Sunday, October 14, 2012

Wayne Rooney ataka Ukepteni wake England uwe wa kudumu

Jumapili, 14 Oktoba 2012 18:29
Chapisha 
WAYNE_ROONEY-KEPTENIStraika wa England Wayne Rooney amesema angependelea itokee Siku awe Kepteni wa kudumu wa Timu ya Taifa ya England baada ya kuiongoza vyema kama Kepteni wa Timu hiyo hapo juzi ilipoitwanga San Marino bao 5-0 huku yeye akipiga bao mbili.
Rooney, Miaka 26, alishika wadhifa huo wa Ukepteni kwa muda kwenye Mechi hiyo baada ya Nahodha wa England, Steven Gerrard, kutokuwepo kufuatia kutumikia Kifungo cha Mechi moja.
Rooney ametamka: “Ukiwa mdogo unaota kuichezea England na ukiichezea kinachofuata ni kutaka kuwa Nahodha!”
Rooney alianza kuichezea England akiwa na Miaka 17 hapo Mwaka 2003 na juzi Ijumaa amefikisha Mechi 77 za kuichezea England.
Bao zake mbili za hiyo Ijumaa zimemfanya afikishe bao 31 akiwa ni wa 5 kwa ufungaji bao nyingi kwa England na sasa amewapiku Nat Lofthouse, Sir Tom Finney na Alan Shearer.
Meneja wa England, Roy Hodgson, amekiri kuwa Rooney anastahili kuwa Kepteni na ipo Siku hilo litatimia.
MATOKEO:
ULAYA-Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014
Ijumaa Oktoba 12
Russia 1 Portugal 0
Finland 1 Georgia 1
Armenia 1 Italy 3
Faroe Islands 1 Sweden 2
Kazakhstan 0 Austria 0
Albania 1 Iceland 2
Czech Republic 3 Malta 1
Liechtenstein 0 Lithuania 2
Turkey 0 Romania 1
Belarus 0 Spain 4
Bulgaria 1 Denmark 1
Moldova 0 Ukraine 0
Slovakia 2 Latvia 1
Estonia 0 Hungary 1
Netherlands 3 Andorra 0
Serbia 0 Belgium 3
Greece 0 Bosnia-Hercegovina 0
Rep of Ireland 1 Germany 6
Wales 2 Scotland 1
England 5 San Marino 0
Luxembourg 0 Israel 6
Macedonia 1 Croatia 2
Switzerland 1 Norway 1
Slovenia 2 Cyprus 1
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Oktoba 16
Albania v Slovenia
Andorra v Estonia
Belarus v Georgia
Belgium v Scotland
Bosnia-Hercegovina v Lithuania
Czech Republic v Bulgaria
Hungary v Turkey
Iceland v Switzerland
Israel v Luxembourg
Latvia v Liechtenstein
Macedonia v Serbia
Portugal v Northern Ireland
Romania v Netherlands
Russia v Azerbaijan
San Marino v Moldova
Slovakia v Greece
Spain v France
Ukraine v Montenegro
2000 Cyprus v Norway
2100 Faroe Islands v Rep of Ireland
2130 Austria v Kazakhstan
2130 Croatia v Wales
2145 Germany v Sweden
2145 Italy v Denmark
2200 Poland v England
FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9
-Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.


MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI WA MKOA WA TABORA BWIRE MKAMA AZUNGUMZIA KUHUSU MCHAKATO WA UCHAGUZI WA MKOA WA TABORA TAREFA

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa mkoa wa tabora bwana bwire mkama amezungumzia kuhusu mchakato wa uchaguzi unavyoendelea kwa sasa hapa mkoani tabora na kuelekea katika uchaguzi ambao unatarajia kufanyika November,4 mwaka huu hapa mkoani tabora.

