torres lakini sasa mambo yanazidi kuwa mabovu. Mashabiki wengi hawana imani tena na mwendo wa Klabu na hili linaibomoa Klabu.”
Vile vile, Mashabiki hao wamekasirishwa na jinsi Klabu inavyomtendea Kiungo Nguli Frank Lampard ambae ameshaambiwa hatapewa Mkataba mpya na yuko huru kuondoka.
Fiorellino amesema: “Uamuzi huo hauungwi mkono na sasa John Terry atafuatia!”
Mmiliki Abramovich, ambae yuko Vakesheni huko Visiwa vya Caribbean, ameshajulishwa kuhusu hasira za Mashabiki mara baada ya kufungwa na Swansea City.

WARATIBU WA MASHINDANO YA DAKARA WASEMA WAWILI WAFA DAKAR RALLY.


WARATIBU wa mashindano ya Dakar Rally wamesema kuwa watu wawili wamekufa na wengine saba wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika mashindano hayo karibu na mpaka wa Peru na Chile. Ajali hiyo ilitokea wakati ambapo gari moja ya mashindano ilipoligonga gari la kutoa msaada wakati gari nyingine ilipinduka wakati dereva wake akijaribu kukwepa magari hayo yaliyogongana. Tukio hilo lilipekea watu wawili katika gari ndogo ya kwanza akiwemo dereva na msaidizi wake kufa na saba wengine wanne wakiwa raia wa Peru na watatu Waingereza waliokuwepo katika gari ya kutoa msaada waliumia. Waingereza waliojeruhiwa ambao walikuwa katika Land Rover ya kutoa msaada walikuwa wanatoka timu ya Race2Recovery ambao shughuli yao kubwa ni kutoa msaada kwa madereva wanaopata matatizo njiani. Kiongozi wa Race2Recovery, Tony Harris alituma salamu za rambirambi kwa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo mbaya na kusema majeruhi walichukuliwa na kusafirishwa na helikopta kwa ajili ya kwenda kupatiwa matibabu zaidi. Mpaka sasa watu wapatao 59 wakiwemo mashabiki 20 wamepoteza maisha katika mbio za Dakar Rally katika miaka ya karibuni lakini waratibu wa mashindano hayo wamekuwa wagumu kuongesha tahadhari za usalama katika mashindano hayo.

AUSTRALIA OPEN DRAW: DJOKOVIC, MURRAY KUKUTANA FAINALI KAMA WAKIFANIKIWA KUFIKA HUKO.


MCHEZAJI nyota anayeshika namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic na Andy Murray ambaye ni bingwa wa michuano ya US Open wamepangwa tofauti katika ratiba ya michuano ya wazi ya Australia inayotarajiwa kuanza jijini Melbourne Jumatatu ijayo. Katika ratiba rasmi iliyopangwa mapema leo, Djokovic anaweza kukutana katika nusu fainali na David Ferrer anayeshika namba nne wakati bingwa mara 17 wa mataji ya Grand Slam Roger Federer anaweza kukutana na Murray anayeshika namba tatu katika hatua kama hiyo. 
Djokovic ataingia katika mashindano hayo akitaka kunyakuwa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kumfunga Rafael Nadal na kunyakuwa taji hilo mwaka jana ambapo anatarajiwa kuanza kampeni zake kwa kucheza na Paul-Henry Mathieu wa Ufaransa. Federer anayeshika nafasi ya pili kwa ubora anatarajia kuanza kampeni zake za kutafuta taji la tano la michuano hiyo kwa kupambana na Benoit Paire pia wa Ufaransa wakati Murray ataanza na Robin Haase wa Uholanzi.

KOCHA WA BLACK STARS KWESI APPIAH ANNAN YUKO FITI


KOCHA wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah amedai kuwa mchezaji nyota wa timu hiyo Anthony Annan alitolewa nje wakati wa kujipima nguvu dhidi ya Misri kwa tahadhari lakini mchezaji huyo atarejea tena uwanjani baada ya siku moja au mbili. Annan ambaye alikuwa nahodha katika mchezo huo aliteleza na kuanguka vibaya kabla ya kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Derek Boateng lakini Appiah amesema hakupatwa na madhara makubwa sana katika tukio hilo. Appiah amesema wachezaji wake wote wako fiti na ni Annan pekee ambaye bado anaonekana kuwa na tatizo lakini amehakikishiwa na daktari kwamba tatizo lake sio kubwa na atarejea katika hali ya kawaida muda mfupi ujao. Annan amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Ghana toka alipoitwa katika michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2008 na kwasasa mchezaji huyo anacheza katika klabu ya Osasuna ya Hispania ambayo imempeleka kwa mkopo katika klabu ya Schalke 04 ya Ujerumani.

DAKAR RALLY: AL-ATTIYAH AMZIDI MBIO PETERHANSEL KATIKA HATUA YA SITA.


