AFCON 2013: UHABA WA MABAO WATAWALA MECHI ZA UFUNGUZI.
HALI ya baridi kali,
mvua, soka lisilovutia na uhaba wa mabao ndio mambo yaliyoonekana
kuchukua nafasi katika ufunguzi wa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon
inayofanyika nchini Afrika Kusini jana. Michuano
ya 29 inayoandaliwa na Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF kuanzia
mwaka 1957 ilishuhudia michezo miwili kuisha ya kundi A kumalizika huku
hakuna timu iliyoona lango la mwenzake. Wenyeji
wa michuano hiyo Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana walishindwa
kuwapa raha mashabiki wao wapatao 85,000 waliojitokeza katika Uwanja wa
Soccer City jijini Johannesburg pale alipong’ang’aniwa na timu ngeni
katika mashindano hayo ya Cape Verde. Baada
ya mchezo ulifuatiwa na mchezo mwingine katika huohuo kati ya Morocco
na Angola lakini mpaka dakika tisini zinamalizika hakuna timu iliyoona
lango la mwenzake. Michuano
hiyo inaendelea tena baadae leo kwa michezo miwili ya kundi B ambapo
katika mchezo wa kwanza Ghana itacheza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo-DRC ukifuatiwa na mchezo kati ya Mali na Niger katika Uwanja wa
Nelson Mandela Bay jijini Port Elizabeth.
No comments:
Post a Comment