Saturday, November 3, 2012

 UCHAGUZI WA VIONGOZI MKOANI TABORA KESHO NI KESHO KATIKA UKUMBI WA TUWASA MANISPAA KUCHAGUA VIONGOZI WATAKAOWAKILISHA

Uchaguzi wa viongozi wa mpira wa miguu TAREFA ambao ulikuwa unasubiliwa kwa hamu na wakazi wa tabora sasa umesogezwa mbnele kutokana na baadhi ya viongozi kutokuwa na vigezo vya kuongoza  wamefoji vyeti..

Katika uchaguzi huo ambao ulikuwa unatarajiwa kusimamiwa na   mwakilishi wa TFF taifa ambaye ameteuliwa kuja kusimamia bwana MOSES KALUA ambaye alifika jana hapa mkoani tabora kuja kusimamia uchaguzi huo utakaofanyika kesho novemba 4 mwaka huu.

Katika uchaguzi huo nafasi zinazowaniwa ni nafasi ya mwenyekiti ambayo inawagombea watatu ambao ni,MUSA NTIMIZI,PAULO WELEMA,NA KHAMIS KITUMBO,nafasi ya katibu ina wagombea wawili,ALBERT SITTA,FATTY REMTULLA DEWJ.Mweka hazina msaidizi mjumbe mmoja,nafasi ya wajumbe wa  mkutano mkuu TFF ina wagombea wanne ambao ni MILAMBO KAMILI,DICK MLIMKA,ABDRAHMAN,Wajumbe 3 wa kamati ya utendaji ambayo inamgombea mmoja,mjumbe mwakilishi wa vilabu kwenye  mkutano mkuu TFF ina wagombea wawili na mwakilishi wa mpira wa wanawake  inamgombea mmoja,,,,

Wakati nafasi ambazo hazina wagombea ni nafasi ya makamu mwenyekiti,katibu msaidizi,mweka hazina msaidizi.

 Sasa uchaguzi huo utatangazwa upya katika mchakato wa uchaguzi ambayo ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi BW.MKAMA BWIRE na sasa mchakato huo utatangazwa kesho kutwa jumatatu katika ofisi za TUWASA mkoa wa tabora

LIGI DARAJA LA KWANZA  YAZIDI KUPAMBA MOTO HAPA NCHINI

Ligi daraja la kwanza imezidi kupamba moto hapa nchini na jumatano iliendelea kwa michezo kadhaa hapa nchini katika KUNDI C kuna michezo minne ilichezwa na katika uwanja wa lake tanganyika kule kigoma timu ya KANEMBWA iliitandika timu ya MWADUI FC mabao 3-2,POLISI MARA VS RHINO RANGERS 0-0,MORAN VS POLISI TABORA 1-1,POLISI DODOMA VS PAMBA 2-0

Ligi hiyo imeendelea tenaleo  katika viwanja kadhaa hapa nchini novemba 4 kulikuwa  na mechi kati ya MWADUI VS PAMBA[kambarage shinyanga,  POLISI MARA VS POLISI TABORA [karume mara],MORAN VS POLISI DODOMA[kiteto manyara], RHINO RANGERS VS KANEMBWA FC [ally hasan mwinyi]

MATOKEO

NOVEMBA 4

polisi tabora vs polisi mara 1-1

polisi dodoma vs moran 0-0

rhino rangers vs kanembwa fc 3-1

pamba vs mwadui bado matokeo sijayapata

MSIMAMO KUNDI C ULIOPITA KUACHA MECHI ZA LEO

1.KANEMBWA FC  pont 9 mechi 3

2.MWADUI FC point 6 mechi 3

3.POLISI DODOMA  point 6 mechi 3

4.RHINO RANGERS point 5 mechi 3

 5.PAMBA FC point 4 mechi 3

6. POLISI TABORA point 2 mechi 3

7.POLISI  MARA point 1 mechi 3

8.MORAN FC point 1 mechi 3


CAF yatangaza Listi Mchujo ya kuwania MCHEZAJI BORA AFRIKA!


