Saturday, December 22, 2012

YUSUPH KITUMBO AWA BOSSI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TABORA BAADA YA KUIBUKA KIDEDEA HII LEO DHIDI YA WENZAKE AKINA MUSA NTIMIZI NA LAURENT PAUL


Uchaguzi wa mkoa wa tabora leo umefanyika kuwasaka wale viongozi watakaowakilisha mkoa w atabora ngza ya TFF ,uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa tuwasa mkoani tabora na umehudhuriwa na wajumbe 24 waliopiga kura hii leo.

 

Katika nafasi ya mwenyekiti ilikuwa inawaniwa na wagombea watatu na mshindi amepatikana ni bwana yusuph kitumbo aliyepata kura 16 za ndiyo na wapinzani zake Mussa Ntimizi alipata kura 8 za ndiyo na Laurent Paul aliambulia sifuri kwani hata kwenye uchaguzi hakuwepo kutokana na majukumu ya kikazi yaliyombana.

 

Katika nafasi ya katibu mkuu nayo ilikuwa inawaniwa na wagombea wawili bw.Abert Sitta alikuwa anatetea nafasi yake ya ukatibu kwa mwaka wa tatu sasa na alibwagwa na mpinzani wake bw.Fattey Dewj Remtula aliyejikusanyia kura 17 dhidi ya kura 7 alizopata mzee sitta.

 

DICCK MLIMKA alichaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu TFF kwa kujikusanyia kura 14 akiwashinda wapinzani zake Charles Mwakambaya aliyepata kura 7,Milambo Kamili alipata kura 2 na wa mwisho alikuwa  Ramadhani Maghembe aliyepata kura 1 katika nafasi hiyo ya ujumbe wa mkutano mkuu TFF.


Na katika nafasi ya mwakilishi w avilabu ilikuwa inawaniwa na wagombea watatu  na bw.Razack j.Kumba alipata kura 13 na kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa vilabu kwa kuwabwaga Achery Manjory ALIYEPATA KURA 7 na bwana Lwamba Yussa alijipatia kura 4.


Kwenye nafasi ya ujumbe kamati tendaji ilikuwa na wagombea wawili nao ni Stanlaus Sizya na James Erick Kabepele na bwana stanslaus alijipatia kura 22 na james erick kabepele alijipatia kura 21 hivyo wamepitishwa wote katika nafasi hiyo kutokana na wajumbe waliokuwa wanahitajika katika nafasi hiyo kuwa watatu.


Na katika nafas iya mwakilishi wa mpira wa miguu kwa upende wa  wanawake ilikuwa na mgombea mmoja B.Janeth Michael naye alipita kwa kishindo kikubwa baada ya kupata kura za ndiyo kura 22 na kura mbili za hapana hivyo b.janeth michael ni mwakilishi wa kinamama kw aupande wa mpira w amiguu mkoa wa tabora.


Katika nafasi ambazo hazikuwa na wagombea ni nafasi ya makamu mwenyekiti ambayo ilikuwa na mgombea mmoja bw.Alaija Mwiga ambaye alijitoa katika uchaguzi huo kutokana na majukumu kuwa mengi,pia katika nafasi ya katibu msaidizi haikuwa na mgombea,mweka hazina ilikuwa na mgombea mmoja naye alikuwa ni MUSSA MSANANGA ambaye alijiondoa katika uchaguzi huo kutokana naye kuelemewa na majukumu ya kitaifa.


Mara baada ya uchaguzi huo mwakilishi wa TFF kitaifa ambaye alikuwa anasimamia uchaguzi huo bw.MOSES KALUWA alisema viongozi waliochaguliwa hii leo ni kutokana na jisni wajumbe walivyo na imani kwao na amesema TFF itakuwa bega kwa bega na hao viongozi ili kuinua soka la mkoa wa tabora


YUSUPH KITUMBO TUMAINI LA KUPANDA KWA SOKA TABORA

 Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora Yusuph Kitumbo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi huo
 Safu ya uongozi wa Tarefa
Baadhi ya wadau wakimpongeza Yufusu Kitumbo kwa ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu wa Tarefa.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Tabora Tarefa Mkama Bwire akitangaza matokeo ya uchaguzi huo ambapo amemtangaza Yusuph Kitumbo kuwa Mwenyekiti wa Tarefa kwa kupata kura 16 kati ya kura halali 24,nafasi ya pili imeshikwa na Mussa Ntimizi ambaye amepata kura 8 huku Laurent Paul akiwa ameambulia patupu.

Aidha matokeo hayo ya uchaguzi Fath Dewij ameshinda nafasi ya katibu wa Tarefa kwa kumshinda Albert Sitta ambaye alikuwa akitetea nafasi yake aliyoiongoza kwa muda mrefu.




