Wednesday, December 26, 2012

TUSKER YAILEWESHA TILA LILA YANGA TAIFA KWA GOLI KIDUDE



MABINGWA wa Kenya, Tusker FC jioni hii wameiangusha Yanga SC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki jioni hii.
Huo ulikuwa mchezo maalum kwa Yanga kuwaaga mashabiki wake, kabla ya safari ya Uturuki Jumamosi usiku kwenda kuweka kambi ya wiki mbili.   
Wachezaji wa Tusker wakimpongeza mfungaji wa bao lao,
 Ismail Dunga kulia
Hadi mapumziko, Tusker walikuwa tayari mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa kimiani na kiungo Ismail Dunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 44.
Refa Charles Oden Mbaga alitoa penalti hiyo baada ya kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari kumuangusha kwenye eneo la hatari, kiungo Khalid Aucho.
Yanga walicheza vema katika kipindi hicho, lakini hawakufanikiwa kutengeneza nafasi za kufunga na hilo lilitokana na mipango haba ya safu yake ya kiungo leo, ikiongozwa na Kabange Twite na Nurdin Bakari.
Pamoja na kocha Mholanzi Ernie Brandts kufanya mabadiliko kipindi cha pili, akiwaingiza Hamisi Kiiza, Jery Tegete, Simon Msuva, Omega Seme na Nizar Khalfan kuchukuwa nafasi za akina David Luhende, Said Bahanuzi, George Banda, Rehani Kibingu na Oscar Joshua, lakini matokeo hayakubadilika.
Zaidi Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi kupitia kwa Msuva na Kiiza na hata Nizar alipoingia, lakini kwa ujumla bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Hii ni mechi ya pili Brandts anafungwa kati ya mechi 10 alizoiongoza Yanga tangu aanze kazi akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, nyingine saba ameshinda na moja ametoa sare.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladislaus Mbogo, Nurdin Bakari, Rehani Kibingu, Kabange Twite, George Banda, Said Bahanuzi na David Luhende.
Tusker FC; George Opiyo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Justin Monda, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk, 

TAARABT NJE MOROCCO AFCON 2013, QPR KUNUFAIKA!!


Kiungo wa QPR Adel Taarabt ameachwa kwenye Kikosi cha Morocco kitakachocheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini kuanzia tarehe 19 Januari 2013.
Juzi, Taarabt, mwenye Miaka 23, alitangaza kuwa akichaguliwa ataichezea Morocco AFCON 2013 msimamo ambao ulipokelewa kwa masikitiko na Klabu yake QPR ambayo iko mkiani kwenye Ligi Kuu England na yeye ndio tegemezi lao kubwa.
Wachezaji wanaocheza Ligi Kuu England ambao wamechukuliwa na Morocco ni Mchezaji wa Liverpool Oussama Assaidi na Karim El Ahmadi wa Aston Villa.
+++++++++++++++++++
MECHI ZA QPR AMBAZO ANGEZIKOSA TAARABT AKIWA AFCON 2013:
-19 Jan - West Ham v QPR
-29 Jan - QPR v Man City
-2 Feb - QPR v Norwich
-9 Feb - Swansea v QPR
+++++++++++++++++++
Kocha wa Morocco Rachid Taoussi ameteua Wachezaji 24 na atalazimika kumtema Mchezaji mmoja kabla Fainali hizo kuanza.
Taarabt, ambae ameichezea Morocco Mechi 15 na kufunga Bao 4, amekuwa na uhusiano mbovu na Nchi yake na kuna wakati aligomea kuichezea.
Kwenye AFCON 2013, Morocco wapo Kundi A pamoja na Wenyeji Afrika Kusini, Angola na Cape Verde.
KIKOSI KAMILI (Kwenye Mabano ni Klabu za Morocco labda itajwe):
MAKIPA: Nadir Lamyaghri (Wydad Casablanca), Anas Zniti (MAS), Khalid Askiri (Raja Casablanca)
MABEKI: Abderahim Chakir and Younes Bekakhdar (both FAR Rabat), Mehdi Benatia (Udinese, Italy), Issam El Adoua (Guimaraes, Portugal), Ahmed Kantari (Stade Brest, France), Abdelhamid El Kaoutari (Montpellier, France), Zakarya Bergdich (Lens, France)
VIUNGO: Karim El Ahmadi (Aston Villa, England), Adil Hermach (Al Hilal, Saudi Arabia), Kamal Chafni (Stade Brest, France), Mehdi Namli (Moghreb Tetouan), Younes Belhanda (Montpellier, France), Abdelaziz Barrada (Getafe, Spain), Chahir Belghazouani (Ajaccio, France)
MAFOWADI: Oussama Assaidi (Liverpool, England), Adeliliah Hafidi (Raja Casablanca), Youssef Kadioui (FAR Rabat) Abderrazak Hamdallah (Olympique Safi), Youssef El Arabi (Granada, Spain), Mounir El Hamdaoui (Fiorentina, Italy), Nordin Amrabat (Galatasaray, Turkey).

