Tuesday, January 1, 2013

MANCINI;ASEMA BALOTELI NI MUHIMU KKWA MMILIKI WA TIMU SHEIKH MANSOUR


Roberto Mancini amesisitiza kuwa Mario Balotelli atasalia katika klabu yake ya Manchester City kufuatia mmiliki wa klabu Sheikh Mansour kumsajili mtaliano huyo kutokana na kile alichokiita kama uwekezaji mkubwa katika klabu hiyo.

Balotelli hajaonyesha kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu, ambapo amefunga magoli 3 tu katika mashindano yote, jambo ambalo lilianzisha minong’ono ya chini chini kuwa mshambuliaji huyo huenda akaondoka ligi kuu ya England ‘Premier League’ na kuelekea Italia ‘Serie A’ kwa kigogo cha soka nchini humo AC Milan mwezi huu wa January.

Hata hivyo meneja Mancini ameweka wazi kuwa’

"Sheikh Mansour anampenda Balotelli kwakuwa anaamini anakipaji na analitangaza jina la City duniani"

"tunapaswa kukubali kuwa Mario alisaini kama uwekezaji mkubwa,  na hii si klabu ambayo inatupa mtaji wake kupitia dirishani

"nadhani Mario atasalia lakini huko baadaye itategemea na yeye mwenyewe"


REDKNAPP AMETHIBITISHA KUMTAKA JOE COLE KUINUSURU QPR
 Bosi wa Queens Park Rangers Harry Redknapp amethibitisha kuwa ataongea na meneja wa Liverpool  Brendan Rodgers kuhusiana na usajili wa Cole.

Redknapp anamjua vema Cole tangu wakati huo wakiwa pamoja katika klabu ya West Ham, na baadaye kufanya vema katika timu ya taifa ya England.

Cole alikuwa katika mpango wa Redknapp tangu wakati huo akifundisha Tottenham, lakini kiungo huyo akaamua kuelekea kwa meneja Roy Hodgson katika klabu klabu ya Liverpool ambako bado hajafanikiwa kuonyesha mafanikio.


MKURUGENZI W APSG LEONARDO AKANUSHA MAZUNGUMZO NA COLE .

Mkurugenzi wa michezo wa Paris Saint-Germain, Leonardo amepuuza taarifa kuwa yuko katika jaribio la kumshawishi Ashley Cole aondoke Chelsea katika dirisha hilo dogo lililoanza hii leo barani ulaya.

Cole atakuwa huru baada ya mkataba wake kumalizika  Stamford Bridge mwishoni mwa msimu na bosi wa sasa Rafael Benitez alinukuliwa akiweka wazi katika moja ya mikutano yake na wandishi wa habari kwamba mlinzi huyo wa England ataondoka darajani majira ya kiangazi.

Hata hivyo baadaye alirekebisha kauli yake na kusema kuwa Cole ataendelea kusalia Chelsea mara baada ya mkataba kumalizika jambo ambalo si Cole mwenyewe wala Frank Lampard ambaye naye yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake aliyekubaliana na masharti mapya ya kusalia hapo.

Kwasasa PSG ambayo inafanya kufuru kifedha katika matumizi ya usajili inanolewa na Carlo Ancelotti, ambaye huko nyuma alikuwa pamoja na Cole wakati huo akiifundisha Chelsea.

Leonardo pia amekanusha taarifa kuwa Wesley Sneijder anampango wa kujiunga PSG ambapo amesema katika nafasi yake tayari PSG inawachezaji watano

Hata hivyo klabu hiyo ambayo kwasasa inamilikiwa na wamiliki wapya wa Qatar Investment Authority, imeanzisha mpango wa kumtaka Lucas Moura akitokea Sao Paulo ambaye tayari ameshakubali kujiunga nao na huenda wengi wakafuata.


CUDICINI AAMUA KUELEKEA GALAXY BAADA YA KUKOSA NAMBA YA KUDUMU TOTTENHAM NAMBA ILIYOCHUKULIWA NA HUGO LlORIS
 Mlinda mlango wa Tottenham goalkeeper Carlo Cudicini ameamua kujiunga na LA Galaxy inayoshiriki ligi ya soka ya nchini Marekani MLS kwa mkataba wa miaka miwili.