Ameyazungumza haya pale nilipokuwa nafanya naye interview katika ofsi yake ya TUWASA hapa mkoani tabora tupate kumsikiliza kiundani zaidi nini amekizungumza????ingia katika you tube ya tano juma utapata kusikia nini amekizungumza leo

MABAO YA DROGBA YALIVYOCHAFUA AMANI SENEGAL, DAKAR YANUKA MOSHI

MIAKA 13 TANGU KIFO CHA MWALIMU NYERERE MWENYE KADI NAMBA MOJA YANGA, WATANZANIA TUTAMKUMBUKA SANA

Katikati ni Mwalimu Nyerere akiwa na Katibu wa DABA wa enzi hizo, Jakcosn Kalikumtima kulia na aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje, Jakaya Kikwete kushoto, sasa rais wa Jamhiri ya Muungano Tanzania Aprili mwaka 1998 Uwanja wa Ndani wa Taifa 


KADI namba moja ya uanachama wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, inadaiwa alipewa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye leo anatimiza miaka 13 tangu kifo chake, Oktoba 14, mwaka 1999.
 
Wakati Mwalimu Nyerere anafariki dunia, mimi nilikuwa mwandishi mchanga sana- wakati huo nipo kampuni ya Habari Corporation Limited, chini ya wamiliki wake wa awali akina Jenerali Ulimwengu.
 
Aliyekuwa bosi wangu wakati huo, Kenny Manara, aliyekuwa Mhariri wa gazeti DIMBA alinipa kazi ya kwenda Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru ulipowekwa mwili wa marehemu kwa ajili ya kuagwa ili kuandika habari juu ya wanamichezo waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu na kuchukua maoni yao.
 
Hakika nilijifunza mengi sana kupitia msiba huo kwa kusikia, kuambiwa na kujionea. Miongoni mwa niliyoambiwa ni kwamba, Mwalimu Nyerere ndiye alikuwa ana kadi namba moja ya Yanga SC na kadi namba mbili, alikuwa nayo hayati Abeid Amaan Karume, rais wa zamani wa Zanzibar.
 
Sijabahatika kuiona ‘leja’ ya Yanga hadi leo tangu nisikie habari hizo, kwa hivyo siwezi kusadiki, lakini kulingana na historia ya klabu ya Yanga katika harakati za ukombozi wa taifa letu, siwezi kupinga hilo.
 
Nashukuru Mungu nikiwa Mwandishi wa Habari, nimewahi kufanya kazi za kuandika habari katika tukio ambalo Mwalimu Nyerere alikuwepo.
Ilikuwa ni Aprili mwaka 1998 katika mechi ya mpira wa kikapu, iliyoandaliwa maalum kusherehekea kuzaliwa kwake, Mwalimu Nyerere Uwanja wa Ndani wa Taifa, kati ya Pazi na Don Bosco.
 
Nakumbuka siku hiyo, mtangazaji wa East Africa TV, Patrick Nyembele alikuwa bado anacheza mpira wa kikapu na ndiye alikuwa Nahodha wa Pazi ambayo ilishinda na kukabidhiwa na Kombe.
 
Mechi hiyo iliandaliwa na Chama cha Mpira wa Kikapu Dar es Salaam (DABA), likiwa wazo la aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa DABA, Fakhrudin Amijee.
Vyama vyote vya michezo vilialikwa kushiriki sherehe hiyo na vilitoa zawadi mbalimbali kwa Mwalimu.
 
Bendi ya Varda Arts ilikuwepo kutumbuiza na ilimpigia wimbo mzuri Mwalimu wa Happy Birth Day. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa Kimataifa wakati huo, alikuwepo na ndiye aliyekuwa amekaa meza kuu pamoja na Nyerere.
 
Nilifarijika sana siku hiyo kufanya kazi mbele ya baba wa taifa na kwa kuwa pia nimefanya kazi mara kibao mbele ya marais waliomfuatia, Alhaj Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete, najivunia sana hayo.
Nilimpenda Mwalimu Nyerere tangu nasoma shule ya msingi pale Mgulani, Dar es Salaam na ninavutiwa sana na sera na misimamo yake enzi za uhai wake.
 
Sijui, nasema sijui kama bila ya Nyerere Tanzania ingekuwepo na hata hiyo Tanganyika ingekuwaje. Sijui! Leo tunaishuhudia Tanzania ambayo mambo mengi yaliyoonekana ya ajabu wakati wa Nyerere yamekuwa ya kawaida.
 
