Thursday, November 1, 2012

 

Kikapu Taifa yapamba moto

Brown Msyani,Tanga
Timu ya mpira wa kikapu ya mkoa wa Arusha imeichapa timu ya mkoa wa Tanga kwa pointi 87-50 katika mfulilizo wa mashindano ya Kombe la Taifa kwenye Uwanja wa mkwakwani mjini hapa.

Katika mchezo huo, mchezaji Bariki Kilimbo wa Arusha alifunga pointi 18 peke yake na kuzuia mara 6, pasi mara 6.

Aliyemfuatia kwa kujaza pointi nyingi alikuwa Martin Ajesa aliyepata 15, huku upend wa Tanga B Sefu Semboya akifunga pointi 25 akifutiwa na Abasi Omary aliyefunga pointi 10.

Timu zote ziliingia dimbani na kucheza mchezo wa kasi uliojaa pasi za haraka haraka, huku Arusha ikiongoza kwa pointi 16-9 robo ya kwanza.

Katika nusu ya pili, walikuwa Arusha waliendelea kuipeleka puta Tanga B iliyolazimika kuutafuta mpira kwa 'tochi' na kujikuta wakiwa nyuma kwa pointi 28-11.

Arusha walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa 44-20, na robo ya mwisho, Arusha walikuwa mbele kwa 30-11.

Katika mchezo mwingine, timu ya Mkoa wa Singida iliifunga Kilimanjaro kwa point 79-58.

Mashindano hayo yaliyoanza juzi kwa wenyeji Tanga kuanza vizuri baada kuifunga Pwani pointi 64-4.

Mashindano ya mwaka jana, Dar es Salaam, Singida ndiyo walioibuka na ubingwa baada ya kuifunga Unguja katika mchezo wa fainali.

Kwa upande wa wanawake, mabingwa walikuwa timu ya mkoa wa Mbeya.

 

VPL: Stewart Hall arudi Chamazi kwa kishindo, AZAM yaishindilia Coastal 4-1!!

>>NI SALAM SPESHO kwa Yanga Jumapili!!!
VPL_LOGOWakiwa kwao Uwanja wa Azam Complex huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC leo wameitwanga Coastal Union kwa bao 4-1 katika Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, VPL, ikiwa ni Mechi ya kwanza tu kwa Kocha Stewart Hall alierejeshwa tena Klabuni hapo baada ya kuondolewa Mwezi Agosti na nafasi yake kutwaliwa na Kocha kutoka Nchini Serbia Boris Bunjak aliefukuzwa majuzi baada ya kutwangwa na Simba.
++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za Juu:
1 Simba Mechi 11 Pointi 23 [Mabao: Kufunga: 20 Kufungwa: 8 Tofauti: 12]
2 Yanga Mechi 11 Pointi 23 [Mabao: Kufunga: 21 Kufungwa: 10 Tofauti: 11]
3 Azam FC Mechi 10 Pointi 21
4 Coastal Mechi 11 Pointi 19
++++++++++++++++++++++++++
Ushindi huu wa leo umeifanya Azam ikamate nafasi ya 3 ikiwa na Pointi 21 kwa Mechi 10 wakiwa wamecheza Mechi moja pungufu ya Timu za juu yao Simba na Yanga ambazo zote zina Pointi 23 kila mmoja.
Bao za Azam, ambao waliongoza 3-0 hadi mapumziko, zilifungwa na Gaudence Mwaikimba, Kipre Tchetche, Khamis Mcha na Othman wa Coastal aliejifunga mwenyewe.
Bao pekee la Coastal Union lilifungwa na Jeery Santo.
Mechi inayofuata kwa Azam FC ni hapo Jumapili ndani ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam watakapoivaa Yanga.
RATIBA:
Novemba 3
Ruvu Shooting v Toto Africans [Mabatini, Pwani]
African Lyon v Mgambo JKT [Azam Complex, Dar es Salaam]
Kagera Sugar v Tanzania Prisons  [Kaitaba, Kagera]
Novemba 4
Azam v Yanga [National Stadium, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Simba [Jamhuri, Morogoro]
Azam v JKT Oljoro [Azam Complex, Dar es Salaam]
++++++++++++++++++++++++++

 PICHA MBALI MBALI KATIKA MECHI YA AZAM NA WAGOSI WA KAYA HAPO JANA

Samir Hajji Nuhu na Khamis Mcha 'Vialli' wakimpongeza Gaudence Mwaikimba (katikati) kufunga bao la kwanza katika mchezo wa  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam dhidi ya Coastal Union ya Tanga. Azam ilishinda mabao 4-1.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen akimuelekeza jambo kuhusu mechi hiyo Kocha wa timu za vijana, Jacob Michelsen kulia 

Kim na Jacob wakifuatilia mechi

Meneja wa Taifa Stars, Leopold Tasso Mukebezi kushoto akiwa na Ofisa wa TFF, Saad Kawemba

Kocha wa timu za vijana wa Azam, Vivek Nagul akinukuu mambo muhimu kuhusu mchezo huo, na baada ya hapo anakutana na Kocha Mkuu, Stewart kumpa ripoti ili mapungufu yafanyiwe kazi

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Coastal kulia

Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani Madega alikuwepo Chamazi leo

Makocha wa Yanga, Ernie Brandts kulia na Msaidizi wake, Freddy Felix Minziro walikuwepo kuifanyia ushushushu Azam Chamazi leo

Bado Yanga; Gaudence akishangilia bao lake, ambalo ni tamu kwa kweli

Hajji Nuhu na Gau Mwaikimba

Gau baada hya kufunga

Kama yupo mtu leo alikuwa anatia huruma, basi ni M kurugenzi wa Ufundi wa Coastal, Nassor Bin Slum...hapa anatuliza mawazo kwa sigara yake

Bosi leo alikuwa anatia huruma

Kama vile amtukane TANO JUMA  baada ya kumshitukia anampiga picha...lakini busara ikamzuia

Samir Hajji Nuhu anaambaa kulia

Kipre Balou anamtoka Othman Tamim

Kipre Tcheche anamtoka Juma Jabu

Daniel Lyanga kulia na Said Mourad kushoto

Lyanga na Mourad

Balou na Othman

Tcheche na Jabu kulia

Mwadini Ali akiwa amedaka moja ya michomo iliyoelekezwa langoni mwake leo

Cheki pande la Salum Abubakr linavyopasua msitu kuelekea kwa Mwaikimba (hayupo pichani)

Stewart kazini

Mwaikimba katikati ya msitu wa mabeki wa Coastal        

 Gor Mahia yatangaza jihad

Hiki ni kikosi cha timu ya Footprints inayoshiriki Ligi ya Kikapu ya Nairobi. Chipukizi hawa wameonyesha mchezo wa kuvutia msimu huu. Picha na John Kimwere

KOCHA wa Gor Mahia, Zdravko Logarusic, ambaye sasa vijana wake wameishika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Kenya, amesema wameshainusa harufu ya ubingwa hivyo hakuna kulala tena, bali ni mwendo wa dozi tu katika mechi nne zilizosalia.

Jumatano usiku wana K'Ogalo walitwaa nafasi hiyo hivyo kuishusha AFC Leopards kwa nafasi moja ilipoilaza Rangers mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Nyayo.

Kwa kufanya hivyo imekuwa kama mchezo wa vigogo hivyo kubadilisha nafasi hiyo iliyo nyuma ya vinara, Tusker FC.

Lakini Logarusic alisema: "Hakuna kurudi nyuma tena, ni lazima tuhakikishe tunazishinda Karuturi Sports, Tusker, Muhoroni Youth na Thika United ili kutimiza ndoto zetu za ubingwa."

Gor ina kazi kubwa kwani Leopards nayo inaonekana bado kuwa na kiu ya ubingwa huku Tusker iliyo kileleni kwa pointi 51 nayo ikiwa macho mbele. Gor kwa sasa ina pointi 49, moja mbele ya Leopards.

"Tumeshainusa harufu ya ubingwa, huu sasa ni wakati wa kazi nzito. Ni lazima tujitume kwa nguvu zetu zote ili kufanikisha azma, upinzani ni mkali lakini ninaamini tuna uwezo," alisema kocha huyo.

Kwa sasa Logarusic ana wiki mbili za kukiimarisha zaidi kikosi chake kwani ligi hiyo imesimama kupisha mechi za Kombe la FKF 'President Cup' na maandalizi ya timu ya taifa, Harambee Stars, inayojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi Afrika Kusini.

WENGER: “Hatumuongelei RVP, hamna kisasi! Nataka Mashabiki wamuheshimu!”


