Monday, December 3, 2012

STARS YATINGA NUSU FAINALI TUSKER CHALLEN

 


Wafungaji wa mabao ya Stars leo, Kiemba kulia na Bocco kushoto wakipongezana
TANZANIA Bara imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge baada ya kuilaza Rwanda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Lugogo mjini hapa mchana huu.
Hadi mapumziko, Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na kiungo Amri Kiemba, dakika mya 33 akiunganisha pasi ya Mwinyi Kazimoto aliyewapunguza wachezaji wawili wa Rwanda kabla ya kutoa pasi maridadi.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Mohamed El Fadil kutoka Sudan, mshambuliaji John Raphael Bocco ‘Adebayor’ alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Rwanda na aliwafanya waende kwenye vyumba vya kupumzikia wakiwa hoi.
Katika hicho kipindi cha kwanza, Rwanda walikosa bao la wazi dakika ya 12 baada ya krosi ya Jean Claude Iranzi kuokolewa na beki Kevin Yondan kwa kichwa na dakika ya 19 Jean Baptiste Mugiraneza alipiga juu akiwa nje kidogo ya eneo la hatari.
Stars pamoja na kufunga bao hilo kipindi hicho cha kwanza, katika dakika ya 30 krosi nzuri ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa na Bocco walishindwa kuiunganisha na ikawapita wote.
Ngassa tena, katika dakika ya 38 alipiga shuti kali kutoka wingi ya kushoto, lakini likaenda nje sentimita chache.
Kipindi cha pili,
Kipindi cha pili Stars walirudi vizuri tena na kuendelea kucheza kwa kuonana, ingawa na Rwanda nao waliendelea kucheza kwa bidii kutafuta bao la kusawazisha.
Hata hivyo, walikuwa ni Stars tena waliofanikiwa kupata bao la pili 53 baada ya John Bocco kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Jean Claude Ndoli kufuatia shuti kali la Mwinyi Kazimoto kutoka nje ya eneo la hatari.
Baada ya bao hilo, Rwanda walionekana kupagawa, lakini hawakusahau kushambulia lango la Stars na dakika ya 86 Dadi Birori hakujali ameotea akasukuma mpira nyavuni, lakini refa akakataa bao hilo.
Kwa ushindi huo, Stars sasa inasubiri mshindi kati ya Uganda na Ethiopia kesho kukutana naye kwenye Nusu Fainali.
Stars; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Amri Kiemba, Salum Abubakar/Athumani Iddi dk51, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa na John Bocco/Shaaban Nditi dk 85.
Rwanda; Jean Claude Ndoli, Emery Basiyenge, Ismail Nshutimayamangara/Fabrice Twagizimana dk19, Jimmy Mbaraga/Imran Nshiyimana dk67, Charles Tibingana/Barnabe Mbuyumbyi dk61, Michel Rusheshangoga, Jean Baptiste Mugiraneza, Haruna Niyonzima, Jean Claude Iranzi, Dadi Birori na Tumaine Ntamuhanga. 

 

CECAFA TUSKER CUP: KILIMANJARO STARS USO KWA USO NA ZANZIBAR HEROES NUSU FAINALI.

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Cecafa Tusker Cup kwa kuifunga Rwanda kwa mabao 2-0 katika Uwanja wa KCC uliopo eneo la Lugogo, Kampala Uganda. Katika mchezo huo ambao vijana wa Kilimanjaro walionyesha ufundi mkubwa na kuwafunika kabisa Rwanda walifanikiwa kupata bao la kwanza katika dakika ya 33 bao ambalo lilifungwa na kiungo Amri Kiemba baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Mwinyi Kazimoto. Bao hilo lilionyesha kuamsha ari ushindi wa ambapo Kilimanjaro waliongeza kasi ya mashambulizi na kukosa mabao kadhaa kabla ya timu hizo hazijakwenda mapumziko Rwanda au Amavubi wakiwa vichwa chini kwa kuwa nyuma kwa bao moja. Vijana wa Kilimanjaro ambao wananolewa na kocha Kim Poulsen walianza kupindi cha kwa kasi kubwa na kuenyesha hawakutosheka na bao walilopata katika kipindi cha na juhudi zao hizo zilizaa matunda dakika ya 55 baada ya John Bocco kufunga bao la pili akimalizia mpira uliotemwa na kipa baada ya kushindwa kumudu kunyaka shuti kali la Kazimoto. Kikosi cha Amavubi ambacho kilikuwa kikiongozwa na nahodha wake Haruna Niyonzima katika mchezo wa leo hakikuonyesha kuwa na madhara sana kwa vijana wa Kilimanjaro baada ya kubanwa kila idara. Katika robo fainali nyingine Zanzibar Heroes nayo ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Burundi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5 baada ya timu hizo kutoka sare ya bila ya kufungana katika muda wa kawaida. Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Zanzibar Heroes watakutana na ndugu zao Kilimanjaro Stars katika nusu fainali ya michuano hiyo.

UHALIFU HUPUNGUA PINDI CHICHARITO ANAPOKUWA AKICHEZA - POLISI.

