Sunday, January 20, 2013

MAREFA WA KENYA KUICHEZESHA AZAM KATIKA KOMBE LA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA


Wachezaji wa Azam mazoezini

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limewateua waamuzi kutoka Kenya kuchezesha mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam ya Tanzania na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini itakayofanyika jijini Dar es Salaam kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.
Mwamuzi wa kati atakuwa Davies Omweno na atasaidiziwa na mwamuzi msaidizi namba moja Peter Keireini, mwamuzi msaidizi namba mbili Gilbert Cheruiyot wakati mwamuzi wa mezani Anthony Ogwayo.
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Hassan Mohamed Mohamud kutoka Somalia. Waamuzi wa mechi ya marudiano itakayochezwa jijini Juba watatoka Rwanda wakiongozwa na Gervais Munyanziza.
Wakati huo huo: Waamuzi wa Tanzania wakiongozwa na Israel Mujuni wameteuliwa kuchezesha pambano la awali la raundi ya kwanza kuwania Kombe la Shirikisho kati ya UFC Haut Nkam ya Cameroon na US Bougouni ya Mali.
Kwa uteuzi huo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Mujuni na wenzake Ali Kinduli, Samuel Mpenzu na Waziri Sheha watachezesha mechi hiyo itakayofanyika kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.
Pierre Alain Mouguengui kutoka Gabon ndiye atakayekuwa Kamishna wa mechi hiyo. UFC Haut Nkam na US Bougouni zitarudiana wiki mbili baadaye nchini Mali.

No comments:

Post a Comment