>>OLD TRAFFORD Jumamosi: Man United v Arsenal!
>>MECHI ya kwanza Robin van Persie kukutana na Ze Ganaz tangu ahame!!
>>WENGER aungama: “RVP ni Denja!!”
ARSENE_WENGER-13Arsene Wenger amepoza maneno ya Mashabiki wa Arsenal kutaka kisasi kwa Robin van Persie kwa RVP_in_RED2kuihama Timu hiyo na kwenda Manchester United wakati Timu hizo zitakapokutana Jumamosi Uwanjani Old Trafford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na hiyo ikiwa mara ya kwanza kwa Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal kukutana na Timu yake ya zamani tangu ahame.
Wenger amewataka Mashabiki wa Arsenal watakaokuwepo Old Trafford kumwonyeshea heshima Robin van Persie na si kumkashifu na kumtukana.
Wenger alitamka: “Kwetu, muhimu ni matokeo na uchezaji wetu. Hatumzunguzii kabisa Van Persie. Natumaini Mashabiki watamuheshimu kwani kachezea kwetu Miaka minane na alifanya vizuri sana!”
Alihoji: “Tunapiga vita Ubaguzi, Wiki iliyopita ilikuwa hivyo na kwa nini isiwe sasa?”
Akiichezea Arsenal, Robin van Persie, mwenye Miaka 29, aliifungia Arsenal jumla ya Mabao 132, 37 yakiwa Msimu uliopita na kuwawezesha kushika nafasi ya 3 kwenye Ligi.
Wenger amesema: “Daima unataka uongoze Watu vizuri wawe na maisha mazuri! Wakifanikiwa unaridhika, sidhani kwake nilifanya vibaya!”
Hadi sasa, kwa Kipindi kifupi, Van Persie ameifungia Man United Bao 7 kwenye Ligi na yeye na Demba Ba wa Newcastle ndio wanaongoza kwenye Ufungaji.
Hilo halikumshangaza Wenger ambae ametamka: “Sishangazwi na yeye kufanya vizuri. Man United ina Wachezaji wazuri sana, na Robin ni mjanja kwenye boksi, mwenye kasi na kujua nafasi huashangaza! Wapo Wachezaji wazuri na Robin atanufaika tu. Robin ni Straika hatari sana!”


LIGI ULAYA: Juve kuivaa Inter, wawania kutofungwa Mechi 50!


EL_SHAARAWY-AC_MILAN>>BUNDESLIGA: Baada kichapo, vinara Bayern wataka faraja!
>>LA LIGA: Barca na Atletico zafukuzana, Real yajivuta!!
ZIFUATAZO ni Taarifa fupi kuhusu Ratiba na hali ya Ligi za Serie A, Bundesliga na La Liga:
SERIE A: Juve yawania kutofungwa Mechi ya 50 ikicheza na Inter Jumamosi!
RATIBA:
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
[SAA za BONGO]
Alhamisi Novemba 1
Genoa v Fiorentina [Comunale Luigi Ferraris]
Jumamosi Novemba 3
2000 AC Milan v Chievo Verona [Stadio Giuseppe Meazza]
2245 Juventus v Inter Milan [Juventus Stadium]
Jumapili Novemba 4
US Pescara v Parma [Adriatico]
Bologna v Udinese [Stadio Renato Della`Ara]
Catania v Lazio [Stadio Angelo Massimino]
Fiorentina v Cagliari [Stadio Artemio Franchi]
Napoli v Torino [Stadio San Paolo]
Sampdoria v Atalanta [Comunale Luigi Ferraris]
Siena v Genoa [Artemio Franchi]
AS Roma v Palermo [Stadio Olimpico]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Juventus wanaweza kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika Mechi 50 za Ligi ya Serie A Jumamosi watakapocheza na Inter Milan ambao wako nafasi ya pili nyuma ya Juventus kwa Pointi 4.
Baada ya Mechi 10, Juventus wana Pointi 28 kwa kushinda Mechi zote kasoro sare katika Mechi moja tu lakini Inter Milan wanakuja na moto baada ya kushinda Mechi zao 9 zilizopita, za Ligi na Mashindano mengine, na hilo linaifanya Mechi hiyo kuwa ni tamu.
Juventus, ambao ndio Mabingwa watetezi, walitwaa Taji Msimu uliopita bila kufungwa hata Mechi moja na mara ya mwisho kufungwa kwenye Ligi ilikuwa ni katika Msimu wa 2010/11 walipofungwa na Parma Mechi moja kabla Ligi kwisha.
Rekodi ya kutofungwa katika Mechi nyingi inashikiliwa na AC Milan waliyoiweka katika Miaka ya 1990 kwa kutofungwa Mechi 58.
BUNDESLIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Ijumaa Novemba 2
Eintracht Frankfurt v SpVgg Greuther Fürth [Commerzbank-Arena]
Jumamosi Novemba 3
Borussia Dortmund v VfB Stuttgart [Signal-Iduna-Park]
Borussia Monchengladbach v SC Freiburg [Borussia-Park]
Hannover 96 v FC Augsburg [AWD-Arena]
Nurnberg v  VfL Wolfsburg [EasyCredit-Stadion]
TSG Hoffenheim v Schalke 04 [Rhein-Neckar-Arena]
Hamburg SV v Bayern Munich [HSH Nordbank Arena]
Jumapili Novemba 4
Bayer Leverkusen v Fortuna Düsseldorf [BayArena]
Werder Bremen v Mainz [Weserstadion]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Vinara wa Bundesliga Bayern Munich Jumamosi wanatinga kwenye Dabi watakapocheza ugenini na Hamburg kwenye Mechi ya Ligi ya Bundesliga lakini ndio kwanza wanatoka kwenye kipigo chao cha kwanza cha Ligi hiyo walipofungwa Wiki iliyopita 2-1 na Bayer Leverkusen.
Hata hivyo, Bayern, Jumatano, waliichapa Kaiserslautern bao 4-0 katika Mechi ya kugombea German Cup.
Bayern wapo kileleni wakiwa na Pointi 24 wako Pointi 4 mbele ya Schalke na Hamburg wapo nafasi ya 7 wakiwa na Poniti 13.
Schalke watakuwa ugenini kucheza na Timu ya chini Hoffenheim.
Mabingwa watetezi Borussia Dortmund, ambao wapo nafasi ya 4, watacheza Jumamosi na Stuttgart.
LA LIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Jumamosi Novemba 3
Málaga v Rayo Vallecano [Estadio La Rosaleda]
2000 Barcelona v Celta Vigo [Estadio Camp Nou]
2200 Real Madrid v Real Zaragoza [Estadio Santiago Bernabéu]
Jumapili Novemba 4
Deportivo La Coruña v Mallorca [Estadio Riazor]
Granada v Athletic Bilbao [Estadio Los Cármenes]
Osasuna v Valladolid [Estadio El Sadar]
Real Sociedad v Espanyol [Estadio Anoeta]
Sevilla FC v Levante [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan]
Valencia v Atlético Madrid [Estadio Mestalla]
Jumatatu Novemba 5
Getafe v Real Betis [Coliseum Alfonso Perez]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Baada ya kushinda kwenye Mechi zao za Copa del Rey katikati ya Wiki vinara Barcelona, Timu ya pili Atletico Madrid na Mabingwa watetezi Real Madrid wote wapo dimbani Wikiendi hii kucheza Mechi za La Liga.
Barcelona ambao waliwafunga  Alaves 3-0 kwenye Mechi ya Copa del Rey na kuwapumzisha Mastaa wao, Kipa Victor Valdes, Xavi Hernandez, Lionel Messi na Pedro Rodriguez, wanatarajiwa kuwarudisha wote hao watakapocheza na Celta Vigo Uwanjani Nou Camp.
Atletico Madrid, ambao nao waliipiga Jaen 3-0 kwenye Copa del Rey, wataenda ugenini kucheza na Valencia.
Nao Mabingwa Real Madrid, ambao pia walishinda kwenye Copa del Rey kwa kuichapa Alcoyano bao 4-1, watakuwa nyumbani Estadio Santiago Bernabeu kucheza na Real Zaragoza huku wakijijua wako Pointi 8 nyuma ya Barca na ni lazima wapate matokeo mazuri.
 

BPL: Wikiendi kuanza mapema kwa moto wa Man United v Arsenal!


