Tuesday, November 27, 2012

KAMATI YA UCHAGUZI MKOA WA TABORA TAREFA YAPITIA USAILI WA MAJINA YA WAGOMBEA HII LEO


MWENYEKITI wa kamati ya uchaguzi mkoa wa tabora TAREFA bw.MKAMA BWIRE leo wamepitia usaili wa majina na kuthibitisha hayana kasoro yoyote katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi wa mkoa wa tabora katika mpira wa miguu majina 19.

Katika usaili huo alijumuika na kufanya kazi vizuri ipasavyo bila kufoji jina lolote la mgombea na wagombea 19 ndiyo wanaingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi mbalimbali katika mpira wa miguu mkoa wa tabora TAREFA.

Majina yaliyopitishwa hii leo katika usaili huo tarehe 27/11/2012  katika nafasi ya MWENYEKITI.

1.Musa Ntimizi

2.Yusuph kitumbo.

3.Laurent paul

-===NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI

1.A laija Mwiga

===NAFASI YA KATIBU

1.Albert sitta

2.Fatteh Dewj

===NAFASI YA KATIBU MSAIDIZI

,,,,,,HAKUNA MGOMBEA

====NAFASI YA MWEKA HAZINA

1.Mussa Msananga

===NAFASI YA MWEKA HAZINA MSAIDIZI

,,,,HAKUNA MGOMBEA

===NAFASI YA MJUMBE MKUTANO MKUU TFF

1.Dick Mlimuka

2.Milambo Kamili

3.Ramadhani Maghembe

4.Charles Mwakambaya

===NAFASI YA MWAKILISHI WA VILABU

1.Achery manjori

2.Razack j.Kumba

3. Lwamba yussa

===NAFASI YA UJUMBE KAMATI YA UTENDAJI

1.Stanslaus Sizya

2.Abdul mohamed Aman

3.James Erick Kabepele

===NAFASI YA MWAKILISHI WA MPIRA WA MIGUU KWA UPANDE WA WANAWAKE

1.Janeth Michael

Na kesho  tarehe 28/11/2012 ni siku ya kuwasilisha pingamizi kama zitakuwa zipo kwa wagombea wanaowania nafasi mbali mbali za uongozi.kama rufaa zitakuwepo na kama hazitakuwepo kuanzia tarehe 6/12/2012  wagombea wataruhusiwa kuanza kampeni mpaka tarehe 21/12/2012,na tarehe 22/12/2012 ni siku ya uchaguzi mkoa wa tabora TAREFA

 

KIM POULSEN AKIPIGA CHABO WAGANDA NA WAHABESHI NAMBOOLE

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Polusen (kulia) akishuhudia kwa makini mchezo wa Kundi A, kati ya Uganda na Ethiopia, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Kagame Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda. Wengine kushoto kwake ni Michael Mukunza wa Executive Solutions, Waratibu wa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Stars na Kocha Msaidizi, Sylvester Marsh. 

JB ATUA KIFALME DAR, AAHIDI SHOO YA KUFA MTU IJUMAA LEADERS


JB Mpiana akizungumza mna Waandishi Dar es Salaam leo
MWANAMUZIKI nguli wa dansi Afrika, JB Mpiana ametua jijini Dar es Salaam juzi tayari kwa maonyesho kadhaa, likiwamo lile la uzinduzi wa albamu ya Mashujaa Band inayokwenda kwa jina la Risasi Kidole, litakalofanyika Ijumaa katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.
Kabla ya shoo hiyo ya Ijumaa, JB Mpiana ambaye amekuja na kundi lake zima la Wenge Musica BCBG, likiwahusisha wanamuziki wake za zamani na wapya, atauwasha moto jijini Arusha kesho kabla ya kufanya kweli jijini Mwanza Jumapili.
Akizungumza katika Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki, Dar es Salaam, JB Mpiana ameahidi kutoa shoo ya aina yake ambayo anaamini itakonga nyoyo za Watanzania.
Alisema kuwa amefurahisa sana kuja Tanzania kwa mara nyingine, ikiwa ni pamoja na mapokezi aliyoyapata, akiahidi kutoa burudani ya nguvu kwa Watanzania kuwalipa mapokezi waliyomwonesha.
 “Nina imani waandaaji wamefanya maandalizi ya kutosha, nimekuja na wanamuziki wangu wote 25, nimekuja na vifaa vyangu vyote vilivyopo katika kundi langu, ili kutoa burudani ya kutosha kwa Watanzania.
 “Nimewaletea albamu inayojulikana kwa jina la Biloko (chakula), watanzania wajiandae kula, yaani kupata burudani ya nguvu kutoka kwangu na kundi langu,” alisema JB Mpiana.
Kati ya wasanii aliokuja nao, alisema wapo wale wa zamani aliokuwa nao enzi hizo ndani ya kundi lake hilo lilipoanza kutamba katika anga ya muziki, na wengine wapya ambao wapo fiti.
Katika programu yake hapa nchini, amesema atapiga nyimbo zake za zamani na mpya ili kuwapa watanzania fursa ya kupata vionjo vya zamani na vipya, kuweza kupima ubora wa kazi hizo.
Akizungumzia muziki wa Tanzania, amewataka wasanii wa hapa nchini kujituma na kuzipenda kazi zao na kuiheshimu waweze kufanikiwa katika kazi zao hizo.
Juu ya kiongozi wa safu ya unenguaji, alisema safari hii inaongozwa na mwanadada Zambrota, ikiwa ni baada ya kufariki kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Monica.
 “Nimefurahi sana kuja Tanzania kwa mara nyingine, wapenzi wa burudani wajiandae kupata shoo ya nguvu kutoka kwa JB Mpiana,” alisema mkali huyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya QS Muhonda, Joseph Muhonda, waratibu wa maonesho hayo, amesema kuwa ni matarajio yao wakazi wa Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, watafurahia shoo hiyo kutoka kwa JB Mpiana na Mashujaa kutokana na maandalizi ya nguvu waliyofanya, akiwataka wakazi wa maeneo hayo, kujitokeza kwa wingi.
Alisema kuwa katoka onesho la JB Mpiana jijini Arusha, atatumbuiza katika ukumbi wa Triple A kuanzia saa tatu usiku, wakati Desemba Mosi atakuwa katika ukumbi wa Villa Park kuanzia saa tatu usiku.
 “Maandalizi yote yapo sawa, kila kitu kimekamilika, tuliahidi JB Mpiana anakuja na kweli amekuja kama mlivyomuona,” alisema na kuongeza kuwa JB Mpiana atasindikizwa na wasanii wa Bongo Fleva kama H Baba, MB Doggy, Ney wa Mitego na wengineo.

