Sunday, February 3, 2013

WENYEJI SOUTH AFRICA WALIVYOKUFA JANA KWA MALI YA AKINA KEITA.

SIMBA SARE NA JKT RUVU, KAPOMBE AKOSA PENALTI, MGOSI ATOA PASI YA BAO


Kiungo wa Simba, Amri Kiemba akiwapiga chenga beki Jimmy Shoji na kipa Shaaban Dihile, kabla ya kuifungia bao la kuongoza Simba SC.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC leo wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Ruvu ya Pwani katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo haya yanaiongezea pointi moja tu Simba SC na sasa imetimiza 27, baada ya kucheza mechi 15, ikiendelea kushika nafasi ya tatu, nyuma ya Azam yenye 30 na Yanga 32.
Hadi mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na kiungo Amri Ramadhan Kiemba, aliyewapiga chenga beki Jimmy Shoji na kipa Shaaban Dihile dakika ya 17, kabla ya kutumbukiza mpira nyavuni.
Kwa ujumla Simba walicheza vema kipindi cha kwanza, wakitawala safu ya kiungo na gonga zao safi za uhakika na kama wangekuwa makini wangeweza kutoka uwanjani baada ya nusu hiyo ya kwanza wakiwa na hazina kubwa ya mabao.
Kipindi cha pili mchezo ulibadilika na zaidi Simba ilionekana kuathiriwa na mabadiliko ya wachezaji iliyomfanya, haswa kumtoa Mrisho Ngassa aliyekuwa akiisumbua ngome ya JKT.
Maafande hao wa Ruvu walizidisha kasi ya mashambulizi langoni mwa Simba, wakiamini Wekundu wa Msimbazi hawana mtu hatari mbele.
Hilo liliisaidia timu hiyo kupata bao la kusawazisha dakika ya 63, lililofungwa na Nashon Naftali akiunganisha krosi ya Mussa Hassan Mgosi.
Baada ya kufungwa bao hilo, Simba walicharuka kusaka bao la ushindi, lakini jitihada zao ziliishia kwenye ngome ya JKT iliyokuwa imara kipindi cha pili na kutorudia makosa ya kipindi cha kwanza.
Refa Alex Mahagi wa Mwanza aliwapa Simba penalti dakika ya 87, baada ya beki Damas Makwaya kugongana na Haruna Moshi ‘Boban’ kwenye eneo la hatari.
Nahodha Msaidizi wa Simba SC, Shomary Kapombe alikwenda kupiga penalti yake vizuri, lakini kipa Shaaban Dihile aliipangua ikagonga mwamba na kurudi uwanjani, akaichupia kuidaka.
Simba SC hawakukata tamaa hata baada ya kukosa penalti dakika za lala salama, waliendelea kufanya mashambulizi ya haraka haraka kusaka  bao, lakini bahati haikuwa yao.   
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Shomary Kapombe, Komabil Keita, Abdallah Seseme/Haruna Moshi, Haroun Chanongo, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma, Amri Kiemba, Ramadhan Chombo/Kiggi Makassy.
JKT Ruvu; Shaaban Dihile, Credo Mwaipopo, Kessy Mapande, Kisimba Luambano, Damas Makwaya, Jimmy Shoji, Hussein Bunu, Nashon Naftali, Mussa Mgosi, Zahor Pazi na Emmanuel Pius.

OBI MIKEL MCHEZAJI WA MWAKA WA GOAL.COM NIGERIA.


KIUNGO nyota wa kimataifa wa Nigeria na klabu ya Chelsea John Obi Mikel amekubali tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa mashabiki wa Nigeria waliopiga kura katika mtandao wa Goal.com. Asilimia 36.84 ya wasomaji wa mtandao huo nchini Nigeria walimpigia kura Obi Mikel ambaye alikuwa akipambanishwa na mchezaji mwenzake wa Chelsea Victor Moses huku wengine wakiwa ni Ahmed Musa, Kano Pillars na Rueben Gabriel wote wanacheza CSKA Moscow ya Urusi na John Utaka wa klabu ya Montpellier ya Ufaransa. Akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mhariri Mtendaji wa mtandao wa Goal.com nchini Nigeria Lalade Adewuyi, Obi Mikel aliwashukuru mashabiki na kueleza nia yake ya kuingoza nchi hiyo kunyakuwa taji la michuano ya Mataifa ya Afrika pamoja na nchi yao kutopewa nafasi hiyo. Nigeria ambayo itakwaana na Ivory Coast katika mchezo wa robo fainali ya Afcon baadae leo huku wadau wengi wa soka wakiipigia chapuo Ivory Coast iliyosheheni wachezaji nyota wanaong’ara kwenye vilabu mbalimbali barani Ulaya kusonga mbele katika mchezo huo.