BPL_LOGO>>REFA CLATTENBURG hakupangiwa Mechi Wikiendi hii kupisha uchunguzi wa malalamiko ya Chelsea!
Ligi Kuu England, BPL [Barclays Premier League], inaingia kwenye Raundi yake ya 10, isipokuwa kwa Sunderland na Reading ambazo zina kiporo cha Mechi kati yao, na baada ya Wikiendi iliyopita vinara Chelsea kunyukwa bao 3-2 wakiwa kwao Stamford Bridge na Manchester United, lile pengo kati ya Chelsea na Timu za nyuma yake, Man United na Mabingwa Man City, limebaki Pointi 1 tu.
Mbali ya Man United ambao wako nyumbani kupambana na Arsenal katika Mechi ya kwanza kabisa hapo Jumamosi, Chelsea na Man City zote zipo ugenini kwa Chelsea kucheza na Swansea City na Man City kukipiga na West Ham huko Upton Park, Jijini London.
Kufuatia Chelsea kuwasilisha malalamiko kwa FA, Chama cha Soka England, kuhusu Refa Mark Clattenburg kutumia lugha isiyofaa katika Mechi Chelsea waliyofungwa 3-2 na Manchester United Jumapili iliyopita dhidi ya Wachezaji wake John Mikel Obi na Juan Mata na pia kuwepo kwa uchunguzi wa Polisi baada ya Kikundi cha Wanasheria Weusi kulalamika kuhusu tukio hilo, Refa huyo ameondolewa kuchezesha Mechi za Wikiendi hii.
ZIFUATAZO NI RATIBA, MSIMAMO, MAREFA waliopangwa Mechi zote za Wikiendi na WAFUNGAJI BORA:
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 3, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Manchester United v Arsenal
[SAA 12 Jioni]
Fulham v Everton
Norwich City v Stoke City
Sunderland v Aston Villa
Swansea City v Chelsea
Tottenham Hotspur v Wigan Athletic
[SAA 2 na Nusu Usiku]
West Ham United v Manchester City
Jumapili, Novemba 4, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Queens Park Rangers v Reading
[SAA 1 Usiku]
Liverpool v Newcastle United
Jumatatu, Novemba 5, 2012
[SAA 5 Usiku]
West Bromwich Albion v Southampton
MAREFA wa MECHI za WIKIENDI:
Jumamosi Novemba 3
Manchester United v Arsenal
Refa: M Dean
Wasaidizi: S Ledger, A Garratt
Refa wa Akiba: P Dowd
Fulham v Everton
Refa: N Swarbrick
Wasaidizi: D Bryan, M Wilkes
Refa wa Akiba: M Oliver
Norwich City v Stoke City
Refa: A Marriner
Wasaidizi: G Beswick, A Holmes
Refa wa Akiba: P Tierney
Sunderland v Aston Villa
Refa: M Jones
Wasaidizi: D C Richards, J Brooks
Refa wa Akiba: C Foy
Swansea City v Chelsea
Refa: K Friend
Wasaidizi: C Breakspear, M Scholes
Refa wa Akiba: J Moss
Tottenham Hotspur v Wigan Athletic
Refa: M Atkinson
Wasaidizi: S Child, M McDonough
Refa wa Akiba: C Pawson
West Ham United v Manchester City
Refa: H Webb
Wasaidizi: D Cann, P Bankes
Refa wa Akiba: L Mason
Jumapili Novemba 4
Queens Park Rangers v Reading
Refa: M Oliver
Wasaidizi: S Long, D England
Refa wa Akiba: M Atkinson
Liverpool v Newcastle United
Refa: A Taylor
Wasaidizi: S Burt, A Halliday
Refa wa Akiba: M Jones
Jumatatu Novemba 5
West Bromwich Albion v Southampton
Refa: M Halsey
Wasaidizi: R Ganfield, J Flynn
Refa wa Akiba: M Dean
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 9 isipokuwa inapotajwa]
1 Chelsea Pointi 22
2 Man Utd  21
3 Man City  21
4 Tottenham 17
5 Everton 16
6 Arsenal 15
7 Fulham 14
8 West Brom 14
9 West Ham 14
10 Newcastle 13
11 Swansea 11
12 Liverpool 10
13 Stoke  9
14 Sunderland Mechi 8 Pointi 9
15 Wigan 8
16 Norwich 7
17 Aston Villa 6
18 Reading Mechi 8 Pointi 4
19 Southampton 4
20 QPR 3
WAFUNGAJI BORA:
Demba Ba [Newcastle] Mabao 7
Van Persie [Man United] 7
Michu  [Swansea] 6
Suarez [Liverpool] 6
Defoe [Tottenham] 5
Dzeko [Man City]5
Fletcher [Sunderland] 5
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi, Novemba 10, 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Fulham
Everton v Sunderland
Reading v Norwich City
Southampton v Swansea City
Stoke City v Queens Park Rangers
Wigan Athletic v West Bromwich Albion
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Manchester United
Jumapili, Novemba 11, 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Manchester City v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Newcastle United v West Ham United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Liverpool
 

MVUA ya MAGOLI Jumamosi Man United v Arsenal Old Trafford??

>>ARSENAL haijashinda Old Trafford katika Mechi 8 za mwisho!!
>>RVP kuivaa Timu yake ya zamani kwa MARA ya KWANZA!!
RVP_in_RED>>PATA DONDOO na REKODI za Mechi Man United v Arsenal!
Jumamosi Novemba 3, ndani ya Uwanja wa Old Trafford, Manchester United itaikaribisha Arsenal katika moja ya Mechi za Ligi Kuu England, BPL, ambayo inangojewa kwa hamu kubwa kwani inazikutanisha Timu ambazo, kati yao, zimefunga na kufungwa jumla ya Magoli 41 katika Mechi 8 kuanzia Oktoba 20 na pia mvuto upo kumuona Nahodha wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie, akiivaa Klabu yake ya zamani kwa mara ya kwanza tangu ahamie Man United mwanzoni mwa Msimu huu.
Bila shaka, Arsenal watakuwa na wasiwasi kumvaa Straika ambae wakiwa nae Msimu uliopita aliifungia jumla ya Magoli 37 na tangu atue Man United mtambo wake wa magoli umeendelea mtindo mmoja.
Juzi Jumanne, Arsenal walitoka nyuma kwa Bao 4-0 walipocheza kwenye Kombe la Ligi na kuifunga Reading 7-5 katika Dakika 120 za Mchezo huku Theo Walcott akipiga hetitriki.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 9]
1 Chelsea Pointi 22
2 Man United 21 [Tofauti ya Magoli 11]
3 Man City 21 [Tofauti ya Magoli 9]
4 Tottenham 17
5 Everton 16
6 Arsenal 15
7 Fulham 14
8 WBA 14
9 West Ham 14
10 Newcastle 13
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRA+++++++++++++++++++++++WALCOTT_WILSHERE_OX
Msimu uliopita, Mwezi Agosti Mwaka jana Uwanjani Old Trafford, Arsenal walichabangwa bao 8-2 kwenye Mechi ya Ligi na Msimu huu Man United wamekuwa wakiendeleza wimbi lao la kufunga Mabao mengi kila Mechi baada ya Jumapili iliyopita kushusha kipigo cha kwanza kwenye Ligi kwa vinara wa Ligi Chelsea Uwanjani Stamford Bridge walipoifunga 3-2 lakini Siku 3 baadae, Jumatano, Chelsea walilipa kisasi kwa kuifunga Man United, iliyochezesha Kikosi cha Pili,  bao 5-4, kwenye Mechi ya Kombe la Ligi iliyochukua Dakika 120 baada ya kutoka 3-3 katika Dakika 90.
Katika Mechi 8 za mwisho kucheza Old Trafford, Arsenal hawajashinda hata moja baada ya kuchapwa na Man United katika Mechi 7 kati ya hizo na sare 1 tu.
Kimsimamo kwenye Ligi, Arsenal wapo nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 15 na Man United wapo nafasi ya pili, Pointi moja nyuma ya vinara Chelsea, na wana Pointi 21.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
USO kwa USO-Man United v Arsenal:
-WAMECHEZA JUMLA MECHI: 214
-Arsenal: Ushindi: 78
-Man United: Ushindi 90
-Sare: 46
NYUMBANI kwa Arsenal: Mechi 101
-Arsenal: Ushindi: 57
-Man United: Ushindi 27
-Sare: 17
NYUMBANI kwa Man United: Mechi 102
-Man United: Ushindi 60
-Arsenal: 17
-Sare: 25
MATOKEO Misimu ya hivi karibuni:
2011/12:
Januari 22-Arsenal 1 Man United 2 [BPL]
Agosti 28-Man United 8 Arsenal 2 [BPL]
2010/11:
Mei 1-Arsenal 1 Man United 0 [BPL]
Machi 12-Man United 2 Arsenal 0 [FA Cup]
Desemba 13-Man United 1 Arsenal 0 [BPL]
2009/10
Januari 31-Arsenal 1 Man United 3 [BPL]
Agosti 29-Man United 2 Arsenal 1 [BPL]
2008/9:
Mei 16-Man United 0 Arsenal 0 [BPL]
Mei 5-Arsenal 1 Man United 3 [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Aprili 29-Man United 1 Arsenal 0 [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Novemba 8-Arsenal 2 Man United 1 [BPL]
2007/8:
Aprili 13-Man United 2 Arsenal 1 [BPL]
Februari 16-Man United 4 Arsenal 0
Novemba 3-Arsenal 2 Man United 2
REKODI-Mabao Mengi:
-2011/12: Man United 8 Arsenal 2
-1946/47: Arsenal 6 Man United 2
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

