Thursday, October 18, 2012

NGASSA AAHIDI MAMBO YA HATARI SIMBA SC

Mrisho Ngassa; Nipeni muda muone mambo ya hatari

KIUNGO Mrisho Khalfan Ngassa, amesema kwamba bado anaizoea taratibu staili ya uchezaji ya timu yake mpya, Simba SC na nafasi mpya anayopangwa kwa sasa na anaamini hadi Januari mwakani atakuwa ameizoea na kufanya ‘mambo ya hatari’.
Akizungumza   jana, Ngassa alisema kwamba Simba wanacheza mfumo tofauti na ambao ulikuwa unatumiwa na timu yake ya zamani, Azam FC hivyo anaendelea kujifunza na kuizoea.
“Mchezaji unapoingia timu mpya, kawaida unakutana na mambo mengi mapya, inabidi sana ujifunze na kuzoea.  Unacheza na watu wapya, ambao inabidi ujifunze namna ya kucheza nao na kuzoeana nao,”alisema Ngassa.
Ngassa alisema angalau anekutana na wachezaji ambao anacheza nao timu ya taifa, lakini safu ya ushambuliaji ya Simba inaundwa na wachezaji wengi wa kigeni kama Emmanuel Okwi, Daniel Akuffo na Felix Sunzu.
“Inabidi sana nijifunze taratibu, hata hivyo najisifu kwamba naendelea vizuri na hadi kufika Januari hivi, nitakuwa nimekwishazoea na kufanya mambo ya hatari,”alisema Ngassa na kusistiza hajashuka kiwango, ni mazingira mapya tu.    
Ngassa juzi alifunga bao lake la tatu tangu ajiunge na Simba Agosti mwaka huu, akitokea Azam FC wakati Simba ikilazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja, akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.

AZAM WAPO CHAMAZI TANGU JANA USIKU TAYARI KWA KIPUTE NA JKT RUVU JUMAPILI

Kikosi cha Azam

AZAM FC imerejea Dar es Salaam jana majira ya saa 1:00 ikitokea Mbeya, ambako juzi ililazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Azam sasa wanaingia kambini kujiandaa na mchezo wao ujao, Jumapili dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex, Dar es Salaam. 
Pamoja na sare hiyo, Azam wamelalamikia uchezeshaji mbaya wa marefa wa mechi hiyo, kwamba uliwapokonya ushindi.
Azam FC wanadai refa alikataa mabao yao mawili yaliyofungwa na Abdi Kassim ‘Babbi’ na penalti ya wazi, baada ya kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ kuangushwa kwenye eneo la hatari
Wanadai bao la kwanza, refa alilolikataa ulikuwa ni mkwaju wa mbali wa Abdi Kassim ambao ulitinga nyavuni, kabla ya kurudi uwanjani na refa licha ya kuona kuwa lilikuwa ni bao halali, bado akaamua kukataa
Wanadai baadaye, Sure Boy alifanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari na kwa mshangao wa wengi, wakiwemo viongozi na wachezaji wa Prisons ambao walishashika vichwa, refa akapeta na mpira kuendelea
Zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mpira kumalizika, Azam FC wanadai walipata adhabu ndogo na Abdi Kassim aliupiga mpira ule na kutinga nyavuni, lakini kwa mara nyingine tena refa akakataa bao kwa madai kuwa kabla ya kufunga, Babbi alikuwa ameotea.
Baada ya ‘kufanyiwa dhuluma’ hiyo, Azam wanaendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa wana pointi 17, baada ya kucheza mechi sana, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wapo kileleni kwa pointi zao 18 na wamecheza mechi nane.  

BAHANUZI, YONDAN HAWAPO KESHO YANGA NA RUVU

Bahanuzi

BEKI Kevin Yondan na mshambuliaji Said Bahanuzi wataendelea kuwa nje ya Uwanja mwishoni mwa wiki, wakati timu yao, Yanga SC itakapokuwa ikiwania pointi tatu katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutokana na hali zao kutoimarika.
Wawili hao ambao ni majeruhi, wapo kwenye programu ya mazoezi mepesi na hadi jana hakuna mmoja kati yao aliyekuwa tayari kuanza programu kamili ya mazoezi ya kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
Maana yake, Mbuyu Twite ataendelea kucheza pamoja na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika beki ya kati, wakati Jerry Tegete ataendelea kucheza na Didier Kavumbangu katika safu ya ushambuliaji.
‘Dogo’ Simon Msuva amemaliza adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa Oktoba 3, mwaka huu katika mechi dhidi ya Simba na Hamisi Kiiza amerejea kutoka Uganda, alipokwenda kuichezea timu yake ya taifa, The Cranes katika mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.
Uganda ilitolewa na Zambia kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, Zambia wakianza kushinda nyumbani 1-0 na Uganda wakashinda kwao 1-0 pia mwishoni mwa wiki, hivyo mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti, ambako timu ya Kiiza ilitolewa.
Yanga imeweka kambi katika hoteli ya Uplands, Changanyikeni, Dar es Salaam huku ikiendelea kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Beki Kevin Yondan aliyeumizwa na kiungo wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ katika mechi baina ya wapinzani hao wa jadi, Oktoba 3, mwaka huu, wakati Bahanuzi ‘Spider Man’ alichanika nyama za paja la mguu wa kulia katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba Oktoba 8, mwaka huu.
Bahanuzi aliumia dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete katika mechi ambayo Yanga ililala 1-0, beo pekee la Themi Felix.
Bahanuzi ndiye tegemeo la mabao la Yanga kwa sasa, kwani tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, ameifungia mabao 12 katika mechi 13, ikiwemo ile dhidi ya Kagera aliyocheza kwa dakika 23 kabla ya kuumia na kutoka. 
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 11, baada ya kucheza saba, kushinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili.
Simba iliyocheza mechi nane, inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 18, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 17, iliyocheza mechi saba.

VPL: Wikiendi Taifa ni Yanga v Ruvu Shooting, Simba v Mgambo Tanga!

VPL_LOGOLIGI KUU VODACOM itanguruma tena Wikiendi hii na Jumamosi Vigogo Yanga, ambao sasa wameafikiana na Wadhamini VODACOM kuhusu Nembo kwenye Jezi zao, wapo nyumbani Uwanja wa Taifa, Dar es Saalam kucheza na Ruvu Shooting na Mahasimu wao Simba watacheza ugenini Jumapili huko Mkwakwani na Timu ‘íliyofufuka’ kwa kushinda Mechi 3 mfululizo, Mgambo JKT.
>>BONGO, KENYA-Sisi Sote ni Ndugu wapyaaa!
>>SIMBA v KAGERA: Watazamaji 9,842 watengeneza Milioni 58!!
RATIBA:

Jumamosi Oktoba 20
Yanga v Ruvu Shootings
Coastal Union v Mtibwa Sugar [Mkwakwani, Tanga]

Jumapili Oktoba 21
JKT Ruvu v JKT Oljoro [Azam Complex, Dar es Salaam]
Mgambo JKT v Simba [Mkwakwani, Tanga]
Tanzania Prisons v Toto Africans [Sokoine, Mbeya]
++++++++++++++++++++++++++
Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, na Shirikisho la Soka Kenya,FKF, wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuinua kiwango cha mpira wa miguu katika nchi hizo.
TAARIFA YA TFF:
Release No. 171
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 18, 2012

TFF, FKF ZAANZISHA USHIRIKIANO MPYA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuinua kiwango cha mpira wa miguu katika nchi hizo.