FRIEDEL ASAINI MYPA SPURS!
Kipa mkongwe wa Tottenham Hotspur Brad Friedel amekubali kusaini Mkataba mpya utakaomweka hadi Mwaka 2014.
Friedel, alijiunga na Spurs kutoka Aston Villa Mwaka 2011 na ameichezea Klabu hiyo mara 49 na atafikisha Miaka 43 Mkataba wake ukimalizika Mwaka 2014.
Kwa sasa Friedel, ambae aliichezea USA mara 82, ameporwa Nambari Wani hapo Spurs na Kipa wa Kimataifa wa France, Hugo Lloris.
Brad Friedel yupo kwenye Ligi Kuu England tangu Mwaka 1997 na awali alikuwa Klabu za Liverpool na Blackburn.
Kipa huyo ndie anaeshikilia Rekodi ya kwenye Ligi Kuu England ya kucheza zaidi ya Mechi 300 mfululizo.


RIO KUSUBIRI KUSAINI MPYA MWAKANI!!
Beki wa Manchester United Rio Ferdinand amekiri kuwa kitu pakee kitakachompa Mkataba mpya Mwakani wakati Mkataba wake wa sasa utakapomalizika Mwezi Juni ni ikiwa yeye atakuwa fiti bila kuandamwa na majeruhi.
Katika Miaka ya hivi karibuni, Rio amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara lakini katika Miezi 18 iliyopita tatizo hilo limepungua na amekuwa akicheza Mechi nyingi.
Hivi majuzi, Meneja wa Man United, Sir Alex Ferguson, alidokeza Rio, mwenye Miaka 34, anaweza kuendelea kucheza kwa Miaka kadhaa na hilo lilileta matumaini ya kuongezewa Makataba.
Mwenyewe Rio ametamka: “Kumsikia Ferguson akisema naweza kucheza kwa Miaka mingine miwili au mitatu kunatia moyo! Lakini nitaangalia hali yangu na kuamua kama niendelee hapo baadae!”

LAMPARD ‘APIGWA BUTI’ CHELSEA, TERRY NAE……!!!
Hivi juzi Mkongwe wa Chelsea alipiga Bao safi katika ushindi wa Bao 8-0 dhidi ya Aston Villa katika Mechi ya Ligi Kuu England lakini habari za kuaminika toka ndani ya Stamford Bridge zimedokeza kuwa Kiungo huyo ameshaambiwa hana lake ndani ya Klabu hiyo na atafute kwingine.
Lampard, Miaka 34, ameshaambiwa yuko huru Januari 1 kusaka Klabu nyingine.
Katika utumishi wake, Lampard ameiwezesha Chelsea kuwa Mabingwa wa Ulaya, Mabingwa wa England mara 3, FA CUP 4 na LIGI CUP 2.
Hali kama ya Lampard pia inaelekea itamkumba Mkongwe mwingine wa Chelsea, Nahodha wao John Terry.

