Saturday, November 24, 2012

MMLAKA YA MAJI TABORA TUWASA YAFANYA BONZA BAB!!!!! KUBWA LEO KATIKA DIMBA LA VITA STADIU

Idara ya maji mkoani tabora  TUWASA leo imefanya bonaza la family day katika uwanja w avita kuanzia majira ya sa moja kamili za asubuhi mpaka saa sita mchana kwa kucheza michezo mbali mbalina timu mwalikwa timu ya MILLENIUM MBOLA.

Michezo iliyofanyika ni pamoja na volley ball,mpira wa miguu,mbio za kupokezana vijii,kukimbiza kuku,kuvuta kamba,kukimbia kwenye magunia na kucheza kwa watoto .

Mchezo wa awali kabisa ulikuwa mchezo wa kukimbia mbio fupi kati ya timu ya millenium na TUWASA na timu ya idara ya maji mkoa wa tabora TUWASA iliweza kuwabwaga millenium ,washindi walioibuka na ushindi kwa tuwasa ni KHAMIS MASHAKA,EDWARD MIHAMBO na ABUBAKARY YUSUPH.

mshindi wa kwanza alichukua kitita cha shilingi elfu 20,000 wa pili 15,000 na watatu shili ngi 10;000 na mchezo uliofuatia ni akina mama wa millenium na tuwasa kukimbia hizo mbio fupi na mshindi aliyeibuka wa kwanza ni NELLY ZEBEDAYO kutoka mbola amejichukulia shilingi elfu 20,000 na mshindi wa pili ni FADHILA LEMBA kutoka mbola naye amejichukulia sh.15,000na watatu ni PRISILA MUSHI kutoka tuwasa na kuzawadiwa sh.10000.

Mchezo uliofuata ni mchezo wa kuvuta kamba kati ya millenium na tuwasa na hapa wafanya kazi wa idara ya maji walionyesha umwamba wao kwa kuwaburuza wafanyakazi kutoka millenium na kujinyakulia kitita cha sh.30,000 na cheti.

Timu hizi zilioneshana umwamba tena katika mchezo wa volleyball na timu ya TUWASA iliibuka na ushindi kwa kujinyakulia pointi 45-13 za millenium na kuzawadiwa kitita cha shilingi elfu 50,000 pamoja na cheti.

Mchezo uliofuatia ni mchezo wa wa kukimbia kwenye gunia kati ya timu zote hizi ya tuwasa na millenium  kwa upande wa wanawake na mwanadada PRISILA MUSHI kutoka tuwasa  alionesha ujuzi wake baada ya kuibuka kinara na kuchukua kitita cha shilingi  elfu 20,000 na kufuatiwa na wadada wenzakke kutoka tuwasa nafasi ya pili ilichukuliwa na  REBECA MALALE  na kupewa 15,000 naye kutoka tuwasa na ya tatu ikachukuliwa na MARY MUSHI na kuzawadiwa shilingi elfu 10000.

Na mpira wa miguu ulifuata kati ya timu ya wafanyakazi wa millenium mbola na timu ya wafanya kazi ya TUWASA na timu ya  millenium imeweza kuchomoza na ushindi wa mabao 10-9 kwa mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kufungana bao 2-2 katika dakika 90 za kimchezo na timu ya millenium kukabiziwa kitita cha shillingi laki moja 100,000 pamoja na cheti.

Mchezo wa mwisho ulikuwa ni mchezo wa watoto kushindana kucheza index,,,,,,,,index waswahili wanasema kiduku na watoto wanne wa wafanya kazi wa tuwasa hao waliweza kuibuka na ushindi na kila mmoja kuzawadiwa kitita cha shilingi elfu tano kila mmoja.

Na nafasi ya mwisho ilikuwa ya kutoa zawadi kwa watumishi wa tuwasa waliomaliza muda wao wa utumishi nao ni MR.MRISHO,ROSEMARY MERICHERY,MR.SEIF SHOMARY,MR.SHABANI ATHUMAN,MR.NASSORO NGWASA,MR.GAUDENCE JANUARY,MR.UMEME DAIEL na MR.ALLY MTIPULA na kila mmoja kuzawadiwa shilingi laki moja [100,000]kila mmoja na cheti.

