Tuesday, January 22, 2013

KAGERA SUGAR ASHINDWA KUTAMBA MBELE YA MAAFANDE WA TABORA POLISI TABORA ALLY HASSAN MWINYI.


Timu ya kagera sugar kutoka katika mashamba ya miwa bukoba kule leo imeshindwa kutamba mbele ya wapiga kwata wa mkoani tabora polisi tabora baada ya kufungana bao 1-1 mchezo wa mwisho wa ziara wa kagera sugar ambayo ilikuwa tabora ikitoka burundi ilikokuwa imeenda kucheza mechi za kirafiki.

Kama kawaida timu ya wakatamiwa kagera sugar walikuwa wa kwanza kujipatia bao lao kupitia kwa mshambuliaji wao kutoka nigeria Wilfredy Emme aliyewachambua mabeki wa polisi tabora na kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa polisi tabora Abdul Aziz.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza timu ya kagera sugar walienda mbele kwa bao lao 1-0 kama jana ilivyokuwa kwa rhino rangers na kipindi cha pili timu ya maafande wa polisi tabora walirudi wakiwa wamerekebisha makosa yao.

Na mnamo dakika ya 57 daniel msengi aliunganisha krosi vizuri iliyochongwa na mshambuliaji w atimu hiyo iddy kibwana na kufanya matokeo kuwa 1-1.Hadi dakika 90 za mchezo mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho timu zote zilitoka hakuna mbabe baada ya kutoshana nguvu ya bao moja kwa moja 1-1.

Na kesho katika dimba hilo hilo la ALLY HASSAN MWINYI kutakuwa na mpambano mwingine wa kirafiki kati ya wanakisha mapanda wa mwanza toto african dhidi ya wanajeshi wa hapa mkoani tabora rhino rangers mchezo wa kujipima nguvu kuelekea katika duru la pili la ligi kuu tanzania VPL na ligi daraja la kwanza tanzania FDL ammbapo michuano hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi jan 26.1.2013 katika viwanja tofauti hapa tanzania.

Mchezo wa leo umeingiza shilingi laki nane na elfu hamsini na nane 858,000 kutokana na mashabiki mia nane na hamsini na nane 858 waliokata tiketi kuangalia mchezo huu kwa shilingi 1000 ikumbukwe jana waliingia watazamaji 1630 na kupata shilingi mil.1630000 kuangalia mechi ya rhino rangers na kagera sugar.
Leo wachezaji wa

KAGERA SUGAR+Andrew ntala,luhende kanyata,martin muganyizi,lamban kambole,malegesi mwangwa,zubery dabi,mecky maiko,shamte odiro,shija mkina,paul ngwai,
walioingia kipindi cha pili ni adam oseja,juma nade,benjamin asukile,george kavilla,daudi jumanne,rashid madawa,paul kabange na kamana salum.
POLISI TABORA+Abdul aziz,kaizar kilowoko,josephy manyira,jeremia ng'ambi,jamali jumanne,benard adam,mussa boaz,hussein abdalah,ramadhan semwa,daniel msengi na iddy kibwana.
BECHI+husein abdalah,david joseph,ibrahim mussa,baraka adim,ernest nkadi,na john matuli.

LUIS SENDEU AIDAI YANGA MILIONI 79


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjL7bky_xkCecaHrkLz53N93fdXiI_qBVDhPZqZONc7FErW33vqPVeimu5VouVYTfjDYIPnANcWjj2hcuTL_bJ4m7hH3rXh6detOwFc9WSIKpli3ucFVQ6obqTYJwk807mIsLaSbu2yQC-d/s1600/sendeu.JPG


 Tuhuma za ufujaji wa fedha zitokanazo na jengo la kibiashara la Yanga lililopo katika Mtaa wa Mafia, Kariakoo jijini Dar es Salaam ni miongoni mwa mambo yaliyozua mjadala mkubwa wakati wa mkutano mkuu wa mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) kwenye ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi jijini Dar es Salaam .

Baadhi ya wanachama waliohudhuria mkutano huo walitaka maelezo ya kutosha kutoka kwa viongozi kuhusiana na jengo lao hilo, hasa mahala zinakokwenda fedha za kodi ya pango zinazokadiriwa kuwa ni mamilioni ya fedha.


