matukio

 

WAWILI WAZIKWA WAKIWA HAI MBEYA


diwani 0e655
                                    
WAKAZI wawili wa Kijiji cha Karungu, Kata ya Ivuna, Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya wamefariki dunia baada ya kufukiwa wakiwa hai katika kaburi moja na marehemu wanaodaiwa kumuua, tukio linalohusishwa na imani za kishirikina.

Watu hao, Ernest Molela anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 60 na Bibi Mizinala Nachela ambaye umri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya miaka 50, walizikwa wakiwa hai pamoja na aliyekuwa mkazi wa kijiji hicho, marehemu Nongwa Hussein.

Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ivuna, Joseph Silwimba aliliambia gazeti hili jana kwa simu kuwa, tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa tano na sita mchana, muda mfupi kabla ya maziko ya Hussein.

Kabla ya kufukiwa katika kaburi moja na marehemu, Molela na Nachela kwa nyakati tofauti walipigwa hadi kuzirai na watu wanaodaiwa kushiriki kuchimba kaburi kwa ajili ya kumzika marehemu Hussein.

Silwimba alisema Hussein alifariki dunia Jumamosi saa 10 jioni baada ya kuugua kwa muda mrefu, lakini inaonekana kuwa baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walihusisha ugonjwa huo ambao ulisababisha kifo chake na ushirikina.

Jana mchana, Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), Momba aliyefahamika kwa jina la Wendo aliongoza operesheni ya kufukua kaburi walimozikwa watu hao, ambao walikutwa wakiwa wameshafariki dunia.

Silwimba alisema miili ya Molela na Nachela ilifanyiwa uchunguzi, kisha kukabidhiwa kwa ndugu na jamaa zao ambao waliifanyia mazishi jana mchana.
Mkasa wenyewe
Kundi la vijana tisa ambao wanadaiwa kuwa ndiyo waliokuwa wakichimba kaburi la marehemu Hussein walianza msako katika Kijiji cha Karungu wakiwatafuta wale waliowatuhumu kwamba ni wachawi na kwamba walihusika na kifo chake.

Silwimba alisema katika harakati zao, walikwenda nyumbani kwa George Hussein ambaye ni kaka wa marehemu lakini hawakumkuta, hivyo kuamua kuchoma moto nyumba yake kwa kuwa walikuwa wakimtuhumu kuhusika na kifo hicho.

“Baada ya kufanya uharibifu huo, walikwenda hadi nyumbani kwa Mzee Molela kisha wakamkamata na kumpiga sana hadi hali yake ikawa mbaya kisha wakambeba hadi eneo la maziko,” alisema na kuongeza:

“Waliporejea kwenye msiba walimkuta Mama Nachela naye wakamkamata na kuanza kumpiga hadi akazimia na yeye pamoja na Molela waliwavuta hadi kwenye kaburi ambako mazishi ya Nongwa (Hussein) yalifanyika.”

Alisema baada ya jeneza kushushwa kaburini, vijana hao wanaodaiwa kwamba walikuwa na hasira walimvuta Molela na kumwamuru kuweka udongo kaburini, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na hali yake kuwa mbaya.

“Baada ya kushindwa walimsukumiza kaburini na baadaye walimvuta yule mama (Nachela) ambaye naye alikuwa hajitambui na kumtupa ndani ya kaburi halafu wakawafukia wote, kisha wakaondoka,” alisema Kaimu Ofisa Mtendaji huyo.

TIMBWILI LA UJAMBAZI KARIAKOO JANA

 
  Mtu anaedaiwa Kuhusika katika tukio la Ujambazi lililotokea Maeneo ya Kariakoo Jijini Dar es Salaam jana akiwa chini ya Ulinzi baada ya kukamatwa. Watu wawili waliuwawa jana na majambazi wakati wakipora fedha. 
 
