Sunday, January 13, 2013

MANCHESTER UNITED WAIADABISHA LIVERPOOL OTRAFORD NA KUWARUDISHA KATIKA JIJI LA MERCYSIDE VICHWA CHINI

>>UNITED WAKO POINTI 10 MBELE, KILELENI!
BPL_LOGOManchester United leo wamezidi kupaa kileleni baada ya kuwachapa Mahasimu wao wakubwa Liverpool Bao 2-1 Uwanjani Old Trafford na kukwea juu kileleni mwa BPL, Barclays Premier League, wakiwa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Man City ambao muda mfupi baadae leo wana kibarua kigumu Uwanjani Emirates watakapoivaa Arsenal.RVP-BAO_NA_LIVERPOOL
++++++++++++++++
MAGOLI:
Man United 2
-Van Persie Dakika ya 19
-Vidic 54
Liverpool 1
-Sturridge Dakika ya 57
++++++++++++++++
Man United, ambao walitawala kabisa Kipindi cha Kwanza, walifunga Bao lao la kwanza kupitia Robin van Persie kufuatia pasi murua kati ya Danny Welbeck, Tom Cleverley, Shinji Kagawa na Patrice Evra kumtilia pasi ya chini Van Persie aliepachika wavuni kiakili.
Frikiki ya Robin van Persie iliunganishwa kwa kichwa na Patrice Evra na kumparaza Nemanja Vidic na kutinga wavuni na kuwapa Man United Bao la Pili.
Lakini, Dakika chache baadae, makosa ya Man United yaliwapa Liverpool Bao laini baada ya shuti la Steven Gerrard kutemwa na Kipa David De Gea na kutua njiani kwa Mchezaji mpya Daniel Sturridge alieunganisha vizuri na kufunga Bao lake la kwanza kwenye BPL kwa Timu yake mpya na Bao lake la pili baada ya pia kuifungia kwenye FA CUP walipoichapa Mansfield 2-1 kwenye Mechi yake ya kwanza kabisa hivi majuzi.
VIKOSI:
Manchester United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Vidic, Evra, Carrick, Cleverley, Young, Kagawa, Welbeck, van Persie
Akiba: Amos, Jones, Valencia, Anderson, Giggs, Smalling, Hernandez.
Liverpool: Reina, Wisdom, Skrtel, Agger, Johnson, Lucas, Downing, Gerrard, Allen, Sterling, Suarez
Akiba: Jones, Henderson, Sturridge, Carragher, Borini, Shelvey, Robinson.
Refa: Howard Webb
+++++++++++++++++++++++
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 1 Usiku]
Arsenal v Man City
Jumatano Januari 16
[SAA 4 DAK 45 Usiku]
Chelsea v Southampton
Jumamosi Januari 19
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Swansea v Stoke
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United

UKURASA WA DONDOOO ZA USAJILI NA HABARI ZA KIMATAIFA NI HAPA WENGER ANAAMINI FABREGAS ANAWEZA KURUDI EMIRATES

 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema upo uwezekano mkubwa wa kiungo wake wa zamani Cesc Fabregas kurejea Emirates Stadium.
Fabregas mwenye umri wa miaka 25, aliichezea kwa miaka minane Arsenal kabla ya kurejea nyumbani Hispania katika klabu iliyomkuza tangu akiwa mtoto ya Barcelona kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 30 mwaka 2011.
Wenger anaamini kuwa kiungo huyo wa kimataifa ya Hispania kwasasa ametulia Camp Nou, na timu yake ikiongoza ligi ya nchi hiyo Liga lakini bado anaamini anaweza kurejea kusaini tena Arsenal.
"Sidhani kama hararejea moja kwa moja iko siku moja " amekaririwa na gazeti la Guardian.
"ni mtu wa Arsenal. Anaipenda Arsenal na anaangalia kila mchezo wa Arsenal. Lakini bila shaka Barcelona kulikuwa ndiyo nyumbani alikokulia lazima ukubali hilo.
"Huenda asije mwakani au miaka miwili au mitatu kwasababu ana uhusiano mkubwa na Barcelona. Lakini baadaye linawezekana."
Wenger kwasasa amepata faraja kubwa kwa wachezaji wake vijana waingereza Kieran Gibbs, Carl Jenkinson, Jack Wilshere, Aaron Ramsey na Alex Oxlade-Chamberlain – kusaini mkataba mpya na klabu hiyo.

KOCHA WA ZAMANI W ATIMU YA TAIFA YA ENGLAND FABIO CAPELO ANATARAJIA KUWA MGENI WA KUHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 150 CHA FA
 Meneja wa zamani wa timu ya taifa ya England Fabio Capello atakuwa ni miongoni mwa watu watakao hudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 150 ya chama cha soka cha England jumatano jijini London.
Sherehe hizo ambazo pia zitahudhuriwa na meneja wa sasa wa England na zitafanyika Connaught Rooms huko Holborn.
Kwasasa Capello ni meneja wa timu ya taifa ya Russia, na tayari ameuarifu uongozi wa FA ataudhuria katika sherehe hizo.
Capello aliondoka kuifundisha England kwa mizengwe mwezi February 2012 baada ya kutofautiana na maamuzi ya kumvua unahodha John Terry kwa mara ya pili na tangu wakati huo hakuwa na mawasiliano na FA.
Ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 150 ya FA, pia kumeandaliwa michezo miwili ya kirafiki kati ya England na Brazil na mchezo mchezo mwingine kati ya Scotland dhidi ya jamhuri ya Ireland. Michezo mingine dhidi ya Ujerumani na Argentina inatarajiwa kuchezwa baadaye mwaka huu.
O'BRIEN ASAINI MKATABA KATIKA WAGONGA NYUNDO W ALONDON WEST HAM UNITED
 Mlinzi wa West Ham Joey O'Brien ameongeza mkataba mwingine na klabu hiyo ambao utamuweka klabuni hapo mpaka 2016.
O'Brien akiwa chini ya Sam Allardyce katika klabu ya Bolton alipelekwa Upton Park mwaka 2011 na bosi wa washika nyundo.
Klabu hiyo imetangaza hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa maneno yaliyosomeka “West Ham United inayofuraha kubwa kutangaza kuwa Joey O'Brien amesaini mkataba mpya utakamuweka klabu mpaka kiangazi 2016.”
O'Brien mwenye umri wa miaka 26, ameitumikia timu ya taifa ya jamhuri ya Ireland michezo mitano na ameitumikia klabu yake michezo 16 huu wa ligi kuu ya England ‘Premier League’ akifunga magoli mawili.
 