TENGA ASEMA WATAKUTANA NA SERIKALI KUMALIZA UTATA WA TRA

Tenga

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, wanatarajiwa kukutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kuzungumzia mustakabali mzima wa suala la makato katika michezo mbalimbali.
Hatua hiyo inafuatia TRA kuzifunga akaunti za udhamini wa ligi hiyo kama shinikizo kwa TFF  kulipa makato ya kodi kwenye mishahara ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ tangu kipindi cha kocha Mbrazil Marcio Maximo kwa madai kwamba imekuwa haikatwi kodi za mishahara ya makocha na hivyo kufikia sh milioni 157,407.968.00.
Rais wa TFF, Leodger Tenga amesema leo kwamba kitendo walichokifanya TRA ni jambo la heri kwani kinaonyesha majukumu ya Serikali katika soka.
Alisema ukaribu uliopo sasa baina ya Serikali chini ya Rais Kikwete na soka ni mkubwa kutokana na ukweli kwamba  inachangia kwa kiasi kikubwa kulipa mishahara ya makocha wa timu za Taifa.
Alisema suala hilo linahitaji mazungumzo baina ya pande hizo ili kuweza kulipatia ufumbuzi na hakuna haja ya kuilaumu TRA kwa sababu inafuata taratibu zilinazostahili kwa mujibu wa kanuni.
 “Hawana njia nyingine ya kufanya hivyo ufumbuzi ni sisi ni kukutana na Wizara na TRA ili kulizungumza hili na katika siku mbili hizi tunarajiwa kukutana,”alisema
Tenga aliongeza kuwa TFF haina uwezo wa kulipa fedha hizo na kwamba hela zilizochuliwa si za Shirikisho hilo bali ni za ligi kuu Bara ambazo zimetolewa na wadhamini wake, kampuni ya simu za mkononi,Vodacom kwa maelekezo maalum.
 “Ni jambo nyeti na lazima lifanyiwe kazi, hatuwezi kumlamu mtu na nimatumaini tutakapoketi pamoja tutapata ufumbuzi,”alisema.
Aidha, Tenga alisema wanatarajia kuzungumzia suala la makato ya michezo mbalimbali ambayo yamekuwa yakilalamikiwa na vilabu kwa muda mrefu.
 “Changamoto za namna hiyo tumekuwa tukizifanyia kazi kwa muda mrefu na ndiyo maana tangu mwaka 2005 asilimia ya makato ya TFF imekuwa ikipunguzwa, nadhani ni kuendelea kuwa na subira.

TFF NA TAMTHILIYA TIKETI ZA ELEKTRONIKI



SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) linaamini kutumika kwa tiketi za kielektroniki katika mechi mbalimbali nchini utakuwa ni muarobaini wa tatizo la mapato.
Benki ya CRDB ndiyo imepewa tenda ya kutayarisha tiketi hizo ambazo zitaanza kutunmika rasmi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom mwezi Februari mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Rais wa TFF Leodger Tenga alisema kwamba hatua hiyo ni jambo la heri na muhimu sana katika kipindi hiki ambacho wadau wamekuwa wakilalamikia suala la upatikanaji wa mapato kiduchu.
Alisema pamoja na uzuri wa jambo hilo, lakini wengi watashtuka na kutaka kurudisha nyuma mchakato huo utakaojenga heshima, lakini Shirikisho hilo halitakubali kurudishwa nyuma.
 “Najua wengi litawaathiri sana kwa namna moja ama nyingine na hivyo kuanza kuleta vikwazo ili lisifanikiwe, tumesimama imara kuhakikisha hili linatimia ili kujenga heshima,”alisema Tenga

TFF YAPUUZA SUALA LA VIJEBA U17 YA KONGO BRAZZAVILLE

Tenga

RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga amewataka wachezaji wa timu hiyo kuachana na fikra ya kuwa wapinzania wao, Congo Brazaville inaundwa na wachezaji waliozidi umri ‘Vijeba’ , badala yake vijana hao wajitume ili ushindi upatikane.
Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa malalamiko ya Congo Brazavile kuchezesha Vijeba katika mechi yao ya awali ya kuwania kucheza fainali za Afrika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo Serengeti ilishinda bao 1-0.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Tenga alisema haoni sababu ya kuwakatia rufaa kama ilivyoelezwa awali, kwani tayari walisharipoti kwa kamishna wa mchezo huo na  kama watafanya hivyo itakuwa baadaye.
Alisema wachezaji hao hawana budi kuelekeza akili zao kwenye mechi ya marudiano itakayopigwa ugenini mwishoni mwa wiki hii na kuhakikisha wanashinda ili kusonga mbele.
 “Nisingependa hili neno la Vijeba liingie katika akili za hawa watoto ili waende kupambana na kurudi na ushind,”alisema.
Aidha, Tenga amewapongeza vijana hao kwa ushindi walioupata katika mchezo wao wa awali licha ya kuwa ni finyu na kuwataka kuendelea na moyo wa kujituma ili waweze kufika mbali.
 “Pia TFF inashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timu yao, sambamba na kamati ya kuisaidia Serengeti kwa mchango wao wa hali na mali,”alisema.
Katika hatua nyingine, Tenga ametolea ufafanuzi suala la mgawo wa sh mil 1 kati ya mil 23 zilizopatikana katika mchezo wa Serengeti Boys na wenzao wa Congo Brazaville baada ya kamati ya kuisaidia Serengeti ambayo ilichanga milioni 35 kulalamika.
Tenga alisema mil.35 zilizochangwa na kamati hiyo zilitumika kufidia hasara iliyopatikana katika mchezo huo kwani mchezo unaofanyika katika uwanja wa Taifa na kuingiza chini ya mil.80 ni lazima TFF ibaki na madeni.
 “Ndiyo maana tumekuwa tuklipeleka mechi bndogondogo na zile za vijana katika uwanja wa Uhuru kwa sababu ya gharama za Uwanja wa Taifa, lakini kutokana na uwanja wa Uhuru kutotumika ndo hatuna dudi kubaki Taifa na matokeo yake ndiyo kama hivyo.”alisema Tenga.
Tenga aliongeza kwamba, mara nyingi TFF imekuwa ikipata mzigo wa kulipa madeni yanayotokana na hasara za michezo mbalimbali inayofanyika kwenye uwanja wa Taifa.
Tenga alisema kwa sasa timu hiyo inatakiwa kuendelea kujengwa kisaikolojia ili iweze kuwa katika hali nzuri na kufanikisha malengo yake ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya soka la Tanzania.
Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi saba wa Serengeti  Boys kinatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Congo Brazzavile tayari kwa mchezo huo.

