Tuesday, February 5, 2013

SKANDALI UPANGAJI MATOKEO: LIVERPOOL YAKANUSHA KUFUATWA NA EUROPOL!!

PAKA_WA_ANFIELD
>>MECHI LIVERPOOL v DEBRECEN SEP 16, 2009 MIONGONI MWA MECHI 680 ZINAZOSHUKIWA KUPANGWA!!
KLABU ya Liverpool imesema wao hawajawahi kuongea na EUROPOL, Polisi wa Kimataifa Ulaya, kuhusiana na uchunguzi wao wa Mechi 680 zenye mashaka ya Matokeo yake kupangwa ingawa jana Mechi yao na Debrecen ilitajwa kuwa ni miongoni mwa Mechi tata katika Skandali kubwa ambalo limeitikisa Ulaya huku FA, UEFA na FIFA zote zikidai hawakuwa na habari yeyote kuhusu Uchunguzi wa EUROPOL.
++++++++++++++++++++++++
EUROPOL=UCHUNGUZI WAO:
-Ulianza Miezi 18 iliyopita:
Ulianzia Germany, Finland na Hungary na kusambaa Nchini Slovenia na Austria.
-Walichunguza Mechi 680 katika Nchi 30:
Barua Pepe 13,000 zilichunguzwa.
-Watuhumiwa 425 walitambuliwa:
Watu 50 wamekamatwa.
-Hati za Upekuzi 80 zilitolewa:
Katika kusaka ushahidi, Hati za Upekuzi 80 zilitolewa.
++++++++++++++++++++++++
Katika Mechi hiyo ya Liverpool na Debrecen ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa Tarehe 16 Septemba 2009 na Liverpool kushinda kwa Bao 1-0 Mfungaji akiwa Dirk Kuyt, inadaiwa kuna Kundi la Wahalifu wa Mashariki ya Mbali huko Asia walimuhonga Kipa wa Debrecen, Vukasin Poleksic, aachie Bao 3 ili wazoe Mihela kwenye Kamari.
Lakini Kipa huyo wa Klabu hiyo ya Hungary alikuja kunaswa baadae kwa kuhusishwa na kupanga Matokeo katika Mechi kati ya Debrecen na Fiorentina ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambao wote walikuwa Kundi moja na Liverpool Mwaka huo 2009 na Kipa huyo akafungiwa Miaka Miwili kwa Kosa hilo.
EUROPOL wamekuwa wakiendesha uchunguzi wao kwa Miezi 18 na Mechi pekee kwa Klabu ya England kuchunguzwa ni hiyo ya Liverpool na pia zipo Mechi za Kombe la Dunia, Mechi za Mchujo Ulaya na baadhi ya Ligi za Ulaya.
Inadaiwa Wapangaji wa Matokeo Mechi ni Wahalifu kutoka Asia ambao wanawarubuni Wachezaji na Marefa kupoteza Mechi ili wao wanufaike kwa Uchezaji Kamari.

DIWANI WA WILAYA YA IGUNGA MJINI AMSIFIA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA UVCCM MKOA WA TABORA SEIF GULAMALI KUANZISHA KOMBE HILI