Cudicini, mwenye umri wa miaka 39, alishindwa kurejea katika ubora wake wa kunyaka mipira kule White Hart Lane baada ya kupata ajali ya pikipiki ambayo ilimtengua kiuno na maumivu makali yaliyotona na kuumia mfupa wa nyonga.

Kufuatia kusajiliwa kwa Hugo Lloris na kupelekea yeye kuwa mlinda mlango namba tatu nyuma ya mlinda mlando mfaransa Brad Friedel ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mpya, sasa Cudicini ameamua kutafuta mwelekeo mpya nchini Marekani.

Mtaliano huyo ameamua kuondoka kusaka namba nchini Marekani na inaarifiwa kuwa anakuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara mnono.

Cudicini alijiunga White Hart Lane mwezi January 2009 kwa uhamisho huru baada ya kuidakia Chelsea miaka tisa na sasa anajiunga na mchezaji mwenzake wa zamani wa  Tottenham Robbie Keane katika klabu ya Galaxy.

WALCOT;ASEMA HATMA YAKE ITAJULIKANA HIVI PUNDE KUANZIA SASA
 Theo Walcott ameelezea juu ya hitajio lake la kutaka kusalia katika klabu yake ya Arsenal licha ya mshambuliaji huyo sasa kuwa anaweza kufungua mazungumzo na klabu nyingine.

Makataba wa Walcott wa sasa utafikia kikomo mwishini mwa msimu huu ambapo kwasasa majadiliano juu ya mkataba mpya yakitazamiwa kuanza baadaye mwezi huu.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ana matumaini kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England atafuata nyayo za wachezaji wenzake vijana wa England Jack Wilshere, Alex Oxlade-Chamberlain, Aaron Ramsey, Kieran Gibbs na Carl Jenkinson ambao walisaini mikataba mipya muda kabla ya sikukuu ya Christmas.

Hata hivyo Wenger amesema mwezi uliopita alitarajia mambo hayo yangekuwa yamemalizwa kabla ya mwaka mpya.

Licha ya songombingo hiyo, bado Walcott anasisitiza kuwa anataka kusalia Emirates Stadium.

Amenukuliwa na The Sun akisema

“nina imani kila kitu kitakwenda vizuri hivi karibuni"

“siku zote nimekuwa nikisema kuwa nataka kusalia na kufurahia kucheza katika timu hii. Hebu tuone nini kitafuata”

Kwa mujibu wa sheria za uhamisho ni kwamba kwasasa  Walcott anaweza kusaini mkataba wa awali na klabu nyingine yoyote ya nje ambayo atapenda mpaka mkataba wake utakapo kwisha rasmi mwezi June ambako ambako atasaini kama mchezaji huru.

WACHEZAJI YANGA WAFURAHIA KAMBI UTURUKI




Wachezaji na bechi la ufundi la timu ya Young Africans wamefurahishwa na hali ya kambi hapa katika mji wa Antalya kwamba hali ya hewa ni nzuri, vyakula aina zote vinapatiikana na huduma za mazoezi kwa ajili ya kambi ni za kiwango cha juu sana.


Wakiongea na www.youngafricans.co.tz Kocha wa makipa Razaki Siwa amesema kw akeli hali ya hewa sio mbaya kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali, hali ya hewa ni nzuri, mazingira ya kambi ni ya kuridhisha vifaa vya kwa ajili ya mazoezi vipo kwa wingi hivyo inakuwa nio rahisi kwetu walimu kuwaelekeza wachezaji wafanye nini.

Kocha Siwa amesema pia wanaushukuru uongozi wa Young Africans kwa kuamua kuileta timu kambini nchini Uturuki kwani wachezaji wanapata nafasi nzuri ya kujifunza kwa pamoja, mafunzo ambayo hayana bughuza kwani kambi ipo katika hadhi ya kimataifa ndio maana timu nyingi za Ulaya
zinapenda kuja kuweka kambi eneo tulivu kama hili la Antalya.