AVEVA WA SIMBA KUPAMBANA NA N YEZI WA YANGA DRFA



HATIMAYE wagombea  23 wamepitishwa kuwania uongozi katika Uchaguzi wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), unaotarajiwa kufanyika Desemba 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA, Juma Simba, alisema majina hayo yamepitishwa baada ya kufanyika usaili pamoja na kujadili pingamizi na rufaa zilizowasilishwa.
Alisema awali wagombea 36 walijitokeza na kuomba nafasi mbalimbali, kabla ya wengine kuenguliwa ama kujitoa katika kinyang’anyiro kwa sababu mbalimbali.
Aliwataja waliopitishwa kuwania nafasi ya uenyekiti ni pamoja na  Ayoub Nyenzi, Evans Aveva, Brown Ernest na Almasi Kasongo, huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti itawaniwa na Meba Ramadhan, Salum Mwaking'inda, Gungurungwa Tambaza na Ally Mayai.
Kwa upande wa nafasi ya Katibu watakaochuana ni pamoja na  Msanifu Kondo na Khamis Ambari, huku waliopitishwa kuwania  nafasi ya mjumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania ni Shafii Dauda, Muhsin Balhabouh na Shufaa Jumanne
 “Wanaowania ujumbe wa kamati ya utendaji ni Shaban Kupasya, Siza Chenja, Sunday Mwanahewa, Hamis Kisiwa, Franck Mchaki na Baraka Mapande wakati watakaowania ujumbe kuwakilisha klabu ni Benny Kisaka, Juma Pinto, Frank Mchaki na Philemon Ntahilaja”, alisema
Aidha, Simba aliwataja wajumbe ambao wamechujwa ni Salum Mkemi na Juma Jabir (Uenyekiti), Issac Mazwile (Makamu Mwenyekiti), Said Tully na Kassim Mustaffa (Katibu Mkuu), Isaack Mazwile (Mjumbe Mkutano Mkuu TFF) na Chano Karaha (Mjumbe Kamati ya Utendaji).

KENYA YAFUFUA MATUMAINI CECAFA TUSKER CHALLENGE

Kiungo wa Kenya, Kevin Omondi akimdhibiti mshambuliaji wa Sudan Kusini, Martin Kamis anayejaribu kuondoka na mpira katika mechi ya Kundi A, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge, Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda jioni hii. Kenya ilishinda 2-0 mabao ya David Ochieng dakika ya 24 na Clifton Miheso dakika ya 72. Kenya sasa inaongoza Kundi A kwa wastani wa mabao, ikiwa na pointi sawa na Uganda na Ethiopia ambazo zinamenyana baadaye kidogo.

Beki David Owino akiwatoka wachezaji wa Sudan

Kenya wakishangilia bao la pili

SIMBA SC WAMLILIA SHARO MILIONEA

Marehemu Sharo Milionea

MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa aliyekuwa msanii maarufu wa muziki na filamu, Hussein Ramadhani Mkiety, maarufu kwa jina la Sharo Milionea, kilichotokea jana usiku mkoani Tanga.
Kwa niaba ya klabu ya Simba na kwa niaba yake binafsi, Mwenyekiti anapenda kutuma salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu kutokana na msiba huu mkubwa sana si kwao pekee bali kwa taifa zima la Tanzania.
Sharo Milionea hakuwa msanii wa kawaida. Yeye ni miongoni mwa kizazi kipya cha vijana wa Kitanzania walioamua kutafuta maisha kwa kutumia vipaji walivyopewa na Mungu. Yeye alijitumbukiza zaidi katika uchekeshaji na baadaye akaonyesha uwezo mkubwa katika fani ya muziki.
Sharo alikuwa maarufu kiasi kwamba makampuni makubwa yalikuwa yameanza kumtumia kwenye matangazo yao ya kibiashara. Hii ilionyesha kwamba makampuni yalibaini faida itakayopatikana kwao kwa kumtumia msanii huyu ambaye bado alikuwa na heshima kubwa kwenye jamii kutokana na haiba yake na uwezo wake kwenye kazi alizokuwa akifanya.
Msiba huu umekuwa pigo kubwa kwa tasnia ya filamu ambayo bado inaomboleza vifo vya wasanii kama Steven Kanumba, Mlopelo na John Steven Maganga, waliofariki dunia mwaka huu pia.
"Ifahamike kwamba Sharo Milionea alikuwa miongoni mwa wasanii wa Kitanzania waliotuma maombi Simba ya kutaka kushiriki kwenye mchakato wa kutengeneza wimbo rasmi wa klabu ya Simba. Yeye alikuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa wakiumizwa na ukweli kwamba klabu kama Simba inashindwa kufanya biashara ya kuuza nyimbo zake ilhali wanunuaji wapo," alisema Rage.
Kwa klabu ya Simba, namna pekee ya kumuenzi marehemu ni kufanyia kazi mambo ambayo alikuwa akitushauri kwenye eneo la biashara. Ni matumaini yetu kwamba iwapo tutafanya lile alilokuwa akitushauri, atakuwa mwenye amani huko alikotangulia mbele ya haki.
Rage amewaomba wasanii wa tasnia ya filamu na muziki kuwa watulivu na wenye subra kwenye kipindi hiki kigumu kwao. Kila kitu katika maisha ya wanadamu kinapangwa na Mwenyezi Mungu na ndiyo maana Waswahili wana msemo kuwa Kazi ya Mungu haina makosa.
Mola na ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Hussein Ramadhani Mkeity (Kamwaga ni Ofisa Habari wa Simba SC).