DZEKO MGUU NDANI MGUU NJE CITY KUICHEZEA MAN CITY.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Edin Dzeko ameonyesha nia yake ya kurejea katika Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga baada ya kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Manchester City. Dzeko amefunga mabao sita msimu huu akitokea benchi na kuna taarifa kuwa mchezaji huyo hafurahishwi kuwepo katika klabu hiyo na hivyo yuko tayari kusikiliza ofa kutoka katika timu yoyote kwenye kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili. Nyota huyo amesema kila kitu kinawezekana hivyo anaweza kuondoka kuondoka kipindi hiki au katika majira ya kiangazi lakini kwasasa anajaribu kutofikiria hilo na kujaribu kutumia nafasi anayopewa na City. Mbali na mchezaji huyo pia kumekuwa na tetesi za kuondoka kwa mshambuliaji mwingine nyota wa klabu Sergio Aguero lakini taarifa hizo zilikanushwa na mchezaji mwenzake Pablo Zabaleta ambaye alidai kuwa nyota huyo anafurahia maisha katika klabu hiyo na hama mpango wa kuondoka.

AFCON KUMPELEKA MPUTU ULAYA.

KIUNGO wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC, Tresor Mputu amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia katika vilabu vya Ulaya mara nyingi zaidi kuliko alivyofunga mabao kwa klabu yake na timu ya taifa. Mputu mwenye umri wa miaka 27 mpaka sasa amefanikiwa kufunga mabao zaidi ya 200 kwa timu yake ya taifa ya DRC na klabu ya TP Mazembe yenye maskani yake jiji la Lubumbashi lililo kusini mwa nchi hiyo. Zikiwa zimebakia siku chache kabla ya kuanza michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika nchini Afrika Kusini vyombo vya habari vimeanza tena kumfuatilia mchezaji huyo na kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi ya nyingine kwa nyota huyo kuonekana kwa vilabu vya Ulaya.  Vyombo vimeanza kutabiri kuwa kiwango alichonacho Mputu katika kukokota mpira pamoja na umahiri wa kufunga na kutengeneza mabao kitawavutia maskauti kutoka barani Ulaya ambao watakuwepo wakifuatilia kwa karibu michuano hiyo.

MOURINHO UNDER MORE PRESSURE BAADA YA JANA KUTOA SARE NA KUTOA KABISA MATUMAINI YA UBINGWA .

MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho ameingia katika shinikizo zaidi jana wakati klabu hiyo ilipolazimishwa sare ya bila kufungana na klabu ya Osasuna ambayo inashika mkia matokeo ambayo yamewaacha nyuma kwa alama 15 mbele ya mahasimu wao Barcelona ambao wanaongoza La Liga. Katika mchezo Madrid ambao hawakutengeneza nafasi nyingi za kufunga walimkosa mshambuliaji wake nyota Cristiano Ronaldo ambaye alifunga mabao matano kati ya nane ambayo timu hiyo imeshinda katika michezo yake miwili iliyopita. Madrid sasa wanabakia katika nafasi ya tatu wakiwa na alama 37 ikiwa ni alama nne nyuma ya Atletico Madrid wanaoshika nafasi ya pili ambapo pia kuna uwezekano wa kutofautiana na Barcelona kwa alama 18 kama timu hiyo ikishinda mchezo wake wa leo dhidi ya Malaga. Pamoja na matokeo hayo lakini Mourinho alikataa kuwalaumu wachezaji kwa kuwasifia kucheza vizuri na kufanya kila waliloweza kujaribu kufunga pamoja na kwamba hawakutengeneza nafasi nyingi.

AYEW AREJEA KATIKA KIKOSI CHA MARSEILLE BAADA YA KUPONA.

WINGA machachari wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa, Andre Ayew ambaye aliondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, ameitwa katika kikosi cha Marseille ambacho kinatarajia kucheza na Sochaux katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa. Taarifa iliyolewa na mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa Ayew ambaye ameichezea Ghana mechi 44 amepona majeraha ya paja aliyopata wakati wa mazoezi na klabu yake siku 10 zilizopita. Ayew mwenye umri wa miaka 23 ambaye ni mtoto wa nguli wa zamani wa Ghana Abeid Pele, alitarajiwa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya majeraha yake lakini hakutokea kwa wakati kitendo ambacho kilipelekea kocha Kwesi Appiah kumuengua kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon. Kama ilivyo kwa Ayew, golikipa wa Togo Kossi Agassa naye pia anatarajia kuwepo katika kikosi cha Marseille Jumapili pamoja na kuenguliwa katika michuano ya Afcon kutokana na kupata majeraha ya mguu. Michuano ya Afcon inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januri 19 na kumalizika Februari 10 mwaka huu.

CHANETA KUADHIBU MIKOA AMBAYO HAIJAFANYA UCHAGUZI


Chama cha netiboli nchini (CHANETA) kimesema kitatoa adhabu kwa viongozi wa mikoa ambayo haijaitisha uchaguzi wa viongozi bila ya kutoa sababu za msingi.

Kaimu Katibu Mkuu wa CHANETA, Rose Mkisi amesema mikoa hiyo tayari viongozi wake wamemaliza muda wao lakini wanashindwa kuitisha uchaguzi wa viongozi.

Mkisi aliitaja mikoa hiyo ambayo iko hatarini kupewa adhabu na CHANETA ni pamoja na Tanga, Manyara, Arusha,Kilimanjaro Mara, na Rukwa.

Mikoa mingine ambayo bado haijaitisha chaguzi zake ni pamoja na Dodoma, Tabora, Shinyanga, Iringa,Kagera, na Kigoma.

 "Tunaomba mikoa hiyo ifanye chaguzi ili kufanikisha CHANETA kuitisha uchaguzi mkuu, bila ya kufanya hivyo itapewa adhabu," aliongeza  Mkisi.

 Mkisi aliongeza  mikoa hiyo ndio chanzo kikubwa cha CHANETA kuchelewa kuitisha uchaguzi mkuu kwa ajili ya kupata viongozi wapya watakaokiongoza chama hicho kwa muda wa miaka minne.

Mkisi aliitaja mikoa ambayo tayari imefanya chaguzi zake ni kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza, Lindi, Mtwara,Morogoro, Ruvuma, Mbeya, na Singida.

Alisema wakitekeleza zoezi hilo mapema itakuwa rahisi kwa CHANETA kuanza harakati za uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi wapya wa chama hicho.

Wakati huo huo, Mkisi aliwataka wachezaji wa timu ya taifa ya netiboli kujitokeza mazoezini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa yaliyopo kwenye kalenda ya mwaka.

 mazoezi hayo kwa sasa yatakuwa yanakwenda na kurudi nyumbani chini ya makocha Mary Protasi na Mary Waya kwa ajili ya kuiandaa timu hiyo na mashindano ya kimataifa yaliyopo kwenye kalenda ya mwaka. Aliongeza  wachezaji wote wanatakiwa kuhudhuria mazoezi hayo ili iwe rahisi kwa kocha kuweza kuchagua kikosi cha kwanza cha timu hiyo kitakachoiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

KAMATI TENDAJI YA MPIRA WA MIGUU MKOA WA TABORA TAREFA YAKUTANA KWA MARA YA KWANZA TOKA ICHAGULIWE DEC 22 MWAKA JANA KATIKA UKUMBI WA FRANKMAN

Add caption
 
 Kamati tendajiya uongozi wa mpira wa miguu mkoa wa tabora TAREFA  leo imekutana kwa mara ya kwanza toka ichaguliwe tarehe 22 dec.2012 mwaka jana kujadili mambo mbali mbali ya soka la mkoa wa tabora kubwa zaidi ajenda zilizojadiliwa  ni pamoja na maandalizi ya timu za daraja la kwanza kuweza kupandisha timu mojawapo ya daraja la kwanza ipande ligi kuu tanzania bara kati ya timu hizo mbili za mkoani tabora Rhino Rangers ama Polisi Tabora.