Photo: >>"NATANGULIZA SHUKRANI ZA DHATI KWA WADAU WALIONICHANGIA KUFANIKISHA KOMBE LA LIGI YA VIJANA KAWE CUP TAREHE 27/1/2013 VIWANJA TANGANYIKA PACKERZ TIMU ZILIZOSHIRIKI 16 ZILIZOTINGA FAINALI 2 COCOZ FC VS NYARA FC,PAMOJAH NA ZAWADI KWA MFUNGAJI BORA-KAWE,MCHEZAJI BORA WA MWAKA-KAWE,BEKI BORA WA MWAKA-KAWE,KIPA BORA WA MWAKA-KAWE..MUNGU AWABARIKI WAFUATAO KWANZA KATIBU MKUU WA UVCCM TAIFA NDG.MARTINE SHIGELA KWA KUJITOLEA FEDHA TASLIMU LAKI 8 KWA MSHINDI WA KWANZA ATAYEPATA ZAWADI YA NG'OMBE NA KIKOMBE WA PILI MBUZI NA JEZI SHUKRANI SANA SHIGELA VIJANA WA KATA YA KAWE WANAKUSHUKURU SANA,PIA WADAU WALIONICHANGIA KWA UKARIBU ZAIDI ZAWADI ZINGINE MH.MAHADH J.MAHADH-NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE,MH.PHARES MAGESSA-MNEC,MH.RICHARD KASESELA,MH.DEO NDEJEMBI-MNEC,MH.FENELLA MUKANGARA-WAZIRI WA MICHEZO,MH.NAMELOK SOKOINE,MH.UMMY MWALIMU-NAIBU WAZIRI WA JINSIA NA WATOTO>>MUNGU AWAZIDISHIE SINA CHA KUWALIPA ZAIDI YA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU"UMOJA NI USHINDI-VIJANA NA MAENDELEO"TWENDE NA MWAKIBINGA
Kombe la GULAMALI CUP wilayani Igunga linaendelea kutimua vumbi kwa  timu mbali mbali kuoneshana umwamba wa kutafuta bingwa wa wilaya hiyo itakayofikia tamati mwezi wa tatu mwaka huu wa 2013 katika uwanja wa wilaya ya Igunga.
Photo: Tukiwa ktk uwekaji wa jiwe la msingi Daraja la Mto Mbutu wilayani Igunga

Akizungumza na TANOJUMAINSPORTS diwani wa Chama Cha Maendeleo CHADEMA wilayani humo ambaye hakutaka kuonesha itikadi ya vyama amesema ligi ndani ya wilaya ya igunga inaendelea vizuri na inatarajia kuendelea mpaka tarehe kumi ya mwezi w atatu mwaka huu ambapo bingwa atazawadiwa kitita cha shilingi millioni moja na mshindi wa pili atapatiwa ngombe mmoja na mshindi wa tatu atapatiwa jezi pair moja .

MABINGWA W AULAYA CHELSEA WAKUMBWA NA MAJERUHI SASA KUZIKOSA MECHI ZA KESHO ZA NCHI ZAO ZA FIFA DATE ,,,BA AVUNJIKA PUA,CECH AVUNJIKA KIDOLE CHA MKONO NA DAVID LUIZ MISULI

>>NAE LUIZ YUPO KIKOSI CHA BRAZIL, HATIHATI KUCHEZA!!
CHELSEA_ULAYA_2012MABINGWA wa ULAYA, Chelsea, wamekumbwa na balaa ya Wachezaji wao Nyota na wa Kimataifa kuzikosa Mechi za Nchi zao za Jumatano Februari 6 na pia wataikosa Mechi ya Klabu yao ya Ligi Kuu England hapo Jumamosi dhidi ya Wigan Uwanjani Stamford Bridge na hao ni Kipa Petrc Cech, alievunjika Kidole mkononi, Demba Ba, alievunjika Pua na David Luiz, ambae ana matatizo ya Musuli za Mguu.
Demba Ba amelazimika kujitoa kwenye Kikosi cha Nchi yake Senegal baada ya kuvunjwa Pua na Buti ya Beki wa Newcastle Fabricio Coloccini Jumamosi iliyopita Chelsea ilipotwangwa 3-2 kwenye Mechi ya Ligi na Kipa Petr Cech alilazimika kujitoa kwenye Kikosi cha Czech Republic ambao wanacheza na Uturuki baada ya kuwa na maumivu ya Kidole kidogo cha Mkononi na uchunguzi kuthibitisha kimevunjika.
Lakini, huko Kambi ya Brazil, Kocha Luiz Felipe Scolari, amesema hatamchezesha Beki David Luiz ikiwa hataonekana fiti kutokana na maumivu ya Musuli za Mguu wake.
Luiz aliumia kwenye Dakika za mwisho za Mechi ya CAPITAL ONE CUP walipocheza na Swansea City Januari 23.
Kwenye Mechi hiyo na Wigan, Chelsea watamkaribisha tena Winga wao Eden Hazard ambae alikuwa Kifungoni kwa Mechi 3 alichopata baada ya kuchapwa Kadi Nyekundu kwa kumpiga teke Kijana muokota Mipira wakati wa Mechi ya Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP kati ya Swansea City na Chelsea iliyochezwa Uwanja wa Liberty.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Februari 9
[Saa 9 Dak 45 Mchana]
Tottenham Hotspur v Newcastle United
[Saa 12 Jioni]
Chelsea v Wigan Athletic
Norwich City v Fulham
Stoke City v Reading
Sunderland v Arsenal
Swansea City v Queens Park Rangers
[Saa 2 na Nusu Usiku]
Southampton          v Manchester City
Jumapili Februari 10
[Saa 10 na Nusu Jioni]
Aston Villa v West Ham United
[Saa 1 Usiku]
Manchester United v Everton
Jumatatu Februari 11
[Saa 5 Usiku]
Liverpool v West Bromwich Albion
++++++++++++++++++++++
BPL:
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 25]
1 Man United  Pointi 62
2 Man City   53
3 Chelsea   46
4 Tottenham   45
5 Everton   42
6 Arsenal   41
7 Liverpool  36
8 Swansea  34
9 WBA  34
10 Stoke  30
11 West Ham  30
12 Sunderland  29
13 Fulham  28
14 Norwich  28
15 Newcastle  27
16 Southampton  24
17 Reading  23
18 Wigan  21
19 Aston Villa  21
20 QPR  17