NYOTA wa kimataifa wa Mexico na klabu ya Manchester United, Juvier Hernandez amekuwa maarufu nchini kwake mpaka kufikia hatua ya matukio ya uhalifu kupungua pindi anapocheza. Mbali na uhalifu kupungua lakini wanawake wajawazito wanaokaribia kujifungua nao hushikwa na uchungu kwa furaha pindi nyota huyo anapoifungia bao timu yake ya United hivyo idadi ya watoto kuzaliwa kuongezeka. Ofisa wa juu wa polisi wa mji mkuu wa nchi hiyo Mexico City, Jorge Carlos Martinez amesema kuwa uhalifu kama wa kuteka magari, uvamizi na ukabaji hupungua na inavyoonekana wahalifu hutumia muda huo kumuona shujaa wao wakati anacheza. Ofisa huyo wa polisi amesema kuwa ana matumaini meneja wa United Sir Alex Ferguson ataendelea kumtumia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 wakati wa kipindi hiki ambacho mji huo unakumbwa na matukio mengi ya uhalifu. Watu zaidi ya 15,000 huuliwa kila mwaka na magenge ya wauza madawa ya kulevya.

TASWA KUFANYA MKUTANO MKUU BAGAMOYO.

Amir Mhando, Katibu Mkuu TASWA.
MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utafanyika Desemba 21 na 22 mwaka huu Kiromo View Resort Hotel, Bagamoyo mkoani Pwani. Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha wanachama 100, na pia watakuwepo wadau mbalimbali wa TASWA wakiwemo waandishi wakongwe wa habari za michezo wambao watapewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano huo. Wanachama wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama, Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu waandishi wa habari za michezo kwa ujumla. Pia kutakuwa na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo ili wawe na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo itajadiliwa kwenye mkutano huo. Kamati ya Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea kwa kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza iwaite wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na kukishakuwa na uelewa wa kutosha suala hilo lipelekwe kama ajenda kamili ya kuanzisha chama hicho kwenye Mkutano Mkuu. Nia yetu ni kuona tunapiga hatua za kimaendeleo na kuwafanya wanachama wetu wafurahie kujiunga na chama hiki na waweze kupata mikopo ya kuwasaidia katika masuala mbalimbali. Tunawaomba wanachama wote ambao wanatarajia kuhudhuria mkutano huo wathibitishe ushiriki wao kwa Katibu Mkuu wa TASWA kwa njia ya email: mgosius@yahoo.com au taswatz@yahoo.com. Mwisho wa kuthibitisha ni Desemba 15, 2012 saa kumi alasiri ili maandalizi mengine yaendelee na uwepo wao katika mkutano uthaminike. Wanachama ambao wanajua hawajalipa ada ni vyema wakafanya hivyo, kwa kuwasiliana na Mhazini Mkuu wa TASWA, vinginevyo chama kitafanya utaratibu mwingine wa kuhakikisha ada zao zinapatikana siku ya mkutano. TASWA inaendelea na mazungumzo na wadhamini mbalimbali na Jumatatu Desemba 10, 2012 saa tano asubuhi katika mgahawa wa City Sports Lounge Dar es Salaam itatangaza mdhamini wa mkutano huo.

MARIGA AREJEA UWANJANI.

KIUNGO wa kimataifa wa Kenya, Mcdonald Mariga ameshindwa kuzuia kuonyesha furaha yake wakati aliporejea tena uwanjani wakati Inter Milan ikishinda bao 1-0 dhidi ya Palermo Jumapili Jioni. Mariga amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi nane baada ya kuwa majeruhi na kudai kuwa kilikuwa kipindi kigumu mno lakini anashukuru amepona na amerejea tena kuitumikia klabu yake ya Inter. Kocha wa Inter, Andrea Stramaccioni alimpanga Mariga katika kikosi chake ikiwa ni mara ya kwanza msimu huu kwa mkenya huyo kucheza mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A. Pamoja na kushindwa kufunga katika mchezo huo Mariga alionyesha kufurahishwa kurejea tena uwanjani na kuahidi kufanya vizuri zaidi huko mbeleni kama atapewa nafasi ya kucheza mara nyingi zaidi. Mariga alitengeneza historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati huo Jose Mourinho ambaye ni kocha Real Madrid ya Hipsnia kwasasa alipokuwa akiifundisha Inter Milan. 

ADEBAYOR AJIENGUA KUSHIRIKI MATAIFA YA AFRIKA.

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Tottenham Hotspurs Emmanuel Adebayor amempa ahueni kocha wake Andre Villas-Boas baada ya kujiondoa kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika ambayo inatarajiwa kufanyika Januari mwakani. Adebayor mwenye umri wa miaka 28 alitishia kujitoa katika timu ya taifa ya Togo kama wachezaji ahwatalipwa fedha ambazo walikuwa wakidai katika Shirikisho la Soka la nchi hiyo. Akihojiwa nyota huyo amesema kuwa kama hakutakuwa na mabadiliko yoyote atastaafu rasmi soka la kimataifa na wachezaji wengi wataacha kuichezea nchi yao. Kufuatia shirikisho la nchi hiyo kushindwa kutatu suala hilo mshambuliaji huyo ambaye amewahi kucheza katika klabu za Arsenal na Manchester City aliamua kujiondoa kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika yatakayofanyika nchini Afrika Kusini ili kuonyesha msisitizo wa nia yake.

