Monday, December 24, 2012

MTIGINJOLA KUONGOZA KAMATI YA RUFANI YA UCHAGUZI TFF


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemteua Idd Mtiginjola kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF iliyoundwa kutokana na marekebisho ya Katiba yaliyofanyika hivi karibuni. Mtiginjola ambaye ni Wakili wa kujitegemea ataongoza kamati hiyo yenye wajumbe watano ambayo sasa itakuwa chombo cha mwisho kusikiliza rufani zinazotokana na uchaguzi wa TFF, na wanachama wa TFF ambao hawatakubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Kabla ya uteuzi huo, Mtiginjola alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF inayoongozwa na Kamishna wa Polisi (CP) mstaafu Alfred Tibaigana. Nafasi yake katika kamati hiyo na ile ya mjumbe mwingine Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shabani Semlangwa aliyefariki dunia Julai mwaka huu zitajazwa hivi karibuni. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF ambayo vinara wake (Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti) wanatakiwa kitaaluma kuwa wanasheria ni Francis Kabwe. Kabwe ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Wajumbe wengine walioteuliwa na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake cha jana (Desemba 23 mwaka huu) ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Mohamed Mpinga ambaye pia kitaaluma ni Mwanasheria. Wengine ni mshambuliaji wa zamani wa timu ya Reli Morogoro, Profesa Madundo Mtambo ambaye kwa sasa ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mjini Morogoro, na mdau wa soka Murtaza Mangungu ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini.

MECHI YA STARS, CHIPOLOPOLO YAINGIZA MIL 109/-
 
 Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zambia (Chipolopolo) lililochezwa juzi (Desemba 22 mwaka huu) limeingiza sh. 109,197,000. Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 17,383 waliokata tiketi kushuhudia mechi kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 16,657,169.49, maandalizi ya mchezo sh. 55,339,510, tiketi sh. 5,803,900, ulinzi na usafi kwa Uwanja wa Taifa sh. 2,350,000, Wachina (technical support) sh. 2,000,000, umeme sh. 300,000 na maandalizi ya uwanja (pitch marking) sh. 400,000. Nyingine ni bonasi kwa Taifa Stars sh. 13,826,313, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 2,504,022, asilimia 10 ya uwanja sh. 1,252,011, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 626,005 na asilimia 65 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 8,138,070. Mapato ya mechi nyingine za Taifa Stars ilizocheza nyumbani mwaka huu yalikuwa Taifa Stars vs Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC (Leopards) iliyofanyika Februari 23 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sh. 32,229,000. Taifa Stars vs Msumbiji (Mambas) iliyochezwa Februari 29 mwaka huu sh. 64,714,000. Taifa Stars vs Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 40,980,000. Taifa Stars vs Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zilipatikana sh. 124,038,000 na Taifa Stars vs Kenya (Harambee Stars) iliyofanyika Novemba 14 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza iliingiza sh. milioni 45.

CASILLAS AKATAA KUMKOSOA MOURINHO.

NAHODHA wa klabu ya Real Madrid, Iker Casillas amekataa kukosoa maamuzi ya kocha wake Jose Mourinho baada ya kumuweka benchi katika mchezo wa Jumamosi ambao walifungwa mabao 3-2 na Malaga. Uamuzi wa kumuacha Casillas ulielezewa na kocha huyo Mreno kama la kiufundi lakini ilisababisha Madrid kupoteza alama tatu muhimu katika mchezo huo wa La Liga. Akihojiwa Casillas amekiri kuwa hakuzoea hali hiyo ya kutocheza lakini siku zote kocha ndio anachagua nani acheze na asicheze hivyo akiwa kama mchezaji lazima aheshimu maamuzi yao kocha. Amesema wachezaji wenzake wote wamekuwa wakimfariji kama walivyokuwa wakimfariji Antonio Adan ambaye ni golikipa namba mbili aliyechukua namba ya Casillas katika mchezo dhidi ya Malaga. Suala la Mourinho kumuacha Casillas limechukuliwa tofauti na wadau wengi wa soka mmojawapo akiwa mkurugenzi wa zamani wa michezo wa Madrid Jorge Valdano ambaye anaamini kuwa kocha huyo alikuwa akifikisha ujumbe kwamba yeye ndiye bosi katika klabu hiyo. 