 

AZAM YATUMA SALAMU YANGA, YAIPA COASTAL KIPIGO CHA MWANA UKOME

Khamis Mcha 'Vialli' na Gaudence Mwaikimba wakishangilia leo Chamazi
KOCHA Muingereza Stewart Hall amerejea na ‘bonge la zali’, baada ya leo kuiongoza timu hiyo kuichapa Coastal Union ya Tanga mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Stewart alitua jana usiku Dar es Salaam akitokea Kenya alipokuwa anaifundisha Sofapaka ya Ligi Kuu ya huko, baada ya kufukuzwa Azam Agosti mwaka huu na leo ameanza kazi, akirithi mikoba ya Mserbia, Boris Bunjak aliyefukuzwa Jumatatu.
Kwa ushindi huo, Azam imefikisha pointi 21, baada ya kucheza mechi 10 na sasa inarejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Simba na Yanga, zenye pointi 23 zote baada ya kucheza mechi 11, kila timu.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Simon Mbelwa, aliyesaidiwa na Abdallah Rashid wote wa Pwani na Michael Mkongwa wa Njombe, hadi mapumziko Azam tayari walikuwa wanaongoza kwa mabao 3-0.
Gaudence Mwaikimba aliifungia Azam bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 23 kabla ya Kipre Tcheche kufunga la pili dakika ya 36, baada ya kuipasua ngome ya Coastal na Khamis Mcha ‘Vialli’ akafunga la tatu dakika ya 44.
Coatsal walianza vizuri mechi hiyo na kusukuma mashambulizi langoni mwa Azam, lakini baada ya dakika 20, wakapoteza mwelekeo na kuanza kuwaruhusu wapinzani wao kuvuna mabao. 
Kipindi cha pil, Azam walirudi na moto wao, lakini kidogo Coastal walibadlika nao na kufanya mchezo uwe mgumu kidogo.
Hata hivyo, walikuwa ni Azam tena waliotikisa nyavu za Coastal, baada ya kiungo Othman Tamim kujifunga dakika ya 73 katika harakati za kuokoa.
Baada ya bao hilo, Coastal walizinduka na kuanza kushambulia kupitia pembeni, jambo ambalo liliwasaidia kupata bao la kufutia machozi lililofungwa ma kiungo Jerry Santo.
Kwa ujumla katika mchezo wa leo, Coastal walizidiwa katika safu ya kiungo ambako leo Stewart alipanga viungo wengi waliotekeleza majukumu yao vyema.
Baada ya mchezo huo, kocha wa Coastal, Hemed Morocco alisema kwamba walizidiwa uwezo na wapinzani wao na kwa ujumla vijana wake walicheza chini ya kiwango leo, hata hivyo anakwenda kufanyia kazi makosa ili timu irejeshe makali yake.
Stewart alisema anafurahi kukaribishwa na ushindi huo mnono na kwamba hizo ni dalili njema. Aliwapongeza vijana wake kwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake na akasema kwamba sasa anaelekeza nguvu zake katika mchezo ujao dhidi ya Yanga Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   
 
 
Azam FC; Mwadini Ally, Samir Hajji, Ibrahim Shikanda, Aggrey Morris, Said Mourad, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz, Salum Abubakar/Himid Mao, Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim, Kipre Tcheche na Khamis Mcha ‘Vialli’.
 
Coastal Union; Jackson Chove, Said Swedi, Juma Jabu, Mbwana Hamisi, Jamal Machelanga/Salim Gilla, Jerry Santo, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Razack Khalfan/Hamisi Shango, Daniel Lyanga, Atupele Green/Lameck Dayton na Othman Tamim

LEO TFF: UAMUZI KUHUSU RUFANI ZA CHAGUZI ZA WANACHAMA!!