AL BADRY ASIKITIKA KUONDOKEWA NA NYOTA WAKE KADHAA.


MENEJA wa klabu ya Al Ahly ya Misri, Hossam Al Badry amebainisha kuwa alitaka kuachana na timu hiyo wiki iliyopita baada ya bodi ya klabu hiyo kuwauza kwa mkopo baadhi ya wachezaji wake nyota. Klabu hiyo iliwapeleka wa mkopo mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Mohammed Abo Trika katika klabu ya Baniyas ya Muungano wa Falme za Kiarabu-UAE pamoja na Ahmed Fathi na Mohammed Nagy Gedo katika klabu ya Hull City ya Uingereza. Al Badry amedai kuwa alitaka kuondoka mara tu nyota hao walipoondoka lakini hivi ameelewa kuwa ni kutokana na matatizo ya kifedha yanayoikabili klabu hiyo ndio maana bodi ikaamua kufanya hivyo. Kocha amesema anafikiri ataendelea kuwepo klabuni hapo ingawa hata hivyo amesikitishwa kuondokewa na nyota wake hao.

GAZZA AHITAJI MSAADA WA HARAKA KUTOKANA NA MATATIZO YA ULEVI YANAYOMSUMBUA.


WAKALA wa kiungo wa zamani wa kimataifa wa Uingereza Paul Gascoigne maarufu kama Gazza anaamini kuwa maisha ya nyota huyo yako hatarini baada ya kuanza tena ulevi wa kupitiliza. Gazza ambaye amewahi kusumbuliwa na matatizo ya unywaji wa pombe uliopitiliza na kulazwa katika hospitali moja ya waginjwa wa akili miaka mitano iliyopita, alionekana kuwa katika hali ya kilevi wakati wa shughuli za kijamii jijini Northampton Alhamisi iliyopita. Wakala wake Terry Baker amesema nyota huyo hawezi kumshukuru kwa kusema hivyo lakini anahitaji msaada wa haraka ili kumuepusha na kadhia hiyo. Baker amesema wakati alipomuona katika mipindi kabla ya sherehe za Noel Novemba mwaka jana alikuwa yuko sawa lakini hivi sasa hali hiyo imebadilika na anadhani hata mwenyewe Gazza analijua hilo. Naye golikipa nyota wa zamani wa klabu ya Manchester United, Peter Schmeichel alikitaka Chama cha Wachezaji wa Kulipwa kuingilia kati suala hilo na kuangalia jinsi ya kumsaidia nyota huyo ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Newcastle United, Tottenham Hotspurs, Lazio na Rangers.

UKURASA WA HABARI ZA KIMATAIFA: Wenger akunwa na mwanzo mzuri wa Nacho Monreal. Dembele awaonya wenzake kukosa nafasi nne za juu mwisho wa msimu na Michael Owen kukumbana na adhabu ya FA.




Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amefurahishwa na kiwango cha soka kilionyeshwa na nyota wake mpya Nacho Monreal katika mchezo ambao washika bunduki waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stoke hapo jana.
Katika mchezo huo Lukas Podolski alifunga goli pekee kunako dakika ya 78 ambalo limeifanya Arsenal kujikita katika nafasi ya 4 ya msimamo wa ligi huku Monreal akiwaonyesha jitihada kubwa katika sehemu ya ulinzi kwa mara ya kwanza.
Mlinzi huyo mpya alikuwa na muda mdogo sana wa kuzoea kikosi chake kipya akihitaji kijigeuza kidogo tu na kufanana na aina ya uchezaji wa timu hiyo yenye maskani yake Emirates kabla ya kuingia katika kikosi cha kwanza ambapo Wenger anaamini ulikuwa ni usajili chanya kumpata mhispania huyo.
Amekaririwa akisema kuwa pengine ingekuwa ni ngumu kwake kwani alikuwa anakutana na timu inayotumia nguvu sana nay eye akitokea katika soka la Hispania lakini anadhani Monreal ameweza.
"Jambo linalo ridhisha ni kwamba Monreal amekuwa na mwanzo mzuri, kwa mchezaji kuwasili jana na leo kuwa katika timu kwa ujumla alikuwa akiimarika kadri mchezo ulivyokuwa unaendelea"
Dembele akatishwa tamaa na kupata nafasi 4 za juu za msimu huu.
 Kiungo wa Tottenham Moussa Dembele amewaonya wachezaji wenzake kwamba wako katika hatari ya kuwa nje ya nafasi nne za juu katika ligi kuu ya soka nchini England, na kusema labda wabadilike na kurudi katika njia ya kusaka ushindi katika michezo inayoendelea ya ligi hiyo.
Amenukuliwa akisema
"Ukiangalia timu tuliyonayo hatuna sababu ya kuogopa timu yoyote katika Premier League, lakini tunakosa nafasi nyingi za kufunga, wakati mwingine tunapoteza points katika mchezo ambao tulistahili kushinda, inachanganya sana. Tuliposhinda Old Trafford msimu uliopita tulicheza mchezo mzuri sana.
Angalia sasa Arsenal, Chelsea, Liverpool wanapoteza points tulipaswa kuwa mbele yao”
Michael Owen kukabiliwa na adhabu ya FA
 Mshambuliaji wa Stoke Michael Owen huenda akakumbana na adhabu ya chama cha soka nchini England FA baada ya kuonekana akimfanyia kitendo kisichokuwa cha kiungwana kiungo wa Arsenal Mikel Arteta.
Wawili hao walikumbana katika harakati za kuwania mpira dakika za lala salama katika mchezo uliomalizika kwa Arsena kuibuka na ushindi wa bao 1-0 hapo jana, ambapo Arteta alikwenda kumkabili Owen ambaye alimsukuma kwa nyuma.
Mwamuzi Chris Foy hakutoa adhabu kwa ya kadi kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33 lakini kamera ilimuonyesha Owen akifanya kitendo hicho.
Hata hivyo bosi wa Stoke Tony Pulis baadaye akikaririwa akisema
"Arteta ndiye aliyemkabili ndivyo sivyo Owen na kwamba Michael hakufanya hivyo”

