Thursday, November 15, 2012

UNAIKUMBUKA SIKU SAFU NZIMA YA CHELSEA ILIVYOTESWA NA JAMAA HUYU RADAMEL FALCAO.???KAMA ULIMISS KUIANGALIA MECHI HIYO INGIA HUMU


DABI ya LONDON Jumamosi: AVB adai Spurs ni lazima wawe juu ya Arsenal!! 

>>AVB akata tamaa Ubingwa, ataka nafasi ya 4 tu!!

>>AKIRI BINGWA Ni Man United, City au Chelsea, walobaki kugombea 4!
AVB_ACHUCHUMAAIli kuishika nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England ili wapate fursa ya kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, Andre Villas-Boas anaamini Tottenham ni lazima wamalize Ligi wakiwa juu ya Arsenal Msimu huu.
Lakini mara ya mwisho kwa Tottenham kumaliza Ligi wakiwa mbele ya Arsenal ni Mwaka 1995 wakati hata Arsene Wenger, Meneja wa sasa wa Arsenal, hajaanza kibarua.
Msimamo huo wa Villas-Boas umetolewa kwenye mahojiano na Wanahabari kuhusu Dabi yao na Arsenal itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Emirates.
Villas-Boas alijibu swali kuhusu nini lengo lao Msimu huu kwa kusema: “Ninachoona ni dhahiri Man United, Man City na Chelsea wapo kwenye mbio kubwa za Ubingwa. Ingawa ngumu kumaliza nafasi ya 4 lakini ni lazima tumalize juu ya Arsenal ili kuipata.”
++++++++++++++++++++++++
DONDO za DABI: Arsenal v Tottenham
-Tottenham wamepoteza Mechi moja tu kati ya 5 walizocheza mwisho na Arsenal.
-Magoli 100 yamefungwa katika Dabi 32 tangu Arsene Wenger atue Arsenal
++++++++++++++++++++++++
Kimsimamo, kwa sasa, Tottenham wapo nafasi ya 7 wakiwa Pointi 1 mbele ya Arsenal walio nafasi ya 8.
Tottenham wapo Pointi 7 nyuma ya Timu ya 3 Chelsea na Pointi 10 nyuma ya vinara Manchester United.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
Msimu uliopita Arsenal walimaliza wakiwa nafasi ya 3 na Tottenham nafasi ya 4 lakini Tottenham hawakupewa nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kama ilivyotakiwa kwa vile Chelsea walitwaa Ubingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI na hivyo kupewa nafasi ya kutetea Taji lao na Tottenham kutupwa kwenye EUROPA LIGI.
Wakati huo huo, Villas Boas amethibitisha Kiungo wa Belgium Mousa Dembele hatacheza Dabi hiyo na Arsenal kwa vila bado ana tatizo la nyonga.
Baada ya kuumia nyonga, Dembele amezikosa Mechi 8 za Tottenham.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City
MAREFA-Ratiba ya Mechi zao:
Jumamosi Novemba 17
Arsenal v Tottenham
Refa: H Webb
Refa Wasaidizi: M Mullarkey,  D Cann
Refa wa Akiba: C Foy
Reading v Everton
Refa: M Atkinson
Refa Wasaidizi: P Kirkup, J Flynn
Refa wa Akiba: A Marriner
West Bromwich Albion v Chelsea
Refa: M Oliver
Refa Wasaidizi: S Child, D England
Refa wa Akiba: S Attwell
Manchester City v Aston Villa
Refa: J Moss
Refa Wasaidizi: S Beck, A Holmes
Refa wa Akiba: L Probert
Newcastle United v Swansea City
Refa: P Dowd
Refa Wasaidizi: A Garratt, S Ledger
Refa wa Akiba: A Bates
Queens Park Rangers v Southampton
Refa: M Dean
Refa Wasaidizi: J Collin, J Brooks
Refa wa Akiba: L Mason
Liverpool v Wigan Athletic
Refa: K Friend
Refa Wasaidizi: R Ganfield, A Halliday
Refa wa Akiba: J Adcock
Norwich City v Manchester United
Refa: A Taylor
Refa Wasaidizi: R West, P Bankes
Refa wa Akiba: N Swarbrick
Jumapili Novemba 18
Fulham v Sunderland
Refa: L Probert
Refa Wasaidizi: D Bryan, L Betts
Refa wa Akiba: A Marriner
Jumatatu Novemba 19
West Ham United v Stoke City
Refa: C Foy
Refa Wasaidizi: H Lennard, M McDonough
Refa wa Akiba: H Webb
 

BPL: Baada Robo Msimu, Msimamo kufuata Historia, kubaki hivi hivi??


>>KWA MIAKA 20, BAADA Mechi 10, ni mara 3 tu Man United kileleni na mara zote 3 walimaliza Mabingwa!!!
>>FAHAMU MAREFA MECHI ZA WIKENDI HII!
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
FERGIE_MAZOEZINIAkijibu swali mara baada ya kuifunga Manchester United Bao 1-0 katika Wikiendi ya ufunguzi ya MsimuWENGER_AHIMIZA12 huu wa Ligi Kuu England, Meneja wa Everton David Moyes alisema ni mapema kuitathmini Timu yake labda baada ya Mechi 10, msimamo ambao ulichukuliwa pia na Mameneja wa Arsenal, Arsene Wenger, na wa Newcastle, Alan Pardew, na leo hii Timu zimeshacheza Mechi 11, Robo ya Ligi nzima, na Manchester United ndio wako kileleni, hii ikiwa mara yao ya 3 tu kuwa hapo baada ya Mechi 10 ingawa wametwaa Taji mara 12 lakini katika mara zote hizo 3 walizokuwa kileleni wao ndio waliibuka Mabingwa.
Akiongea, Meneja wa zamani wa England, Graham Taylor, alisema: “Msimamo wa Ligi wa Kipindi hiki huwa haubadiliki sana ifikapo Mwezi Mei. Pengine zitatokea Klabu moja au mbili ambazo zitaleta maajabu lakini si zaidi.”
Nae David Pleat, Meneja wa zamani wa Tottenham, amesema: “Baada ya Robo ya Msimu, unapata fununu nini kitaendelea. Klabu mbili za Manchester zipo juu pamoja na Chelsea. Inawezekana Masimu huu Timu ngeni ikakamata nafasi ya 4 ingawa Arsenal na Tottenham hawatakuwa mbali.”
Akiongeza, David Pleat, alisema wasiwasi mkubwa ni ule uwezekano wa Klabu mbili au tatu kufungua pengo kubwa kileleni na pia Klabu za mkiani kuachwa mbali nyuma.
Ingawa kwa wakati huu Msimamo hauleti dira ya kweli nini kitatokea mwishoni mwa Msimu lakini takwimu zinaonyesha katika Miaka 20 Man United, chini ya Sir Alex Ferguson, imetwaa Taji mara 12 na katika mara hizo walikuwa kileleni mara 3 tu baada ya Mechi 10 lakini katika mara zote hizo 3 walimaliza Msimu wakiwa Mabingwa na hilo limemfanya Graham Taylor atamke: “Hiyo ni dalili mbaya kwa Wapinzani wa Man United. Kawaida hawaanzi Ligi vizuri na ni baadae ndio wanakaza uzi lakini sasa wapo juu bila hata kuonekana wamegangamara.”
Mbali ya mbio za Ubingwa na kumaliza kuwa katika Timu 4 bora ili kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, pia ipo vita ya kujinusuru kutimuliwa kwa Mameneja wa Timu zinazofanya vibaya na pia ile vita ya kukwepa kuporomoka Daraja.
Wakiwa mkiani, Meneja wa Southampton, Nigel Adkins, amekiri yeye ndie anaeongoza kwa kuwa Meneja wa kwanza kutegemewa kumwaga unga hali ambayo pia inampa presha Mark Hughes, Meneja wa QPR, ambae Timu yake ipo juu tu ya Southampton.
Katika historia ya Ligi Kuu England, Klabu ambayo pia ilifungwa bao nyingi kufikia hatua hii ya Mechi 10 kama ambavyo Southampton imefungwa, Mabao 28, ni Barnsley katika Msimu wa 1997/8 na ikashushwa Daraja.
Graham Taylor amezitambua West Bromwich Albion chini ya Meneja Steve Clarke, ambao wapo nafasi ya 5, Fulham, nafasi ya 8 na Wigan, nafasi ya 13, kuwa ndizo Timu zinazostahili pongezi kwa mafanikio yao kufikia hatua hii ya Mechi 10.
Pamoja na hizo pia aliipa mkono Everton kwa wanzo mwema ambapo sasa wapo nafasi ya 4.
Akiizungumzia Wigan, ambayo katika hatua hii Msimu uliopita ilikuwa mkiani na hatimae kujikokota na kujinusuru na kumaliza ikiwa nafasi ya 15, David Pleat amesema: “Timu zinazosuasua hubadilisha Mameneja, hubadilisha Wachezaji kwenye Dirisha la Uhamisho, lakini Wigan hawakufanya hata moja kati ya hayo! Meneja Roberto Martinez alibadilisha Mfumo wa Uchezaji na hilo limeleta mafanikio makubwa! Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na wengine!”
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City
MAREFA-Ratiba ya Mechi zao:
Jumamosi Novemba 17
Arsenal v Tottenham
Refa: H Webb
Refa Wasaidizi: M Mullarkey,  D Cann
Refa wa Akiba: C Foy
Reading v Everton
Refa: M Atkinson
Refa Wasaidizi: P Kirkup, J Flynn
Refa wa Akiba: A Marriner
West Bromwich Albion v Chelsea
Refa: M Oliver
Refa Wasaidizi: S Child, D England
Refa wa Akiba: S Attwell
Manchester City v Aston Villa
Refa: J Moss
Refa Wasaidizi: S Beck, A Holmes
Refa wa Akiba: L Probert
Newcastle United v Swansea City
Refa: P Dowd
Refa Wasaidizi: A Garratt, S Ledger
Refa wa Akiba: A Bates
Queens Park Rangers v Southampton
Refa: M Dean
Refa Wasaidizi: J Collin, J Brooks
Refa wa Akiba: L Mason
Liverpool v Wigan Athletic
Refa: K Friend
Refa Wasaidizi: R Ganfield, A Halliday
Refa wa Akiba: J Adcock
Norwich City v Manchester United
Refa: A Taylor
Refa Wasaidizi: R West, P Bankes
Refa wa Akiba: N Swarbrick
Jumapili Novemba 18
Fulham v Sunderland
Refa: L Probert
Refa Wasaidizi: D Bryan, L Betts
Refa wa Akiba: A Marriner
Jumatatu Novemba 19
West Ham United v Stoke City
Refa: C Foy
Refa Wasaidizi: H Lennard, M McDonough
Refa wa Akiba: H Webb