Suala la jingo la Mafia, kuuzwa kwa kipa Shaaban Kado na ujenzi wa uwanja wa kisasa, ndizo ajenda zilizokuwa gumzo kwa kiasi kikubwa wakati wa mkutano huo uliohudhuriwa na wanachama hai 1,444.


Iliwachukua takriban saa moja na nusu wajumbe wa mkutano huo kulijadili jengo la mtaa wa Mafia ambapo mwishowe, uongozi ulishindwa kutoa jibu la moja kwa moja na badala yake kuahidi kuunda kamati ya uchunguzi na kutoa maelezo ya kina ifikapo Februari 7 mwaka huu.


“Naona suala la Mafia ni kubwa, kila anayeinuka anazungumza kuhusu jingo la Mafia, wazee wetu Francis Kifukwe na Mama Fatma Karume wataunda kamati kufuatilia jengo letu maana wao ndiwo watunza mali za Yanga. Uhakiki utatolewa Febrauri 7,” alisema Clement Sanga ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Yanga.


Wanachama wengi waliopata nafasi ya kuchangia katika mkutano huo, walitaka kujua watu wanaokusanya mapato ya jengo hilo.


“Tunataka watu wanaojiona wajanja kwa kuhujumu mapato ya jengo la Mafia wajulikane na pia watambue kwamba jengo hilo ni mali ya Yanga. Si mali ya mtu ile,” alisema Hassan Chombe kutoka tawi la Dodoma.


UWANJA WA BIL. 32/-

Uongozi wa klabu hiyo ulitangaza kwa wanachama kuwa ujenzi wa uwanja wao wa kisasa utakaogharimu Sh. bilioni 32  utaanza rasmi Juni mwaka huu huku ukisimamiwa na kampuni ya Beijing Construction ya China, ambayo ndiyo iliyojenga Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Sanga alisema kuwa wameandaa mikakati mbalimbali itakayowawezesha kupata fedha za kufanikisha ujenzi huo ikiwamo ya kuwachangisha wanachama, kufanya harambee kwa wafanya biashara wakubwa na kuingia ubia na makampuni makubwa.


“Mpaka sasa hatujaamua uwanja huo utapewa jina gani. Kama kuna kampuni inataka tutumie jina lao, waje mara moja na kutupa pesa ili tujenge,” alisema Sanga huku akionesha michoro mbalimbali ya namna uwanja huo utakavyokuwa.


Akifafanua zaidi, Sanga alisema kuwa ujenzi wa uwanja huo utakamilika baada ya miaka miwili na wana mpango wa kulipanua eneo la makao makuu yao lilopo mitaa ya Twiga na Jangwani.


Kwa maelezo ya uongozi wa Yanga, uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watu 40,000.


SENDEU, MWESIGWA WATIMULIWA

Aidha, uongozi wa ‘Wanajangwani’ ulitoa orodha ya watu wanaoidai klabu hiyo hadi kufikia jana, ikionesha kuwa thamani ya madeni hayo inazidi Sh. milioni 200.

Miongoni mwa watu wanaoidai Yanga ni aliyekuwa katibu mkuu wa klabu hiyo, Celestine Mwesigwa (Sh. milioni 183.4) na aliyekuwa afisa habari wao, Louis Sendeu (Sh. milioni 79.9). Wote walisimaishwa kazi Septemba mwaka jana. Wadai wengine ni kampuni mbalimbali, zikiwamo za uwakili, hoteli na usafiri.


Mkutano huo uliamua kuwafuta uanachama Sendeu na Mwesigwa kwa kitendo chao cha kutokubaliana na klabu kuhusiana na fedha wanazodai ili kupata muafaka kwa njia za kiungwana, hasa kwa kuzingatia kuwa nao walikuwa ni Wanayanga.


KADO

Kuhusiana na Kado, gumzo lilikuwa ni kuuzwa kwa kipa huyo kwa Sh. milioni nne kwenda Coastal Union ya Tanga wakati Yanga walimtwaa kwa Sh. milioni 40 kutoka Mtibwa.

Hata hivyo, mwishowe wanachama waliusamehe uongozi kwa uamuzi huo ulioonekana kuwa ulifanywa kimakosa.