BANGOURA, NANTES WAPEWA ADHABU FIFA.


MAHAKAMA Usuluhishi wa Migogoro ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA imewataka mchezaji wa kimataifa wa Guinea, Ismael Bangoura na klabu yake ya Nantes ya Ufaransa kuilipa klabu ya Al Nasr kiasi cha euro milioni 4.5 kama fidia kwa kuvunja mwkaubaliano ya mkataba. Mchezaji huyo alihamia nchini Ufaransa mwaka jana lakini sasa inaonekana kuwa uhamisho huo ulienda kinyume na makubaliano na klabu ya Al Nasr yenye maskani yake jijini Dubai. Mbali na kutakiwa kulipa faini hiyo, Nantes watatakiwa kutosajili mchezaji yoyote mpya kwa misimu miwili ya kipindi cha usajili majira ya kiangazi kutokana na kukiuka mkataba huo. Pia mchezaji huyo naye alifungiwa kucheza mechi yoyote kwa kipindi cha miezi minne huku tayari akiwa ameshatumikia miezi mitatu kwenye adhabu hiyo.

NGULI WA ZAMANI WA ENGLAND GAZZA APELEKWA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU YA ULEVI.


MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Uingereza, Paul Gascoigne maarufu kama Gazza amepelekwa nchini Marekani kwa matibabu ikiwa ni masaa 24 baada ya wakala wake kubainisha kuwa nyota huyo afya yake iko hatarini kutokana na ulevi uliopindukia. Gazza ambaye amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya ulevi kwa miaka mingi alionekana akiongea kwa kutetemeka mwili mzima wakati alipoalikwa katika shughuli ya kijamii jijini Northampton Alhamisi iliyopita. Picha za video za nyota huyo zilichapishwa katika mtandao wa gazeti la The Sun nchini humo wakimkariri wakala wake Terry Baker akidai kuwa mteja wake huyo alikuwa akihitaji msaada wa haraka kutokana na maisha yake kuwa hatarini. Katika taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari imedai kuwa nyota huyo wa zamani wa klabu za Tottenham Hotspurs, Lazio, Rangers na Newcastle alikubali mwenyewe kwa hiari yake kulazwa katika kliniki inayoshughulika na watu wenye matatizo hayo huko Marekani. Gazza ambaye anahesabika kama mmoja wa wachezaji wenye vipaji zaidi kuwahi kutokea nchini Uingereza aliichezea nchi hiyo mechi 57 za kimataifa.

PETR CECH MCHEZAJI BORA WA MWAKA NCHINI KWAO.


GOLIKIPA nyota wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech na klabu ya Chelsea, Petr Cech amepigiwa kura ya kuwa mchezaji bora wa mwaka 2012 nchini humo. Cech mwenye umri wa miaka 30 alishinda tuzo hiyo jana katika kura zilizopigwa na wachezaji, makocha, maofisa wa shirikisho la soka nchini humo pamoja na waandishi habari hiyo ikiwa ni mara ya tano mfululizo kushinda. Beki anayekipiga katika klabu ya Werder Bremen Theodor Gebre Selassie alishika nafasi ya pili kwenye tuzo hizo huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Petr Jiracek. Mwaka uliopita, Cech alinyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na klabu ya Chelsea na baadae aliisaidia timu yake ya taifa kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya iliyofanyika huko Poland na Ukraine.

