Friday, November 9, 2012

 

KAMATI YA UCHAGUZI YA TFF YATOA TAREHE YA UCHAGUZI WA TABORA NA CHAMA CHA MAKOCHA


KAMATI ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka nchini limesema Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA) na Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika Desemba 22 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba za uchaguzi za vyama hivyo, Kamati za uchaguzi zitatangaza mchakato wa uchaguzi Novemba 10 mwaka huu na fomu kwa wagombea uongozi zitaanza kutolewa Novemba 12 mwaka huu. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Novemba 16 mwaka huu.

Vileveile Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetoa mwongozo huo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA baada ya kuomba hivyo kutokana na wagombea sita tu kujitokeza kuomba nafasi tatu za uongozi katika mchakato wa awali.

Wakati huohuo Shirikisho la Soka nchini (TFF) limetoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba 8 mwaka huu.

Viongozi waliochaguliwa kuongoza MZFA ni Patrick Songora, Mwenyekiti, Nassoro Mabrouk, Katibu Mkuu na Richard Kadutu ambaye ni Mwakilishi wa vilabu TFF

Taarifa hiyo inasema ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa MZFA walivyo na imani kubwa katika kusimamia mchezo huo katika Mkoa wa Mwanza.

TFF inaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Kamati za Utendaji ya MZFA iliyochaguliwa chini ya uenyekiti wa Patrick Songora aliyechaguliwa kwa kipindi cha pili mfululizo.
 
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya MZFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.

 

TIMU ZA POLISI ZASHINDWA KUONESHA MAKUCHA LIGI DARAJA LA KWANZA

 
TIMU ya Kanembwa ya Kigoma juzi iliifunga Polisi Tabora mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora

Kanembwa ambayo mpaka sasa ndio inaongoza kundi C ilijipatia mabao yake kupitia kwa Ali Bilal aliyefunga hat-trick dakika za 46, 60 na 89 na Baruani Akilimalui dakika ya 49.

Polisi Tabora ambayo inaonekana kuchechemea ilijipatia bao hilo la kufuta machozi kupitia kwa Ibrahimu Musa dakika ya 86.

Kwenye uwanja wa CCM Kirumba timu ya Pamba waliweza kuutumia vema uwanja wa nyumbani kwa kuifunga Moran ya Kiteto 3-0.

Uwanja wa Jamhuri Polisi Dodoma na Polisi Mara walitoka suluhu ya bila kufungana.

Ligi iliendelea kwa kundi A kuchezwa michezo miwili, kwenye uwanja wa Majimaji wenyeji Mlale waliweza kuondoka na pointi tatu kwa kuifunga Polisi Iringa bao 1-0.

Huko Mbeya uwanja wa Sokoine  wenyeji Mbeya City waliifunga Kurugenzi mabao 3-0.

Mabao ya Mbeya City yalifungwa na Alex Seth dakika ya 34, Patrick Mangunguru dakika ya 80 na Haruni Mohamedi dakika za nyongeza (dakika 92)

 

ASHANTI UNITED NA RHINO TABORA ZAUA LIGI DARAJA LA KWANZA

 
TIMU ya Ashanti United jana  iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Tesema ya Temeke bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Mabatini Pwani.

Ashanti ambayo ipo kundi B imefikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi nne inashikilia usukani kwenye kundi hili.

Bao la Ashanti lilifungwa kipindi cha kwanza dakika ya 38 na Abdul Mwarami.

Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Polisi Dar es Salaam iliifunGA Ndanda ya Mtwara mabao 4-0.
Mabao ya Polisi yalifungwa na Magige Belence dakika ya nne, Henrinco Kayombo dakika ya  51, Patrick Mrope dakika ya 60 na Arnoor Salim dakika ya 83.

Kundi C ulichezwa mchezo mmoja kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora ambapo wenyeji Rhino waliifunga Mwadui ya Shinyanga mabao 2-0.

Mabao ya Rhino, mmoja lilitokana na beki wa Mwadui Lulanga Mapunda kujifunga dakika ya 18 na la pili lilifungwa na Victor Hagaya dakika ya 86.

Mjini Morogoro, uwanja wa Jamhuri uliochezwa mchezo mmoja kati ya Burkina Faso na Small Kids na walitoka suluhu ya 0-0.

Mchezo huu ulikuwa kiporo baada ya kuahirishwa kutokana na Small Kids kuchelewa kufika Morogoro kwasababu gari lao liliharibika.

 

SIMBA YAWAANGUKIA MASHABIKI WAKE.

