Sunday, January 20, 2013

YANGA YAENDESHA MKUTANO MKUU WAKE KISASA!!

>>CLOUDS TV YAPEPERUSHA MKUTANO LAIVU!!
>>YATOA VYETI, FEDHA, PIKIPIKI KWA BAADHI YA WANACHAMA KWA UTUMISHI ULIOTUKUKA!!
>>UWANJA WAO WA WATAZAMAJI 40,000 KUANZA KUJENGWA MEI!!
YANGA_MKUTANO_MKUUKLABU KONGWE NCHINI, Yanga, leo chini ya Mwenyekiti wake Yusuf Manji wamefanya Mkutano Mkuu kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam huku ukihudhuriwa na Wanachama 1440 na kuweka Historia kwa kuendeshwa kisasa kabisa na kwa utulivu mkubwa na pia kuonyeshwa moja kwa moja kupitia Kituo cha TV cha Clouds.
Mara baada ya Mwenyekiti Manji kuufungua Mkutano huo, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga, na Mzee Ibrahim Akilimali waliongoza Sala fupi huku Sanga akiongoza ile ya Madhehebu ya Kikristo na Mzee Akilimali ile ya Kiislam.
Miongoni mwa mambo yaliyoamuliwa kwenye Mkutano huo ni kuongeza muda wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mama Fatma Karume na Francis Kifukwe, na pia kuteua Wajumbe wapya wa Bodi hiyo ambao ni Captain George Mkuchika na Balozi Ameir Mpumbwe.YANGA_MJENGO
Miongoni mwa mambo makubwa yaliyotajwa Mkutanoni ni kuhusu Ujenzi wa Uwanja utakaochukua Watazamaji 40,000 na kugharimu Shilingi Bilioni 32 huku Wanachama wakionyeshwa Michoro yake na pia kujulishwa Ujenzi wake unatarajiwa Kuanza Mwezi Mei chini ya Kampuni ya Ujenzi ya BCCG iliyojenga Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Pia, Mkutano huo uliwatimua Uanachama Mwesigwa Selestine, Lousi Sendeu na Godwin Muganyizi kwa kosa la kufungua Kesi za Madai dhidi ya Yanga.
Pia Uongozi wa Yanga ulitoa Vyeti vya Utambuzi kwa baadhi ya Wanachama na Wachezaji/Viongozi kwa mchango wao katika Klabu ya Yanga..
Waliotunukiwa ni:
1.Abdallah Bin Kleb-Kongozi kwa kujitolea sana katika kuhakikisha Timu inafanya vizuri na kushinda michezo inayoikabili
2.Shadrack Nsajigwa-Mchezaji aliyechezea Yanga kwa muda mrefu ambae alipewa Barua na Fedha Shilingi 1,000,000/=.
3.Mahmoud Momar-Mfanyakazi Mtunza Vifaa wa siku nyingi katika Benchi la Ufundi (Barua na Fedha taslimu Sh. 1,000,000/=)
4.Stephen Samuel-Mwanachama Bora na mwenye uchungu na Yanga (Barua na zawadi ya Pikipiki mpya)
5.Hayati Isamail Rashid-Mwanachama aliyesaidia kupatikana kwa muafaka (Barua).

No comments:

Post a Comment