ZANZIBAR WAOMBA RADHI KWA SARE YA JANA


Wachezaji wa Zanzibar baada ya mechi jana
NAHODHA wa Zanzibar, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amewaomba radhi mashabiki wa soka wa Zanzibar kwa kushindwa kuifunga Etritrea jana na kuahidi watafanya vizuri katika michezo ijayo.
Akizungumza  kutoka uganda  beki huyo wa Yanga alisema kwamba matokeo ya jana yaliwasononesha mno na hawakuyatarajia kabisa, na ndiyo maana baada ya mchezo wachezaji wote walikuwa wenye huzuni.
“Kwa kweli hatukutarajia kabisa, na hatuwezi kumlaumu mtu yeyote, sisi wenyewe tu hatukucheza vizuri. Hayo ni mambo ambayo yanatokea kwenye soka,”alisema.
Cannavaro alisema kwamba si kweli kama waliwadharau Eritrea, hapana bali ilitokea tu hali ya wao kutokuwa vizuri kimchezo.
“Tulikuwa tunajiamini na tuna uzoefu na Eritrea, ni timu inayosumbua sana, lakini leo (jana) mipango yetu yote waliinasa, inatokea hiyo kwenye mchezo, tunawaomba radhi mashabiki wetu nyumbani na tunaomba waendelee kutusapoti na kuwa na imani na timu yao,”alisema.
Cannavaro alisema wamejifunza kutokana na makosa ya jana na baada ya mechi kila mchezaji alisema kuna kazi ya kufanya. “Tumekubali wote, kuna kazi ya kufanya, na kweli tutafanya kazi kweli, tunajua mechi zote zilizobaki ni ngumu, lakini tutapigana,”alisema.

KIBOKO YA SIMBA, YANGA ATUA AZAM FC


Seif Abdallah
MSHAMBULIAJI wa Ruvu Shooting, Seif Abdallah amethibitisha kwamba kuanzia Januari mwakani atakuwa akichezea Azam FC ya Dar es Salaam katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Seif ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu akiwa na Ruvu Shooting,alisema jana mjini uganda  kwamba amekwishafikia makubaliano na Azam kujiunga nao mwakani.
“Azam ni timu kubwa, nitafurahi sana kuanza kuichezea mwakani, naamini ni hatua moja mbele ya mafanikio katika maisha yangu ya mpira na ninaamini pia nitafanya vizuri kwa sababu najiamini,”alisema chipukizi huyo.
Seif ana mabao saba hadi baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, akiwa anachuana na Didier Kavumbangu wa Yanga na Kipre Tcheche wa Azam, ambao kila mmoja ana mabao nane. 
Seif, ambaye katika CECAFA Tusker Challenge anaichezea Zanzibar alizifunga timu zote kubwa katika mzunguko wa kwanza, Simba, Yanga na Azam na baada ya hapo, vigogo wote hao wakawa wanamuwinda.
Yanga walifanya jitihada, wakati Simba walikuwa wanasikilizia, lakini Azam imewapiku wote.

NIYONZIMA ATAMANI KUBAKI YANGA, LAKINI...


Haruna Niyonzima
KIUNGO wa Yanga, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima amesema kwamba iwapo Yanga watakubali ofa ya klabu ya El Merreikh ya Sudan, atakuwa radhi kuondoka klabu hiyo na kwenda kuanza maisha mapya Khartoum.
Akizungumza  jana mjini uganda na waandishi wa habari Nahodha huyo wa Rwanda katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge alisema kwamba anaipenda sana Yanga lakini soka kwa sababu ni kazi yake, anaangalia maslahi pia.
“Mimi walinifuata Merreikh, nikawaambia nina mkataba na Yanga, wawasiliane na Yanga. Kama Yanga watakubali, mimi nitaangalia maslahi tu, Merreikh wakinipa maslahi mazuri kuliko nayopata Yanga sitakuwa na tatizo,”.
“Lakini kwanza, Yanga wao wenyewe wakubali kuniuza, wakikubali mimi sina tatizo, nawaheshimu sana Yanga wamenilea vizuri kwa kipindi chote nilichokuwa nao na ndiyo maana uwezo wangu haujayumba,”alisema Niyonzima.
Lakini Haruna alisema ana ofa pia ya kwenda kucheza Ubelgiji, ingawa alisema hiyo ipo nusu kwa nusu tofauti na ya Merreikh ambao wameonyesha nia ya moja kwa moja ya kumuhitaji.
“Kucheza Ulaya ni kitu ambacho kila mchezaji wa Afrika anakitaka, kama Mungu atapenda niondokee Yanga kwenda Ulaya, nitafurahi, na kama kuondokea Sudan, yote sawa, au nitamalizia soka yangu Afrika, yote sawa pia,”alisema.
Niyonzima ni kati ya wachezaji wa Yanga wanaong’ara katika CECAFA Tusker Challenge, wengine wakiwa ni Hamisi Kiiza wa Uganda, Frank Domayo wa Tanzania Bara na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wa Zanzibar.   
Niyonzima aliyesajiliwa Yanga mwaka jana kutoka APR ya nyumbani kwao, Rwanda jana aliiongoza nchi yake, kuifunga mabao 2-0 Malawi katika mchezo wa Kundi C, akiifungia Amavubi bao la pili kipindi cha pili, baada ya Jean Baptiste Mugiraneza kufunga la kwanza kipindi cha kwanza. 


KENYA HATARINI KUPOKONYWA TONGE MDOMOIN NA RWANDA


Kikosi cha Kenya
KENYA wako hatarini kupokonywa uenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwakani na badala yake wakapewa Rwanda.
Habari kutoka kwenye Mkutano wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) uliofanyika Ijumaa iliyopita, zimesema kwamba Rwanda wameambiwa wakae tayari kwa uenyeji wa michuano hiyo, iwapo Kenya itachemsha.
Habari zinasema Mwenyekiti wa Shirikiasho la Soka Kenya (FKF), Sam Nyamweya, awali alisema katika Mkutano Mkuu wa CECAFA kwenye hoteli ya Serena, kwamba Kenya tayari imekwishapata mfadhili wa mashindano hayo.
Kasha baadaye, Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Rwanda, FERWAFA, Celestin Ntagungira, akasema itakuwa tayari kutaja jina la mdhmaini  wa Challenge ndani ya wiki mbili wakipewa uenyeji.
Katika kuamua utata huo, Rais wa CECAFA Injinia Leodegar Tenga alisema haki za uenyeji wa Challenge ya mwakani zitakwenda kwa nchi ambayo kwanza itawahakikishia mdhamini wa mashindano.