Matokeo yameanza kutangazwa sasa



 Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Tarefa wakiendelea kupiga kura

Baadhi ya wadau wa soka mkoa wa Tabora nao walikuwa na shauku ya kutaka kujua nini kinachojiri katika chumba cha mkutano huo wa uchaguzi,wengine walishindwa kuzuia hisia zao wakalazimika kuchungulia madirishani 
 Kura zinahesabiwa!!!!ADAM FUNDIKIRA MWENYE NJANO

 Baadhi ya wadau wa soka mkoani Tabora  wakiwa wameketi nje ya ukumbi wa uchaguzi wakisubiri mchakato wa uchaguzi ufanyike.
Baadhi ya wagombea wa nafasi ya Uenyekiti na katibu wakiwa nje ya ukumbi wakisubiri kuitwa ukumbini kwa ajili ya kujieleza na kuomba kura kwa wajumbe,kushoto ni Yusuph Kitumbo mgombea nafasi ya Mwenyekiti na Fath Dewij nafasi ya Katibu mkuu Tarefa.
 Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Tarefa wakisubiri kuanza kupiga kura ili kuwapata viongozi watakaoongoza Soka la mkoa wa Tabora,mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya maji Safi Tuwasa.
Mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya TFF Moses Kaluwa akijitambulisha mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha mpira wa miguu mkoani Tabora Tarefa.

STEWART AIACHA AZAM KINSHASA, AENDA KULA SIKUKUU NYUMBANI

Stewart wa kwanza kushoto akifutiwa na Kali
KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall ameondoka jana usiku mjini hapa kwenda kwao Uingereza kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya, akiiacha timu inakabiliwa na mchezo wa fainali ya Kombe la Hisani hapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
STEWART HALL akizungumza jana mara kuondoka mjini kishansa Stewart alisema kwamba anamuachia timu hiyo msaidizi wake, Kali Ongala na anaamini atafanya kazi nzuri.
Stewart alisema Kali ni mtu ambaye siku zote amekuwa akimuandaa kuwa kocha wa baadaye wa Azam na hii si mara ya kwanza kumuachia timu, kwani aliwahi kufanya hivyo mara kadhaa ikiwemo kwenye Kombe la Urafiki, ambalo aliiongoza timu kufika Fainali.
“Siku moja nitaondoka Azam na kumuacha Kali awe kocha Mkuu, siku zote namtayarisha, namjengea kujiamini, naamini atakuwa kocha bora sana wa Azam, sina wasiwasi naye, namuachia timu na anaweza kurudisha Kombe Dar es Salaam,”alisema Stewart ambaye atarejea mwakani.
Azam kesho itacheza fainali, baada ya jana kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
Nahodha Jabir Aziz Stima ndiye aliyekwenda kupiga penalti ya mwisho, Shark wakitoka kupoteza, kufuatia mpira kugonga mwamba. Aiziz aliwainua vitini wachezaji wenzake na makocha wake pamoja na viongozi wa wachache wa timu hiyo waliopo hapa kwa kupiga penalti maridadi iliyotinga nyavuni.
Azam iliuanza mchezo huo vizuri na ikicheza kwa maelewano makubwa sambamba na kushambulia kwa kasi kutokea pembeni, kulia Kipre Herman Tchetche na kushoto Seif Abdallah.
Hata hivyo, shambulizi la kushitukiza la Shark liliwapa bao la kuongoza dakika ya 16, lililofungwa na Ngulubi Kilua, baada ya mabeki wa Azam kudhani ameotea.
Iliwachukua dakika 10 tu Azam kusawazisha bao hilo, mfungaji akiwa Gaudence Exavery Mwaikimba aliyeunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya nyota wa mchezo huo, Kipere Herman Tcheche kutoka wingi ya kulia.
Baada ya bao hilo, Azam iliendelea kuwashambulia Shark na dakika ya 37, Kipre Tchetche aliifungia timu hiyo bao la pili, kufuatia kazi nzuri ya Mwaikimba. Mwaikimba alipokea mpira mrefu, akatuliza na kumtangulizia kwa mbele mfungaji, ambaye hakufanya makosa, alimchambua kipa wa timu inayomilikiwa na mdogo wa rais wa DRC, Joseph Kabila.       
Hadi mapumziko, Azam ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-1 na kipindi cha pili Shark waliingia kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha kwa penalti dakika ya 47, iliyotiwa nyavuni na Bukasa Kalambai, ambaye yeye mwenyewe alijiangusha kwenye eneo la hatari baada ya kuzongwa na beki David Mwantika.
Baada ya dakika 90 kutimu timu hizo zikiwa zimefungana 2-2, sheria ya matuta ilichukua mkondo wake na wachezaji wote watano wa Azam waliopewa dhamana hiyo na kocha Muingereza Stewart Hall, walitimiza wajibu wao vizuri.
Kipre Tchetche alifunga ya kwanza, Mwaikimba ya pili, Jaockins Atudo ya tatu, Himid Mao ya nne na Stima akapiga ya ushindi.