Rushwa, ukatili, unafiki, ulafi wa madaraka, ubifansi, ukabila, udini, ufisadi na uzandiki haya si ya ajabu tena katika Tanzania ya leo. Tena watu hawana aibu wala woga, wamekuwa jasiri wa uovu na hawamuogopi hata Mungu.
 
Tuna kila sababu ya kumlilia Mwalimue Nyerere na kumkumbuka sana leo akitimiza miaka 13, tangu kifo chake.  
   
HUYU NDIYE NYERERE
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania. Alizaliwa Butiama, mkoani Mara pembezoni mwa Ziwa Nyanza Aprili, 13, mwaka 1922. Alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999. Aliiongoza Tanzania tangu mwaka 1961 hadi mwaka 1985.
 
Yeye ni mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hii ndiyo ilimpatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la ‘Mwalimu’.
 
Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada ya kutawala kwa muda mrefu.
Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
 
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika).
 
Alikuwa miongoni mwa watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya baba yake na alipofikisha umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma.
 
Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya Wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.
 
Mapadri wakaona akili yake wakamsaidia kusomea Ualimu katika Chuo Kikuu cha Uganda, Makerere kilichopo Kampala, kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.
 
Akiwa Makerere, Mwalimu akaanzisha tawi la Umoja wa Wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary´s. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko, Scotland ambako alisoma M.A. ya historia na uchumi, akiweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na Mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.
 
Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam.
 
Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.
 
Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA.
Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.
 
Uwezo wa Mwalimu Nyerere uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.
 
Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru.
 
Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship council na Fourth committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana Richard Turnbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.
 
Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na Desemba 9, 1961 na Nyerere alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika.
 
Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.
 
Februari 5, mwaka 1977 aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa Mwenyekiti wake.
 
Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi rais wa pili Ali Hassan Mwinyi. Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na hadhi kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.
 
Inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamini W.Mkapa kama mgombea wa rais wa mwaka 1995 na ambaye aliteuliwa kuwa rais kwenye uchaguzi wa mwaka 1995.
 
Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

SIASA ZA UJAMAA NA KUJITEMEA
Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa na kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais baada ya uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani Ali Hassan Mwinyi aliyetawala kwa siasa za uchumi wa soko huria.
 
Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere alitamka katika tafrija ya kumuaga juu ya siasa yake kiuchumi “Nimefeli. Tukubali hivyo.”
 
Wapo ambao wanamlaumu Mwalimu Nyerere kwa siasa zake za ujamaa kwa madai zilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania.
 
Mwalimu bado anakumbukwa na Watanzania hasa wa hali ya chini kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu na pia ataendelea kukumbukwa na Waafrika kote barani hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika.
 
Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.
 
Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama, ingawa wakati mwingine alikuwa akija kwenye nyumba yake ya Msasani, Dar es Salaam.
 
Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) na kufariki dunia nchini Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London Oktoba 14, 1999. Alizikwa mahali pale alipozaliwa, kijiji cha Butiama.
 
Ni miaka 13 leo tangu, mwenye kadi namba moja ya Yanga afariki dunia, Watanzania bado tunamkumbuka na kumlilia.

MASHALI ULINGONI NA MGANDA LEO MANZESE

Kulia ni Thomas Mashali wa Tanzamia na kushoto ni Sebyala Meddy wa Uganda wakiwa na rais wa ECAPBA, Onesmo Ngowi wakati wa kupima uzito jana kwa ajili ya pambano la leo kwenye ukumbi wa Friends Corner, Manzese, Dar es Salaam.

Kushoto ni Thomas Mashali wa Tanzamia na kulia ni Sebyala Med wa Uganda wakiwa na rais wa ECAPBA Onesmo Ngowi wakati wa kupima uzito jana

MAGDALENA NDIYE TOP MODEL MISS TANZANIA 2012

Top 5

Mshindi wa Top Model Miss Tanzania 2012,Magdalena Roy

Mshindi wa Top Model Miss Tanzania 2012, Magdalena Roy (katikati anaepungia mkono) akiwa na washiriki wenzake alioingia nao hatua ya tano bora katika shindano lililomalizika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa hoteli ya Naura Springs,Jijini Arusha.