UNAIKUMBUKA SIKU SAFU NZIMA YA CHELSEA ILIVYOTESWA NA JAMAA HUYU RADAMEL FALCAO.???KAMA ULIMISS KUIANGALIA MECHI HIYO INGIA HUMU



 

WACHIMBA ALMASI WA SHINYANGA TIMU YA MWADUI FC WAISHINDILIA KIKAPU CHA MAGOLI TIMU YA  WAPIGA KWATA YA POLISI DODOMA 4-0


Timu ya mwadui FC ya mkoani shinyanga leo imeicharaza timu ya maafande wa polisi dodoma mabao 4-0 mchezo uliochezwa katika dimba la kambarage shinyanga mchezo wa kiporo ambao ungechezwa jana lakini ukaahirishwa kutokana na timu ya taifa ya tanzania taifa stars kuwa na mchezo wa kirafiki ulioko katika kalenda ya FIFA .

Mabao ya timu ya mwadui fc yamefungwa na CHIKA CHUKU aliyefunga 2,la tatu limefungwa na MWANDENGE SADICK na bao la nne limefungwa na EYE SALIM na kuhitimisha idadi ya mabao 4-0 dhidi ya wapiga kwata wa polisi dodoma .

Nao maafande wa polisi tabora wameshindwa kutamba mbele ya watoto wa mjini timu ya pamba katika dimba la CCM KIRUMBA mwanza baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 na kuhitimisha raundi ya kwanza wakiwa wanashika nafasi ya saba na pointi zao 3 baada ya kucheza michezo saba.

Na kule katika dimba la lake tanganyika kigoma timu ya wnajeshi la wananchi JKT kanembwa wameibamiza timu ya maafande wa polisi mara bao 1-0 na kuhitimisha raundi ya kwanza ya ligi daraja la kwanza katika KUNDI C

Ambapo jana Timu ya maafande wa jeshi la wananchi  ya mkoani tabora  RHINO RANGERS jana waliendelea  kuwapa raha wakazi wa tabora baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya moran fc ya kiteto manyara kule.

Mabao ya rhino rangers hiyo jana yalifungwa  na SHIJA MONGO na ABDALAH SIMBA mshambuliaji ambaye ananguvu ,kasi,mashuti na mtaalaamu wa kumiliki mpira .

  MSIMAMO KUNDI C
1.RHINO RANGERS MECHI 7 POINTI 17
2.KANEMBWA JKT MECHI 7 POINTI 16
3.MWADUI FC MECHI7 POINTI 13
 4.PAMBA MECHI 7 POINTI 11
5.POLISI DODOMA MECHI 7 POINTI 8
6.POLISI MARA MECHI 7 POINTI 5
7.POLISI TABORA MECHI 7 POINTI 3
8.MORAN FC MECHI 7 POINTI 2

FAHAMU;Kila kundi litatoa timu moja ambayo itapanda ligi kuu ya vodacom tanzania bara VPL msimu ujao na tayari timu ya maafande ya polisi moro imeonyeshwa mlango wa kutokea kwani imemaliza mzunguko wa kwanza wa  VPL ikiwa imecheza mechi 13 na ina pointi 4 inashika mkia.timu zitakazo panda ni kutoka kundi A,B,na C

 MATOKEO TOKA LIGI IANZE oktoba 24
===Kanembwa vspolisi dodoma 3-0
===pamba vs polisi mara 3-2
===rhino rangers vs polisi tabora 2-1
===mwadui vs moran 3-0

oktoba 27
====polisi tabora vs polisi dodoma 0-1
====mwadui vs polisi mara 3-0
====kanembwa JKT vs moran 2-0
====pamba vs rhino rangers 1-1

oktoba 31
====polisi mara vs rhino rangers 0-0
====moran vs polisi tabora 1-1
====polisi dodoma vs pamba2-0
====kanembwa vs mwadui 3-2

novemba 4
===polisi mara vs polisi tabora 1-1
===moran vs polisi dodoma1-1
===rhino rangers vs kanembwa JKT 3-1
===mwadui vs pamba...2-0......

novemba 7
====polisi tabora vs kanembwa  JKT 1-4
====polisi dodoma vs polisi mara 0-0
====pamba vs moran ya manyara 2-0
novemba 8
====rhino rangers vs mwadui FC 2-0

novemba 11
====kanembwa vs pamba 0-0
====polisi tabora vs mwadui 0-0
====polisi dodoma vs rhino rangers 0-2
====polisi mara vs moran 3-1

  Novemba 14

===rhino rangers vs moran fc 2-1

novemba 15

===JKT kanembwa vs polisi mara 1-0

===mwadui fc vs polisi dodoma 4-0

===pamba vs polisi tabora 2-1

 

SERENGETI BOYS WAKIKUSANYA SUMU ZA KUULIA WAKONGO JIONI HII TAIFA

Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys wakifanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii kujiandaa na mchezo dhidi ya Kongo Brazzaville, Jumapili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika nchini Morocco mwakani.

Kocha wa makipa wa Serengeti Boys, Manyika Peter akiwanoa vijana wake 

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen akiwaelekeza vijana wake

Makipa wakiranya mazoezi

Makipa

Julio akiwaongoza vijana wake

Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Jacob Michelsen akiwaelekeza kwa mifano vijana wake

Julio akiwaongoza kwa mifano vijana wake

Darasa, makocha wakiwapa mawaidha vijana

Kocha Msaidizi wa Serengeti Boys, Jamhuru Kihwelo ‘Julio’ akijiandaa kuingia uwanjani kuwanoa vijana

Dk Nassor Matuzya akimtibu jeraha mchezaji wa Serengeti Boys, Nizar Criston

Vijana mazoezini

Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys wakiomba dua kabla ya kuanza mazoezi yao Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii kujiandaa na mchezo dhidi ya Kongo Brazzaville, Jumapili kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika nchini Morocco mwakani.