Akizungumza baada ya mkutano uliowakutanisha vinara wa mashirikisho hayo Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema wameamua kurejesha uhusiano huo uliokuwepo zamani baada ya kuwepo utulivu katika uendeshaji mpira wa miguu nchini Kenya.

Amesema maeneo ya ushirikiano ambayo wameagiza yafanyiwe kazi na sekretarieti za pande zote (TFF na KFF) ili baadaye yaingizwe katika Hati ya Makubaliano (MoU) ni mafunzo, waamuzi, mechi za timu za Taifa za wakubwa, vijana na wanawake, na Ligi Kuu.

Rais Tenga pia amesema wameamua kuwepo ziara za mafunzo (study tours) katika maeneo mbalimbali ambapo kwa Kenya wao Ligi Kuu yao iliingia katika mfumo wa kampuni mapema, hivyo itakuwa fursa nzuri kwa Bodi ya Ligi Kuu ambayo iko kwenye mchakato wa kuanzishwa kupata uzoefu kwa wenzao wa Kenya.

Naye Rais wa FKF, Sam Nyamweya aliyefuatana na Makamu wake wa Rais, Robert Asembo amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya ni wa kihistoria, hivyo wameamua kuuanzisha upya kwa faida ya nchi hizo.

Amesema hivi karibuni FKF ilichukua waamuzi kutoka Tanzania waliochezesha mechi ya kirafiki kati ya Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana), hivyo wameamua kubadilishana waamuzi kwa lengo la kuwaongezea uzoefu.

“Waamuzi wa Tanzania walichezesha vizuri mechi ile. Unajua kwetu kuna upinzani mkubwa katika klabu kama AFC Leopards na Gor Mahia, ukipanga refa utasikia wengine wanalalamika, mara huyo ni Mjaluo. Hata akichezesha vizuri bado watalalamika tu kutokana na upinzani uliopo katika klabu hizo,” amesema.

Rais Nyamweya ameongeza kuwa ili kuondoa malalamiko katika mechi za aina hiyo wanaweza kuchukua waamuzi kutoka Tanzania, na vilevile waamuzi kutoka Kenya wakachezesha mechi za aina hiyo nchini Tanzania.
Amesema vilevile wamepanga kuangalia uwezekano wa kuwa na mechi za kuandaa timu kabla ya kuanza Ligi Kuu za nchi hizo ambapo washindi watatu au wanne wa kwanza katika ligi hizo kushindana.

Kwa upande wa mafunzo, wamekubaliana kuwa kwa vile kila nchi ina wakufunzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na la Afrika (CAF) watawatumia kuandaa mafunzo ya mara kwa mara kwa waamuzi, makocha, madaktari wa tiba ya michezo na viongozi badala ya kusubiri mafunzo ya aina hiyo kutoka kwa mashirikisho hayo ya kimataifa.

PAMBANO LA SIMBA, KAGERA SUGAR LAINGIZA MIL 58/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera Sugar lililochezwa jana (Oktoba 17 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 limeingiza sh. 58,505,000.
Watazamaji 9,842 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 11,013,785.54 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,924,491.53.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 440,000, mtathimini wa waamuzi sh. 254,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,183,890. Gharama za mchezo sh. 3,671,261.85, uwanja sh. 3,671,261.85, Kamati ya Ligi sh. 3,671,261.85, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,202,757.11 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,468,504.74.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
++++++++++++++++++++++++++

MSIMAMO VPL:
1 Simba Mechi 8 Pointi 18
2 Azam FC Mechi 7 Pointi 17
3 JKT Oljoro Mechi 8 Pointi 13
4 Kagera Mechi 8 Pointi 12
5 Yanga SC Mechi 7 Pointi 11
6 Coastal Mechi 7 Pointi 10
7 JKT Ruvu Mechi 8 Pointi 10
8 Prisons Mechi 7 Pointi 9
9 Ruvu Shooting Mechi 7 Pointi 9
10 JKT Mgambo Mechi 8 Pointi 9
11 Mtibwa Sugar Mechi 6 Pointi 8
12 Toto African Mechi 8 Pointi 7
13 African Lyon Mechi 8 Pointi 7
14 Polisi Moro Mechi 8 Pointi 2
 
LIGI za ULAYA: Zarudi tena kilingeni!

BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAA>>LA LIGA, SERIE A & BUNDESLIGA ni moto Wikiendi!!
Kufuatia ‘vakesheni’ ya Wiki mbili ya Ligi huko Barani Ulaya kupisha Mechi za Kimataifa kwa mujibu wa Kalenda ya FIFA, Ligi Vigogo, zile za La Liga, Serie A na Bundesliga, zitarudi tena kilingeni Wikiendi hii na Bundesliga itakuwa ya kwanza dimbani kwa Mechi pekee ya Ijumaa Oktoba 19 kati ya TSG Hoffenheim na SpVgg Greuther Fürth ndani ya Rhein-Neckar-Arena.
ZIFUATAZO ni RATIBA na MISIMAMO ya Ligi hizo:

LA LIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Jumamosi Oktoba 20
Málaga v Valladolid [Estadio La Rosaleda]
Real Madrid v Celta Vigo [Estadio Santiago Bernabéu]
Valencia v Athletic Bilbao [Estadio Mestalla]
Deportivo La Coruña v Barcelona [Estadio Riazor]

Jumapili Oktoba 21
Getafe v Levante [Coliseum Alfonso Perez]
Espanyol v Rayo Vallecano [Cornellà - El Prat]
Granada v Real Zaragoza [Estadio Los Cármenes]
Osasuna v Real Betis [Estadio El Sadar]
Real Sociedad v Atlético Madrid [Estadio Anoeta]

Monday, October 22, 2012
Sevilla FC v Mallorca [Estadio Ramon Sanchez Pizjuan]
================================
MSIMAMO:
[Timu za juu tu]
[Kila Timu imecheza Mechi 7]
1 Barcelona Pointi 19
2 Atletico Madrid 19
3 Malaga 14
4 Real Betis 12
5 Real Madrid 11
6 Real Mallorca 11
7 Sevilla 11
8 Real Valladoid 10
9 Getafe 10
10 Rayo Vallecano 10
================================

SERIE A
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Jumamosi Oktoba 20
Juventus v Napoli [Juventus Stadium]
Lazio v AC Milan [Stadio Olimpico]

