Friday, January 4, 2013

YANGA KIBARUANI KESHO UTURUKI.


Timu ya Yanga kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na tim ua Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo utakaofanyika mjini Antalya majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati. Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya imekuwa ikifanya mazoezi tangu siku ya jumatatu na wachezaji wote wameonekana kufurahia mazingira ya kambi na huduma zote kwa ujumla. Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tano (5) mfiululizo itatumia mchezo wa kesho dhidi ya timu ya Arminia Bielefed kama kipimo tosha cha maendeleo ya mafunzo yanayoendelea nchini Uuturuki. Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Ernie Brandts amesema anashukuruika wachezaji wake wapo fit kwa ajili ya mchezo kesho, na kwa kuwa hakuna mchezaji majeruhi atakuwa na fursa ya kumtumi amchezaji yoyote katika mechi hiyo. Aidha Brandst amesema kuwa anajua mchezo wa kesho utakua mgumu kwani timu ya Arminia Bielefeld ni timu nzuri na imekua ikishiriki ligi kuu ya ujerumani mara kadhaa, hivyo ni timu ambayo itatoa ushindani mkubwa sana

INNA LILLAHI WA INNA ILAYHI RAJ'UN [MUNGU IWEKE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU JUMA KILOWOKO A.K.A. SAJUKI LEO ALIVYOPUMZISHWA KATIKA MAKABURI YA KISUTU




 Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini Marehemu  Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni, wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.
Mwili wa Marehemu Sajuki ukipakiwa kwenye gari
Dua ikisomwa kabla ya kuondoka kwa Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo

Pamoja na mvua kubwa kunyesha haikuzuia watu kufika kwa aajili ya kuomboleza kifo cha Marehemu sajuki
Waombolezaji wakiwa wanajifunika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar
Mwili wa marehemu Sajuki ukiondoka nyumbani kuelekea makaburi ya Kisutu
 Sehemu ya waliohudhuria msiba wa Sajuki katika makaburi ya Kisutu 
Wadau mabali mbali wakisubiria mwili wa Marehemu Sajuki, huku Profesa Jay akionekana kwa mbali miongoni mwa wanaousubiri mwili.
Umati wa watu ukiwa makaburini Kisutu Dar
 Mwili wa marehemu Sajuki ukiwasili katika makaburi ya Kisutu tayari kwa mazishi
 Rais Kikwete pia alihudhuria mazishi ya marehemu Sajuki
 Jeneza liliobeba mwili wa marehemu Sajuki
Hili ndilo kaburi alilo zikiwa Maehemu Sajuki
 Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
Msanii Z Anto akiswali juu ya kaburi la Marehemu Sajuki.
This is it! Hapa ndipo sajuki amelala! May his soul R.I.P

Inna Lillahi Wa Inna Ilayhi Raj'un

MOUNTAIN BIKER STANDER KILLED IN CRASH.


MWENDESHA baiskeli za milimani raia wa Afrika Kusini, Burry Stander amefariki dunia kutokana na ajali jana huko KwaZulu-Natal na taarifa hizo kuthibitishwa na Chama cha Waendesha Baiskeli nchini humo-CSA. Kwa mujibu wa CSA Stander alikuwa akirejea kutoka mazoezini katika ufukwe wa Shelly Beach ambapo aligongwa na gari na polisi wanafanyia uchunguzi tukio hilo la kusikitisha. Stander mwenye umri wa miaka 25 alikuwa mshindi wa tano katika mashindano ya Cross Country kwenye michuano ya Olympiki iliyofanyika London mwaka jana. Mbali na kushiriki michuano hiyo ya London Stander pia alishiriki mashindano kama hayo ya Cross Country katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika Beijing, China mwaka 2008 na kufanikiwa kushika nafasi ya 15 wakati huo akiwa na miaka 20.

PRINCE-BOATENG AWATUMIA SALAMU ZA 2013 MASHABIKI WABAGUZI.