Vijana mazoezini

Julio akishuhudia vijana wake wanavyopitisha mipira kwenye njia zake

Vijana mazoezini, Michelsen kulia

Kocha wa makipa wa Serengeti Boys, Manyika Peter akiwanoa vijana wake 

Kipa wa Serengeti Boys, Peter Manyika, mtoto wa kocha wa makipa wa timu hiyo, Manyika Peter akidaka kwa uhodari

Kipa wa Serengeti Juma Hamadi akidaka kwa umahiri

 

NAHODHA WA ZAMANI CAMEROON AFARIKI DUNIA.

SHIRIKISHO la Soka la Cameroon limesema kuwa aliyekuwa nahodha wa zamani wa Cameroon, Theophile Abega ambaye alikiongoza kikosi cha nchi hiyo kushinda taji lake la kwanza karibu miongo mitatu iliyopita amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58. Katika taarifa ya shirikisho hilo iliyotumwa katika mtandao haikufafanua haswa chanzo cha kifo cha nyota huyo lakini kuna taarifa zilizozagaa kwamba nyota amefariki dunia kutokana na tatizo la moyo wake kusimama ghafla inayojulikana kitaalamu kama Cardiac Arrest. Abega alikuwa nahodha wa Cameroon wakati iliponyakuwa kwa mara kwanza Kombe la Mataifa ya Afrika mwkaa 1984 wakati alipofunga bao katika ushindi wa mabao 3-1 iliyopata nchi hiyo dhidi ya Nigeria jijini Abidjan, Ivory Coast. Katika mwaka huo Abega ambaye pia alikuwa ya kikosi cha Cameroon kilichoshiriki michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1982, alitajwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kutokana na mchango wake alioonyesha katika michuano hiyo. Nyota hyo amewahi kucheza katika klabu ya Canon Younde katika miaka ya 80 kabla ya kutimkia Ulaya katika klabu ya Toulouse ya Ufaransa na baadae Vevey Sport ya Switzerland na baadae kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 33.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Barcelona, Alexis Sanchez atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nne baada ya kuumia mguu. Sanchez mwenye umri wa miaka 23 alilazimika kutolewa baada ya dakika 20 toka kuanza kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya nchi yake na Serbia Jumatano ambapo matokeo ya uchunguzi yamethibisha kuwa nyota huyo atakuwa nje ya uwanja kipindi hicho. Kama majeraha hayo yakimuweka nje ya uwanja kwa kipindi hicho kama Barcelona wanavyohofia inamaanisha kuwa nyota huyo atakosa michezo muhimu miwili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Spartak Moscow na Benfica pamoja na ule wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid. Sanchez amekuwa na historia ya kurejea katika majukumu ya kimataifa akiwa amjeruhi mara kwa mara kitu ambapo kimekuwa kikimnyima usingizi kocha wa Barcelona Tito Vilanova ambaye majeruhi katika kikosi chake kimekuwa kitu cha kawaida.

SUAREZ NOT FOR SALE - RODGERS.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amesema uwa mshabuliaji nyota wa kikosi chake Luis Suarez atabakia klabuni hapo na kusisitiza kuwa hakuta kuwa na dau lolote la kuuzwa kwa mchezaji hyo katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Suarez mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia kwa mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Manchester City hatahivyo Rodgers alikanusha tetesi hizo na kudai kuwa nyota huyo atabakia klabuni hapo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay alisaini mkataba mpya na Liverpool katika kipindi cha ajira ya kiangazi na amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu akiwa amefunga mabao 11 katika michezo 16 aliyocheza. Suarez alihamia Liverpool akitokea Ajax Amsterdam ya Uholanzi kwa ada ya paundi milioni 22.7 Januari mwaka 2011.

 

NDANDA NA MORO UNITED NGUVU SAWA


 TIMU ya Moro United inayoshiriki ligi daraja la kwanza juzi zilitoshana nguvu na Ndanda FC ya Mtwara kwa kufungana bao 1-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume jijini, Dar es Salaam.

Ndanda ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya kwanza kupitia kwa Elias Ndokezi lakini Moro walisawazisha bao hilo dakika ya 30 kupitia kwa Gideon Benson.

Timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko lakini hakuna timu iliyoweza kuongeza bao.

Kocha wa Ndanda Amri Ibrahim alisema wachezaji wake hasa safu ya viungo na washambuliaji wamesababisha kupoteza mchezo huo kwani walikosa nafasi nyingi za wazi za kufunga.

"Washambuliaji na viungo wamesababisha tupoteze mchezo ila tutajipanga turekebishe makosa", alisema Amri.

Naye kocha wa Moro United, Mwinyi Kassembo alisema wanashukuru kwa matokeo hayo kwani yanatia matumaini kutokana na kuwa alipokea timu ikiwa haina pointi baada ya kucheza michezo mitatu.

"Nashukuru leo ni mchezo wa pili tunatoka sare baada ya kupokea timu ikiwa haina pointi", alisema Kassembo.

Awali Moro ilikuwa inafundishwa na Yusuph Macho na kutokana na matokeo mabovu uongozi uliamua kumfukuza.

Uwanja wa Mabatini, Pwani timu ya Polisi ya Dar es Salaam ilipokea kipigo cha bao 1-0 toka kwa Tesema ya Temeke.

 

RAGE AWAPOTEZEA WANACHAMA WALIOJIORODHESHA KUMNG'OA

MWENYEKITI wa klabu ya Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema kwamba uongozi umebaini kwamba wengi wa wanachama wa tawi la Mpira Pesa waliojiorodhesha ili kushinikiza kufanyika  kwa mkutano wa dharura wa klabuu hiyo si hao. 
Hatua hiyo inafuatia wanachama hao kufanya maadhimio ya kujiorodhesha ili kufikisha akidi itakayotimiza mashaerti ya kufanyika kwa mkutano ili kuwaonmdoa madarakani viongozi wa sasa kwa madai ya kushindwa kuongoza. 
Rage amesema pamoja na  kubaini hilo, pia uongozi umegundua kwamba majina  ya wanachama hao yamenakiliwa katika leja ya wanachama ambayo ilipotea mikononi mwa kiongozi mmoja wa zamani. 
Alisema uongozi unaheshimu jitihada zinazofanywa na wanachama hao na kuzifanyia kazi, lakini hauwezi kutekeleza vitu ambavyo havikidhi vigezo vilivyopo katika katiba ya klabu hiyo.
 Rage alisema, katiba ya sasa ya Simba haiwatambui wanachama waliopo kwenye leja, badala yake inawatambua wale waliosajiliwa katika kompyuta.
 “Pamoja na wanachama hao kunakiliwa katika leja,tumebaini hata saini zilizowekwa ni za kughushi na tukifanya uchunguzi hasa tutabaini ni wengi tu hawana sifa,  kitu ambacho kinakwenda kinyume na katiba ya Simba,”alisema Rage
 Rage aliongeza kuwa, wanaamini mchakato huo unafanywa na baadhi ya watu wanaotaka kuleta chokochoko ndani ya klabu hiyo kitu ambacho ni kigumu kukitimiza kwa vile uongozi upo imara na unafuata katiba ya klabu hiyo.
 “Hatuwezi kujiuzuilu kwa ajili ya shinikizo la watu ambao tunafahamu wanatumika, sisi tunaongoza kwa kufuata katiba na tutachukua uamuzi kwa mujibu wa katiba pindi inapostahili,”alisema
 Aidha, Rage aliongeza kwamba uongozi wa klabu hiyo ulitarajiwa kukutana jioni ya jana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mwenendo mbaya wa timu hiyo katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom uliomalizika wiki iliyopita na Simba kushika nafasi ya tatu.
 Hivi karibuni baadhi ya wanachama waliutakla uongozsi wa Simba chini ya Rage kuachia ngazi baada ya timu hiyo ambayo ilikuwa ikiongoza ligi kwa kipindi kirefu kupoteza mwelekeo baada ya kupoteza michezo yake.

