Thursday, December 27, 2012

YANGA KUPAAA KESHO KUTWA JUMAPILI KWENDA UTURUKI



 YANGA inaondoka Jumapili alfajiri kwenda mjini Antalya, Uturuki kwa kambi ya wiki mbili itakayomalizika Januari 13 bila wachezaji Salum Telela, Shamte Ally, Ibrahim Job, Yaw Berko na Rashid Gumbo waliopelekwa kwa mkopo timu mbalimbali.

Uongozi umethibitisha kwamba kambi itakuwa Antalya ambao ni mji ulioko kilomita 490 kutoka Instanbul yalipo makao makuu ya nchi hiyo yenye baridi kali muda mwingi.

Umbali kutoka Dar es Salaam mpaka Instanbull kwa ndege ni kilomita 5,394.5 ambao ni mwendo wa saa saba kwa ndege.
Lakini kocha wake Ernest Brandts alisema: "Lengo letu ni kutwaa ubingwa kwenye ligi kuu, tupo kileleni hivi sasa tutang'ang'ania hapo hapo."

"Kila kitu katika soka ni nidhamu, iwe ndani ya uwanja au hata nje, mazoezi na hata kwenye mechi. Kama mchezaji hana nidhamu hawezi kuwa bora, ninachoshukuru wachezaji wangu wanafuata kile ambacho mimi ninataka.

"Mimi ni mkali wakati mwingine ninapoona mchezaji anakwenda tofauti nampa adhabu."

Yanga inaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kesho Jumatano itacheza na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

KADI NYEKUNDU GIBSON, COLE ZAFUTWA, FERGIE ANUSURIKA…REDKNAPP, MANCINI….!!!


MANCINI_n_MICAHBosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson hatapata adhabu yeyote toka kwa FA baada ya kumvaa Refa Mike Dean na Wasaidizi wake lakini Mameneja wa Man City, Roberto Mancini, na wa QPR, Harry Redknapp, huenda wakaadhibiwa kwa kauli zao na wakati huo huo Kadi Nyekundu kwa Darron Gibson wa Everton na Carlton Cole wa West Ham zimefutwa.
Chama cha Soka England, FA, kimethibitisha kuwa Sir Alex Ferguson, hatapewa adhabu yeyote kwa kitendo chake cha kabla Kipindi cha Pili kuanza, cha kumvaa Refa Mike Dean na kumlalamikia kisha kumkabili Refa wa Akiba Neil Swarbrick na pia Refa Msaidizi Jake Collin, kwa vile Refa Dean hakuzungumza lolote kuhusu tukio hilo katika Ripoti ya Mechi.
Hata hivyo, Mameneja wa Man City na QPR, Roberto Mancini na Harry Redknapp, wako matatani kufuatia kauli zao baada ya Mechi zao za kulalamika kuhusu Marefa na kudokeza uchezeshaji usio wa haki kitendo ambacho ni kinyume cha Kanuni za FA.
Mancini, Meneja wa Man City, alilalamika kuhusu Refa Kevin Friend baada kufungwa 1-0 na Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Desemba 26 kwa Refa huyo kutopiga Filimbi ya Faulo aliyochezewa Mchezaj wake Pablo Zabaleta na badala yake kuachia mpira uchezwe na kuzaa Goli la Adam Johnson, Winga wa zamani wa Man City, lililowaua City 1-0.
Mancini alidai: “Pengine Refa alivimbiwa na Mlo wa Krismasi! Haiwezekani Waamuzi wawili wasione tukio hilo! [Akimaanisha Refa Na Msaidizi wake]”
Nae Harry Redknapp, Bosi wa QPR, yuko matatani baada ya kuhamaki na maamuzi ya Refa Chris Foy ambayo alidai ni ‘Skandali!’ wakati walipofungwa 2-1 na West Brom na kutupwa mkiani mwa Ligi Kuu England Siku ya Boxing Dei.
Refa Chris Foy alilikubali Goli la kujifunga mwenyewe Kipa Robert Green ambae alionekana akibanwa waziwazi na Mchezaji wa WBA, Marc-Antoine Fortune, na pia aliwayima Penati ya wazi mwishoni baada ya Beki Liam Ridgewell kuunawa mpira.
Redknapp amewaka: "Ile ni Faulo ya wazi kwa Kipa wetu na ile ni Penati ya wazi! Hii ni kashfa!”
Msimamo wa FA kwa Mameneja ni kwamba hawatakiwi kuwalaumu Marefa kuhusu maamuzi yao na wakifanya hivyo wanaandikiwa Barua kutaka maelezo yao na kama hayaridhishi hufunguliwa Mashitaka.
Wakati huo huo, FA imetangaza kuwa Rufaa za Everton na West Ham kupinga Kadi Nyekundu kwa Wachezaji wao, Darron Gibson wa Everton na Carlton Cole, zimekubaliwa na Adhabu za kufungiwa Mechi 3 kila mmoja kwa Wachezaji hao zimefutwa.
Wachezaji hao wote wawili walitolewa katika Mechi moja na Refa Mark Anthony Uwanjani Upton Park Wikiendi iliyopita ambako Everton walishinda 2-1 baada ya kutoka nyuma kwa kwa Bao la Carlton Cole na kutolewa kwa Mfungaji huyo kuliwapa mteremko kusawazisha na kushinda huku Mchezaji wao Gibson akitolewa Dakika za majeruhi.
Wachezaji hao wote wawili sasa wako huru kuziwakilisha Klabu zao Mechi za Ligi Wikiendi hii

PIA HII NAYO STAISAHAU KWANI ILIKUWA MBAYA SANA HUKO ZANZIBAR

KATIKA MWAKA 2012 TANOJUMAINSPORTS INAKULETEA PIA AJALI HII ILIYOHEAD LINE SANA TANZANIA NA ULIMWENGUNI YA AJALI YA MV.SKAGIT R.I.P MAREHEMU WOTE ISHALAAAAAAH

MARWA NA KIRWA KUCHEZESHA KOMBE LA MATAIFA KULE AFRIKA KUSINI,HAWA KUTOKA KENYA LAKINI TANZANIA NA UGANDA HALI TETE HATA WA KUFUTIA MACHOZI HAKUNA

Marwa Waamuzi wawili wakubwa nchini Kenya wamechaguliwa kwenda nchini Afrika ya Kusini kwenda kuamua mechi ya Africa Cup of Nations (Afcon) zitakazoanza mwezi ujao huko kusini mwa bara la afrika. 