 



STARS WALALAMIKIA UWANJA MBOVU WA MAZOEZI KAMPALA

Kevin Yondan aliyeipa mgongo kamera (5) akitaniana na wenzake

TIMU ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars imelalamikia Uwanja mbovu wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, waliopelekwa kufanya mazoezi leo kujiandaa na mechi ya kesho ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge 2012 dhidi ya Sudan, itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini hapa.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura amewasilisha malalamiko hayo kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Rodgers Mulindwa ambaye ameahidi kuyafanyia kazi.
“Tutalifanyia kazi suala hilo, tutakuwa na kikao kesho litawasilishwa na litapatiwa usumbufu, mwanzo huwa na matatizo, lakini mambo yatakuwa mazuri,”alisema Mulindwa.
Hata hivyo, inashangaza Stars kupelekwa katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara, wakati kwenye mpango wa awali kabisa wa FUFA ilitakiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nakawa.    
Kwa upande wake, kocha wa Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesikitishwa na kutowasili kwa washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
“Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika, lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.
“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.
Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo zitacheza leo pia.
Kipa wa Kilimanjaro Stars, Juma kaseja akitoka Uwanja baada ya
kumalizika kwa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha
Kampala Kampasi ya biashara nchini Uganda jana. Stars inadhaminiwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Edward Christopher
akikokota mpira wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo
Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara nchini Uganda jana kwa kujianda
na mchezo wa michuoano ya Cecafa. Stars inadhaminiwa na Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakitoka Uwanjani baada ya kufanya
mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Kampala Kampasi ya Biashara
nchini Uganda jana. Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium
Lager


KILI STARS NDANI YA KAMPALA TAYARI KWA TUSKER CHALLENGE 2012

Mshambuliaji wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, John Bocco wa Azam FC ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, akiwangoza wenzake kutoka Uwanja wa Ndege wa Entebe, Uganda jana kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Tusker Challenge inayoanza leo mjini hapa Kampala, Uganda. Stars imefikia hoteli ya Mt Zion na itakuwa ikifanya mazoezi Nakawa, wakati kesho itaanza kampeni zake kwa kumenyana na Sudan, Uwanja wa Mandela, Namboole sa 12:00 jioni.

BENITEZ AWATIMUA LAMPARD, COLE BAADA YA KIKAO CHA SAA TATU NA ABRAMOVICH


MAGWIJI wa Chelsea, Frank Lampard na Ashley Cole wataondoka mwishoni mwa msimu baada ya Rafa Benitez kuthibitisha kubomoka kwa kikosi cha ubingwa cha Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wachezaji wote hao wanamaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu na kocha mpya wa Chelsea amesema hawastahili kuendelea kubaki Stamford Bridge baada ya msimu huu.
Lampard, mfungaji bora namba tatu wa kihistoria wa Chelsea, ameshinda mataji matatu ya Ligi Kuu England, manne ya FA na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika miaka yake 11 ndani ya klabu hiyo.
Going: Ashley Cole and Frank Lampard (below) will be allowed to leave Chelsea
Safari: Ashley Cole na Frank Lampard (chini) watatemwa Chelsea
Legend: Frank Lampard
Cole, aliyejiunga na Chelsea akitokea Arsenal mwaka 2006, ameshinda taji la Ligi Kuu ya England, manne ya FA na Ligi ya Mabingwa kwa kipindi chake cha kuishi Stamford Bridge.
Benitez alionekana kwenye picha na Mkurugenzi wa Ufundi, Michael Emenalo wakiwa kwenye chakula cha usiku na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich.
"Nilitumia saa kama mbili au tatu na mmiliki, tulizungumzia kila kitu. Anafahamu mawazo yangu, lakini hatukuwa na muda wa kutosha pamoja. Labda wakati mwingine tena.
"Kama unajiamini na kujieleza, kila mmoja anaweza kukuelewa. Mtazamo wangu kwa mmiliki, ni mtu mzuri. Unaweza kuzungumza naye na ni mwelewa. Anapenda kuona una mawazo mazuri
Short term: Rafa Benitez still plans to use the players until their contracts are up
Mipango ya muda mfupi: Rafa Benitez anataka kuendelea na wachezaji waliopo Chelsea hadi mwisho wa mikataba yao
Not just Torres: Benitez wants to improve the whole team
Si Torres pekee: Benitez anataka kuiboresha timu nzima
 
 
 

ABOU-TRIKA AMONG THREE NOMINEES OF AFRICAN BASED PLAYER OFO THE YEAR AWARD.

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetangaza orodha ya majina matatu ya wachezaji wanaocheza soka barani Afrika watakaogombania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2012.  
 
Majina hayo yaliyotajwa na CAF ni pamoja na wachezaji wa kimataifa wa Zambia ambao wanacheza katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Reinford Kalaba na Stopila Sunzu pamoja na nyota wa kimataifa wa Misri na klabu ya Al Ahly Mohamed Abou-Trika. 
 