NI AZAM NA COASTAL FAINALI KOMBE LA UHAI


TIMU za Azam ya Dar es Salaam na Coastal Union ya Tanga ndizo zitakazoumana kwenye fainali ya michuano ya Kombe la Uhai 2012 itakayochezwa kesho jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Timu hizo zimepata fursa hiyo baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali ya michuano hiyo inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom jana. Michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia maji Uhai.
Azam ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata tiketi ya fainali baada ya kuitoa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa mikwaju ya penalti 3-2. Matokeo ya dakika 90 yalikuwa bao 1-1. Nayo Coastal Union iliivua ubingwa Simba kwa kuifunga mabao 2-1.
Mechi ya fainali itaanza saa 10 kamili jioni, na itatanguliwa na ile ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Mtibwa Sugar na Simba ambayo itachezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye uwanja huo huo.
Mbali ya kombe, bingwa wa michuano hiyo atapata sh. milioni 1.5, makamu bingwa sh. milioni 1 wakati mshindi wa tatu atajinyakulia sh. 500,000. Timu iliyoonesha zaidi mchezo wa kiungwana (fair play) itapata sh. 400,000, mchezaji bora wa mashindano sh. 350,000, mfungaji bora sh. 300,000 na kipa bora sh. 300,000.
Naye kocha bora katika mashindano hayo atazawadiwa sh. 300,000 kama itakavyokuwa kwa refa bora.

YANGA WAMPA MTU 4-0, KINDA LA B LAPIGA HATTRICK

Kocha wa Yanga, Ernie Brandts
YANGA SC jana imeitandika mabao 4-0 Kijitonyama Stars katika mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Kijitonyama, Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga jana yalifungwa na George Banda matatu na Rehani Kibingu moja, ambao wote wamepandishwa kutoka timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20.

Kikosi cha Yanga jana kilikuwa mseto; Ally Mustafa ‘Barthez’/Said Mohamed, Juma Abdul/Nssajigwa Shadrack, Oscar Joshua/Stefano Mwasyika, Ladislaus Mbogo/Job Ibrahim, Mbuyu Twite, Nurdin Bakari, Rehani Kibingu/Godfrey Taita, Kabange Twite, Jerry Tegete/Omega Seme, George Banda na David Luhende.
Yanga inaendelea na mazozi mjini Dar es Salaam kujiandaa na safari yake ya Uturuki wiki ijayo ambako inakwenda kuweka kambi ya wiki mbili. Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuwa kamili kesho, baada ya wachezaji wake wengine kumaliza majukumu yao ya kitaifa leo, katika mechi kati ya Tanzania na Zambia leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MAGWJI WA MUZIKI IKULU NA KUWAAHIDI NISHANI ZA KUTAMBUA UMUHIMU WAO KATIKA JAMII



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kikumbi Mwanza Mpango "King Kikii"
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Comandoo Hamza Kalala
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Cosmas Thobias Chidumule
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Abdul Salvador "Father Kidevu"
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Flora Mbasha na mumewe
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Addo Mwasongwe
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwana FA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwana FA
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Ally
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Shakila huku Carolla Kinasha na Waziri Ally wakisubiri zamu zao
---

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali imeanza kutoa Nishani kwa wasanii kwa vile inatambua umuhimu wao katika jamii.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza wawakilishi wa sanaa mbalimbali nchini waliofika Ikulu leo asubuhi kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kuwatambua na kuwapa heshima kubwa ya Tuzo na Nishani wasanii katika siku ya sherehe za Uhuru za tarehe 9 Disemba, Ikulu, Dar-Es-Salaam.

“Tumetoa Nishani kwa vile wasanii wanatoa mchango mkubwa, tumeanza kutoa nishani mwaka huu na tutaendelea kutoa miaka ijayo kwani kwa kuitambua sanaa, mnawapa moyo wasanii kuendelea kujituma na kuwa wabunifu zaidi” Rais amesema na kuongeza, “Tumeingiza Nishani ya Wasanii na Watafiti maana nao wanafanya kazi kubwa sana ya kutafiti mazao na mbegu mbalimbali ambazo zinaongeza tija katika kilimo nchini”.

Katika kumbukumbu ya kusherehekea miaka 51 ya  Uhuru wa Tanzania bara mwaka huu, Rais Kikwete alitunuku nishani kwa makundi mbalimbali ya watu waliotoa mchango mkubwa katika jamii na waliotumikia taifa kwa uadilifu.