Ajenda ya pili ni pamoja na kuandaa ligi za wilaya pamoja na mkoa wa tabora ili kupata timu ambazo zitakuwa na makali ya kurudisha taswira ya soka la mkoa wa tabora ni pamoja na kupata timu 2 ambazo zitapatikana wilayani kote za tabora wilaya ya uyui ,skonge,urambo,nzega,igunga na tabora mjini kila wilaya ipate timu 2 na mkoa timu moja.

Ajenda ya tatu ni pamoja na makabidhano ya  nyaraka za TAREFA ikiwemo na vifaa vya ofisi,kwani mpaka sasa ivi katibu wa zamani wa TAREFA bw. Albert Sitta hataki kukabidhisha nyaraka hizo kw auongozi mpya uliochaguliwa tarehe 22 dec.2012 chini ya uenyekiti wa Yussuph Kitumbo.

Ajenda nyingine ni pamoja na kujaza nafasi zilizowazi katika uongozi kama nafasi ya katibu msaidizi  kwani mwenyekiti aliridhia kumjaza katibu mkuu wa TUFA bw.Juma Mapunda kuwa kaimu katibu msaidizi na kamjaza bi Janethi Michael kuwa kaimu  mweka hazina wa TAREFA.

Ajenda nyingine iliyojadiliwa ni pamoja na maendeleo ya soka mawilayani mkoani tabora wamehakikisha kuwa soka la wilayani liwe na taswira ya kisoka siyo kama ilivyopotea kutokana na uongozi uliopita chini ya uenyekiti wa Ismail Aden Ragge pamoja na katibu mkuu wake Albert Sitta kuwa hawana organization nzuri juu ya uongozi wao pamoja na ajenda nyingine mengineyo kama kuandaa vitega uchumi,kuandaa ligi mbalimbali,kuandaa kozi za waamuzi,marefarii pamoja na kozi za makocha..







   

HII NDIYO HOTELI WALIYOFANYIA WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA TAREFA MKOA WA TABORA LEO

 
KAMATI TENDAJI IKIPATA BREAKFAST KATIKA HOTELI YA KITALII YA FRANKMAN


BWANA KITUMBO HUYO WA KWANZA KULIA AKIWA TAYARI KWA KUPATA BREAKFAST
 
WA KWANZA KUTOKA KUSHOTO NI KATIBU MKUU WA TAREFA BWANA FATTY DEWJ REMTULA AKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MWENYEKITI WA TAREFA BWANA YUSUPH KITUMBO


KATIBU MKUU WA TAREFA FATTY DEWJ REMTULA AKIWA ANAANDIKA MOJA YA HOJA TOKA KWA WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI


BI JANETH MICHAEL MWAKILISHI W AVILABU KWA WANAWAKE AKIWA ANAPATA MENYU
 
BWANA KITUMBO NA JOPO LAKE LA KAMATI TENDAJI YA TAREFA WAKIPATA BREAKFAST KWA PAMOJA KATIKA HOTELI YA FRANKMAN


KATIBU MKUU WA TAREFA FATTY DEWJ REMTULA AKIJIVINJALI KWA BREAKFAST KATIKA MKUTANO WAO WA KAMTI TENDAJI
 
WAHUDUMU WA FRANKMAN PALACE HOTELI

 
KATIBU WA TUFA JUMA MAPUNDA W AKWANZA KUTOKA KULIA,BW.KABEPELE ,BI.JANETH MAICHAEL NA RAZACK HUMBA WAKIMSIKILIZA KW AUNDANI MWENYEKITI WA TAREFA KITUMBO


MJUMBE WA KAMATI TENDAJI YA TAREFA DICK MLIMKA AKITOA HOJA KWA WAJUMBE WALIOHUDHURIA KIKAO HICHO
 
KIJANA MDOGO KWA WENYEKITI WA MIKOA TANZANIA NZIMA BW.YUSUPH KITUMBO AKIJADILIANA NA WAJUMBE ILI KUONDOA TASWIRA MBAYA YA SOKA LA MKOA W ATABORA

KAMA KAWAIDA ANAONGEA KWA UCHUNGU ILI SOKA LA MKOA WA TABORA LIWE NA TASWIRA NZURI KWA WANATABORA

MWENYEKITI WA TAREFA  YUSUPH KAHAMIS KITUMBO NA  KATIBU WAKE BWANA FATTY DEWJ REMTULA

TIMU YA RHINO RANGERS YAIVUNJA VUNJA TIMU ILIYOCHAGULIWA KUUNDA KOMBAINI WILAYA


 

 Timu ya wanajeshi ya mkoani Tabora ambayo inajiandaa na ligi daraja la kwanza imewatandika bila huruma kombaini ya wilaya mkoani Tabora mabao 2-0 katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kuelekea katika mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza FDL ambayo inatarajia kuanza kutimua vumbi tarehe 26/1/2013.

Mabao ya Rhino rangers yalifungwa na shija sanju dk ya 33 na mchembe dk ya 44  kipindi cha kwanza  baada ya mabeki wa kombain wilaya kujichanganya na kuwaruhusu rhino kujipatia mabao hayo mawili yaliyowawezesha kutoka uwanjani kifua mbele kwa mabao 2-0.

 Timu hiyo ya rhino inaendelea na mazoezi yake tena kesho jumatatu katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi wakiwapashia nguvu wakata miwa wa bukoba  KAGERA SUGAR ambao wanatarajia kuja kucheza nao tarehe 18/1/2013 pia wanatarjia kucheza na timu ya Azam Fc na timu ya Simba B katika uwanja wa A.H. MWINYI ili kujua ni jinsi gani wanamapungufu yao.

Naye mwenyekiti wa TAREFA mkoa wa tabora bw. YUSUPH KHAMIS KITUMBO amewahakikishia timu ya RHINO RANGERS pamoja na polisi kuwa wajiandae kwani anafanya mawasiliano ili waje kuwapa nguvu kazi ya mzunguko wa pili wa daraja la kwanza FDL.

WACHEZAJI WA RHINO RANGERS WAKIWA WAMEPOOZI BAADA YA HLF TIME WAKIWA MBELE KWA BAO 2-0

WACHEZAJI WA TIMU YA KOMBAINI WILAYA  MKOA WA TABORA WAKIWA HOI BAADA YA KUPIGISHWA KWATA NA WANAJESHI KIPINDI CHA KWANZA 2-0
 
KOCHA MSAIDIZI NA MCHEZAJI WA ZAMANI WA MILAMBO DIDAS KUNDE  AKIWAPA SOMO WACHEZAJI WAKE PEMBENI NI KOCHA MKUU ANDREW ZOMA

AFCON 2013: MFALME wa MAGOLI AFRIKA, NANI KUTWAA TAJI??