Aden Marwa, ambaye ni mwalimu kutoka Nyanza kusini, amechaguliwa pamoja na refa mwingine Sylvester Kirwa, kutoka Eldoret. 

Wawili hao wamechaguliwa kuamua mechi za michuano hiyo baada ya kushiriki katika kozi ya CAF ya marefa iliyofanyika huko Egypt mapema mwezi uliopita.

Marefa hao wa pekee kutoka ukanda huu wa Afrika mashariki wataenda South Africa siku ya jumanne tarehe 15, siku nne kabla ya michuano kuanza.

Marwa – ambaye alishiriki katika 2012 AFCON, zilizofanyika nchini  Gabon na Equatorial Guinea – amesema kuchaguliwa kwao kwenda AFCON ni ishara nzuri kwa soka la Kenya.
bafana pitso mosimane sylvester kirwa kenya 
Sylvester Kirwa

KOCHA MPYA SIMBA KUKISHUHUDIA KIKOSI CHAKE KIKIIVAA TUSKER FC JUMAMOSI



KOCHA mpya wa Simba Mfaransa Patrick Liewang anatarajia kukishuhudia kikosi ya timu hiyo jumamosi ya keshokutwa kitakapokwaana na mabingwa wa soka wa Kenya, Tusker Fc.
Mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki unatarajiwa kupigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam ambapo pia Simba itautumia kutambulisha nyota wake wapya iliyowasijili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa.
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema leo kwamba, kocha huyo ambaye alikuwa awasili nchini leo imeshindikana baada ya kukosa nafasi kwenye ndege, hali itakayomfanya asubiri mpka jumamosi.
Alisema kocha huyo ambaye anakuja kurithi mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic, atakishuhudia kikosi cha Simba kikicheza mechi hiyo kabla ya kuendelea na taratibu nyingine ikiwemo kusaini mkataba wa kazi na baadaye kuanza kutumikia kibarua chake kipya.
Naye mratibu wa mchezo huo, George Wakuganda alisema kwamba maandalizi ya mchezo huo yamekamilika ambapo viingilio ni sh 15,000, 10,000, 7,000 na 5,000.
Tusker Fc jana ilikwaana na Yanga na kuitandika bao 1-0 mchezo ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa.

NYOTA 27 YANGA SC KUKWEA PIPA LA UTURUKI USIKU WA JUMAMOSI



KIKOSI cha wachezaji 27 wa Yanga Sc kinatarajiwa kuondoka nchini usiku wa jumamosi kuelekea nchini uturuki kwa ajili ya kuweka kambi maalum ya kujiandaa na mashindano mbalimbali.
Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Yanga, Abdallah Binkleb ameiambia Sports Lady  maandalizi ya safari hiyo yamekamilika na kwamba wachezaji watakaokwenda huko pamoja na viongozi watajulikana kesho.
Amesema kwamba kambi hiyo itakisaidia sana kikosi katika maandalizi yake ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom pamoja na michuano ya Kagame itakayofanyika Kigali, Rwanda ambapo Yanga ni bingwa tetezi.
"Ndo maana tumetaka kwenda Uturuki kwani huko kuna facilities nzuri kwa ajili ya kambi...pia huko tunataraji kiucheza mechi kadhaa za kirafiki,"amesema.

Yanga inayonolewa na Ernie Brandts jana ilichapwa bao 1-0 na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker Fc katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

MAPINDUZI CUP :AL AHLY YAJITOA ,RAGE TUNAWACHEZAJI 36 ,YANGA HATUTASHIRIKI LABDA KIKOSI CHA PILI



Katika hari isiyotarajiwa klabu kubwa nchini simba na yanga zinaonekana kuitolea nje michuano ya mapinduzi cup inayotarajia kuanza mwezi january mwakani huku timu zote zikititoa sababu binafsi Mabingwa tanzania simba ambao wanasafari ya kwenda muscat Mwezi january wameshasema Kupitia Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage  kuwa timu yao ina wachezaji 36 hiii inamaana kuwa kuna uwezekano mkubwa wapereka kikosi cha pili.

huko zanzibari kwani wanasafari ya kwenda oman kujiandaa na mzunguko wa pili ligi ya primia Tanzania Bara 

Yanga kupitia katibu mkuu wake Mwalusako imesema haita shiriki huku sababu kubwa ikiwa kama ya simba kwenda uturuki kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi huku akisistiza kuwa labda wapereke kikosi cha pili

mwenyekiti wa kamati inayosimamia mashindano hayo said Khamis Abdallah amesema kuwa watatoa jibu kesho kama timu hizo zitashiriki au hazitoshiriki huku Tusker ya kenya ikisibithia kushiriki wakati Al ahly ya Masir imetangaza kujitoa kutokana na sababu sizizo weza kuzuirika  Timu pekee zilizo thibithisha kushiri kutoka bara ni Azam na coast union ambapo michuno hiyo inataraji  kuanza tarehe pili january  .

aidha michuano itachezwa unguja pekee tofauti na ilivyopangwa awali kuwa ingechezwa na pemba .