>>IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI YA TFF:
TANZANIA FOOTBALL FEDERATION (TFF)
ELECTIONS COMMITTEE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UAMUZI KUHUSU RUFANI DHIDI YA KAMATI ZA UCHAGUZI ZA VYAMA VYA MPIRA WA MIGUU MKOA WA MWANZA (MZFA), MKOA WA GEITA (GEREFA) NA KUHUSU MICHAKATO YA UCHAGUZI YA VYAMA WANACHAMA WA TFF NA WANACHAMA WAO
OKTOBA 31, 2012
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 8(2), 10(6), 12(1) na 26(2) na (3) katika kikao chake kilichofanyika Oktoba 30, 2012 ilijadili rufani dhidi ya Kamati za Uchaguzi za MZFA na GEREFA na michakato ya uchaguzi ya vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Mwanza, Rukwa, Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake (TWFA), Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) na Chama cha Wanasoka Tanzania (SPUTANZA) na kutoa uamuzi kama ifuatavyo;
1.      Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA)
(a)    Rufani ya Ndg. Jackson Manji Songora: Kamati ilijadili rufani iliyowasilishwa na Ndg. Jackson Manji Songora dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya MZFA, iliyoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF kubatilisha uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya MZFA kumpitisha Ndg. Jumbe O. Magati kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa MZFA, kwamba Kamati ya Uchaguzi ya MZFA ilikosea:
(i)Kupokea Statement of Results ya Baraza la Mitihani Tanzania yenye jina la Fredrick J. Magati wakati jina la mgombea alilojaza kwenye fomu ya maombi ya uongozi ni Jumbe O. Magati.
(ii)Kumsaili Jumbe O. Magati kwa kuwa hakuwasilisha nakala halisi ya cheti cha elimu yake.
(iii)Kumpitisha Ndg. Jumbe O. Magati kugombea uongozi na kuwa Ndg. Jumbe O. Magati hana sifa zinazokidhi matakwa ya Katiba ya MZFA Ibara ya 29(2).
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilipitia maelezo ya Mrufani na ilijiridhisha kuwa rufani iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Songora haikutanguliwa na pingamizi mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya MZFA, hivyo ilikosa sifa ya kuwa rufani kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF. Hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba ya TFF Ibara ya 49(1); Katiba ya MZFA Ibara ya 47 na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 26(2), Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kwa kutumia mamlaka yake ya kikatiba na kanuni za uchaguzi, ilimuhoji Ndg. Magati kuhusu elimu yake na majina yaliyo kwenye Statement of Results na fomu yake ya maombi ya uongozi.
Baada ya kupitia vielelezo na maelezo yaliyowasilishwa mbele ya Kamati kuhusu majina ya Ndg. Jumbe O. Magati, Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilijiridhisha kuwa Jumbe O. Magati na Fredrick J. Magati ni mtu huyo huyo. Kamati ya Uchaguzi imetupa rufani ya Ndg. Patrick Manji Songora.
2.      Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA)
(a)    Rufani ya Ndg. Abdallah H. Hussein: Kamati ilijadili rufani iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Abdallah H. Hussein ikipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya GEREFA kuliondoa jina lake kugombea nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, kwa kigezo cha kutokuwa Mkazi wa Mkoa wa Geita. Kamati ilipitia vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake na Mrufani na ilijiridhisha kuwa vielelezo hivyo vinakidhi kuthibitisha kuwa mwombaji uongozi ni Mkazi wa Mkoa wa Geita. Kamati inakubaliana na maombi ya mrufani na inamrejesha Ndg. Abdallah H. Hussein kugombea nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.
(b)   Rufani ya Ndg. Aziz Mwamcholi: Kamati ilijadili rufani iliyowasilishwa mbele yake na Ndg. Aziz Mwamcholi ikipinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya GEREFA kuliondoa jina lake kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa GEREFA, kwa kigezo cha kushindwa kuwasilisha cheti cha elimu ya sekondari.  Kamati ilipitia maelezo ya Ndg. Mwamcholi na ya Kamati ya Uchaguzi ya GEREFA na ikajiridhisha kuwa Ndg. Mwamcholi hakukidhi matakwa ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hususan Ibara ya 10(5). Kamati imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya GEREFA wa kutompitisha Ndg. Mwamcholi kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa GEREFA. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetupa rufani hiyo.
(c)    Rufani ya Ndg. Kaliro Samson: Ndg. Samson aliwasilisha rufani kupinga uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya GEREFA kuliondoa jina lake kugombea nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa kigezo cha kutowasilisha cheti cha kuhitimu elimu ya kidato cha nne. Kamati ilipitia maelezo na vielelezo vya rufani ya Ndg. Samson nay a Mrufaniwa na kujiridhisha kuwa nakala ya cheti cha elimu ya kidato cha sita inakidhi matakwa ya Katiba ya GEREFA Ibara ya 29(2). Kamati inakubaliana na maombi ya mrufani na inamrejesha Ndg. Kaliro Samson kugombea nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.
3.      Mchakato wa Uchaguzi Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA)
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilijadili mchakato wa uchaguzi wa MZFA ikiwa ni pamoja na mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ukerewe (UDFA), baada ya uchaguzi wa awali wa UDFA kuwa umefutwa na Kamati ya Uchaguzi ya MZFA kutokana na Kamati ya Uchaguzi ya UDFA kutozingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
Baada ya maelezo ya kina ya Kamati ya Uchaguzi ya MZFA na vielelezo vilivyowasilishwa mbele ya Kamati kuhusu mwenendo wa uchaguzi wa UDFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilibaini kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa Kanuni na taratibu za uchaguzi uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya UDFA kwa kutozingatia kikamilifu maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya MZFA na hivyo kusababisha mkanganyiko katika mchakato wa Uchaguzi ambao kwa wakati mmoja ulikuwa na Kamati mbili za Uchaguzi kusimamia uchaguzi huo. Mikanganyiko inayojionyesha dhahiri na kusababisha nafasi zote sita zinazogombewa katika mchakato unaoendelea kuwa na mgombea mmoja mmoja tu katika kila nafasi, imeufanya mchakato wa uchaguzi wa UDFA kupoteza hadhi ya uchaguzi unaozingatia Kanuni za Uchaguzi na misingi ya demokrasia na uwazi kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Uchaguzi za TFF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa mamlaka yake ya kikatiba Ibara ya 49(1) ya Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya 10(6) na 26(2) na (3) imeamua:
(i)Kuzifuta Kamati zote za Uchaguzi za UDFA zilizoteuliwa na Kamati ya Utendaji ya   UDFA kabla ya baada ya mchakato wa uchaguzi wa sasa wa UDFA.
(ii) Kuufuta Uchaguzi wa UDFA uliokuwa ufanyike Novemba 5, 2012. Mchakato wa uchaguzi utaanza upya kwa tarehe zitakazopangwa na Kamati ya Uchaguzi ya MZFA baada ya kupata maelekezo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
(iii) Kuiagiza Kamati ya Uchaguzi ya MZFA katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ibara ya 6 ya Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF kutoiruhusu UDFA kushiriki Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa MZFA kwa kuwa UDFA imeshindwa kuzingatia matakwa ya Katiba kuhusu ukomo wa mamlaka ya Kamati ya Utendaji na kufanya uchaguzi kwa wakati muafaka unaozingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
4.      Mchakato wa Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake (TWFA)
Kwa kuzingatia changamoto za kuijenga TWFA ambayo bado ni change, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imekubali ombi la TWFA la kusogeza mbele tarehe ya uchaguzi kwa wiki mbili. Uchaguzi wa TWFA ngazi ya Taifa sasa utafanyika Novemba 18, 2012.
5.      Mchakato wa Uchaguzi wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT)
Uchaguzi wa viongozi wa FRAT utafanyika Novemba 17, 2012 kama ulivyopangwa.
6.      Mchakato wa Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA)
TFF imesimamisha kuanza kwa mchakato wa uchaguzi wa RUREFA kutokana na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya RUREFA kuendeleza malumbano kati yao kuhusu uhalali wa uteuzi wa Kamati mpya ya Uchaguzi ya RUREFA, uteuzi ambao ulifanywa na Kamati ya Utendaji ya RUREFA, Oktoba 18, 2012. Kwa kuwa hali hii imetokea tena baada ya Kamati ya Utendaji ya RUREFA kuwa imepewa fursa ya kikatiba kuteua Kamati ya Uchaguzi na ni mwendelezo wa mgawanyiko ndani ya Kamati ya Utendaji ya RUREFA unaoathiri mchakato wa uchaguzi wa chama hicho, Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatafakari hatua muafaka za kikatiba na kikanuni zitakazoondoa ukwamishaji wa mchakato wa Uchaguzi wa RUREFA unaosababishwa na Kamati ya Utendaji ya RUREFA. Uamuzi kuhusu mustakabali wa Uchaguzi wa RUREFA utatolewa baada ya kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF kitakachofanyika Novemba 6, 2012. 
7.      Mchakato wa Chama cha Wanasoka Tanzania (SPUTANZA) na Chama cha Makocha (TAFCA)
Uamuzi kuhusu mustakabali wa uchaguzi wa SPUTANZA na TAFCA utatolewa baada ya vyama hivyo kuwasilisha taarifa za kina kuhusu michakato ya chaguzi za wanachama wao katika ngazi ya mikoa, katika kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF kitakachofanyika Novemba 6, 2012.
Moses Kaluwa
Mjumbe- Kamati ya Uchaguzi TFF

WACHEZAJI YANGA WAPO BAGAMOYO, BRANDTS ANAIFANYIA USHUSHUSHU AZAM CHAMAZI

Brandts akiwa Uwanja wa Chamazi mida hii


YANGA SC leo imeingia kambini katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani kujiandaa na mchezo wake wa Jumapili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, Jumapili, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa kawaida, Yanga huweka kambi Bagamoyo katikati ya Ligi, inapokuwa inajiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC hivyo kwa kwenda huko kuweka kujiandaa na mchezo huo, maana yake wanaupa uzito sawa na pambano la watani.
Wakati vijana wa Yanga wakiwa Bagamoyo, Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mholanzi Ernie Brandts yupo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, akiwafanyia ‘ushushushu’ wapinzani wake hao wanaomenyana na Coastal Union ya Tanga mida hii, kipindi cha kwanza wakiwa wanaongoza 3-0.    
Brandts jana aliiongoza Yanga SC kuendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa Mgambo JKT ya Handeni, Tanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga sasa iwe na pointi sawa na mabingwa watetezi, Simba SC waliotoa sare ya 1-1 na Polisi mjini Morogoro leo, ingawa inazidiwa bao moja tu katika wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Didier Kavumbangu.
Cannavaro alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oscar Joshua dakika ya pili kutoka wingi ya kulia, wakati Kavumbangu alimalizia pasi ya Hamisi Kiiza dakika ya 39.
Pamoja na kutoka uwanjani wamelowa kipindi cha kwanza, lakini Mgambo JKT walicheza soka ya kuvutia na mara mbili walikaribia kufunga kupitia kwa Juma Mwinyimvua.
Yanga walicheza vema dakika 45 za kipindi cha kwanza, tofauti sana na mechi za awali ambazo wamekuwa ‘wakichezewa’ sana na wapinzani.
Ilishuhudiwa katika kipindi hicho, Yanga wakimiliki zaidi mpira na kupeana pasi za uhakika, ingawa mashambulizi yao mengi walipitisha pembeni, hasa upande wa kulia.
Hamisi Kiiza, Msuva na Kavumbangu walicheza kwa uelewano mkubwa pale mbele na kulitia misukosuko haswa lango la Mgambo. 
Kipindi cha pili, Yanga walirudi na moto wao tena na kuendelea kuwachachafya Mgambo.
Hata hivyo, iliwachukua Yanga dakika 34 kupata bao la tatu, mfungaji akiwa ni Jerry Tegete aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Kavumbangu.
Tegete alifunga bao hilo akiunganisha krosi maridadi ya beki wa kushoto, Oscar Joshua.
Pamoja na kufungwa, Mgambo waliendelea kusukuma mashambulizi langoni mwa Yanga, ingawa leo mabeki wa timu hiyo, inayofundishwa na Mholanzi, Ernie Brandts walicheza kwa uelewano mkubwa na kudhibiti hatari zote langoni mwao. 
Mgambo inayofundishwa na Mohamed Kampira, ilipata pigo dakika ya 85, baada ya beki wake wa kulia, Salum Mlima kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu mbaya Mbuyu Twite. 