ABRAMOVICH KUMUITA GRANT ILI KUMUONGEZEA NGUVU BANITEZ.

MMILIKI wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich anafikiria kuchukua hatua ya kushangaza ambayo itashuhudia kocha wa zamani wa klabu hiyo Avram Grant akirejea Stamford Bridge. Abramovic ambaye ni raia ya Urusi anahofia kuwa alifanya makosa kumleta Rafa Banitez kuinoa klabu hiyo na anaona kuna umuhimu wa kumuita tena Grant ili awe mshauri wa Banitez ili kutatua tatizo la klabu hiyo kuboronga. Toka Banitez apewe mikoba ya kuinoa klabu hiyo katika michezo mitatu iliyopita ameshindwa kubata ushindi na amekuwa akipata upinzani mkali kutoka kwa mashabiki ambao hawakufurahishwa na uteuzi wake. Baada ya kipigo cha mabao 3-1 walichopata kutoka kwa West Ham United Jumamosi, Abramovic alizungumza na viongozi wa klabu hiyo kuangalia uwezekano wa kumleta Grant ambaye alimtimua mwaka 2008 baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ili amsaidie Banitez. Grant ambaye ni raia wa Israel amekuwa hana kibarua chochote toka alipoacha kuifundisha klabu ya Partizan Belgrade mwishoni mwa msimu uliopita.

JOHN BOCCO WA PILI KWA UBORA DUNIANI WIKI ILIYOPITA, AMPIKU HADI INIESTA WA BARCELONA


John Bocco
World Player of the Week
Mario Gotze 
AGE20
POSITIONMidfielder
FORBorussia Dortmund
WEEK IN NUMBERS
APPS (GOALS SCORED)2 (1)
TIME ON PITCH153
PREVIOUS WINS0
Ajax
Mainz
1-4
1-2
Borussia Dortmund
Borussia Dortmund

Mario Gotze was in scintillating form this week as Borussia Dortmund laid down a marker both in the Bundesliga and the Champions League, and took his personal tally to two goals and seven assists in his last five appearances.

The 20-year-old was simply too hot to handle for Ajax on Wednesday, setting up three goals for the rampant German champions, while notching a strike of his own.

On Saturday, the Germany starlet was pivotal again as his side maintained their hopes of clinching a third consecutive Bundelisga title, picking out Robert Lewandowski with a delightful pass for the game's decisive goal.

@GeoffKm on  says: "#WPOTW should easily go to Mario Gotze, his performance against Ajax was Messi-like, plus it confirmed first place in group D!"

Goal.com Germany expert Christian Ehrhardt was equally impressed with Gotze's past week: "Right before the match against Ajax, Gotze played 'Hacky-Sack' with his chewing-gum and this shows the coolness of this young and talented player. He spit out his gum, kicked it into the air four times and caught it with his mouth again (see above video).

"When he was sidelined with his injury a lot of critics predicted some sort of decline in his career. But he responded and as you can see on the pitch and in this video, he got his laughter back, and he's playing with a lot of fun!"

Congratulations to Mario Gotze, Goal.com's 184th World Player of the Week winner!

The Shortlist
John Bocco - Tanzania
Goal.com's Dennis Mabuka: "Popularly compared to Emmanuel Adebayor in Tanzania, he has a great partnership with Morisho Ngassa."
Andres Iniesta - Barcelona
 @CampNouboY: "Simply unbelievable. Take a bow!"

Goal.com's Ben Hayward: "The midfielder even outshone Lionel Messi against Levante, which is just about the highest praise a player can receive at the moment."
Felipe Melo - Galatasaray
@ardaeroll "How many times can you see a midfielder saving a penalty???"Goal.com's Oguz Ozturk: "After Melo palmed Turkdogan’s shot to safety, he crawled along the floor, pulling a silly face to celebrate as his team-mates rushed to congratulate him."
Philippe Mexes - AC Milan
@Mosbah98 on Twitter: "Mexes. How can we forget his overhead-kick goal??"
Goal.com's Kris Voakes: "Massimiliano Allegri said he was very proud of his players in what was a very big week, and he can have been no more proud with anyone than he was Mexes."