Jumapili Oktoba 21
Cagliari v Bologna [Sant'Elia]
Atalanta v Siena [Atleti Azzurri d'Italia]
Chievo Verona v Fiorentina [Bentegodi]
Inter Milan v Catania [Stadio Giuseppe Meazza]
Palermo v Torino [Renzo Barbera]
Parma v Sampdoria [Ennio Tardini]
Udinese v US Pescara [Stadio Friuli]
Genoa v AS Roma [Luigi Ferraris]

MSIMAMO:
[Timu za juu tu]
[Kila Timu imecheza Mechi 7]
1 Juventus Pointi 19
2 Napoli 19
3 Lazio 15
4 Inter Milan 15
5 AS Roma 11
6 Fiorentina 11
7 Catania 11
8 Sampdoria 10 [Wamekatwa Pointi 1]
9 Genoa 9
10 Torino 8 [Wamekatwa Pointi 1]
11 AC Milan 7
================================

BUNDESLIGA
[Kwenye Mabano Jina la Uwanja]
Ijumaa Oktoba 19
TSG Hoffenheim v SpVgg Greuther Fürth [Rhein-Neckar-Arena]

Jumapili Oktoba 20
Bayer Leverkusen v Mainz [BayArena]
Borussia Dortmund v Schalke 04 [Signal-Iduna-Park]
Eintracht Frankfurt v Hannover 96 [Commerzbank-Arena]
Fortuna Düsseldorf v Bayern Munich [LTU Arena]
VfL Wolfsburg v SC Freiburg [Volkswagen Arena]
Werder Bremen v Borussia Monchengladbach [Weserstadion]

Jumapili Oktoba 21
Nurnberg v FC Augsburg [EasyCredit-Stadion]
Hamburg SV v VfB Stuttgart [HSH Nordbank Arena]
=================================

MSIMAMO:
[Timu za juu tu]
[Kila Timu imecheza Mechi 7]
1 Bayern Munich Pointi 21
2 Eintracht Frankfurt 16
3 Schalke 14
4 Borussia Dortmund 12
5 Hannover 11
6 Bayer Leverkusen 11
7 Fortuna Dusseldorf 10
8 Hamburger 10
9 Mainz 10
10 Borussia Dortmund 9
=================================
 
CAF CHAMPIONZ LIGI: Nani Fainali kujulikana Wikiendi hii!!

>>SAMATTA: Ataibeba Mazembe ugenini kuwafurahisha Wabongo?
NUSU FAINALI:
[MARUDIANO]
[SAA za BONGO]
Jumamosi Oktoba 20         
22:30 Espérance Sportive de Tunis v TP Mazembe [Stade El Menzah]

Jumapili Oktoba 21         
20:30 Al Ahly v Sunshine Stars [Cairo International Stadium]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Baada ya sare katika Mechi zote mbili za kwanza za Nusu Fainali za kusaka Klabu Bingwa Afrika, CAF CHAMPIONZ LIGI, Mabingwa watetezi Eseperance ya Tunisia na Vigogo Al Ahly wote wako nyumbani huku macho, masikio na dua za Watanzania wengi zikimwombea mwenzao Straika shupavu Mbwana Ally Samatta apate mafanikio kwa kuivusha Klabu yake Tout Poissant Mazembe ya Congo DR ugenini watakaporudiana na Esperance.
Wiki mbili zilizopita, TP Mazembe ikicheza nyumbani Lubumbashi ilitoka 0-0 na Esperance na safari hii huko Tunisia hamna budi ila magoli yapatikane ili kupata Mshindi atakaesonga Fainali.
Mazembe, ambao tegemezi lao ni Straika Samatta na Mputu, wataingia kwenye Mechi hii bila Stoppila Sunzu ambae ana Kadi na huenda wakawakosa majeruhi Rainford Kalaba na Hichani Himonde, wote wanatoka Zambia.
Tegemezi kubwa kwa Esperance ni Straika wa Ghana Harrison Afful, ambae Msimu uliopita ndie aliwapa Ubingwa kwa kufunga bao la ushindi kwenye Fainali, na Youssef Msakni.
Katika Mechi nyingine itakayochezwa bila ya Watazamaji huko Cairo, Misri, Al Ahly watakuwa nyumbani kuwakaribisha Sunshine Stars ambayo walitoka nayo sare ya bao 3-3 huko Ijebu Ode, Nigeria.
NUSU FAINALI:
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 6        
Sunshine Stars [Nigeria] 3 Al Ahly [Egypt] 3
Jumapili Oktoba 7         
TP Mazembe [Congo, DR] 0 Espérance Sportive de Tunis [Tunisia] 0
 
NAE Cole apigwa Faini…..SPAIN: Copa del Rey, Barca, Real kukutana Nusu Fainali??

ASHLEY_COLEHuko England, mara baada ya Nahodha wa Chelsea John Terry kunyoosha mikono juu na kukubali adhabu yake aliyopewa na FA ya kufungiwa Mechi 4 na Faini Pauni 220,000 huku akiomba radhi, mwenzake wa Chelsea Ashley Cole amepigwa Faini na FA ya Pauni 90,000 kwa kuikashifu kwenye Twitter wakati pia Klabu ya Chelsea imetangaza ‘kumshikisha adabu’ Terry kwa siri na huko Spain Droo ya Copa del Rey imefanywa na upo uwezekano kwa Mahasimu wakubwa, Real Madrid na Barcelona, kukutana Nusu Fainali.
>>KISIRISIRI: Chelsea yatangaza ‘kumshikisha adabu’ Terry kwa Ubaguzi!
>>‘KICK IT OUT’ yapinga Chelsea kumwadhibu kwa siri Terry!!
Chelsea na ‘Wabaguzi!’
Beki wa Chelsea na England, Ashley Cole, leo amepigwa Faini ya Pauni 90,000 na FA, Chama cha Soka England, kwa kosa la kutoa maneno yenye kashfa dhidi ya FA kwenye mtandao wa Twitter.
Cole, ambae alikubali makosa na kuomba radhi mara baada ya kushitakiwa, alitoa maneno hayo mara baada ya FA kumpata na kosa John Terry na kumwadhibu huku wakiuita ushahidi wa Ashley Cole kwenye Kesi hiyo kuwa hauaminiki na kuwapanga, kitu ambacho kilimwudhi Cole.
Wakati huo huo, Klabu ya Chelsea ambayo imekuwa ikilaumiwa na Wadau wanaopigania usawa kwenye Soka, Kundi la ‘Kick It Out’, ambalo hutaka ubaguzi utokomee kwenye Soka, imetangaza kuwa mara baada ya John Terry kuamua kutokata Rufaa kupinga adhabu yake, imemwadhibu Terry kwa ubaguzi lakini haiwezi kutangaza adhabu hiyo kwa vile ndio Msimamo wa Klabu yao kutotangaza adhabu za ndani ya Klabu.
Lakini Msimamo huu wa Chlesea umepingwa na Mwenyekiti wa ‘Kick It Out’, Lord Herman Ouseley, ambae amesema unaibomoa Chelsea na kuifanya ionekane si wa wazi kwenye Ubaguzi.