YANGA WAFURIKA DRFA, SEIF MAGARI MWENYEKITI, ALLY MAYAY MAKAMU WAKE

seif magari akipokea fomu leo hii
MDAU maarufu wa soka nchini, Ahmed Seif Hemed ‘Magari’ amechukua fomu za kugombea Uenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) mchana wa leo katika ofisi za chama hicho, zilizopo makutano ya Mtaa wa Mafia na Bonde, kariakoo, Dar es Salaam.
Seif, ametimiza wajibu huo kufuatia ombi la wazee na wadau wa soka mkoani Dar es Salaam, kumtaka ajitokeze kuiokoa soka ya Jiji hilo, ambayo imebakiza umaarufu wa Simba na Yanga pekee.
Wadau wa soka Dar es Salaam tangu wiki iliyopita wamekuwa wakimbembeleza Seif kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo, wakiahidi kumuunga mkono mfanyabiashara huyo wa magari na fedha za kigeni kwa asilimia 100 ashinde nafasi hiyo.
Kwa kujitosa huko DRFA, Seif sasa atachuana na Salum Mkemi, Evans Aveva, Ayoub Nyenzi, Juma Jabir na Meba Ramadhan katika nafasi hiyo, ambao ndio pekee hadi sasa wamechukua fomu.
Wagombea wengine waliochukua fomu hadi leo Ally Mayay, nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Said Tuliy, Msanifu Kondo, Hamisi Ambari, ambao wanawania nafasi ya Ukatibu Mkuu, Shaffi Dauda na Muhisn Balhabou, Ujumbe wa Mkutano Mkuu, Shaaban Mohamed, Andrew Tupa, Siza Abdallah Chenje, Sunday Mwanahewa na Lameck Nyambaya Ujumbe wa kamati ya Utendaji na Philemon Ntahilaja, Mwakilishi wa Klabu.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Seif aliyesindikizwa na swahiba wake, Abdallah Bin Kleb, alisema kwamba ameamua kuitikia wito huo wa wazee na wadau wa soka Dar es Salaam kwa sababu ana nguvu, uwezo, upeo na dira ya kuendeleza soka ya Dar es Salaam.
“Naamini, kabisa nikifanikiwa kuwa Mwenyekiti mpya wa DRFA, nitaleta mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa ya soka katika Jiji la Dar es Salaam,”alisema Seif.
Seif amekuwa kwenye Kamati za Yanga tangu wakati wa uongozi wa Francis Mponjoli Kifukwe miaka saba iliyopita na pia amewahi kuwa mmiliki mshiriki wa klabu ya Moro United iliyokuwa Ligi Kuu.
Seif ameendelea kuwa ndani ya Kamati za Yanga katika zama za viongozi waliomfuatia Kifukwe katika klabu hiyo, Imani Madega, Lloyd Nchunga na sasa Yussuf Manji.
Kuna uwezekano mkubwa mpinzani mkuu wa Seif, akawa Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Evans Aveva ambaye naye pia ana uzoefu wa kutosha katika uongozi wa soka.
Aveva, aliyekuwa Meneja wa Hoteli ya Embassy na sasa mfanyabiashara mwenye maduka kibao ya simu, amekuwa kwenye Kamati mbalimbali za uongozi Simba tangu enzi za Yussuf Hazali, Mwenyekiti wa klabu hiyo na ameendelea pia hata katika zama za viongozi waliofuatia akina Juma Salum (sasa marehemu) na Hassan Daalal.
Aveva pia amewahi kuwa mmoja wa viongozi wa iliyokuwa Tanzania Stars, timu iliyokuwa ikiundwa na wachezaji wakongwe nchini, ambayo mwaka 1998 na 1999 ilicheza Kombe la Washindi Afrika.
Uchaguzi wa DRFA utafanyika Desemba 8, mwaka huu na fomu za kugombea nafasi mbalimbali zilianza kutolewa tangu Oktoba 29, wakati Novemba 4 hadi 8, Kamati ya Uchaguzi, chini ya Mwenyekiti wake, Juma Simba itapitia fomu za walioomba uongozi.
Novemba 9 hadi 13 utakuwa muda wa pingamizi kwa wagombea, ambazo zitajadiliwa Novemba 14 hadi 16, wakati Novemba 17 hadi 19 watatoa fursa ya kukata rufaa, ambazo zitasikilziwa Novemba 20 hadi 24 na baada ya hapo, Novemba 25 yatatangazwa majina ya wagombea waliopitishwa.
Uchaguzi wa DRFA utafanyika siku chache tu kabla ya uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwishoni mwa Desemba, mwaka huu.   

Seif Magari kulia akiwa na Abdallah Ahmad Bin Kleb na Ally Mayay

Seif akiipitia fomu yake

Ally Mayay kulia akipokea fomu yake

Ayoub Nyenzi akipokea fomu yake

Philemon Ntahilaja akipokea fomu





 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 


BRANDTS: WACHEZAJI YANGA SASA WANANIKOSHA

Brandts

KOCHA Mhoalanzi wa Yanga, Ernie Brandts amesema kwamba taratibu wachezaji wa klabu hiyo wanaanza kushika mafundisho yake na anaamini kama wataendelea hivyo, hadi kufika Januari timu hiyo itakuwa inacheza anavyotaka.
Akizungumza  jana mara baada ya mechi  , Brandts alisema kwamba wana Yanga bado wanahitaji kuwa na subira ili kumpa fursa ya kuijenga timu vyema.
“Si kazi ya wiki moja au mwezi mmoja, unahitajika muda ili kocha aweze kutengeneza timu ya ushindi na kucheza soka nzuri. Nahitaji muda kuwajua zaidi wachezaji na kujua namna ya kuwabadilisha, unaweza kuona taratibu timu inaanza kucheza soka ya kuvutia,”alisema.
Brandts aliiongoza Yanga SC kuendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuichapa Mgambo JKT ya Handeni, Tanga mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga sasa iwe na pointi sawa na mabingwa watetezi, Simba SC waliotoa sare ya 1-1 na Polisi mjini Morogoro leo, ingawa inazidiwa bao moja tu katika wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na mshambuliaji Didier Kavumbangu.
Cannavaro alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Oscar Joshua dakika ya pili kutoka wingi ya kulia, wakati Kavumbangu alimalizia pasi ya Hamisi Kiiza dakika ya 39.
Pamoja na kutoka uwanjani wamelowa kipindi cha kwanza, lakini Mgambo JKT walicheza soka ya kuvutia na mara mbili walikaribia kufunga kupitia kwa Juma Mwinyimvua.
Yanga walicheza vema dakika 45 za kipindi cha kwanza, tofauti sana na mechi za awali ambazo wamekuwa ‘wakichezewa’ sana na wapinzani.
Ilishuhudiwa katika kipindi hicho, Yanga wakimiliki zaidi mpira na kupeana pasi za uhakika, ingawa mashambulizi yao mengi walipitisha pembeni, hasa upande wa kulia.
Hamisi Kiiza, Msuva na Kavumbangu walicheza kwa uelewano mkubwa pale mbele na kulitia misukosuko haswa lango la Mgambo. 
Kipindi cha pili, Yanga walirudi na moto wao tena na kuendelea kuwachachafya Mgambo.
Hata hivyo, iliwachukua Yanga dakika 34 kupata bao la tatu, mfungaji akiwa ni Jerry Tegete aliyeingia dakika ya 68 kuchukua nafasi ya Kavumbangu.
Tegete alifunga bao hilo akiunganisha krosi maridadi ya beki wa kushoto, Oscar Joshua.
Pamoja na kufungwa, Mgambo waliendelea kusukuma mashambulizi langoni mwa Yanga, ingawa leo mabeki wa timu hiyo, inayofundishwa na Mholanzi, Ernie Brandts walicheza kwa uelewano mkubwa na kudhibiti hatari zote langoni mwao. 
Mgambo inayofundishwa na Mohamed Kampira, ilipata pigo dakika ya 85, baada ya beki wake wa kulia, Salum Mlima kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumchezea rafu mbaya Mbuyu Twite.
Baada ya mchezo huo, Brandts alisema dakika 10 za mwanzo timu yake ilikuwa inashindwa kumalizia vizuri mashambulizi yake, lakini baadaye ikatulia na hatimaye kupata ushindi huo, ambao ameufurahia kwani unamuweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Kwa upande wake, Kampira wa Mgambo alisema kufungwa ni sehemu ya mchezo, akawasifu Yanga kwa kutumia nafasi walizopata, huku akijutia nafasi walizopoteza wachezaji wake leo.
Kikosi cha Yanga leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Nsajigwa Shadrack/Kevin Yondan dk 46, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo/Nurdin Bakari dk 76, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete dk68, Hamisi Kiiza na Haruna Niyonzima.
Mgambo JKT; Godson Mmasa, Salum Mlima, Yassin Awadh, Salum Kipanga/Godfrey Komba dk80, Bakari Mtama, Ramadhani Malima, Chande Magoja, Mussa Ngunda, Issa Kandulu/Nassor Gumbo dk 60, Fully Maganga na Juma Mwinyimvua/Omar Matwiko dk76.
Katika mchezo wa utangulizi, timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yanga, imeifunga Mgambo JKT ya vijana pia 1-0, bao hilo pekee la Clever Charles dakika ya 65.
Katika mechi nyingine, Simba ilitoka sare ya 1-1 Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji wakitangulia kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa Mokili Rambo kabla ya Amri Kiemba kusawazisha dakika ya 57. 