JOHN BOCCO ATABIRIWA MAISHA SUPERSPORT

John Bocco 'Adebayor'

JOHN Raphael Bocco amezidi kuwa gumzo kubwa katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayoendelea mjini hapa.
Wapiga picha wa Televisheni ya SuperSport wanamsifia sana Bocco na wanasema kuna uwezekano sasa klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini ikamgeukia tena.
“Amefunga katika kila mechi aliyocheza, huyu ni mfungaji wa uhakika, ni mshambuliaji mwenye nguvu, kasi na uwezo wa kumiliki mpira, anapiga sana vichwa, ana kiwango cha kucheza PSL (Ligi Kuu ya Afrika Kusini),”alisema mmoja wa wapiga picha hao jana.
Jamaa wa SuperSport wanemuhesabia Bocco hata bao ambalo alifunga kwenye mechi dhidi ya Burundi lakini refa akakataa, ndiyo maana wanasema amefunga katika kila mechi.
Hadi sasa, rasmi Bocco ana mabao manne, ukiondoa hilo ambalo refa ameminya. Alifunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Sudan na akarudia kufunga idadi hiyo dhidi ya Somalia.
Bocco anazidiwa bao moja tu na Mrisho Khalfan Ngassa, aliyefunga matano, lakini yote katika mechi moja dhidi ya Somalia.    
Bocco maarufu kwa jina la utani ‘Adebayor’ anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam, alifanya vizuri katika majaribio yake kwenye klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini Agosti mwaka huu, lakini klabu hiyo ikashindwa kufika dau la kumng’oa Chamazi.
SuperSport ilivutiwa na soka ya Bocco, katika michuano ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Julai mwaka huu mjini Dar es Salaam hivyo kumuita kwa majaribio, ambayo alifuzu.
Katika Kombe la Kagame, Bocco alifunga mabao matano na kushika nafasi ya tatu katika wafungaji bora, nyuma ya Hamisi Kiiza aliyefungana na Tadi Etikiama kwa mabao sita, na Said Bahanuzi wa Yanga, aliyeibuka mfungaji bora kwa mabao yake saba.
Lakini Bocco pia alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, kwa mabao yake 18 akiwapiku hadi washambuliaji wa kigeni waliocheza ligi hiyo msimu huo, Emmanuel Okwi, Kenneth Asamoah, Davies Mwape na Dalington Enyiana.
Tangu aipandishe Ligi Kuu Azam FC msimu wa 2008/2009 kwa mabao yake, akiibuka mfungaji bora wa Ligi Daraja la Kwanza, Bocco amekuwa akiingia kwenye mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu, msimu wa kwanza akizidiwa na Boniphace Ambani aliyekuwa Yanga, msimu wa pili Mussa Mgosi aliyekuwa Simba na msimu wa tatu na Mrisho Ngassa, kabla ya msimu uliopita kutimiza ndoto zake za kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo.
Iwapo atanunuliwa na SuperSport, Bocco ataweka historia ya kuwa mchezaji wa pili wa Tanzania kuchezea klabu hiyo, baada ya Suleiman Matola 2005 hadi 2007, akitokea Simba SC.

AZAM WATUA KAMPALA KUSAKA SAINI, OKWI...

Okwi katika Challenge ya mwaka huu

AZAM FC wametuma mwakilishi wao hapa kufuatilia wachezaji katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Masahariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayoendelea mjini hapa tangu Novemba 24, hadi Desemba 8, mwaka huu.
Mwakilishi huyo alitua hapa jana na kuanzia leo ataanza kufanya kilichomleta mjini hapa.
Rasmi Azam inakuwa klabu ya pili kutuma mwakilishi wake hapa baada ya El Merreikh ya Sudan.
Mapema mwanzoni mwa mashindano haya, ilielezwa wawakilishi wa Simba, Yanga na Coastal Union watakuja pia hapa kutazama vipaji vya kuongeza katika klabu zao, lakini hadi jana hakukuwa na taarifa za mwakilishi yoyote wa klabu hizo kufika hapa.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal Union, Nassor Bin Slum ilielezwa atatua leo sawa na Seif Ahmad ‘Seif Magari’, Abdallah Ahmad Bin Kleb wa Yanga na Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ wa Simba.
Kiongozi wa zamani wa Simba SC, Alhaj Juma Nkamia, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini yeye tayari yupo hapa kwa wiki nzima, lakini ameletwa na mapenzi yake kwa timu yake ya taifa.
Kuna wasiwasi, mmoja wa wachezaji ambao Azam imekuja kuwatazama huku ni mshambuliaji wa Simba SC, Mganda Emmanuel Okwi ambaye inadaiwa mkataba wake umemalizika, ingawa klabu yake imesema unaisha Mei mwakani.  