 

KAMATI YA UTENDAJI SIMBA SC YAPITISHA KAMATI MPYA


Aden Rage kulia akiwa na Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Hassan Daalal


KAMA ya Utendaji ya Simba imepitia na kuidhinisha majina ya Wajumbe wa Kamati mbalimbali za klabu lengo likiwa kuiboresha klabu na pia kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa ambayo Simba inashiriki mwaka huu.
Taarifa ya Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage, inawapongeza wote walioteuliwa kwa ajili ya kazi hii na kuwatakia mafanikio mema katika kuijenga klabu ili iwe ya kisasa kama walivyo wajumbe wenyewe.
Uteuzi huu wa wajumbe unaanza mara moja na wenyeviti wa kamati hizo wamepewa nguvu ya kuitisha vikao vya kamati zao mapema iwezekanavyo.
Aidha, taarifa hiyo imesema kwamba timu ya Simba inarejea kesho kutoka Oman saa 10 jioni na itaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya African Lyon Jumamosi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
KAMATI MPYA ZA SIMBA SC:
KAMATI YA UFUNDI
1.   DAMIAN MANEMBE-MWENYEKITI
2.   IBRAHIM MASOUD-MAKAMU MWENYEKITI
3.   CRESCENCIUS MAGORI
4.   KHALID ABEID
5.   SAID TULLY
6.   DR. KATEGILE
7.   ZAMOYONI MOGELA
8.   JOHN WILLIAM (DEL PIERO)
9.   YUSUFU MACHO
10.      JEFF LEA
11.      BITA JOHN
12.      SHABAAN BARAZA
KAMATI YA FEDHA
1.   GEOFREY IRICK NYANGE (MWENYEKITI)
2.   RAHMA AL KHALOOS-MAKAMU MWENYEKITI
3.   FRANCIS WAYA
4.   ZITTO KABWE
5.   JUMA NKAMIA
6.   RUGE MUTAHABA
KAMATI YA MASHINDANO
1.   SWEDY MKWABI-MWENYEKITI
2.   SAID PAMBA-MAKAMU MWENYEKITI
3.   SELEMANI ZEDDY. (MB)
4.   JERRY YAMBI
5.   IDDI KAJUNA
6.   CHAUREMBO
7.   GERLAD LUKUMAY
8.   HABBIB NASSA
9.   BUNDALA KABULWA
10.      CHARLES HAMKAH
11.      SAID RUBEYA
12.      ABDULFATAH SALUM (SAPHIRE)
13.      HATIBU MWINYI (BUSTA)
14.      ABDUL  MSHANGAMA
15.      HUMPHREY ZEBEDAYO
16.      MAJALIWA MBASSA
17.      SULEIMAN ZAKAZAKA
18.      KESI MOHAMED RASHID
19.      MOHAMED ISSA MBENA
KAMATI YA PROGRAMU ZA VIJANA
1.   IBARHIM MASOUD –MWENYEKITI
2.   RUGE MUTAHABA-MAKAMU MWENYEKITI
3.   JOSEPH ITANG’ARE-MJUMBE/MLEZI
4.   WILFRED KIDAU
5.   MOHAMED ABDALLAH
6.   SAID TULLY
7.   CANISIUS MASOMBOLA
8.   HAMIS MRISHO
9.   DAMAS NDUMBARO
10.      TALIB HILAL

LIGI KUU LALA SALAMA YAANZA JUMAMOSI, DARAJA LA KWANZA YAPIGWA KALENDA


Pilika za Ligi Kuu
WAKATI mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Jumamosi (Januari 22 mwaka huu), mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) umesogezwa mbele kwa wiki moja ambapo sasa utaanza Februari 2 mwaka huu.
Uamuzi wa VPL kuendelea Januari 26 mwaka huu ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na klabu za ligi hiyo kilichofanyika jana (Januari 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, uamuzi huo umefikiwa huku yakiwepo masharti kadhaa kutokana na uamuzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukamata sh. milioni 157 kwenye akaunti za TFF, fedha ambazo zilitoka kwa mdhamini wa VPL (Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom) kwa ajili ya timu zinazoshiriki ligi hiyo.
Masharti hayo yatawasilishwa na Kamati ya Ligi kwa maandishi kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), nakala kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Awali klabu kupitia Kamati ya Ligi zilisisitiza zisingecheza ligi hadi fedha hizo zitakaporejeshwa.
Kwa upande wa FDL itaanza bila timu ya Small Kids ya Rukwa ambayo imeshushwa daraja kwa mujibu wa kanuni baada ya kushindwa kucheza mechi mbili katika mzunguko wa kwanza.
Kwa mujibu wa kanuni za ligi hiyo, matokeo yote ya mechi ambazo Small Kids ilicheza katika mzunguko huo wa kwanza yamefutwa. (Ratiba ya VPL imeambatanishwa).