 

MGOSI ACHUKUA NAFASI YA BAHANUZI CHINA

Mussa Mgosi

MUSSA Hassan Mgosi ameondoka jana kwenda China kucheza soka ya kulipwa, akichukua nafasi ya Said Bahanuzi, ambaye klabu yake, Yanga imemzuia.
Habari  ambazo nimezipata  zimesema kwamba Mgosi ambaye amesajiliwa JKT Ruvu ya Pwani msimu huu, akitokea DC Motemba Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ameondoka na wachezaji wengine wawili wa ‘mchangani.
“Baada ya Yanga kuwazuia Cannavaro (Nadir Haroub) na Bahanuzi, nafasi zao wamechukua Mgosi na vijana wengine wawili, mmoja kipa na mwingine beki, kutoka mchangani tu, lakini wanajua sana,”kilisema chanzo cha habari.
Mgosi hakucheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kutokana na kukosa hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kutoka DRC.
Cannavaro na Bahanuzi waliotarajiwa kuondoka juzi saa 10:00 jioni kwa ndege ya Qatar Airways kwenda China, kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa, walizuiwa na klabua yao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Ahmad Bin Kleb alisema kwamba, sababu za kuzuiwa kwa wachezaji hao ni kutokana na klabu inayowataka kutofuata taratibu.
“Hawajatuma barua, hawa wanataka kwenda kienyeji tu, na sisi si kama tumewazuia, tumeitaka kwanza hiyo klabu ifuate taratibu kwa kutuma barua huku na kujitambulisha, ili hata hao wachezaji wakipata matatizo tujue tunaanzia wapi,”alisema Bin aKleb.
Mapema wiki hii, Cannavaro, Nahodha Msaidizi wa Yanga  alisema  kwamba wanakwenda China kwa wiki mbili na baada ya majaribio kama wakifuzu, klabu inayowataka itafanya mazungumzo na klabu yao.
“Sisi wote tuna mikataba na klabu, hivyo tukifuzu jamaa itabidi watuhamishe Yanga,”alisema  beki huyo kati aliyezaliwa Februari 10, mwaka 1982.
Cannavaro yupo Yanga tangu mwaka 2006, aliposajiliwa kutoka Malindi ya Zanzibar wakati Bahanuzi amesajiliwa msimu huu akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Mwaka 2009, Cannavaro alichukuliwa kwa mkopo na klabu ya Vancouver Whitecaps ya Canada na baada ya miezi sita alirejeshwa Yanga alikoendelea kucheza hadi leo anakwenda kujaribu bahati yake China.
Bahanuzi ameingia na zali la aina yake Yanga SC, kwani katika mashindano ya kwanza kuichezea klabu hiyo alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame.
Hadi sasa, Said Bahanuzi   maarufu kama Spider Man, ameifungia Yanga mabao 12 katika mechi 14, yakiwemo matatau ya penalti tangu ajiunge na timu hiyo Julai mwaka huu.
Kwa sasa China ni nchi ambayo mastaa wengi waliokuwa Ulaya wanakwenda kumalizia soka yao, mfano washambuliaji wawili wa zamani wa Cheslea, Didier Drogba na Nicolas Anelka waliopo Shenghua Shanghai. Anelka ni kocha mchezaji.   

 

CONGO YAWASILI KUIVAA SERENGETI BOYS


Congo Brazzaville imewasili leo alfajiri (Novemba 15 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya Tanzania (Serengeti Boys) itakayochezwa Jumapili.

Timu hiyo imewasili kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 18 ambapo imefikia kwenye hoteli ya Sapphire. Mechi hiyo itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Serengeti Boys inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa chini ya Kocha wake Jackob Michelsen wakati Congo inafanya mazoezi leo jioni Uwanja wa Karume, na kesho (Novemba 16 mwaka huu) asubuhi na jioni itafanya mazoezi kwenye uwanja huo huo.

Timu hiyo ambayo katika raundi ya pili iliitoa Zimbabwe itafanya mazoezi yake ya mwisho Jumamosi jioni kwenye Uwanja wa Taifa. Viingilio kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa VIP A, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP C ni sh. 2,000 tu. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu ni sh. 1,000 tu.

Makocha wa timu zote mbili na manahodha wao watakutana na waandishi wa habari Jumamosi saa 5 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuzungumzia maandalizi yao kwa ajili ya mechi hiyo kabambe.

 

Shola Ameobi NIMEFARIJIKA KUCHEZEA NIGERIA

Mshambuliaji wa Newcastle United  Shola Ameobi amefarijika  kuichezea kwa mara ya kwanza Timu ya taifa ya   Nigeria pale walipo ifunga   Venezuela huko  Florida jna  Jumamatano katika mechi ya kirafiki .

 Mchezaji huyo wa zamani wa Timu ya taifa ya uingereza Chini ya Miaka 21 aliingia kipindi cha pili baada ya kocha wa Nigera Stephen Keshi kufanya mabadiliko kwa kumtoa Onazi Ogenyi anayekipiga Lazio ya italia  katika mechi ya kirafiki ambayo Nigeria ilishinda mabao   3-1 .

 Japokuwa alicheza kwa nusu saa ,Mshambuliaji huyo  alifarijika baada yakucheza moja ya mechi ya kimataifa maishani mwake 
 "Ni mechi yangu ya kwanza ,Nina jiskia heshima kucheza soka ya kimataifa aliimbia tovuti ya BBC

 Ameobi alishangiliwa na mashabiki na maofisa baada ya kusaidia kupatikana kwa bao la tatu  kijana huyo mwenye miaka 31- hana jingine bali kuwaheshimu wachezaji kwa kazi waliyoifanya kiwanjani hapo jana .

 

TENGA NAKUOMBA RADHI POPOTE ULIPO :SAAD KAWEMBA

Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la kandanda la Tff .
Saad Kawemba amemuomba radhi Rais wa shirikisho la kandanda la Tanzania Leodgar Chila Tenda ,
Mara baada ya moja ya watazamaji katika kipindi cha Tuongee Asubuhi Kinachorushwa na Star Tv ya Mwanza kumtuhumu waziwazi kuwa Rais wa shirikisho aache kupendelea na kutumbua pesa za shirikisho hilo.

Akijibu kwa hudhuni ya hari ya juu mkurugenzi wa mashindano ya tff ambaye yupo mwanza kikazi alijibu swali hilo kwa kusema kuwa Rais wa tff hausiki katika maamuzi ya aina yoyote ile yanayofanywa na baadhi ya kamati teule zinazosimamia mambo mbalimbali yahusuyo soka  katika shirikisho hilo.  Kawemba alisema kama Tenga angeamua kupendelea basi leo hii Pan Afrika isingeshuka daraja kwani ndiyo timu yake tena aliongeza kwa kusema kuwa timu hiyo imeshuka daraja wakati yeye akiwa Madarakani .

Kwa upande mwingine amesema hari ariyonayo Bwana Tenga kifedha ni kwa mambo yake mengine ambayo haiusiani kabisa na fedha za shirikisho hilo na sio mbadhilifu kama watu wanavyoweza kufikiri .
alimaliza kwa kusema kuwa Rais tenga hana sifa hizo kwani  ni moja kati ya viongozi waadilifu katika soka la tanzania na kusisitiza kuwa kila kamati imepewa majukumu yake na yeye huwa aingilii kamati ya aina yeyote ikiwemo ya usajiri.

Mtazamaji huyo ailipiga simu kutoka katika mkoa wa Mmoja hapa Tanzania ambapo alimtuhumu rais wa TFF kuwa amekuwa akipendelea moja ya klabu kubwa Tanzania na amekuwa akitumia pesa za shirikisho la soka kujinufaisha Binafsi  jambo lililomfanya kawemba kumuomba radhi rais Tenga  ambaye ilibidi aweke sawa kutokana kuwa alikuwa akiheshimu kipindi na mtazamaji aliyepiga simu.

 

BONDIA KING CLASS MAWE AENDELEA KUJIFUA KUMKABILI SAIDI MUNDI DESEMBA 9



Bondia Mohamed Hemedi 'Kadogo Ninja' kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika Kambi ya Ilala Dar Es salaam Class anajiandaa na mpambano wake na Said Mundi utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam picha na  www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mohamed Hemedi 'Kadogo Ninja' kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika Kambi ya Ilala Dar Es salaam Class anajiandaa na mpambano wake na Said Mundi utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam picha na  www.superdboxingcoach.blogspot.com


bondia Ibrahimu Class 'King Class mawe' akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Mohamed Hemedi 'Kadogo Ninja' wakati wa mazoezi yao yanayoendelea Katika Kambi ya Ilala Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake na Said Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

 

 

LIGI za ULAYA: Kuendelea Wikiendi!