WACHEZAJI TENISI WANAHITAJI KUPIMWA DAMU ZAIDI.


MCHEZAJI nyota wa mchezo wa tenisi, Andy Murray anataka wadau wa mchezo huo kujifunza kutokana na kashfa ya utumiaji dawa za kuongeza iliyomkumba Lance Armstrong kwa kuongeza umakini kwenye suala hilo. Murray anaamini kuwa zawadi zinazotolewa katika mchezo huo zinaweza kupunguzwa kama ndio njia pekee ya kuwezesha wachezaji wa mchezo huo kupata vipimo vya damu mara kwa mara ili kulinda hadhi ya mchezo huo. Nyota huyo anayeshika namba tatu katika orodha za ubora duniani amesema hiyo ni juu ya Shirikisho la Tenisi la Kimataifa kuwekeza fedha zaidi ili kuhakikisha vipimo zaidi vinafanyika na kuepukana na kashfa zozote za utumiaji dawa za kuongeza nguvu. Daktari mmoja wa Hispania aitwaye Eufemiano Fuentes kwasasa ana kesi jijini Madrid baada ya kukiri kuwasaidia wanamichezo kuwapa dawa zilizokatazwa michezoni. Shirika la Kimataifa linapambana na matumizi ya dawa hizo michezoni lilidai kuwa wachezaji wa tenisi ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wateja wa Fuentes wakati mpango wake huo ulipostukiwa na polisi nchini Hispania mwaka 2006.

AFCON 2013: NUSU FAINALI: NIGERIA v MALI & GHANA v BURKINA FASO!


AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZE>>BAADA VIPIGO: DROGBA: ‘NIGERIA BINGWA’, ADEBAYOR AMPONDA KOCHA TOGO!
WAKATI NUSU FAINALI za Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zikitarajiwa kuchezwa Jumatano  huko Nchini Afrika Kusini, Masupastaa wa Afrika, Didier Drogba wa Ivory Coast na Emmanuel Adebayor wa Togo, ambao Timu zao zilinyukwa Robo Fainali na kutupwa nje, wameibuka na kuongea kuhusu michuano hiyo huku Drogba akiisifia Nigeria iliyowafunga lakini Adebayor yeye amemzukia Kocha wao Didier Six na kumtwisha lawama.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Ghana v Burkina Faso [Mbombela Stadium, Nelspruit Saa 12 Jioni]
Mali v Nigeria [Moses Mabhida Stadium, Durban Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium, Port Elizabeth Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City, Johannesburg Saa 3 Usiku]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Drogba, baada ya kuchapwa 2-1 na Nigeria kwenye Robo Fainali hapo Jumapili, ameisifia Nchi hiyo na kusema imekuwa ikipanda kiwango Mechi hadi Mechi na Timu hiyo inaweza kutwaa Ubingwa wa Afrika.
Drogba ametamka: “Nimevutiwa na Nigeria walipotufunga. Walifanya kazi ngumu na kubwa na wamejitayarisha vizuri. Sidhani kama kuna Timu itaisimamisha Nigeri!”
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
WAMEFIKAJE NUSU FAINALI:
GHANA:
Makundi:
-Ghana 2 Congo DR 2
-Ghana 1 Mali 0
-Niger 0 Ghana 3
Robo Fainali:
-Ghana 2 Cape Verde 0 
BURKINA FASO:
Makundi:
-Nigeria 1 Burkina Faso 1
-Burkina Faso 4 Ethiopia 0
-Burkina Faso 0 Zambia 0
Robo Fainali:
-Burkina Faso 1 Togo 0 [Dakika 120 za Mchezo]
MALI:
Makundi:
-Mali 1 Niger 0
-Ghana 1 Mali 0
-Congo DR 1 Mali 1
Robo Fainali:
-Afrika Kusini 1 Mali 1[Mali yashinda Penati 3-1]
NIGERIA:
Makundi:
-Nigeria 1 Burkina Faso 1
-Zambia 1 Nigeria 1
-Ethiopia 0 Nigeria 2
Robo Fainali:
-Ivory Coast 1 Nigeria 2
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Nae Nahodha wa Togo, Emmanuel Adebayor, amemvaa Kocha wa Timu yao, Didier Six, na kudai Kocha huyo hakuwa na maamuzi mazuri na uendeshaji wa Timu ulikuwa hauridhishi.
Togo walitolewa kwenye Robo Fainali na Burkina Faso baada ya kuchapwa 1-0 katika Dakika 120 za Mchezo na Adebayor amesema: “Kocha hatukusaidia. Mie nilikuwa Uwanjani sasa siwezi kucheza na kuwa Kocha. Nilijitihidi sana lakini yeye hatukusaidia!”
Jumatano, Nusu Fainali zote mbili za AFCON 2013 zitachezwa kwa Ghana kucheza na Burkina Faso Uwanja wa Mbombela huko Nelspruit na kufuatiwa na Mechi kati ya Mali na Nigeria kwenye Moses Mabhida Stadium Mjini Durban.