STEWART AWASILI KUICHINJA COASTAL UNION CHAMAZI LEO


LEO NI LEO kwenye Uwanja wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ambako timu mbili zinazopigana vikumbo katika nafasi ya tatu, wenyeji Azam FC watamenyana na Coastal Union ya Tanga katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Hiyo ni moja kati ya mechi tamu za Ligi Kuu, zisizozihusisha Simba na Yanga, kwani ukiondoa wababe hao wa soka Tanzania, kama kuna timu nyingine inayoweza kufikiriwa japo kushika nafasi ya pili kwenye ligi hiyo, ni kati ya hizo, Azam na Coastal.
Azam imekuwa katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu kwa muda mrefu, kabla ya kushushwa hadi nafasi ya nne ndani ya siku mbili mwishoni mwa wiki na Coastal ndio ya tatu sasa, nyuma ya Yanga na Simba, zinazolinganana kwa pointi.
Coastal inayofundishwa na kocha mtaalamu, lakini ‘simpo tu’, Ahmed Morocco itamenyana na Azam leo ambayo itaongozwa na Kali Ongala, anayekaimu Ukocha Mkuu, kufuatia kufukuzwa kwa Mserbia, Boris Bunjak Jumatatu.
Baada ya kufukuzwa kwa Bunjak, Azam imekwishamrejesha kocha wake wa zamani, Muingereza Stewart Hall ambaye alitua jana usiku na leo atakuwapo Chamazi.
Bunjak ameondoka Azam baada ya kuiongoza timu katika mechi 16, akifungwa nne tu, zote dhidi ya Simba ikiwemo ya juzi ya Ligi Kuu, waliyofungwa 3-1 na kutoa sare tatu.
Bunjak mwenye leseni ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), alitua Azam, Agosti 7, mwaka huu akitokea FC Damac ya Saudia Arabia aliyoanza kuifundisha mwaka jana na kabla ya hapo alifundisha klabu kibao za kwao, zikiwemo FK Sloga Kraljevo, FK Javor Ivanjica, Crvena Zvezda Gnjilane, FK Radnicki Nis, FC Uralan Elista, FK Mladi Radnik, FK Crvena Zvezda Beograd, Al-Shaab, FK Hajduk Kula na Al-Nasr.
Awali, Bunjak aliyezaliwa Novemba 17, mwaka 1954 ( miaka 57), alicheza soka katika klabu za FK Sloga (Kraljevo), FK Vozdovac (Beograd), FK Radnicki (Kragujevac), FK Olimpia (Ljubljana), FK Sumadija (Arandjelovac), FK Sloga (Kraljevo), FK Borac (Cacak) na FK Sloga (Kraljevo).
Stewart alifukuzwa kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya Yanga.
Mserbia huyo anakuwa kocha wa tano kufukuzwa Azam, ndani ya miaka minne tangu ianze kucheza Ligi Kuu, 2008 baada ya Stewart, Mbrazil Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin, Mbrazil mwingine.
Lakini Stewart angalau aliacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada ya kuiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari, kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame mwezi uliopita, mambo ambayo bila shaka yamemfanya afikiriwe tena.
Stewart ana sifa ya kutokuwa mbinafsi na mwenye kuwaamini watu wa chini yake, kwa mfano namna ambavyo alikuwa akimpromoti Kali Ongala. Alimkuta Kali kama mchezaji, lakini kwa sababu ya umri kumtupa mkono, akashauriana naye awe Kocha Msaidizi na mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, akakubali.
Chini ya Stewart, Kali alikuwa akiachiwa timu aiongoze ili kumjengea kujiamini zaidi na mwezi uliopita aliachiwa timu kwenye Kombe la Urafiki, akaifikisha fainali, ambako ilifungwa na Simba kwa penalti kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90. 
Yote kwa tote, Chamazi leo kinachotarajiwa ni soka safi, ile ya burudani, isiyokuwa na presha kutokana na timu hizo kutokuwa na mashabiki wenye ugonjwa wa moyo kama wale wa Simba na Yanga.
Wakati huo huo: Stewart Hall alitua jana usiku mjini Dar es Salaam na kusema anataka Azam ishinde kila mechi kuanzia sasa baada ya kurejea kazini.
Hall amerejea katika klabu yake ya zamani ya Azam baada klabu aliyokuwa akiifundisha Sofapaka ya Kenya inayomilikiwa na tajiri kukiri kwamba haiwezi kupambana na kampuni kubwa ya Azam ambayo imeahidi kumpa mshahara mara mbili ya waliokuwa wakimlipa Wakenya hao.
Mashabiki waliokuwa uwanjani hapo wakipuliza mavuvuzela na kupiga ngoma, waliimba nyimbo mbalimbali ukiwamo uliosema "Hall amerejea, homa na presha za Simba na Yanga ziko juu."
Baada ya kutua kocha huyo, alivishwa mataji ya maua na viongozi wa Azam waliokuwapo kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya kumpokea



RATIBA TUSKER CHALLENGE YASOGEZWA MBELE.

Rogers Mulindwa, Cecafa Media Officer.
RATIBA ya michuano ya Kombe la Tusker kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA ambayo ilikuwa ipangwe Novemba 8 mwaka huu jijini Kampala imesogezwa mbele kwa siku nne zaidi. 

 Michuano hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi Novemba 24 mpaka Desemba 8 jijini Kampala katika Uwanja wa Taifa wa Mandela uliopo Namboole ratiba yake sasa itapangwa Novemba 12.

 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini Uganda-FUFA ambaye pia anafanya shughuli hiyo CECAFA, Rogers Mulindwa aliwaambia waandishi wa habari jijini Kampala mabadiliko ya tarehe hiyo bila kutoa maelezo zaidi ya sababu iliyopelekea kusogezwa mbele kwa uapngwaji huo wa ratiba. 

 Wakati michuano hiyo ikianza Uganda haitakuwa ikitetea taji hilo pekee lakini pia kushinda taji kwa rekodi ya mara 13 toka michuano hiyo ianzishwe.

MVUA ya MAGOLI Jumamosi Man United v Arsenal Old Trafford??