Mwaka yanga ilifukuzwa katika mashindano ya super8 kwa kupereka kikosi cha pili na kamati hiyo hiyo sababau kubwa ikiambiwa imedharau mashindano 

MAKUNDI:
KUNDI A:
Simba (Dar-es-Salaam),
Tusker (Kenya)
Bandari (Unguja)
Jamhuri (Pemba).
KUNDI B:
Azam FC (Dar-es-Salaam)
Mtibwa Sugar (Morogoro)
Coastal Union (Tanga)
Miembeni (Unguja).

FERGIE KULIKWAA RUNGU LA FA? MANCINI AKIRI MATATIZO!!


>>REDKNAPP AMLAUMU REFA KWA KURUDISHWA MKIANI!!
>>BENITEZ ASEMA 1-0 NI MUHIMU KAMA 8-0!!
FERGIE_KAZINIMENEJA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anasubiri nini kitamkuta endapo Refa Mike Dean atamtaja kwenye Ripoti yake ya Mechi ya jana ambayo Man United waliifunga Newcastle Bao 4-3 baada ya kumkabili Refa huyo na Wasaidizi wake kabla Kipindi cha Pili kuanza akilalamikia Bao la pili la Newcastle.


Ferguson alikuwa amekasirishwa na Refa Mike Dean kufuta Ofsaidi iliyotolewa ishara na Msaidizi wake Jake Collin na kuamua ni Bao kwa vile Jonny Evans alijifunga mwenyewe.
Wakati Kipindi cha Pili kinataka kuanza, Ferguson alimvaa Refa Mike Dean na kumlalamikia kisha akamvaa Refa wa Akiba Neil Swarbrick na pia Refa Msaidizi Jake Collin.


Ikiwa tukio litatajwa kwenye Ripoti ya Mechi ya Refa Mike Dean basi huenda Sir Alex Ferguson akaadhibiwa FA lakini kwa vile Refa Dean hakumchukulia hatua yeyote Ferguson huenda akakwepa adhabu.
Akielezea tukio hilo Ferguson alisema: “Refa alimfanya Mshika Kibendera abadilishe uamuzi wake wa Ofsaidi. Alisema ni Goli la kujifunga mwenyewe lakini ukilirudia Goli lile, yule Mchezaji wa Newcastle alikuwa Ofsaidi na tena alimvuta mkono Evans! Sasa hilo kama si kuingilia uchezaji ni nini? Ni uamuzi mbovu!”



ROBERTO MANCINI AKIRI MATATIZO MANCHESTER CITY!!

Roberto Mancini 008.jpg 
Roberto Mancini amekiri kuwa ana matatizo makubwa mara baada ya jana kuchapwa 1-0 na Sunderland.

Mancini amesema: “Tatizo kubwa Mastraika hawafungi nafasi wanazopata!”
Sasa ni mara ya 3 mfululizo kwa Man City kufungwa Stadium of Light na Sunderland ambao jana Bao lao pekee lilifungwa na Winga wa zamani wa Man City, Adam Johnson.

Msimu huu, Man City wamefunga Bao 34 katika Mechi 19 za Ligi Kuu England ikiwa ni Magoli 14 nyuma ya vinara Man United.
Lakini, ingawa Man City sasa wako Pointi 7 nyuma ya Man United, Roberto Mancini amesema wao bado wana nafasi ya kutetea Taji lao.
Ametamka: “Man United wanafunga Bao nyingi kupita sisi lakini pia wanafungwa Bao nyingi kupita sisi! Msimu ni mrefu na ni juu yetu kubadilika!”


HARRY REDKNAPP CRITICISES REFEREE AFTER QPR'S LOSS TO WEST BROM

 Bosi wa Queens Park Rangers Harry Redknapp amekasirishwa na maamuzi ya Refa Chris Foy ambayo amedai ni ‘Skandali!’ wakati jana walipofungwa 2-1 na West Brom na kuwatupa mkiani mwa Ligi Kuu England.


Refa Chris Foy alilikubali Goli la kujifunga mwenyewe Kipa Robert Green ambae alionekana akibanwa waziwazi na Mchezaji wa WBA, Marc-Antoine Fortune, na pia aliwayima Penati ya wazi mwishoni baada ya Beki Liam Ridgewell kuunawa mpira.

Redknapp amewaka: "Ile ni Faulo ya wazi kwa Kipa wetu na ile ni Penati ya wazi! Hii ni kashfa!”


BENITEZ ASEMA 1-0 NI MUHIMU KAMA 8-0!!

Chelsea’s new interim 1st team manager Rafa Benitez during his 1st training session
Bosi wa Chelsea Rafael Benitez anaamini ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Norwich hapo jana ni muhimu kama kile kipondo cha 8-0 walichowashushia Aston Villa Siku 3 zilizopita.
Ingawa Wadau wengi wa Klabu hiyo watahisi kimchezo ushindi wa 1-0 ni tofauti na ule wa 8-0, Benitez ametetea matokeo hayo kwa kusema: “Ni muhimu kuiona Timu ikicheza kwa bidii na kujilinda kisawasawa! Muhimu ni kuwa hatukufungwa Bao.”
Chelsea sasa wako nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 tu nyuma ya Man City na Mechi moja mkononi.
+++++++++++++++++++++++
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

SIKU YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU HUSSEIN RAMADHANI ALI MAARUFU SHARO MILLIONEA SITAISAHAU HII KWANI KAACHA PENGO SANA MWAKA HUU WA 2012

HAKIKA TANZANIA TUMEPOTEZA NGUVU KAZI KATIKA TASNIA YA MUZIKI ===MWAKA 2012 SITAWASAHAU HAWA KATIKA MATUKIO YALIYOTOKEA YA KUSIKITISHA

BRUNO GOMES MBRAZIL ANAYEKUJA OLD TRAFFORD MWAKANI - AIPA UBINGWA TIMU YAKE - ACHUKUA KIATU CHA DHAHABU

Mchezaji aliyesajiliwa na Manchester United kutoka Brazil Bruno Gomes ameiongoza klabu yake ya Desportivo Brasil kutwaa ubingwa nchini hiyo wa vijana wenye miaka U17. 