>>AFCON 2012 WACHEZAJI 7 WALIFUNGANA UFUNGAJI BORA!!
AFCON_2013_LOGO>>UNAMJUA WILFRIED BONY, MWAFRIKA PEKEE ANAEONGOZA ULAYA KWA UFUNGAJI LIGI KUBWA??
AFCON 2013, Kombe la Mataifa ya Afrika, linaanza huko Afrika Kusini Januari 19 na ikifika Februari 10 Bingwa wa Afrika atapatikana miongoni mwa Nchi 16 ambazo zipo kwenye Fainali lakini pia kinyang’anyiro kingine ni ule ushindani wa Wachezaji Masupastaa kutaka kuibuka kama Mfungaji Bora, kitimtim ambacho ni kigumu hasa ukizinagatia katika Mashindano yaliyopita, AFCON 2012, yaliyochezwa Nchini Equatorial Guinea na Gabon  Mwezi Januari 2012, Wachezaji 7 walifungana kwa kupiga Bao 3 kila mmoja.
Saba hao wa AFCON 2012 ni Manucho (Angola), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Didier Drogba (Ivory Coast), Cheick Tidiane Diabate (Mali), Houcine Kharja (Morocco) Chris Katongo na Emmanuel Mayuka (Wote Zambia).
Kati ya hao 7, Drogba, Wazambia Chris Katongo na Emmanuel Mayuka, Cheick Tidiane Diabate wa Mali na Manucho wa Angola watakuwepo AFCON 2013.
Lakini, Samuel Eto’o wa Cameroun, Mchezaji ambae ndie anashikilia Rekodi ya kufunga Bao nyingi kwenye AFCON, Bao 18 katika Fainali 6, hayupo kwenye Mashindano haya kwa vile Cameroun, kwa mara nyingine tena, haimo kwenye AFCON 2013.
Mbali ya Majina yaliyozoeleka kama kina Didier Drogba, ipo ‘Mashine mpya ya Magoli’ ya Ivory Coast, Wilfried Bony, ambae anachezea Klabu ya huko Holland, Vitesse Arnhem, na tayari kwenye Ligi Nchini humo ashapiga Bao 16 katika Mechi 18 na kumfanya awe ndie aneongoza kwa Magoli kwenye Ligi hiyo, akiwa ni Mchezaji pekee toka Barani Afrika ambae anaongoza kwa Ufungaji katika Ligi kubwa huko Ulaya.
Wengine toka Afrika wanaotamba kwa Ufungaji Mabao na watakuwepo kwenye AFCON 2013 ni Lancina Traore ambae ameshaifungia Anzhi Makhachkala kwenye Ligi ya Urusi Bao 9 ikiwa ni Bao moja zaidi ya Ahmed Mussa wa CSKA Moscow ambae yupo na Timu ya Taifa ya Nigeria huko Afrika Kusini.
Manucho, ambae aliwahi kuichezea Manchester United, anazo Bao 6 kwa Klabu yake ya Spain, Real Valladolid, zikiwamo Bao 2 alizoipiga Real Madrid walipokutana Mwezi uliopita.
Mchezaji wa Togo anaecheza Tottenham Hotspur, Emmanuel Adebayor, Siku zote amekuwa akifunikwa na kina Didier Drogba na Samuel Eto’o lakini pengine safari hii ni muda wake.
WAFUNGAJI BORA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA:
-1957 (Sudan) - Ad El Diba (Egypt) MABAO 5
-1959 (Egypt) - Mahmoud Al Gohari (Egypt) 3
-1962 (Ethiopia) - Mohamed Al Badawi (Egypt), Worku Mengistu (Ethiopia) 3
-1963 (Ghana) - Ahmed Al Chazli (Egypt) 6
-1965 (Tunisia) - Abbrey Osei Kofi (Ghana), Eustace Mangli (Ivory Coast) 3
-1968 (Ethiopia) - Laurent Pokou (Ivory Coast) 6
-1970 (Sudan) - Laurent Pokou (Ivory Coast) 8
-1972 (Cameroon) - Salif Keita (Mali), 5
-1974 (Egypt) - Mulamba Ndaye (Zaire) 9
-1976 (Ethiopia) - William Njo Lea (Guinea) 4
-1978 (Ghana) - Phillip Omondi (Uganda) 4
-1980 (Nigeria) - Segun Odegbami (Nigeria) 3
-1982 (Libya) - George Al Hassan (Ghana) 4
-1984 (Ivory Coast) - Taher Abou Zeid (Egypt) 4
-1986 (Egypt) - Roger Milla (Cameroon), Abdoulaye Traore (Ivory Coast) 4
-1988 (Morocco) - Lakhdar Belloumi (Algeria), Roger Milla (Cameroon), Gamal Abdelhamid (Egypt), Abdoulaye Traore (Ivory Coast) 4
-1990 (Algeria) - Djamel Menad (Algeria) 4
-1992 (Senegal) - Rachidi Yekini (Nigeria) 4
-1994 (Tunisia) - Rachidi Yekini (Nigeria) 5
-1996 (South Africa) - Kalusha Bwalya (Zambia) 5
-1998 (Burkina Faso) - Hossam Hassan (Egypt), Benni McCarthy (South Africa) 7
-2000 (Ghana and Nigeria) - Shaun Bartlett (South Africa) 5
-2002 (Mali) - Patrick Mboma, Salomon Olembe (both Cameroon), Julius Aghahowa (Nigeria) 3
-2004 (Tunisia) - Patrick Mboma (Cameroon), Frederic Kanoute (Mali), Austin Okocha (Nigeria), Youssef Mokhtari (Morocco), Francileudo dos Santos (Tunisia) 4
-2006 (Egypt) - Samuel Eto'o (Cameroon), Ahmed Hassan (Egypt) and Francileudo dos Santos (Tunisia) 4
-2008 (Ghana) - Samuel Eto'o (Cameroon) 5
2010 (Angola) - Mohamed Nagui (Egypt) 5
2012 (Equatorial Guinea and Gabon) - Manucho (Angola), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Didier Drogba (Ivory Coast), Cheick Tidiane Diabate (Mali), Houcine Kharja (Morocco) Chris Katongo, Emmanuel Mayuka (Wote Zambia) 3.

BPL JANA ILIENDELEA NA CHELSEA KUTOA DOZI YA 4-0 NA LLEO BIG MECHI MAN U VS LIVERPOOL,ARSENAL VS MAN CITY NANI MBABE???????????

BPL_LOGO>>MBILI ZA KUJIFUNGA WENYEWE, MOJA PENATI, MOJA HAZARD!!
>>READING YAZINDUKA TOKA 2-0 NYUMA DAKIKA 8 ZA MWISHO NA KUSHINDA 3-2!!