DEREVA Nasser al-Attiyah wa Qatar amefanikiwa kumpita bingwa mara 10 wa mashindano ya Dakar Rally Stephane Peterhansel kwa zaidi ya dakika nane jana na kuibuka mshindi katika hatua ya sita ya mashindano hayo. Al-Attiyah ambaye alikuwa bingwa wa jumla wa mbio hizo mwaka 2011 alianza mbio hizo jana akiwa nyuma ya bingwa mtetezi wa mbio hizo Peterhansel lakini alifanikiwa kumaliza wa kwanza katika mbio hizo za jana zilizokuwa na kilometa 438 ukiwa ni ushindi wa tatu. Dereva huyo wa Qatar aliyekuwa akitumia gari aina Buggy alitumia muda wa saa 4 na dakika 52 huku Peterhansel anayetumia gari la Mini akikamata nafasi ya pili na nafasi ya tatu ilishikwa na Mmarekani Robby Gordon anayetumia NASCAR. Mbio hizo za Dakar Rally zinafanyika Amerika Kusini katika nchi za Peru na Chile baada ya kuhamishwa kutoka Kaskazini mwa Afrika mwaka 2009 kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea huko.

WERE AJIUZA KWA MABAO YAKE KOMBE LA MAPINDUZI



MSHAMBULIAJI wa mabingwa wa Kenya, Tusker FC, Jesse Were anaelekea kuwa mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajiwa kufikia tamati kesho kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa.
Were amefunga mabao manne hadi sasa katika mechi nne alizocheza kwenye mashindano haya na kesho atakuwa na nafasi ya kuongeza mabao akiiongoza timu yake katika fainali dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Azam FC.
Mkenya huyo, anafuatiwa kwa karibu na Adeyum Saleh Mohamed wa Miembeni mwenye mabao matatu, ambaye hata hivyo timu yake jana imetolewa.
Kwa mantiki hiyo, kuelekea mchezo wa kesho wa fainali, mpinzani haswa wa Were kwenye kiatu cha dhahabu cha mashindano haya anabaki kuwa beki Joackins Atudo, Mkenya anayechezea Azam FC.
Atudo atatakiwa kufunga mara tatu kwenye mchezo wa kesho na huku akimuombea dua mbaya Were asizione nyavu ili ampiku Mkenya mwenzake huyo.
Wengine wenye mabao mawili kila mmoja ni Michael Olunga wa Tusker, Haruna Chanongo wa Simba SC, ambaye timu yake imetolewa na Azam katika Nusu Fainali na Mfanyeje Mussa wa Jamhuri, iliyotolewa mapema tu katika hatua ya makundi.
WAFUNGAJI WA MABAO:
Jesse Were                    Tusker FC    3
Adeyum Saleh                Miembeni     3
Joackins Atudo               Azam FC      2
Haruna Chanongo          Simba SC     2
Mfanyeje Mussa             Jamhuri        2

Michael Olunga              Tusker FC    2

KALI ASEMA KOMBE MAPINDUZI NI LA AZAM


Kali Ongala
KALI Ongala, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kwamba wana matumaini ya kubeba Kombe la Tusker kesho, ingawa anakiri utakuwa mtihani mzito kwa sababu wapinzani wao, Tusker FC ya Kenya ni timu nzuri.
Akizungumza  leo, Kali alisema kwamba Wakenya wanawazidi Watanzania mambo mengi sana kisoka, lakini kwa hali yoyote Azam itapambana kubakisha taji nyumbani.
“Itakuwa mechi ngumu, kama ulivyoiona Tusker ni timu nzuri kwa kweli, imekamilika kila idara, lakini sisi pia tuna timu nzuri na tutapigana kufa na kupona kesho,”alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga SC.
Pamoja na hayo, Kali ameomba wapenzi wa soka Zanzibar kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuishangilia Azam FC kwa sababu ni timu ya nyumbani, ili iweze kubakiza taji hilo.
“Sisi ni timu ya Tanzania, na Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, hivyo tunaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutushangilia ili tuweze kubakiza taji hapa nyumbani,”alisema.

MSHAMBULIAJI WA UGANDA NA KLABU YA SIMBA OKWI AMESHINDIKANA SIMBA SC


Okwi
AMESHINDIKANA. Emmanuel Arnold Okwi, mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda anayechezea Simba SC ya Dar es Salaam ameondolewa kabisa katika programu ya kambi ya timu hiyo nchini Oman.
Hiyo inafuatia mshambuliaji huyo wa Uganda kutowasili Dar es Salaam hadi sasa na mbaya zaidi hata anapopigiwa simu na viongozi wa klabu hiyo hapokei.
“Okwi tumemuondoa kabisa katika programu ya Oman, hatuwezi kubembeleza mchezaji kiasi hiki,”alisema Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ leo alipozungumza
Okwi anaifanyia Simba SC ‘nyodo’ hizo akitoka kusaini mkataba mpya wa miaka miwili, Desemba mwaka jana na kuongezewa mshahara kwa zaidi ya nusu, hadi kuwa Sh. Milioni 3. 
Kaburu alisema kwamba baada ya kundi la kwanza kuondoka juzi, kundi lingine la wachezaji waliokuwa Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi litaondoka leo na kesho.
Amesema wachezaji walio na timu ya taifa, Taifa Stars nchini Ethiopia wataondokea nchini humo kwenda Oman, baada ya mechi dhidi ya Wahabeshi kesho
Simba SC itakuwa kambini Oman kwa wiki mbili tangu jana ikijifua kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ikiwa huko, Simba SC itapatiwa kambi ya mazoezi na mechi tatu za kujipima nguvu, kujiandaa na changamoto zinazowakabili mbele.