Gomes, 16, atajiunga na United kipindi kijacho kiangazi, alifunga hat trick katika fainali ya pili ya kugombea ubingwa huo dhidi  Marília, na mwishowe Desportivo wakashinda 6-0

Mshambuliaji huyo hatari, tayari amekuwa chaguo muhimu katika kikosi cha Brazil cha vijana chini ya umri wa miaka 17, amefunga mabao 27 katika mechi 32 na kubeba kiatu cha dhahabu.

United wana mahusiano rasmi na klabu ya Desportivo Brasil, ambao wachezaji wao wamefunga mabao 88 katika mechi 32 msimu huu.

Inaeleweka kwamba pamoja na Gomes, United wapo katika mazungumzo ya kumsajili winga wa Desportivo aitwaye Welder.
Desportivo pia walishinda ubingwa Milk Cup huko Northern Ireland mwaka huu.

ASILIMIA 82 YA MASHABIKI WA MADRID WANATAKA MOURINHO ATIMULIWE KAZI REAL MADRID

Mashabiki wa Real Madrid wameamua. Wanataka Mourinho aondoke Bernabeu.

Kufuatia kupigwa benchi kwa Casillas katika mechi dhidi ya Malagamtandao wa gazeti maarufu nchini Hispania MARCA.com uliuliza "Je inabidi Real Madrid imtimue Mourinho?" na majibu ya takribani wasomaji 100,000 yalikuja yakisema ndio kwa asilimia  82.4%.

Kwa mujibu wa MARCA, mapenzi baina ya washabiki wa Los Blancos na Mourinho yamekwisha kabisa. Madrid wamekuwa na mfululizo wa matokeo mabaya katika kipindi cha hivi karibuni na kusababisha maneno mengi juu ya mustakabli wa kocha Jose Mourinho ndani ya klabu hiyo.

Real Madrid wapo nyuma kwa 16 dhidi ya viongozi wa La Liga Barcelona, na tayari Mourinho ameshasema kwamba ubingwa wa La liga msimu huu hawawezi kushinda tena, na inasemekana kwamba ikiwa atashindwa kuiongoza klabu hiyo kushinda ubingwa wa 10 wa mabingwa wa ulaya basi Mreno huyo atatemeshwa kibarua chake mwishoni mwa msimu.

MENEJA WA LIVERPOOL BRENDAN RODGERS AKUBALIANA NA MATOKEO YA JANA DHIDI YA STOKE CITY


 Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza kuwa hawakuwa na la kujivunia katika mchezo ambao walipoteza kwa kuchapwa mabao 3-1 na Stoke City iliyocheza vema hapo jana kule katika dimba la Britannia jioni ya jana.

Wekundu hao walipata bao la mapema kupitia kwa nahodha Steven Gerrard kwa njia ya penati baada ya Luis Suarez kuangushwa katika eneo la hatari na Ryan Shawcross. 

Hata hivyo Stoke wakafanikiwa kusawazisha na baadaye kuandika bao la pili la uongozi kupitia kwa Jonathan Walters na kisha bao la kichwa la Kenwyne Jones.

Brendan Rodgers amekiri kikosi chake kuvurunda katika mchezo huo lakini pia akionekana kuhuzunishwa na aina ya magoli yaliyokuwa yakifungwa na kusema timu yake inapaswa kujifunza namna ya kulinda kama inataka kupata alama katika michezo ya ugenini.

“ulikuwa ni mwanzo mzuri kwetu kwa kupata goli la mapema kupitia njia ya penati, lakini tulishindwa kujilinda nadhani magoli yote matatu na makosa ya ulinzi, kiukweli hatukustahili chochote katika mchezo huu”

TIMU YA BLACKBURN ROVERS YAMTIMUA KOCHA WAKE HENNING BERG NA MAAFISA WATATU WA TIMU HIYO

 Blackburn Rovers imemfukuza kazi meneja wake Henning Berg na maafisa wengine watatu katika safu ya makocha ikiwa ni hatua ambayo imefuatia klabu hiyo kutereza katika vibaya katika msimamo wa ligi ndogo ya nchini England, Championship.

Meneja huyo raia wa Norway, ambaye aliajiriwa mwezi  October, katika jumla ya michezo 10 amefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu katika kipindi chake cha utumishi wake wa siku 57.

Berg, ambaye alikuwa mchezaji wa Rovers mwaka 1995 wakati huo Rovers ilishinda taji la ligi kuu ya England “Premier League”  na baadaye akishinda taji la “League Cup” akiwa nahodha wa kikosi mwaka 2002, alirejeshwa katika klabu hiyo kama meneja mwezi Oktoba.

Baada ya Blackburn kuanza kwa kusuasua chini ya meneja wake wa zamani Lyn Oslo na Lillestrom klabu hiyo ikaamua kumpa Berg jukumu la kukinoa kikosi hicho katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Middlesbrough jana Boxing Day kilipelekea Rovers kujikuta katika nafasi ya 17 ikifanikiwa kukusanya alama 7 ndani ya uwezo wake wa kukusanya alama 30 kama wangeshinda michezo yote chini ya meneja Henning Berg.