DROO ya COPA del REY
Huko Spain, FC Barcelona, Mabingwa watetezi wa Kombe la Mfalme, Copa del Rey, wamepangwa kukutana na Timu ya Daraja la chini Alaves kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 32 kwenye Drro iliyofanyika leo ambayo pia imepanga Mechi zote hadi hatua ya Nusu Fainali.
Timu nyingine ya Daraja la chini liitwalo Segunda B, Alcoyano, imepangwa kucheza na Mabingwa wa La Liga, Real Madrid, kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
Wapinzani wa Barcelona, Alaves, wanakumbukwa sana pale kwenye Msimu wa Mwaka 2000/01 walipocheza vizuri na kufika Fainali ya UEFA CUP walipotolewa na Liverpool kwa Bao 5-4 katika Mechi iliyoamuliwa kwa ‘Goli la Dhahabu’ katika muda wa nyongeza.
Katika Droo hiyo ya leo, upo uwezekano kwa Mahasimu, Barcelona na Real Madrid, kukutana kwenye hatua ya Nusu Fainali ikiwa watashinda Mechi zao.
Msimu uliopita, Barca iliibwaga Real kwenye Robo Fainali ya Copa del Rey kwa jumla ya bao 4-3 katika Mechi mbili.
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zinatakiwa kuchezwa Oktoba 31 na marudiano ni Novemba 28.
 
TERRY ASALIMU AMRI, akubali Kifungo Mechi 4, aomba Radhi!!

>>KUZIKOSA Spurs, Man United mara mbili na Swansea!
FREDINAND-TERRY_MKNO_HAMNAHatimae Nahodha wa Chelsea John Terry ameamua kutokata Rufaa kupinga Adhabu yake ya kufungiwa Mechi 4 na Faini ya Pauni 220,000 baada ya kupatikana na hatia na FA, Chama cha Soka England, ya kumkashifu kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand.
Uamuzi huu wa Terry, ambao umekuja katika Siku ya mwisho ya yeye kutakiwa akubali au apinge adhabu yake, unamaanisha atazikosa Mechi za Klabu yake Chelsea za Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham, Manchester United na Swansea City na pia Mechi ya CAPITAL ONE CUP dhidi ya Man United.
Tukio lililomsulubu Terry lilitokea Oktoba 23 Mwaka jana huko Uwanja wa Loftus Road kwenye Mechi ya Ligi ambayo QPR iliifunga Chelsea bao 1-0.
Baada ya hapo Kesi hiyo ilitinga Mahakamani baada ya Shabiki mmoja kupeleka malalamiko Polisi lakini Mwezi Julai Mahakama ya Westminster ilimwachia huru na hapo ndipo FA ikaamuru Jopo lake Huru la Nidhamu lisikilize Kesi hiyo na ndipo ikamtia hatiani baada ya kutoukubali utetezi wake.
Akikubali adhabu yake, Terry Miaka 31, amesema: “Naomba nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa kila mtu kwa lugha niliyotumia.”
Pia aliongeza: “Ingawa nimehuzunishwa na hukumu ya FA, ninakubali kuwa lugha niliyotumia, ukiachilia mbali mazingira yake, haikubaliki kwenye Uwanja wa mpira au popote pale maishani. Kama nilivyosema Mahakamani, ningekuwa najua nini kitatokea, lugha niliyotumia ni wazi haikufaa kwa Mtu wa nafasi kama yangu. Uamuzi uko chini ya kile Klabu ya Chelsea inataka na kwangu pia na hili halitarudiwa tena.’’
Hadi sasa Klabu ya Chelsea haijatoa tamko itamchukulia hatua gani Terry mbali ya kusema inasubiri uamuzi wa Terry kama atakata Rufaa au la.

SIMBA NA KAGERA WACHANGA MILIONI 58

Benjamin Effe wa Kagera Sugar akimdhibiti Mrisho Ngassa wa Simba katika mechi ya jana

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Kagera Sugar iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 limeingiza sh. 58,505,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, watazamaji 9,842 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000, na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 11,013,785.54 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,924,491.53.
Amesema mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 440,000, mtathimini wa waamuzi sh. 254,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Amesema umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,183,890. Gharama za mchezo sh. 3,671,261.85, uwanja sh. 3,671,261.85, Kamati ya Ligi sh. 3,671,261.85, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,202,757.11 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,468,504.74.
Katika mechi hiyo, Simba ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngassa tangu ajiunge na Simba katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja, akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.

TFF YAFUNGA NDOA NA FKF YA KENYA

Rais wa TFF, Tenga

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Kenya (FKF) wamefikia makubaliano ya kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuinua kiwango cha mpira wa miguu katika nchi hizo.
Akizungumza baada ya mkutano uliowakutanisha vinara wa mashirikisho hayo Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema wameamua kurejesha uhusiano huo uliokuwepo zamani baada ya kuwepo utulivu katika uendeshaji mpira wa miguu nchini Kenya.
Amesema maeneo ya ushirikiano ambayo wameagiza yafanyiwe kazi na sekretarieti za pande zote (TFF na KFF) ili baadaye yaingizwe katika Hati ya Makubaliano (MoU) ni mafunzo, waamuzi, mechi za timu za Taifa za wakubwa, vijana na wanawake, na Ligi Kuu.
Rais Tenga pia amesema wameamua kuwepo ziara za mafunzo (study tours) katika maeneo mbalimbali ambapo kwa Kenya wao Ligi Kuu yao iliingia katika mfumo wa kampuni mapema, hivyo itakuwa fursa nzuri kwa Bodi ya Ligi Kuu ambayo iko kwenye mchakato wa kuanzishwa kupata uzoefu kwa wenzao wa Kenya.
Naye Rais wa FKF, Sam Nyamweya aliyefuatana na Makamu wake wa Rais, Robert Asembo amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya ni wa kihistoria, hivyo wameamua kuuanzisha upya kwa faida ya nchi hizo.
Amesema hivi karibuni FKF ilichukua waamuzi kutoka Tanzania waliochezesha mechi ya kirafiki kati ya Kenya (Harambee Stars) na Afrika Kusini (Bafana Bafana), hivyo wameamua kubadilishana waamuzi kwa lengo la kuwaongezea uzoefu.
“Waamuzi wa Tanzania walichezesha vizuri mechi ile. Unajua kwetu kuna upinzani mkubwa katika klabu kama AFC Leopards na Gor Mahia, ukipanga refa utasikia wengine wanalalamika, mara huyo ni Mjaluo. Hata akichezesha vizuri bado watalalamika tu kutokana na upinzani uliopo katika klabu hizo,” amesema.
Rais Nyamweya ameongeza kuwa ili kuondoa malalamiko katika mechi za aina hiyo wanaweza kuchukua waamuzi kutoka Tanzania, na vilevile waamuzi kutoka Kenya wakachezesha mechi za aina hiyo nchini Tanzania.
Amesema vilevile wamepanga kuangalia uwezekano wa kuwa na mechi za kuandaa timu kabla ya kuanza Ligi Kuu za nchi hizo ambapo washindi watatu au wanne wa kwanza katika ligi hizo kushindana.
Kwa upande wa mafunzo, wamekubaliana kuwa kwa vile kila nchi ina wakufunzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na la Afrika (CAF) watawatumia kuandaa mafunzo ya mara kwa mara kwa waamuzi, makocha, madaktari wa tiba ya michezo na viongozi badala ya kusubiri mafunzo ya aina hiyo kutoka kwa mashirikisho hayo ya kimataifa.