>>SAMATTA atolewa!!!
CAF_LOGOCAF imetoa Listi iliyochujwa ya Wachezaji 10 kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2012 na ndani yake yupo anaeshikilia Tuzo hiyo, Yaya Toure wa Manchester City na Ivory Coast, na Listi hiyo itachujwa tena kubakisha Wachezaji watatu baadae Mwezi huu.
Kwa ile Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika, Listi hiyo imebakishwa Wachezaji watano tu na yule Straika hatari wa Tanzania anaechezea TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta, ambae alikuwemo kwenye uteuzi wa awali ametolewa.
Listi za awali zilikuwa na Wachezaji 34 kwa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika na Wachezaji 32 kwa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.
Pamoja na Tuzo za Wachezaji Bora pia Kocha Bora na Klabu Bora watazawadiwa Tuzo katika Sherehe maalum hapo Desemba 20 huko Mjini Accra, Ghana.
LISTI ya MCHEZAJI BORA AFRIKA 2012:
Alexander Song, Cameroon
Andre Ayew, Ghana
Christopher Katongo, Zambia
Demba Ba, Senegal
Didier Drogba, Cote D’Ivoire
Gervinho, Cote D’Ivoire
John Obi Mikel, Nigeria
Pierre-Emerick Aubameyang, Gabon
Yaya Toure, Cote D’Ivoire
Younes Belhanda, Morocco
LISTI ya MCHEZAJI BORA AFRIKA KWA Wachezaji wanaocheza ndani Afrika 2012:
Mohamed Aboutreika, Egypt
Rainford Kalaba, Zambia
Stoppila Sunzu, Zambia
Yannick N’Djeng, Cameroon
Youssef Msakni, Tunisia
TUZO NYINGINE:
1. Timu ya Taifa ya Mwaka
2. MCHEZAJI BORA AFRIKA kwa Wanawake
3. Timu ya Taifa ya Mwaka kwa Wanawake
4. Klabu ya Mwaka
5. Kipaji kinachovutia cha Mwaka
6. Kocha Bora
7. Refa Bora
8. Nguli Bora
9. Uchezaji wa Haki [Fair Play Award]
10. Tuzo Iliyotukuka [Platinum Award]
11. Kikosi Bora cha Afrika
FAHAMU: Listi hizo zimeamuliwa na Kamati za CAF za Ufundi, Soka na Utangazaji na sasa Makocha Wakuu na Wakurugenzi wa Ufundi wa Timu za Taifa za Wanachama wa CAF ndio watapiga Kura kuamua Washindi.
 

CAF CHAMPIONZ LIGI FAINALI: Al Ahly 1 Esperance 1

walid hicheri est 01
>>MARUDIANO Novemba 17 huko Tunis!
Mechi ya kwanza ya Fainali ya kutafuta Klabu Bingwa Afrika, CAF CHAMPIONZ LIGI, kati ya Al Ahly ya Misri na Mabingwa watetezi Esperance ya Tunisia imechezwa Jumapili ndani ya Borg El Arab Stadium Mjini Alexandria, Misri mbele ya Mashabiki 15,000, na Timu hizi kutoka sare ya Bao 1-1.
Esperance ndio walitangulia kufunga katika Dakika ya 49 kwa bao la Walid Hicheri na Al Ahly kusawazisha katika Dakika ya 88 mfungaji akiwa Al-Sayed Hamdy.
Timu hizi zitarudiana huko Tunis, Tunisia hapo Novemba 17.
Mshindi wa Fainali hii atatawazwa kuwa Klabu Bingwa Afrika na kuzoa kitita cha Dola Milioni 1 na Nusu na pia ataiwakilisha Afrika katika Mashindano ya FIFA ya kusaka Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa huko Japan Mwezi Desemba.
AFRICAN CONFEDERATION CUP 2012
NUSU FAINALI
Ijumaa Novemba 2
Al Hilal [Sudan] 2 Djoliba AC [Mali] 0
Jumapili Novemba 4
AC Leopards de Dolisie [Congo] 2 El Merreikh [Sudan] 1
Marudiano
Jumamosi Novemba 10
El Merreikh [Sudan] v AC Leopards de Dolisie [Congo]
Jumapili Novemba 11
Djoliba AC [Mali] v Al Hilal [Sudan]
 

