Sunday, December 30, 2012

DJOKOVIC ANYAKUWA TAJI LA MUBADALA.


MCHEZAJI tenisi nyota anayeshika namba moja duniani, Novak Djokovic ameanza msimu mpya wa michuano ya tenisi baada ya kumfunga Nicolas Almagro kwa 6-7 6-3 6-4 katika fainali ya mashindano ya maonyesho ya Mubadala iliyofanyika jijini Abu Dhabi. Djokovic ambaye alionyesha kiwango kizuri katika mchezo wa nusu fainali baada ya kumtoa David Ferrer anayeshika namba tano wakati Almagro ambaye aliziba nafasi ya Rafael Nadal aliyejitoa alimfunga Janko Tipsarevic. Akihojiwa mara baada ya ushindi huo Djokovic alifurahia kunyakuwa taji la michuano hiyo ya Abu Dhabi kwa mara nyingine na kuwasifu wapinzani wake aliokutana nao kwamba walimpa changamoto kubwa ambayo itamsaidia katika michuano iliyo mbele yake. Wachezaji wote wanne walioshirki michuano hiyo wanatarajiwa kuelekea nchini Australia kwa ajili ya michuano ya wazi itakayoanza Januari 14 jijini Melbourne huku Djokovic akiwa bingwa mtetezi.

WALCOTT ATABAKIA - WENGER.


MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa mshambuliaji wake nyota Theo Walcott atabakia klabuni hapo baada ya kuisaidia kupata ushindi mnono kwa mabao matatu aliyofunga katika Uwanja wa Emirates dhidi ya Newcastle. Arsenal ilifanikiwa kuisambaratisha Newcastle kwa mabao 7-3 ambao ushindi huo unakuwa watatu mfululizo baada ya kutolewa katika Kombe la Ligi na Bradford City inayoshiriki Ligi Daraja la pili. Walcott alionyesha kuimudu vyema nafasi ambayo anaitaka ya kuwa mshambuliaji wa kati akifunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza kabla ya kufunga mengine mawili katika kipindi cha pili na kukabidhiwa mpira baada ya mchezo huo kwa kufunga hat-trick. Nyota huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 23 bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo pamoja na kuahidiwa kuongezewa marupurupu. Lakini Wenger alionyeshwa kufurahishwa na kiwango cha nyota huyo na ana matumaini watafikia makubaliano kuhusu mkataba wake mpya.

RONALDINHO ATAMANI MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA 2014.


MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Ronaldinho Gaucho ameeleza kuwa anahitaji kuwamo katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kitashiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014. Nyota huyo wa zamani wa Barcelona ana matumaini kuwa atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki michuano hiyo katika kipindi cha miezi 18 ijayo ambayo itaandaliwa nchini kwake. Ronaldinho amesema hakuna kitu kinacholeta furaha kama kucheza michuano ya Kombe la Dunia mbele ya mashabiki wa nyumbani na hapendi kupoteza nafasi hiyo muhimu. Kwasasa nyota huyo ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Atletico Mineiro amekuwa akipambana kurejesha makali yake ya zamani ili aweze kuitwa katika kikosi hicho na anaamini katika kipindi cha miezi 18 ijayo atakuwa amefikia kiwango hicho. Luiz Felipe Scolari ambaye ameisaidia Brazil kunyakuwa Kombe la Dunia mwaka 2002 wakati huo Ronaldinho akiwa ndio nyota nchi hiyo ndio amekabidhiwa tena mikoba ya kuinoa timu ya taifa Novemba.

BOJAN ATAREJEA TENA BARCELONA - BABA


BABA wa mshambuliaji nyota wa zamani wa klabu ya Barcelona Bojan Krkic amesema mwanae huyo anaweza kurejea tena katika klabu hiyo pamoja na kutong’aa katika Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama Serie A. Mshambuliaji huyo aliuzwa kwenda klabu ya AS Roma mwaka 2011 kwa ada ya paundi milioni 12 lakini alitolewa tena kwa mkopo katika klabu ya AC Milan msimu huu lakini Barcelona wanapanga kumnunua tena mchezaji wao huyo wa zamani. Baba wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 alidokeza kuwa Tito Vilanova kuwa meneja wa Barcelona kunafanya mwanae kuwa nafasi kubwa kurejea pale baada ya kuingia matatizoni na kocha wa zamani wa klabu hiyo Pep Guardiola. Klabu yake ya sasa ya Milan inatarajiwa kukutana na Barcelona katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Februari mwakani.