CHELSEA YAVUTA PAUNDI MILIONI 12 KWA STURRIDGE.

KLABU ya Chelsea imekubali kumuuza mshambuliaji wake Daniel Sturridge kwenda Liverpool kwa ada ya paundi milioni 12. Mshambuliaji huyo ambaye alifanyiwa vipimo vya afya Jumapili anategemewa kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na Liverpool katika muda wa saa 24 zijazo. Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa akitaka kupigania namba Chelsea mpaka mkataba wake utakapomalizika mizei 18 ijayo, atakuwa akilipwa na Liver mshahara wa paundi 60,000 kwa wiki. Chelsea itakuwa imepata faida kubwa kwa kumuuza mshambuliaji huyo ambaye walimnunua kwa ada ya paundi milioni 1.5 akitokea klabu ya Manchester City mwaka 2009.

MDOGO WAKE BALOTELLI AKAMATWA.

KAKA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Italia, Mario Balotelli alikamatwa Jumapili kwa tuhuma za kujeruhi maofisa wawili wa polisi wakati wa vurugu zilizotokea mtaani. Enoch Barwuach ambaye ni mdogo wake Balotelli ambaye anacheza katika klabu ya Manchester City anakabiliwa na mashtaka ya kushambulia na kukataa kukamatwa baada ya kujihusisha na ugomvi katika klabu ya usiku Jumamosi huko Brescia, Italia. Barwuah mwenye umri wa miaka 20 ambaye amezaliwa tumbo moja na Balotelli alilala lupango kabla ya kuhamishwa ambapo anatarajiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili. Mdogo wake Balotelli ameonyesha kufuata nyendo za kaka yake ambaye amekuwa akikumbwa na matukio mbalimbali ya vurugu ndani na nje ya uwanja.

HUNTERLAAR AKUBALI KUONGEZA MKATABA SCHALKE.

KLABU ya Schalke 04 ya Ujerumani imethibitisha kuwa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uholanzi, Klaas-Jan Hunterlaar amekubali kuongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo. Hunterlaar mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa kuhamia katika vilabu mbalimbali vya Ulaya ikiwemo Inter Milan, Arsenal na Liverpool lakini sasa tayari amesaini mkataba mpya utakaombakisha hapo mpaka 2015. Mhsmabuliaji huyo aliwaambia wavuti wa klabu hiyo kuwa amefikiri kwa muda mrefu na makini kabla ya kuamua kusaini mkataba mpya na anajisikia furaha kuendelea kuwepo katika klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili mingine. Hunterlaar alijunga na Schalke akitokea AC Milan mwaka 2010 akiwa pia amepitia katika vilabu vya Real Madrid ya Hispania na Ajax Amsterdam ya nyumbani kwao.

VAN ANA BAHATI KUWA HAI - FERGUSON.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amedai kuwa beki wa Swansea City Ashley Williams angewewa kumuua Robin van Persie wakati wa mchezo baina ya timu hizo uliochezwa katika Uwanja wa Liberty jana. Beki huyo wa kimataifa wa Wales alipiga mpira uliomgonga kichwani Van Persie katika kipindi cha pili na kupelekea mshambuliaji huyo kunyanyuka kwa hasira na kumvaa Williams na wote kupelekea kupewa kadi nyekundu. Ferguson amesema kuwa tukio hilo ni bay asana kwani lingeweza kusababisha madhara makubwa kama kifo hivyo aliomba Chama cha Soka cha Uingereza-FA kuchunguza na kutoa adhabu. Williams akihojiwa mara baada ya mchezo huo alidai kuwa lilikuwa tukio la bahati mbaya hakudhamiria kumbutua na mpira kichwani Van Persie na kusababisha nyota huyo kushikwa na jazba. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 hiyo ikiwa ni sare ya kwanza United katika michezo 21 waliyocheza ambapo bado wamebakia kileleni mwa Ligi Kuu nchini humo wakiongoza kwa alama 43.