YANGA IMEPANGA KUMUUZA NIYONZIMA.


Haruna Niyonzima
KLABU ya soka ya Yanga imepanga kumuuza kiungo wake, Haruna Niyonzima kwa dau la dola 150,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya Sh. 225 milioni kwenda El-Merreikh ya Sudan iliyoomba kumnunua.

Jumamosi wiki iliyopita, El-Merreikh iliiandikia Yanga ikionyesha nia yake ya kutaka kumnunua Niyonzima na kuomba iambiwe thamani ya mchezaji huyo ili iweze kumsajili haraka iwezekanavyo.

Mtandao huu una uhakika El-Merreikh ambayo makao makuu yake yapo mjini Khartoum, imepanga kwa gharama yoyote kuhakikisha inamsajili kiungo huyo ili aweze kuisaidia katika nafasi ya kiungo.

“Klabu yetu ina fedha za kutosha, tunachotaka ni kumsajili Niyonzima ili kuimarisha safu ya kiungo kwa sasa kwani tunadhani yeye ni miongoni mwa viungo wa Afrika Mashariki na Kati kwa wakati huu,” kilisema chanzo chetu makini cha habari kutoka El-Merreikh.

Katika barua pepe ya maombi ya kumsajili Niyonzima kutoka El-Merreikh, klabu hiyo imesisitiza kujibiwa haraka kuhusu dau la mchezaji ili mchakato wa usajili ufanyike haraka pindi makubaliano yakifikiwa. Dirisha dogo la usajili Tanzania Bara limeanza 15 Novemba hadi 15 Desemba mwaka huu.

Uongozi wa Yanga uliketi wikiendi hii na kukubaliana kumuuza Niyonzima kwa dau la dola 150,000 kwa El-Merreikh lakini ikisisitiza kuwepo kwa mazungumzo kati ya klabu hizo kwani kiungo huyo amebakisha si zaidi ya miezi sita kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga.

“Tulipokea maombi ya El-Merreikh wikiendi iliyopita na ndani ya muda mfupi tulikaa na kujadili kisha tukapata jibu la kumuuza Niyonzima kwa dola 150,000 lakini tunaweza kuzungumza zaidi na timu hiyo.

“Lengo letu ni kumuona mchezaji ananufaika na uwezo wake wa uwanjani na siyo kumzibia njia ya kutoka hasa inapopatikana nafasi ya kufanya hivyo. Tumeshawajibu El-Merreikh na sasa tunasikiliza watasemaje,” alisema kiongozi mmoja wa Yanga aliye ndani ya kamati ya usajili ambaye hakutaka jina lake litajwe.



Hata hivyo viongozi wa El-Merreikh kutoka Sudan, wamesema bado hawajapata majibu ya Yanga, na walipoambiwa klabu hiyo inahitaji dola 150,000 ili imuachie Niyonzima, mmoja wa viongozi hao alisema; “Mbona nyingi mno?”


Kiongozi huyo alisema kiasi hicho ni kikubwa kulinganisha na thamani ya mchezaji uwanjani na umri wake, pia muda uliobaki katika mkataba wake.


“Hata hivyo, majibu ya Yanga yakitufikia tutajadiliana na kuamua nini cha kufanya japokuwa Niyonzima ni mchezaji mzuri kweli,” alisema kiongozi huyo.


Niyonzima ambaye Yanga ipo katika mchakato huo wa kumuuza, kwa sasa yupo Rwanda akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kinachojiandaa na michuano ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Chalenji itakayoanza wikiendi hii huko Kampala, Uganda.


Kiungo huyo alipomtafutwa kwa njia ya simu, hakuweza kupatikana kuzungumzia maombi hayo ya El-Merreikh.

KATONGO AKABANA NA YAYA, DROGBA KUWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA BBC


Tuzo mchezaji Bora wa BBC 2012
Tuzo mchezaji Bora wa BBC 2012
Majina ya wachezaji watano wanaowania tuzo la BBC la mchezaji bora zaidi barani Afrika mwaka 2012 yametangazwa.
Yaya Toure, kwa mwaka wa pili mfululizo, yupo kwenye orodha hiyo.
Mwenzake katika timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba pia yumo.
Wachezaji wengine ni pamoja na Demba Ba kutoka Senegal, Younes Belhanda wa Morocco na nahodha wa timu ya Zambia, Christopher Katongo.
Huu umekuwa ni mwaka wa ufanisi kwa wachezaji hao, na timu za wachezaji wanne zikionyesha ustadi kwa kupata vikombe.
Inaelekea Drogba aliondoka Chelsea wakati muwafaka, mara tu baada ya timu yake kukamilisha msimu kwa ushindi wa klabu bingwa barani Ulaya, hii ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya klabu, na vile vile akipata bao la ushindi katika fainali ya Kombe la FA.Raia mwenzake wa Ivory Coast, Toure, naye akiichezea Manchester City, aliihakikishia timu yake ubingwa wa ligi kuu ya Premier kwa mara ya kwanza; kombe lao muhimu zaidi katika kipindi cha miaka 44.
Belhanda aliisaidia timu yake ya Ufaransa ya Montpellier kupata ushindi katika ligi ya Ufaransa daraja la kwanza, kwa kufanikiwa kupata magoli 12 katika msimu.
Katika mapambano ya kimataifa, Katongo, kutoka Zambia, naye akiiongoza timu kama nahodha, alifanikiwa kuiwezesha timu yake ya Chipolopolo kuishinda Ivory Coast, na kuibuka mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kuishinda Ivory Coast katika fainali, kupitia mikwaju ya penalti.
Ba hakung'ara katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya Senegal kuondolewa katika hatua ya makundi, lakini binafsi aliweza kuifanyia timu yake ya Newcastle kazi nzuri, na msimu uliopita alitangazwa kuwa mshambulizi bora zaidi, kwa kufunga jumla ya magoli 17, na kuiwezesha timu kumaliza katika nafasi ya tano.


KIM POULSEN: NITAWAGONGA TU BURUNDI SINA SHAKA YOYOTE.



Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Bara ( The Kilimanjaro Stars) Kim Poulsen amesema amesha isoma vizuri timu ya taifa ya Burundi na sasa anasubiri kuwafunga.