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana na klabu ya AC Milan, Kevin-Prince Boateng jana amewaongoza wachezaji wenzake kuondoka uwanjani kwa kususia mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya daraja la nne ya Pro Patria baada ya mashabiki kuwafanyia vitendo vya kibaguzi wachezaji weusi. Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Tottenham Hotspurs na Portsmouth alikamata mpira na kuupiga kuelekea kwa mashabiki waliofanya vitendo hivyo katika dakika ya 26 ya mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Busto Arsizio kilometa 20 kaskazini-magharibi mwa jiji la Milan. Mchezo huo ulisitishwa baada ya wachezaji wote wa Milan kuungana na Boateng kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo huku wachezaji wa Pro Patria wakijaribu kuwabembeleza ili warejee kuendelea na mchezo huo. Wachezaji weusi waliolengwa kufanyiwa vitendo hivyo kwenye mchezo huo mbali na Boateng ni pamoja na M’Baye Niang, Urby Emanuelson na kiungo wa zamani wa Portsmouth Sulley Muntari ambapo juhudi za mshehereshaji wa mchezo huo kujaribu kuwakanya mashabiki hao zilishindikana.

AZARENKA AMKWEPA SERENA WILLIAMS


MCHEZA tenisi nyota anayeshika namba moja katika orodha za ubora wa mchezo duniani kwa upande wa wanawake, Victoria Azarenka amejitoa katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya kimataifa ya Brisbane ambapo alikuwa apambane na Serena Williams. Zikiwa zimebakia dakika 30 kabla ya mchezo wake na Williams wa Marekani kuanza, Azarenka ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano ya wazi ya Australia alitangaza kujitoa baada kuumia kidole gumba katika mkono wake wa kulia. Azarenka mwenye umri wa miaka 23 raia wa Belarus amesema amekuwa na maumivu hayo kwa kipindi cha siku kumi na yamekuwa yakiongezeka ndio maana ameamua kujitoa ili apate muda wa kujitibu kabla ya kuanza kwa michuano ya Australia. Nyota huyo amesema kulikuwa na kucha ambayo ilikuwa ikimsumbua katika kidole chake gumba lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele tatizo hilo lilizidi na kumnyima raha ya kucheza kwa kiwango chake.

ULIKUWA UAMUZI RAHISI KUHAMIA CHELSEA - BA.


MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Chelsea, Demba Ba amesisitiza kuwa ulikuwa ni uamuzi rahisi kusaini mkataba na mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya uhamisho wake kuthibishwa na klabu hiyo mapema leo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu akitokea klabu ya Newcastle kwa uhamisho wa paundi milioni 7.5. 
Ba mwenye umri wa miaka 27 ambaye atakuwepo katika benchi la wachezaji wa akiba kwa ajili ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Southampton kesho atakuwa anavaa fulana yenye namba 29. Akihojiwa nyota huyo amesema uamuzi wa kujiunga na Chelsea ulikuwa rahisi kwake haswa ikizingatiwa kuwa timu hiyo ndio mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

AYEW HATIHATI KUSHIRIKI AFCON.


KLABU ya Olympique Marseille ya Ufaransa imesema kuwa mshambuliaji wake nyota Andre Ayew ameumia goti wakati wa mazoezi Januari 2 ambapo waliliandikia Shirikisho la Soka la Ghana-GFA juu ya taarifa hizo. Habari za kuumia kwa Ayew zitakuwa ni pigo lingine kwa kocha wa timu ya taifa ya Ghana baada ya mshambuliaji wake mwingine kati ya wanne aliowateua kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon Yahaya Mohammed naye kuwa majeruhi. GFA nayo imewaagiza Marseille kumuachia Ayew kwenda jijini Abu Dhabi ili waweze kumfanyia uchunguzi wenyewe kama ataweza kushiriki michuano ya Afcon ambayo itafanyika nchini Afrika Kusini kuanzia Januari 19 mwaka huu. Ghana kwasasa ipo UAE kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Misri na Tunisia kabla ya kuelekea nchini Afrika Kusini.