SIMBA SC YAKUBALI YAISHE KWA OCHIENG NA KEITA


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akimkabidhi jezi ya timu hiyo, Paschal Ochieng wakati wa kumsajili


KAMATI ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji iliyokutana Januari 19 mwaka huu chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imeliondoa shauri lililokuwa mbele yake dhidi ya klabu ya Simba lililowasilishwa na wachezaji Pascal Ochieng na Daniel Akuffo baada ya pande hizo kufikia makubaliano.
Wachezaji hao kutoka Kenya na Uganda waliwasilisha malalamiko mbele ya kamati wakipinga kukatizwa mikataba yao bila kulipwa stahili zao. Hata hivyo, pande zimefikia makubaliano ya kuvunja mikataba nje ya kamati, na wachezaji hao kulipwa stahili zao.
Aidha, Simba imekiri kudaiwa na wachezaji Shija Mkina, Swalehe Kabali, Victor Costa na Rajab Isiaka na kuahidi kuwalipa wachezaji hao wakati Coastal Union na mchezaji wake Mohamed Issa wamefikia makubaliano ya malipo, hivyo kuvunja mkataba kati ya pande hizo mbili.

KADO AIDHINISHWA KUCHEZA COASTAL UNION, MTIBWA YALA ZA USO


Kado

KAMATI ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ilikutana Januari 19 mwaka huu kupitia maombi ya usajili wa dirisha dogo kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo kipa Shabani Kado ameidhinishwa kuidakia timu ya Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji wengine waliodhinishwa kwenye dirisha dogo na klabu zao kwenye mabano ni Humphrey Mieno, Brian Umony, Jockins Atudo, David Mwantika, Abdallah Seif, Malika Ndeule na Uhuru Selemani- kwa mkopo (Azam), Juma Mdindi, Njaidi Mohamed na Mahmoud Mbulu (Ruvu Shooting), Mohamed Kayi na Emmanuel Gabriel (Tanzania Prisons).
Nurdin Selemani, Shaibu Nayopa, Hamidu Hassan, Paul Malipesa, Josephat Moses, Muharami Mnyangamala, Majaliwa Mbaga na Alphonce Peter (Oljoro JKT), Shukuru Kassim, Chacha Marwa, Salum Machaku, Mzamiru Said, Victor Bundala, Delta Thomas, Edward Mzeru na Tizzo Chomba (Polisi Morogoro), Edmund Kashamila na Julius Mrope (Kagera Sugar).
Rajab Mohamed, Zakayo Joseph, Baraka Anthony na Mussa Chambo (Mtibwa Sugar), Zahoro Pazi- kwa mkopo, Emmanuel Linjechele, Kisimba Luambano na Nashon Naftali (JKT Ruvu), Moaka Shabani, Ismail Mkaima na Damas Milanzi (Mgambo Shooting), Donald Obimma, Exavery Muhollery, Mohamed Hussein na Ulugbe Odia (Toto Africans).
Obadi Mungusa, Juma Seif, Yusuf Mgwao, Ibrahim Job- kwa mkopo, Shamte Ally- kwa mkopo, Buya Jamwaka, Takang Valentine, Nurdin Mussa, Salvatory Jackson, Mohamed Athuman, Athuman Kajembe na Jarufu Kizombi (African Lyon), Mussa Mudde na Abel Dhaila (Simba).
Rashid Simba, Zuberi Hamisi, Shaongwe Ramadhan, Castory Mumbara, Tinashe Machemedze na Shabani Kado (Coastal Union).
Mchezaji Martin Mlolere aliyeombewa usajili Mgambo Shooting kutoka Majimaji amekataliwa kwa vile taratibu za uhamisho hazijakamilika, hivyo anabaki kwenye timu yake ya Majimaji.