APR WATAKA KUIPIKU YANGA BOOONGE LA STRIKER

Taddy Etikiama

KLABU ya A.P.R. ya Rwanda inataka kumsajili mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Taddy Etikiama wa A.S. Vita.
Etikiama anayeichezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, akitumia jina la Dadi Birori, tayari amekwishaonyesha nia ya kujiunga na Yanga.
Habari kutoka ndani ya kambi ya Rwanda, zimesema kwamba A.P.R. inayomilikiwa na jeshi la nchi hiyo imevutiwa na uwezo wa mchezaji huyo na kwa kuwa amekwishamaliza mkataba wamke Vita, inataka kumsajili.
“Huyu Dadi APR wanataka kumsajili, akirudi tu Kigali watazungumza naye, na kwa vile amekwishamaliza mkataba wake AS Vita, watamsajili, ni  mzuri sana,”kilisema chanzo kutoka kambi ya Rwanda, hoteli ya Sports View mjini hapa.
Mwishoni mwa wiki, Etikiama aliwaambia Yanga SC ya Dar es Salaam, wasikosee kusajili mshambuliaji mwingine yeyote zaidi yake, kwani yeye ndiye mkali anayewafaa zaidi.
Akizungumza mjini uganda , Taddy ambaye hadi ameifungia Rwanda mabao mawili katika Kombe la CECAFA Tusker Challenge alisema kwamba huu ni wakati mzuri Yanga kumsajili, kwani amemaliza mkataba na klabu yake A.S. Vita ya DRC.
Alisema anaijua Yanga vizuri na mfumo wake wa uchezaji pia na anaamini akijiunga nayo atawafungia sana mabao. “Najua wana wapinzani wao wakubwa, Simba, mimi nikisajiliwa Yanga nitakuwa nawafunga sana hao Simba,”alisema Etikiama na kuongeza.
“Mimi ni mkali kweli, nimekuwa mfungaji bora wa Kongo (DRC), nimefunga mabao 15 ligi yenye timu nzuri kama TP Mazembe, St Eloi Lupopo na DC Motema Pembe, nimewashinda akina Mbwana Samatta, Yanga wakinipata watapata mchezaji mzuri wa ushindi,”alisema.
Taddy alikuwa na A.S. Vita kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambayo Yanga iliibuka bingwa.
Katika mashindano hayo yaliyofanyika mjini Dar es Salaam Taddy alikaribia kuwa mfungaji bora baada ya kushika nafasi ya pili kwa mabao yake sita, nyuma ya Said Bahanuzi wa Yanga aliyefunga saba na kutwaa kaitu cha dhahabu cha michuano hiyo.
Taddy alifunga idadi sawa ya mabao na mshambuliaji mwingine wa Yanga, Hamisi Kiiza ‘Diego‘, ambaye katika Challenge hii naye anachezea nchi yake, Uganda.   

EL MERREIKH YAVAMIA ANGA ZA SIMBA, CHELEWA CHELEWA UTAKUTA MWALI SI WAKO

Umony akiwa na ramadhan Sarpei,

MSHAMBULIAJI wa Uganda, Brian Umony amekwishasema yuko tayari kujiunga na klabu ya Simba ya Dar es Salaam, lakini kabla Wekundu hao wa Msimbazi hawajachukua hatua yoyote, El Merreikh ya Sudan imetuma mwakilishi wake hapa azungumze na mchezaji huyo.
Habari  zimesema kwamba, Merreikh inayosuka upya kikosi chake baada ya kukosa ubingwa wa Sudan, imetuma mwakilishi wake hapa afanye mazungumzo na Umony, aliyekoswakoswa kidogo tu na Simba mwaka 2009, alipokuwa KCC ya hapa.
Mwandishi mmoja wa habari wa Sudan, alisema  jana katika hoteli ya Silver Springs mjini hapa kwamba, tayari mwakilishi huyo wa Merreikh yuko hapa kwa kazi hiyo.
Aidha, Mwandishi huyo amesema mwakilishi huyo wa Merreikh atatazama vipaji zaidi kuanzia hatua ya Robo Fainali kwa ajili ya kupendekeza wachezaji wapya wa kusajiliwa na klabu hiyo. 
Mwandishi huyo alisema tayari Merreikh pia imekubaliana biashara na Yanga juu ya kiungo Haruna Niyonzima, Nahodha wa Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge. 
Mwishoni mwa wiki, akizungumza mjini uganda baada ya kuiongoza Uganda kuifunga Sudan Kusini maao 4-0 katika mechi ya mwisho ya Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA Tusker Challenge, Umony alisema Simba kama wanamtaka wamfuate haraka wamalizane.
Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na Express baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu.