NI SIMBA SC NA TUSKER PATASHIKA KATIKA KOMBE LA MAPINDUZI USIKU LEO AMAAN


Simba SC
SIMBA SC inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa kuanzia saa 2:00 usiku wa leo, kumenyana na Tusker ya Kenya katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi.
Mchezo huo, utatanguliwa na mchezo mwingine wa kundi hilo, kati ya Jamhuri na Bandari kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung kuanzia saa 10:30.
Kocha Msaidizi wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ amesema kwamba mabingwa hao wa Kenya watarajie shughuli tofauti kutoka kwa mabingwa wa Bara leo, tofauti na ilivyokuwa timu hizo zilipokutana wiki iliyopita Dar es Salaam na Tusker wakashinda 3-0.
“Tusker wajue Dar es Salaam hawakuifunga Simba, walikafunga ka Simba, sasa ndio wanacheza na Simba na watake wasitake wataumia,”alisema Julio.
Kocha mpya wa Simba SC ya Dar es Salaam, Mfaransa Patrick Liewig aliyerufahishiwa na uwezo wa wachezaji wa timu hiyo baada ya kuwashuhudia juzi wakiwachapa mabingwa wa Zanzibar, Jamhuri ya Pemba mabao 4-2 kwenye Uwanja huo huo wa Amaan mjini hapa, jana alianza kazi rasmi.
Mfaransa huyo aliyetua Dar es Salaam Jumatatu kabla ya Jumanne kusaini mkataba wa miezi 18 wa kuifundisha timu hiyo na kuja Zanzibar juzi kuungana na timu, leo anaweza kukaa kwenye benchi pamoja na wasaidizi wake, Julio na Mganda, Moses Basena.
Liewig ni kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, ambaye ana Stashahada ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller, anatarajiwa kwenda Zanzibar kesho.
Liewig pia amehudhuria kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Dijon.
Kwa upande wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia mwaka 1989 hadi 1990:  alikuwa Meneja Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi 1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez, 1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia

WAFUNGAJI WA MABAO:
Haruna Chanongo        Simba SC    2
Jesse Were                  Tusker FC    2
Adeyum Saleh              Miembeni     2
Mfanyeje Mussa            Jamhuri       2
Ismail Dunga                 Tusker FC   1
Michael Olunga             Tusker FC   1
Andrew Tolowa              Tusker FC   1
Amour Janja                  Bandari       1
Mohamed Hamdani       Miembeni     1
Rashid Roshwa             Miembeni     1
Juma Mpakala               Mtibwa        1
Felix Sunzu                   Simba SC   1
Shomary Kapombe        Simba SC   1

KIGGI ACHAFUA HALI YA HEWA KAMBINI SIMBA SC


Chanongo akimshukuru Kiggi kwa kona ya bao
KIUNGO wa Simba, Kiggi Makassy jana alimpamia kocha Msaidizi wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo katika mazoezi kwenye Uwanja wa Fuoni, visiwani hapa wakati anawahi mpira akapige kona na hilo limehusishwa na kutolewa kwake dakika ya 27 katika mechi ya juzi, lakini uongozi wa klabu hiyo umesema hakuna kitu kama hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Simba SC, Daniel Manembe amesema hakuna ugomvi kati ya Kiggi na Julio, bali kama ilivyo kawaida ya wanadamu, baada ya tukio hilo la jana maneno yameanza kuwa mengi.
“Ilikuwa bahati mbaya, yule anawahi mpira akapige kona, akampamia Julio kwa bahati mbaya, naomba tafadhali msilitafsiri vibaya tukio hilo, hakuna tofauti yoyote kati ya Julio na Kiggi,”alisema Manembe.  
  asubuhi ya leo imeripoti kuwa Makassy hafurahii maisha Simba SC na lolote linaweza kutokea juu yake wakati wowote.
Kiungo huyo aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu kutoka mahasimu Yanga, amekutana na kile amabcho alikimbia timu yake ya zamani, benchi mfululizo.
Katika mchezo wa juzi wa Kombe la Mapinduzi visiwani hapa, Kiggi alionyesha dhahiri kuchukizwa na kitendo cha kutolewa dakika ya 27 nafasi yake ikichukuliwa na Edward Christopher.
Akitoka kupiga maridadi iliyounganishwa nyavuni na Haruna Chanongo, Kiggi aliitwa benchi kumpisha Edward na alionekana kutoka kwa huzuni na alipofika benchi alikataa hata kupokea chupa ya maji aliyopewa.
Habari zaidi zinasema, tayari Kiggi amekwishaanza mishemishe za kusaka timu nyingine ya kwenda kuchezea baada ya kuona yupo katika wakati mgumu Simba SC.   
Simba SC leo inashuka tena dimbani kumenyana Tusker ya Kenya katika mchezo wa pili wa Kundi A, baada ya kushinda 4-2 dhidi ya Jamhuri ya Pemba juzi. Je, Kiggi atapangwa? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.