NAIKUMBUKA NA HII KALI YA MWAKA YA MCHEZAJI HUYU WA PSG NA TIMU YA TAIFA YA SWEDEN ALIVYOWAFANYA ENGLAND TAREHE 14/11/2012 INGIA UIONEEEEEEEEEE

MAAJABU: IBRAHIMOVIC AIPIGA UINGEREZA MABAO 4, LA MWISHO BAO LA ‘MILELE’!

 

Zlatan Ibrahimovic akiruka ‘tick-tack’ akiwa umbali wa mita 27 na kufunga bao.

MCHEZAJI soka wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic, mwezi wa 11 tarehe 14 mwaka 2012  alipiga mabao manne peke yake dhidi ya timu ya England katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa  jijini Stockholm, Sweden.  Timu hizo zilimaliza mchezo kwa mabao 4 – 2.
Maajabu ya Ibrahimovic ni goli lake la mwisho -- la nne.  Goli hili alilifunga kwa ‘tick-tack’ akiwa umbali wa mita 27 akiwa amelipa goli mgongo.  Aliupiga mpira huo kwa nyuma na ukapaa juu kwa mita 7.5 na ukatua moja kwa moja golini bila ya kudunda popote!
                      ..
.akiwa hewani.
..
.akishangilia baada ya kufunga bao hilo.

TANOJUMAINSPORTS INAKULETEA HABARI KALI KUMI ZA KUAGA MWAKA WA 2012 ZILE AMBAZO ZIMEHEADLINE SANA SANA KATIKA VICHWA VYA WATU HAPA TANZANIA NA ULIMWENGUNI KOTE.....NAANZA NA KIFO CHA NGULI WA MUZIKI TANZANIA STEVEN CHARLES KANUMBA....TAREHE 7/4/2012 R.I.P THE GREAT

BPL: HAKUNA KULALA, JUMATANO UPYA, ZOTE 20 DIMBANI!

BPL: HAKUNA KULALA, JUMATANO UPYA, ZOTE 20 DIMBANI!

BPL_LOGOZILE Mechi mfululizo za Ligi Kuu England zitaendelea tena Jumatano, Desemba 26, kwa Timu zote 20 kushuka Dimbani na Siku 3 baadae zote zitakuwa kazini.

RATIBA:
Jumatano 26 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Ham
Everton v Wigan
Fulham v Southampton
Man United v Newcastle
Norwich v Chelsea
QPR v West Brom
Reading v Swansea
Sunderland v Man City
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Tottenham
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Stoke v Liverpool

MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 18 Pointi 43
2 Man City Mechi 18 Pointi 39
3 Chelsea Mechi 17 Pointi 32
4 Arsenal Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 14]
5 Everton Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 8]
6 Tottenham Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 5]
7 WBA Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 4]
8 Liverpool Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 4]
9 Stoke Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
10 Norwich Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -7]
11 Swansea Mechi 18 Pointi 24
12 West Ham Mechi 18 Pointi 23
13 Fulham Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -5]
14 Newcastle Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -6]
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 18 Pointi 18
17 Southampton Mechi 17 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9

MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton
 

BPL: Chelsea yarudi Ligi kwa Kishindo cha 8-0, Man United yabanwa!!