Meneja msaidizi, Eric Black, kocha wa namba moja Iain Brunskill kocha wa makipa Bobby Mimms nap wamekumbwa na dhahma hiyo ya kufukuzwa kazi pamoja na Berg kutoka katika viunga vya Ewood Park.

GARETH BALE AFURAHIA HAT TRICK YAKE YA KWANZA BPL

Winga wa Tottenham Gareth Bale amefurahia kufanikiwa kufunga mabao matatu ya kwanza katika mchezo mmoja ‘Hat trick’ katika ligi kuu ya soka ya England ‘Premier League’ lakini anasema kikubwa ulikuwa ni ushindi ambao uliipatia alama tatu muhimu Spurs baada ya kuichapa Aston Villa mabao 4-0 hapo jana.

Jermain Defoe alifunga goli la kwanza kwa Spurs kunako dakika ya 58 kabla ya Bale kufunga magoli mengine matatu yaliyowapa uhakika wa ushindi katika mchezo huo.

Vijana hao wanaotoka London ya Kaskazini waliingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya sare ya bila kufungana dhidi ya Stoke, ambapo walikuwa wakijua wazi kwamba muhimu kwao ulikuwa ni ushindi ili kuendelea kuleta ushindani katika nafasi ya juu katika msimamo wa ligi.

Akinukuliwa kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter  wa klabu yake, Bale amesema,

 "vizuri kufunga magoli na kupata ‘hat trick’ yangu ya kwanza katika ‘Premier League’ lakini muhimu ni kupata alama 3".

"wachezaji wote walifanya kazi nzuri, sasa tunajipanga kwa ajili ya mchezo na Sunderland"

Kwa upande wake meneja Andre Villas-Boas amepongeza vijana wake walivyokuwa uwanjani tangu kuanza kwa mchezo mpaka mwisho

NEW CASTLE KUKUMBANA NA RUNGU LA FIFA


  Newcastle na Millwall huenda wakakumbana na adhabu ya shirikisho la soka duniani FIFA kufuatia vilabu hivyo kugomea kuwaachia wachezaji wa kimataifa wa Nigeria  Shola Ameobi na Danny Shittu kwa ajili ya kulitumikia taifa lao katika michuano ya fainali za mataifa ya Afrika nchini Afrika Kusini mwezi Januari

Bosi wa Newcastle Alan Pardew anasema mshambuliaji wake Shola Ameobi hatasafiri kuelekea Afrika katika fainali hizo.

Ameobi na Shittu wote wanatarajiwa kujitoa rasmi katika uteuzi wao katika timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles), jambo ambalo limeonekana kulikasirisha shirikisho la soka la nchi hiyo (NFF).

Meneja wa Newcastle Alan Pardew amesema Ameobi hatatokezea katika michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuanza January 19, wakati ambapo mlinzi wa Millwall er Shittu naye anatarajiwa kutolea nje uteuzi wake kama ilivyo kwa Ameobi.

Sheria za FIFA zinasema mchezaji yoyote ambaye atashindwa kuripoti katika timu yake ya taifa baada ya kutajwa na nchi yake kwa ajili ya majukumu ya kimataifa , basi mchezaji huyo atakuwa si halali kutumika katika kipindi chote kilichopendekezwa wakati wa jukumu hilo pamoja na kuongezewa siku tano zaidi kama itawezekana vinginevyo kuwepo na makubaliano mengine kati ya klabu yake na nchi husika.

Mjumbe wa bodi ya shirikisho la soka la Nigeria Chris Green amesema watahakikisha klabu za wachezaji hao zinaadhibiwa kama watagomea kuwaachia wachezaji hao.

SIMBA SC YAPANGWA NA TUSKER FC YA KENYA MAPINDUZI CUP


Simba SC
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba SC wamepangwa kundi moja, A na Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Aidha, katika Kundi B, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara, Azam FC ya Dar e Salaam pia, imepangwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union  ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Kamati Maalum ya Kusimamaia michuano hiyo, inaonesha kuwa katika mchezo wa kwanza utakaochezwa siku ya ufunguzi itakuwa ni kati ya Bandari kutoka Unguja ambayo itacheza na Jamhuri kutoka kisiwani Pemba ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika, pamabano litakalochezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja, huku usiku wa siku hiyo hiyo katika Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja pambano la ufunguzi rasmi katika mashindano hayo likiwakutanisha mabingwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC ambao watapambana na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo jumla ya timu nane zitashiriki katika mashindano hayo ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa visiwani hapa, timu hizo zimegawanya katika makundi mawili ambayo ni kama ifuatavyo:
Awali michuano hiyo ilitarajiwa kuanza kisiwani Pemba tarehe 1 Januari, lakini kutokana na kujitoa katika mashindano kwa klabu ya Al-Ahly ya Misri kutokana na klie kilichoelezwa sababu za kiusalama, mechi zote sasa zitachezwa kisiwani Unguja na ufunguzi ukipangwa kuanza tarehe 2 badala ya tarehe 1 januari.
Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na zawadi ya kombe na fedha taslim Tsh. Milioni kumi (10,000,000), mshindi wa pili Milioni tano (5,000,000), pamoja na zawadi nyengine ambazo zimegawanywa katika makundi tofauti ikiwemo zawadi ya mfungaji bora, mchezaji bora, mwamuzi bora, kipa bora, mwandishi wa habari bora, timu bora na zawadi nyeanginezo.
Kupitia matandao wako makini wa http://bongostaz.blogspot.com/ tutakuwa ukiwaletea kila kitakachoendelea katika mashindano hayo kuanzia mwanzo mpaka mwisho

RIDHIWANI KIKWETE MGENI RASMI MKUTANO MKUU TASWA

 