UEFA KUJIKATIA WENYEWE RUFAA KUHUSU ‘WABAGUZI ’SERBIA!!
UEFA inatarajiwa kuzikatia Rufaa Adhabu zote ambazo Serbia imepewa kuhusiana na Mechi yao ya EURO 2013 na England ya Vijana Chini ya Miaka 21 ambayo iligubikwa na tuhuma za Ubaguzi toka Mashabiki wa Serbia kwa Wachezaji wa England na pia vurugu za Maafisa wa Nchi hiyo.
Timu hiyo ya Serbia ya U-21 iliaadhibiwa kwa kutakiwa kucheza Mechi 1 bila Watazamaji na pia kupigwa Faini Pauni 65,000 kwa Ubaguzi wa Washabiki wao waliofanya kwenye Mechi na England U-21 iliyochezwa Uwanja wa Mladost, Mjini Krusevac, Serbia Oktoba 16.
Adhabu hizo zilitolewa na Jopo Huru la Udhibiti na Nidhamu la UEFA lakini leo UEFA, kupitia Tovuti yake, imeamua kuzikatia Rufaa adhabu zote hizo baada ya kupokea malalamiko mengi kuhusu uhafifu wake dhidi ya Tuhuma nzito.
Sambamba na Adhabu hizo kwa Serbia, Wachezaji wa England U-21, Steven Caulker alifungiwa Mechi mbili na Tom Ince, Mechi 1.

KUNG'ARA KWA MIGUEL MICHU TOKA AANZE KUCHEZA LIGI YA ENGLAND KUMEKUWA LULU KWA DEL BOSQUE,,,,EBU ANGALIA MABAO YAKE YOTE ANAYOFUNGA

KUNG'ARA KWA MICHU KUMEMFANYA KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA HISPANIA DEL BOSQUE AANZA KUMMEZEA MATE KUWMITA TIMU YA TAIFA KWA MARA YA KWANZA


MSHAMBULIAJI nyota wa Swansea City Michu anatarajiwa kuitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya taifa ya Hispania mapema mwakani kufuatia kucheza katika kiwngo cha juu katika msimu wake wa kwanza katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Kocha wa Hispania ambao ni mabingwa wa Ulaya na Dunia, Vicente del Bosque anatarajia kumuita mchezaji katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Uruguay Februari 26 mwakani mchezo ambao utafanyika jijini Doha, Qatar. Katika kikosi hicho Michu ataungana na Iago Aspas ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Celta Vigo na amekuwa akihusihwa na tetesi za kwenda Swansea. Michu amekuwa akionyesha kiwango cha juu kwa upachikaji mabao toka liponunuliwa kwa ada ya dola milioni 3.2 kutoka klabu ya Rayo Vallecano katika kipindi cha majira ya kiangazi ambapo kwasasa anaongoza katika orodha ya wafungaji akiwa amefunga mabao 13 katika michezo 18.

UDHAIFU W AENGLAND KUPIGA MIKWAJU YA PENALTI KOCHA HODGSON ASEMA MECHI ZA KIRAFIKI ZIAMULIWE KWA PENALTI


KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson anaamini kuwa changamoto ya mikwaju ya penati katika michezo ya kirafiki ambayo watatoa sare inaweza kuisadia timu hiyo kuondokana na jinamizi la kupoteza nafasi katika michuano mikubwa. Uingereza imekuwa mhanga mkubwa wa kutolewa katika michuano mikubwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati wakiwa wamepoteza mara sita kati ya saba mara mwisho ikiwa katika robo fainali ya michuano ya Ulaya dhidi ya Italia iliyofanyika Juni mwaka huu. Wakiwa katika maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014, Hodgson amesema kuwa katka mojawapo ya mechi za kirafiki watakazotoka sare atashauri wapinzani wake wamalize mchezo huo kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Amesema kwa kufanya hivyo kutawaongezea uzoefu zaidi wachezaji mbele ya mashabiki wengi kuliko kufanya hivyo wakiwa mazoezini peke yake. Mwaka 2013 Uingereza itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Brazil na baadae dhidi ya Ireland kabla ya kucheza na Scotland katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.

MESSI AZUNGUMZA ASEMA MABAO YANGU SIO MUHIMU KAMA TIMU HAISHINDI - MESSI.


MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesisitiza kuwa mabao anayofunga hayatakuwa na maana yoyote kama timu yake itakuwa haiwezi kushinda`mechi zake. Mshambuliaji huyo amekuwa katika kiwango kizuri miezi 12 ambapo amefunga mabao 91 na kuipita rekodi iliyowekwa miaka 40 iliyopita na Gerd Muller aliyefunga mabao 85 katika kipindi cha mwaka mmoja lakini nyota huyo amesema ushindi wa timu yake ndio wenye umuhimu kuliko rekodi binafsi. Messi ambaye yuko nchini kwao Argentina kwa mapumziko ya kipindi cha baridi katika La Liga amesema amefurahi kufunga mabao mengi na kuvunja rekodi lakini mwaka ungekuwa mzuri zaidi kama wangishinda mataji kwani siku zote amekuwa akisisitiza mabao hayani maana yoyote kama timu haishindi chochote. Messi ambaye pia mwaka huu alipata mtoto wake wa kwanza aitwae Thiago amesema ujio wa mtoto huyo umemfanya awe mtu mwenye furaha na kuwashukuru wapenzi wote wa soka wa Argentina ambao husafiri kwenda kumshangilia wakati akicheza.

BPL MECHI BOXING DEI:MECHI 9 KUCHEZWA KATIKA VIWANJA TOFAUTI TOFAUTI

BPL_LOGOLEO huko England Mechi 9 za Ligi Kuu England zitachezwa na zifuatazo ni Taaarifa fupi kuhusu Hali za Wachezaji wa Kila Timu, Marefa wa Mechi za leo na Ratiba ya Mechi zijazo:
Jumatano Desemba 26
SAA 12 JIONI
EVERTON V WIGAN ATHLETIC
Kiungo wa Everton Darron Gibson anaweza kucheza Mechi hii licha ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi na West Ham baada ya kukata Rufaa na sasa anasubiri isikilizwe hapo kesho lakini Everton watamkosa Marouane Fellaini anaetumikia Kifungo na hii ni Mechi ya pili kati ya 3 alizofungiwa.
Wigan watamkosa James McCarthy mwenye matatizo ya enka.
MECHI ILIYOPITA: West Ham 1 Everton 2, Wigan 0 Arsenal 1
Refa: Lee Mason
[Gemu: 11 Kadi za Njano: 36, Kadi Nyekundu: 0]
Wasaidizi: A Garratt & S Massey
Refa wa Akiba: M Oliver
MANCHESTER UNITED V NEWCASTLE UNITED
Kama kawaida, Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson anatarajiwa kubadilisha Kikosi chake toka kile kilichotoka sare 1-1 na Swansea.
Javier Hernandez, Darren Fletcher na Danny Welbeck huenda wakaanza na Rafael huenda akapangwa baada ya kupona maumivu ya paja.
Newcastle United watamkosa Kiungo Chieck Tiote ambae amefungiwa Mechi moja baada ya kuzoa jumla ya Kadi za Njano 5.
Majeruhi watakaokosekana kwa Newcastle ni Hatem Ben Arfa, Steven Taylor, Yohan Cabaye na Ryan Taylor.
MECHI ILIYOPITA: Swansea 1 Man United 1, Newcastle 1 QPR 0
Refa: Mike Dean
[Gemu: 12, Kadi za Njano: 44, Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: J Collin & J Brooks
Refa wa Akiba: N Swarbrick
QUEENS PARK RANGERS V WEST BROMWICH ALBION
Kipa toka Brazil wa QPR, Julio Cesar, anaweza kupangwa baada ya kupona mgongo lakini Armand Traore, Nedum Onuoha, Park Ji-sung, Bobby Zamora na Andrew Johnson bado majeruhi.
Baada ya kutumikia Kifungo cha Mechi moja, Kiungo wa West Brom Youssouf Mulumbu ruksa kurejea Uwanjai lakini Claudio Yacob na Steven Reid bado majeruhi.
MECHI ILIYOPITA: West Brom 2 Norwich 1, Newcastle 1 QPR 0
Refa: Chris Foy
[Gemu: 12, Kadi za Njano: 20, Kadi Nyekundu: 0]
Wasaidizi: S Beck & H Lennard
Refa wa Akiba: A Davies
READING V SWANSEA CITY
Reading watawakosa Straika Jason Roberts, Sean Morrison na Alex McCarthy wote wakiwa majeruhi.
Swansea wanaweza kuwa nae Winga Pablo Hernandez aliezikosa Mechi 5 baada ya kuumia lakini Angel Rangel bado nje kwa maumivu.
MECHI ILIYOPITA: Swansea 1 Man United 1, Man City 1 Reading 0
Refa: Mike Jones
[Gemu: 11, Kadi za Njano: 41, Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: R Ganfield & M Wilkes
Refa wa Akiba: D Phillips
SUNDERLAND V MANCHESTER CITY
Winga wa Sunderland Adam Johnson yupo kwenye hatihati kucheza baada ya kuumia mguu Mechi iliyopita na pia upo wasiwasi kuhusu kucheza kwa Sebastian Larsson ambae ana maumivu ya goti.