BPL_LOGO>>FERGIE ATAKA WILLIAMS AFUNGIWE!!!
Baada ya kushindwa kutwaa Ubingwa wa Dunia huko Japan kwa kufungwa Fainali na Corinthians na jana kujikuta wakiporomoshwa hadi nafasi ya 7, leo Chelsea wamerudi kwa kishindo kwenye Ligi Kuu England na kutwaa tena nafasi yao ya 3 walipoishindilia Aston Villa Bao 8-0 Uwanjani Stamford Bridge na mapema, vinara Manchester United, walitoka sare ya 1-1 na Swansea City huko Liberty Stadium.
DONDOO FUPI za MECHI HIZO:
CHELSEA 8 ASTON VILLA 0
Chelsea leo wakicheza kwao Uwanja wa Stamford Bridge wamerejea kwenye nafasi ya 3 baada ya kuishindilia Aston Villa Bao 8-0.

WAFUNGAJI:
-Torres Dakika ya 3
-Luiz 29
-Ivanovic 34
-Lampard 58
-Ramires 75 & 90
-Oscar 79 (Penati)
-Hazard 83
Aston Villa 0

Mbali ya kufunga Goli hizo 8 Chelsea pia walikosa Penati baada ya Chipukizi toka Brazil, Piazon, kuipiga na Kipa Guzan kuipanchi.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Luiz, Lampard, Moses, Mata, Hazard, Torres
Akiba: Turnbull, Ramires, Oscar, Ferreira, Marin, Piazon, Ake.
Aston Villa: Guzan, Herd, Clark, Baker, Lowton, Bannan, Westwood, Lichaj, Weimann, Holman, Benteke
Akiba: Given, Ireland, El Ahmadi, Albrighton, Delph, Bowery, Bennett.
Refa: Phil Dowd
SWANSEA 1 MAN UNITED 1
Manchester United bado wapo kileleni mwa Ligi Kuu England kwa Pointi 4 mbele ya Mahasimu wao Man City licha ya leo kutoka sare ya Bao 1-1 na Swansea City Uwanjani Liberty.
Man United walitangulia kufunga kwa Bao la kichwa la Patrice Evra kufuatia kona ya Robin van Persie katika Dakika ya 16 lakini Swansea walisawazisha katika Dakika ya 29 kwa Bao la Michu baada ya shuti la Jonathan De Guz kutemwa na Kipa De Gea na kutua kirahisi miguuni mwa Michu.
Kipindi cha Pili Man United walikosa Bao nyingi pamoja na mbili zilizogonga mwamba  lakini tukio ambalo huenda likaleta mjadala ni pale Robin van Persie alipofanyiwa faulo na Refa kupiga Filimbi lakini Beki wa Swansea, Williams, akaupiga mpira kwa nguvu na kumbabatiza kichwani Van Persie wakati akiwa amelala chini na Van Persie akapandwa na jazba na kuanza kuvutana na Williams.
Refa Michael Oliver aliwapa Kadi za Njano Wachezaji wote hao wawili lakini Sir Alex Ferguson ametaka FA ichukue hatua zaidi kwa Williams ambae alidai angeweza kumvunja shingo Van Persie.
VIKOSI:
Swansea: Vorm, Tiendalli, Chico, Williams, Davies, Dyer, Britton, Agustien, de Guzman, Routledge, Michu
Akiba: Tremmel, Graham, Monk, Shechter, Moore, Ki, Richards.
Man United: De Gea, Jones, Evans, Vidic, Evra, Valencia, Carrick, Cleverley, Young, Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Giggs, Hernandez, Welbeck, Scholes, Fletcher, Buttner.
Refa: Michael Oliver

MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 18 Pointi 43
2 Man City Mechi 18 Pointi 39
3 Chelsea Mechi 17 Pointi 32
4 Arsenal Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 14]
5 Everton Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 8]
6 Tottenham Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 5]
7 WBA Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 4]
8 Liverpool Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 4]
9 Stoke Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
10 Norwich Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -7]
11 Swansea Mechi 18 Pointi 24
12 West Ham Mechi 18 Pointi 23
13 Fulham Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -5]
14 Newcastle Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -6]
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 18 Pointi 18
17 Southampton Mechi 17 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumatano 26 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Ham
Everton v Wigan
Fulham v Southampton
Man United v Newcastle
Norwich v Chelsea
QPR v West Brom
Reading v Swansea
Sunderland v Man City
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Tottenham
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Stoke v Liverpool