UEFA YAMTUNUKU TUZO RONALDO KWA MECHI 100

Ronaldo
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amepewa tuzo na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), baada ya kufikisha mechi 100 za kuichezea timu yake ya taifa, Ureno.
Katika mechi zake 100, Ronaldo amefunga mabao 37; bao lake la kwanza akifunga katika ushindi wa 2-1 timu yake ikifungwa na Ugiriki katika hatua ya makundi ya Euro 2004. 
Akiwa ana umri wa miaka 27, Ronaldo anakuwa mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo kufikisha idadi hiyo ya mechi, baada ya Wajerumani Lukas Podolski na Estonia's Kristen Viikmäe.
Nyota huyo wa Real Madrid amesema katika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa Facebook, akizungumzia mechi zake 100. 
"Nakumbuka ilikuwa Agosti 20, mwaka 2003 dhidi ya Kazakhstan kwa mara ya kwanza nilipovaa jezi ya Ureno ya timu ya taifa ya wakubwa,"alikumbushia.
Mabao 11 zaidi yatamfanya Ronaldo ampiku Pauleta kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa Ureno na anahitaji mechi 28 zaidi kumpiku Luis Figo. 
Kwa sasa, Ureno ina pointi tano katika Kundi F ikichuana na Urusi kileleni katika kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014. 

KIIZA DIEGO AREJEA KUONGEZA NGUVU YANGA

Kiiza

HAMISI Friday Kiiza maarufu Diego Milito, amerejea jana Dar es Salaam na leo anaingia kambini, Uplands Hotel, Changanyikeni kuungana na wenzake kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Jumamosi wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiiza alikuwa Uganda, kuichezea timu yake ya taifa, The Cranes katika mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.
Uganda ilitolewa na Zambia kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya jumla ya 1-1, Zambia wakianza kushinda nyumbani 1-0 na Uganda wakashinda kwao 1-0 pia mwishoni mwa wiki, hivyo mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti, ambako timu ya Kiiza ilitolewa.
Pamoja na kuweka kambi Changanyikeni, lakini Yanga inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Beki Kevin Yondan aliyeumizwa na kiungo wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ katika mechi baina ya wapinzani hao wa jadi, Oktoba 3, mwaka huu, anaendelea vizuri na mazoezi mepesi sawa na mshambuliaji Said Bahanuzi aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Bahanuzi ‘Spider Man’ alichanika nyama za paja la mguu wa kulia katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba Jumatatu wiki iliyopita.
Bahanuzi aliumia dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete katika mechi ambayo Yanga ililala 1-0, beo pekee la Themi Felix.
Bahanuzi ndiye tegemeo la mabao la Yanga kwa sasa, kwani tangu ajiunge na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, ameifungia mabao 12 katika mechi 13, ikiwemo ile dhidi ya Kagera aliyocheza kwa dakika 23 kabla ya kuumia na kutoka. 
Yanga kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 11, baada ya kucheza saba, kushinda tatu, sare mbili na kufungwa mbili.
Simba iliyocheza mechi nane, inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 18, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 17, iliyocheza mechi saba.

MILOVAN: IMENISIKITISHA, LAKINI NDIYO SOKA, TUNAGANGA YAJAYO

Simba na Kagera jana

PROFESA Milovan Cirkovick, amesema sare mbili mfululizo ambazo timu yake imezipata katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni kweli zimemsononesha, lakini hayo ni mambo ya kawaida katika soka.
Akizungumza baada ya sare ya jana dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam alisema matokeo hayo yamemsikitisha kwa ujumla na hana jinsi zaidi ya kukubali kwa kuwa hiyo ndiyo soka.
Alipotoka 0-0 na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga alisema ni kwa sababu ya Uwanja mbaya na kuwakosa nyota wake kadhaa, wakiwemo Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa, lakini jana alikuwa katika Uwanja mzuri na alikuwa na nyiota wake hao pia.
“Ni soka, katika soka yanatokea mambo haya, sasa najipanga kwa ajili ya mchezo ujao, ili tusiendelee na matokeo haya,”alisema Milovan, ambaye Jumapili anarudi kwenye Uwanja mbaya, Mkwakwani kukipiga na JKG Mgambo katika mfululizo wa ligi hiyo.
Simba jana ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngassa tangu ajiunge na Simba katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja, akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.
Katika mechi nyingine, Mgambo imeshinda mechi ya tatu mfululizo, baada ya kuifunga Toto African 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. JKT Ruvu imezinduka baada ya kuifunga Polisi Morogoro 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na JKT Oljoro imetoka 0-0 na African Lyon.
Simba SC; Juma Kaseja (Nahodha), Nassor Masoud ‘Chollo’/Uhuru Suleiman, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi/Jonas Mkude, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa.
Kagera Sugar; Andrew Ntala, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Amandus Nesta (Nahodha), Benjamin Effe/Themi Felix, Malegesi Mwangwa, Daudi Jumanne/Kamana Salum, George Kavilla, Shijja Mkinna, Enyinna Darlington na Wilfred Ammeh/Paul Nwai.
Katika mchezo wa awali, Simba B iliifunga Moro United mabao 3-0 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   
Mabao ya Simba B inayofundishwa na Suleiman Matola, akisaidiwa na Amri Said ‘Stam’ yalipatikana yote kipindi cha pili, wafungaji Ramadhan Salum dakika ya 65 na 70 na Miraj Athumani dakika ya 85.  Moro United inajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza, inayotarajiwa kuanza Oktoba 24, mwaka huu.