Fred Felix Minizro kocha msaidizi kwa upande wake amesema hali ya kambi kwa ujumla ni nzuri, na kuhusu hali ya hewa ni baridi ya kisai tu kama Mbeya na Arusha hivyo haoni kama hali ya hewa inaweza kuwa ni kikwazo katika kambi hii ya mafunzo.

Naye kiungo mshambuliaji Saimon Msuva amesema wanafurahia kupata nafasi hii ya kuja kuweka kambi nchini Uturuki, kwani anaamin mazingira na huduma z akambi ni nzuri kabisa hivyo wanayapokea vizuri mafunzo ya kocha mkuu Brandts na pindi watakaporudi Tanzania wataweza kuwapa raha wapenzi wa soka kwa kuwaonyesha ni nini hasa wamekipata kwa kipindi cha wiki mbili

FERGUSON APUUZA SUALA LA KUSTAAFU



Football | Barclays Premier League

Fergie dismisses retirement talk



Alex Ferguson has quashed retirement talk by revealing he has no plans to step down as Manchester United manager in the near future.
Ferguson, who turned 71 on Monday, has been forced to deal with questions about his retirement plans since the time he reversed his decision to leave the club in 2002.
With Pep Guardiola due to end his post-Barcelona sabbatical in a few months, Jose Mourinho tipped to leave Real Madrid and David Moyes' Everton contract close to expiring, three of the main candidates to replace Ferguson could be available at the end of the season, prompting a new round of speculation about the Scot's future.
But Ferguson, who has been in charge at Old Trafford since 1986, marked the new year by making it clear he won't be leaving United for some while.
"I'm hoping to stay on for a bit of time," he said in an interview with the Abu Dhabi Sports channel.
It is widely accepted few will get to know when Ferguson is ready to call it a day, with chief executive David Gill the man tasked with advising the Glazer family about a replacement.
And, though Guardiola, Mourinho and Moyes are bound to be at the top of the list if they are available, Ferguson knows plenty of other candidates are likely to have emerged by the time he finally quits.
"It's very difficult," Ferguson said. "Over the years, names have been bandied about but football is such a precarious industry.
"But you could be talking about one of the potentially exciting young managers in the game, but is he going to be here in two or three years' time?
"The sack race is horrendous. Sometimes a manager can only survive four games if he doesn't win a match.
"Top managers will always been in demand but nobody knows where they are going to be in two or three years' time."

MANCINI: “RVP ndie anafanya Man United iwe tofauti na City!”

RVP_in_RED2Bosi wa Manchester City Roberto Mancini anaamini Straika wa Manchester United Robin van Persie ndie anaeleta tofauti kati ya Timu hizo mbili ambazo zinafukuzana kwenye Ligi Kuu England huku Man United wakiwa kileleni Pointi 7 mbele ya Man City ambao ni Mabingwa watetezi.
Mancini amesema: "Tulimtaka Van Persie kwa sababu tulijua ni Mchezaji muhimu! Yuko tofauti kabisa na Mastraika wengine! Van Persie ni muhimu kwa United na huyu ndie alieleta tofauti kati ya United na sisi hivi sasa!”
Mancini alibainisha kuwa walikuwa karibu kidogo kumsaini Robin van Persie lakini hilo halikutokea.
Hivi karibuni Mancini amekuwa akilia na Mastraika wake Sergio Aguero, Carlos Tevez, Edin Dzeko na Mario Balotelli kwa ubutu wa kufunga.
Amesema: “Msimu uliopita tulifunga Bao nyingi kupita Timu nyingine kwenye Ligi na tungempata Van Persie tungecheza Mfumo wa kutumia Mastraika watatu.”
Kwa sasa, Robin van Persie ndie anaongoza kwa ufungaji Bao nyingi kwenye Ligi Kuu England.