AZAM YAKANDAMIZA WAKENYA KWAO, TIMU YAREJEA DAR KESHO NA MAKALI YA KUTISHA


Shujaa wa Azam leo, Mwaipopo

AZAM FC ya Dar es Salaam imemaliza vema ziara yake ya wiki moja nchini Kenya, baada ya kuifunga timu ya Benki ya Biashara Kenya, KCB bao 1-0 kwenye Uwanja wa City, Nairobi jioni hii.
Bao pekee la ushindi la Azam jioni hii limefungwa na kiungo Ibrahim Mwaipopo kwa shuti la mpira wa adhabu katika dakika ya pili ya muda wa nyongeza, baada ya kutimu kwa dakika 45 za kawaida za kipindi cha kwanza.
Hata hivyo, Azam ingeweza kuondoka na ushindi mnene zaidi leo, kama si kiungo wake mwingine Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ kukosa penalti dakika ya 83 baada ya shuti lake la kudakwa na kipa wa KCB.
Huo unakuwa ushindi wa pili katika mechi zake tatu za kujipima nguvu nchini humo, kwani awali bao pekee la Gaudence Exavery Mwaikimba kwa penalti dakika ya 58 juzi liliipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Sofapaka ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Katika mchezo wake wa kwanza, mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi walifungwa mabao 2-1 na AFC Leopard kwenye Uwanja huo huo wa Nyayo.
Pamoja na kufungwa na Leopard, Azam watajilaumu wenyewe, kwani walipoteza penalti mbili kupitia kwa Joackins Atudo na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Mabao ya Leopard katika mchezo huo, yalifungwa na Paul Were na Mike Barasa, wakati la Azam lilifungwa na Sammih Hajji Nuhu kwa penalti.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Malika Ndeule, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika/Omar Mtaki, Joackins Atudo, Kipre Balou/Abdulhalim Humud, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo/Humphrey Mieno, Abdi Kassim, Brian Umony/Uhuru Suleiman na Khamis Mcha/Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Azam kesho watapanda basi lao kuvuka boda la Namanga kurejea nyumbani Dar es Salaam, tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

FLYING EAGLES WASHINDWA KULINDA BAO LAO WATOKA SARE NA BURKINA FASO

ANGALIA RISASI YA SHABA ZAMBIA WALIVYOBANWA MBAVU NA WAHABESHI WA ETHIOPIA 1-1

FALACAO NJE WIKI TATU.JE LITAKUWA PENGO KWA RONALDO KUMKIMBILIA MESSI KATIKA UFUNGAJI WA MABAO LALIGA???????


MATARAJIO madogo ya kuwafikia vinara wa Ligi Kuu nchini Hispania Barcelona, waliyokuwanayo Atletico Madrid yaliingia katika kikwazo Jumapili baada ya mshambuliaji wake tegemeo Radamel Falcao kupata majeruhi ya mguu ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu akijiuguza. Falcao alianza kuchechea wakati akikokota mpira na mara moja aliomba kutolewa katika dakika ya 57 wakati Atletico ilipopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Levante na kupunguza pengo la alama na Barcelona ambao walifungwa mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Real Sociedad. Meneja wa Atletico Diego Simeone alithibitisha kuumia kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia na kudai kuwa anaweza kukaa kwa siku 20 au zaidi. Falcao ameifungia Atletico mabao 18 msimu huu na kuisaidia timu hiyo kukaa katika nafasi ya pili wakiwa alama nyuma ya Barcelona.

AUSTRALIA OPEN: FEDERER, MURRAY WATINGA ROBO FAINALI.


WACHEZAJI nyota wa mchezo wa tenisi, Roger Federer anayeshika namba mbili katika orodha za ubora duniani na Andy Murray anayeshika namba tatu wameonyesha ubora wao kwa kutinga robo fainali ya michuano ya wazi Australia. Federer raia Switzerland alifanikiwa kutinga hatu hiyo baada ya kumfunga Milos Raonic wa Canada kwa 6-4 7-6 6-2 akitumia muda wa saa moja na dakika 53 wakati Murray alimsambaratisha Gilles Simon wa Ufaransa kwa 6-3 6-1 6-3 akitumia muda wa saa moja na dakika 35. Murray sasa takutana na Jeremy Chardy katika hatua ya robo fainali wakati Federer atapambana na Jo-Wilfried Tsonga katika hatua ya robo fainali. Kwa upande wa wanawake bingwa mtetezi wa michuano hiyo Victoria Azarenka ametinga hatua ya robo fainali baada ya kumfunga kirahisi Elena Vesnina na kujiweeka katika nafasi nzuri ya kukwaana na Serena Williams katika hatua ya nusu fainali. Azarenka alimfunga Vesnina kirahisi kwa 6-1 6-1 na kukata tiketi ya robo fainali ambayo atacheza na Svetlana Kuznetsova wakati Williams ambaye anaonekana yuko katika kiwango bora alimsambaratisha Maria Kirilenko kwa 6-2 6-0 na kutinga hatua hiyo.