BPL: Liverpool v Newcastle, QPR v Reading, ZOTE 1-1!!


BPL_LOGOKatika Mechi mbili za Ligi Kuu England zilizochezwa leo, Liverpool na Newcastle walitoka 1-1 na pia matokeo kuwa kama hayo kwa Mechi kati ya QPR na Reading.
Liverpool 1 Newcastle 1
Wakicheza kwao Uwanjani Anfield, Liverpool wamefanikiwa kutoka sare ya Bao 1-1 na Newcastle ambao walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Sentahafu wao Fabricio Coloccini kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya kwa Luis Suarez.
Newcastle ndio waliotangulia kupata bao safi la Yohan Cabaye katika Dakika ya 43 lakini nae Luis Suarez alisawazisha kwenye Dakika ya 67 pia kwa bao zuri.
Matokeo haya yamewaacha Newcastle wakamate nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 14 kwa Mechi 10 na Liverpool wapo nafasi ya 12 wakiwa na Pointi 11 kwa Mechi 10.
VIKOSI:
Liverpool: Jones, Wisdom, Skrtel, Agger, Jose Enrique, Gerrard, Allen, Sahin, Fernandez Saez, Suarez, Sterling
Akiba: Gulacsi, Assaidi, Henderson, Coates, Downing, Carragher, Shelvey.
Newcastle: Krul, Anita, Steven Taylor, Coloccini, Santon, Perch, Cabaye, Gutierrez, Ben Arfa, Cisse, Ba
Akiba: Harper, Simpson, Williamson, Shola Ameobi, Obertan, Sammy Ameobi, Ferguson.
Refa: Anthony Taylor
QPR 1 Reading 1
Sare hii haikuzisaidia Timu zote hizi mbili ambazo zipo mkiani na bado zinasaka ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi Msimu huu.
Reading ndio walitangulia kupata Bao katika Dakika ya 16 alilofunga Kaspars Gorkss baada ya kona ya Nicky Shorey kuleta kizaazaa golini.
QPR walisawazisha katika Dakika ya 66 kwa Bao la Djibril Cisse.
Matokeo haya yanawaacha Reading wakamate nafasi ya 18 wakiwa na Pointi 5 kwa Mechi 9 wakifuatiwa na QPR wenye Pointi 4 kwa Mechi 10 na mkiani wapo Southampton wenye Pointi 4 kwa Mechi 9.
VIKOSI:
QPR: Julio Cesar, Bosingwa, Ferdinand, Nelsen, Traore, Mackie, Granero, Diakite, Taarabt, Hoilett, Cisse
Akiba: Green, Derry, Hill, Wright-Phillips, Onuoha, Zamora, Faurlin.
Reading: McCarthy, Gunter, Morrison, Gorkss, Shorey, McCleary, Leigertwood, Tabb, McAnuff, Roberts, Hunt
Akiba: Federici, Pearce, Pogrebnyak, Le Fondre, Kebe, Robson-Kanu, Cummings.
Refa: Michael Oliver
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatatu, Novemba 5
[SAA 5 Usiku]
West Bromwich Albion v Southampton
Jumamosi, Novemba 10
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Fulham
Everton v Sunderland
Reading v Norwich City
Southampton v Swansea City
Stoke City v Queens Park Rangers
Wigan Athletic v West Bromwich Albion
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Manchester United
Jumapili, Novemba 11
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool
 

ABEDI PELE atembelea Bongo, atoa Mawaidha kwa Vijana!!