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
MATOKEO:
Jumamosi 12 Januari 2013
QPR 0 Tottenham 0
Aston Villa 0 Southampton 1
Everton 0 Swansea 0
Fulham 1 Wigan 1
Norwich 0 Newcastle 0
Reading 3 West Brom 2
Stoke 0 Chelsea 4
Sunderland 3 West Ham 0

NORWICH 0 NEWCASTLE 0
Hii ilikuwa ni Mechi iliyopooza na sare ya 0-0 ni matokeo ya haki kwa kila Timu.
VIKOSI:
Norwich: Bunn, Martin, Bassong, Turner, Garrido, Pilkington, Johnson, Tettey, Snodgrass, Hoolahan, Jackson
Akiba: Rudd, Holt, Fox, Elliott Bennett, Barnett, Ryan Bennett, Kane.
Newcastle: Krul, Debuchy, Williamson, Coloccini, Santon, Perch, Anita, Obertan, Marveaux, Gutierrez, Cisse
Akiba: Harper, Cabaye, Amalfitano, Bigirimana, Sammy Ameobi, Ranger, Tavernier.
Refa: Anthony Taylor
FULHAM 1 WIGAN 1
Bao la kwanza kwa Franco Di Santo katika Ligi Kuu England katika Miezi mitatu leo limewapa sare ya ugenini ya Bao 1-1 walipocheza na Fulham ambao ndio walitangulia kufunga kwa kigongo cha Giorgos Karagounis cha Mita 25.
VIKOSI:
Fulham: Schwarzer, Riether, Hangeland, Hughes, Richardson, Duff, Karagounis, Ruiz, Kacaniklic, Berbatov, Petric
Akiba: Stockdale, Riise, Senderos, Baird, Kasami, Rodallega, Dejagah.
Wigan: Al Habsi, Figueroa, Caldwell, Ramis, Beausejour, McArthur, Jones, Boyce, McCarthy, Maloney, Di Santo
Akiba: Pollitt, Henriquez, Gomez, McManaman, Boselli, Stam, Golobart.
Refa: Mark Clattenburg
SUNDERLAND 3 WEST HAM 0
Wakicheza kwa kuonana sana, Sunderland wakiwa kwao Stadium of Light waliitandika West Ham Mabao 3-0.

MAGOLI:
Sunderland 3
-Larsson Dakika ya 12
-Johnson 47
-McClean 74
West Ham 0

VIKOSI:
Sunderland: Mignolet, Gardner, O'Shea, Bramble, Colback, Johnson, Vaughan, Larsson, McClean, Fletcher, Sessegnon
Akiba: Westwood, Bardsley, N'Diaye, Campbell, Wickham, McFadden, Kilgallon.
West Ham: Jaaskelainen, Demel, Collins, Reid, Potts, Collison, Diarra, Joe Cole, Nolan, Jarvis, Carlton Cole
Akiba: Spiegel, Tomkins, Vaz Te, Taylor, Diame, Chamakh, O'Neil.
Refa: Neil Swarbrick
EVERTON 0 SWANSEA 0
Kwa mara ya kwanza katika Mechi 19 za Ligi, Everton wameshindwa kupata Bao baada ya leo kutoka 0-0 na Swansea Uwanjani Goodison Park.
VIKOSI:
Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, Anichebe, Neville, Osman, Pienaar, Fellaini, Jelavic
Akiba: Mucha, Oviedo, Naismith, Hitzlsperger, Vellios, Kennedy, Duffy.
Swansea: Vorm, Tiendalli, Chico, Williams, Davies, Agustien, Ki, Rangel, Dyer, Michu, Hernandez
Akiba: Tremmel, Bartley, Britton, Graham, Routledge, Monk, de Guzman.
Refa: Phil Dowd
STOKE 0 CHELSEA 4
Bao mbili za kujifunga wenyewe na Penati ya Frank Lampard ziliwapa Chelsea ushindi wa Bao 4-0 Uwanjani Britannia dhidi ya Stoke City huku Bao lao la nne likifungwa kwa utamu sana na Eden Hazard.

MAGOLI:
Stoke 0
Chelsea 4
-Walters Dakika ya 45 & 62 [Kajifunga mwenyewe]
Lampard 65 (Penati)
Hazard 73

Mchezaji alieweka historia ya kujifunga mwenyewe mara mbili katika Mechi moja ya Ligi Kuu England ni Jon Walters ambae pia alikosa kufunga Penati waliyopewa Stoke City baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa Rafu na John Terry na kuona shuti lake la Penati likiota mbawa.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Wilkinson, Walters, Whelan, Nzonzi, Etherington, Adam, Jones
Akiba: Sorensen, Whitehead, Upson, Kightly, Crouch, Shotton, Jerome.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Cole, Hazard, Lampard, Ramires, Bertrand, Mata, Ba
Akiba: Turnbull, Torres, Oscar, Ferreira, Marin, Terry, Ake.
Refa: Andre Marriner
READING 3 WEST BROM 2
Wakiwa nyuma kwa Bao 2-0 huku zikiwa zimebaki Dakika 8 mpira kwisha, Reading walizinduka na kupiga Bao 3 ndani ya Dakika hizo zilizobaki.

MAGOLI:
Reading 3
-Kebe Dakika ya 82
-Le Fondre 88 (Penati)
-Pogrebnyak 90
West Brom 2
-Lukaku Dakika ya 19  69

Mchezaji wa Mkopo kutoka Chelsea, Romelu Lukaku, ndie alieifungia WBA Bao zao mbili lakini Reading walizinduka Dakika za mwishoni na kusawazisha na kufunga Bao la ushindi katika Dakika ya 90.
VIKOSI:
Reading: Federici, Gunter, Mariappa, Pearce, Harte, Kebe, Karacan, Daniel Carrico, Guthrie, McAnuff, Pogrebnyak
Akiba: Taylor, Le Fondre, Hunt, McCleary, Morrison, Cummings, Akpan.
West Brom: Foster, Jones, McAuley, Olsson, Ridgewell, Thorne, Brunt, Dorrans, Morrison, Thomas, Lukaku
Akiba: Myhill, Popov, Rosenberg, El Ghanassy, Dawson, Tamas, Nabi.
Refa: Kevin Friend
ASTON VILLA 0 SOUTHAMPTON 1
Penati ya Dakika 34 ya Rickie Lambert imewapa Southampton ushindi wa Bao 1-0  dhidi ya Aston Villa ambao, bila shaka, wana kila haki ya kulalamika kwani ilitolewa baada ya Jay Rodriguez kujidondosha bila kuguswa na Mtu.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Lowton, Clark, Baker, Stevens, Holman, Westwood, Delph, N'Zogbia, Benteke, Weimann
Akiba: Marshall, Vlaar, Ireland, Agbonlahor, Bowery, Bannan, Lichaj.
Southampton: Boruc, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Shaw, Rodriguez, Cork, Schneiderlin, Puncheon, Ramirez, Lambert
Akiba: Kelvin Davis, Steven Davis, Fox, Ward-Prowse, Lee, Seaborne, De Ridder.
Refa: Mark Halsey
QPR 0 TOTTENHAM 0
QPR leo walingangamara na kuweza kutoka sare ya 0-0 na Tottenham na hii ikiwa ni Mechi ya kwanza kwa Meneja wa QPR, Harry Redknapp, kukutana na Timu yake ya zamani Tottenham tangu atimuliwe huko mwanzoni mwa Msimu huu.
Shujaa wa QPR alikuwa Kipa wao kutoka Brazil Julio Cesar aliekoa Bao kutoka kwa Jermain Defoe na pia kuokoa tena mpira huo ulipomrudia Emmanuel Adebayor.
VIKOSI:
QPR: Julio Cesar, Onuoha, Hill, Nelsen, Da Silva, Mbia, Park, Derry, Wright-Phillips, Taarabt, Mackie
Akiba: Green, Ferdinand, Cisse, Ben Haim, Faurlin, Bothroyd, Campbell.
Tottenham: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton, Lennon, Dembele, Sandro, Bale, Adebayor, Defoe
Akiba: Friedel, Dempsey, Huddlestone, Parker, Sigurdsson, Assou-Ekotto, Caulker.
Refa: Lee Probert

BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man United v Liverpool
[SAA 1 Usiku]
Arsenal v Man City
Jumatano Januari 16
[SAA 4 DAK 45 Usiku]
Chelsea v Southampton
Jumamosi Januari 19
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Norwich
Man City v Fulham
Newcastle v Reading
Swansea v Stoke
West Ham v QPR
Wigan v Sunderland
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Brom v Aston Villa
Jumapili Januari 20
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Chelsea v Arsenal
[SAA 1 Usiku]
Tottenham v Man United

HALI NDANI YA REAL MADRID YAZIDI KUYEYUKA LA LIGA: REAL MAJI SHINGONI YABANWA NA VIBONDE 0-0 HIYO JANA

>>YASHINDWA KUIFUNGA OSASUNA ILIYO MKIANI!!
>>LEO VINARA BARCA DIMBANI!!
BARCA_v_REALJose Mourinho na Timu yake Real Madrid wamezidi kuingia kwenye presha kubwa ya kusakamwa na Mashabiki baada ya jana kushindwa kuifunga Osasuna ambayo ni moja ya Timu 3 zilizo mkiani baada ya kutoka sare 0-0 katika Mechi ya La Liga iliyozidi kuwathibitishia kuwa Msimu huu Ubingwa umewatoka.
Usiku wa jana ulikuwa wa balaa kwa Real Madrid ambao walicheza bila Nyota wao, Cristiano Ronaldo na Sergio Ramos, ambao wanatumikia Kifungo, nae Mchezaji wao Kaka, alieanzia Benchi, alidumu Dakika 19 tu Uwanjani na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kupata Kadi za Njano mbili na Bao lao safi lililofungwa na Jose Maria Callejon kukataliwa kwa Ofsaidi ya utata.
Matokeo hayo yamewafanya Real Madrid wawe Pointi 4 nyuma ya Atletico Madrid, walio nafasi ya pili, na Pointi 15 nyuma ya Vinara Barcelona.
Barcelona na Atletico Madrid wanaweza kuzidisha mapengo yao hayo hivi leo baada ya Mechi zao.
HUKO Italy, jana kulikuwa na Mechi mbili za Serie A kwa Bologna kuipiga Chievo Verona 4-0 na Inter Milan kuifunga Pescara 2-0.
RATIBA/MATOKEO:
LA LIGA
Jumamosi Januari 12
Real Valladolid 3 Real Mallorca 1
RCD Espanyol 1 Celta de Vigo 0
Osasuna 0 Real Madrid 0
Valencia 2 Sevilla FC 0
Jumapili Januari 13
Real Betis v Levante
Real Sociedad v Deportivo La Coruna
Atletico de Madrid v Real Zaragoza
Malaga CF v FC Barcelona
Jumatatu Januari 14
Getafe CF v Granada CF
SERIE A
Jumamosi Januari 12
Bologna 4 Chievo Verona 0
Inter Milan 2 Pescara 0
Jumapili Januari 13
Torino FC v Siena
SS Lazio v Atalanta
Parma v Juventus
Udinese v Fiorentina
Napoli v Palermo
Cagliari v Genoa
Catania v AS Roma
Sampdoria v AC Milan

BPL: LEO ni MAN UNITED v LIVERPOOL & ARSENAL v MAN CITY!!!


BPL_LOGOZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU KUHUSU BIGI MECHI ZA LEO:
MANCHESTER UNITED v LIVERPOOL
-UWANJA: Old Trafford
-TAREHE: Jumapili, 13 Januari
HALI za WACHEZAJI
Nani na Anderson wamepona maumivu yao na wamerejea kwenye Kikosi na huenda leo wakapata nafasi ya kucheza kwa wakati fulani.
Nae Wayne Rooney amepona tatizo la Goti lakini Mechi hii imedaiwa ni mapema kwake na atacheza Mechi ya marudiano ya FA Cup dhidi ya West Ham hapo Jumatano.
Liverpool watawakosa Jose Enrique na Martin Kelly na hilo litawalazimu kumchezesha Andre Wisdom kama Fulbeki wa kulia na Glen Johnson kucheza kama Fulbeki wa kushoto.
Mchezaji mpya wa Liverpool Daniel Sturridge, alienunuliwa kutoka Chelsea, leo anaweza kuanza Mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England baada ya kucheza na kufunga Bao kwenye FA CUP Wiki iliyopita Liverpool walipoifunga Mansfield Bao 2-1.
USO kwa USO 
-Manchester United wameshinda Mechi 7 kati ya 8 za Ligi zilizochezwa mwishoni Uwanjani Old Trafford na ushindi pekee wa Liverpool ni ule wa Machi 2009 waliposhinda 4-1.
VIKOSI:
Manchester United (Mfumo: 4-3-1-2): De Gea; Rafael, Ferdinand, Evans, Evra; Valencia, Carrick, Cleverley; Kagawa; Hernandez, Van Persie.
Liverpool (Mfumo: 4-3-3): Reina; Wisdom, Skrtel, Agger. Johnson; Lucas, Gerrard, Downing; Sterling, Suárez, Sturridge.
Refa: Howard Webb (Mechi 16, Kadi Nyekundu 2, Kadi za Njano 57).
ARSENAL v MANCHESTER CITY
-UWANJA: Emirates Stadium
-TAREHE: Jumapili, 13 Januari
HALI za WACHEZAJI
Arsenal huenda wakamkosa Olivier Giroud ambae alichanika Goti walipotoka sare na Swansea katika Mechi yao ya mwisho.
Baada ya kuwa nje kwa Miezi mitatu akijiuguza Paja, Kiungo Abou Diaby huenda akapata Namba baada Juzi kurejea Uwanjani kwa kuichezea Timu ya Vijana ya Arsenal ya chini ya Miaka 21.
Manchester City itawakosa Sergio Aguero, tatizo la Goti,  Samir Nasri, Kifungoni, na Ndugu wawili, Yaya na Kolo Toure, ambao wako na Timu yao ya Taifa ya Ivory Coast kwa ajili ya AFCON 2013.
USO kwa USO 
-Manchester City wameshacheza Mechi 27 za Ligi bila kushinda nyumbani kwa Arsenal. Ushindi wao wa mwisho ulikuwa Uwanja wa Highbury katika ile Ligi ya zamani ya Daraja la 1 Mwaka 1975.
-Manchester City hawajafunga hata Bao moja katika mara 5 za mwisho walizotua kwenye Uwanja wa Arsenal. Mchezaji wao wa mwisho kufunga Bao alikuwa ni DaMarcus Beasley, aliefunga Bao lao pekee walipochapwa 3-1 Aprili 2007.
VIKOSI:
Arsenal (Mfumo: 4-2-3-1): Szczesny; Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs; Arteta, Wilshere; Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Podolski; Walcott.
Manchester City (Mfumo: 4-2-3-1): Hart; Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy; Garcia, Barry; Silva, Tévez, Milner; Dzeko.
Refa: Mike Dean (Mechi 14, Kadi Nyekundu 1, Kadi za Njano 49).