MR & MRS KAMNA WAPATIKANA USIKU WA MWAKA MPYA WA 2013 USIKU WA SAA SITA MKOANI TABOR


Wa  Katikati ni mshindi wa kwanza wa shindano la Miss Kamna,Mariam Wilfred akifuatiwa na mshindi wa pili kulia ni Mwasiti Thabit,kushoto ni mshindi wa tatu  Sabrina Michael.
 Baadhi ya washabiki waliofurika katika ukumbi wa Theophilo Kisanji wakiwa wanashuhudia mashindano ya kuwasaka Mr. na Mrs Kamna usiku wa mwaka mpya.
 Washindi wa tano bora wakiwa Jukwaani mara baada ya kutangazwa wakisubiri kuulizwa maswali ili kujiongezea idadi ya point katika mashindano hayo yaliyokuwa na mvuto mkubwa.
 Majaji walikuwa na kazi ngumu ya kuhesabu na kutoa point kwa washindi katika mashindano hayo
 Huyu ndiye Mr.Kamna 2013 Daniel Kisanga muda mfupia mara baada ya kutangazwa mshindi katika mashindano hayo.
 Washindi wa tano bora kuwania Mr.Kamna 2013 wakiwa jukwaani wakisubiri maswali ya kizushi ambayo kwakweli yalikuwa ni mtihani mkubwa kwao.
 Washabiki
 Mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kmchaya akicheza muziki wakati wa mashindano hayo akiwa na Naibu Meya manispaa ya Tabora Waziri Mrenda kulia,na kushoto ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora Moshi Nkonkota,ilikuwa ni mara baada ya kutimu saa sita kamili usiku hii ilikuwa ni ishara ya kuupokea mwaka mpya wa 2013. 

UCHAGUZI MKUU WA TAFCA MKOA WA TABORA KUFANYIKA JANUARY 10 MWAKA HUU 2013



Uchaguzi  wa TAFCA mkoani Tabora unatarajia kufanyika tarehe 10 mwezi wa kwanza mwaka huu wa 2013 .Nafasi zinazowaniwa ni nafasi ya Uenyekiti,Makamu mwenyekiti,Katibu mkuu, ,Katibu msaidizi,Mweka hazina,,Mjumbe anayewakilisha TAFCA,kwenye mkutano mkuu wa TAFCA Taifa,na Wajumbe 3 wa kamati ya utendaji waliochaguliwa na Mkutano Mkuu.

Fomu zimeanza kutolewa leo kwa katibu wa kamti ya uchaguzi ya TAFCA TTC kwa mwalimu kapaya kuanzia leo terehe 1.1.2013 na mwisho w akurudisha fomu itakuwa tarehe 05/1/2013 saa kumi alasiri.

Kwa nafasi ya Uenyekiti ,Makamu mwenyekiti,Katibu ni shilingi 10,000/= na nafasi za ujumbe wowote ni shilingi elfu tano 5000 pia mwombaji atatakiwa na TAFCA kujaza fomu moja na atatia saini yake pamoja na maelezo ya chama chake.

Pia kila mgombea atalazimika kurudisha fomu hiyo kwa katibu kamati ya uchaguzi ya TAFCA ikiwa na vielelezo vyenye kuthibitisha sifa yake na picha 2 za passport size .tarehe ya usaili katika uchaguzi huo itakuwa ni siku ya tarehe 07/01/2013 kuanzia saa kumi kamili jioni kwenye ukumbi utakaojulikana hapo badae na tarehe ya uchaguzi utakuwa tarehe 10/1/2013 saa nne asubuhi

MFARANSA AANGUKA MIEZI MINANE SIMBA SC



Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange Kaburu akimshuhuidia kocha mpya wa klabu hiyo, Mfaransa Patrick Liewig akisaini mkataba wa miezi minane leo katika hoteli ya Spice, Lumumba, Dar es Salaam.  

Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange Kaburu akisaini kwa niaba ya klabu mkataba wa kocha mpya wa klabu hiyo, Mfaransa Patrick Liewig

Katibu wa Simba, Mtawala akiwaongoza Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange Kaburu na kocha mpya wa klabu hiyo, Mfaransa Patrick Liewig kusaini. Nyuma ni Meneja Moshi.  
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange Kaburu akibadilishana mikataba na kocha mpya wa klabu hiyo, Mfaransa Patrick Liewig baada ya kusaini mkataba wa miezi minane leo katika hoteli ya Spice, Lumumba, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Simba, Evodius Mtawala na nyuma ni Meneja wa hoteli ya Spice, Mzee Moshi Omar Mbury. 