 Wachezaji nyota wa timu ya Esperance ya Tunisia Youssef Msakni na Tannick N’Djeng waliachwa katika orodha hiyo pamoja na kukiongoza kikosi cha timu hiyo katika mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa ya Afrika ambao walipoteza kwa Al Ahly kwa mabao 3-2.  
 
Mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa katika sherehe zitakazofanyika jijini Accra, Ghana Desemba 20 mwaka huu.

REDKNAPP KUINOA QPR.

HARRY Redknapp ametajwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Queens Park Rangers kufuatia kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Mark Hughes. 
 
 Redknapp ambaye alitimuliwa katika klabu ya Tottenham Hotspurs June mwaka huu amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ambayo haijashinda mchezo hata mmoja katika Ligi Kuu nchini Uingereza msimu huu.  
 
Katika taarifa iliyotumwa katika wavuti wa klabu hiyo wasaidizi wa Hughes, Mark Bowen na eddie Niedzwiecki ndio watakaokuwa makocha wa muda wakati wa mchezo dhidi ya Manchester United na Redknapp atakuwa akitazama mchezo huo jukwaani.  
 
Akihojiwa mara baada ya uteuzi huo Redknapp mwenye umri wa miaka 65 amesema kuwa amefurahishwa kuinoa klabu hiyo pamoja na changamoto zilizopo mbele yake za kuhakikisha klabu hiyo inarejesha makali yake ili kuepuka balaa la kushuka daraja.

ARSENAL YALAMBA MKATABA MNONO.

KLABU ya soka ya Arsenal, imekubali kuongeza mkataba wenye thamani ya paundi milioni 150 kwa ajili ya udhamini wa fulana wa kampuni ya ndege ya Emirates.  
 
 
Mkataba huo mpya ambao utamalizika mwishoni mwa msimu wa 2018-2019 utakuwa na thamani ya paundi milioni 30 mwaka kwa timu hiyo inayotoka kaskazini mwa jiji la London.  
 
Ofisa Mkuu wa klabu hiyo Ivan Gazidis alithibisha katika wavuti wao juu makubaliano yaliyofikiwa katika mkataba huo mpya ambao utaifanya kuwa mojawapo ya vilabu zenye mikataba minono ya fulana zake.
 
 Gazidis ameapa kuwa meneja wa klabu hiyo Arsenal Wenger atapewa sehemu ya pesa hizo ili kuimarisha kikosi chake kiweze kukata kiu ya mashabiki wake kwa kunyakuwa kombe mwishoni mwa msimu. 
 
 Chini ya mkataba huo kampuni ya Emirates itaendelea kutumia jina lake katika uwanja wa Arsenal mpaka 2028.

MENEZES ATIMULIWA KUINOA BRAZIL.

Shirikisho la Soka nchini Brazil limetangaza kusitisha mkataba na kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Mano Menezes.  
 
 
Menezes amekuwa akiandamwa na wadau wengi wa soka nchini Brazil kwa kushindwa kuifanya timu kurejesha makali yake ya miaka ya nyuma kitu mara nyingi shirikisho la nchi hiyo limekuwa likifumbia macho lawama hizo.
 
 
 Kocha huyo ambaye amechukua mikoba ya kuinoa timu hiyo mwaka 2010 amekuwa akiandamwa kwa kushindwa kuiongoza Brazil kunyakuwa medali yake ya kwanza ya dhahabu katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini London mwaka huu pamoja na kutolewa kwa timu hiyo kushiriki michuano ya Copa America mwaka 2011.  
 
 
Shirikisho hilo limesema kuwa kocha mpya ambaye atachukua nafasi ya Menezes atatangazwa mapema Januari mwakani.

ESSIEN HATI HATI KUCHEZA MWAKA HUU.

KIUNGO wa kimataifa wa Ghana, Michael Essien bado hajajua rasmi lini atarejea tena uwanjani na kuna uwezekano wa kutocheza tena mwaka huu kutokana majeruhi yanayomsumbua.  
 
 
Majeruhi yanayomsumbua Essien ambayo bado madaktari wa timu hiyo hawajayachunguza kwa undani yamekuwa yakimzuia mchezaji kushindwa kufanya mazoezi na timu hiyo.  
 
 
Essien amekuwa akikumbwa na tatizo la kuwa majeruhi kwa muda mrefu kabla ya hajanunuliwa kwa mkopo kutoka Chelsea kitu ambacho kimemfanya kushindwa hata kuitumikia timu yake ya taifa ya Ghana. 
 
 
 Tatizo la Essien lilianza wakati wa mchezo dhidi ya timu ya Real Mallorca, baada ya kucheza dakika 90 katika michezo mitatu mfululizo dhidi ya Celta Vigo, Borussia Dortmund na Mallorca.