Rais alitoa Nishani ya Sanaa na Michezo kwa mara ya kwanza kwa wasanii nchini ambapo Bi. Fatma Baraka Khamis (Bi Kidude) kupitia Baraza la Sanaa Zanzibar, Kiongozi wa Muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma Muhidin Maalim Gurumo, Kiongozi wa Zamani wa Bendi ya Dar Intrenational Marehemu Marijan Rajab walipata tuzo hiyo.

Wengine ni Msanii wa maigizo na filamu nchini Marehemu Fundi Said (Mzee Kipara) na Mwanariadha mkongwe John Steven Akwari.
Rais amewataka wasanii kushirikiana na serikali lakini pia wawe mstari wa mbele katika kupigania haki zao na sio kusubiri serikali tu iwafanyie hivyo.

Wasanii hao wamefika Ikulu wakiongozwa na Bw. Ruge Mutahaba wa Clouds Media Group.
Wengine ni Addo Mwasongwe, Rais wa Shirikisho la Muziki na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Injili, Bw. Juma Ubao Mwenyekiti wa Chama cha Muziki Tanzania (CHAMUDATA), aliyewakilishwa na Hamza Kalala.

Bibi  Shakila Said, Mkongwe wa Muziki wa Taarab Nchini, Bi Carola Kinasha Msanii wa Muziki , Mzee King Kiki msanii wa Muziki wa Dansi Mwana FA, msanii wa Kizazi Kipya na Bw. Waziri Ally , msanii wa Muziki.

Wawakilishi hao pia wamemshukuru Rais kwa msaada wa hali na mali anaotoa kwa wasanii mbalimbali wanapopata matatizo ambao hivi sasa wapo katika hatua mbalimbali za matibabu ya afya zao hapa nchini na nchi za Nje.

“Haya mengine ninayafanya tukama wajibu wa  kibinadamu kwa vile nina nafasi ya kufanya hivyo na pale tunapokua na uwezo tunasaidia kama binadamu wenzetu” Rais Amesema.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu - DSM
21 Desemba, 2012

ULAYA: Mabingwa Juve wapiga Bao Dakika za majeruhi!

>>BARCA, REAL KUAGA 2012 LEO!!
JUVENTUS-Claudio_MarchisioMabingwa wa Italy, Juventus, jana walipiga Bao mbili Dakika za majeruhi na kujipatia ushindi wa Bao 3-1 dhidi ya Cagliari ambao walitangulia kufunga Bao lao.
Jventus, ambao ndio vinara wa Serie A na wakicheza Mechi yao ya mwisho kwa Mwaka 2012 kwani Ligi inaenda Likizo hadi Januari 6, walijikuta wako nyuma kwa Bao la Penati iliyofungwa na Pinilla katika Dakika ya 16 na wao wakashindwa kusawazisha baada ya kukosa Penati.
Lakini Matri akawafungia Juve Bao la kusawazisha katika Dakika ya 75 na Vucinic, alieingizwa Kipindi cha Pili, alipiga Bao la pili Dakika za majeruhi na Matri kuongeza Bao la 3 kipindi hicho hicho.
Juventus wanaomgoza Ligi wakiwa Pointi 10 mbee ya Inter Milan ambao leo wanacheza na Genoa.
Huko Spain, La Liga leo inatarajiwa kushuhudia Mechi zao za mwisho za Mwaka 2012 kabla kwenda Mapumzikoni hadi Januari 6.
MATOKEO/RATIBA:
LA LIGA
Alhamisi Desemba 20
RCD Espanyol 2 Deportivo La Coruna 0
Real Sociedad 2 Sevilla 1
Rayo Vallecano 3 Levante 0
Ijumaa Desemba 21
Valencia 4 Getafe 2
Atletico Madrid 1 Celta Vigo 0
Jumamosi Desemba 22
1800 Real Betis v Real Mallorca
2000 Real Valladolid v FC Barcelona
2200 Malaga v Real Madrid
2200 Osasuna v Granada
Jumapili Desemba 23
Athletic Bilbao v Real Zaragoza
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 6
SERIE A
Ijumaa Desemba 21
Pescara 2 Catania 1
Cagliari 1 Juventus 3
Jumamosi Desemba 22
14:30 Inter Milan v Genoa
17:00 Atalanta v Udinese
17:00 Bologna v Parma
17:00 Torino FC v Chievo Verona
17:00 Sampdoria v SS Lazio
17:00 Siena v Napoli
17:00 Palermo v Fiorentina
22:45 AS Roma v AC Milan
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 6

NYUZI FUPI: Zidane-BRAZIL BINGWA DUNIANI, MESSI BURE ARGENTINA, RONALDO NA MAN!!