Mwanasheria wa Simba, Allan Maduhu (kulia) akigonga muhuri mkataba huo

SPAIN ILIVYOWAADHIBU WAITALY NA KUJINYAKULIA KOMBE LA EURO NA KUENDELEEA KUTAWALA KWA TIMU YA TAIFA YA SPAIN NA VILABU VYAKE KUTAWALA KATIKA VIKOMBEEEEEEEEE

2012: SPAIN YATAWALA KWA MATAJI!

Jumatatu, 31 Disemba 2012 20:54
Chapisha Toleo la kuchapisha
CHELSEA_ULAYA_2012AUEFA leo, wakiaga 2012 na kuikaribisha 2013, wametoa pongezi kwa Spain,SPAIN_V_FRANCE Chelsea na Atletico Madrid kwa kutwaa Mataji katika Mwaka 2012 ambapo Spain ilitwaa Mataji 6 kati ya 11 katika Mashindano ya UEFA kwa Mwaka 2012 yakiwemo yale ya EURO 2012 kwa Timu ya Taifa ya Spain na Mataji ya EUROPA LIGI na UEFA SUPER CUP ambayo yote yalichukuliwa na Atletico Madrid.
Ingawa imeshindwa kutetea Taji lake na kuwa Bingwa wa kwanza wa Ulaya kutolewa hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Chelsea imetajwa kuwa imefuata nyayo za Borussia Dortmund kutwaa Taji hilo kwa mara ya kwanza tangu Dortmund walipofanya hivyo Msimu wa 1996/7.
UEFA=WASHINDI MWAKA 2012
MASHINDANO
MSHINDI
MSHINDI WA PILI
UEFA EURO 2012
Spain
Italy
UEFA Champions League
Chelsea FC (ENG)
FC Bayern München (GER)
UEFA Europa League
Club Atlético de Madrid (ESP)
Athletic Club (ESP)
UEFA Super Cup
Club Atlético de Madrid (ESP)
Chelsea FC (ENG)
FIFA Club World Cup
SC Corinthians Paulista (BRA)
Chelsea FC (ENG)
UEFA European U-19
Spain
Greece
UEFA European U-17
Netherlands
Germany
FIFA U-20 -WANAWAKE KOMBE la DUNIA
United States
Germany
UEFA U-19 WANAWAKE
Sweden
Spain
FIFA U-17 -WANAWAKE KOMBE la DUNIA
France
North Korea
UEFA U-17 WANAWAKE
Germany
France
FIFA Futsal World Cup
Brazil
Spain
UEFA Futsal EURO 2012
Spain
Russia
UEFA Futsal Cup
FC Barcelona (ESP)
MFK Dinamo (RUS)
UEFA WANAWAKE CHAMPIONZ LIGI
Olympique Lyonnais (FRA)
1. FFC Frankfurt (GER)

MABINGWA MAN CITY WAHAHA KUSAINI WAPYA JANUARI, BA ALETA BALAA!

>>CITY WAIKUBALI NYEKUNDU YA NASRI, KUIKOSA ARSENAL!
>>PARDEW ALIA NA WASHIRIKA WA DEMBA BA!
MANCINI_n_MICAHMABINGWA wa England, Manchester City, wamedokeza kuwa upo uwezekano wa kusaini Wachezaji wapya Mwezi Januari na pia wamethibitisha kutokata Rufaa kuipinga Kadi Nyekundu ya Mchezaji wao Samir Nasri aliyopewa Juzi na huko Klabuni Newcastle, Meneja Alan Pardew, amelalamika kuhusu Washirika wa Straika wake Demba Ba ambae imetobolewa anasaka Klabu mpya Mwezi Januari.
MAN CITY
Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amedokeza kuwa athari za kuwakosa Wachezaji wao, watakaokwenda kucheza AFCON 2013 na pia kuwa majeruhi, itawalazimisha kuingia Sokoni Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa ili kuimarisha Kikosi chao.
Mancini amethibitisha Mwezi Januari watawakosa Wachezaji watatu walioitwa kuichezea Ivory Coast kwenye AFCON 2013 ambao ni Yaya Toure, Kolo Toure na Abdul Razak, na pia inao majeruhi Micah Richards, JackRodwell, Aleksandar Kolarov na Maicon.
WAKATI HUO HUO, Man City imethibitisha haitakata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Mchezaji wao Samir Nasri aliyopewa Jumamosi huko Carrow Road wakati City ilipoifunga Norwich 4-3 kwa kumpiga kichwa Sebastien Bassong.
Mara baada ya uamuzi wa Man City, FA imetangaza kuwa Nasri atazikosa Mechi 3 ambazo ni za Ligi dhidi ya Stoke City Januari 1, FA CUP na Watford Januari 5 na ile ya Ligi ugenini na Arsenal hapo Januari 13.
PARDEW na BA
BOSI wa Newcastle Alan Pardew amewashambulia Washirika wa Demba Ba kwa kumshauri vibaya Straika huyo kutoka Senegal ambae juzi waliripotiwa kufanya mazungumzo na Chelsea kuhusu kuhama kwake lakini makubaliano hayakufikiwa.
Pardew amesema : “Kwa namna fulani, namsikitikia Demba kwani nadhani amezungukwa na Watu ambao si Wakilishi wake na wamekua wakisema hili na lile!”
Kwa Miezi kadhaa sasa, Newcastle imekuwa ikijitahidi kumpa Mkataba mpya Demba Ba ambao pia utaondoa Kipengele cha sasa kuwa anaweza kuuzwa wakati wowote ikiwa Malipo ya Pauni Milioni 7.5 yatatolewa.