KIBADENI AFICHUA SIRI YA KUWAKAMATIA MBAVUNI SIMBA

Kibadeni

Na Mahmoud Zubeiry
KOCHA wa Kagera Sugar, Abdallah Athumani Seif ‘Kibadeni’ amesema kwamba alijua ataifunga Simba jana, lakini bahati mbaya ikawa sare na ameridhika na matokeo hayo pia kwa ilikuwa mechi ya ugenini.
Kibadeni alisema kwamba katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kilichompa matumaini ya kuifunga Simba ni kwa sababu anamjua vizuri kocha wa timu hiyo, Mserbia, Profesa Milovan Cirkovick kwa kuwa alifanya naye kazi.
“Mimi nilijua tu nitawapa tabu Simba, kwa sababu Milovan ninamjua, nimefanya naye kazi mimi Simba, ufundishaji wake naujua,”alisema Kibadeni.    
Kagera jana ilitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2 na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hiyo ikiwa sare ya pili mfululizo kwa Wekundu hao wa Msimbazi, baada ya Jumamosi pia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union mjini Tanga.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, kutokana na Azam FC kulazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Hadi mapumziko, Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. dakika ya nane, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’ kutoka wingi ya kulia.
Kwa ujumla kipindi cha kwanza timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa ni Simba walioonekana kufanya mashambulizi ‘yenye akili’ zaidi.
Kipindi cha pili Simba ilirudi na moto tena na katika dakika ya 51, Mrisho Khalfan Ngassa aliifungia timu hiyo bao la pili kwa shuti kali lililowababatiza mabeki wa timu hiyo na kutinga nyavuni.
Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Ngassa tangu ajiunge na Simba katika mechi tisa alizoichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Kagera walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Simba kupitia pembeni na katika dakika ya 64 Themi Felix aliunganisha kwa kichwa krosi ya George Kavilla na kuifungia Kagera bao la kwanza.
Bao liliwazindua Kagera, ambao waliongeza kasi ya kulishambulia lango la Simba na katika dakika ya 66, Juma Nyosso alimkwatua kwenye eneo la hatari Paul Ngwai na Salum Kanoni akaenda kumtungua Juma Kaseja, akiisawazishia Kagera.
Baada ya hapo timu zilianza kushambuliana kwa zamu na mpira ulinoga zaidi kutokana na mashambulizi ya pande zote mbili.
Katika mechi nyingine, Mgambo imeshinda mechi ya tatu mfululizo, baada ya kuifunga Toto African 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. JKT Ruvu imezinduka baada ya kuifunga Polisi Morogoro 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na JKT Oljoro imetoka 0-0 na African Lyon.
Simba SC; Juma Kaseja (Nahodha), Nassor Masoud ‘Chollo’/Uhuru Suleiman, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi/Jonas Mkude, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi na Mrisho Ngassa.
Kagera Sugar; Andrew Ntala, Salum Kanoni, Martin Muganyizi, Amandus Nesta (Nahodha), Benjamin Effe/Themi Felix, Malegesi Mwangwa, Daudi Jumanne/Kamana Salum, George Kavilla, Shijja Mkinna, Enyinna Darlington na Wilfred Ammeh/Paul Nwai.
Katika mchezo wa awali, Simba B iliifunga Moro United mabao 3-0 katika mchezo wa utangulizi kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.   
Mabao ya Simba B inayofundishwa na Suleiman Matola, akisaidiwa na Amri Said ‘Stam’ yalipatikana yote kipindi cha pili, wafungaji Ramadhan Salum dakika ya 65 na 70 na Miraj Athumani dakika ya 85.  Moro United inajiandaa na Ligi Daraja la Kwanza, inayotarajiwa kuanza Oktoba 24, mwaka huu.

TERRY ASALIMU AMRI, akubali Kifungo Mechi 4, aomba Radhi!!

FREDINAND-TERRY_MKNO_HAMNAHatimae Nahodha wa Chelsea John Terry ameamua kutokata Rufaa kupinga Adhabu yake ya kufungiwa Mechi 4 na Faini ya Pauni 220,000 baada ya kupatikana na hatia na FA, Chama cha Soka England, ya kumkashifu kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand. 

>>KUZIKOSA Spurs, Man United mara mbili na Swansea!
Uamuzi huu wa Terry, ambao umekuja katika Siku ya mwisho ya yeye kutakiwa akubali au apinge adhabu yake, unamaanisha atazikosa Mechi za Klabu yake Chelsea za Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham, Manchester United na Swansea City na pia Mechi ya CAPITAL ONE CUP dhidi ya Man United.
Tukio lililomsulubu Terry lilitokea Oktoba 23 Mwaka jana huko Uwanja wa Loftus Road kwenye Mechi ya Ligi ambayo QPR iliifunga Chelsea bao 1-0.
Baada ya hapo Kesi hiyo ilitinga Mahakamani baada ya Shabiki mmoja kupeleka malalamiko Polisi lakini Mwezi Julai Mahakama ya Westminster ilimwachia huru na hapo ndipo FA ikaamuru Jopo lake Huru la Nidhamu lisikilize Kesi hiyo na ndipo ikamtia hatiani baada ya kutoukubali utetezi wake.
Akikubali adhabu yake, Terry Miaka 31, amesema: “Naomba nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa kila mtu kwa lugha niliyotumia.”
Pia aliongeza: “Ingawa nimehuzunishwa na hukumu ya FA, ninakubali kuwa lugha niliyotumia, ukiachilia mbali mazingira yake, haikubaliki kwenye Uwanja wa mpira au popote pale maishani. Kama nilivyosema Mahakamani, ningekuwa najua nini kitatokea, lugha niliyotumia ni wazi haikufaa kwa Mtu wa nafasi kama yangu. Uamuzi uko chini ya kile Klabu ya Chelsea inataka na kwangu pia na hili halitarudiwa tena.’’
Hadi sasa Klabu ya Chelsea haijatoa tamko itamchukulia hatua gani Terry mbali ya kusema inasubiri uamuzi wa Terry kama atakata Rufaa au la.
 
BPL WKIENDI-DABI ya LONDON: Jumamosi AVB kulipa kisasi kwa Chelsea!

RATIBA
Jumamosi Oktoba 20
[SA 8 DAK 45 Mchana]
Tottenham v Chelsea
[SAA 11 JIONI]
Fulham v Aston Villa
Liverpool v Reading
Man Utd v Stoke
Swansea v Wigan
West Brom v Man City
West Ham v Southampton

[SAA 1 na Nusu Usiku]
Norwich v Arsenal
Jumapili Oktoba 21
[SAA 9 na Nusu Mchana]
Sunderland v Newcastle
[SAA 12 Jioni]
QPR v Everton
=============================
BPL_LOGOAndre Villas-Boas, Meneja alietimuliwa kazi na Chelsea baada ya Miezi 9 tu mwanzoni mwa Mwaka huu, Jumamosi atapata nafasi safi ya kulipa kisasi wakati Timu yake anayoiongoza sasa Tottenham itakapoikaribisha Chelsea Uwanjani White Hart Lane katika Mechi ya Ligi Kuu England ambayo ni Dabi ya Jiji la London.
Msimu uliopita, Chelsea walimaliza Ligi wakiwa nafasi ya 6, nafasi mbili nyuma ya Tottenham lakini Chelsea wakaichukua nafasi ya Tottenham kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa vile Chelsea ndio Mabingwa watetezi wa Mashindano hayo na wao Tottenham kutupwa kucheza EUROPA LIGI.
Baada ya kutimuliwa Andre Villas-Boas, mwenye Miaka 34, nafasi yake huko Chelsea ikachukuliwa na aliekuwa Msaidizi wake, Roberto Di Matteo, ambae ndie aliiongoza Chelsea kutwaa Ubingwa wa Ulaya walipoitoa Bayern Munich kwa matuta Mwezi Mei kwenye Fainali huko Munich, Germany.
Chelsea watatinga White Hart Lane wakiwa ndio vinara wa Ligi wakiwa na Pointi 19 baada ya kushinda Mechi 6 na sare 1 na Tottenham wamepanda hadi nafasi ya 5 baada ya kuchinda Mechi zao 4 za mwisho ukiwemo ule ushindi wao murua huko Old Trafford walipoifunga Manchester United bao 3-2 huo ukiwa ushindi wao wa kwanza Uwanjani hapo katika Miaka 23.
Ikiwa Tottenham watamudu kuisimamisha Chelsea hilo litatoa mwanya kwa Timu zinazoifukuza Chelsea ambazo ni Manchester United, Mabingwa Manchester City na Everton.
Man United, ambao wako nafasi ya pili na wenye Pointi 15, wapo kwao Old Trafford kucheza na Stoke City, Man City, ambao pia wana Pointi 15, wapo ugenini kucheza na WBA ambao wako nafasi ya 6, na Everton, walio nafasi ya 4, wanacheza na Timu ya mkiani Queens Park Rangers.