KILA LA HERI STARS NA HEROES ROBO FAINALI TUSKER CHALLENGE LEO, MAANA NI SHUGHULI PEVU

Kikosi cha Tanzania Bara

DUA njema za Watanzania kwa ujumla, leo zitaelekezwa mjini hapa, wakati timu mbili kutoka Jamhuri ya Muungano wetu, Bara na Zanzibar zitakapokuwa zikipigana katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Lugogo.
Bara, maarufu Kilimanjaro Stars watakuwa wa kwanza kutupa kete yao leo kuanzia saa 8:00 mchana kwa kumenyana na Rwanda, kwa jina la utani Amavubi, yaani Nyigu, wakati Zanzibar Heroes watasubiri hadi saa 10:00 kukipiga na Burundi, Int’hamba Murugamba, yaani Mbayuwayu.
Robo Fainali nyingine zinatarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kenya ikianza na Malawi saa 10:00 jioni kabla wenyeji Uganda kumenyana na Ethiopia saa 1:00 usiku.
Zanzibar wakiomba dua kabla ya mechi na Rwanda waliyoshinda 2-1
Mchezo kati ya Burundi na Zanzibar unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua, na zaidi Mashujaa wa Visiwani wanatakiwa kumchunga sana Nahodha wa Mbayuwayu, Suleiman Ndikumana kwa sababu ndiye amekuwa akiiongoza vema timu yake.
Ndikumana amekuwa akihaha Uwanja wa mzima, akicheza kwa kuwahamasisha wadogo zake na hadi sasa ndiye Nahodha bora zaidi katika mashindano haya.
Hazina ya Zanzibar ni safu nzuri ya kiungo inayoongozwa na Suleiman Kassim Selembe na Khamis Mcha ‘Vialli ’bila kusahau ukuta imara chini ya mabeki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Aggrey Morris na hata kipa hodari, Mwadini Ally.
Safu ya ushambuliaji leo hakuna shaka itaongozwa na Jaku Juma, mkali wa mabao katika Ligi Kuu ya Zanzibar na Seif Abdallah, nyota wa Ruvu Shooting ya Bara aliye mbioni kuhamia Azam FC. 
Mambo zaidi ni Rwanda na Bara; jezi namba nane (8) leo zinatarajiwa kuwa kila kitu. Jezi hiyo kwa upande wa Rwanda anavaa Haruna Hakizimana Niyonzima na Bara Mrisho Khalfan Ngassa.
Wawili hawa ndio wamekuwa kama roho ya timu zao katika mashindano haya na leo wanatarajiwa kuendelea kubeba jukumu hilo.
Ngassa anacheza wingi ya kushoto kwa sasa kwenye kikosi cha Bara, wakati Niyonzima anapangwa wingi ya kulia katika kikosi cha Rwanda. Niyonzima huwa anabadilika na kuingia ndani na wakati mwingine upande wa pili na kwa ujumla huhaha Uwanja mzima, vivyo hivyo kwa Ngassa.
Dadi Birori au Taddy Etikiama kwa jina lingine atasimama mbele bila kuongoza mashambulizi kwa Rwanda na langoni atakuwapo kipa mgumu kufungika, Jean Claude Ndoli.
Kocha wa Bara, Mdenmark Kim Poulsen anacheza na mshambuliaji mmoja, John Bocco, lakini anatumia mawinga wenye kushambulia mno- Ngassa na Simon Msuva, wakati Micho pia hutumia washambuliaji wawili na hana viungo wenye kasi sana, ila mafundi.
Mabeki wa pembeni wa Rwanda wanapitika kwa urahisi na leo Ngassa na Msuva washindwe wenyewe tu. Beki ya kati ya Rwanda ni ugonjwa wa moyo, maana yake John Bocco leo ni umakini wake tu.
Kwa ujumla, Bara ina nafasi kubwa ya kuitoa Rwanda, tena kwa kuipa kipigo kitakatifu tu kama watatumia vyema nafasi zao.
Mwinyi Kazimoto amepona na bila shaka atakuwa mmoja wa viungo watatu leo, wengine Frank Domayo na Amri Kiemba maana yake, kwenye benchi watakuwapo Athumani Iddi ‘Chuji’ na Shaaban Nditi.
Piga, ua Juma Kaseja atasimama langoni, kulia Erasto Nyoni na kushoto uzoefu utambeba Amir Maftah ingawa Issa Rashid anakuja vizuri, wakati katikati Kevin Yondan atacheza pacha na Shomary Kapombe.
Hii ni mara ya pili ndani ya miaka mitatu Bara kukutana na Rwanda katika hatua hii na mara ya mwisho ilikuwa Desemba 8, mwaka 2010 wakati bao pekee la mkwaju wa penalti la aliyekuwa Nahodha wa Stars, Nsajigwa Joel Shadrack Mwandemele dakika ya 61 lilipoipa Bara ushindi wa 1-0 na kutinga Nusu Fainali hadi kutwaa ubingwa Dar es Salaam.
Lakini mwaka jana pia timu hizo zilikutana Dar es Salaam katika michuano hii, Kundi A na Rwanda iliilaza Bara 1-0 Novemba 26, katika michuano ambayo wenyeji waliboronga vibaya na kutolewa mapema.
Tangu mwaka 2001, timu hizi zimekutana mara tisa katika Challenge na Rwanda imeshinda mechi sita, wakati Bara imeshinda mechi tatu tu. Idadi kubwa ya mabao Tanzania kuifunga Rwanda ni 3-0, wakati Amavubi wamewahi kuichapa Bara 5-1.
Pamoja na yote, Robo Fainali za leo ni nzuri- zaidi Watanzania kwa ujumla Bara na Visiwani, wanatakiwa kuziombea dua njema timu zao zivuke hatua hii, kwani katika soka lolote hutokea.  Mungu ibariki Bara na Zanzibar, ibariki Tanzania. Amin.
REKODI YA TANZANIA NA RWANDA CHALLENGE:
Desemba 17, 2001; Nusu Fainali Rwanda
Tanzania 1-2 Rwanda B
Desemba 11, 2002; Nusu Fainali Mwanza
Tanzania 3-0 Rwanda
Desemba 19, 2004; Kundi A Ethiopia
Tanzania 1-5 Rwanda
Desemba 6, 2005; Kundi A Rwanda
Tanzania 1-3 Rwanda
Desemba 5, 2006; Robo Fainali Ethiopia
Tanzania 1-2 Rwanda
Januari 7, 2009; Kundi A Uganda
Tanzania 2-0 Rwanda
Desemba 10, 2009: Nusu Fainali Kenya
Tanzania 1-2 Rwanda
Desemba 8, 2010; Robo Fainali Dar es Salaam
Tanzania 1– 0 Rwanda
Novemba 26, 2011; Kundi A, Dar es Salaam
Tanzania 0 – 1 Rwanda
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
Mrisho Ngassa               Tanzania  5
John Bocco                    Tanzania  4
Suleiman Ndikumana     Burundi    3 (1 penalti)
Brian Umony                  Uganda    3
Chris Nduwarugira         Burundi    3
Khamis Mcha                 Zanzibar   2
David Ochieng               Kenya       2
Clifton Miheso                Kenya       2
Dadi Birori                      Rwanda    2