Pambano hilo litapigwa hapo kesho kwenye dimba la Uwanja wa Namboole ukiwa ni mchezo wa pili baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sudani Kusini mchezo uliopigwa jumapili iliyopita.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa ugumu wa aina yake kwakuwa linazikutanisha timu ambazo zote zilianza kwa matokeo ya ushindi ambapo wao Burundi walianza kwa kuwaning'iniza Somalia kwa mabao 5-1.
Timu yoyote itakayo shinda katika mchezo huo itakuwa imefuzu moja kwa moja kucheza hatua ya robo fainali kwani itakuwa imefikisha alama sita.
Kim Poulsen alitumia muda wa takribani dakika 45  kuzishuhudia Burundi na Somalia na baada ya hapo alisikika akisema kazi imekwisha.
 "Nimeziangalia timu hizi ambazo tuko katika kundi moja kwa dakika 45 nadhani kazi imekwisha, Burundi wana mchezo mzuri lakini wana makosa mengi ya kimchezo hivyo nitatumia makosa yao kupata ushindi"
"Ninakikosi kizuri ukilinganisha na jinsi walivyocheza hawa na ninakiamini"

"Kikosi changu kina wachezaji vijana ambao kila siku wanabadilika na wanajiamini sina shaka hata kidogo na uwezo wao na nina matumaini tutawashinda na kusonga mbele katika hatua ya robo fainali,".
Kim pia alisifu ushirikiano wa winga Mrisho Ngasa na mshambuliaji John Bocco akisema utazaa matunda mazuri katika kikosi chake.
"Ngasa na Bocco wanafanya kazi nzuri naamini wakiendelea na ushirikiano huu mambo yatakuwa mazuri zaidi kwetu,".alisema Kim.

 

 

CECAFA CHALENJI CUP: Rwanda 2-0 Malawi Zanzibar 0-0 Eritrea


Mabao mawili yaliyofungwa katika kila kipindi yametosha kuwapa ushindi wa mabao 2-0 timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi “The Flames” na hivyo kuanza vema kampeni ya kuwania taji la michuano ya ‘Cecafa Tusker Chalenji Cup 2012’mchezo wa kundi C uliopigwa katika dimba la Namboole.

Rwanda ilianza kulisakama lango la Malawi tangu mapema kunako dakika ya 8 kupitia kwa Jimmy Mbagara lakini hata alikuwa tayari mwamuzi wa pembeni alikuwa ashiria kuwa mfungaji alikuwa ameotea.

Jean Baptiste Muginereza hata aliamsha shamrashamra kwa mashabiki wa Amavubi kunako dakika ya 38 baada ya kunasa mpira wa krosi wa mlinzi wa Mwemere Ngiritushi.

Kabla ya goli hilo washambuliaji wa Malawi Joseph Kamwendo, Chimango Kayira na Green Harawa walikuwa wakishambulia ngome ya Rwanda lakini mlinda mlango wa Amavubi  Jean Claude Ndoli alikuwa alikuwa akifanya kazi ya ziada kuokoa michomo yao.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika huku mwamuzi Ali Kalyango alipopuliza filimbi ya kuashiria kuwa ni mapumziko Rwanda walikuwa mbele kwa bao hilo 1-0.

Baada ya mapumziko, Malawi walirejea kwa ari kwa kusukumu mashambulizi katika ngome ya Rwanda huku wakipata kona tano ndani ya dakika chache za kipindi hicho cha pili.

Dakika ya 78 kiungo ‘skipper’  Haruna Niyonzimana aliandika bao la pili kwa mabingwa hao wa mwaka 1999 baada ya kazi nzuri ya kuwazunguka mabeki wa Malawi kabla ya kuachia shuti kali lilikwenda moja kwa moja upande wa kulia wa mlinda mlango wa Malawi.

Ushindi huo umewapa uongozi wa kundi C wakiwa na alama 3 na magoli mawili na Malawi wakiwa mkiani.
Katika mchezo wa mapema Eritrea na Zanzibar zilikwenda sare ya bila kufungana

WILSHERE KUONGEZEWA MSHAHARA NA UNAHODHA JUU ARSENAL


KIUNGO Jack Wilshere yuko mbioni kupewa mkataba mpya wakati kocha Arsene Wenger akijiandaa kumpa beji ya Unahodha wa Arsenal mchezaji huyo.
Mjadala unaoendelea utamfanya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 aongezewe mshahara wake wa pauni 50,000 kwa wiki anaolipwa.
Nyota huyo wa England bado ana miaka miwili na nusu katika mkataba wake, lakini Arsenal inataka kumtia pingu ili asiote mbawa.
Perfect 10: Jack Wilshere was honoured by the famous shirt in the summer
Jack Wilshere sasa anavaa jezi namba 10
 
Mshambuliaji Mjerumani, Lukas Podolski ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi kwa sasa Arsenal, pauni 90,000 kwa wiki, na mshahara mpya wa Wilshere unatarajiwa kuwa katika kiwango hicho.

ANELKA KUTUA QPR JANUARI AKIJUTIA KWENDA CHINA


KOCHA mpya wa Queens Park Rangers, Harry Redknapp anataka kumsajili Nicolas Anelka Januari mwakani.
Redknapp atapewa pauni Milioni 10 za kusajili katika dirisha dogo, lakini atahitaji fedha zaidi ili kuingia sokoni.
Loan ranger: QPR want Nicolas Anelka to boost their survival bid
Nicolas Anelka 
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 anafahamu anatakiwa kuboresha safu yake ya ushambuliaji kutokana na kukabiliwa na majeruhi Andrew Johnson na Bobby Zamora, wanaomfanya abaki na Djibril Cisse kama mshambuliaji pekee.
Na Redknapp amemtambulisha mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea, Anelka kama mtu anayemtaka kwa mkopo.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 ana mkataba na  Shanghai Shenua, lakini anaweza kurejea kuwa muda kucheza England, baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu ya China.
Anelka kwa ujumla yuko tayari kurejea Ulaya baada ya kusema alifanya kosa kuhamia China.


WAZO LA KUONGEZA NCHI WENYEJI KATIKA MICHUANO YA EURO 2020 KUJADILIWA BRUSSELS.