>>HABARI FUPI FUPI ZA SOKA ZILIZOTANDA ULIMWEMGU WA SOKA:
ZIDANE ATABIRI BRAZIL KUTWAA KOMBE LA DUNIA 2014
Mchezaji wa Kimataifa wa France Zinedine Zidane anaamini Brazil ndio Timu itakayokuwa moto kwenye Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Nchini humo Mwaka 2014.


Mara ya mwisho Brazil kutwaa Kombe la Dunia ilikuwa Mwaka 2002 walipoifunga Germany 2-0 kwenye Fainali lakini Zidane ana imani kubwa wao ndio watakuwa Bingwa Duniani Mwaka 2014.
Alisema "Brazil ni Nchi ya Soka. Watakuwa nyumbani na wana Wachezaji wazuri, Nyota!"
Hivi karibuni Brazil ilimtimua Kocha Mano Menezes na kumrudisha Kocha mzoefu Luiz Felipe Scolari ambae aliipa Brazil Kombe la Dunia Mwaka 2002.


RAUL MEIRELES: MCHEZAJI wa ZAMANI-LIVERPOOL & CHELSEA KIFUNGO MECHI 11

 Another massive club: Raul Meireles claimed Fenerbahce are as big as Chelsea and Liverpool
Mchezaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea, Raul Meireles, amefungiwa Mechi 11 baada ya kutuhumiwa kumtemea mate Refa huko Uturuki.
Meireles, mwenye Miaka 29, anaechezea Fenerbahce, alitolewa nje kwenye Mechi ya Dabi na waliyofungwa 2-1 na Galatasaray lakini mwenyewe amepinga tuhuma hizo na kuapa kuchukua hatua za Kisheria kujisafisha.

JONNY EVANS ASAINI MKATABA MPYA MAN UTD
Sentahafu wa Manchester United, Jonny Evans, amesaini Mkataba mpya utakaomweka Klabuni hapo kwa Miaka mitatu na nusu zaidi.
Evans, Miaka 24, alikuwa amebakisha Miezi 18 kwenye Mkataba wake wa sasa.


RONALDO: SITOSHANGILIA GOLI DHIDI YA MAN UNITED
 
 CRISTIANO RONALDO ametamka kuwa hatashangilia Goli lolote atakaloifunga Manchester United wakati Timu yake Real Madrid itakapokutana na Man United kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI hapo Februari 13 Mwakani Uwanjani na kurudiana Machi 5.
Ronaldo, mwenye Miaka 27, aliihama Man United Juni 2009 baada ya kukaa hapo Miaka 6 na kutwaa Ubingwa wa England mara 3, Ubingwa wa Ulaya mara moja pamoja na yeye binafsi kuteuliwa Mchezaji Bora Duniani.
Ronaldo ametamka: “Sitashangilia nikiifunga Man United!”
Aliongeza: “Mpaka leo naongea na Ferguson. Kila mara namkumbuka sana na naikumbuka Man United. Nilijisikia raha sana pale! Ni Familia kwangu!”
Ronaldo pia alisema Wachezaji wengi wa Man United ni Rafiki zake na ameishukuru Man United kwa kumfanya afikie kiwango ambacho anacho sasa.
ARGENTINA HAIMTHAMINI MESSI!
Ingawa Lionel Messi ameshafunga Jumla ya Bao 90 kwa Mwaka 2012 zikiwemo Bao  12 kwa Nchi yake Argentina lakini Wanahabari Nchini humo hawamthamini na badala yake wamemteua Bingwa wa Uzito wa Kati wa Ngumi wa Nchi hiyo na wa Dunia, Sergio Martinez, kuwa ndio Mwanamichezo Bora wa Argentina kwa Mwaka 2012 na nafasi ya Pili kushikwa na Sebastian Crismanich ambae ndie pekee aliipa Medali ya Dhahabu Argentina kwenye Michezo ya Olimpiki iliyofanyika London Mwezi Juni na Julai Mwaka huu.
Argentina imempa Lionel Messi nafasi ya Tatu kwenye Ubora.


STEPHEN KESHI AMWACHA ODEMWINGIE NA OBAFEMI MARTINS KATIKA KIKOSI CHAKE CHA SUPER EANGLES


Kocha wa Timu ya soka ya Nigeria  Stephen Keshi amewaacha washambuliaji wawili wa timu hiyo  Peter Odemwingie na  Obafemi Martins kwenye kikosi cha timu hiyo kitachoshiriki mataifa ya afrika mwezi january nchini afrika kusini.  