Wachezaji toka Mechi za Kimataifa
Klabu nyingi za Ligi Kuu England zitakuwa zikisubiri kurudi kwa Wachezaji wao kutoka kuzichezea Nchi zao huku wakiwa na wasiwasi kama wako fiti lakini Chelsea watacheza na Spurs bila ya majeruhi Frank Lampard na Ryan Bertrand.
Manchester United, ambao wana listi ndefu ya majeruhi, wanaweza kupata ahueni baada ya Ashley Young na Chris Smalling kupona na kurejea mazoezini tangu Wiki iliyopita.
Man City wataenda huko Hawthorns kucheza na WBA bila ya David Villa ambae aliumia hivi juzi akiichezea Nchi yake Spain na pia Kiungo Jack Rodwell lakini machachari wao Mario Balotelli amepona na juzi alifunga bao wakati Nchi yake Italy ilipoichapa Denmark bao 3-1.
Arsenal, ambao wameteleza hadi nafasi ya 7 wakiwa na Pointi 12, watasafiri kwenda kucheza na Norwich City ambao Msimu huu hawajashinda hata Mechi moja ya Ligi.
Arsenal watacheza bila ya Theo Walcott  alieumizwa kifua kwenye Mechi ya Nchi yake England ilipocheza na San Marino Ijumaa iliyopita lakini Straika wao Olivier Giroud anaweza kucheza baada ya kuifungia Arsenal bao lake la kwanza kwenye Ligi Arsenal ilipoicharaza West Ham 3-1 katika Mechi iliyopita na pia kufunga bao muhimu kwa Nchi yake France ilipotoka 1-1 na Mabingwa wa Dunia Spain katika Mechi ya Kombe la Dunia juzi Jumanne.

MAREFA wa MECHI za WIKIENDI:
Jumamosi Oktoba 20

Tottenham Hotspur v Chelsea
Refa: M Dean
Wasaidizi: S Ledger, J Brooks
Refa wa Akiba: L Mason

Fulham v Aston Villa
Refa: C Foy
Wasaidizi: M McDonough, D C Richards
Refa wa Akiba: I Williamson

Liverpool v Reading
Refa: R East
Wasaidizi: A Garratt, R West
Refa wa Akiba: K Friend

Manchester United v Stoke City
Refa: A Taylor
Wasaidizi: D Cann, S Long
Refa wa Akiba: M Halsey

Swansea City v Wigan Athletic
Refa: M Jones
Wasaidizi: H Lennard, A Halliday
Refa wa Akiba: K A Woolmer

West Bromwich Albion v Manchester City
Refa: M Clattenburg
Wasaidizi: S Beck, S Child
Refa wa Akiba: C Pawson

West Ham United v Southampton
Refa: N Swarbrick
Wasaidizi: J Collin, L Betts
Refa wa Akiba: J Moss

Norwich City v Arsenal
Refa: L Probert
Wasaidizi: R Ganfield, D Bryan
Refa wa Akiba: A Marriner

Jumapili Oktoba 21
Sunderland v Newcastle United
Refa: M Atkinson
Wasaidizi: M Mullarkey, S Burt
Refa wa Akiba: A Taylor

Queens Park Rangers v Everton
Refa: J Moss
Wasaidizi: J Flynn, C Breakspear
Refa wa Akiba: P. Dowd
 
KWA LEO: Mtigila atimuliwa Denmark, France ni mpya!

MARTEN_OLSEN-DENMARKMTIGILA apashwa: ‘HUTAICHEZEA DENMARK TENA!’
Beki wa Kimataifa wa Denmark, Patrick Mtigila, ameambiwa hataichezea Timu ya Taifa tena baada ya kugoma kucheza Mechi  ya juzi ya Nchi hiyo ambayo Denmark ilichapwa 3-1 na Italy kwenye Mechi ya Kombe la Dunia.
Kocha wa Denmark, Morten Olsen, alisema Beki huyo awali alijulishwa atakuwa Benchi na Simon Poulsen ataanza badala yake lakini, wakati Wachezaji wanapasha moto kabla Mechi kuanza huko Mjini Milan, Poulsen aliumia na Mtigila akajulishwa atacheza Mechi hiyo lakini akagoma.
Olsena amesema: “Nipo kwenye Soka kwa Miaka 40 sasa lakini sijashuhudia kitu kama hiki. Amewaangusha wenzake!”
Olsen aliongeza: “Nilimwambia Patrick Mtigila ajipashe lakini alikuwa amehuzunika baada ya kwanza kuambiwa hachezi Mechi hiyo atakuwa Benchi na akasema hawezi kucheza. Hapo hapo nikamwambia aondoke kwenye Timu kwa kuwa amecheza Mechi yake ya mwisho!”
Huko Denmark, Mtigila ni Mchezaji wa Klabu Bingwa yao FC Nordsjaelland.

FRANCE yajipa matumaini!
Baada ya kuchapwa na Japan bao 1-0 katika Mechi ya Kirafiki iliyochezwa Ijumaa iliyopita huko Paris, Watu walianza kuibeza France na walitegemea itatandikwa bao nyingi na Mabingwa wa Dunia Spain Siku 3 zinazifuata huko Madrid katika Mechi ya Kundi I la Kombe la Dunia Barani Ulaya lakini hiyo Jumanne France iligangamala na kutoka 1-1 na Spain.
Katika Mechi hiyo, Spain walitangulia kupata bao lililofungwa na Sergio Ramos na Wadau wakahisi ni ile ile ya EURO 2012 ambapo Mwezi Juni Spain iliichapa France 2-0 kwenye Robo Fainali lakini safari hii France waliibuka kwa nguvu, wakanyimwa Bao safi, Kipa wao Hugo Lloris akaokoa Penati na mwishowe Olivier Giroud akasawazisha bao.
Wachezaji wa France wamekiri Kocha wao, Didier Deschamps, aliwainua morali wakati wa mapumziko wa Mechi hiyo kwa maneno yake.
Sentahafu Mamadou Sakho aliongea: “Hotuba yake ilituinua tukapigana kiume. Alituambia tusikate tamaa, tunaweza kupata sare na kushinda Mechi hii.”
Kwa sasa katika Kundi I Spain na France zimefungana kila moja ikiwa na Pointi 7 kwa Mechi 3 na zitapambana katika marudiano ndani ya Stade de France Jijini Paris hapo Machi 26, 2013.
Mechi zinazofuata kwa France ni mbili za Kirafiki na Italy na Germany kasha Mechi ya Kundi I la Kombe la Dunia dhidi ya Georgia na kufuatia marudiano yao na Spain.
Kocha Deschamps, ambae wakati akiwa Mchezaji wa France alitwaa Ubingwa wa Dunia Mwaka 1998 na wa Ulaya Mwaka 2000, amekiri: “Hii ni Timu changa lakini tunaweza kufanya vizuri na inabidi tuijenge zaidi. Tunajua sisi sio bora lakini pia sisi si Timu mbaya!”
 