KWA mujibu wa Chama cha soka cha Ujerumani-DFB mpango wa kuandaa michuano ya Ulaya mwaka 2020 katika nchi zote za bara hilo tofauti na nchi moja au mbili kama ilivyo hivi sasa linaonekana kuungwa mkono na mashirikisho mengi mengi ya soka barani humo. Kuelekea mkutano wa siku mbili wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA ambao utafanyika jijini Brussels, Katibu Mkuu wa DFB Helmut Sandrock amesema kuwa mara ya kwanza walishangazwa na wazo hilo lililotolewa na rais wa UEFA Michel Platini. Pendekezo hilo ambalo bado halijapitishwa na Kamati ya Utendaji ya UEFA litashuhudia nchi 12 mwenyeji wa michuano hiyo ambayo itajumuisha nchi 24 zitakazoshiriki tofauti na 16 kama ilivyo hivi sasa. Sandrock aliendelea kusema kuwa mara ya kwanza walishangazwa na wazo hilo lakini baadae walikaa chini kama DFB kuangalia upya pendekezo hilo na kuona kama kweli linafaa wazo linaonekana linawezekana. Platini alitoa wazo hilo la kuongeza nchi wenyeji kwenye michuano hiyo ili kupunguza muda mrefu wa maandalizi pamoja na gharama ambazo nchi hupata wakati wa maandalizi ya michuano hiyo.

SIMEONE AFURAHISHWA NA KIWANGO CHA ATLETICO.

MENEJA wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone ameonyesha kufuruhishwa na kiwango cha timu yake katika msimu huu wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga. Atletico wamefanikiwa kushinda michezo yao 13 kati ya 15 waliyocheza katika ligi hiyo na wapo nyuma kwa vinara wanaaongoza ligi hiyo Barcelona kwa alama tatu. Simeone aliwasifia wachezaji wake kwa kiwango walichokionyesha katika mchezo dhidi ya Sevilla Jumapili iliyopita na kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0. Hatahivyo kocha huyo alikataa kuzungumzia mchezo wa la Liga dhidi ya Real Madrid ambao utachezwa Jumamosi kwasababu ya mchezo wa Copa del Rey dhidi ya Real Jean ambao wanatarajia kucheza katikati ya wiki hii. Simeone ambaye ana umri wa miaka 42 amesema kuwa haitakuwa jambo la busara kuwazungumzia Real Madrid na kuwadharau Real Jean ambao wanatarajiwa kucheza nao kabla ya Real.

BRAZIL WACHOMOA KUMUHITAJI GUARDIOLA.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Brazil, Jose Maria Marin amekanusha taarifa kuwa watamteua kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola kukiongoza kikosi cha nchi hiyo katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014. Marin amesema kuwa kuna nafasi ndogo sana wa kuchukua kocha mgeni kwani wameshinda mara tano michuano ya Kombe la Dunia wakiwa na kocha mzawa hivyo hawaoni umuhimu wa kuwa na kocha wa kigeni katika kampeni za michuano ya 2014. Chanzo kimoja cha habari kilichokaribu na Guardiola kilidai Jumamosi kuwa Brazil ndio timu pekee ambayo kocha huyo yuko tayari kufundisha baada ya Mano Menezes kutimuliwa baada ya kuinoa timu hiyo kwa miaka miwili na nusu. Wakati akiinoa Brazil, Menezes amekiongoza kikosi cha nchi hiyo kushinda michezo 21 kati ya 40 ukiwemo mchezo wa fainali ya olimpiki ambao walipoteza kwa Mexico na kukosa medali ya dhahabu.

GERRARD, LAMPARD MIONGONI KATIKA ORODHA YA VIUNGO 15 WA FIFPRO 2012.

VIUNGO nyota wa kimataifa wa Uingereza, Steven Gerrard na Frank Lampard wametajwa kuwa miongoni wa viungo 15 waliopo katika orodha itakayounda kikosi cha dunia 2012 maarufu kama FIFPro. Eden Hazard, David Silva na Yaya Toure ni miongoni mwa wachezaji wengine ambao wanacheza katika Ligi Kuu nchini uingereza ambao nao wametajwa katika orodha hiyo. Viungo watatu kati ya hao ndio watachaguliwa kuunda kikosi cha dunia majina ambayo yatatangazwa wakati wa sherehe za utoaji tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or Januari 7 mwakani. Klabu ya Barcelona imetoa wachezaji viungo wanne kwenye orodha hiyo ambao ni Sergio Busquets, Csec Fabregas, Andres Iniesta na Xavi Hernandez ambao waliisaidia timu ya taifa ya Hispania kutetea taji lao la Ulaya. Mbali na hao wachezaji wengine waliokuwepo katika orodha ya viungo 15 pamoja na nchi na vilabu wanavyotoka ni pamoja na Xabi Alonso-Hispania na Real Madrid, Luka Modric-Croatia na Real Madrid, Mesut Ozil-Ujerumani na Real Madrid. Wengine ni Andrea Pirlo-Italia na Juventus, Franck Ribery-Ufaransa na Bayern Munich. David Silva-Hispania na Manchester City, Bastian Schweinsteiger-Ujerumani na Bayern Munich.

JOHN TERRY AJIFARIJI KWA KUVAA JEZI YA DI MATTEO.

 Nahodha wa Chelsea John Terry amemtumia maneno ya faraja na pole meneja wake wa zamani Roberto Di Matteo muda mfupi kabla ya mchezo wa kwanza wa mrithi wake Rafa Benitez dhidi ya Manchester City mchezo uliochezwa jumapili.
Mlinzi huyo yuko kwasasa yuko nje ya uwanja kufuatia maumivu ya mguu.
Mlinzi huyo katika kujifariji na kuonyesha ni namna gani alivyoguswa na kuondolewa kwa Di Matteo Stamford Bridge,  alilazimika kuweka pembeni jezi yake yenye nambari 26 japo kwa muda na kuvalia jezi nambari 16 kabla ya kuingia uwanjani kufanya mazoezi ya viungo na wataalamu wa viungo wa klabu yake.
Jezi hiyo namba 16 ilikuwa ikivaliwa na Di Matteo enzi za uchezaji wake wakati alipokuwa mchezaji wa Chelsea kwa kipindi cha miaka minne.
Hata hivyo licha ya kumuunga mkono meneja wake huyo wa zamani, Terry amesisitiza kuwa ndani ya chumba cha kubadilishia nguo hali ni shwari na vijana wameungana na Benitez licha ya upinzani kutoka katika viunga vya  Merseyside.
"Alhamisi tulimkaribisha Rafa Benitez kama meneja wetu mpya na wachezaji wote wanaangalia mbele kufanya naye kazi"


CHELSEA wamwangukia Refa Clattenburg!!