>>NI LA LIGA, SERIE A & BUNDESLIGA!!
BORUSSIA_DORTMUND_JUKWAABaada ya Nyota kadhaa wanaowika huko Barani Ulaya kurudi Makwao kuziwakilisha Nchi zao katika Mechi za Kimataifa za Kirafiki za katikati ya Wiki zilizokuwepo kwenye Kalenda ya FIFA, Wachezaji hao Wikiendi hii wapo kwenye Vilabu vyao kucheza Ligi za Nchi mbalimbali Barani Ulaya.
ZIFUATAZO ni RATIBA na MISIMAMO ya zile Ligi Vigogo za LA LIGA, SERIE A na BUNDESLIGA:
LA LIGA
RATIBA:
Jumamosi Novemba 17
Osasuna v Malaga
Valencia v Espanyol
Barcelona v Real Zaragoza
Real Madrid v Athletic Bilbao
Jumapili Novemba 18
Deportivo La Coruna v Levante
Celta Vigo v Real Mallorca
Getafa v Real Valladoid
Granada v Atletico Madrid
Sevilla v Real Betis
Real Sociedad v Rayo Vallecano
MSIMAMO-Timu za juu tu:
[Kila Timu imecheza Mechi 11]
1 Barcelona Pointi 31
2 Atletico Madrid 28
3 Real Madrid 23
4 Real Betis 19
5 Malaga 18
6 Levante 17
SERIE A
RATIBA:
Jumamosi  Novemba 17
Juventus v Lazio
Napoli v AC Milan
Jumapili Novemba 18
Bologna v Palermo
Inter Milan v Cagliari
Udinese v Parma
Siena v Pescara
Catania v Chievo Verona
Fiorentina v Atalanta
Sampdoria v Genoa
Jumatatu Novemba 19
AS Roma v Torino
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 12]
1 Juventus Pointi 31
2 Inter Milan 27
3 Napoli 26
4 Fiorentina 24
5 Lazio 22
6 Atalanta 18
BUNDESLIGA
RATIBA:
Jumamosi Novemba 17
Borussia Dortmund v SpVgg Gr. Furth
Borussia Monchengladbach v Stuttgart
Hamburger v Mainz
Hannover v Freiburg
Nuremberg v Bayern Munich
Eintracht Frankfurt v Augsburg
Bayer Leverkusen v Schalke
Jumapili Novemba 18
Werder Bremen v Fortuna Dusseldorf
Hoffenheim v Wolfsburg
MSIMAMO-Timu za juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 11]
1 Bayern Munich Pointi 30
2 Schalke 23
3 Eintracht Frankfurt 20
4 Borussia Dortmund 19
5 Bayer Leverkusen 18
6 Hannover 17

 

 Benzema aanza mazoezi kuelekea mchezo wa Athletic Bilbao






Jose Mourinho ameanza kupata matumaini mapya baada ya majeruhi Karim Benzema kuanza mazoezi kuelekea katika mchezo wa Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao.



Mfaransa huyo alipatwa na majeraha katika mchezo dhidi ya Real Zaragoza wiki mbili zilozopita na kupelekea kukosekana katika michezo miwili ya UEFA dhidi ya  Borussia Dortmund na Levante.

Jose Mourinho ameanza kupata matumaini mapya baada ya majeruhi Karim Benzema kuanza mazoezi kuelekea katika mchezo wa Real Madrid dhidi ya Athletic Bilbao.
 

Kama hiyo haitoshi Benzema huenda akarejea dimbani rasmi katika mchezo dhidi ya Bilbao jumamasi endapo atamaliza mazoezi hii leo bila ya matatizo yoyote. 

Kurejea kwake ni faraja katika kikosi cha Mourinho, ambaye kwasasa anaendelea kumkosa mshambuliaji mwingine Gonzalo Higuain ambaye naye ni majeruhi

 

KAMATI YA SERENGETI YAKUSANYA MZIGO WA KUTOSHA KUISHINDISHA TIMU

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Serengeti Boys Ishinde, Kassim Mohamed Dewji akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Serengeti, ndani ya hoteli ya JB Bellmonte, katikati ya Jiji la Dar es Salaam asubuhi ya leo kuhusu maandalizi ya mechi ya Jumapili dhidi ya Kongo Brazzaville, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za U-17 Afrika. Dewji amesema Kamati yake imefanikiwa kukusanya Sh. Milioni 35 kati ya Milioni 60 zinazotakiwa kwa maandalizi ya mchezo huo wa kwanza. Wengine kulia ni Henry Tandau, Katibu wa Kamati na kushoto, Angetile Osiah, Mjumbe wa Kamati.  

Mjumbe wa Kamati, Abdallah Ahmad Bin Kleb 

Kutokas kulia Bin Kleb, Tandau, Dewji, Osiah na Mjumbe mwingine wa Kamati, Salim Abdallah

Salim Abdallah kushoto na Osiah kulia

Makamu Mwenyekiti wa Kamati, KD akizungumza kwa simu na Mwenyekiti wake, Ridhiwani Kikwete ambaye hakuhudhuria mkutano kwa sababu yupo msibani kwao Bagamoyo.  

 

LADY JAYDEE SASA NDANI YA EATV KATIKA DIARY

Mwanamuziki maarufu nchini, Lady Jaydee (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam kuhusu kipindi chake kipya cha Lady Jaydee Diary, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku. Kushoto ni Mkuu wa vipindi EATV, Lydia Igarabuza.  


MWANAMUZIKI mkongwe nchini, Lady Jadee ameanzisha kipindi cha TV kiitwacho Diary Ya Lady Jaydee, kitakachokuwa kikirushwa hewani na kituo cha East African TV, maarufu kama Channel 5 kila Jumapili saa 3:00 usiku.
Kama msanii, Lady Jaydee amefanikiwa na kutambulika katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi, huku akitunukiwa tunzo nyingi zaidi akiwa albamu zake tano. Pamoja na kuwa anaendelea na fani yake ya muziki, Lady Jaydee ameamua kuwafikia na kuwaburudisha wapenzi wa kazi zake kwa njia nyingine.
Lady Jaydee sasa anaanza sura mpya ya burudani kwa kuleta kipindi cha TV kiitwacho DIARY YA LADY JAYDEE, ambacho kutaonekana katika kituo cha TV cha EATV
Diary Ya Lady Jaydee itaonesha maisha na hadithi za kweli za Lady Jaydee kwa lengo la kuburudisha kwa kuonyesha mambo yate mazuri anayopitia au kuyaona Lady Jaydee kuelimisha kwa kushiriki mambo ya kijamii, kutia moyo wengine wafuate ndoto zao kwa uadilifu, kuongeza kipato kama msanii kwa kutangaza biashara mbalimbali na hatimae kudumisha ajira binafsi kwa njia ya sanaa.
Lady Jaydee anatoa shukrani kwa mashabiki kwa kuendelea kumpokea, jambo ambalo linampa nguvu zaidi ya kufanya kaza.
Pia anashukuru sana vyombo vya habari na zaidi anawashukuru EATV na washirika wake kwa kumpa nafasi ya kurusha kipndi chake kipya Diary Ya Lady Jaydee. EATV imekuwa mchango wa aina yake katika kuwakuza wasanii Tanzania.
Lady Jaydee anatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kushirikiana na naye kwa kila namna, ili kukuza na kuendeleza kipaji chake na sanaa ya muziki wa Tanzania kwa ujumla wake.
Zaidi anatoa wito kwa makampuni kishiriki na kuungana nae ili waweze kumpa nguvu msanii, kutangaza biashara zao na kushawishi ajira katika fani ya muziki.
Na mwisho Lady Jaydee anawaribisha wote kusikiliza CDs zake au kuburidika na kundi lake la Machozi Band au kupata chakula ktk mgahawa wake wa kisasa Nyumbani Lounge au ukiwa umepumzika nyumbani utazame kipindi chake Diary Ya Lady Jaydee ktk EATV.