MISS Dar City Center ambaye pia alishika nafasi ya pili katika shindano la Miss ilala, Magdalena Roy amefanikiwa kuingia 15 Bora ya Miss Tanzania baada ya juzi usiku kufanikiwa kutwaa taji la Top Model.
 
Magdalena anakuwa mshindi wa pili kuingia katika hatua hiyo, akiungana na Miss Mbulu, Lucye Stephano ambaye wiki iliyopita alitwaa taji la Miss Photogenic.
Katika shindano la Top Model lililofanyika kwenye hoteli ya Naura Spring, mjini hapa lilikuwa na upinzani mkali kutoka kwa washiriki wote wa Miss Tanzania.
 
Mbali na Magdalena warembo wengine waliofanikiwa kuingia katika tano bora walikuwa ni Mary Chizi (Ilala), Irene Veda (Lindi), Belinda Mbogo (Dodoma) na Sina Revocatus (Elimu ya Juu).
 
Warembo hao jana waliondoka kuelekea Tanga kwa ajili ya kutembelea mapango ya Amboni, kabla ya kurejea Dar es Salaam.
 
Warembo wapatao 30 wanawania taji la Miss Tanzania, ambalo kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

MILOVAN AKIKASIRIKA HASIKILIZI LA MTU, MTAZAME HANS POPPE SASA...


Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia Profesa Milovan Cirkovick, akisikiliza anayombiwa na Meneja wa timu, Nico Nyagawa kulia na Daktari, Cossmass Kapinga
wakati wa mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. timu hizo zilitoka 0-0.

Vigogo wa SimbaSC 
wakati wa mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. timu hizo zilitoka 0-0.
 

Makocha wa makipa,Juma Pondamali wa Coastal Union na James Kisaka wa Simba SC, aliyeipa mgongo kamera wakipongezana baada ya mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya timu zao Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. timu hizo zilitoka 0-0.
Mwenyekiti wa Friends Of Simba, Zacharia Hans Poppe kulia akijadiliana na wenzake wakati wa mchezo wa jana wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. timu hizo zilitoka 0-0.

KOMBE la DUNIA: Higuain hatihati kucheza na Chile


>>ARGENTINA kileleni huko Marekani ya Kusini!!
BRAZIL_2014_BESTStraika wa Real Madrid Gonzalo Higuain ameumia mguu na yupo kwenye hatihati kama atachea Mechi ya Mchujo Kanda ya Marekani ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil hapo Jumatano dhidi ya Chile baada ya kupata majeruhi hayo kwenye Mechi ya Ijumaa ambayo Nchi yake Argentina iliifunga Uruguay bao 3-0.

Katika Mechi hiyo bao za Argentina zilifungwa na Lionel Messi, bao mbili, na Sergio Aguero.
Hadi sasa Argentina ndio wapo kileleni mwa Kundi hilo wakiwa na Pointi 17 kwa Mechi 8 na wapinzani wao wa Jumatano, Chile, wapo nafasi ya 5 wakiwa Pointi 5 nyuma yao.
========================
MATOKEO:
Jumamosi Oktoba 13
Ecuador 3 Chile 1
Argentina 3 Uruguay 0
Ijumaa Oktoba 12
Bolivia 1 Peru 1
Colombia 2 Paraguay 0
RATIBA:
Jumatano Oktoba 17
Bolivia v Uruguay
Venezuela v Ecuador
Paraguay v Peru
Chile v Argentina

MSIMAMO KANDA ya NCHI za MAREKANI ya KUSINI:
Timu zote zimecheza Mechi 8
1 Argentina Pointi 17
2 Colombia 16
3 Ecuador 16
4 Uruguay 12
5 Chile 12
6 Venezuela 11
7 Peru 8
8 Bolivia 5
9 Paraguay 4