 


BUSQUETS AWASIHI WENZAKE KUTOBWETEKA.

KIUNGO nyota wa klabu ya Barcelona, Sergio Busquets amesisitiza kuwa hawatakiwi kujibweteka kama wanataka kushinda taji la Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga msimu huu. Barcelona wametofautia alama sita na Atletico Madrid ambao wanashika nafasi ya pili kufuatia ushindi wa mabao 5-1 waliopata kutoka kwa Athletic Bilbao wakati bado wameacha pengo la alama 11 dhidi ya mahasimu wao Real Madrid ambao wanashika nafasi ya tatu. Busquests aliiambia wavuti ya klabu hiyo kuwa pamoja na kuongoza La Liga kwa tofauti ya alama nyingi lakini safari bado ni ndefu kufikia mwishoni mwa msimu hivyo bado hakuna muda wa kupumzika kwa sasa. Kiungo huyo alimsifu mchezaji mwenzake nyota Lionel Messi na kudai kuwa ndio mchezaji bora wa dunia kwasasa kwasababu anaweza kufunga mabao na kuwa sehemu ya mashambulizi yote ambayo klabu imekuwa ikifanya. Messi alifunga mabai mawili katika mchezo dhidi ya Bilbao uliochezwa Jumamosi na kufikisha mabao 21 katika mechi 14 alizocheza msimu huu.

FERGUSON AMTAKA MOURINHO KUVAA VIATU VYAKE OLD TRAFORD.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson ameonyesha imani yake kuwa Jose Mourinho ndio meneja anayefaa kuchukua nafasi yake wakati atakapoondoka Old Traford. Ferguson mwenye umri wa miaka 70 amekuwa kocha wa United toka mwaka 1986 na bado hajaamua rasmi lini ataachia nafasi hiyo kwa ajili ya kustaafu lakini alimsifia Mourinho ambaye anaifundisha Real Madrid kuwa kocha mwenye viwango vya kuingoza United katika siku za mbeleni. Kocha huyo amesema kuwa hakutegemea mtu ambaye hajawahi kucheza soka kama anaweza kuwa kocha bora lakini Mourinho mwenye umri wa miaka 39 amebadilisha dhana hiyo na anaweza kufundisha popote na kwa kiwango cha juu kabisa. Ferguson anakumbuka wakati Mourinho anaingia Uingereza na kujiita yeye wa kipekee na kuwaambia wachezaji wa Chelsea watashinda taji la Ligi Kuu nchini humo alimuona kama mwehu lakini alipoanza kazi alithibitisha usemi wake.

FIFA KOMBE la MABARA: Wenyeji Brazil kufungua na Japan, Kundi moja na Italy!

>>SPAIN pamoja na Uruguay!!
FIFA_CONFEDERATION_CUP_2013+++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A:
-Brazil
-Japan
-Mexico
1Italy
KUNDI B:
-Spain
-Uruguay
-Tahiti
-Bingwa wa Afrika (Kujulikana Februar10, 2013)
+++++++++++++++++++++++++++++
Wenyeji Brazil watacheza Mechi ya ufunguzi ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara kwa kucheza na Japan Mjini Brasilia hapo Juni 15, 2013 baada ya Droo ya Mashindano hayo kufanyika huko Sao Paulo ambayo ilipanga Makundi mawili.
Mara baada ya Mechi hiyo, Brazil watacheza na Mexico na kumaliza na Italy katika Mechi za Kundi A.
Kundi B lina Mabingwa wa Dunia Spain, Uruguay, Tahiti na Bingwa wa Afrika (Kujulikana Februar10, 2013).
FIFA ilishatangaza Miji ambayo itatumika kwa ajili ya Mashindano hayo ambayo ni Brasilia, Belo Horizonte, Fortaleza, Rio de Janeiro, Recife na Salvador.
RATIBA:
Juni 15
Brazil v Japan
Juni16
Mexico v Italy
Spain v Uruguay
Juni 17
Tahiti v Bingwa Afrika
Juni 19
Brazil v Mexico
Italy v Japan
Juni 20
Spain v Tahiti
Bingwa Afrika v Uruguay
Juni 22
Japan v Mexico
Italy v Brazil
Juni 23
Bingwa Afrika v Spain
Uruguay v Tahiti
NUSU FAINALI
Juni 26
Mshindi A v Mshindi wa Pili B
Juni 27
Mshindi B v Mshindi wa Pili A
FAINALI
Juni 30
 

FA CUP RAUNDI ya 3: Droo yafanyika, Man United kuivaa Hammers Upton Park!!