>>KUANZA tena kuchezesha Jumatano Southampton na Norwich City!!
CLATTENBURG1REFA Mark Clattenburg amekutana na Mwenyekiti wa Chelsea Bruce Buck jana katika kile kinachodhaniwa kutafuta suluhu baada ya Refa huyo kuoshwa na Chama cha Soka England, FA, kuhusu tuhuma za Chelsea kwamba alimkashifu Kibaguzi Mchezaji wao John Mikel Obi.
Mkutano huo, ambao pia ulihudhuriwa na Viongozi wa Marefa na Marefa wengine 16 pamoja na Mkuu wa Ligi Kuu England, Richard Scudamore, ulifanyika kwenye Kituo cha Soka cha St George.
Baada ya uchunguzi, Wiki iliyopita FA ilizikataa tuhuma za Chelsea dhidi ya Clattenburg na sasa Refa huyo anatarajiwa kuchezesha Mechi yake ya kwanza Siku ya Jumatano tangu Chelsea waibue sakata hilo katika Mechi iliyochezwa Oktoba 28 Uwanjani Stamford Bridge kati ya Chelsea na Manchester United na Chelsea kuchapwa Bao 3-2.
Jumatano, Clattenburg atacheza Mechi kati ya Southampton na Norwich City na Jumamosi ijayo amepangiwa Mechi kati ya Arsenal na Swansea City.
Usuluhishi huu pia unafuta kikwazo cha Clattenburg kuchezesha Mechi za Chelsea hapo baadae.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa v Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool
[SAA 5 Usiku]
Wigan v Man City
Man United v West Ham
Jumamosi 1 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Ham v Chelsea
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Swansea
Fulham v Tottenham
Liverpool v Southampton
Man City v Everton
QPR v Aston Villa
West Brom v Stoke
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Reading v Man Utd
Jumapili Desemba 2
[SAA 1 Usiku]
Norwich v Sunderland
Jumatatu Desemba 3
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Wigan


SIR ALEX FERGUSON: Anderson ataanza Mechi Jumatano!


MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRAMeneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, amethibitisha kuwa Anderson ataanza Mechi ya Jumatano ya Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford na West Ham baada ya kucheza vizuri sana alipoingizwa Mechi ya Jumamosi wakati Man United wapo nyuma kwa Bao 1-0 walipocheza na QPR na kuisukuma Timu kushinda 3-1.
Ushindi huo, na sare ya Chelsea na Man City Siku ya Jumapili, imewafanya Man United wakae na kubaki kileleni kwenye Msimamo wa Ligi.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu tu:
1 Man United Mechi 13 Pointi 30
2 Man City Mechi 13 Pointi 29
3 WBA Mechi 13 Pointi 26
4 Chelsea Mechi 13 Pointi 25
5 Everton Mechi 13 Pointi 21
6 Arsenal Mechi 13 Pointi 20
7 Tottenham Mechi 13 Pointi 20
8 West Ham Mechi 13 Pointi 19
9 Swansea Mechi 13 Pointi 17
10 Fulham Mechi 13 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, Ferguson alithibitisha kutokuwepo kwa Winga Nani ambae bado ni majeruhi na pia kuwepo kwa wasiwasi kuhusu Antonio Valencia anaeuguza maumivu ya paja ingawa hatima yake itajulikana Jumanne.
Kiungo Paul Scholes yeye haruhusiwi kucheza Mechi hii baada ya kuzoa jumla ya Kadi za Njano 5.
Mbali ya Mashabiki wa Man United kumchagua Anderson kuwa ndie Mchezaji Bora wa Mechi kati ya Man United na QPR, hata Ferguson mwenyewe amekiri hilo alipotamka: “Ando ndie alitupa ushindi. Uchezaji wake ulikuwa wa hali ya juu sana. Yeye aliibeba Timu na kulazimisha gemu iwe kwetu na hilo limempa uhakika kucheza Mechi ya Jumatano.”
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa v Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool
[SAA 5 Usiku]
Wigan v Man City
Man United v West Ham
Jumamosi 1 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Ham v Chelsea
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Swansea
Fulham v Tottenham
Liverpool v Southampton
Man City v Everton
QPR v Aston Villa
West Brom v Stoke
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Reading v Man Utd
Jumapili Desemba 2
[SAA 1 Usiku]
Norwich v Sunderland
Jumatatu Desemba 3
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Wigan

BPL: Ya kati ya Wiki kunguruma Jumanne & Jumatano!

BPL_LOGO>>TAMU: Chelsea v Fulham, Everton v Arsenal, Spurs v Liverpool!
>>VINARA Man United wapo Old Trafford v West Ham!
>>MABINGWA Man City ugenini DW kuivaa Wigan!!
BPL, Barclays Premier League, kwa sisi Ligi Kuu England, itarindima tena kati ya Wiki, Jumanne na Jumatano, kwa Timu zote 20 kutinga dimbani na vinara wa Ligi, Manchester United, watakuwa nyumbani Old Trafford, kumkaribisha Rafiki mkubwa wa Sir Alex Ferguson, Meneja Sam Allardyce, atakapoiongoza Timu yake West Ham.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu tu:
1 Man United Mechi 13 Pointi 30
2 Man City Mechi 13 Pointi 29
3 WBA Mechi 13 Pointi 26
4 Chelsea Mechi 13 Pointi 25
5 Everton Mechi 13 Pointi 21
6 Arsenal Mechi 13 Pointi 20
7 Tottenham Mechi 13 Pointi 20
8 West Ham Mechi 13 Pointi 19
9 Swansea Mechi 13 Pointi 17
10 Fulham Mechi 13 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
Bila shaka, Mechi za mvuto ni hasa 3 za Chelsea v Fulham, Everton v Arsenal na Spurs v Liverpool.
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa v Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool
[SAA 5 Usiku]
Wigan v Man City
Man United v West Ham
Jumamosi 1 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Ham V Chelsea
[SAA 12 Jioni]
Arsenal V Swansea
Fulham V Tottenham
Liverpool V Southampton
Man City V Everton
QPR V Aston Villa
West Brom V Stoke
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Reading V Man Utd
Jumapili Desemba 2
[SAA 1 Usiku]
Norwich V Sunderland
Jumatatu Desemba 3
[SAA 5 Usiku]
Newcastle V Wigan