AZAM BINGWA KOMBE LA UHAI, NI FURAHA DABO DABO CHAMAZI


TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Azam, maarufu kama Azam Academy, imehitimisha wiki ya furaha kwa klabu hiyo, baada ya kunyakua ubingwa wa Kombe la Uhai, linaloshirikisha timu za vijana za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Azam Akademy imetwaa ubingwa huo, baada ya kushinda kwa penalti 3-1, kufuatia sare ya 2-2 na Coastal Union ya Tanga ndani ya dakika 120 za pambano kali na la kusisimua.
Ushindi wa Azam Academy, unakuja siku moja tu baada ya kaka zao, Azam FC kutwaa ubingwa wa Kombe la Hisani juzi mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa kuwafunga wenyeji Dragons FC kwa penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Juzi Azam walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha dakika ya 75 na katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na Samih Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
Katika mchezo wa leo, Azam ilimenyana kiume na Coastal ambayo inaonekana kuinukia vizuri katika uwekezaji kwenye soka ya vijana kabla ya bingwa kupatikana kwa mikwaju ya penalti.  
Mapema asubuhi katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Simba waliokuwa mabingwa watetezi, waliifunga 3-0 Mtibwa Sugar na kunyakua nafasi hiyo.
Aidha, Bakari Shime wa Coastal Union ametwaa tuzo ya Kocha bora, Mansur A. Mansur wa Coastal Union kipa bora, Ramadhan wa Simba aliyefunga mabao sita, ameibuka mfungaji bora, Ruvu Shooting timu yenye Nidhamu, Joseph Kimwaga wa Azam mchezaji bora na Isiaka Mwalile refa bora.

SWANSEA CITY VS MANCHESTER UNITED JANA,SHUJAA EVRA NA MICHU WALIOAMUA KUGAWANA POINTI MOJA MOJA EBU ICHEKI

MGANGA WA TORRES LABDA KAPATIKANA EBU CHEKI HILI GOLI ALILOFUNGA DAKIKA YA 3 HIYO JANA DHIDI YA ASTON VILLA WAKIWA WANAIADHIBA A.VILLA DARAJAN 8 BILA

MABINGWA AZAM WAREJEA NYUMBANI KIFUA MBELE KUSAKA MATAJI MENGINE


Kikosi cha Azam kilichokuwa tishio DRC
MABINGWA wa Kombe la Hisani, linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Azam FC ya Dar es Salaam wanaondoka leo saa 5:00 za hapa, sawa na saa 7:00 mchana za Afrika Mashariki, kurejea nyumbani Tanzania kwa furaha baada ya kutwaa taji hilo.
Azam wanaondoka kwa ndege ya Kenya Airwarys na watapitia Nairobi, ambako wataunganisha ndege ya kurejea Dar es Salaam.
Katibu wa Azam, Nassor Idrisa amesema kwamba timu ikirejea Dar es Salaam, wachezaji watapewa mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya sikukuu ya Krisimasi na baada ya hapo watakutana kujiandaa kwa safari ya Zanzibar kwenda kutetea Kombe lao la Mapinduzi.
Azam juzi ilitwaa ubingwa wa Kombe la Hisani baada ya kuwafunga wenyeji, Dragons FC kwa penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs mjini hapa.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha dakika ya 75 na katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na Samih Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
Azam juzi ilicheza bila kocha wake Mkuu, Muingereza Stewart Hall ambaye aliondoka juzi usiku mjini hapa kwenda kwao Uingereza kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya na iliongozwa na Kocha Msaidizi, Kali Ongala.
Azam iliingia fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
Kikosi cha Azam kilichoshiriki mashindano haya ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki, Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey Mieno na Joackins Atudo.
Katika mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti.