Saturday, October 20, 2012

VPL: Yanga yatoka nyuma 2-0, yashinda 3-2!

VPL_LOGOMATOKEO:
Jumamosi Oktoba 20
Yanga 3 Ruvu Shootings 2
Coastal Union 3 Mtibwa Sugar 1
++++++++++++++++++++++
Katika mfululizo wa Mechi za Ligi Kuu Vodacom zilizochezwa leo, Yanga, ikicheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ilijikuta iko nyuma kwa bao 2-0 ndani ya Dakika 9 za kwanza walipocheza na Ruvu Shooting lakini wakazinduka na kushinda bao 3-2.
Ruvu Shooting walipiga bao zao 2 kupitia Seif Abdallah katika Dakika ya 2 na ya 9.
Bao za Yanga zilifungwa na Mbuyu Twite, Dakika ya 20, Jerry Tegete, Dakika ya 35 na Didier Kavumbagu katika Dakika ya 65.
Katika Mechi nyingine ya VPL iliyochezwa huko Mkwakwani, Jijini Tanga, wenyeji Coastal Union waliifunga Mtibwa Sugar bao 3-1.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumapili.
++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili Oktoba 21
JKT Ruvu v JKT Oljoro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mgambo JKT v Simba [Mkwakwani, Tanga]
Tanzania Prisons v Toto Africans [Sokoine, Mbeya]
++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO VPL:
1 Simba Mechi 8 Pointi 18
2 Azam FC Mechi 7 Pointi 17
3 Yanga SC Mechi 8 Pointi 14
4 Coastal Mechi 8 Pointi 13
5 JKT Oljoro Mechi 8 Pointi 13
6 Kagera Mechi 8 Pointi 12
7 JKT Ruvu Mechi 8 Pointi 10
8 Prisons Mechi 7 Pointi 9
9 Ruvu Shooting Mechi 8 Pointi 9
10 JKT Mgambo Mechi 8 Pointi 9
11 Mtibwa Sugar Mechi 7 Pointi 8
12 Toto African Mechi 8 Pointi 7
13 African Lyon Mechi 8 Pointi 7
14 Polisi Moro Mechi 8 Pointi 2

Man United safi, Mtu 10 Man City poa, Liverpool yashinda!

>>’KINDA’ Rahim Sterling aipa ushindi Liverpool!
BPL_LOGORATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 20
Fulham 1 Aston Villa 0
Liverpool 1Reading 0
Man United 4 Stoke 2
Swansea 2 Wigan 1
West Brom 1 Man City 2
West Ham 4 Southampton 1
[SAA 1 na Nusu Usiku]
Norwich v Arsenal
=============================
Man United 4 Stoke 2
Manchester United, wakicheza kwao Old Trafford, walitoka nyuma kwa bao 1-0 alilojifunga mwenyewe Wayne Rooney na kuichapa Stoke City kwa bao 4-2.
++++++++++++++++++++

MAGOLI:
Man United= 4 Rooney 27′, 65′ Van Persie 44′ Welbeck 46′ .
Stoke= 2 Rooney 11′ (Kajifunga mwenyewe) Kightly 58′ .
++++++++++++++++++++
Ushindi huu umeifanya Man United iendelee kukamata nafasi ya pili wakiwa na Pointi 18 na wapo nyuma ya vinara Chelsea kwa Pointi 4 huku Mechi inayofuata ni safari ya kwenda huko Stamford Bridge kupambana na Chelsea Wiki ijayo.

VIKOSI:
Man United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Evans, Evra, Valencia, Scholes, Carrick, Welbeck, van Persie, Rooney
Akiba: Lindegaard, Anderson, Giggs, Hernandez, Nani, Powell, Wootton.
Stoke: Begovic, Cameron, Huth, Shawcross, Wilson, Nzonzi, Whitehead, Walters, Adam, Kightly, Crouch
Akiba: Sorensen, Palacios, Jones, Owen, Upson, Etherington, Wilkinson.
Refa: Anthony Taylor
+++++++++++++++++++++++++++++++
Fulham 1 Aston Villa 0
Bao la Dakika ya 84 la Chris Baird limewapa Fulham ushindi wa bao 1-0 wakiwa nyumbani kwao Craven Cottage walipocheza na Aston Villa.

VIKOSI:
Fulham: Schwarzer, Riether, Hughes, Hangeland, Riise, Sidwell, Baird, Richardson, Rodallega, Berbatov, Petric
Akiba: Stockdale, Senderos, Kasami, Karagounis, Diarra, Dejagah, Kacaniklic.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Bennett, Ireland, El Ahmadi, Delph, Holman, Bent, Agbonlahor
Akiba: Given, N'Zogbia, Albrighton, Benteke, Bannan, Weimann, Lichaj.
Refa: Chris Foy
+++++++++++++++++++++++++++++++
West Ham 4 Southampton 1
West ham leo wameichapa Southampton bao 4-1 kwa bao za Mark Noble, bao mbili,  Kevin Nolan na Modibo Maiga.
Bao pekee la Southampton lilifungwa na Adam Lallana.

VIKOSI:
West Ham: Jaaskelainen, Tomkins, Collins, Reid, McCartney, Noble, Diame, Benayoun, Nolan, Jarvis, Carroll
Akiba: Spiegel, Cole, Maiga, Spence, O'Neil, Chambers, Hall.
Southampton: Boruc, Clyne, Hooiveld, Fonte, Yoshida, Puncheon, Schneiderlin, Steven Davis, Lallana, Rodriguez, Do Prado
Akiba: Kelvin Davis, Lambert, Ward-Prowse, Mayuka, Seaborne, Chaplow, Reeves.
Refa: Neil Swarbrick
+++++++++++++++++++++++++++++++
Liverpool 1 Reading 0
Bao pekee la Kinda Raheem Sterling limewapa Liverpool ushindi wao wa kwanza Uwanjani kwao Anfield chini ya Meneja Brendan Rodgers.

VIKOSI:
Liverpool: Jones, Wisdom, Skrtel, Agger, Johnson, Gerrard, Allen, Sahin, Fernandez Saez, Suarez, Sterling
Akiba: Gulacsi, Jose Enrique, Assaidi, Henderson, Downing, Carragher, Shelvey.
Reading: McCarthy, Cummings, Gorkss, Mariappa, Shorey, Kebe, Guthrie, Leigertwood, Karacan, McAnuff, Pogrebnyak
Akiba: Stuart Taylor, Gunter, Pearce, Le Fondre, McCleary, Robson-Kanu, Roberts.
Refa: Roger East
+++++++++++++++++++++++++++++++
Swansea 2 Wigan 1
Wachezaji kutoka Spain, Pablo Hernandez na Miguel Michu, leo wamepiga bao na kuipa Swansea ushindi wa bao 2-     1 dhidi ya Wigan.
Bao la Wigan lilifungwa na Emmerson Boyce.

VIKOSI:
Swansea: Vorm, Rangel, Chico, Williams, Davies, Routledge, de Guzman, Ki, Britton, Hernandez, Michu
Akiba: Tremmel, Graham, Dyer, Monk, Shechter, Moore, Tiendalli.
Wigan: Al Habsi, Caldwell, Figueroa, Ramis, McCarthy, McArthur, Boyce, Beausejour, Kone, Maloney, Di Santo
Akiba: Pollitt, Jones, Watson, Gomez, McManaman, Boselli, Miyaichi.
Refa: Mike Jones
+++++++++++++++++++++++++++++++
West Brom 1 Man City 2
Dakika moja toka aingingizwe kutoka benchi Edin Dzeko aliwaokoa Mabingwa Manchester City, waliokuwa wakicheza Mtu 10 baada ya James Milner kupewa Kadi Nyekundu, kutoka kwenye kipigo kwa kusawazisha bao katika Dakika ya 80 na kufunga bao la pili na la ushindi katika Dakika ya 90.
++++++++++++++++++++

MAGOLI:
WBA= 1 Shane Long, 67
Man City= 2 Edin Dzeko 80 na 90
++++++++++++++++++++
Ushindi huu umewafanya Man City wabakie nafasi ya 3 kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa na Pointi 18 sawa na Timu ya pili Man United ambayo imewazidi kwa ubora wa mabao na vinara bado ni Chelsea wenye Pointi 22.

VIKOSI:
West Brom: Foster, Ridgewell, Olsson, McAuley, Tamas, Yacob, Mulumbu, Dorrans, Morrison, Fortune, Long
Akiba: Luke Daniels, Popov, Rosenberg, Jara Reyes, Lukaku, Gera, Odemwingie.
Man City: Hart, Clichy, Lescott, Kompany, Richards, Milner, Barry, Nasri, Toure, Balotelli, Tevez
Akiba: Pantilimon, Zabaleta, Dzeko, Sinclair, Kolarov, Aguero, Toure.
Refa: Mark Clattenburg
+++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA
Jumapili Oktoba 21
[SAA 9 na Nusu Mchana]
Sunderland v Newcastle
[SAA 12 Jioni]
QPR v Everton
 
BPL: Chelsea yaidunda Spurs wazidi kupaa kileleni!

BPL_LOGOChelsea leo wamepata ushindi wao wa kwanza Uwanja wa White Hart Lane tangu Mwaka 2005 walipoibonda Tottenham mabao 4-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyoanza mapema na ushindi huo umewafanya Chelsea waendelee kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 22 kwa Mechi 8.
Chelsea ndio walitangulia kufunga bao katika Dakika ya 17 mfungaji akiwa Gary Cahill na bao hilo kudumu hadi mapumziko.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Tottenham 2= Gallas 47′ Defoe 54′ .
Chelsea 4= Cahill 17′ Mata 66′, 69′ Sturridge 90′
+++++++++++++++++++++++++++++++
Kipindi cha Pili, Spurs walizinduka na kufunga bao mbili kupitia William Gallas na Jermain Defoe.
Hata hivyo, Chelsea waliendelea kutawala na Juan Mata akasawazisha na kupiga bao jingine na kuwafanya waongoze kwa bao 3-2 kabla Mchezaji alietoka benchi Daniel Sturridge kupiga bao la 4.
Haya ni matokeo ya kumvunja nguvu Meneja wa Tottenham manager Andre Villas-Boas ambae alikuwa kisimamia Mechi yake ya kwanza dhidi ya Chelsea ambayo ilimfukuza mwanzoni mwa Mwaka huu.
=============================
VIKOSI:
Tottenham: Friedel, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Huddlestone, Sandro, Lennon, Sigurdsson, Dempsey, Defoe
Akiba: Lloris, Adebayor, Naughton, Dawson, Falque, Livermore, Townsend.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Ramires, Mikel, Oscar, Hazard, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Lampard, Moses, Sturridge, Azpilicueta, Bertrand.
Refa: Mike Dean (Wirral)
=============================

PETER_CROUCH>>LEO ni ‘ALMASI’ au ‘MAWINGA’??MAN_UNITED_ALMASI
Ingawa Sir Alex Ferguson ametoboa kuwa atakuwa akibadilisha Mifumo ya Uchezaji ya Timu yake ya Manchester United kutoka Fomesheni ya ‘Almasi’  na wakati mwingine kutumia Mfumo wenye Mawinga kama ilivyozoeleka kwa Kikosi chake lakini kwa ajili ya Mechi yao ya leo ya Ligi Kuu England itakayochezwa Uwanjani Old Trafford dhidi ya Stoke City, Meneja huyo amekataa kuthibitisha nini kitatumika.
Akichezesha Kikosi cha bila ya Mawinga, kwa kutumia Mfumo wa ‘Almasi’,  Wayne Rooney hurudishwa kwenye Kiungo na kucheza nyuma ya Mastraika Robin van Persie na Danny Welbeck mtindo ambao waliutumia walipoifumua Newcastle bao 3-0 kwenye Mechi yao ya mwisho ya Ligi.
Lakini kwa Mechi ya leo, na hasa baada kupona kwa Ashley Young, na pia kuwepo kwa Nani na Valencia, huenda Sir Alex akawatumia Wachezaji hao kucheza kwenye Wingi.
Sir Alex Ferguson amesema: “Ni ngumu kupanga Timu. Nadhani wakati mwingine Fomesheni ya Almasi inafanya kazi vizuri, wakati mwingine tunahitaji Mawinga. Tunaweza kucheza yeyote. Tony Pulis [Meneja wa Stoke City] atakuwa akijiuliza tutacheza Fomesheni ipi lakini pia naweza kutumia vyote, Almasi na Mawinga, na kuwa na Walinzi wawili tu!”
Hata hivyo Stoke City ni Timu ya kipekee kwenye Ligi Kuu inayotumia nguvu na mipira mirefu, hasa ya kurusha, wakimlenga ‘Ngongoti’ Peter Crouch lakini Sir Alex Ferguson amesema hilo watalidhibiti na haliwasumbii.
Amesisitiza: "Cheza mchezo wako huna haja ya kuogopa au kufikiria sana wao watacheza vipi. Tunajua watapata frikiki, tunajua watatumia mipira mirefu kuingiza ndani ya boksi letu na watatumia mipira mirefu kwa Peter Crouch."
Amemalizia: “Matayarisho ni rahisi tu. Tunajua kile watakachokifanya. Mara nyingine unacheza na Timu hujui watafanya nini. Dhidi ya Stoke tunajua kila kitu watakachofanya. Wacha tu tucheze gemu yetu wenyewe. Pengine hilo litafanya kazi vyema kwetu.”
 
Kiongozi FIFA ataka ‘Wabaguzi’ Serbia wafungiwe, Terry bado Kepteni Chelsea, Shabiki amtwanga Kipa Uwanjani!

FREDINAND-TERRY_MKNO_HAMNAKufuatia vitendo vya Mashabiki wa Serbia vilivyokithiri vya Ubaguzi, Kiongozi wa juu wa FIFA ameitaka Nchi hiyo ifungiwe na huko Stamford Bridge, Chelsea imetamka John Terry atabaki kuwa Kepteni licha ya kusulubiwa kwa Ubaguzi wakati huko Uwanja wa Hillsborough Shabiki mmoja alivamia Uwanjani na kumpiga Kipa hadi akamwangusha chini.
UBAGUZI Serbia v England:  Makamu Rais FIFA, Jim Boyce, aitaka Serbia ifungiwe!
Makamu wa Rais wa FIFA, Jim Boyce, ameitaka UEFA ifikirie kuifungia Serbia katika Mashindano yajayo kufuatia tuhuma za Ubaguzi wa Washabiki wao zilizotokea kwenye Mechi ya kuwania kuingia Fainali za EURO 2013 kwa Vijana wa Chini ya Miaka 21 iliyochezwa huko Nchini Serbia Jumanne iliyopita na England kufuzu kwenda Fainali baada ya kushinda Mechi zote mbili kwa bao 1-0 kila moja.
Tayari UEFA imeshaifungulia Serbia Mashitaka ya Ubaguzi na pia kushindwa kudhibiti Wachezaji wake kosa ambalo pia FA ya England imeshitakiwa.
Kuhusu shutuma za Ubaguzi, Jim Boyce, ametamka: “Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya FA ya Serbia! Wafungiwe Viwanja vyao na pia uangaliwe uwezekano wa kutowashirikisha Mashindano yajayo.”
Boyce pia alidai vitendo vya Ubaguzi vya Serbia si mara ya kwanza na inabidi hatua kali zichukuliwe kuvikomesha.

Terry abakishwa Kepteni Chelsea
Licha ya kusulubiwa kwa Ubaguzi na FA pamoja na Klabu yake mwenyewe, Nahodha wa Chelsea, John Terry, ataendelea kubaki kama Kepteni wa Timu hiyo kufuatia uamuzi huo kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Bruce Buck.
Terry amefungiwa na FA Mechi 4 na pia kupigwa Faini Pauni 220,000 na pia Chelsea imethibitisha kumpiga ‘Faini kubwa.’ kwa kosa la kumkashifu Kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand kwenye Mechi iliyochezwa Loftus Road hapo Oktoba 23, 2011.

Kipa Chris Kirkland apigwa Uwanjani na Shabiki wa Leeds!
Kipa wa Sheffield Wednesday Chris Kirkland hapo jana alivamiwa Uwanjani wakati wa Mechi ya Timu yake na Leeds United na kushambuliwa na Shabiki wa Leeds kwa nguvu kubwa na kumfanya aanguke chini na kuhitaji matibabu.
Hata hivyo, Kipa huyo wa zamani wa Liverpool mwenye Miaka 31, na ambae pia aliwahi kuichezea England Mechi moja, aliweza kuendelea na kumaliza Mechi hiyo iliyokwisha matokeo yakiwa 1-1.
Akiongelea tukio hilo, Meneja wa Sheffield Wednesday, Dave Jones, alisema: “Hawa ni kama Wanyama. Wapigwe marufuku kwenye Viwanja vyote vya ugenini ikiwa tabia yao ni hii!”
Kwenye Mechi hiyo waliyocheza ugenini, Leeds ilikuwa na Mashabiki 5,300 kati 28,582 waliokuwepo Uwanjani.
Mara baada ya Mechi hiyo Klabu ya Leeds iliomba radhi kwa tukio hilo na kusema itashirikiana na Polisi ili kumtambua Shabiki huyo.

BPL: Wachezaji gani kukosekana kila Timu kwa Mechi Wikiendi hii!

BPL_LOGOIfuatayo ni Taarifa fupi kutoka Kambi ya kila Timu ya Ligi Kuu England, BPL, kuhusu hali za Wachezaji wao na yupi atakosekana kwa Mechi za Ligi Wikiendi hii:
JUMAMOSI Oktoba 20
Tottenham v Chelsea
Uwanja: White Hart Lane Saa: 8 Dakika 45 Mchana
Kwa Tottenham Scott Parker (Kifundo cha Mguu) hatacheza lakini Jake Livermore na Kyle Naughton wanaweza kuwemo Kikosini.
John Terry anaanza kutumikia Kifungo cha Mechi 4 kwa Chelsea kuanzia Mechi hii.
Refa: M Dean
Fulham v Aston Villa
Uwanja: Craven Cottage Saa: 11 Jioni
Dimitar Berbatov, aliekuwa akijiuguza paja, na Mladen Petric ,mguu, wote wamepona na wanaweza kuichezea Fulham pamoja na Mahamadou Diarra, aliepona goti, lakini Bryan Ruiz, maumivu ya nyonga, huenda asicheze.
Aston Villa hawana matatizo.
Refa: C Foy
Liverpool v Reading
Uwanja: Anfield Saa: 11 Jioni
Liverpool huenda wakamkosa Kipa wao Pepe Reina, alieumia musuli ya Mguu akiwa na Spain, na pia Straika Fabio Borini, alievunjika mguu, hatacheza lakini Jonjo Shelvey anarudi Kikosini baada ya kutumikia Kifungo.
Reading wanasubiri Madaktari waamue kama Noel Hunt, aliekuwa kaumia Kifundo cha Mguu, kama anweza kucheza lakini Mikele Leigertwood tayari ameruhusiwa na Madaktari.
Refa: R East
Man United v Stoke
Uwanja: Old Trafford Saa: 11 Jioni
Winga Ashley Young (Goti) amepona na anaweza kuichezea Manchester United baada ya kuwa nje kwa Miezi miwili lakini Chris Smalling bado kuwa fiti kwa Mechi. Stoke wana wasiwasi juu ya Glenn Whelan, Mguu, na Michael Owen, nyonga lakini Andy Wilkinson amepona.
Refa: A Taylor
Swansea v Wigan
Uwanja: Liberty Saa: 11 Jioni
Swansea hawana matatizo lakini Wigan watawakosa Antolin Alcaraz na Albert Crusat.
Refa: M Jones
West Brom v Man City
Uwanja: The Hawthorns Saa: 11 Jioni
Wasiwasi kwa West Bromwich Albion ni juu ya Youssouf Mulumbu na Manchester City watawakosa Viungo David Silva na Jack Rodwell, wote wakiwa na maumivu ya musuli za pajani pamoja na Javi Garcia, paja, na Maicon, mguu.
Refa: M Clattenburg
West Ham v Southampton
Uwanja: Upton Park Saa: 11 Jioni
West Ham watamkosa Ricardo Vaz Te alieteguka bega huku Winston Reid, mgongo, na Guy Demel, paja, wakingonja kupasishwa kuwa fiti. Gaston Ramirez na Frazer Richardson ni majeruhi na hawataichezea Southampton.
Refa: N Swarbrick
Norwich v Arsenal
Uwanja: Carrow Road Saa: 1 na Nusu Usiku
Norwich wako poa lakini Arsenal watawakosa Laurent Koscielny, mgongo, Kieran Gibbs, paja, na Theo Walcott, kifua. Jack Wilshere na Emmanuel Frimpong huenda wakawemo Kikosini baada ya kupona maumivu ya muda mrefu.
Refa: L Probert
JUMAPILI Oktoba 21
Sunderland v Newcastle
Uwanja: Staium of Light Saa: 9 na Nusu Mchana
Sunderland watamkosa Titus Bramble, maumivu ya paja na Lee Cattermole ambae amefungiwa. Hawana matatizo baada ya kupona Fabricio Coloccini na Steven Taylor.
Refa: M Atkinson
QPR v Everton
Uwanja: Loftus Road Saa: 12 Jioni
QPR wana wasiwasi na Armand Traoré na Fabio bado majeruhi lakini Samba Diakité amepona. Everton watacheza bila ya Marouane Fellaini alieumia goti.
Refa: J Moss

Kiongozi FIFA ataka ‘Wabaguzi’ Serbia wafungiwe, Terry bado Kepteni Chelsea, Shabiki amtwanga Kipa Uwanjani!

FREDINAND-TERRY_MKNO_HAMNAKufuatia vitendo vya Mashabiki wa Serbia vilivyokithiri vya Ubaguzi, Kiongozi wa juu wa FIFA ameitaka Nchi hiyo ifungiwe na huko Stamford Bridge, Chelsea imetamka John Terry atabaki kuwa Kepteni licha ya kusulubiwa kwa Ubaguzi wakati huko Uwanja wa Hillsborough Shabiki mmoja alivamia Uwanjani na kumpiga Kipa hadi akamwangusha chini.
UBAGUZI Serbia v England:  Makamu Rais FIFA, Jim Boyce, aitaka Serbia ifungiwe!
Makamu wa Rais wa FIFA, Jim Boyce, ameitaka UEFA ifikirie kuifungia Serbia katika Mashindano yajayo kufuatia tuhuma za Ubaguzi wa Washabiki wao zilizotokea kwenye Mechi ya kuwania kuingia Fainali za EURO 2013 kwa Vijana wa Chini ya Miaka 21 iliyochezwa huko Nchini Serbia Jumanne iliyopita na England kufuzu kwenda Fainali baada ya kushinda Mechi zote mbili kwa bao 1-0 kila moja.
Tayari UEFA imeshaifungulia Serbia Mashitaka ya Ubaguzi na pia kushindwa kudhibiti Wachezaji wake kosa ambalo pia FA ya England imeshitakiwa.
Kuhusu shutuma za Ubaguzi, Jim Boyce, ametamka: “Lazima hatua kali zichukuliwe dhidi ya FA ya Serbia! Wafungiwe Viwanja vyao na pia uangaliwe uwezekano wa kutowashirikisha Mashindano yajayo.”
Boyce pia alidai vitendo vya Ubaguzi vya Serbia si mara ya kwanza na inabidi hatua kali zichukuliwe kuvikomesha.

Terry abakishwa Kepteni Chelsea
Licha ya kusulubiwa kwa Ubaguzi na FA pamoja na Klabu yake mwenyewe, Nahodha wa Chelsea, John Terry, ataendelea kubaki kama Kepteni wa Timu hiyo kufuatia uamuzi huo kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Bruce Buck.
Terry amefungiwa na FA Mechi 4 na pia kupigwa Faini Pauni 220,000 na pia Chelsea imethibitisha kumpiga ‘Faini kubwa.’ kwa kosa la kumkashifu Kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand kwenye Mechi iliyochezwa Loftus Road hapo Oktoba 23, 2011.

Kipa Chris Kirkland apigwa Uwanjani na Shabiki wa Leeds!
Kipa wa Sheffield Wednesday Chris Kirkland hapo jana alivamiwa Uwanjani wakati wa Mechi ya Timu yake na Leeds United na kushambuliwa na Shabiki wa Leeds kwa nguvu kubwa na kumfanya aanguke chini na kuhitaji matibabu.
Hata hivyo, Kipa huyo wa zamani wa Liverpool mwenye Miaka 31, na ambae pia aliwahi kuichezea England Mechi moja, aliweza kuendelea na kumaliza Mechi hiyo iliyokwisha matokeo yakiwa 1-1.
Akiongelea tukio hilo, Meneja wa Sheffield Wednesday, Dave Jones, alisema: “Hawa ni kama Wanyama. Wapigwe marufuku kwenye Viwanja vyote vya ugenini ikiwa tabia yao ni hii!”
Kwenye Mechi hiyo waliyocheza ugenini, Leeds ilikuwa na Mashabiki 5,300 kati 28,582 waliokuwepo Uwanjani.
Mara baada ya Mechi hiyo Klabu ya Leeds iliomba radhi kwa tukio hilo na kusema itashirikiana na Polisi ili kumtambua Shabiki huyo.

BPL: Chelsea yaidunda Spurs wazidi kupaa kileleni!

BPL_LOGOChelsea leo wamepata ushindi wao wa kwanza Uwanja wa White Hart Lane tangu Mwaka 2005 walipoibonda Tottenham mabao 4-2 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyoanza mapema na ushindi huo umewafanya Chelsea waendelee kuongoza Ligi wakiwa na Pointi 22 kwa Mechi 8.
Chelsea ndio walitangulia kufunga bao katika Dakika ya 17 mfungaji akiwa Gary Cahill na bao hilo kudumu hadi mapumziko.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Tottenham 2= Gallas 47′ Defoe 54′ .
Chelsea 4= Cahill 17′ Mata 66′, 69′ Sturridge 90′
+++++++++++++++++++++++++++++++
Kipindi cha Pili, Spurs walizinduka na kufunga bao mbili kupitia William Gallas na Jermain Defoe.
Hata hivyo, Chelsea waliendelea kutawala na Juan Mata akasawazisha na kupiga bao jingine na kuwafanya waongoze kwa bao 3-2 kabla Mchezaji alietoka benchi Daniel Sturridge kupiga bao la 4.
Haya ni matokeo ya kumvunja nguvu Meneja wa Tottenham manager Andre Villas-Boas ambae alikuwa kisimamia Mechi yake ya kwanza dhidi ya Chelsea ambayo ilimfukuza mwanzoni mwa Mwaka huu.
=============================
VIKOSI:
Tottenham: Friedel, Walker, Gallas, Caulker, Vertonghen, Huddlestone, Sandro, Lennon, Sigurdsson, Dempsey, Defoe
Akiba: Lloris, Adebayor, Naughton, Dawson, Falque, Livermore, Townsend.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Cahill, Cole, Ramires, Mikel, Oscar, Hazard, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Lampard, Moses, Sturridge, Azpilicueta, Bertrand.
Refa: Mike Dean (Wirral)
=============================
Fulham - Aston Villa 57' 0 - 0  
Liverpool - Reading 56' 1 - 0  
Man. United - Stoke City 56' 3 - 1  
Swansea - Wigan 57' 0 - 0  
West Bromwich - Man. City 54' 0 - 0  
West Ham - Southampton FC 57' 2 - 0
Fulham - Aston Villa HT 0 - 0  
Liverpool - Reading HT 1 - 0  
Man. United - Stoke City HT 2 - 1  
Swansea - Wigan HT 0 - 0  
West Bromwich - Man. City HT 0 - 0  
West Ham - Southampton FC HT 0 - 0
Tottenham - Chelsea   2 - 4                                                 
Fulham - Aston Villa 34'                                                             0 - 0  
Liverpool - Reading 34' 1 - 0  
Man. United - Stoke City 34' 1 - 1  
Swansea - Wigan 34' 0 - 0  
West Bromwich - Man. City 33' 0 - 0  
West Ham - Southampton FC 34' 0 - 0

SAMATTA, ULIMWENGU KUIBEBA MAZEMBE LEO TUNISIA?

Samatta ataibeba Mazembe leo?

TOUT Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo ina mtihani mgumu mbele ya Esperance ya Tunisia katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mjini Tunis.
 
Hiyo inatokana na Mazembe kulazimishwa sare ya bila kufungana na mabingwa hao wa Afrika, katika mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Stade du TP Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wiki mbili zilizopita.
 
Sare yoyote ya mabao inaweza kuivusha Mazembe hadi fainali, lakini Esperance inapewa nafasi kubwa ya kushinda kwa kuwa itakuwa ikicheza nyumbani.
 
Mchezo huo tayari umekuwa gumzo kubwa, kutokana na upinzani mkubwa baina ya timu hiyo na hasa baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kubadilisha refa wa mechi hiyo siku tatu kabla ya timu hizo kurudiana.
 
CAF imeteua marefa wapya wa kuchezesha mechi hiyo ya leo kufuatia malalamiko yaliyowasilishwa na Mazembe dhidi ya refa Bakary Gassama kutoka Gambia na sasa Badara Diatta wa Senegal ndiye ambaye sasa atachezesha mechi hiyo mjini Tunis.
 
Magazeti nchini Tunisia yamepinga uteuzi wa refa mpya kwa sababu anatoka nchi moja na kocha wa Mazembe, Lamine N’Diaye, ambaye ni Msenegal pia.
 
Mazembe ina washambuliaji hatari wa Kitanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu ambao wote kwa sasa ni tegemeo la timu hiyo.
 
Katika mchezo wa leo, Mazembe itamkosa beki wake tegemeo, Stopila Sunzu aliyepewa kadi ya pili ya njano (nyekundu) dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida kwenye mechi ya kwanza.
 
Awali, Sunzu kaka wa mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu, alionyeshwa kadi ya kwanza ya njano dakika ya kwanza ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 45 za kipindi cha kwanza.
 
Washambuliaji wote wawili wa Kitanzania walicheza mechi hiyo, Mbwana Ally Samatta alicheza hadi dakika 83 alipompisha Sinkala, wakati Thomas Emanuel Ulimwengu alitokea benchi dakika ya 58 kwenda kuchukua nafasi ya D. Kanda.
Nusu Fainali nyingine ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa kesho kati ya mabingwa mara sita Afrika, Al Ahly ya Misri na Sunshine Stars ya Nigeria mjini Cairo. Katika mechi ya kwanza ya iliyopigwa huko Ijebu-Ode kwenye Uwanja wa kimataifa wa Dipo Dina, timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 3-3.
 
Nahodha wa Sunshine, Godfrey Oboabona aliikosa mechi hiyo baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano katika mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Esperance ya Tunisia, wakati Mohamed Aboutrika alikuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi miwili na Ahly.
 
Ahly ilipata bao la kwanza dakika ya 18 kupitia kwa Mohamed Nagy, aliyefumua shuti kutoka nje ya boksi na kumtungua Moses Ocheje, kabla ya Mahdy El Sayed kuifungia bao la pili timu hiyo dakika ya 30, wakati Sunshine ilipata bao la kwanza dakika ya 40, kupitia kwa kiungo Mcameroon, Tamen Medrano aliyemtungua kwa shuti la mbali kipa wa Ahly, Sherif Elkramy.
 
Wenyeji walisawazisha dakika ya 73 kwa mkwaju wa penalti wa Dele Olorundare baada ya Ajani Ibrahim kuangushwa kwenye eneo la hatari na Mohamed Nagy.
Pamoja na hayo, Mashetani Wekundu wa Cairo walipata bao lililoelekea kuwa la ushindi, dakika moja badaaye kupitia kwa kijana mwenye umri wa miaka 25, Nagy ambalo lilikuwa bao lake la pili kwenye mechi hiyo.
 
Beki wa Sunshine, Precious Osasco aliisawazishia timu yake dakika ya 83 kwa shuti la mpira wa adhabu lililomshinda kipa Elkramy.  Nagy alipata nafasi ya kukamilisha hat-trick dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho, lakini kichwa chake kiliupaisha mpira alipokuwa anaunganisha kona. 

SIMBA SC TAYARI WENYEJI TANGA, KAPOMBE, BOBAN, NYOSSO WAACHWA DAR

Simba SC

MABINGWA watetezi, Simba SC tayari wako mjini Tanga tangu jana jioni kwa ajili ya mechi yao ya kesho dhidi ya wenyeji JKT Mgambo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
Simba iliyoanza Ligi Kuu kwa kishindo, ikishinda mechi sita mfululizo, imelazimishwa sare katika mbili mfululizo zilizopita 0-0 na Coastal Union mjini Tanga na 2-2 na Kegara Sugar mjini Dar es Salaam na 
 kesho imepania kumaliza mduduwa sare.
 
Kocha Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick amesema yeye na wachezaji wake wamejifunza jambo baada ya sare ya pili na Kagera Jumatano na sasa wataongeza juhudi zaidi ili kuhakikisha matokeo hayo hayajirudii.
 
Lakini Mgambo nayo, iliyoanza Ligi kizembe, imezinduka na kushinda mechi tatu mfululizo, tena moja ya ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar 2-1 wiki iliyopita kabla ya kushinda 2-0 dhidi ya Toto African mjini Tanga.   
 
Simba imeenda Tanga na wachezaji wake 24, ambao ni makipa; Juma Kaseja Juma, Wilbert Mweta William na Waziri Hamad Mwinyiamani, mabeki Nassor Said Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah Mrisho, Paulo George Ngalema, Koman Bili Keita, Pascal Ochieng Akullo, Hassan Hatibu Kondo.
 
Viungo ni Jonas Mkude Gerrald, Ramadhani Chombo Redondo, Amri Kiemba Athumani, Abdallah Omar Seseme, Ramadhani Singano Yahya, Uhuru Selemani Mwambungu, Mrisho Khalfan Ngassa, Mwinyi Kazimoto Mwetula na Salim Abdallah Kinje na washambuliaji Abdallah Juma, Daniel Akuffo, Felix Mumba Sunzu, Edward Christopher Shija, Haruna Athumani Chanongo na Emmanuel Arnold Okwi.
 
Waliobaki Dar es Salaam ni Haruna Moshi ‘Boban’ anayesumbuliwa na maumivu ya misuli, Haruna Shamte, anayeumwa goti, Kigi Makassy anayeumwa goti pia, Shomari Kapombe anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na Juma Said Nyosso anayetumikia adhabu ya kadi (tatu za njano).
 
Simba bado inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 18, baada ya kucheza mechi nane, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 17, baada ya kucheza mechi saba, wakati Yanga inayocheza mechi ya nane na Ruvu Shooting leo Dar es Salaam ni ya tatu kwa pointi zake 11.   