>>FIFA yamleta kuangalia shughuli za Maendeleo ya Soka!
ABEDI_PELENyota wa zamani aw Ghana na klabu ya Olympique Marseille, Abedi Pele, amewaambia Wachezaji chipukizi wa Tanzania kuwa "hakuna njia ya mkato katika kutafuta mafanikio" na kuwataka kufanya jitihada ili watimize ndoto, ikiwa ni pamoja na Serengeti Boys kuhakikisha inafuzu kucheza Fainali za Afrika mwakani.
Pele, ambaye aliiongoza Marseille kutwaa ubingwa wa Ulaya mwaka 1992 akifunga moja ya mabao dhidi ya AC Milan ya Italia, alisema hayo Jana asubuhi wakati alipotembelea Kiti cha ufundi cha Karume kushuhudia programu ya mazoezi ya vijana wadogo inayofanyika kila misho wa wiki kwenye Uwanja wa Karume ambako watoto wa kuanzia umri wa miaka sita hadi 17 hufundishwa mbinu za kusakata soka.
"Katika kufikia mafanikio hakuna njia ya mkato," alisema Pele ambaye ameletwa nchini na Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
"Tunaona wachezaji wenye vipaji vikubwa duniani wakifanya jitihada kubwa ili waweze kucheza kwa kiwango cha juu. Bila ya kufanya juhudi, kujituma na kudhamiria huwezi kufanikiwa.
"Wale wenye vipaji vikubwa, lakini hawafanyi jitihada watabakia I. Wale wasiojaliwa kuwa na vipaji, lakini wanafanya jitihada, watakwenda mbele na kupata mafanikio," alisema nyota huyo ww Ghana ambaye alijijengea jina kwa kufunga mabao safi na muhimu kwa nchi yake na klabu ya Olympique Marseille wakati ikitamba katika soka barani Ulaya.
"Soka barani Afrika Lina mazingira yanayofanana. Hakuna motto wa waziri anayecheza soka. Wala hakuna mtoto wa mwanasheria au mfanyakazi ww benki ambaye anacheza soka. Soka inachezwa na watu wanaotoka kwenye familia ambazo hazina maisha mazuri na hivyo man nafasi sawa na wengine wote. Mnachotakiwa kufanya ni kujituma, kudhamiria na kufanya jitihada ili mfungue mlango wa mafanikio.
Pele, ambaye jina lake halisi ni Abedi Ayew na ambaye watoto wake wainaichezea Marseille, pia aliwataka wacheaji aw timu ya Taifa ya Vijana walio na umri china ya miaka 17 kufanya kila wawezalo ili wafuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Algeria mapema mwakani.
"Mkifuzu mtakuwa mmefungua milango ya mafanikio ya maisha yenu," alisema gwiji huyo ambaye anaiwakilisha FIFA katika kufuatilia programu mbalimbali za maendeleo. "nikiwaangalia naona mna man uwezo wa kuwaondoa wapinzani wenu na nitafuatilia mechi yenu. Mkifuzu tutakuwa wote na nitawaunga mkono.
Pele, ambaye kwa sasa anamiliki shule ya mpira wa miguu ambayo imeshanikiwa kutwaa Kombe la FA mara moja, ameambatana na Mkurugenzi wa Maendeleo wa FIFA kwa nchini za Kusini mwa Afrika, Ashford Mamelodi na mmoja wa viongozi wa Idara ya Mawasiano ya FIFA, Emmanuel, atakuwa nchini kwa siku tatu ambazo atazitumia kupata taarifa za shughuli mbalimbali za maendeleo, zikiwemo za soka la watoto (grassroots), soka la vijana, soka la wanawake na miradi mingine ya maendeleo.
>>RIPOTI imesambazwa na Boniface Wambura, AFISA HABARI TFF
 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Jumanne & Jumatano ndio USIKU wake!


UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZ>>MECHI DEI 4-NI LALA SALAMA kwa baadhi ya Klabu!!
>>MAN CITY kuaga? MAN UNITED kufuzu?
Wakati FC Porto, Málaga, FC Barcelona na Manchester United ndio Klabu pekee zenye ushindi wa Asilimia 100 wakiingia kwenye Mechi za Raundi ya 4 ya Makundi, MECHI DEI 4, na matokeo mema yatawapeleka Raundi ya Mtoano huku wakiwa na Mechi mbili mkononi, kwa baadhi ya Timu Mechi za Jumanne na Jumatano ndio lala salama yao kwani matokeo yeyote mabovu yatawabwaga nje.
+++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku Bongo Taimu]
Jumanne Novemba 6
FC Dynamo Kyiv v FC Porto
Paris SaintvGermain FC v GNK Dinamo
FC Schalke 04 v Arsenal FC
Olympiacos FC v Montpellier Hérault SC
RSC Anderlecht v FC Zenit St. Petersburg
AC Milan v Málaga CF
Manchester City FC v AFC Ajax
Real Madrid CF v Borussia Dortmund
Jumatano Novemba 7
Juventus v FC Nordsjælland
Chelsea FC v FC Shakhtar Donetsk
Valencia CF v FC BATE Borisov
FC Bayern München v LOSC Lille
SL Benfica v FC Spartak Moskva
Celtic FC v FC Barcelona
CFR 1907 Cluj v Galatasaray A.S.
SC Braga v Manchester United FC
+++++++++++++++++++++++++++++++
ZIFUATAZO NI DONDOO FUPI ZA MECHI HIZI:
GEMU ZA Jumanne:
KUNDI A
FC Dynamo Kyiv v FC Porto;
Paris Saint-Germain FC v GNK Dinamo Zagreb
MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Porto Pointi 9
2 PSG 6
3 Dinamo Kiev 3
4 Dinamo Zagreb 0
TATHMINI:
FC Porto wameshinda Mechi zao zote 3, kwa kuzifunga Dinamo Zagreb 2-0, PSG 1-0 na Dynamo Kyiv 3-2 na ushindi kwenye Mechi yao ya Jumanne utawafanya wasonge mbele.
Dinamo Zagreb hawana rekodi nzuri wakicheza na Klabu za Ufaransa kwa kushinda Mechi 1 tu kati ya 7 walipoifunga Auxerre 1-0 kwenye UEFA CUP Mwaka 1989/90.
KUNDI B
FC Schalke 04 v Arsenal FC
Olympiacos FC v Montpellier Hérault SC
MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Schalke Pointi 7
2 Arsenal 6
3 Olympiacos 3
4 Montpellier 1
TATHMINI:
Ingawa Schalke hawana rekodi nzuri dhidi ya Klabu za England wakicheza kwao na mara ya mwisho walichapwa 2-0 na Manchester United katika Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2010/11, safari hii wanatinga kwao baada ya kuichakaza Arsenal 2-0 Uwanjani Emirates katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi hili.
Olympiacos ni wazoefu kwa Mechi za Ulaya lakini mbali ya Misimu ya 2009/10 na 2007/8 hawajawahi kufika Raundi ya Mtoano.
KUNDI C
RSC Anderlecht v FC Zenit St Petersburg
AC Milan v Málaga CF
MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Malaga Pointi 9
2 AC Milani 4
4 Zenit St Petersburg 3
3 Anderlecht 1
TATHMINI:
Baada ya kufungwa na Malaga 3-2 katika Mechi yao ya mwisho kucheza nyumbani, Uwanja wa Constant Vanden Stock, Anderlecht bado wanasaka ushindi wao wa kwanza wa hapo nyumbani katika Miaka 9 kwenye Mashindano ya Ulaya.