MILANOV MCHEZAJI BORA WA MWAKA BULGARIA.


CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini Bulgaria-PFC kimemteua mshambuliaji wa klabu ya Litex Lovech, Georgi Milanov kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo mbele ya wachezaji wengine nyota akiwemo Dimitar Berbatov anayecheza katika klabu ya Fulham ya Uingereza. Milanov mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni mchezaji mdogo kuwahi kushinda tuzo hiyo na mchezaji wa kwanza ambaye anacheza soka chini humo kushinda tuzo hiyo toka mwaka 2001. Kiungo huyo amefunga mabao nane katika michezo 14 aliyocheza na kuwa mhimili wa kuisaidia klabu yake kukwea mpaka nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini humo. Akihojiwa mara baada ya sherehe hizo nyota huyo amesema ni heshima kubwa kwake kupokea tuzo huyo na kuwashukuru waandaji, wachezaji wenzake pamoja na kocha wake Hristo Stoichkov kwa kumsaidia kufikia kiwango alichonacho hivi sasa.

FA CUP RAUNDI ya 3: DIMBANI JANUARI 5!

>>MECHI 4 TU KUKUTANISHA TIMU ZA LIGI KUU!!
FA_CUP-NEW_LOGOMABINGWA WATETEZI wa FA CUP, Chelsea, wataanza utetezi wao wa FA CUP kwenye Raundi ya 3 kwa kucheza ugenini na Southampton hapo Januari 5 na hiyo ni Mechi moja kati ya 4 itakayozikutanisha Timu za Ligi Kuu England pekee.
Raundi ya 3 ya FA CUP ndiyo ambayo imejumuisha Timu toka Ligi Kuu England.
Mechi nyingine ambazo zitakutanisha Timu za Ligi Kuu England pekee ni zile za Manchester United kutua Upton Park kucheza na West Ham United, QPR kuikaribisha West Brom na Arsenal kusafiri kucheza na Swansea.
Timu nyingine vigogo wa Ligi Kuu, kama vile Mabingwa wa Ligi Manchester City, wao watacheza na Watford, Tottenham kucheza na Coventry.
Liverpool watakuwa ugenini kuivaa Mansfield.
RATIBA:
RAUNDI ya TATU:
Jumamosi Januari 5
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Brighton v Newcastle
[SAA 12 Jioni]
Crystal Palace v Stoke
Tottenham v Coventry City
Wigan v Bournemouth
Fulham v Blackpool
Aston Villa v Ipswich
Charlton v Huddersfield
Barrow au Macclesfield v Cardiff
Barnsley v Burnley
Manchester City v Watford
Leicester v Burton
Millwall v Preston
Derby v Tranmere
Crawley v Reading
Aldershot v Rotherham
Middlesbrough v Hastings
Oxford v Sheffield United
Southampton v Chelsea
QPR v West Brom
Peterborough v Norwich
Bolton v Sunderland
Nottingham Forest v Oldham
Hull v Alfreton or Leyton Orient
Blackburn v Bristol City
Leeds v Birmingham
Southend v Brentford
Luton v Wolves
Sheffield Wednesday v MK Dons
[SAA 2 na Dak 15 Usiku]
West Ham v Manchester United
Jumapili Januari 6
Swansea v Arsenal [SAA 10 na Nusu Jioni]
Mansfield v Liverpool [SAA 1 Usiku]
Jumatatu Januari 7
Cheltenham v Everton [SAA 4 Dak 45 Usiku]

MKONGWE LAMPARD AIPAISHA CHELSEA NAFASI YA 3!!