Ridhiwani, mtu wa watu
MAANDALIZI ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) yanaenda vizuri na wajumbe wanatarajiwa kufika Bagamoyo kesho (Desemba 28, 2012) mchana kwenye hoteli ya Kiromo View Resort watakapolala na kufanyia mkutano.
Ijumaa hiyo washiriki watatembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria Bagamoyo na jioni kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya timu ya soka ya TASWA FC na Bagamoyo Veterani itakayofanyika Uwanja wa Mwanakalenge na usiku wajumbe watakuwa na chakula cha pamoja na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali yahusiyo michezo na taaluma ya habari.
Mkutano Mkuu utafunguliwa Jumamosi Desemba 29, saa tatu asubuhi na mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia timu za Taifa za Vijana, Ridhiwani Kikwete.TASWA imechukua jukumu la kumualika kutokana na kuwa mdau mkubwa na rafiki wa chama chetu.
Mkutano utafungwa jioni ya siku hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene ambaye hiyo pia itakuwa nafasi nzuri kwake kuweza kuzungumza na wana habari kuhusiana na masuala mbalimbali ya kitaaluma.
Katika mkutano huo wanachama wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama, Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu waandishi wa habari za michezo na maendeleo ya michezo kwa ujumla
Pia kutakuwa na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo, ili wawe na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo nayo itajadiliwa kwenye mkutano huo.
Kamati ya Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea kwa kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza iwaite wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na kukishakuwa na uelewa wa kutosha suala hilo litakuwa kama ajenda kamili ya kuanzisha chama hicho kwenye mkutano wetu.
(Mwandishi wa habari hizi ni Katibu Mkuu wa TASWA)

VIBONDE WA CHELSEA ASTON VILLA JANA WALIBONDWA KWA MARA YA PILI MFULULIZON MABAO MENGI NA TIMU YA AVB TOTTENHAM 4-0

MABINGWA WATETEZI WA BPL JANA KILIWAKUTA HIKI EBU KICHEKI KUTOKA KWA SUNDERLAND

MAN U WATAALAMU WA KUTOKA NYUMA NA KUJA KUSHINDA ANGALIA HII YOU TUBE MECHI YA JANA WALITOKA NYUMA WAKASHINDA 4-3 DHIDI YA NEWCASTLE

GOAL LA JUAN MATTA JANA LILILOWAWEZESHA CHELSEA KUSHIKILIA NAFASI YA TATU

BAADA YA JANA KLUISAIDIA TIMU YAKE YA MAN U ROONEY ANATARAJIA KUKAA NJE WIKI MBILI.


MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney anatarajiwa kukaa nje ya uwanja wa kipindi cha wiki mbili hadi nne baada ya kuumia mguu wakati wa mazoezi ya timu hiyo kabla ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Newcastle United. Rooney hakuwemo katika kikosi kilichoanza katika mchezo ambao walishinda mabao 4-3 dhidi ya Newcastle katika Uwanja wa old Trafford na meneja wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson amesema kuwa mshambuliaji huyo atakosa michezo yote kwa mwaka huu. Kocha huyo aliiambia tovuti ya klabu hiyo kuwa nyota huyo aliumia dakika za mwisho mazoezini wakati akijaribu kuruka juu ndipo alipojiumiza kifundo cha mguu wake wa kulia. United inakabiliwa na mchezo dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi kabla ya kusafiri kufuata Wigan Athletic Januari Mosi ambapo wanajipanga kujizatiti kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

BAADA YA JANA KUFUNGWA BAO 1-O MANCINI ALIA NA MWAMUZI ASEMA HAKUWA FITI - NA FAIR PLAY


MENEJA wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini ameponda kiwango alichochezesha mwamuzi Kevin Friend katika mchezo dhidi ya Sunderland ambao umepelekea kufungwa bao 1-0 jana. Winga wa zamani wa City Adam Johnson ndiye aliyeipatia Sunderland bao la ushindi katika mchezo huo lakini Mancini anaamini kuwa kabla ya bao hilo kufungwa Pablo Zabaleta alitakiwa apewe mpira wa adhabu baada ya kuchezewa vibaya na Graig Gardner. Mancini amedai kuwa labda mwamuzi pamoja na mshika kibendera wake pengine walikula chakula kingi wakati wa sikukuu ya Noel ndio maana hawakuwa katika kiwango bora wakati wakichezesha mchezo huo. Kipindi hicho kimeifanya City kubakia nyuma mbele ya vinara wa ligi hiyo Manchester United kwa alama saba na Mancini anamlaumu mwamuzi kwa kipigo hicho ambacho ni cha kwa klabu hiyo msimu huu.

FOMENKO KOCHA MPYA UKRAINE.


SHIRIKISHO la Soka nchini Ukraine-FFU limemtaja kocha Mikhail Fomenko kama kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo. Nafasi hiyo ambayo iliachwa wazi toka Septemba mwaka huu baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Oleg Blokhin kuondoka na kwenda kuifundisha klabu ya Dynamo Kiev baada ya michuano ya Ulaya kumalizika. Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester Ciy, Sven-Goran Eriksson ndio alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa kocha wan chi hiyo lakini mwishoni Fomenko ndio amethibitishwa kuchukua nafasi hiyo. Fomenko aliwashukuru maofisa FFU kwa kumwamini kumpa kibarua hicho na kwamba anatambua jukumu lake na changamoto zinazoikabili timu ya taifa ya nchi hiyo ambapo kazi yake ya kwanza itakuwa ni kuhakikisha wanafuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspurs aliwahi kukiri kuitaka nafasi hiyo kabla ya kukubali kuinoa Queens Park Rangers wakati mshambuliaji nyota wa zamani wa nchi hiyo Andriy Shevchenko alikataa nafasi ya kuifundisha nchi yake.