>>MECHI 4 tu kukutanisha Timu za Ligi Kuu!!
FA_CUP-NEW_LOGOManchester United watatua Upton Park kucheza na West Ham United katika Raundi ya 3 ya FA CUP kwa mujibu wa Droo iliyofanyika leo hiyo ikiwa moja ya Mechi 4 tu zitakazokutanisha Timu za Ligi Kuu England.
Mechi nyingine za Timu za Ligi Kuu England ni zile za Southampton watakaokuwa nyumbani kucheza na Mabingwa watetezi Chelsea, QPR kuikaribisha West Brom na Arsenal kusafiri kucheza na Swansea.
Timu nyingine vigogo wa LigI Kuu, kama vile Mabingwa wa Ligi Manchester City, wao watacheza na Watford, Tottenham kucheza na Coventry.
Mechi zitachezwa Jumamosi Januari 5, 2013 na Jumapili Januari 6, 2013.
RATIBA:
RAUNDI ya TATU:
Crystal Palace v Stoke
Brighton v Newcastle
Tottenham v Coventry City
Wigan v Bournemouth
Fulham v Blackpool
Aston Villa v Ipswich
Charlton v Huddersfield
Barrow or Macclesfield v Cardiff
Barnsley v Burnley
Manchester City v Watford
Swansea v Arsenal
Leicester v Burton
Millwall v Preston
Cheltenham or Hereford v Everton
Derby v Tranmere
Crawley v Reading
Aldershot v Rotherham or Notts County
Middlesbrough v Harrogate or Hastings
Accrington Stanley or Oxford v Sheffield United
Southampton v Chelsea
QPR v West Brom
Peterborough v Norwich
Lincoln or Mansfield v Liverpool
Bolton v Sunderland
Nottingham Forest v Oldham
West Ham v Manchester United
Hull v Alfreton or Leyton Orient
Blackburn v Bristol City
Leeds v Birmingham
Bury or Southend v Bradford or Brentford
Luton v Wolves
Sheffield Wednesday v MK Dons

Ferguson adokeza Difensi yake dhidi ya Cluj!

Sir Alex Ferguson amesema anategemea Nahodha wake Nemanja Vidic atacheza Mechi yao ya Jumatano ya kukamilisha Ratiba tu ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya CFR Cluj baada ya kupona goti lake.
Pia alidokeza Mechi hiyo ni muafaka kwa Difensi yake kuwa na Phil Jones, Chris Smalling na Alexander Büttner.
Manchester United tayari wameshafuzu toka Kundi H wakiwa vinara wa Kundi hilo lakini nafasi ya pili bado inagombewa na Galatasaray na Cluj hivyo ni muhimu kwao kuchezesha Kikosi imara ili kutoa haki kwa ushindani wa Timu mbili zinazogombea nafasi ya pili.
Katika Mechi iliyopita ya Kundi H wakati tayari wakiwa wamefuzu, Man United walibadili Kikosi na kufungwa 1-0 huko Uturuki na Galatasaray.

Anderson NJE WIKI KADHAA!!
Sir Alex Ferguson amethibitisha Anderson atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki kadhaa baada ya kuumia kwenye Mechi ya Ligi Kuu England walipoifunga Reading Bao 4-3 juzi Jumamosi.
Anderson, ambae amecheza Mechi 8 za mwisho za Man United, Jumamosi wakicheza na Reading alifunga Bao la kwanza zuri lakini ikabidi atolewe kabla haftaimu baada ya kuumia musuli za pajani.

Adebayor asusa kuichezea Togo, kuikosa AFCON 2013!


Emmanuel Adebayor, ambae ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Togo, ametangaza kusimama kuichezea Nchi hiyo kutokana na mgogoro wa Wachezaji kutolipwa stahili yao baada ya kucheza Mechi ya Kirafiki na Morocco na uamuzi huo huenda ukamfanya asicheze Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini kuanzia Januari 19 na kumalizika Februari 10, Mwaka 2013.
Uamuzi huo, bila shaka, utaufurahisha Klabu yake Tottenham ambayo itakuwa na uhakika wa kuweza kumtumia katika kipindi hicho.
Akitangaza uamuzi wake, Adebayor alisema Shirikisho la Soka la Togo lilipokea EURO 35,000 toka kwa wenzao wa Morocco lakini wao hawakuwalipa Wachezaji ila baadhi tu walipewa nusu wakati pesa zilipokelewa na Rais wa Shirikisho hilo.
Adebayor alistaafu kuichezea Togo Mwaka 2010 mara baada ya Basi la Timu ya Togo kushambuliwa kwa risasi Nchini Angola na kutokea vifo lakini Mwaka huu alirudia tena kuichezea na kufanikisha kutinga kwao Fainali za AFCON 2013.