BPL_LOGOFrank Lampard, Miaka 34, ambae mwishoni mwa Msimu Mkataba wake unamalizika na inadaiwa tayari hana nafasi Klabu hapo, leo alivaa utepe wa Nahodha na kuibeba Chelsea toka Goli 1 nyuma Uwanjani Goodison Park na yeye mwenyewe kupiga Bao mbili na kuwapa ushindi wa Bao 2-1, ukiwa ni ushindi wao wa kwanza kwa Miaka minne Uwanjani hapo.
Hi ilikuwa ni Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England kwa Mwaka 2012 kwa Klabu zote mbili ambazo zitacheza Mechi zao za Ligi zinazofuata hapo Januari 2, Mwaka 2013 kwa Chelsea kuikaribisha QPR Uwanjani Stamford Bridge na Everton kuwa ugenini huko St James Park kuivaa Newcastle.
++++++++++++
MAGOLI:
Everton 1
-Pienaar Dakika ya 2.
Chelsea 2
-Lampard Dakika ya 42 & 72
++++++++++++
Ushindi huu wa leo umeipaisha Chelsea kukamata nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya Pili Manchester City huku wao wakiwa na Mechi moja mkononi.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za Juu:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 20 Pointi 49
2 Man City Mechi 20 Pointi 42
3 Chelsea Mechi 19 Pointi 38
4 Tottenham Mechi 20 Pointi 36
5 Arsenal Mechi 19 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 18]
6 Everton Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 8]
7 WBA Mechi 20 Pointi 33 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Stoke Mechi 20 Pointi 29
9 Swansea Mechi 20 Pointi 28
10 Liverpool Mechi 19 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
+++++++++++++++++++++++
Ingawa Everton wamefungwa Mechi hii lakini walitoa upinzani mkubwa na wangeweza hata kushinda kwani Straika wao Nikica Jelavic alipiga posti na kukosa nafasi ya wazi mwishoni.
VIKOSI:
Everton: Howard, Jagielka, Heitinga, Distin, Baines, Naismith, Osman, Hitzlsperger, Pienaar, Anichebe, Jelavic.
Akiba: Mucha, Oviedo, Gueye, Barkley, Vellios, Duffy, Browning.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Ramires, Luiz, Lampard, Mata, Torres, Hazard.
Akiba: Turnbull, Oscar, Moses, Ferreira, Marin, Piazon, Ake.
Refa: Howard Webb
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:  
Jumapili 30 Desemba 2012
[SAA 1 Usiku]
QPR v Liverpool
Jumanne 1 Januari 2013
SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Brom v Fulham
[SAA 12 Jioni]
Man City v Stoke
Swansea v Aston Villa
Tottenham v Reading
West Ham v Norwich
Wigan v Man United
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Southampton v Arsenal
Jumatano 2 Januari 2013
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v QPR
Liverpool v Sunderland
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Everton

WALCOTT KUBAKI ARSENAL, NANI HAENDI KOKOTE, REFA MATATANI…!!