 

MIAKA 51 YA UHURU: UHURU NA MAANA YAKE KWA WATANZANIA


 Watanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali hapa Changchun, Jilin, China wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mjadala mfupi wa maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Juma
 Mchangiaji Hamza Ibrahim akichangia kwenye mjadala mfupi wa maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili. (0696)
 Captain Mwita Vedasto Wambura akichangia kwenye mjadala wa maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili
 Captain Mwita Vedasto Wambura akichangia kwenye mjadala wa maadhimisho ya 51 ya Uhuru wa Tanzania uliofanyika kwenye Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang Jumapili

Changchun, Jilin,China

Elimu Maalum kuhusu Uzalendo inabidi itolewe ili kuwafanya watanzania waendelee kuheshimu Uhuru na dhana nzima, hayo yalisemwa na wachangiaji kwenye mjadala mfupi ulioandaliwa ili kuadhimisha miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania hapa.

Mjadala huo mfupi, uliofanyika katika Mgahawa wa Chun Yuan Kao Rou Wang jana (Jumapili), ulikuwa umeandaliwa na watanzania wanaoishi hapa, ambao wengi ni wanafunzi kwenye Vyuo Vikuu mbalimbali vilivyopo kwenye jimbo hili.

Walisema kuwa elimu ya Uraia imeonyesha mapungufu makubwa kwa kuwa haiwafanyi vijana kuwa na uzalendo kwa nchi yao, kama ilivyokuwa mwanzo.  

Walipendekeza kuwa watengenezaji wa mitaala waangalie utengenezaji wa elimu hiyo katika changamoto za uchumi wa soko huria, ambalo linapingana kwa kiasi kikubwa na dhana ya uzalendo.

Walionya kuwa hata mmomonyoko wa maadili na ubinafsi unaolisumbua taifa kwa sasa ni matokeo ya kukosekana kwa elimu hiyo ya Uzalendo. Wachangiaji Wakuu walikuwa Yazidu Saidi, Hamza Ibrahim, Captain Mwita Vedasto Wambura, Tessua Ally na Albert Memba.  Mjadala huo uliratibiwa na Innocent Mugisha.

Rais Kikwete atunuku Nishani Ikulu wakati wa Sherehe za miaka 51 ya Uhuru

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo mchana ametunuku  nishani kwa watu kutoka makundi mbalimbali yajamii waliotumikia taifa kwa uadilifu na kutoa mchango wa pekee.Miongoni wa waliotunukiwa nishani leo ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Eusebia Munuo pamoja na Msanii Mkongwe Bi.Fatma Baraka Khamis(Bi.Kidude).Wengine waliotunikiwa nishani ni pamoja na Watumishi wa umma na askari Jeshi na Polisi. (Picha na Freddy Maro).

 Bi. Kidude akiveshwa nishani na Rais Jakaya Kikwete Ikulu leo
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Eusebia Munuo akivishwa nishani
Rais jakaya Kikwete akimvisha nishani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue

SHEREHE ZA MIAKA 51 YA UHURU WA TANGANYIKA KATIKA PICHA

Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho ya sherehe  za miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. 
 Ngoma ya kitamaduni kutoka Zanzibar.
 Ngoma ya kitamaduni kutoka Rwanda
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete wakati wa maadhimisho ya sherehe  za miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. 
 Askari wa Kikosi  cha majini akitolewa nje ya viwanja kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kuishiwa nguvu
 Kikundi cha sanaa cha Taifa kutoka Rwanda kikitumbuiza katika sherehe hizo
 Wasanii wa kikundi cha Taifa kutoka Zanzibara wakitumbuiza kwa ngooma ya kitamaduni kutoka Pemba.
Askari wa Jeshi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipita kwa mwendo wa haraka mbele ya Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete wakati wa maadhimisho ya sherehe  za miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. 
 Watoto wa alaiki wakiwa katika gwaride la miaka 51 vya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Watoto, Gozibety Mbwele (3) na Nyamburi Mganga (5) wa kikundi cha Utandawazoi kutoka Mwanza wakionesha manjonjo yako wakati wa sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo. 
Vijana wa alaiki wakitengeneza maumbo ya vitabu.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mama Maria Nyerere wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo.

Angelina Jolie kung’atuka uigizaji ili awe mama wa nyumbani na alee watoto.