ULIMWENGU: TUTAWACHINJA CAMEROON KESHO


Ulimwengu akiwa mazoezini Stars jana

MSHAMBULIAJI wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Thomas Ulimwengu amesema kwamba ana imani wataifunga Cameroon katika mchezo wa kesho wa kirafiki wa kimataifa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza  baada ya mazoezi ya jana, Uwanja wa Taifa, Ulimwengu alisema kwamba kwa kuwa kikosi chao kimekamilika kambini na wachezaji wa ari kubwa, anaamini watashinda mchezo wa kesho.
Uli, anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alisema kwamba wachezaji wa Tanzania sasa wana uzoefu wa kucheza dhidi ya timu kubwa na anaamini kesho watashinda.
“Kweli Cameroon ina wachezaji wengi wanaocheza Ulaya, wazoefu na wazuri hata kiufundi kuliko sisi, lakini hata sisi kwa maana ya wachezaji wa Tanzania tunabadilika sana siku hadi siku, hivyo wapenzi watarajie burudani nzuri kesho,”alisema.
Kwa upande wake, kiungo Simon Msuva alisema kwamba anafurahi sana kuwapo katika kikosi cha timu ya taifa na kupata mechi za kumkomaza kisoka.
“Mechi hizi zinamjenga mchezaji, sana tena. Naamini nikipewa nafasi Jumatano nitafanya vizuri na mashabiki watafurahia,”alisema Msuva, anayechezea Yanga.
Amri Kiemba alisema kwamba anafurahia umoja uliopo ndani ya timu yao kwa sasa na hiyo ni chachu ya ushindi kesho.
“Wachezaji tunakaa vizuri, pamoja na tunapendana, viongozi wanatujali, kwa kweli tupo katika mazingira mazuri na hii naamini ni chachu ya ushindi kwetu,”alisema Kiemba, anayechezea Simba SC.       
Wachezaji 21 wapo kambini Stars katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ambao ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

MAMIA SIMBA KUMPOKEA TAJIRI WAO, MALKIA WA NYUKI


Mama Rahma akiwa na Simba Oman

WANACHAMA wa klabu ya Simba SC, wametakiwa kufika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Februari 10, mwaka huu kumpokea mfadhili wao wa ziara ya Oman, Mama Rahma Al Kharoos, Malkia wa Nyuki, anayetarajiwa kutua nchini siku hiyo.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba, wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wanatakiwa kufika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam siku hiyo kumpokea mfadhili huyo.
“Mama huyu ametusaidia sana kwa kweli, katika kambi yetu ya Oman alitumia zaidi ya Sh. Milioni 80 ambazo ziliisaidia sana timu kwa maandalizi, kwa hiyo tunaomba twende tukampokee, ili kulipa fadhila kwake,”alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema kwamba Mama Rahma atakuwa Mkuu wa Msafara wa Simba itakapokwenda nchini Angola kucheza na Libolo ya huko katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu wiki iliyopita, Simba iliweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na hatua hiyo kwa ufadhili kamili wa Malkia wa Nyuki. Hayo yalikuwa majibu kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC walioweka kambi ya wiki mbili pia nchini Uturuki.
Matunda ya ziara ya Oman ni Simba kuanza Ligi Kuu ya kishindo ikiitandika 3-1 African Lyon na keshokutwa itaingia kwenye mchezo wa pili kusaka pointi dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani.

BIN KLEB: YANGA TUNAWAHOFIA AZAM KULIKO SIMBA SC MBIO ZA UBINGWA



Bin Kleb
MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga SC, Abdallah Ahmad Bin Kleb amesema kwamba wanaihofia sana Azam FC kuliko Simba SC katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Akizungumza  jana, Kleb alisema kwamba hadi sasa safari bado ni ndefu kuelekea kwenye kilele cha ubingwa na timu zote tatu, Yanga, Azam na Simba SC zina nafasi ya kutwaa taji hilo.
“Lakini kwa mwenendo wa ligi jinsi ulivyo, kuna kila sababu ya kuihofia Azam kuliko Simba ambao ni mabingwa watetezi. Kwanza hawa ndio wapo nyuma yetu tukiwa tunawazidi pointi tatu tu. Pili, ni timu nzuri na ina nyenzo za kutosha za kupambana,”alisema Bin Kleb.
Mwenyekiti huyo alisema anafurahia ushindani uliopo katika Ligi Kuu, kwani ni kipimo kizuri kwa timu na ndiyo maana wao wameamua kujipanga upya kwa ajili ya mechi zijazo.
“Tumetoa sare ambayo kwa kweli haikutarajiwa (dhidi ya Mtibwa), tumepunguza idadi ya pointi ambazo tulikuwa tunawazidi Azam kutoka tano hadi tatu, sasa hii maana yake tukiteleza tena, watatukamata, hatuko tayari kwa hilo, tunajipanga upya kuelekea mechi zijazo,”alisema Bin Kleb.
Bin Kleb alisema kwamba wana imani na timu yao na maandalizi waliyofanya kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, hivyo ndoto za ubingwa zipo pale pale. “Matumaini ya ubingwa yapo sana tu, nachozungumzia hapa ni changamoto ambazo tutakabiliana nazo, ndiyo kama hivyo Azam ni timu ambayo tunaihofia zaidi kuliko Simba,”alisema.
Yanga ipo kileleni mwa Ligi Kuu kwa pointi zake 33, ikifuatiwa na Azam yenye 30, wakati SImba ina pointi 27, timu zote zikiwa zimecheza mechi 15 kila moja.

POULSEN: NATAKA MECHI NGUMU ZAIDI KUJENGA STARS IMARA YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2014


Kim katikati akizungumza na Waandishi mchana wa leo, kulia Nahodha Juma Kaseja na kushoto, Katibu wa TFF, Angetile Osiah


KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Poulsen amesema kwamba anataka mechi ngumu zaidi ili kujenga timu imara ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Pouslen alisema kwamba yuko tayari kwa mchezo wowote dhidi ya timu ngumu kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake.
Kaseja akizungumza na Waandishi leo TFF
Poulsen alisema kwamba ameiandaa vyema timu yake kwa ajili ya mchezo wa kesho na vijana wake wameonyesha kabisa wako tayari kwa mechi hiyo, inayotarajiwa kuwa kali na ya kusisimua.
“Tulikuwa tuna mazoezi mazuri jana, wachezaji wote wameripoti na wako vizuri, wanafahamiana na wamecheza baina yao, Mtibwa Sugar, Yanga na Azam, wanapeana changamoto. Wanapendana. Napenda sana kaulimbiu ya Umoja ni nguvu, wachezaji ni wamoja, sisi wote ni wamoja”alisema.
Poulsen alisema kwamba wachezaji wake wanajua wanatakiwa kucheza vizuri kesho, ili kuwapa changamoto Cameroon katika mchezo huo, ambao mashabiki wanausubiri kwa hamu.
Kim alisema wananawaheshimu Cameroon ni timu nzuri na kubwa, yenye wachezaji wazuri, lakini hilo haliwazuii kusema watashinda mechi ya kesho.
“Tunaamini staili yetu ya uchezaji itatupeleka katika zama nyingine. Mtindo wetu ni kupiga pasi kwa wingi na kutengeneza nafasi na kufunga, tukicheza kwa haraka. Na hata tukipoteza mpira, tunajituma wote kuutafuta. Nina uhakika wachezaji wako tayari kwa mechi,”alisema.
Kwa upande wake, Nahodha wa timu hiyo Juma Kaseja amesema kwamba wako tayari kwa mchezo huo na wanaomba Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kesho kuiunga mkono timu yao.
“Sisi wote ni Watanzania, na wote tunahitaji furaha, wenyewe watakuwa 11 na sisi tutakuiwa 11 na tunatarajia utakuwa mchezo mzuri, mgumu na tutaonyesha kile tulichokionyesha kwenye mchezo uliopita na Zambia,”alisema Kaseja.
Wachezaji 21 wapo kambini Stars katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam ambao ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Cameroon ilianza kutua jana kwa mafungu, kundi la kwanza lenye watu 13 likiingia nchini saa 4.40 usiku, kundi la pili linaloongozwa na Nahodha, Eto’o linatarajiwa kutua leo saa 3.45 asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Eto’o anayechezea timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi atatua kwa ndege ya Kenya Airways akiwa na Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik.
Saa moja baadaye baada ya Eto’o kutua na wenzake, Kocha wa timu hiyo Jean Paul Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways wakitokea Afrika Kusini.
Leo pia kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM ambalo lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya Ufaransa.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ikiwa inashika nafasi ya pili katika kundi lake kuwania tiketi ya Brazil mwakani, nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.

KUTOKUWA MAKINI KWA TIMU ZA TANZANIA KATIKA USAJILI WA KUSAJILI BILA KUMFANYIA MAJARIBIO MCHEZAJI ZINAWEZA KUMSAJILI RIGOBRT SONG YUKO TAYARI KUSAINI SIMBA, AU YANGA HATA AZAM


Song leo; Nipo tayari kucheza klabu yoyote Tanzania

BEKI wa zamani wa Liverpool ya England, Rigobert Song Bahanag amesema yuko tayari kusaini klabu yoyote ya Tanzania, iwe Yanga, Azam hata Simba SC achezee kumalizia soka yake, iwapo watampa ofa ya kuridhisha.
Akizungumza  leo mchana mjini Dar es Salaam, Song ambaye kwa sasa amestaafu soka na kuwa Meneja wa timu ya taifa ya Cameroon, amesema kama ipo klabu kweli ya hapa itakayoonyesha nia naye, atakuwa tayari kwa mazungumzo. 
"Kwa nini nikatae ofa ya kunirudisha uwanjani?" alihoji Song baada ya kuulizwa iwapo itatokea klabu ya Tanzania kumuhitaji amalizie soka yake. "Sijui timu za hapa, ila yoyote ikinitaka inifuate hotelini tuzungumze,"aliasema.
Song alisema ameamua kustaafu ingawa anajiona bado yuko fiti ili kuwapisha wachezaji wengine, kwani anaona umri wa miaka 36 ni mkubwa na amecheza kwa muda mrefu. 
Song, aliyezaliwa Julai 1, mwaka 1976, baada ya kustaafu soka kwa sasa mbali na kuwa Meneja wa timu ya taifa ya nchi yake aliyoichezea kuanzia mwaka 1993 hadi 2010, pia ni mchambuzi wa masuala ya kabumbu katika Televisheni ya Channel Orange Sports.
Kisoka, Song aliibukia katika klabu ya Metz ya Ufaransa mwaka 1994, ambako alidumu hadi 1998 alipohamia Salernitana aliyoichezea hadi 1999 alipotua Liverpool, ambako hata hivyo hakudumu mwaka 2000 akahamia West Ham United ya nchini humo pia, aliyoichezea hadi 2001 akahamia FC Koln kwa mkopo, baadaye Lens ya Ufaransa mwaka 2002 hadi 2004, Galatasaray ya Uturuki 2004 hadi 2008 na kumalizia soka yake Trabzonspor ya Uturuki pia, 2008 hadi 2010.
Jumla katika ngazi ya klabu, Song amecheza mechi 417 na kufunga mabao 11, wakati timu ya taifa amecheza mechi 138 na kufunga mabao matano.