Mshambuliaji wa West Brom Peter Odemwingie alichezea Nigeria katika mechi ya kufuzu dhidi ya Rwanda Mwezi February,
wakati  Martins, ambaye kwa sasa anachezea   Levante ya uispania , alishindwa kumvutia  kocha wake katika mechi ya kirafiki dhidi ya Venevuela 

Danny Shittu, ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika klabu yake ya Millwall inayoshiriki ligi daraja la pili ameitwa baada ya kuchezea kwa mara ya mwisho timu hiyo katika fainali za kombe la dunia 2010 nchini afrika kusini   


Keshi, atafanya mazoezi yake ya mwisho huko ureno kuanzia decmber 27 atatakiwa kupunguza wachezaji hadi 23 kabla ya january 9  siku kumi kabla yamichuano hiyo kuanza .

.Kikosi cha Nigeria 

Goalkeepers: Vincent Enyeama (Maccabi Tel Aviv/Israel), Austin Ejide (Hapoel Be'er Sheba/Israel), Chigozie Agbim (Enugu Rangers), Daniel Akpeyi (Heartland)

Defenders: Elderson Echiejile (Braga/Portugal), Juwon Oshaniwa (Ashdod FC/Israel), Benjamin Francis (Heartland), Joseph Yobo (Fenerbahce/Turkey), Efe Ambrose (Celtic/Scotland), Solomon Kwambe (Sunshine Stars), Azubuike Egwuekwe (Warri Wolves), Danny Shittu (Millwall/England), Kenneth Omeruo (ADO Den Haag/Netherlands), Godfrey Oboabona (Sunshine Stars)

Midfielders: Mikel Obi (Chelsea/England), Nosa Igiebor (Real Betis/Spain), Ogenyi Onazi (Lazio/Italy), Raheem Lawal (Adana Demirspor/Turkey), Obiora Nwankwo (Padova/Italy), Fegor Ogude (Valerenga/Norway), Gabriel Reuben (Kano Pillars), Rabiu Ibrahim (Celtic/Scotland)

Forwards: Ahmed Musa (CSKA Moscow/Russia), Emmanuel Emenike (Spartak Moscow/Russia), Brown Ideye (Dynamo Kiev/Ukraine), Victor Moses (Chelsea/England), Uche Kalu (Rizespor/Turkey), Bright Dike (Portland Timbers/ USA), Shola Ameobi (Newcastle/England), Ikechukwu Uche (Villarreal/Spain), Ejike Uzoenyi, Sunday Mba (Enugu Rangers)

SPECIAL ONE M,OURINHO ASEMA SIMUUZI KAKA NG'O!!! :




Kocha wa Real Madrid  Jose Mourinho amesema hategemei kumuuza  Mshambuliaji wa timu hiyo Ricardo  Kaka Mwezi January .

MBrazil huyo ni moja kati ya wachezaji muhimu katika dimba la Bernabeu, lakini  Mourinho anataka kummbakiza mchezaji ili kuimarisha kikosi chake  .

Amesema : "Sidhani kama Kaka atakwenda popote  . atabaki hapa, na nimeshasema muda mrefu  ,kama akibaki ni vizuri kwanza anatungenezea mbinu mmbadala   ."

Mourinho alitumia nafasi hiyo kumtakia kocha wa  Barcelona  Tito Vilanova unafuu na kupona haraka vilanova mwenye Miaka  44-ameanza matibabu ya kupigana na ugonjwa  kansa .

Vilanova alifanyiwa upasuaji wa tezi ,ambapo klabu yake imesema ulifanikiwa kwa asimilia kubwa na sasa ataanza majuma sita ya mazoezi ya ya kulainisha misuli  .

"Kwa mambo kama haya huwa tunakuwa pamoja ,"aliongeza  Mourinho . "kwa  Tito,Na familia yake  na kwa yeyote mwenye tatizo la kiafya tunamtakia apate unafuu na apone ."

HAKUNA MREMBO KAMA JOCELYNE AFRIKA MASHARIKI

Mrembo Joceline Maro ak,iwapungia mkono mashabiki mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la kumsaka mrembo wa Afrika mashariki jana katika ukumbi wa Mlimani City.

Mshindi wa kwanza Jocelyne amepata dola za Kimarekani 30,000 pamoja na gari aina ya Mazda lenye thamani ya dola 15,000 na mkataba wa kufanya kazi na Oganaizesheni ya Miss East Africa wenye thamani ya dola 15,000.

Mshindi wa pili amepata zawadi zenye thamani ya dola 8,000 ikiwa ni pamoja na kitita cha dola 2,000 na mkataba wa kufanya kazi na Oganaizesheni ya Miss East Africa wenye thamani ya dola 6,000.

Mshindi wa tatu amepata zawadi zenye thamani ya dola 5,000 pamoja na fedha taslimu dola 1,500 na mkataba wa kufanya na Oganazesheni ya Miss East Africa wenye thamani ya dola 3,500.