SUNZU AREJESHWA SIMBA SC, MFARANSA AMWAGA WINO LEO MSIMBAZI


Patrick Liewig

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. ambaye awali ilielezwa atatemwa kwenye kikosi cha Simba SC, amerejeshwa kwenye kikosi hicho.
Sunzu
Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala  alisema Sunzu ameomba mwenyewe kurudi kazini na tayari amekwishawasili Dar es Salaam na ameanza mazoezi.
“Kama utatakumbuka lilikuwa suala la kiafya, Sunzu alikuwa mgonjwa akaomba aachwe, lakini nadhani baada ya kurejea kwao na kutibiwa ameona amepona na ameomba kurudi kazini,”alisema Mtawala.
Mtawala alisema Sunzu ni miongoni mwa wachezaji waliotarajiwa kuondoka jana mjini Dar es Salaam kwenda visiwani Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi. Aidha, Mtawala pia alisema mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa pia ameungana na wenzake mazoezini tangu jana.
Wakati huo huo, kocha mpya wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig aliyewasili jana mchana Dar es Salaam, leo anatarajiwa kusaini mkataba wa kuanza kazi Msimbazi.
Mtawala alisema, Liewig atakaposaini mkataba atakwenda kuungana na kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi visiwani Zanzibar tayari kuanza kazi.
Liewig ambaye ni kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, jana usiku alitambulishwa mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba katika hoteli ya Spice.
Liewig mwenye Stashahada ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller, anatarajiwa kwenda Zanzibar kesho.
Liewig pia amehudhuria kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Dijon.
Kwa upande wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia mwaka 1989 hadi 1990:  alikuwa Meneja Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi 1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez, 1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia.

YANGA WAKIJIFUA UTURUKI JANA





Wachezaji wa Young Africans wakiwa nje ya hotel ya Fame Residence tayari kwa kuelekea kuanza mazoezi


Young Africans Sports Club imeanza mazoezi jana asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.
Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.
Mji wa Antalya ni maarufu katiak medani ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti duniani.
Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameada sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji wa mji huu watasherehekea pamoja. 

KIKOSI STARS KUIKUSANYIA MAKALI MOROCCO CHATAJWA, SAMATTA, ULI NA WALIOTIMULIWA AZAM NDANI



KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.
Katika kikosi hicho, Kocha Mdenmark, Kim Poulsen ameendelea kuwaita wachezaji waliosimaishwa na klabu yao, Azam FC kwa tuhuma na kuhujumu timu, mabeki Erasto Nyoni na Aggrey Morris.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji wote wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Kuhusu kuripoti, kuna kirendawili kigumu juu ya wachezaji wa Yanga, ambao wapo ziarani nchini Uturuki na watarejea kuanzia Janauri 11, mwaka huu.
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limemteua Ofisa wake, Leslie Liunda wa Tanzania kwenda Ethiopia kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa utoaji leseni kwa klabu zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.
Ofisa huyo atawasili nchini Ethiopia kesho (Januari 2 mwaka huu) ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 6 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.
Utekelezaji wa kazi yake hiyo nchini Ethiopia utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirikisho la Soka Ethiopia (EFF), Wizara ya Michezo ya nchi hiyo, viongozi wa klabu na mameneja wa viwanja husika.