  YONDAN: HAIKUWA KAZI NYEPESI KUMDHIBITI OLIECH

Kevin Yondan

BEKI wa Yanga, Kevin Yondan amesema kwamba licha ua kuwafunga Kenya, Harambee Stars, lakini wapinzani wao hao ni wazuri na zaidi akamsifia mshambuliaji wa klabu ya Daraja la Pili Ufaransa, AJ Auxerre, Dennies Oliech kwamba ni mtu hatari.
Akizungumza  kwa simu kutoka Mwanza jana, Yondan alisema kwamba walifanya kazi kubwa mno kumdhibiti Oliech, kwani mtu huyo ni hatari.
“Yule jamaa anajua, mimi binafsi ilinibidi nitulize sana akili katika kukabiliana naye, ndiyo maana hakufunga, bila hivyo Yule mtu angefunga,”alisema Yondan.
Hata hivyo, beki huyo wa kati alisema timu yao ilicheza vizuri kwa ujumla jana na anaamini hizi ni dalili nzuri za kuwapa Watanzania.
“Tunamshukuru Mungu kwa ushindi huu, lakini tunaendelea kuomba mashabiki wetu waendelee kutupa sapoti ili tufanye vizuri zaidi,”alisema.
Taifa Stars, jana iliibwaga Kenya, Harambee Stars bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza katika mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Hadi mapumziko, Stars ilikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na beki Aggrey Morris katika dakika ya nne, baada ya kupanda kusaidia mashambulizi.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa anayetambuliwa na FIFA, Oden Mbaga, Kenya walitawala dakika 10 za mwanzo, lakini baada ya hapo Stars wakafunguka nao na kuanza kula nao sahani moja na Harambee Stars.
Kipindi cha pili, Kenya walianza na mabadiliko kocha Henri Michel akiwapumzisha James Situma, Jerry Santo na Wesley Kemboi na kuwaingiza Christopher Wekesa, Anthony Akumu na Timbe Ayoub.
Pamoja na mabadiliko hayo, mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Harambee Stars, kwani wenyeji waliendelea kucheza kwa makini, wakishambulia na kujilinda zaidi.
Kocha wa Stars naye, Mdemnark, Kim Poulsen aliwatoa Amir Maftah, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Mbwana Samatta, Mrisho Ngassa na Thomas Ulimwengu na kuwaingiza Nassor Masoud ‘Chollo’, Amri Kiemba, Simon Msuva, John Bocco ‘Adebayor’, Shaaban Nditi  na Issa Rashid.  
Baada ya mchezo huo, kocha wa Harambee, Mfaransa Michel alionyesha kukerwa na matokeo hayo na kusema timu yake haikucheza vizuri, wakati Polusen, amefurahia ushindi huo akisema timu yake haijacheza kwa miezi miwili na baada ya siku mbili za mazoezi wameifunga Kenya. 
Taifa Stars; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah/Nassor Masoud ‘Chollo’ dk70, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar/Amri Kiemba dk69, Mwinyi Kazimoto/Simon Msuva dk69, Mbwana Samatta/John Bocco dk 84, Mrisho Ngassa/Shaaban Nditi dk72 na Thomas Ulimwengu/Issa Rashid dk 89.  
Harambee Stars; Frederick Onyango, Brian Mandela, Eugene Asike, James Situma/Christopher Wekesa dk 46, Edwin Wafula, Jerry Santo/Anthony Akumu dk 46, Peter Opiyo/Charles Okwemba dk 67, Patrick Obuya, Patrick Osaika/Mulienge Ndeto dk 73, Dennis Oliech na Wesley Kemboi/Timbe Ayoub dk 46.
REKODI YA STARS MWAKA HUU NA RATIBA YA MECHI ZIJAZO:
Februari 23, 2012
Tanzania 0 – 0 DRC (Kirafiki)
Februari 29, 2012
Tanzania 1 – 1 Msumbiji   (Kufuzu Mataifa ya Afrika)
Mei 26, 2012
Tanzania 0 – 0 Malawi
Juni 2, 2012
Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 10, 2012
Tanzania 2 – 1 Gambia      (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 17, 2012
Msumbiji 1 – 1 Tanzania   (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)
Agosti 15, 2012
Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)
Novemba 14, 2012
Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)
Machi 22, 2013
Tanzania Vs Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 7, 2013
Morocco Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)
Juni 14, 2013    
Tanzania Vs Ivory Coast    (Kufuzu Kombe la Dunia)
Septemba 6, 2013
Gambia    Vs Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)

 

HATIMA YA MILOVAN SIMBA LEO, KIKAO KIZITO MNO CHAFANYIKA

Kocha wa Simba SC, Milovan Cirkovick kushoto akiwa ameishiwa nguvu baada ya kufungwa na Toto Africans mwishoni mwa wiki katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kulia ni wachezaji wake, Shomary Kapombe na Jonas Mkude.

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba ya Dar es Salaam inatarajiwa kuwa na kikao kizito leo, kujadili mambo mbalimbali kuhusu mustakabali wa klabu hiyo na mwenendo wa timu yao ya soka kwa ujumla.
Habari kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba kikao hicho kitashirikisha Wajumbe wote wa Kamati hiyo, chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage.
Miongoni mwa ajenda zinazotarajiwa kuwa mjadala nzito ni matokeo ya timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, licha ya kuanza vyema na kufikia kuongoza kwa wastani wa pointi saba zaidi.
Aidha, katika kikao hicho, habari zinasema Makamu Mwenyekiti, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ atawasilisha rasmi barua ya kujiuzulu kwake uongozi, kufuatia kuibuka watu wanaompinga na kushinikiza ajiuzulu.
Lakini pia bado mjadala mpana utakuwa kuhusu mustakabali wa timu kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Litajadiliwa suala la kipa Juma Kaseja kuomba kung’atuka baada ya kufanyiwa fujo na mashabiki.
Litajadiliwa suala la kusimamishwa kwa beki Juma Said Nyosso na kiungo Haruna Moshi ‘Boban’. Litajadiliwa suala la kuboreshwa kwa timu kuelekea mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa mwakani.
Lakini pia habari zinasema litajadiliwa pendekezo la kutaka kocha wa timu hiyo, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick aondolewe na masuala mengine ya msingi, kama salio la malipo ya kiwanja, ambacho klabu hiyo inataka kujenga uwanja wake wa michezo. 
Kwa ujumla, hamkani si shwari ndani ya Simba hivi sasa, baada ya mabingwa hao wa Ligi Kuu kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu wakiwa katika nafasi ya tatu, tena wakizidiwa pointi sita na wapinzani wao wa jadi, Yanga wanaoongoza ligi hiyo.

 

CHEKA KUPANDA ULINGONI ARUSHA KUMVAA MWAHILA

Bondia maarufu kuliko wote Tanzania Francis Cheka atamvaa Udiadia Mwahia kutoka nchini DRC Kongo kugombea mkanda wa ubingwa wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi.
Mabondia hao watakutana katika mpambano wa kwanza tangu Arusha liwe jiji katika uwanja wa Shekh Amri Abeid tarehe 26 Desemba 2012 siku ya Boxing Day!

Akimtambulisha Francis Cheka kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar Es Salaam jana , mratibu wa mpambano huo na ambaye alishawahi kuwa bingwa wa Tanzania kwenye ngumi za ridhaa George Andrew alisema kuwa bondia Udiadia Mwahila anakaa Lusaka Zambia ambako ndipo anapofanya shughuli zake za ngumi chini ya promota maarufu Anthony Mwamba!
 Udiadia ana rekodi ya mapambano 12 na ametoka sare pambano moja na hajapoteza hata moja wakati Francis Cheka ana rekodi ya mapambano 33 amepoteza 6 na kutoka sare pambano moja.
George alisema kuwa mpambano huo utatumika kulitangaza jiji la Arusha kama Las Vegas ya ngumi katika bara la Afrika na kulifananisha jiji la Arusha na jiji la Geneva lililoko nchini Switzerland.