ROONEY AIPAISHA MAN UNITED POINTI 10 JUU

!


BPL_LOGONDANI ya CRAVEN COTTAGE, iliyozimika Umeme Dakika chache kabla Haftaimu na kusababisha Mechi isimame, Wayne Rooney alipiga Bao moja na la ushindi kwa Manchester United katika Dakika ya 79 walipoitungua Fulham Bao 1-0, na kuwapaisha kileleni wakiwa Pointi 10 mbele ya Timu ya Pili Man City ambao kesho wanaivaa Liverpool Uwanjani Etihad.
++++++++++++++++++++++
BPL:
MSIMAMO-Timu zaJuu:
1 Man United Mechi 25 Pointi 62
2 Man City  Mechi 24 Pointi 52
3 Chelsea  Mechi 25 Pointi 46
4 Tottenham  Mechi 24 Pointi 42
5 Everton  Mechi 25 Pointi 42
6 Arsenal  Mechi 25 Pointi 41
7 Liverpool Mechi 24 Pointi 35
++++++++++++++++++++++
Mechi hii ilikuwa mshikemshike huku kila upande ukikosa Mabao na Rooney kupiga posti lakini ushindi huu, bila shaka, utamfurahisha Sir Alex Ferguson kwa sasa na kuwaachia kibarua kikubwa wapinzani wao kuifukuza.
VIKOSI:
Fulham: Schwarzer, Riether, Hangeland, Senderos, Riise, Duff, Karagounis, Baird, Dejagah, Ruiz, Rodallega
Akiba: Etheridge, Petric, Frimpong, Hughes, Emanuelson, Davies, Kacaniklic.
Man United: De Gea, Da Silva, Ferdinand, Evans, Evra, Valencia, Cleverley, Carrick, Nani, Rooney, van Persie
Akiba: Amos, Anderson, Giggs, Smalling, Hernandez, Welbeck, Kagawa.
Refa: Kevin Friend
++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Februari 2
QPR 0 Norwich 0
Arsenal 1 Stoke 0
Everton 3 Aston Villa 3
Newcastle 3 Chelsea 2
Reading 2 Sunderland 1
West Ham 1 Swansea 0
Wigan 2 Southampton 2
Fulham 0 Man United 1
Jumapili Februari 3
[SAA 10 na Nusu Jioni]
West Brom v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
Man City v Liverpool

RONALDO AFUNGA, REAL YAFUNGWA!