MWAKA MPYA NDO HUU UMEANZA CHEKI NYOTA WANAOTARAJIA KUTAMBA KATIKA USAJILI DIRISHA DOGO LA USAJILI LIKIANZA



While the January sales may have started on Boxing Day on high streets up and down the country, football clubs have had to wait patiently until the first of the month to begin their spending spree.
But finally the 31-day transfer window is officially open for business and clubs all over the country look set to ‘splash the cash’, ‘open their chequebooks’ and ‘break open their war chests’ (as well as other outdated methods of payment) in a bid to challenge for the Premier League, grab a European spot or avoid relegation.
The names most likely to attract the most interest are Arsenal’s hat-trick hero from the weekend, Theo Walcott who is out of contract in the summer, just like Chelsea’s match-winner from Sunday’s game against Everton, Frank Lampard. 
Will he stay or will he go? Theo Walcott could leave Arsenal this month
Will he stay or will he go? Theo Walcott could leave Arsenal this month
Franks for the memories: Chelsea are prepared to let Lampard leave at the end of his contract and he could leave this month
Franks for the memories: Chelsea are prepared to let Lampard leave at the end of his contract and he could leave this month
Liverpool have long been admirers of Walcott while a move abroad looks to be the most likely option for Lampard, unless of course he fancies helping his uncle Harry (Redknapp) out down the road at QPR.
One transfer that should be concluded early on, is Daniel Sturridge’s move from Chelsea to Liverpool after Rafa Benitez revealed the striker had a medical on Merseyside last weekend.
Where will he go? Demba Ba can leave Newcastle for £7m this month
Where will he go? Demba Ba can leave Newcastle for £7m this month
Demba Ba’s imminent departure from Newcastle looked to be one of the most straight forward moves of the window when it was revealed that his advisors were in talks with Chelsea on Sunday. Those talks broke down, however, and now it seems those people charged with helping him look like making the Senegal striker’s move anything but straight forward.
The Football League has been the breeding ground for many Premier League stars in the past, and clubs could look to boost their squads with another star of the future. 
Wilfred Zaha
Will Hughes
Young stars: Palace winger Wilfried Zaha and Derby midfielder Will Hughes could be on the move
Crystal Palace winger Wilfried Zaha and Derby’s England Under 21 midfielder Will Hughes could be two names looking to make the step up. Manchester United are among Zaha's admirers while Fulham and Tottenham are just two of the clubs keen on Hughes. 
Clubs will also look overseas to try and snap up a bargain, and two of the biggest names in European football could be heading to the Premier League, with Inter Milan midfielder Wesley Sneijder and Barcelona striker David Villa both available for moves.
Heading to England? Wesley Sneijder could be on his way out of Inter Milan
Heading to England? Wesley Sneijder could be on his way out of Inter Milan
London calling: David Villa is attracting interest from Chelsea and Arsenal
London calling: David Villa is attracting interest from Chelsea and Arsenal
Spurs and Liverpool are believed to be keen on Sneijder while London duo Arsenal and Chelsea are keeping tabs on Villa, who could be in line to link up with Spain strike partner Fernando Torres at Stamford Bridge.
Money will be spent and players will come and go, but anyone hoping for a repeat of the January window of two years ago will be left disappointed. 
Fernando Torres
Andy Carroll
Be warned: Not all January moves go to plan, as Fernando Torres and Andy Carroll found out in 2011
In January 2011, a record £225m was spent with moves that included Torres swapping Liverpool for Chelsea at a cost of £50m, Aston Villa signing Darren Bent for £18m, Edin Dzeko making a £27m switch to Manchester City and, perhaps most remarkably, Liverpool replacing Torres with Andy Carroll for £35m.
There are bound to be some surprises in 2013 winter window, but it is unlikely there will be any as big and as costly as Carroll.