>>ARSENAL haijashinda Old Trafford katika Mechi 8 za mwisho!!
>>RVP kuivaa Timu yake ya zamani kwa MARA ya KWANZA!!
RVP_in_RED>>PATA DONDOO na REKODI za Mechi Man United v Arsenal!
Jumamosi Novemba 3, ndani ya Uwanja wa Old Trafford, Manchester United itaikaribisha Arsenal katika moja ya Mechi za Ligi Kuu England, BPL, ambayo inangojewa kwa hamu kubwa kwani inazikutanisha Timu ambazo, kati yao, zimefunga na kufungwa jumla ya Magoli 41 katika Mechi 8 kuanzia Oktoba 20 na pia mvuto upo kumuona Nahodha wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie, akiivaa Klabu yake ya zamani kwa mara ya kwanza tangu ahamie Man United mwanzoni mwa Msimu huu.
Bila shaka, Arsenal watakuwa na wasiwasi kumvaa Straika ambae wakiwa nae Msimu uliopita aliifungia jumla ya Magoli 37 na tangu atue Man United mtambo wake wa magoli umeendelea mtindo mmoja.
Juzi Jumanne, Arsenal walitoka nyuma kwa Bao 4-0 walipocheza kwenye Kombe la Ligi na kuifunga Reading 7-5 katika Dakika 120 za Mchezo huku Theo Walcott akipiga hetitriki.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 9]
1 Chelsea Pointi 22
2 Man United 21 [Tofauti ya Magoli 11]
3 Man City 21 [Tofauti ya Magoli 9]
4 Tottenham 17
5 Everton 16
6 Arsenal 15
7 Fulham 14
8 WBA 14
9 West Ham 14
10 Newcastle 13
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRA+++++++++++++++++++++++WALCOTT_WILSHERE_OX
Msimu uliopita, Mwezi Agosti Mwaka jana Uwanjani Old Trafford, Arsenal walichabangwa bao 8-2 kwenye Mechi ya Ligi na Msimu huu Man United wamekuwa wakiendeleza wimbi lao la kufunga Mabao mengi kila Mechi baada ya Jumapili iliyopita kushusha kipigo cha kwanza kwenye Ligi kwa vinara wa Ligi Chelsea Uwanjani Stamford Bridge walipoifunga 3-2 lakini Siku 3 baadae, Jumatano, Chelsea walilipa kisasi kwa kuifunga Man United, iliyochezesha Kikosi cha Pili,  bao 5-4, kwenye Mechi ya Kombe la Ligi iliyochukua Dakika 120 baada ya kutoka 3-3 katika Dakika 90.
Katika Mechi 8 za mwisho kucheza Old Trafford, Arsenal hawajashinda hata moja baada ya kuchapwa na Man United katika Mechi 7 kati ya hizo na sare 1 tu.
Kimsimamo kwenye Ligi, Arsenal wapo nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 15 na Man United wapo nafasi ya pili, Pointi moja nyuma ya vinara Chelsea, na wana Pointi 21.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
USO kwa USO-Man United v Arsenal:
-WAMECHEZA JUMLA MECHI: 214
-Arsenal: Ushindi: 78
-Man United: Ushindi 90
-Sare: 46
NYUMBANI kwa Arsenal: Mechi 101
-Arsenal: Ushindi: 57
-Man United: Ushindi 27
-Sare: 17
NYUMBANI kwa Man United: Mechi 102
-Man United: Ushindi 60
-Arsenal: 17
-Sare: 25
MATOKEO Misimu ya hivi karibuni:
2011/12:
Januari 22-Arsenal 1 Man United 2 [BPL]
Agosti 28-Man United 8 Arsenal 2 [BPL]
2010/11:
Mei 1-Arsenal 1 Man United 0 [BPL]
Machi 12-Man United 2 Arsenal 0 [FA Cup]
Desemba 13-Man United 1 Arsenal 0 [BPL]
2009/10
Januari 31-Arsenal 1 Man United 3 [BPL]
Agosti 29-Man United 2 Arsenal 1 [BPL]
2008/9:
Mei 16-Man United 0 Arsenal 0 [BPL]
Mei 5-Arsenal 1 Man United 3 [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Aprili 29-Man United 1 Arsenal 0 [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
Novemba 8-Arsenal 2 Man United 1 [BPL]
2007/8:
Aprili 13-Man United 2 Arsenal 1 [BPL]
Februari 16-Man United 4 Arsenal 0
Novemba 3-Arsenal 2 Man United 2
REKODI-Mabao Mengi:
-2011/12: Man United 8 Arsenal 2
-1946/47: Arsenal 6 Man United 2
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
 

MECHI KUPIGA VITA UMASIKINI: Ronaldo & Marafiki v Zidane & Marafiki!


MATCH_AGAINST_POVERTY>>DESEMBA 19, Gremio Arena, Porto Alegre, Brazil.MATCH_AGAINST_POVERTY2
Magwiji, ambao pia ni Mabalozi maalum wa UNDP, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Ronaldo na Zidane, wamealika Marafiki zao ili kucheza Mechi maalum ya Programu ya ‘Kupiga vita Umasikini’ hapo Desemba 19 itakayochezwa Gremio Arena huko Porto Alegre, Brazil.
Katika Mechi hii ya 10 ya ‘Kupiga vita Umasikini’, Zidane na Ronaldo, ambao waliwahi kucheza pamoja Real Madrid, kila mmoja atateua Kikosi chake.
Mechi za aina zimekuwa zikichezwa kila Mwaka kuanzia Mwaka 2003, na kubarikiwa na FIFA pamoja na UEFA, huchangisha Fedha ili kusaidia vita ya kuondoa Umaskini.
Kawaida Mechi hizi huchezwa katika Miji tofauti kwa kuikutanisha Timu ya Mabalozi wa UNDP dhidi ya Timu ya Mji inapochezwa lakini safari hii huko Gremio Arena, Porto Alegre, Brazil zitakuwa ni Timu ya Ronaldo, ambae pia atashirikisha wenzake wa Brazil, dhidi ya Timu ya Zidane.
Mwaka jana 2011, Mechi kama hii ilichezwa Mjini Hamburg, Ujerumani kati ya Hamburger HSV na Timu ya UNDP ambayo walikuwemo Ronaldo na Zidane.
Wachezaji wengine waliokuwemo kwenye Mechi hiyo ni  Didier Drogba (Ivory Coast), Dida (Brazil), Serginho (Brazil), Jens Lehmann (Germany), Lucas Radebe (South Africa), Fernando Hierro (Spain), Michel Salgado (Spain), Gheorghe Popescu (Romania), Gheorghe Hagi (Romania), Luís Figo (Portugal), Fernando Couto (Portugal), Christian Karembeu (France), Steve McManaman (England), Pavel Nedved (Czech Republic), Fabio Cannavaro (Italy), na Sami Al-Jaber (Saudi Arabia).
Mapato kwenye Mechi hizi huenda katika Programu za kupiga vita Umasikini katika Nchi zaidi ya 27 za Marekani ya Kusini, Africa na Asia.
Mapato makubwa ya Mechi ya Mwaka jana ya huko Hamburg yalienda kusaidia balaa la njaa lililoikumba Kaskazini Mashariki ya Afrika, hasa Somalia.
Akiongea Zidane alitamka: “Kila tunapokutana kwa Mechi hizi tunaweza kusaidia na kuleta tofauti kwa wenye shida!”
Nae Ronaldo amesema: “Ni muhimu kuonyesha umoja ili kusaidia wale wenye janga la Umasikini!”

Stirring the pot: Manchester United fans display a banner about Clattenburg, mocking the well-known slogan Chelsea fans attach to captain John Terry, who racially abused QPR defender Anton Ferdinand

BIN HAMMAM AGONGA UKUTA CAS.

MGOMBEA wa zamani wa urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Mohamed bin Hammam ameshindwa rufani yake ya kutengua adhabu ya siku 90 alizopewa wakati uchunguzi wa suala la rushwa dhidi yake ukiendelea.
 
 Bin Hammam ambaye ni raia wa Qatar alikata rufani kuhusu kufungiwa kwake huko akidai lilikuwa ni suala la kisiasa baada ya kujitokeza kugombea nafasi hiyo na Sepp Blatter Mei mwaka jana. 
 
 Bin Hammam ambaye pia amewahi kuwa rais wa Shirikisho la Soka barani Asia-AFC alishinda rufani yake ya kufungiwa maisha kwasababu ya kukutwa na hatia ya kuhonga wapiga kura Julai mwaka huu lakini FIFA ilianza uchunguzi mpya dhidi yake juu matumizi mabaya ya fedha wakati akiwa rais wa AFC.  
 
Baada ya kushindwa kuishawishi kamati ya rufani ya FIFA kutengua adhabu ya kufungiwa siku 90 Bin Hammam aliamua kupeleka shauri hilo katika Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo-CAS ambako nako maegonga mwamba. 
 
 Kamati ya maadili ya FIFA ikiongozwa na wakili wa zamani wa Marekani Michael Garcia wataendelea na uchunguzi juu matumizi mabaya ya fedha aliyofanya Bin Hammam kipindi hicho akiwa rais wa AFC.

DJOKOVIC ASHINDWA KUTAMBA PARIS MASTERS.

MCHEZA tenisi nyota kutoka Serbia, Novak Djokovic ameshindwa kutamba katika michuano ya Paris Masters na kujikuta akitolewa na Sam Querrey wa Marekani katika mzunguko wa pili.  

Djokovic ambaye ana uhakika wa kumaliza mwaka akiwa katika nafasi ya kwanza ya orodha za wachezaji bora wa mchezo huo dunia alianza vyema baada ya kushinda seti ya kwanza bila kupoteza alama lakini alijikuta akishindwa kuendelea kufanya vizuri katika seti zingine na kufungwa kwa 0-6 7-6 6-4.

 Djokovic anayeshika namba mbili ambaye anatachukua nafasi ya kukaa namba moja ambayo inashikiliwa na Roger Federer pamoja na kupoteza mchezo huo ka Querrey alitinga uwanjani jijini Paris akiwa amevaa kinyago cha Vader Mask kuazimisha sherehe za Halloween.

 Katika michezo mingine ya iliyochezwa jana David Ferrer ambaye ndiye mchezaji pekee aliyekuwepo katika orodha za juu, Juan Monaco na Janko Tipsarevic walishinda michezo yao na kuinga mzunguko wa tatu wa michuano hiyo ya mwisho kwa mwaka huu.