 


>>LEO NI VALENCIA v BARCELONA, ATLETICO MADRID V REAL BETIS
>>LEO BUNDESLIGA MOTO: BAYER LEVERKUSEN v BORUSSIA DORTMUND!!
BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAAREAL MADRID, Mabingwa watetezi wa La Liga, wameendelea kuzorota kwenye Ligi hiyo na ni wazi washautema Ubingwa wao baada ya jana kuchapwa Bao 1-0 ugenini na Granada na Bao hilo kufungwa na Staa wa Real, Cristiano Ronaldo.
Bao la Granada lilifungwa katika Dakika ya 23 kufuatia Kona ya Gabriel Torje na Ronaldo kujifunga mwenyewe katika harakati za kuokoa.
Kipigo hiki kimewaacha Real wabakie nafasi ya 3 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Atletico Madrid walio nafasi ya pili na ambao wapo Pointi 11 nyuma ya Vinara Barcelona lakini zote, Barca na Atletico, zina Mechi moja mkononi ambazo watacheza leo.
RATIBA:
Jumapili Februari 3
Malaga v Real Zaragoza [Saa 8 Mchana]
Sevilla v Rayo Vallecano [Saa 1 Usiku]
Valencia v Barcelona [Saa 3 Usiku]
Atletico Madrid v Real Betis [Saa 5 Usiku]
Real Socieda v Real Mallorca [Saa 5 Usiku]
BUNDESLIGA
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Februari 2
Schalke 1 SpVgg Greuther Furth 2
VfL Wolfsburg 1 FC Augsburg 1
FSV Mainz 0 Bayern Munich 3
TSG Hoffenheim 2 SC Freiburg 1
Fortuna Dusseldorf 3 VfB Stuttgart 1
Hamburger SV 0 Eintracht Frankfurt 2
Jumapili Februari 3
FC Nuremberg v Borussia Mönchengladbach
Bayer 04 Leverkusen v BV Borussia Dortmund [Saa 1 na Nusu Usiku]
SERIE A
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Februari 2
Torino 0 Sampdoria 0
Napoli 2 Catania 0
Jumapili Februari 3
Chievo Verona v Juventus
Siena v Inter Milan
Pescara v Bologna
Palermo v Atalanta
Genoa v SS Lazio
Fiorentina v Parma
AC Milan v Udinese

AFCON 2013: WENYEJI AFRIKA KUSINI NJE KWA MATUTA!

  

>>LEO NI ROBO FAINALI: IVORY COAST v NIGERIA & BURKINA FASO v TOGO.
AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZEWenyeji wa AFCON 2013, Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Afrika Kusini, wametupwa nje ya Mashindano hayo kwa kushindwa Mikwaju ya Penati tano tano walipopigwa kwa Penati 3-1 na Mali baada ya kwenda sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo.
+++++++++++++++++
PENATI:
Afrika Kusini 1
-Tshabala= Alifunga
-Furman= Iliokolewa
-Mahlagu= Iliokolewa
-Majoro= Alikosa
Mali 3
-Diabate= Alifunga
-Tamboura= Alifunga
-M Traore= Alifunga
+++++++++++++++++
Katika Dakika 90, Afrika Kusini walitangulia kufunga kwa Bao la Tokelo Rantie katika Dakika ya 32 na Mali kurudisha Dakika ya 58 kwa Bao la Seydou Keita.
Mabao hayo yalidumu hadi Dakika 90 za Mchezo na Nyongeza ya Dakika 30 haikubadilisha matokeo hayo ndipo zikaja Penati na Afrika Kusini kufunga moja tu kupitia Siphiwe Tshabalala.
Leo zipo Robo Fainali mbili za mwisho kati ya Ivory Coast v Nigeria na Burkina Faso v Togo.
Mali watacheza na Mshindi kati ya Ivory Coast v Nigeria kwenye Nusu Fainali.
Mapema jana, Ghana waliichapa Cape Verde 2-0 na kutinga Nusu Fainali ambako watacheza na Mshindi kati ya Burkina Faso v Togo.
VIKOSI:
Afrika Kusini: Khune, Gaxa, Masilela, Khumalo, Sangweni, Furman, Mahlangu, Phala (Serero 89’), Letsholonyane, Parker (Tshabalala 105’), Rantie (Majoro 41’)
Mali: So Diakite, Diawara, Tamboura, A.Coulibaly, Wague, Keita, Sissoko (M Traore 55’), Sow, Sa Diakite (Diarra 24’), Maiga, Samassa (Diabate 88’)

UTAMU: ENGLAND v BRAZIL, FRANCE v GERMANY, HOLLAND v ITALY, SPAIN v URUGUAY!!