Mpambano huo unakuja wakati ambapo mpambano mwingine wa Francis Cheka na bondia kutoka Ujerumani wa kugombea mkanda wa IBF wa mabara ulifutwa baada ya Simon kuumia katika mazoezi.
Naye Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi alisema kuwa wao kama IBF wamesharuhusu maandalizi ya mpambano huo. Rais huyo aliwataka wadhamini pamoja na wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa mingine kujitokeza kwa wingi ili kulifanya pambano hilo kuwa la mafanikio.
 Naye bondia Francis Cheka alisema kuwa amejiandaa kwa kiasi kikubwa na atazidi kufanya mazoezi ili kupata ushindi kwake pamoja na nchi ya Tanzania. Aliendelea kusema kuwa kila Mtanzania anajua uwezo wake kwa hiyo amewataka wote wafike kwa wingi ili kupata uhondo na burudani tosha

 

MWAKALEBELA KUANZA HARAKATI ZA KUMNG'OA BAYI TOC LEO HII

Habari za uhakika kutoka kwa aliyekuwa katibu mkuu wa TFF katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Leadgar Tenga, Bwana Frederick Mwakalebela ni kwamba kesho asubuhi ataenda kuchukua fomu za kugombea uongozi wa ukatibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania.

Mwakalebela ambaye ni mmoja ya wadau wenye kuonyesha nia ya dhati katika kukuza michezo kwa kutoa misaada mbalimbali pamoja na kuandaa michuano kama 'Mwakalebela CUP' ambayo imekuwa ikitoa vipaji vingi amesema ameamua kuchukua fomu ya kugombea ukatibu mkuu kwa sababu anaamini ana uwezo na nia ya dhati ya kuongoza kamati hiyo ili kuiwezesha nchi yetu ipige hatua zaidi katika michezo.

Kuchukua fomu kwa Mwakalebela kunamaanisha katibu mkuu huyo wa zamani wa TFF, ameanza mbio za kumng'oa madarakani kidemokrasia Fibert Bayi ambaye amekuwa kiongozi wa kamati hiyo kwa muda mrefu sasa.

Leo ndio siku ya mwisho ya kuchukua fomu.

MATAIFA HURU YA AFRIKA: MAREFA KUFICHWA KUEPUSHA UPANGAJI WA MATOKEO

Marefa  wa fainali zijazo za kombe la mataifa huru ya Afrika watawekwa mbali na watu wengine wakati wa michuano hiyo nchini South Africa ili kuzuia upangaji wa matokeo.

Hali ya ulinzi ilitumika pia katika fainali ya za kombe la dunia mwakak 2010 zilizofanyika nchini SA.

CEO wa kamati ya ndani ya uandaaji Mvuso Mbebe alisema: "Marefa watakuwa mafichoni katika hotel mojawapo ambayo hakuna mtu atakuwa na uwezo wa kuwafikia.

"Hawatokuwa na uwezo wa kuwasiliana na mtu yoyote kutoka nje, kwa sababu hatuwezi kujua nini kinaweza kufanyika katika mawasiliano yao na watu wasioruhusiwa.

Aliongeza: "Watakuwa wanaondoka hotelini, chini ya ulinzi mkali utakaokuwa ukisindikizwa na vikosi maalum vya ulinzi, hali itaendelea mpaka mwisho wa michuano."

Shrikisho la soka la Afrika limepitisha hatua hiyo ya ulinzi wa marefa ambao utaanza kuanzia January 19 mpaka February 10

 

MECHI za KIMATAIFA: Sweden, Ibrahimovitch, waichapa England 4-2! 

>>FRANCE yaifunga ITALY, MESSI ashindwa kutamba JANGWANI, GERMANY, HOLLAND sawa!!

>>BRAZIL 2014: Japan yashinda ugenini, yachungulia safari ya Brazil!!
FIFA_LOGO_BESTWakicheza kwenye Uwanja mpya wa Friends Arena Nchini Sweden, Wenyeji Sweden waliitwanga England Bao 4-2 huku bao zote za Sweden zikifungwa na Straika hatari Zlatan Ibrahimovic.
Bao za England zilifungwa na Danny Welbeck na Caulker.
France, wakicheza ugenini, waliifunga Italy Bao 2-1 kwa bao za Valbuena na Gomis na Bao la Italy kufungwa na Stephan El Shaarawy.
Vigogo Germany na Netherlands walitoka sare ya 0-0.
Huko Jangwani Nchini Saudi Arabia, Nyota Lionel Messi jana alishindwa kuivunja rekodi nyingine ya kuifungia Nchi yake Argentina Bao nyingi ndani ya Mwaka mmoja walipotoka 0-0 na Saudi Arabia.
Nayo Brazil ilitoka 1-1 na Colombia huku Neymar akiifungia Brazil na Cuadrado akiipatia Bao Colombia.
Mabingwa wa Dunia Spain waliicharaza Panama Bao 5-1.
Katika Mechi za Mchujo za kuwania kwenda Brazil 2014 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Japan ilipata ushindi wa ugenini wa Bao 2-1 dhidi ya Oman na matokeo hayo yamewafanya wawe karibu kabisa kufuzu wakiwa na Pointi 13 katika Kundi B huku Timu ya Pili, Australia, ikiwa na Pointi 5 tu.
MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI:
MATOKEO:
Jumatano Novemba 14
Kuwait 1 Bahrain 1
Rwanda  2 Namibia 2
Niger  1 Senegal 1
Angola v Congo
Lesotho v Mozambique
Tanzania 1 Kenya 0
Congo, DR 0 Burkina Faso 1
South Korea 1 Australia 2
Cape Verde 0 Ghana 1
China 1 New Zealand 1
Malaysia 1 Hong Kong 1
Georgia  0 Egypt 0
Russia  2 United States 2
United Arab Emirates 2 Estonia 1
Bulgaria 0 Ukraine 1
Czech Republic 3 Slovakia 0
Andorra  0 Iceland 2
Macedonia 3  Slovenia 2
Algeria  0 Bosnia And Herzegovina 1
Cyprus 0 Finland 3
Israel 1 Belarus 2
Armenia 4 Lithuania 2
Saudi Arabia 0 Argentina 0
Tunisia 1 Switzerland 2
South Africa 0 Zambia 1
Liechtenstein 0 Malta 1
Morocco 0 Togo 1
Romania 2 Belgium 1
Chile 1 Serbia 3
Turkey 1 Denmark 1
Luxembourg 1 Scotland 2
Austria 0 Ivory Coast 3
Hungary 0 Norway 2
Gabon 2 Portugal 2
Sweden 4 England 2
Netherlands 0 Germany 0
Poland  1 Uruguay 3
Ireland 0 Greece 1
Albania 0 Cameroon 0
Italy  1 France 2
Alhamisi Novemba 15
Panama 1 Spain 5
Honduras 0 Peru 0
Paraguay 3 Guatemala 1
Brazil 1 Colombia 1
Venezuela 1 Nigeria 3
Bolivia  1 Costa Rica 1
KOMBE LA DUNIA Brazil 2014: Bara la Asia=MCHUJO
Jumatano Novemba 14
Oman 1 Japan 2
Iraq 1 Jordan 0
Qatar 1 Lebanon 0
Iran 0 Uzbekistan 1
Msimamo:
Kundi A:
1 Uzbekistan Mechi 5 Pointi 8
2 South Korea Mechi 4 Pointi 7
3 Iran Mechi 5 Pointi 7
4 Qatar Mechi 5 Pointi 7
5 Lebanon Mechi 5 Pointi 4
Kundi B:
1 Japan Mechi 5 Pointi 13
2 Australia Mechi 4 Pointi 5
5 Iraq Mechi 5 Pointi 5
3 Oman Mechi 5 Pointi 5
4 Jordan Mechi 5 Pointi 4
 

MAN UNITED: Deni lao lapungua!!