WALTERS YASEMEKANA ATAMNUSURU BENITEZ KWA KUIFUNGIA CHELSEA MABAO YA KUJIFUNGA MAWILI NA CHELSEA KUSHINDA BAO 4-0 INGIA UONE ILIVYOKUWA

UKATA WA MASHABIKI MAPINDUZI WAONEKANA BAADA YA KUPATA SHILINGI MIL.41 TU KWA MECHI 15



JUMLA ya Sh. Milioni 41.3 zimepatikana kutokana na viingilio vya mechi za Kombe la Mapinduzi, michuano iliyomalizika visiwani hapa jana kwa Azam FC kuibuka bingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Aman Ibrahim Makungu alisema jana kwamba, hadi jana wamepata kiasi hicho tu cha fedha kutokana na viingilio.
Aidha, Makungu amesema wadhamini wa michuano hiyo wamechangia kiasi cha Sh. Milioni 67 na kwamba hiyo ndiyo siri ya kufanikiwa kwa mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Mapinduzi.
Mapato hayo yanatokana na jumla ya mechi 15 za mashindano ya mwaka huu hadi fainali jana, kuanzia hatua ya makundi. Timu nane zilishiriki mashindano haya, ambazo ni Simba SC ya Dar es Salaam, Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba zilizokuwa Kundi A, Azam FC ya Dar es Salaam, Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union ya Tanga na Miembeni ya Unguja zilizokuwa Kundi B.
Kutoka Kundi A, Tusker walifuzu kama vinara, wakati Simba SC walifuzu kama washindi wa pili na Kundi B Azam FC walifuzu kama washindi wa kwanza na Miembeni washindi wa pili. Katika Nusu Fainali, Azam iliitoa Simba SC kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120, wakati Tusker walitumia dakika 90 kuibanjua Miembeni 2-0.
Azam FC jana usiku walitetea Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1.
Kwa ushindi huo, Azam walizawadiwa Sh. Milioni 10, wakati washindi wa pili Tusker wamepata Sh. Milioni 5
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ramadhan Rajab Ibada ‘Kibo’ aliyesaidiwa na Mwanahija Makame Mfumo na Mgaza Kindundi, hadi mapumziko hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.
Azam ndio walioshambulia zaidi katika kipindi hicho, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga bao japo moja. Gaudence Mwaikimba alipewa pasi nzuri na Brian Umony dakika ya 44, lakini shuti lake kali lilidakwa na kipa Samuel Odhiambo.
Kipindi cha pili, Tusker walirudi na moto mkali na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Azam.
Hiyo iliwasaidia mabingwa hao wa Kenya kupata bao dakika ya 60, lililofungwa na Jesse Were aliyeunganisha kwa shuti kali la kimo cha mbuzi pasi ya Robert Omunok.
Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha dakika ya 72 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na beki Mkenya, Joackins Atudo baada ya beki wa Tusker, Luke Ochieng kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Katika dakika mbili za nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 90 za mchezo huo, alijitokeza binti mwenye umri kati ya 14 na 16 na kukatiza uwanjani akitokea jukwaa la Urusi.
Refa alijaribu kumsimamisha, lakini aliendelea kukatiza Uwanja hadi nje ambako alipokewa na askari Polisi na kutolewa nje kabisa ya Uwanja. Mtangazaji wa Uwanja wa Amaan, Farouk Karim aliwatuliza mashabiki akisema binti huyo ametoroka hospitali ya vichaa, Kidongo Chekundu na tayari Polisi wamemkamata na kumrejesha huko.
Hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30.
Gaudence Exavery Mwaikimba aliipatia Azam bao la ushindi dakika ya pili tu tangu kuanza kwa muda wa nyongeza baada ya kuwazidi nguvu na maarifa mabeki wa Tusker.
Aidha, Jesse Were mshambuliaji wa Tusker aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matano na kuzawadiwa Sh. 300,000, akifuatiwa na Joackins Atudo wa Azam aliyefunga mabao matatu sawa na Adeyum Saleh Ahmed wa Miembeni.
WAFUNGAJI WA MABAO:
Jesse Were                     Tusker FC     5
Joackins Atudo                Azam FC       3
Adeyum Saleh                 Miembeni      3
Gaudence Mwaikimba      Azam FC      2
Haruna Chanongo            Simba SC    2
Mfanyeje Mussa               Jamhuri        2
Michael Olunga                Tusker FC    2
MATOKEO YA MECHI ZOTE KOMBE LA MAPINDUZI 2013:
Janauri 2, 2013
Tusker 5-1 Bandari
Simba SC 2-2 Jamhuri
Januari 3, 2013
Mtibwa Sugar 1-4 Miembeni
Azam FC 0-0 Coastal Union  
Januari 4, 2013
Jamhuri 2-1 Bandari
Simba SC 1-1 Tusker FC
Januari 5, 2013
Mtibwa Sugar 1-1 Coastal Union
Miembeni 1-2 Azam
Januari 6, 2013
Tusker 1-0 Jamhuri
Simba SC 1-1 Bandari
Januari 7, 2013
Miembeni 0-0 Coastal Union
Azam FC 0-0 Mtibwa Sugar
Januari 9, 2013; NUSU FAINALI
Azam FC 2-2 Simba SC (penalti 5-4)
Januari 10, 2013; NUSU FAINALI
Tusker FC 2-0 Miembeni FC
Januari 12, 2013; FAINALI
Azam FC 2-1 Tusker FC
ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA MAPINDUZI
2003   Mtibwa Sugar
2004   Yanga SC
2005   Yanga SC
2006   Simba SC
2007   Yanga SC
2008   Simba SC
2009   Miembeni FC
2010   Mtibwa Sugar
2011   Simba SC
2012   Azam FC
2013   Azam FC

