Saturday, October 27, 2012

 

TABORA MISS TPSC 2012/13 APATIKANA;


 MISS TPSC 2012/2013
 KUSHOTO NI MSHINDI WA PILI KATIKATI NI MSHINDI WA KWANZA NA KULIA MSHINDI NAMBA TATU
 TANO BORA
 KATIKA VAZI LA UBUNIFU
 VAZI LA USIKU
 BAKARI TAMBWE (JAJI MKUU) AKISOMA WASHINDI WA TANO BORA
 MAJAJI KUTOKA KUSHOTO NI MAMA KAPE, MSHINDI WA 5MISS ILALA 2010
 KING WA MIDUARA AKIWAPA RAHA MASHABIKI WALIOJITOKEZA HAPO
MWANADADA KAPAGAWA NA MIONDOKO YA MIDUARA YA AT MPAKA KAAMUA KUPANDA JUU
AT

 NA MASHABIKI WAKE
 RAISI WA CHUO (KUSHOTO) NA MATRON WA CHUO KATIKATI


MISS TPSC NA SHABIKI WAKI ENJOY NA PHOTO

 WASHINDI WAKITOKELEZEA KWA FOTO NA MASHABIKI WAO
 BABY MAMA MSANII WA TABORA
 K MAREKANI MSANII WA TABORA
 FULL BURUDANI
 MKONGO NA MODO WA CHUO; BURUDANI NENE YA KISANORA
NI NOUUUUUUUMA

 MC's MKALI WA MANENO YA KI MC

AT AKIPAGAWISHA KWA MASHABIKI WAKE HUKU WACHEZA SHOO WAKE NAO FULL MAKAMUZI

 WATU SHAZI
 WADAU
 WAREMBO NA AZONTO
 AZONTO! AZONTO!
 WADAU
 IDRISA NA WAKULICHOMBE

»MAZOEZI YA VOLLEYBALL TPSC

t




A SPIKIER
 
DUKU SWAGA
 
 WADAU WA VOLLEYBALL

baada ya mazoezi wachezaji hawa wa TPSC wanatuliza msuli

NI PATASHIKA SIMBA NA AZAM TAIFA LEO, YANGA WALIVAA GWARIDE LA OLJORO ARUSHA

Azam FC

LIGI Kuu ya soka ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea leo kwa nyasi za viwanja vitano kuwaka moto, huku macho na masikio ya wengi yakiwa katika Viwanja vya Taifa, Dar es Salaam ambako Simba na Azam FC zitakuwa zikimenyana na Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, ambako Yanga SC watakuwa wageni wa JKT Oljoro.
Lakini mechi kali zaidi itakuwa kati ya Azam na Simba ambazo zitagombea usukani wa ligi hiyo, zikiendeleza upinzani wao wa tangu msimu uliopita zilipogombea ubingwa.
Simba ndio inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 19 wakati Azam FC ina pointi 18 na Yanga yenye pointi 14, inashika nafasi ya tatu.
Dhahiri Azam ikishinda leo itapanda kileleni na hali itakuwa mbaya zaidi kwa Simba iwapo na Yanga itashinda, kwani mabingwa hao watetezi watakuwa wanawazidi wapinzani wao wa jadi kwa pointi mbili tu.
Azam ipo kambini kwake Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ilipokuwa ikijifua vikali chini ya kocha wake Mserbia, Boris Bunjak, wakati Simba SC waliweka kambi visiwani Zanzibar tangu Jumanne kujiandaa na mechi ya leo.
Simba iliyokuwa bingwa msimu uliopita na Azam iliyoshika nafasi ya pili, ndizo timu pekee ambazo hadi sasa hazijafungwa hata mechi moja katika Ligi Kuu.
Simba imetoa sare nne, dhidi ya Yanga (1-1), Coastal Union na Mgambo (zote 0-0) na Kagera Sugar (2-2) wakati Azam imetoa sare tatu, 2-2 na Toto Africans, 0-0 na Prisons na 1-1 na Ruvu Shoting.
Mechi ya leo itakuwa kipimo kingine cha kocha Mserbia wa Azam, Bunjak ambaye hadi sasa amekwishaiongoza timu hiyo katika mechi 15 tangu awasili nchini kurithi mikoba ya Muingereza, Stewart Hall, Agosti mwaka huu kati ya hizo akiwa ameshinda tisa, sare tatu na kufungwa tatu.
Mechi zote alizofungwa ni dhidi ya Simba, 2-1 kwenye Nusu Fainali ya BancABC Sup8R, 3-2 kwenye Ngao ya Jamii na 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Chamazi.
Hivyo leo Bunjak atakuwa na wajibu wa kuwaridhisha matajiri wenye asili ya Kiarabu, wanaoimiliki timu hiyo, kwamba yeye si mnyonge kwa Mserbia mwenzake anayeinoa Simba SC, Profesa Milovan Cirkovick.
Simba baada ya sare ya tatu mfululizo ikaamua kwenda kuweka kambi Zanzibar kujiandaa na mechi ya leo na kwa kawaida Wekundu wa Msimbazi wamekuwa wakienda visiwani humo katikati ya Ligi kuweka kambi, wanapokuwa wanajiandaa na mechi dhidi ya mahasimu wao tu, Yanga.
Kitendo cha kwenda Zanzibar kinamaanisha Simba wanaupa uzito mkubwa mchezo huo wa leo- sawa tu na mchezo dhidi ya Yanga.
Lakini pia kambi ya Simba imekumbwa na mtikisiko kidogo kuelekea mechi hii, kiasi cha kuwasimamisha wachezaji wake wawili beki Juma Nyosso aliyeambiwa afanye mazoezi ni kikosi cha pili ili kuboresha kiwango chake na kiungo Haruna Moshi ‘Boban’, ambaye amesimamishwa kwa wiki tatu kwa utovu wa nidhamu.
Pamoja na hayo, bado kuna wachezaji ndani ya Simba wanaangaliwa kwa jicho la tatu juu ya mwenendo wao, wakiwemo beki Amir Maftah, viungo Ramadhan Chombo, Mwinyi Kazimoto na Mrisho Ngassa.
Safu ya ulinzi ya Simba itakuwa tena na beki wake chipukizi mahiri, Shomary Kapombe ambaye amekosa mechi mbili zilizopita kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu na leo anaweza akacheza pamoja na Hassan Kondo katika beki ya kati.
Hayatarajiwi mabadiliko makubwa sana kwenye kikosi cha Simba leo, Juma Kaseja akiendelea kusimama langoni, kulia Nassor Masoud ‘Chollo’, kushoto Amir Maftah, katikati Kapombe na Kondo, kiungo mkabaji Amri Kiemba, kulia Mrisho Ngassa, katikati Mwinyi Kazimoto, kushoto Emmanuel Okwi na washambuliaji Felix Sunzu anaweza akaanza na kinda Christopher Edward leo.
Azam bila shaka Mwadini Ali atasimama langoni, kulia Ibrahim Shikanda, kushoto Erasto Nyoni, katikati Said Mourad na Aggrey Morris, kiungo mkabaji Abdulhalim Humud, kulia Kipre Tcheche, kushoto Kipre Balou, katikati Salum Abubakar na washambuliaji John Bocco ‘Adebayor’ na Abdi Kassim ‘Babbi’.
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Yanga haitarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa sana katika kikosi chake kutoka kile kilichoshinda 3-0 dhidi ya Polisi katika mchezo uliopita.
Ally Mustafa ‘Barthez’ anaweza kuendelea kusimama langoni, kulia Juma Abdul, kushoto Oscar Joshua, katikati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Mbuyu Twite, kiungo mkabaji Athumani Iddi ‘Chuji’, kulia Simon Msuva, kushoto David Luhende, katikati Haruna Niyonzima na washambuliaji Didier Kavumbangu na Jerry Tegete.
JKT Oljoro; Shaibu Issa, Yussuf Nachogote, Nafo Zuberi au Jackson Semfukwe, Salim Mbonde, Marcus Raphael (Nahodha), Emanuel Memba, Karage Gunda, Saleh Iddi au Amir Omar, Paul Nonga, Meshack Nyambele na Sixbert Mohamed au Essau Sanu.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni kati ya African Lyon na Kagera Sugar Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, Mgambo JKT na Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na Ruvu Shooting dhidi ya Polisi Morogoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa michezo miwili kati ya JKT Ruvu na Coastal Union Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Toto Africans dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Simba SC
REKODI YA SIMBA NA AZAM LIGI KUU:
Februari 11, 2012
Simba SC 2 - 0 Azam FC
Sept 11, 2011
Azam FC 0 - 0 Simba SC
Jan 23, 2011    
Simba 2-3 Azam (Dar).              
Sep 11, 2010
Azam 1-2 Simba (Tanga).
Machi 14, 2010
Azam 0-2 Simba (Dar) 
Okt 24, 2009
Simba 1-0 Azam (Dar)         
Machi 30, 2009
Azam 0-3 Simba (Dar)  
Okt 4, 2008
Simba 0-2 Azam 
Yanga SC
YANGA NA OLJORO MSIMU ULIOPITA:
Aprili 25, 2012
JKT Oljoro 1 – 4 Yanga
Oktoba 23, 2011
Yanga 1 – 0 JKT Oljoro  
JKT Oljoro


KOMBE LA TAIFA (TAIFA CUP) NA UJIO WA WALIMU WA KIKAPU TOKA MAREKANI

1.        Kombe la Taifa (Taifa Cup 2012) kufanyika Tanga
PHARES MAGESA amesema anachukua fursa hii kukutaarifu kuwa mashindano ya  kombe la Taifa (Taifa Cup) mwaka huu yatafanyika Tanga tarehe 29 /10/2012 hadi 4/11, 2012.
Mashindano haya ya Kombe la Taifa kwa kawaida ndio hutumika kuchagua timu zetu za Taifa, hvyo ni muhimu kwa mikoa yote kushiriki ili kuwapa nafasi wanamichezo kutoka mikoa yao kuonekana katika ngazi ya Taifa.
Mikoa iliyothibitisha hadi sasa ni Iringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Singida, Mara, Dodoma, Pemba, Unguja, Tanga, Mtwara, Lindi na Dar Es Salaam.
Bado nafasi ya kuthibitisha kushiriki ipo kwa wanaopenda kushiriki katika mashindano haya na ratiba ya mashindano itapangwa tarehe 28/10/2012 katika kikao ambacho wawakilishi wa mikoa yote lazima wawepo na ndo itakuwa mwisho wa kuthibitisha kushiriki.


2.        Walimu wa Taifa wa Mpira wa Kikapu toka Marekani:
Awali tulitangaza kuhusu ujio wa Makocha wa kikapu toka Marekani kuja kufundisha timu yetu ya Taifa, ambao ni Albert Sokaitis (Kocha Mkuu) ambaye ni Kocha mwenye uzoefu wa miaka 24 kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko huko Marekani katika jimbo la Connecticut. Pia amewahi kufundisha timu na kuendesha mafunzo nchi za Uchina, Lebanon, Ugiriki na Japan.
Ambaye  atasaidiwa na Kocha Jocquis L. Sconiers ambaye nae ana uzoefu wa miaka mingi na kwa sasa ni Kocha Mkuu Msaidizi wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko Marekani katika jimbo la Connecticut.
Walimu wote hawa wana shahada za juu kutoka vyuo vikuu  mbali mbali vya Marekani.
Katika utekelezaji wa mpango huo katika awamu ya kwanza Kocha Sconiers anatarajiwa kuwasili nchini  tarehe 30/10/2012 na ataelekea Tanga siku inayofuata katika Mashindano ya Kombe la Taifa ili kuchagua wachezaji watakaonda timu za Taifa (wanawake na wanaume) na baada ya hapo ataanza mafunzo rasmi kwa timu zote 2 tarehe 5/11/2012.
Awamu hii ya kwanza ya mpango wa mafunzo unadhaminiwa na watu wa Marekani kupitia ubalozi wao hapa Tanzania, tunawashukuru sana watu wa Marekani.


3.        Mashindano ya Kanda ya tano ya FIBA Afrika
Kama mipango yote ikienda vizuri tunatarajia Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano ya kanda ya 5 ya FIBA. Mashindano haya yanayotarajiwa kufanyika hapa Dar Es Salaam kuanzia 15 hadi 22 Desemba, 2012.
Hivyo basi Kocha huyo atatumia nafasi hii kuanza maandalizi ya timu zetu za Taifa kuziandaa kwa mashindano haya yanayotarajiwa kushirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Misri Sudan na Sudani ya kusini.

4.        Mkutano Mkuu wa TBF
Tunatarajia pia kufanya Mkutano mkuu wa TBF na wa bodi kwa mujibu wa katiba siku ya tarehe 1 hadi 2 Novemba, 2012. Viongozi wote wa Mikoa na wawakilishi wachezaji,  vyama shiriki wanaombwa kushiriki bila kukosa katika mkutano huu utakaofanyika Tanga.
Tunaomba wadau wote mtuunge mkono kwa hali na mali kufanikisha malengo yetu ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu kwa faida ya vijana wetu na Taifa letu.

PHARES MAGESA
MAKAMU WA RAIS-TBF

 

Roberto Mancini apingana na Beki wake Micah Richards!


MANCINI_n_MICAHMara baada ya kubondwa bao 3-1 na Ajax Amsterdam kwenye Mechi ya Kundi D la UEFA CHAMPIONZ LIGI ambalo limewaacha Mabingwa wa England Manchester City kuwa mkiani mwa Kundi hilo, kumezuka kutoelewana kati ya Meneja wao Roberto Mancini na Mchezaji wake Micah Richards.
Mara baada ya Mechi hiyo na Ajax, Micah Richards aliuponda Mfumo waliotumia Timu yao wa kuwa na Mabeki watatu, Fomesheni ya 3-5-2, badala ya ule wa kawaida 4-4-2 na kusema uliua matumaini yao ya ushindi.
Meneja Mancini alijibu kama mbogo aliejeruhiwa aliposema: “Ukiwa Mchezaji wa juu mfumo si muhimu. Ukiwa hujui Mfumo, hustahili kuwa Mchezaji wa Timu kubwa.”
Walipocheza na Ajax, Man City ndio walitangulia kufunga bao kupitia Samir Nasri lakini Ajax walizinduka kwa bao za Siem de Jong na Niklas Moisander na kuifanya gemu iwe 2-1 na hapo ndipo Mancini alipoamua kubadili Mfumo  toka 3-5-2 kwenda 4-4-2 ili kuokoa Mechi lakini wakajikuta wakipigwa bao la 3 la Christian Eriksen.
Baada ya Mechi hiyo Micah Richards alikiri Wachezaji wa Man City  hawakujisikia vyema na Mfumo wa 3-5-2 na walipendelea kucheza 4-4-2 waliyoizoea kitu ambacho Roberto Mancini amekipinga vikali kwa kutamka: “Alichosema Micah si muhimu. Alijibu swali. Naelewa Wanahabari wanataka kuandika kuhusu hilo lakini kwangu si muhimu. Pengine Micah hajui kwa sababu hii ni Mechi yake ya kwanza baada ya Miezi miwili na nusu!”

BLATTER ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI FA UINGEREZA BAADA KUMPOTEZA John Connelly.

Rais wa shirikisho la soka Duniani FIFA ,Joseph S. Blatter amekiandikia chama cha soka cha uingereza huku akikielezea kwa uchungu kifo cha aliyekuwa mchezaji wa nchi hiyo na moja ya washindi wa kombe la dunia mwaka  1966  John Connelly. 

Connelly, alikuwa  winga katika maisha yake ya soka kiwanjani ambapo alichezea Timu za Burnley, Manchester United, Blackburn Rovers na  Bury, alifariki Alhamisi akiwa na umri wa Miaka 74 
alikuwa moja ya chachu ya ushindi dhidi ya Uruguay 
, Connelly alikuwa moja kati ya wachezaji katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 66  na alifunga magoli saba katika mechi ishirini alizochezea uingereza katika barua hiyo aliyomuandikia mwenyekiti wa FA 
 David Bernstein, Blatter amesema : “ Ningependa kuelezea salamu zangu za rambirambi za uzunu hasa kwa kumpoteza mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya uingereza  John Connelly ambaye amefariki jana asubuhi  .

“John atakumbukwa kwa kushinda ligi ya uingereza akiwa na Burnley’s katika msimu wa  1960, ambapo kwa wakati huo alikuwa mfungaji bora na baadae aliisaidia Manchester United Kushinda ligi  1965 . 

Kwa niaba ya wanachama wa kimataifa wa familia ya mpira wa miguu Duniani nistajiskia amani zaidi kumpa  heshima yetu 

Familia ya  John’s , Marafiki  na wapendwa wote ambao wamepoteza kipenzi chao  

Wanyama kuihama Celtic


Mcheza kiungo wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee stars, anayeichezea klabu ya Celtic ya Scotland Victor Wanyama, anaripotiwa kudinda kusaini kandarasi mpya na klabu hiyo ya Celtic.
Kandarasi ya wanyama na klabu hiyo ya Celtic inatarajiwa kukamilika mwaka wa 2015, na klabu hiyo ilikuwa na matarajio ya kuumpa mchezaji huyo kandarasi mpya, ili kuzuia uwezekano wa mchezaji huyo kuhamia vilabu vingine, vinavyoshiriki kwenye ligi kuu ya Premier ya England ambavyo vimeonyesha nia ya kumsajili kama vile Manchester United.
Lakini Wanyama mwenye umri wa miaka 21 na ambaye alijiunga na Celtic kutoka kwa klabu ya Beerschot ya Ubelgiji mwaka wa 2011, haamini kuwa kandarasi hiyo mpya inawiana na dhamani yake kwa sasa na hivyo amekataa kuisaini.
Kwa mujibu wa agenti wa Wanyama, Rob Moore, tayari Celtic imefahamishwa kuwa kandarasi hiyo haikithi matarajio ya mchezaji huyo.
Ripoti zinasema klabu hiyo ya celtic ilikataa ombi kutoka kwa vilabu kadha ambavyo vilikuwa vikitaka kumsajili mchezaji huyo mapema mwaka huu.Kuna fununu kuwa huenda mchezaji huyo akahamia England msimu ujao wa usajili na miongoni mwa vilabu ambavyo vimeonyesha nia ya kumsajili ni pamoja na Manchester United,Manchester City na Tottenham.

Silvio Berlusconi kwenda jela miaka minne kwa kukwepa kodi.




Waziri mkuu wa zamani wa Italia ambaye pia ni Rais wa klabu ya AC Milan ya nchini humo Silvio Berlusconi amehukumiwa kwenda jela miaka minne kutoka na ukwepaji wa kodi.
Berlusconi na wenzie 10 walikuwa wakituhumiwa kununua haki za kampuni ya kimarekani ya filamu kwa bei ya kutupa kupitia kampuni za nje wakati wa utawala wake kama waziri mkuu.
Waziri huyo mkuu wa zamani wa Italia anatarajiwa kukata rufaa juu ya hukumu hiyo.
Katika usomwaji wa hukumu hiyo aliunganishiwa kesi mbalimbali zinazohusu mambo ya kibiashara lakini zilitupiliwa mbali kwa kigezo cha kwamba zilikuwa nje ya muda.
Wakati akisomewa hukumu hii , waendesha mashitaka walidai kuwa sehemu ya pesa za kununulia haki za filamu zilitumika katika uharamia wa kukwepa kodi kupitia kampuni yake ya Mediaset.
Mahakama imemuhuku Berlusconi muda mrefu jela kuliko miaka mitatu na miezi nane kama ilivyoombwa na waendesha mashtaka.

TENESI: WACHEZAJI BORA WANNE WANAWAKE DUNIANI KUWASHA MOTO LEO KTK NUSU FAINALI YA WTA.


Mchezaji bora No.1 wa Tenesi duniani kwa upande wa wanawake Victoria  Azarenka (Belarus) jana amejihakikishia kubaki akishikilia usukani wa dunia na kufuzu kucheza nusu fainali ya mabingwa wa WTA dhidi ya Maria Sharapova (Urusi) mchezaji bora No.2 wadunia.                                                                          
 Nae bingwa wa Olympic, Wimbledon and US Open ,Serena Williams (USA) ambaye kwasasa ni No.3 anatarajiwa kupambana na World No. 4 Agnieszka Radwanska (Poland).             
Nusu fainali hii inatarajiwa kuendelea leo mjini Istambul, Uturuki na hitimisho la michuano ni jumapili ya tarehe 28, Oktoba.