ODIMWINGIE AMALIZIA HASIRA ZAKE KWA IKPEBA

.

Ikpeba
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya West Bromwich Albion, Peter Odemwingie kwa mara nyingine tena ametumia mtandao wa kijamii wa twitter kuonyesha hasira zake kufuatiwa kutemwa katika kikosi cha wachezaji 32 wa nchi hiyo kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2013. Odemwingie alitumia mtandao huo kuwashambulia kocha wa Nigeria Stephen Keshi maofisa wa Shirikisho la Soka nchini Nigeria-NFF na mchezaji bora wa zamani wa Afrika Victor Ikpeba. Ikpeba alimtupia madongo Odimwingie katika kipindi cha Monday Night Football kinachorushwa hewani na Supersport akidai kuwa nyota huyo hajafikia mafanikio aliyofikia yeye Ikpeba. Odimwingie alijibu dongo hilo katika mtandao wa kijamii kwa kumponda Ikpeba na kudai kuwa alikuwa sehemu ya kikosi cha Nigeria ambacho kilishindwa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika iliyofanyika mapema mwaka huu nchini Gabon na Equatorial Guinea.

AFCON 2013: ZAMBIA, ANGOLA ZAWA TIMU ZA KWANZA KUWASILI AFRIKA KUSINI.


Timu za taifa za Angola na mabingwa wa Afrika Zambia zimekuwa za kwanza kuwasili nchini Afrika Kusini kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika ambapo zimebaki wiki tatu kabla ya kuanza. Timu zote mbili zimefikia jijini Johannesburg na zitabakia hapo katika kipindi chote watakachokuwa wakifanya maandalizi yao kabla ya kuanza michuano hiyo Januari 19, 2013. Angola imesafiri na wachezaji wake wote 20 ambao wanacheza katika ligi ya nyumbani huku waliopo Ulaya wakitegemewa kuungana na wenzao wiki mbili kabla ya michuano hiyo. Shirikisho la Soka nchini Angola limedai kuwa wakiwa nchini humo wanatarajia kucheza michezo kadhaa ya kirafiki dhidi ya timu za Msumbiji, Tanzania na Zambia wakiwa hapohapo jijini Johannesburg lakini bado wako katika mazungumzo juu ya tarehe za kuchezwa mechi hizo. Algeria na Morocco zinatarajiwa kuwa timu zitakazofuata kuwasili nchini humo kwa ajili ya michuano hiyo siku baada ya kuanza mwaka mpya.

BPL: STOKE WAICHARAZA LIVERPOOL, SPURS YAINYUKA VILLA!

BPL_LOGO>>SPURS YAKAMATA NAFASI YA 4, LIVERPOOL NI 10!!
+++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumatano 26 Desemba 2012
Everton 2 Wigan 1
Fulham 1 Southampton 1
Man United 4 Newcastle 3
Norwich 0 Chelsea 1
QPR 1 West Brom 2
Reading 0 Swansea 0
Sunderland 1 Man City 2
Aston Villa 4 Tottenham 0
Stoke 3 Liverpool 1
+++++++++++++++++++++++
STOKE 3 LIVERPOOL 1
Stoke City, wakiwa kwao Uwanja wa Britannia, walizinduka toka kufungwa Bao la Penati la Sekunde 35 iliyofungwa na Nahodha Steven Gerrard kwa kushinda Bao 3-1.
=================
MAGOLI:
Stoke 3
-Walters Dakika ya 5 & 49
-Jones 12
Liverpool 1
-Gerrard Dakika ya 2 [Penati]
=================
Bao mbili za Jon Walters na la Kenwyne Jones ndio yamewapa Stoke City ushindi wao wa kwanza katika Mechi 4 na kuendeleza wimbi lao la kutofungwa katika Mechi 9 ikiwa na pamoja ya kutofungwa Uwanjani kwao tangu Februari.
Kipigo cha Liverpool Uwanjani Britannia kimeendeleza Rekodi yao ya kutoshinda hapo na pia kuwarudisha hadi nafasi ya 10 wakiwa Pointi 8 nyuma ya Timu iliyokamata nafasi ya 4.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Wilkinson, Kightly, Nzonzi, Whelan, Etherington, Walters, Jones
Akiba: Sorensen, Adam, Whitehead, Upson, Crouch, Shotton, Jerome.
Liverpool: Reina, Johnson, Skrtel, Agger, Jose Enrique, Gerrard, Lucas, Downing, Shelvey, Suso, Suarez
Akiba: Jones, Cole, Henderson, Coates, Carragher, Allen, Sterling.
Refa: Howard Webb
ASTON VILLA 0 TOTTENHAM 4
Bao 4 za Kipindi cha Pili, ikiwemo Hetitriki ya Gareth Bale, imewapa ushindi Tottenham wa Bao 4-0 dhidi ya Aston Villa waliokuwa kwao Villa Park na hiki kimekuwa kipigo chao cha pili kizito baada ya kutandikwa 8-0 na Chelsea majuzi.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Lowton, Herd, Clark, Baker, Bennett, Westwood, El Ahmadi, Delph, Holman, Benteke
Akiba: Given, Ireland, Albrighton, Bowery, Bannan, Lichaj, Carruthers.
Tottenham: Lloris, Walker, Gallas, Vertonghen, Naughton, Lennon, Dembele, Sandro, Bale, Defoe, Adebayor
Akiba: Friedel, Parker, Dawson, Sigurdsson, Livermore, Townsend, Caulker.
Refa: Mark Clattenburg
+++++++++++++++++++++++
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

SIMBA: HUKU ‘GOGORO’ LANUKIA, KOCHA MPYA KUTUA LEO!!