WENGER_MASHAKANIWALCOTT KUBAKI ARSENAL? NANI HAENDI KOKOTE! REFA MATATANI…!!
HUKU kukiwa na hatari ya kumpoteza Winga wao Theo Walcott bila kupata Senti hata moja ifikapo mwishoni mwa Msimu, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema bado wanamatumaini Mchezaji huyo atakubali kusaini Mkataba mpya na huko Old Trafford, Sir Alex Ferguson, ametamka Nani hauzwi Mwezi Januari na wakati huo huo, Refa alieboronga atachunguzwa na FA.
THEO WALCOTT: ARSENAL na ARSENE WENGER WANA MATUMAINI!
Arsene Wenger amesema Hetitriki ya Theo Walcott aliyopiga jana Arsenal ilipoitwanga Newcastle 7-3 haina uzito wowote kwenye mustabali wake Klabuni hapo ambapo kuna mvutano huku Mchezaji huyo akigoma kukubali Mkataba mpya wakati Mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa Msimu na kuanzia Januari Mosi yuko huru kuongea na Klabu nyingine zinazomtaka.
Wenger ametamka: “Nia yangu ni asaini Mkataba mpya. Yeye ni Mchezaji wa hapa na hata kama angecheza vibaya na Newcastle bado sisi tunataka aongeza Mkataba!”
Walcott, Miaka 23, amefunga Bao 14 Msimu huu na 4 ni katika Mechi 3 ambazo amechezeshwa kama Straika wa Kati.
Arsenal ilimsaini Walcott akiwa na Miaka 16 kutoka Southampton Mwaka 2006 kwa Dau la Pauni Milioni 5 ambalo lilipanda hadi Pauni Milioni 12.5.
Akiongea mara baada ya Mechi na Newcastle, Walcott alisema: “Mazungumzo na Arsenal yanaeendelea na nina hakika mambo yatakamilika hivi karibuni.”
NANI HAUZWI!
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesisitiza Nani hatauzwa Dirisha la Uhamisho likifunguliwa Mwezi Januari.
Tangu awe hana namba ya kudumu Msimu huu, kulizuka uvumi kuwa Mchezaji huyo kutoka Ureno yuko mbioni kuuzwa lakini Ferguson amepuuzia hayo na kusema: “Hatutamwachia aondoke. Tunamhitaji Nani. Kwanini tumuachie aondoke??”
Aliongeza: “Bado Mkataba wake una Mwaka mmoja na nusu. Yeye anatupa kitu tofauti na Wachezaji wengine hapa. Ana kipaji kikubwa. Bahati mbaya ameumia na tumempeleka Dubai kupumzika na apone. Tunatarajia atarudi Uwanjani katikati ya Januari.”
REFA MATATANI!!
REFA Mick Russell yupo mashakani na FA, Chama cha Soka England, baada ya kutomtoa nje Staa wa Sheffield Wednesday Jeremy Helan licha ya kumpa Kadi za Njano mbili kwenye Mechi waliyotoka sare 0-0 na Huddersfield.
+++++++++++++++++++++++
MAKOSA ya MAREFA WENGINE:
STUART ATTWELL: Mwaka 2008, aliwapa Reading Goli dhidi ya Watford badala ya Kona na akaondolewa kwenye Listi ya Marefa wa Mechi kubwa.
GRAHAM POLL: Alimpa Mchezaji wa Croatia Josip Simunic Kadi za Njano 3 katika Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2006 kabla kumtoa nje kwa Kadi Nyekundu katika Mechi na Australia.
+++++++++++++++++++++++
Tukio hilo liliwapandisha hasira Huddersfield waliotaka Refa huyo apewe adhabu kali.
Helan, ambae yuko kwa mkopo Sheffield Wednesday akitokea Manchester City, alipewa Kadi ya Njano ya kwanza katika Dakika ya 9 kwa kujiangusha kwa makusudi na ya pili katika Dakika ya 26 kwa kucheza Faulo.
Licha ya Wachezaji wa Huddersfield kulalamika kwa Refa Mick Russell wakitaka Helan atolewe, Refa huyo alianzisha tena mpira bila kumtoa ikimaanisha Helan asingeweza kutolewa tena.
Mwenyewe Helan amesema: “Ilishangaza! Lakini mie sio Refa, nilicheza Dakika 90 na nafurahia kwa hilo!”
Baadae Refa Russell alikiri kosa lake na kudai alikosea kuandika Namba wakati akitoa Kadi za Njano.
Chama cha Marefa, PGMO [Professional Game Match Officials Limited] na FA zimesema uchunguzi kuhusu uchezeshaji wa Refa Russell.

AFCON 2013: WENYEJI BAFANA BAFANA WATANGAZA KIKOSI!

AFCON_2013_LOGOWENYEJI wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, Afrika Kusini wametangaza Kikosi chao cha Wachezaji 23 kwa ajili ya Mashindano hayo yatakayochezwa Nchini kwao kuanzia Januari 19 hadi Februari 10.
Akitangaza Kikosi hicho, Kocha Mkuu wa Bafana Bafana Gordon Igesund, amesema ni bahati mbaya hawezi kuchukua zaidi ya Wachezaji 23 lakini anaamini wale walioteuliwa wataiwakilisha vyema Afrika Kusini.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Nahodha wa Kikosi hicho ni Bongani Khumalo.
Kabla ya kuanza rasmi AFCON 2013, Bafana Bafana watacheza Mechi mbili za Kirafiki dhidi ya Norway Mjini Cape Town, Afrka Kusini hapo Januari 8 na Januari 12 kucheza na Algeria huko Soweto, Johannesburg.
Afika Kusini watacheza Mechi ya ufunguzi ya AFCON 2013 dhidi ya Cape Verde Januari 19 Uwanjani Soccer City Mjini Johannesburg.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Itemeleng Khune, Wayne Sandilands, Senzo Meyiwa
MABEKI: Bongani Khumalo, Siboniso Gaxa, Siyabonga Sangweni, Anele Ngcongca, Tsepo Masilela, Thabo Nthethe, Thabo Matlaba
VIUNGO: Lerato Chabangu, Thulani Serero, Kagisho Dikgacoi, Dean Furman, Reneilwe Letsholonyane, Siphiwe Tshabalala, May Mahlangu, Thuso Phala, Oupa Manyisa
MASTRAIKA: Bernard Parker, Tokelo Rantie, Lehlohonolo Majoro, Katlego Mphela.