Joceline Maro katikati mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la mrembo wa Afrika mashariki , kushoto ni mrembo wa kutoka Uganda Ayisha Nagudi aliyeshika nafasi ya pili na kulia ni mrembo kutoka Burundi Ariella Kwizera aliyeshinda nafasi ya tatu.

MALAGA KUTOTETEA UBINGWA WA ULAYA MWAKANI !


Timu ya soka ya  Malaga imefungiwa kwa mmoja kutokushiriki ligi ya mabingwa barani ulaya kwa msimu unaokuja baada ya kushindwa kulipa mishahara na kodi za wachezaji kwa wakati. 

UEFA imesema kuwa Raia wa Qatari-ambaye ndiye anae miliki timu hiyo ameambiwa atafungiwa zaidi miaka minne kama
watashindwa kulipa madeni hayo ,mpaka mwezi  March 31 ambayo ndio siku ya mwisho aliyowekewa kulipa madeni hayo  anatakiwa kulipa dola za kimarekani  $11.6 zikiwa ni mishahara ya wachezaji .

UEFA  imetangaza hayo jana baaada ya timu hiyo kupangwa kucheza na Fc Porto katika hatua ya mtoano kumi na sita bora ya ligi ya mabingwa barani ulaya  timu hiyo haitaruhuisiwa kucheza ligi ya mabingwa au Europa ligi kama watafuzu msimu ujao  .

UEFA's imeipiga faini klabu hiyo ya  Malaga Dola $396,000.Timu hiyo inaruhusiwa kukata rufaa katika mahakama ya usuluhishi wa michezo CAS  

Malaga Inatarajiwa kupata jumla ya dola  a $33 million kutoka uefa ikiwa kama zawadi katika malipo ya runinga baada ya kushiriki ligi ya mabingwa bara ulaya 

Malaga imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza michuano hii mikubwa baada ya kumaliza wa nne katika ligi ya uispania msimu uliopita 
Klabu hii ilipata nguvu baada ya kuchukuliwa na mwekezaji kutoka Qatar  Sheik Abdullah Bin Nasser Al-Thani


Klabu nyingine ambazo zimekumbwa na adhabu hiyo ni  - Bucharest clubs Dinamo  Rapid,  Partizan Belgrade kutoka serbia ,  Hajduk Split , Osijek ya  Croatia - ambazo zimefungiwa kwa miaka mitatu  zaidi kama watashindwa kulipa faini hiyo hadi mwezi march 31 .

BRANDAN RODGERS ASEMA LIVERPOOL IWE MAKINI KATIKA DIRISHA DOGO LA USAJILI KUTOSAJILI WACHEZAJI WENYE NJAA


Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers ameonya kuwa usajili ndani ya klabu hiyo hautatazama thamani ya mchezaji kwa kigezo cha mshahara na ada ya uhamisho, wakati huu ambapo Liverpool inataka kujirekebisha kutoka katika kipindi kirefu kisichokuwa na mafanikio ambapo ilisajili wachezaji kwa mapesa mengi lakini hakuna walichofanya.

Mpaka sasa wekundu hao bado wanaendelea kuwategemea wachezaji waliosajiliwa na meneja aliyetangulia Kenny Dalglish ambao ni Jordan Henderson, Andy Carroll na Stewart Downing ambao kwa pamoja waliigharimu klabu hiyo kiasi cha euro milioni 92.

Ikiwa tayari imesha kamilisha mkataba mwingine wa muda mrefu na Raheem Sterling baada ya mazungumzo ya muda mrefu, Rodgers anasisitiza kuwa anawataka zaidi wachezaji wenye njaa ya mafanikio kuliko wenye zawadi kubwa ya pesa..


Amekaririwa akisema,

"unapaswa kupata wachezaji wenye njaa ambao wanataka kufanya kazi na kupigania mafanikio hilo ndilo kubwa kwangu."

"Hao watapata mikataba mizuri wakija hapa, lakini kama watakuwa wanaulizia pesa na mambo mengine mengi , siwataki, kwa uzoefu wangu wachezaji wa aina hiyo watakuangusha siku tu kwa namna moja ama nyingine.

Kauli hiyo ya Rogers inaarifiwa kuwa imetokana na mazungumzo marefu juu ya Raheem Sterling na uongozi wa klabu hiyo ambapo Sterling alikomaa katika mazunguzo hayo akitaka mshahara wa wiki wa euro elfu 36,800.

Mara baada ya pande hizo kukubaliana na kuingia mkataba wa muda mrefu hapo jana mchana, Sterling aliuambia mtandao wa Liverpool kuwa amefurahishwa na kufikia makubaliano.


Nimeibadilisha Arsenal - Aserna Wenger awajibu wakosoaji wake
 Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa haridhishwi na mwenendo wa Arsenal yake lakini hatakuwa tayari kukubali ukosoaji ambao umekuwa ukielekezwa kwake.