AUSTRALIA OPEN: FERRER, SHARAPOVA WATINGA NUSU FAINALI

.

MCHEZAJI nyota wa tenisi anayeshika namba nne katika orodha za ubora duniani David Ferrer amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Australia baada ya kumfunga Mhispania mwenzake Nicolas Almagro katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Rod Laver Arena jijini Melbourne. Katika mchezo huo Ferrer ilibidi apambane kiume baada ya kuwa nyuma kwa seti mbili na kufanikiwa kumfunga Almagro kwa 4-6 4-6 7-5 7-6 6-2 ambapo sasa anatarajia kukutana na aidha Novak Djokovic au Tomas Berdych katika hatua ya nusu fainali. Kwa upande wa wanawake mwanadada Maria Sharapova aayeshika namba mbili katika orodha za ubora naye alifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kumuondosha Mrusi mwenzake Ekaterina Makarova. Sharapova sasa atachuana na Li Na wa China ambaye naye alitinga hatua hiyo baada ya kumsambaratisha Agnieszka Radwanska.

PLATINI AMPONGEZA PRINCE BOATENG.


RAIS wa Shirikisho la Soka arani Ulaya, Michel Platini ametofautiana na rais wa Shirikisho la Soka la Dunia Sepp Blatter kuhusu suala la Kevin-Prince Boateng kuwaongoza wachezaji wenzake wa AC Milan kutoka uwanjani baada ya kufanyiwa vitendo vya kibaguzi mapema mwezi huu. Blatter amesema wachezaji hawapaswi kujichukuliwa sheria mkononi ingawa alidai kuwa mashabiki wanaokutwa na hatia ya kufanya vitendo hivyo wanapaswa kuchuliwa hatua aidha kwa klabu kukatwa alama au kufungiwa kabisa. Hatahivyo, Platini aliiambia radio moja nchini Ufaransa kuwa anakiunga mkono kitendo kilichofanywa na nyota huyo wa kimataifa kutoka Ghana kwani tatizo hilo linaonekana kuota mizizi katika siku za karibuni. Platini mwenye umri wa miaka 57 amesema ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa uliofanywa na wachezaji wa Milan na baada ya tukio hilo aliwapigia simu na kuwapongeza.

KIUNGO BORA WA BARCA INIESTA ASEMA ATAMALIZA ZAMA ZAKE ZA SOKA BARCELONA


KIUNGO nyota wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Andres Iniesta amebainisha kuwa hana mpango ya kuondoka katika klabu hiyo na kudai kuwa anataka kutundika daruga akiwa hapo. Iniesta mwenye umri wa miaka 28 ameshacheza mechi zaidi ya 400 katika kikosi cha kwanza cha Barcelona toka alipotoka katika shule ya klabu hiyo na anategemea kuendelea kuwepo zaidi hapo. Akihojiwa Iniesta amesema nia yake ni kucheza mpaka atapostaafu akiwa katika klabu hiyo na kitu pekee kinachoweza kubadilisha ni kiwango chake kwani kama kitashuka na klabu kuamua kumuacha ndio anayoweza kuondoka. Nyota pia alikiri kuwa timu hiyo inakabiliwa na wakati mgumu hivi sasa na wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanarejea katika kiwango chao haraka kabla ya mchezo wa Kombe la Mfalme dhidi ya Malaga.

AFCON 2013: KESHI ATEGEMEA KUMTUMIA MOSES IJUMAA.