Malaga, ambao si wazoefu sana kwenye Mashindano ya Ulaya, wameanza kwa kasi mno kwa kushinda Mechi zao zote 3 za Kundi hili na wapo mguu mmoja mbele wakisaka kufuzu kuingia Raundi ya Mtoano.
KUNDI D
Manchester City FC v AFC Ajax
Real Madrid CF v Borussia Dortmund
MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Borussia Dortmund Pointi 7
2 Real Madrid 6
3 Ajax 3
4 Manchester City 1
TATHMINI:
Ingawa Manchester City, tangu Mwaka 2008, wana rekodi nzuri kwenye Mashindano ya Ulaya wakicheza nyumbani kwao kwa kushinda Mechi 14 na sare 4 lakini wanapambana na Ajax Amsterdam ambayo iliwachapa Mabao 3-1 katika Mechi yao ya mwisho Wiki mbili zilizopita.
Ingawa Borussia Dortmund waliipiga Real Madrid 2-1 Wiki mbili zilizopita, Real wana rekodi nzuri wakiwa nyumbani na Dortmund wana rekodi mbovu sana ugenini.
Hadi sasa, Real wameshinda Mechi 7 mfululizo walizocheza mwishoni Uwanjani kwao Santiago Bernabeu katika Mashindano ya Klabu za Ulaya na kufunga jumla ya Bao 27, Dortmund, Msimu uliopita, walifungwa Mechi zao zote 3 za ugenini za Makundi za Mashindano haya.
GEMU ZA Jumatano:
KUNDI E
Juventus FC v FC Nordsjælland
Chelsea FC v FC Shakhtar Donetsk
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
Shakhtar Donetsk 7
Chelsea Pointi 4
Juventus 3
Nordsjaelland 1
TATHMINI:
Juventus wametoka sare Mechi zao 9 zilizopita za Mashindano ya UEFA zikiwemo sare 3 za Kundi hili.
Ingawa Shakhtar wameichapa Chelsea Bao 2-1 katika Mechi iliyopita, hawana rekodi nzuri kwa Mechi wanazocheza England.
KUNDI F
Valencia CF v FC BATE Borisov
FC Bayern München v LOSC Lille
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
Valencia 6
BATE Borisov Pointi 6
Bayern Munich 6
Lille 0
TATHMINI:
Ingawa Kundi hili linaonekana gumu kufuatia matokeo yake na Msimamo ulivyo, BATE hawajawahi kuifunga Klabu ya Spain.
Kwa Miaka ya hivi karibuni, Bayern Munich wana rekodi nzuri kwa Klabu za France.
KUNDI G
SL Benfica v FC Spartak Moskva
Celtic FC v FC Barcelona
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
Barcelona Pointi 9
Celtic 4
Spartak Moscow 3
Benfica 1
TATHMINI:
Celtic walifungwa huko Nou Camp Bao 2-1 katika Dakika za majeruhi na safari hii wanarudiana na Barcelona wakiwa kwao Celtic Park lakini Barca wana rekodi nzuri katika Mashindano ya UEFA kwa Mechi za ugenini kwa kushinda Mechi 12 na kufungwa 3 tu katika Mechi 25 zilizopita.
KUNDI H
CFR Cluj 1907 v Galatasaray AŞ
SC Braga v Manchester United FC
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
Manchester United Pointi 9
CFR Cluj 4
Braga 3
Galatasaray 1
TATHMINI:
Galatasaray hawajashinda ugenini kwenye Mashindano ya Klabu Ulaya tangu Mwaka 2002 wakiwa wamefungwa Mechi 8 na sare 1 tu katika Mechi zao 9 za mwisho.
Wakicheza huko Old Trafford katika Mechi iliyopita, Braga waliongoza 2-0 lakini wakajikuta wakipigwa 3-2 na Manchester United na safari hii wapo kwao Estádio Municipal de Braga ambapo kwenye Mechi ya mwisho waliyocheza hapo kwenye Kundi hili walipigwa 2-0 na CFR Cluj Mwezi Septemba