Angelina Jolie

Muigizaji wa kike Angelina Jolie aliyetamba sana na action movie ya Mr.&Mrs. Smith amefunguka katika interview aliyofanya na kituo cha televisheni cha Uingereza ‘4 News’ kwamba anampango wa kuachana na kazi yake ya uigizaji muda mfupi ujao.
Mshindi huyo wa tuzo za Oscar ambae yuko busy akiandaa movie yake ‘Maleficent’ anaona wakati umefika sasa anataka kuachia ngazi kwa sababu mbalimbali hasa sababu za kifamilia na majukumu ya kazi za nyumbani, “nadhani naelekea kuachana na uigizaji kwa wakati mwanangu anafikia umri wa miaka 13 hivi, anyway, shunguli nyingi sana za kufanya nyumbani.”

Angelina Jolie mwenye watoto sita alikiri kuenjoy kuwa muigizaji na ukizingatia yuko kwenye list ‘A’ ya Hollywood Stars, “nimekuwa naenjoy sana kuigiza, ninajivunia kuwa katika hii kazi na ninauzoefu mkubwa na nimekuwa na uwezo wa kusimulia hadithi na kuwa sehemu ya hadithi ambazo zinamaana na nimefanya mambo for fun, lakini...”, aliongeza ila hakumalizia sentensi yake na kutabasamu.
‘The Salt’ actress alielezea mipango yake kabla hajang’atuka katika tasnia hii ya uigizaji, “nitafanya movie kadhaa na nina bahati nzuri sana kuwa na kazi hii, ni taaluma yenye bahati ukiwa sehemu yake na ninaifurahia, lakini kama ntatoka kesho nitakuwa na furaha sana kuwa nyumbani na watoto wangu. Naamka asubuhi kama mama na ninaangalia habari kama mtu mwingine yeyote na naangalia nini kinatokea na nataka kuwa sehemu ya dunia katika njia chanya.” Alimaliza Angelina Jolie

Video ya David Cosmas-Mama chumbe balaa tupu


                                David Cosmas
Baada ya audio iliyoachiwa wiki iliyopita mdundo wa David Cosmas unaokwenda kwa ajina la Mama chumbe sasa kupatika na katika video.
Ndani ya video hiyo ameonekana mwanadada Tina msanii wa bongo movie ambae amefanya vizuri pia kiatika filamu ya The waiter inayofanya poa katika industry ya filamu bongo.Pia wameonekana dancers wa bads number washindi wa dancing mkoa wa Mwanza na washindi wa pili Tanzania
Models walizingua
Kwa mujibu wa meneja Aziz ambae amesimamia mpango mzima amesema Mchakato wa kufanya video hiyo ulianza kwa kutafuta models ambao wangeshiriki kwenye video kuanzia kitaa cha Chuo kikuu cha Mt.Augustino Mwanza lakini kutoka models tisa hadi wawili amabo mwisho wasiku nao walizingua kutokea. 
                                  Aziz
Audio ya ngoma hii itafanywa upya kwa Maneck AM records kabla haijaachiwa rasmi baada ya mkali huyo (Maneck) kuomba kuirudia audio hiyo kwa studio yake na kujitolea pia kurekodi ngoma moja free nadani ya AM records kama kuonesha jinsi alivomkubali Davi.
 
Maneck

Rihanna kama Aunt Ezekiel

Kuna mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa baada ya Mrs De Monte aka Aunt Ezekiel kupigwa picha alizokuwa amekaa vibaya jukwaani juu ya jukwaa la fiesta Mwanza na baadae kuomba msamaha kwa kitendo hicho lakini kumbe haya mambo hata mbele yamezoeleka.

Moja ya picha ya jukwaani ya Rihanna inamuonesha nae akiwa kaachia maungo yake nje kama kawaida.Diva huyo wa R&B amekua na mafanikio makubwa hususani katika ngoma zake nyingi ikiwemo ile ya Diamonds inayofanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza katika Billboard Chart hot 100 na katika media tofautitofauti duniani
                                                Rihanna
                                             Aunt Ezekiel
Baadhi ya raia wamecomment na kusema kuwa kukaa maungo wazi kwa wasanii wengi pengine nikutokana na mashabiki kushagilia na kuona kama ni safi kwao.Moja ya shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Shaz Billionea alisema "Sasa unadhani kama msanii anashangiliwa ndo maana wanaendelea kuvaa hivo lakini kama mashabiki wakimzomea hawezi kurudia tena".
Picha hizi mbili zinatuonesha kwamba dunia kweli sasa ni kijiji maana kinachofanyika bongo na kinachofanyika Marekani ndo kilekile.

No comments:

Post a Comment