>>TANZANIA KUIVAA CAMEROON, DAR!!
>>MABINGWA DUNIANI SPAIN v URUGUAY, DOHA, QATAR!
BRAZIL_SAMBAJUMATANO FEB 6 ni Siku mahsusi kwenye Kalenda ya FIFA kuchezwa Mechi za Kimataifa na Nchi nyingi zimeandaa Mechi za Kirafiki lakini huko Marekani ya Kaskazini na ya Kati watakuwa na Mechi za Mchujo kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil na Barani Asia wana Mechi za Mchujo za Kombe la Mataifa ya Asia.
Hapa Bongo, Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, itakuwa na Mechi kamambe dhidi ya Vigogo wa Afrika, Cameroon, inayoongozwa na Gwiji Samuel Eto’o itakayochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mabingwa wa Dunia na pia Barani Ulaya, Spain, wao watakuwa Nchini Qatar, Mjini Doha, kuivaa Timu ngumu ya Uruguay.
MECHI== Siku ya Kalenda ya FIFA
[Zote Kirafiki isipokuwa inapotajwa]
Jumatano, Februari 6
France v Germany
Netherlands v Italy
Belgium v Slovakia
Wales v Austria
Turkey v Czech Republic
Greece v Switzerland
Scotland v Estonia
England v Brazil
Republic of Ireland v Poland
Israel v Finland
Sweden v Argentina
Japan v Latvia
Norway v Ukraine
Malta v Northern Ireland
Spain v Uruguay [Doha, Qatar]
Azerbaijan v Liechtenstein [Dubai, UAE]
Portugal v Ecuador
Croatia v Korea Republic
Hungary v Belarus
Slovenia v Bosnia Herzegovina
Moldova v Kazakhstan
FYR Macedonia v Denmark
Albania v Georgia
Nepal v Pakistan
India v Palestine
Guatemala v Colombia
Chile v          Egypt
Iceland v Russia
Romania v Australia
Kenya v Libya
Cyprus v Serbia
Paraguay v El Salvador
Myanmar v Philippines
Trinidad and Tobago v Peru
Bolivia v Haiti
Tanzania v Cameroon
Zimbabwe v Botswana
MCHUJO KOMBE LA DUNIA 2014
Honduras v USA
Mexico v Jamaica
Panama v Costa Rica
MCHUJO KOMBE LA MATAIFA ASIA
Yemen v Bahrain
Iran v Lebanon
Uzbekistan v Hong Kong
Jordan v Singapore
Oman v Syria
Iraq v Indonesia [Kuchezwa Dubai, UAE]
Vietnam v United Arab Emirates
Qatar v Malaysia
Thailand v Kuwait
Saudi Arabia v China PR

AKINA ETOO WANATARAJIA KUWASILI DAAAAR LEO TAYARI KUWAKABILI STARS


Eto'o

WAKATI kundi la kwanza la timu ya Cameroon lenye watu 13 linaingia nchini leo (Februari 3 mwaka huu) saa 4.40 usiku, kundi la pili linaloongozwa na nahodha wa timu hiyo Samuel Eto’o linatua kesho (Februari 4 mwaka huu) saa 3.45 asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Eto’o anayechezea timu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi atatua kwa ndege ya Kenya Airways akiwa na Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha wa SC Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik.
Saa moja baadaye baada ya Eto’oo kutua na wenzake, Kocha wa timu hiyo Jean Paul Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou watawasili saa 4.40 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways wakitokea Afrika Kusini.
Kesho pia kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM ambalo lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa, mshambuliaji Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa Udinese ya Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya Ufaransa.
Wachezaji waliobaki wakiongozwa na kiungo wa Barcelona, Alexandre Song watawasili Februari 5 mwaka huu kwa muda tofauti kwa ndege za KLM na Kenya Airways.
Wakati huo huo: Waamuzi kutoka Rwanda wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ndiyo watakaochezesha pambano katika Tanzania na Cameroon litakalochezwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi wa katikati atakuwa Munyemana Hudu wakati wasaidizi wake ni Simba Honore na Ndagizimana Theogine wakati mwamuzi wa mezani ambaye pia anatambuliwa na FIFA atakuwa Oden Mbaga wa Tanzania.
Hudu na wenzake watawasili nchini kesho (Februari 4 mwaka huu) saa 12.40 jioni kwa ndege ya RwandAir na wamepangiwa kufikia kwenye hoteli ya JB Belmont. Mechi ambayo ni moja kati ya nyingi zitakazochezwa siku hiyo (FIFA Date) itafanyika kuanzia saa 11 kamili jioni.

MECHI YA JANA YA YANGA WA UTURUKI NA MTIBWA WA MANUNGU MOROGORO YAINGIZA MILLIONI 100 NA USHEEEEE


Hamisi Kiiza wa Yanga kulia akijiandaa kupiga mpira mbele ya beki wa Mtibwa jana 


MECHI namba 100 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 125,181,000.
Watazamaji 22,030 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,356,002.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 19,095,406.78.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 19,583 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 97,915,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,435,255.48, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 9,261,153.29, Kamati ya Ligi sh. 9,261,153.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,630,576.64 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,601,559.61.