Deni ambalo linaikabili Manchester United limeshuka kwa Asilimia 18 baada ya Klabu hiyo kuuza Hisa kwenye Soko la Hisa la New York na kuongeza Mapato kupitia Udhamini mpya na kulifanya Deni hilo liporomoke toka Pauni Milioni 436.9 hapo Juni 30 na kufikia Pauni Milioni 359.7 mnamo Septemba 30.
MAN_UNITED_WALLKwa mujibu wa Takwimu za Mahesabu zilizotolewa leo zinaonyesha Man United ilipata Faida ya Pauni Milioni 20.5 kwa Kipindi cha Miezi mitatu iliyoishia Septemba 30.
Mapato ya Kibiashara kwa Klabu yako kwenye malengo na yanategemewa kufikia si chini ya Pauni Milioni 350 Milioni kwa Mwaka huu wa Fedha baada ya kukua kwa Asilimia 24.
Katika Miezi hiyo mitatu, Wadhamini 10 waliingia Mkataba na Klabu ikiwa ni pamoja na Kampuni kubwa ya Magari huko Marekani General Motors ambayo Nembo ya Gari lake la aina ya Chevrolet itaanza kuoneka kwenye Jezi za Man United kuanzia Msimu wa Mwaka 2014/15.
Licha ya kutotwaa Taji lolote Msimu uliopita, Man United Msimu huu ndio inaongoza Ligi Kuu England na tayari imesonga mbele kwenye Raundi nyingine ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huku ikiwa na Mechi mbili mkononi na pengine hii ni kwa sababu ya kuimarisha Kikosi kwa kuwanunua Wachezaji wapya.
Man United imewanunua Shinji Kagawa, Nick Powell na Robin van Persie.
Man United inamilikiwa na Familia ya Kimarekani ya kina Glazer ambao walinunua Mwaka 2005 kwa kutumia Mikopo toka Benki mbalimbali na kuiingiza Klabu hii ambayo ilianzishwa Mwaka 1878 kwenye Deni kubwa ingawa ina Mapato makubwa Kibiashara.
HUKO NYUMA==
TULIANDIKA: Jumanne, 16 Novemba 2010 20:25
Wadau wa Manchester United, hasa Kikundi cha Mashabiki kiitwacho MUST [Manchester United Supporters Turst] kimekuwa kikiwapinga Familia ya Glazer kwa kuitumbukiza Man United kwenye deni na wasiwasi huo ulisababisha kuibuka kwa upinzani uliotaka kuwabwaga Familia hiyo ya Kimarekani na Mashabiki wakivaa Jezi za Kijani na Dhahabu wakati wa mechi za Man United.GREEN_n_GOLD_OF_MAN_UNITED
Rangi za kijani na dhahabu ni rangi za Klabu ya Newton Heath iliyoanzishwa mwaka 1878 na hapo tarehe 26 Aprili 1902 kubadilishwa jina kuitwa Manchester United na rangi kuwa nyekundu, nyeusi na nyeupe zinazotumiwa mapaka sasa.
Newton Heath ilianzishwa na Wafanyakazi wa Depo iliyokuwepo eneo lla Newton Heath la Reli ya Lancashire na Yorkshire..
Mwaka 2005 Familia ya Matajiri kutoka Florida Marekani iitwayo Glazer iliinunua Manchester United na kuiingiza kwenye deni kubwa ambalo, ingawa Menejimenti ya Klabu inadai hilo deni ni kitu cha kawaida na uwezo wa kulilipa upo, Washabiki hawapendeziwi nalo na wameanzisha upinzani mkubwa kwa Familia ya Glazer.
Ndio maana Mashabiki, kwenye mechi za Manchester United, wanavaa skafu, fulana na kofia rangi za kijani na dhahabu ikiwa ni alama ya chimbuko la Manchester United, Klabu ya Newton Heath iliyoanzishwa na Wafanyakazi makabwela wa Depo ya Reli.
Nje ya Uwanja wa Old Trafford fulana za rangi hiyo ya kijani na dhahabu huuzwa huku nyuma zina maandishi [Shairi la Kiingereza] na tafsiri ya haraka ni:
“Roho ya United haiuzwi, Ndio maana kwa fahari tunavaa Kijani na Dhahabu,
Hatutavaa ile Jezi Nyekundu inayosifika, Mpaka Glazer waondoke au wafe,
Hivyo inua viwango vya zamani juu, Kwa Kijani na Dhahabu tutaishi na kufa,
Na hakika siku itafika tena, Tutakapovaa Nyekundu yetu kwa mara nyingine tena!”

GOLI BORA DUNIANI 2012: FIFA yatangaza Wagombea 10!

>>MESSI, NEYMAR wamo, RONALDO hana Bao!!
>>KUPIGIWA KURA, Mshindi kujulikana Januari 7, 2013!!
NEYMAR_v_MESSIZile mbio za kumpata Mshindi wa Tuzo ya FIFA ya PUSKAS kwa ajili ya GOLI BORA la MWAKA zimeanza leo kwa kutangazwa Wagombea 10 na Mabao yao bila ya Jina la Mshindi wake wa kwanza kabisa wa Tuzo hiyo, Cristiano Ronaldo, kuwemo.
Mashabiki Dunia nzima ndio watapiga Kura kuamua lipi Goli Bora kati ya Mabao 10 yaliyoteuliwa na Wataalam wa FIFA.
Mchujo wa kupata Magoli matatu Bora utakamilika hapo Novemba 29 na itaanza Kura nyingine kuchagua Goli Bora kati ya hayo matatu ambapo Mshindi atatangazwa Januari 7, 2013, Siku ambayo pia Dunia itamjua nani atatwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, FIFA Ballon d’Or.
Tuzo ya FIFA ya PUSKAS kwa ajili ya GOLI BORA la MWAKA ilianzishwa Mwaka 2009 na Mshindi wake wa kwanza ni Cristiano Ronaldo alipofunga Bao katika Mechi ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Manchester United dhidi ya FC Porto.
+++++++++++++++++++++++++++++
WASHINDI WALIOPITA:
-2011==Neymar: Goli Santos v Flamengo
-2010==Giovanni van Bronckhorst: Goli Netherlands v Uruguay
-2009==Cristiano Ronaldo: Goli Man United v FC Porto
+++++++++++++++++++++++++++++
Tuzo hii ya Puskas ni kwa heshima na kumbukumbu ya Ferenc Puskás, Nahodha na Nyota wa Hungary katika Miaka ya 1950.
WAGOMBEA GOLI BORA:
Agyemang BADU (Ghana - Guinea 1 February 2012)
Hatem BEN ARFA (Newcastle United - Blackburn Rovers 7 January 2012)
Radamel FALCAO (América de Cali - Atletico Madrid 19 May 2012)
Eric HASSLI (Vancouver Whitecaps - Toronto FC 16 May 2012)
Olivia JIMENEZ (Mexico - Switzerland 22 August 12)
Gastón MEALLA (Nacional Potosí - The Strongest 29 January 2012)
Lionel MESSI (Brazil - Argentina 9 June 2012)
NEYMAR (Santos - Internacional 7 March 2012)
Moussa SOW (Fenerbahce - Galatasaray 17 March 2012)
Miroslav STOCH (Fenerbahçe - Gençlerbirliği 3 March 2012

BPL: Kilingeni Jumamosi, kuanza DABI ya London Arsenal v Spurs!!

WALCOTT_WILSHERE_OX
>>DABI hii ni MSHIKEMSHIKE kwa WENGER na VILLAS-BOAS!!!
Baada ya Mechi za Kimataifa za Kirafiki za katikati ya Wiki, Wikiendi hii Ligi Kuu England, BPL, inarudi kwa kishindo na Mechi ya kwanza kabisa Siku ya Jumamosi ni Dabi ya Jiji la London kati ya Arsenal na Tottenham itakayochezwa Uwanja wa Emirates na Mechi ya mwisho Siku hiyo hiyo ni kati ya Norwich City na vinara wa Ligi Manchester United itakayochezwa Uwanja wa Carrow Road.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
+++++++++++++++++++++++
Arsenal na Tottenham zitaingia kwenye Dabi hiyo huku zikiwa nafasi ya 7 kwa Tottenham na ya 8 kwa Arsenal na kila mmoja atawania ushindi ili kujiiimarisha zaidi hasa baada ya kuwa na mwendo mbovu kwenye Ligi Msimu huu.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
Ikiwa Timu moja itafungwa basi presha kwa Mameneja, Arsene Wenger wa Arsenal na Andre Villas-Boas, itazidi na Wadau wengi watainua Mabango kukandamiza kuwa Klabu ipo mashakani.
Ndio maana Mechi hii ni muhimu mno kwa kila Klabu hasa ukizingatia mwendo wao mbovu wa hivi karibuni ambapo Arsenal wameshinda mara moja tu katika Mechi 8, tena dhidi ya Klabu ya mkian QPR, na wamefungwa jumla ya bao 12 katika Mechi zao 4 zilizopita na wenzao Tottenham wakifungwa katika Mechi 3 kati ya 4 walizocheza mwisho.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City

No comments:

Post a Comment