MBIO ZA MARATHONI ZINATARAJIA KUWA NA WASHIRIKI 600


George Kavishe

MBIO za Kilimanjaro Marathon mwaka huu zinatajiwa kuwa na washiriki wa kigeni wapatao 600 kutoka nchi zaidi ya 40.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana kuwa mbio hizo zinaendelea kuwavutia washiriki wengi wa kimataifa kutokana na jitihada za pamoja zinazofanywa na waandaaji pamoja na bia ya Kilimanjaro Premium Lager katika kutangaza tukio hili. Hii ndi sababu iliyochangia ukuaji wa mbio hizi pamoja na ushiriki kuongezeka kila mwaka.
Addison alisema washiriki wengi zaidi watatoka Marekani ikifuatiwa na Uingereza. Nchi nyingine zinazotarajiwa kushiriki ni pamoja na Canada, Japan, Uganda, Zimbabwe na Kenya. Nyingine ni pamoja na Sweden, Australia, Hungary, Germany,  Zambia, Morocco, Swaziland, Nigeria na Malawi.
Zikiwa zimepangwa kufanyika Moshi tarehe 3 Machi 2013, mbio za Kilimanjaro Marathon zitakuwa zimegawanyika katika sehemu nne ambazo ni 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon,  21km Half Marathon, GAPCO Disabled Half Marathon na Vodacom 5km Fun Run.
Mbio hizo pia zinatarajiwa kuchangamshwa na ushiriki wa timu za makampuni ambapo wafanyakazi wa makampuni wadhamini watashindana katika mbio ya nusu marathon kupitia shindano litakalojulikana kama“Half Marathon Corporate Challenge”. Makampuni ambayo yameishathibitisha kushiriki shindano hilo ni pamoja na TPC Sugar ambao ndio mabingwa watetezi wa shindano hilo wakifuatiwa na CFAO Motors, TanzaniteOne na Tanga Cement.
Addison alisema kuwa mbio za Kilimanjaro Marathon zinaingia katika mwaka wa 11 tangu kuanzishwa zikiwa zimesajiriwa rasmi na shikisho la riadha la kimataifa na kuongeza kuwa kutakuwepo na vituo vya maji pamoja na viburudisho katika njia ya mashindano hayo.
“Mbio hii inafanyika chini ya Mlima Kilimanjaro ambapo kila mtu anaweza kukimbia kwa raka kwani urefu wake kutoka usawa wa bahari ni wastani wa mita 830 mpaka 1150 katika barabara nzuri yenye lami. Inatarajiwa kuwa shamrashamra maana wananchi wengi  watajitokeza pembezoni mwa barabara kuwashangilia na kuwapa moyo wakimbiaji, na wakimbiaji wa kujifurahisha wanaweza hata kusimama kupata kiburudisho njiani”, Addison aliitimisha.
Mbio hizo zinadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (wadhamini wakuu), Vodacom Tanzania (5km Fun Run), GAPCO (Disabled Half Marathon), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, TanzaniteOne, New Arusha Hotel na Kilimanjaro Water.

YANGA WAMALIZA MAKALI YAO YA PROGRAMU YA MAZOEZI UTURUKI




Timu ya  Young Africans leo asubuhi imemaliza mazoezi  yake kwa kufanya mazoezi ya kujenga mwili na uimara (Gym) iliyopo katika hoteli ya Fame Residence leo asubuhi na yakiwa ndio mazoezi ya mwisho katika kambi ya mafunzo ya wiki mbili iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya Fame Residence Football mijini Antlaya.

Kocha mkuu Ernest Brandts akishirikiana na Fred Felix Mizniro na Razaki Siwa leo waliongoza mazoezi ya Gym kuanzia majira ya saa tatu na nusu asubuhi mpaka majira ya saa saa tano na nusu asubuhi ambapo baada ya mazoezi hayo wachezaji wamepewa nafasi ya kupumzika kujiandaa na safari ya hapo kesho kurudi Tanzania.
 
Akiongelea michezo ya kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.
 
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za  mchezo licha ya Arminia kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
 
Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la utata  kisha kupewa penati ya utata pia.
 
Mchezo wa mwisho dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini wa washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango Yusuph abDUL
 
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano yatakayotukabili alisema 'Brandts'
Ally Mustafa 'Barthez, na Nizar Khalfani wakifanya mazoezi ya Gym leo asubuhi katika hoteli ya Fame Residence

WAKALI WA SIMBA NA YANGA JANA WALILEWESHWA NA UTAMU WA ICECREAM 2-1 AMAAAN

Mgeni rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Mapinduzi, Nahodha wa Azam FC, Himid Mao Mkami usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya timu hiyo kutwaa taji hilo kwa kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1 ndani ya dakika 120.

Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akigombea mpira na beki wa Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 
Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akimtoka mpira na beki wa Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 

Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akikimbia na mpira dhidi ya beki wa Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 
Mwaikimba akifumua shuti
Mshambuliaji wa Azam FC, Seif Abdallah akimiliki mpira mbele ya beki wa Tusker FC, Bright Jeremiah katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 
Mshambuliaji wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba akimtoka beki wa beki wa Tusker FC, Joseph Shikokoti katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi usiku wa leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Azam ilishinda 2-1 ndani ya dakika 120 na kutwaa Kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. 
Shuti la bao, Mwaikimba akiwa amefumua shuti kuifungia Azam bao la ushindi
Wachezaji majeruhi wa Azam, John Bocco 'Adebayor' kushoto na Abdulhalim Humud 'Gaucho' kulia wakiingia uwanjani leo
Mpira uko nyavuni, mkwaju wa Penalti wa Joackins Atudo umetinga kimiani kuipatia Azam bao la kusawazisha huku kipa Samuel Odhiambo akigagaa chini 
Hongera shujaa Mwaikimba, wachezaji wa Azam wakimpongeza mfungaji wa bao lao la ushindi
Kikosi cha ubingwa leo
Washindi wa pili Tusker FC kikosi chao cha leo
Nahodha Himi Mao akiinua juu burungutu la fedha, Sh. Milioni 10 za ubingwa 
Mgeni rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akimkabidhi donge nono la Sh. 300,000 mfungaji bora wa Kombe la Mapinduzi, Jesse Were wa Tusker FC aliyemaliza na mabao matano usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Binti aliyevamia uwanjani dakika ya 89 akitolewa nje na askari Polisi

Mgeni rasmi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) akimkabidhi Kombe la ushindi wa pili wa Mapinduzi, Nahodha wa Tusker FC, Joseph Shikokoti usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Polisi wakimtoa nje binti aliyevamia uwanjani dakika ya 89

Azam wakisherehekea na Kombe lao

Mwaikimba akifuaria na mashabiki Kombe lililotokana na juhudi zake 
Azam wakisherehekea na Kombe lao
Brian Umony wa Azam amemuacha chini Joseph Shikokoti wa Tusker FC
Umony na Shikokoti
Mwaikimba aliyeruka hewani kuiga kichwa kwenye lango la Tusker kufuatia mpira wa kona
Mwaikimba mawindoni


Mwaikimba mbele ya Shikokoti