NIGERIA inamatarajio kuwa winga wake anayecheza katika klabu ya Chelsea ya Uingereza, Victor Moses atakuwa amepona goti kwa wakati kabla ya mchezo wao wa Ijumaa dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon Zambia. Moses hakuwemo katika kikosi cha nchi hiyo ambacho kilitoa sare ya bao 1-1 na Burkina Faso kwasababu ya kujiuguza goti lake na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji wa Dynamo Kiev ya Ukraine Brown Ideye. Kocha wa Nigeria Stephen Keshi amesema alimwacha kumtumia Moses kuhofia kujitonesha tena lakini ana matumaini winga huyo atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo dhidi ya Zambia. Beki Efe Ambrose anayecheza klabu ya Celtic Glasgow ataukosa mchezo wa Ijumaa baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Burkina Faso na nafasi yake inategemewa kuchuliwa na Kenneth Omeruo.

ALLAN TRAOREEEEEE AIWEZESHA BURKINAFASO KUTOKA SARE NA MANYIGU WA NIGERIA JANA MICHUANO YA MATAIFA AFCON


AFCON_2013_LOGO>>JUMANNE NI: IVORY COAST v TOGO, ALGERIA v TUNISIA!!
BAO la Dakika ya 94 la Alain Traore la kusawazisha, Mchezaji ambe ndie ameifikisha Burkina Faso Fainali AFCON 2013 kwa pia kusawazisha katika Dakika ya 96 walipocheza Mechi ya mwisho ya Mchujo na CAR, Jamhuri ya Afrika ya Kati, limewapa sare ya 1-1 walipocheza na Nigeria waliokuwa wakicheza Mtu 10 katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi C la Fainali za Mashindano ya Mataifa ya Afrika huko Afrika Kusini.
++++++++++++++++++
KUNDI C-MECHI ZINAZOFUATA:
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
++++++++++++++++++
Nigeria ndio walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 23 la Emmanuel Emenike, Mchezaji wa Spartak Moscow, baada ya uchezaji mzuri wa mwenzake Ideye Brown.
Nigeria walijikuta wakicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 73 baada ya Efe Ambrose kupewa Kadi ya Njano ya pili na Refa Mohamed Benouza wa Algeria.
Burkina Faso, wakiwa nyuma kwa Bao 1-0 huku Dakika 90 zikiwa zimeyoyoma na Bango la Muda wa Ziada kuashiria Dakika 4 za ziada, walisawazisha katika Dakika ya 94 kufuatia uzembe wa Difensi ya Nigeria.
VIKOSI:
Nigeria: Enyeama, Echiejile, Yobo, Oboabona, Ambrose, Ogude, Mikel, Igiebor, Ideye, Emenike, Musa
Akiba: Agbim, Obiorah, Egwueke, Moses, Gabriel, Uche, Onazi, Uzoenyi, Mba, Oshaniwa, Omeruo, Ejide.
Burkina Faso: Soulama, Bakary Kone, Keba Paul Koulibaly, Panandetiguiri, Koffi, Djakaridja Kone, Pitroipa, Rouamba, Dah, Bance, Dagano
Akiba: Diakite, Henri Traore, Alain Traore, Ouattara, Balima, Rabo, Kabore, Pan-Pierre Koulibaly, Wilfried Sanou, Abdou Razak Traore, Nakoulma, Germain Sanou. 
Refa: Mohamed Benouza (Algeria)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
[SAA za BONGO]
Jumamosi Januari 19
South Africa 0 Cape Verde Islands 0
Angola 0 Morocco 0
Jumapili Januari 20
Ghana 2 Congo DR 2
Mali 1 Niger 0
Jumatatu Januari 21
Zambia 1 Ethiopia 1
Nigeria 1 Burkina Faso 1
Jumanne Januari 22
Ivory Coast v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Tunisia v Algeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatano Januari 23
South Africa v Angola [Moses Mabhida Stadium Saa 12 Jioni]
Morocco v Cape Verde Islands [Moses Mabhida Stadium Saa 3 Usiku]
Alhamisi Januari 24
Ghana v Mali [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Niger v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast v Tunisia [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Algeria v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumapili Januari 27
Morocco v South Africa [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Cape Verde Islands v Angola [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatatu Januari 28
Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumanne Januari 29
Ethiopia v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Burkina Faso v Zambia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatano Januari 30
Algeria v Ivory Coast [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Togo v Tunisia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]