Manchester City huenda wakawa nae Nahodha Vincent Kompany baada ya kupona nyonga na Mario Balotelli aliekuwa akiugua maradhi lakini upo wasiwasi kuhusu Aleksandar Kolarov na Gael Clichy, wenye maumivu, lakini Samir Nasri hatacheza kwa vile ni majeruhi.
MECHI ILIYOPITA: Southampton 0 Sunderland 1, Man City 1 Reading 0
Refa: Kevin Friend
[Gemu: 10, Kadi za Njano: 38, Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: A Halliday & G Beswick
Refa wa Akiba: K Wright
FULHAM V SOUTHAMPTON
Fulham hawana uhakika kuhusu kupona kwa Bryan Ruiz, Mahamadou Diarra na Mladen Petric.
Southampton watacheza bila ya Nahodha wao Adam Lallana ambae ni majeruhi.
MECHI ILIYOPITA: Southampton 0 Sunderland 1, Liverpool 3 Fulham 0
Refa: Phil Dowd
[Gemu: 12, Kadi za Njano: 34, Kadi Nyekundu: 2]
Wasaidizi: S Child & L Betts
Refa wa Akiba: D Coote
NORWICH CITY V CHELSEA
Norwich watawakosa majeruhi Steven Whittaker, John Ruddy, Andrew Surman na Ryan Bennett.
Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi anaweza kurudi dimbani baada ya kumaliza Kifungo cha Mechi 3 lakini Nahodha John Terry na Ryan Bertrand bado majeruhi.
MECHI ILIYOPITA: West Brom 2 Norwich 1, Chelsea 8 Aston Villa 0
Refa: Jon Moss
[Gemu: 9, Kadi za Njano: 25, Kadi Nyekundu: 1]
Wasaidizi: P Kirkup & D Bryan
Refa wa Akiba: A Madley
Jumatano Desemba 26
SAA 2 na NUSU USIKU
ASTON VILLA V TOTTENHAM HOTSPUR
Majeruhi wa Aston Villa ni Ron Vlaar, Gabriel Agbonlahor, Charles Nzogbia na Darren Bent.
Wasiwasi wa Tottenham ni juu ya Straika Clint Dempsey lakini Benoit Assou-Ekotto na Scott Parker huenda wakaanzishwa baada ya kuwa fiti kutokana na maumivu yao ya muda mrefu.
MECHI ILIYOPITA: Chelsea 8 Villa 0, Tottenham 0 Stoke 0
Refa: Mark Clattenburg
[Gemu: 9, Kadi za Njano: 34, Kadi Nyekundu: 4]
Wasaidizi: S Ledger & M McDonough
Refa wa Akiba: A Taylor
Jumatano Desemba 26
SAA 4 DAKIKA 45 USIKU
STOKE CITY V LIVERPOOL
Straika wa Stoke Michael Owen, ambae amekuwa nje tangu Oktoba, huenda akaikabili Klabu yake ya zamani Liverpool.
Mchezaji mwingine wa zamani wa Liverpool, Peter Crouch, huenda nae akapata namba baada ya kupigwa Benchi hivi karibuni.
Liverpool huenda wakamwanzisha Raheem Sterling ambae alianzia Benchi katika Mechi iliyopita na Fulham.
Majeruhi pekee wa Liverpool ni Joe Allen.
MECHI ILIYOPITA: Tottenham 1 Stoke 1, Liverpool 3 Fulham 0
Refa: Howard Webb
[Gemu: 13, Kadi za Njano: 48, Kadi Nyekundu: 2]
Wasaidizi: S Burt & D England
Refa wa Akiba: D Drysdale
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 18 Pointi 43
2 Man City Mechi 18 Pointi 39
3 Chelsea Mechi 17 Pointi 32
4 Arsenal Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 14]
5 Everton Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 8]
6 Tottenham Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 5]
7 WBA Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 4]
8 Liverpool Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 4]
9 Stoke Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
10 Norwich Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -7]
11 Swansea Mechi 18 Pointi 24
12 West Ham Mechi 18 Pointi 23
13 Fulham Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -5]
14 Newcastle Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -6]
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 18 Pointi 18
17 Southampton Mechi 17 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++
MECHI ZIJAZO:  
Jumamosi 29 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v Tottenham
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Wigan
Fulham v Swansea
Man United v West Brom
Norwich v Man City
Reading v West Ham
Stoke v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Arsenal v Newcastle
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Everton v Chelsea
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