STARS KUJIPIMA KWA ETHIOPIA JANUARI 11


Taifa Stars
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Januari 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Stars chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen inatarajia kuingia kambini jijini Dar es Salaam keshokutwa (Januari 6 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo. Mechi hiyo itakuwa kipimo cha mwisho kwa Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.
Ethiopia iko kundi C pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina Faso. Ethiopia itacheza mechi yake ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Zambia.
Katika mechi yake ya mwisho, Taifa Stars iliifunga Zambia bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Desemba 22 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa Machi mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wakati benchi la Ufundi lina Kim, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Katika hatua nyingine, Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatarajia kukutana leo mchana (Januari 4 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itapitia maendeleo ya uchaguzi kwa wanachama wa TFF ikiwemo Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
Wanachama wa TFF (vyama vya mikoa) wote wameshafanya uchaguzi ukiondoa mikoa ya Rukwa na Katavi inayotarajiwa kufanya uchaguzi baadaye mwezi huu. Kwa upande wa vyama shiriki ambavyo bado havijafanya uchaguzi ni Makocha (TAFCA), Wachezaji (SPUTANZA), Waamuzi (FRAT) na Tiba ya Michezo (TASMA).
Vilevile Kamati ya Uchaguzi ya TFF baada ya kikao hicho huenda ikatangaza rasmi mchakato wa uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.

CHAMA CHA SOKA MKOA WA TABORA TAREFA KUKABIDHI VYETI VYA MAKOCHA KESHO UWANJA WA ALLY HASSAN MWINYI



Chama cha soka mkoa wa tabora TAREFA chini ya uenyekiti wa Yusuph Kitumbo kesho kinatarajia kutoa vyeti vya wahitimu ngazi ya preliminary ya ukocha ambao bado hawajapatiwa vyeti vyao,ambao walimaliza mafunzo miaka ya nyuma na a mbao wamemaliza mafunzo hivi majuzi chini ya ukufuzi wa SLIVESTER MARSH kocha msaidizi w atimu ya Taifa ya Tanzania.

Makocha ambao wanatarajia kupatiwa vyeti vyao wale wa awali ni hawa wafuatao,Stephen Paulo Luziga,Hassan Omary Morrocco,Balunda K. Njeno,Emmanuel M,Kahuka,Gidion P.K Masunga,Kopa Rashid,Kopa,Bastidi G Protas,Seif Salim Omary,Joseph R Kitwenya,Maganga J Brighton ,Selemani Ally Malenge,na Fredrick D Jairos.

Wengine wanaotarajia kukabidhiwa vyeti hivyo ni Mashaka S Kalunga,Mohamedy J Mkoko,Emmanuely P Kinandikwa,Gift E Mwinuka,Milambo Camil Yusuph,Eliah John Lusinde,Hamady Hamis Simba,Osborn Mathew Msaka,Reuben Maige Lishim ,Donard S Mlawa,Fedinand S Machunde,Goerge Marriot Kazi,Revocatus M Fundi,Peter Seif Sizya,Joel Mathayo Rukutsa,Charles K Kidifu,Bora Frank Nduguru na Yahaya Masimba Mntangi.

WAKATI HUO HUO Chama cha makocha mkoa wa Tabora TAFCA  kimeamua kuufuta uchaguzi ambao ulikuwa unatarajia kufanyika mkoa Tabora tarehe 10/1/2013 hapa mkoani tabora umefutwa kutokana na wanachama wa TAFCA kuridhia kuwa ni bora kwanza chama kikafufuliwa ili kiwe hai kwani kuna baadhi ya wanachama wanalipa pesa zao za uanachama lakini hawatambuliwi kuwa ni wanachama kutokana na ubazilifu wa pesa kwa baadhi ya viongozi wa TAFCA kuziminya pesa za wajumbe hao.