KOMBE la DUNIA-Ulaya: Poland 1 England 1

>>WACHEZAJI England kufidia Mashabiki £ 50,000!!!
BRAZIL_2014_BESTBaada ya Mechi ya Kundi H la Bara la Ulaya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil kutochezwa jana kufuatia Mvua kubwa na uzembe wa kutofunika Paa la Uwanja wa Taifa huko Warsaw, leo Mechi hiyo imepigwa huku Paa likiwa limefungwa na matokeo kuwa Poland 1 England 1.
+++++++++++++++++++++++

KUNDI H
1 England Mechi 4 Pointi 8
2 Montenegro Mechi 3 Pointi 7
3 Poland Mechi 3 Pointi 5
4 Moldova Mechi 4 Pointi 4
5 Ukraine Mechi 3 Pointi 2
6 San Marino Mechi 3 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++
England ndio waliotangulia kupata bao kufuatia kona ya Steven Gerrard kuunganishwa kwa kichwa na Wayne Rooney katika Dakika ya 31 lakini Poland wakasawazisha katika Dakika ya 70 kwa bao la Kamil Glik kufuatia uzembe wa Kipa Joe Hart kukosa kupangua kona.
+++++++++++++++++++++++

MECHI ZIJAZO za ENGLAND:
KIRAFIKI
-Novemba 11: Sweden v England [Ugenini]
-Februari 6: England v Brazil [Wembley, London]

KOMBE la DUNIA KUNDI H:
-Machi 22, 2013: San Marino v England [Ugenini]
-Machi 26, 2013: Montenegro v England [Ugenini]
+++++++++++++++++++++++
Wakati huo huo, Kikosi cha Wachezaji wa England waliokuwepo huko Poland kimetangaza kuwa kitawafidia Mashabiki 2,500 wa England waliosafiri kwenda Poland kushuhudia pambano la jana lililoahirishwa kwa kuchangia Pauni 50,000 na pia kuwaalika wote hao kuhudhuria bure Mazoezi ya Timu hiyo huko England kabla Msimu huu kumalizika.

VIKOSI:
Poland: Tyton, Piszczek, Wasilewski, Wawrzyniak, Glik, Polanski, Krychowiak, Wszolek, Grosicki, Obraniak, Lewandowski
Akiba: Kuszczak, Wojtkowiak, Komorowski, Borysiuk, Murawski, Milik, Mierzejewski, Sobota, Piech, Perquis, Sobiech, Skorupski.

England: Hart, Glen Johnson, Jagielka, Lescott, Cole, Milner, Carrick, Gerrard, Cleverley, Rooney, Defoe
Akiba: Ruddy, Walker, Baines, Cahill, Shawcross, Oxlade-Chamberlain, Shelvey, Lennon, Adam Johnson, Carroll, Welbeck, Forster.
Refa: Gianluca Rocchi (Italy)
++++++++++++++++++++++++++++++

MSIMAMO:
KUNDI A
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Belgium Pointi 10
2 Croatia 10
3 Serbia 4
4 Macedonia 4
5 Wales 3
6 Scotland 2
+++++++++++++++++++++++

KUNDI B
1 Italy Mechi 4 Pointi 10
2 Bulgaria Mechi 4 Pointi 6
4 Czech Mechi 3 Pointi 5
3 Armenia Mechi 3 Pointi 3
5 Denmark Mechi 3 Pointi 2
6 Malta Mechi 3 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++

KUNDI C
1 Germany Mechi 4 Pointi 10
2 Sweden Mechi 3 Pointi 7
3 Ireland Mechi 3 Pointi 6
4 Austria Mechi 3 Pointi 4
5 Kazakhstan Mechi 4 Pointi 1
6 Faroe Island Mechi 3 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++

KUNDI D
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Netherlands Pointi 12
2 Hungary 9
3 Romania 9
4 Turkey 3
5 Estonia 3
6 Andorra 0
+++++++++++++++++++++++

KUNDI E
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Switzerland Pointi 10
2 Norway 7
3 Albania 6
4 Iceland 6
5 Slovenia 3
6 Cyprus 3
+++++++++++++++++++++++

KUNDI F
1 Russia Mechi 4 Pointi 12
2 Israel Mechi 4 Pointi 7
3 Portugal Mechi 4 Pointi 7
4 Northern Ireland Mechi 3 Pointi 2
5 Azerbaijan Mechi 3 Pointi 1
6 Luxembourg Mechi 4 Pointi 1
+++++++++++++++++++++++

KUNDI G
[Timu zote zimecheza Mechi 4]
1 Bosnia & Herzagovina Pointi 10
2 Greece 10
3 Slovakia 7
4 Lithuania 4
5 Latvia 3
6 Liechtenstein 0
+++++++++++++++++++++++

KUNDI H
1 England Mechi 4 Pointi 8
2 Montenegro Mechi 3 Pointi 7
3 Poland Mechi 3 Pointi 5
4 Moldova Mechi 4 Pointi 4
5 Ukraine Mechi 3 Pointi 2
6 San Marino Mechi 3 Pointi 0
+++++++++++++++++++++++

KUNDI I
1 Spain Mechi 3 Pointi 7 [Tofauti ya Magoli 5]
2 France Mechi 3 Pointi 7 [Tofauti ya Magoli 5]
3 Georgia Mechi 4 Pointi 4
5 Belarus Mechi 4 Pointi 3
4 Finland Mechi 2 Pointi 1
+++++++++++++++++++++++

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Novemba 14
Northern Ireland v Azerbaijan
Montenegro v San Marino

Ijumaa Machi 22
Slovenia v Iceland
Israel v Portugal
Cyprus v Switzerland
Norway v Albania
Luxembourg v Azerbaijan
Bosnia And Herzegovina v Greece
Netherlands v Estonia
Austria v Faroe Island
Czech Republic v Denmark
Moldova v Montenegro
Poland v Ukraine
Sweden v Ireland
Hungary v Romania
San Marino v England
Scotland v Wales
Spain v Finland
Northern Ireland v Russia
Macedonia v Belgium
Liechtenstein v Latvia
Slovakia v Lithuania
Bulgaria v Malta
Croatia v Serbia
Andorra v Turkey
Kazakstan v Germany