WACHEZAJI WAPYA WA AZAM MIENO, ATUDO WAREJEA KENYA


Atudo
BEKI Joackins Atudo na kiungo Humphrey Mieno wamebaki nyumbani kwao Nairobi, Kenya na watajiunga tena na kikosi cha Azam FC, baada ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.
Wawili hao, walikuwepo kwenye kikosi cha Azam kilichotwaa Kombe la Hisani, linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jumamosi iliyopita, wakiwachapa wenyeji Dragons FC kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Ikiwa njiani kurejea Dar es Salaam, Meino na Autdo waliteremka Nairobi wakati mabingwa hao wa Kombe la Hisani wakiwasili Tanzania usiku wa saa 7:00 jana.
Katibu wa Azam, Nassor Idrisa amesema wachezaji wengine pia watapewa mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya sikukuu ya Krisimasi na baada ya hapo watakutana kujiandaa kwa safari ya Zanzibar kwenda kutetea Kombe lao la Mapinduzi.
Azam Jumamosi ilitwaa ubingwa wa Kombe la Hisani baada ya kuwafunga wenyeji, Dragons FC kwa penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha dakika ya 75 na katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na Samih Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
Azam iliingia fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya DRC Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
Humprey Mieno joins Azam FC
Kikosi cha Azam kilichoshiriki mashindano hayo ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki, Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey Mieno na Joackins Atudo.
Katika mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti. Mchezaji mwingine wa kigeni wa Azam, Brian Umony wa Uganda, atajiunga na timu hiyo baada ya sikukuu pia.



























































































































































































































YANGA DIMBANI LEO KUWAKABILI TUSKER YA KENYE KATIKA UWANJA WA TAIFA



Historia ya Kombe la Kagame
YANGA SC ya Dar es Salaam, leo itamenyana na mabingwa wa Kenya, Tusker FC katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Huo utakuwa mchezo wa 10 kwa ujumla, Yanga kucheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Ernie Brandts kati ya hiyo, ikishinda saba, sare moja na kufungwa moja.
Brandts aliyerithi mikoba ya Mbelgiji Tom Saintfiet, amekuwa akiinoa timu hiyo kwa takriban wiki tatu sasa kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu pamoja na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Mabingwa hao wa Kagame, mwishoni mwa wiki hii wanatarajiwa kufanya ziara ya wiki mbili nchini Uturuki, kujiandaa na kampeni zake za mwakani. Yanga itaondoka na kikosi chake chote na hakuna mchezaji atakayeachwa.   
REKODI YA ERNIE BRANDTS YANGA
Yanga 1-1 Simba SC            (Ligi Kuu)
Yanga 0-1 Kagera Sugar    (Ligi Kuu)
Yanga 3-1 Toto African      (Ligi Kuu)
Yanga 3-2 Ruvu Shooting  (Ligi Kuu)
Yanga 3-0 Polisi Moro       (Ligi Kuu)
Yanga 1-0 JKT Oljoro          (Ligi Kuu)
Yanga 3-0 JKT Mgambo     (Ligi Kuu)
Yanga 2-0 Azam FC             (Ligi Kuu)
Yanga 2-0 Coastal               (Ligi Kuu)