SIMBA-normalWakati Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, akitamka kuwa Mkutano wa Wanachama uliotishwa na Kundi linalodaiwa kuongozwa na Mohamed Wandi si halali, zipo taarifa kuwa Kocha mpya wa Klabu hiyo, Patrick Liewing, kutoka Ufaransa atatuaNchini leo.
Akizungumzia Mkutano huo ulioitishwa na Kundi la Mohamed Wandi ambalo limeripotiwa kukusanya Saini za Wanachama 698 ili kufanya Mkutano wa Wanachama Jumapili hii kwenye Hoteli ya Traventine Jijini Dar es Salaam, Rage amesema uchunguzi wa Watu hao 698 umebaini kuwa 490 kati yao si Wanachama hai kwa vile hawajalipa Ada zao za Uanachama na wengine kati yao ni Marehemu.
Akithibitisha kupokea Barua ya kuitishwa Mkutano huo wa Dharura wa Wanachama, Rage amesema Kikatiba mwenye mamlaka ya kuitisha Mkutano wa Dharura wa Wanachama ni Mwenyekiti au Wanachama hai 600.
Kutokana na hitilafu hizo za Kisheria, Rage amesema Uongozi wake hautautambua Mkutano huo.
Pia, Rage amedai Kundi la Viongozi wa zamani ndio wanaotaka kuitisha Mkutano huo kinyume cha Katiba yao.
Hata hivyo, Mohamed Wandi amekaririwa akitamka kuwa Mkutano huo hauna nia mbaya ila tu ni kuchambua mwendo mbovu wa Simba katika mzunguko wa Kwanza wa Ligi Kuu Vodacom ambao walianza vizuri mno lakini wakamaliza vibaya na kutupwa nafasi ya 3 huku juu yao wapo Azam FC na vinara ni Mahasimu wao wakubwa, Yanga.
Wakati huo huo, Ismail Aden Rage, amethibitisha ujio wa Kocha wao mpya, Patrick Liewing, kutoka Ufaransa ambae atatua Nchini leo.
Rage amesema Kocha huyo, ambae aliwahi kufundisha Timu za Vijana za Klabu maarufu huko France, Paris Saint Germain, atakuwa Kocha Mkuu na pia atapewa jukumu la kuendeleza vipaji vya Vijana.
Rage amesema: “Simba ndio Timu pekee Nchini yenye mfumo wa kuendeleza Vijana na zipo timu za Vijana chini ya Miaka 14, 16 17 na 20! Ujio wa Liewing utatusaidia sana kwa sababu ana uzoefu wa kukuza vipaji!”
Kocha huyo mpya kesho anatarajiwa kukutana na Wachezaji wote kwenye Kambi yao ya Mazoezi huko TCC Chang’ombe, Dar es Salaam.
Liewing, ambae anambadili Kocha kutoka Serbia Milovan Cirkovic, aliwahi kuwa Kocha wa Asec Mimosa ya Ivory Coast kati ya Mwaka 2004 na 2009 na kuisaidia kutwaa Makombe kadhaa Nchini humo pamoja na kuifikisha Nusu Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2009.
Mwaka 2006, Kocha Liewing pamoja na Kocha wa Al Ahly ya Misri waliteuliwa kuwa Makocha Bora Afrika.

CHEKA AWAPA RAHA MASHABIKI WA NGUMI JIJI LA ARUSHA



 Bondia Francis Cheka leo ametwaa ubingwa wa IBF Afrika baada ya kumpiga kwa pointi bondia toka Malawi Chiotka Chimwemwe kwenye pambano la raundi 12 lililofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Majaji wa pambano hilo ambao walikuwa watatu walitoa maksi kama ifuatavyo: David Chikwanje alimpa Cheka pointi 112/114 za Chimwemwe, Boniface Wambura alimpa Cheka pointi  118/114 za Chimwemwe na James Ligongo alimpa Cheka pointi  120/115 za Chimwemwe

Cheka ambaye alipigwa konde la haja likasababishwa kuchanika katikati ya paji la uso raundi ya pili aliweza kuhimili kumaliza raundi zote huku akitibiwa kila saa.

Baada ya Mpambano kumalizika Cheka allisema anashukuru ameshinda ila mpambano ulikuwa mgumu sana kwake na alikiri hajakutana na bondia mkali kama Chimwemwe kwa karibuni.

 "Nashukuru nimeshinda ila nimeshinda kwa bahati kwani bondia niliyekutana naye ni bondia mzuri kwani angeweza kushinda ila alikosa mbinu chache tu", alisema Cheka.

Naye bondia Chiotka Chimwemwe alikubali matokeo na kusema ni mara yake ya kwanza kupigana nje ya nchi yake  hivyo amechukulia kama changamoto kwake.

Cheka ameweza kutwaa Ubingwa wa IBF Afrika baada ya kunyang'anywa kwa kushindwa kuutetea kwa muda na akaenda kucheza na Karama Nyilawila ubingwa wa UBO ambao pia alimpiga Nyilawila.

Naye Meya wa jijini la Arusha  Gaudence Lyimo alimpongeza promota wa pambano hilo Andrew George na Rais wa TPBC Onesmo Ngowi kwa kuleta pambano hilo la kimataifa Arusha na kusema atashirikiana nao kuwahakikisha anainua mchezo wa ngumi Arusha.

"Nawapongeza walioleta pambano hili Arusha na wnawaahidi tutakuwa tukishirikiana bega kwa bega kuahakikisha tunainua mchezo wa ngumi Arusha", alisema Meya.


Francis Cheka akiongea na waandishi wa Habari baada ya pambano kumalizika


Frincis Cheka akikwepa konde la Chimwemwe

Jaji Boniface Wambura akitafakari kitu kabla mpambano kuanza