Meneja huyo Mfaransa alijikuta katika wakati mgumua katika miezi ya hivi karibuni kufuatia washika mitutu hao kufungwa na katika mchezo wa robo fainali na Bradford City mchezo wa michuano ya Capital One.

Lakini Wenger ameendelea kujitetea kuwa amekuwa na kazi nyepesi sasa kuliko ilivyokuwa huku nyuma wakati akianza.

Akiongea na The Mirror amesema,

“Siridhishwi na hali ya mambo, najitahidi kufanya kila niwezalo na naamini nitafanikiwa na hata nikiondoka niwe nimefanya."

“nimekuwa katika ukosoaji mkubwa katika kipindi cha miaka saba iliyopita , lakini kama meneja ilikuwa ni ngumu zaidi mwaka wa kwanza nilipoanza hapa,

“ninachoami pia ni kwamba klabu imekuwa tangu nilipowasili. Ukilinganisha na tulipo sasa na tulipotoka unaweza kuona hiyo tofauti.

 “Nilipowasili klabu ilikuwa Highbury ambapo kulikuwa hakuna viwanja vya mazoezi na ilikuwa na waajiriwa 80 .

“Leo kuna waajiriwa karibu 500 na tunachezea uwanja mkubwa  na kituo kikubwa cha mazoezi.

“Na pia klabu klabu inayojulikana dunia nzima. Tumekuwa katika vilabu vinavyo cheza kwa kiwango cha juu”

Arsenal inakaribia kufikisha miaka minane bila ya taji lakini Wenger anasisitiza kuwa anajivunia uasisi wake wa uwanja mkubwa wa Emirates ambao anadhani ni jambo kubwa kuliko makombe.

Chelsea inamtaka Walcott, Pjanic & Willian kuziba nafasi ya Sturridge.
 Chelsea imewajumuisha Theo Walcott, Willian na Miralem Pjanic katika orodha fupi ya wachezaji walio katika mpango wao kuziba nafasi ya Daniel Sturridge.

Mabigwa hao wa soka Ulaya wanataka mtu wa pembeni ambaye ataruhusu mpango wa mahitaji ya meneja wao Rafael Benitez wa kuwa na washambuliaji wanao zunguka.

Chelsea imeendelea kuwepo kileleni katika mbio za kumsaini Falcao kutoka Atletico Madrid licha ya kwamba huenda huenda asijiunge na timu hiyo mpaka majira mengine ya kiangazi lakini pia wanamtaka mshambuliaji mwenye uwezo wa sehemu yoyote katika eneo la ushambuliaji.

Taarifa za uhakika zinasema klabu hiyo yenye maskani yake katika jiji la London imethibitisha kumjumuisha mshambuliaji wa  Arsenal Theo Walcott, mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk, Willian na mwingine ni mshambuliaji wa AS Roma, Pjanic.

Sturridge amekuwa kwenye mpango wa kuondoka Stamford Bridge na kwasasa yuko katika mazungumzo na ya kutaka kuelekea Liverpool mwezi ujao kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £12.

Walcott anaweza kuelekea jijini London kama atashindwa kuafikiana na mambo mbalimbali na Arsenal, licha ya kwamba Arsene Wenger kukaririwa akisema mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England hatauzwa.

Willian, winga wa Brazil ambaye aliisumbua sana Chelsea katika mchezo wa vilabu bingwa Ulaya hatua ya makundi anaendelea kuwepo katika darubini ya mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich licha ya euro milioni €25 kukataliwa na Shakhtar.


 Michael Laudrup Van Persie sawa na Michu
 Michael Laudrup amekipongeza kiwango cha Michu msimu huu kiasi kupelekea kumlinganisha mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania na Manchester United Robin van Persie.

Mshambuliaji huyo wa Swansea na mdutch Van Persie wote wamefunga magoli 12 katika ligi kuu ya England msimu huu na wanaungana katika kitabu cha wafungaji bora.

United itakuwa ikielekea katika dimba la Liberty hapo kesho na Laudrup anahofia uwezo wa Van Persie, lakini anaamini kikosi chake kinaweza kuibuka na ushindi endapo wataendelea na utamaduni wa kujiamini na kucheza kwa uwezo wao.

“United ina wachezaji wenye kiwango na wasiofanya makosa katika eneo la hatari kama Van Persie.

“unapaswa kuwa makini naye wakati wote kulinda vizuri na kuwa na hadhari ya kudondosha mipira karibu.

“Michu na Van Persie wako sawa. Ni kama wanafanana wote wanapiga miguu ya kushoto, hawana kasi lakini wanajua niwakati gani wa kukimbia.