 YANGA MABINGWA WATETEZI W A KOMBE LA KAGAME TOKA LIANZISHWE 1974
Mwaka Mshindi Matokeo Mshindi wa pili Mwandaaji
1974 Simba SC  Tanzania - Abaluhya FC  Kenya Tanzania
1975 Young Africans  Tanzania 2-0 Simba SC  Tanzania Zanzibar
1976 Luo Union  Kenya 2-1 Young Africans  Tanzania Uganda
1977 Luo Union  Kenya 2-1 Horsed  Somalia Tanzania
1978 Kampala City Council FC  Uganda 0-0 (3-2 penalty) Simba SC  Tanzania Uganda
1979 Abaluhya FC  Kenya 1-0 Kampala City Council FC  Uganda Somalia
1980 Gor Mahia  Kenya 3-2 Abaluhya FC  Kenya Malawi
1981 Gor Mahia  Kenya 1-0 Simba SC  Tanzania Kenya
1982 AFC Leopards  Kenya 1-0 Rio Tinto  Zimbabwe Kenya
1983 AFC Leopards  Kenya 2-1 ADMARC Tigers  Malawi Zanzibar
1984 AFC Leopards  Kenya 2-1 Gor Mahia  Kenya Kenya
1985 Gor Mahia  Kenya 2-0 AFC Leopards  Kenya Sudan
1986 Al-Merrikh  Sudan 2-2 (4-2 after penalties) Young Africans  Tanzania Tanzania
1987 Villa SC  Uganda 1-0 Al-Merrikh  Sudan Uganda
1988 Kenya Breweries  Kenya 2-0 Al-Merrikh  Sudan Sudan
1989 Kenya Breweries  Kenya 3-0 Coastal Union  Tanzania Kenya
1990 not played
1991 Simba SC  Tanzania 3-0 Villa SC  Uganda Tanzania
1992 Simba SC  Tanzania 1-1 (5-4 after penalties) Young Africans  Tanzania Zanzibar
1993 Young Africans  Tanzania 2-1 Villa SC  Uganda Uganda
1994 Al-Merrikh  Sudan 2-1 Express FC  Uganda Sudan
1995 Simba SC  Tanzania 1-1 (5-3 after penalties) Express FC  Uganda Tanzania
1996 Simba SC  Tanzania 1-0 APR FC  Rwanda Tanzania
1997 AFC Leopards  Kenya 1-0 Kenya Breweries  Kenya Kenya
1998 Rayon Sport  Rwanda 2-1 Mlandege  Zanzibar Zanzibar
1999 Young Africans  Tanzania 1-1 (4-1 after penalties) Villa SC  Uganda Uganda
2000 Tusker FC  Kenya 3-1 APR FC  Rwanda Rwanda
2001 Tusker FC  Kenya 0-0 (3-0 after penalties) Oserian  Kenya Kenya
2002 Simba SC  Tanzania 1-0 Prince Louis FC  Burundi Zanzibar
2003 Villa SC  Uganda 1-0 Simba SC  Tanzania Uganda
2004 APR FC  Rwanda 3-1 Ulinzi Stars  Kenya Rwanda
2005 Villa SC  Uganda 3-0 APR FC  Rwanda Tanzania
2006 Police FC  Uganda 2-1 Moro United  Tanzania Tanzania
2007 APR FC
Rwanda
2-1 Uganda Revenue Authority SC  Uganda Rwanda
2008 Tusker FC
Kenya
2-1 Uganda Revenue Authority SC  Uganda Tanzania
2009 ATRACO FC  Rwanda 1-0 Al-Merreikh  Sudan Sudan
2010 not played
2011 Young Africans  Tanzania 1-0 Simba SC  Tanzania Tanzania
2012 Young Africans  Tanzania 2-0 Azam FC  Tanzania Tanzania
2013 TBA

MWAKA HUU TENA KATIKA SPORTS HABARI YA TIMU YA ZAMBIA CHIPOLOPOLO KUWA BINGWA WA AFCON 2012 KULE GABON NA EQUATORIAL GUINEA KUWAFUNGA TEMBO WA AFRIKA IMEHUSIKA SANA