Klabu ya Simba ambayo ndio mabingwa watetezi wa taji la ligii kuu Tanzania Bara imewataka mashabikiwa wake kujitokeza hapo mkesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzani Bara kati yao na Toto Afrikans utakao fanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam klabu.
Simba imelazimika kuwaangukia mashabiki wao baada ya kuwepo tishio la mashabiki kugomea kwenda uwanjani kuwapa sapoti kufuatia timu hiyo kupata matokeo yasiyoridhisha katika michezo ya hivi karibuni.
Kauli iliyofanana na kuwabembeleza mashabiki hao imetolewa leo na msemaji wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga pale alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi.
Kamwaga ambaye mara kadhaa amekuwa akinukuliwa akitoa mifano ya yale yanayoltokea barani ulaya katika ligi kubwa za huko leo pia amendelea na mifano hiyo pale aliposema hata manchester United ilikaribia kutaka kushuka daraja lakini mashabiki wa vilabu hivyo vikubwa hawakuacha kuvihama vilabu vyao.
Mfano mwingine alioutoa Kamwaga ni kwamba  hata Liverpool ilishawahi kushukua daraja lakini mashabiki wake waliendelea kuisapoti jambo ambalo amelitaka mashabiki wa Simba kuiga mfano huo.
Amewata mashabiki hiyo kesho kujitokeza kwa wingi kwani endapo Yanga akatereza katika mchezo wa jumapili ni kwamba Simba itakuwa imemaliza mzunguko wa kwanza wakiwa wanaongoza ligi hiyo.

 

KOCHA MILOVAN WA SIMBA KUWAKOSA KASEJA NA AMIRI MAFTAHA MCHEZO WA KESHO DHIDI YA TOTO AFRIKANS

 Wakati Simba kesho inajipanga kumaliza duru la kwanza la ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Toto Afrikans mchezo ambao umepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wachezaji wawili muhimu wa timu hiyo Juma Kaseja na Amir Maftaha wenyewe hawatakuwepo katika orodha ya wachezaji wawakilishi katika kikosi cha timu hiyo.
Akiongea hii leo katika makao makuu ya klabu hiyo afisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema kocha Milovan Circovich atamkosa mlinzi wake wa kushoto Amir Maftaha ambaye amefanyiwa upasuaji mdogo wa uvimbe ulikuwepo kichwani upasuaji ambao umefanyika jana.
Pia Milovan atakosa huduma ya mlinda mlango namba moja wa klabu hiyo Juma Kaseja ambaye imearifiwa kuwa ameomba ruhusa ya kupumzika katika kipindi hiki.
Kamwaga amesema kuwa Kaseja ameomba  kupumzika kutokana na tuhuma nzito za kuhujumu timu zilizo elekezwa kwake baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa uliofanyika mwishoni mwa juma lililopota ambapo mabingwa hao watetezi wa taji walifungwa mabao 2-0.
Kwa mantiki hiyo ni dhahiri shahiri kuwa mlinda mlango wa kesho atakuwa ni kati ya William Mweta au Hamadi Waziri Mwinyimani.
 Simba inaingia dimbani katika mchezo wa kesho ikiwa inahitaji ushindi na alama tatu muhimu ambazo zitawasogeza mpaka kufikia alama 26 ambazo ni sawa na za mtani wake Yanga anayeongoza ligi hiyo.
Endapo Simba itashinda mchezo huo basi watakuwa wamerejea kileleni katika msimamo wa ligi angalau kwa siku moja wakisubiri matokeo ya mchezo wa jumapili kati ya Yanga na Coast Union mchezo ambao utachezwa mkoani Tanga katika dimba la Mkwakwani.

 

TAIFA STARS YASIMAMISHA VPL MECHI TANO


 Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ili kupitisha mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Taifa Stars na Kenya (Harambe Stars) itakayochezwa Novemba 14 mwaka huu jijini Mwanza.

Mechi tano za ligi hiyo zilizokuwa zichezwe Novemba 11 mwaka huu, zimerejeshwa nyuma kwa siku moja ambapo sasa zitafanyika Novemba 10 mwaka huu. Mechi hizo ni Simba vs Toto Africans (Uwanja wa Taifa), Kagera Sugar vs Polisi Morogoro (Uwanja wa Kaitaba) na Oljoro JKT vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid).

Nyingine ni Tanzania Prisons vs JKT Ruvu (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine) na African Lyon vs Mtibwa Sugar (Azam Complex). Mechi ya Mgambo Shooting vs Azam (Azam Complex) yenyewe itachezwa Novemba 10 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa.

Nayo mechi ya Coastal Union vs Yanga (Uwanja wa Mkwakwani) itabaki Novemba 11 mwaka huu kwa vile Novemba 10 mwaka huu uwanja huo utakuwa na mechi nyingine. TFF imepanga utaratibu wa kuwapata kwa wakati wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Mabadiliko mengine ni ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo mechi ya Villa Squad vs Transit Camp iliyokuwa ichezwe Novemba 8 mwaka huu sasa inachezwa Novemba 9 mwaka huu, na ile ya Novemba 7 mwaka huu kati ya Burkina Faso na Small Kids inachezwa Novemba 9 mwaka huu. Viwanja ni vilevile.

Kamati ya Ligi imelazimika kufanya mabadiliko hayo kutokana na viwanja husika kuwa na mechi nyingine, na vilevile Small Kids kupata matatizo ya usafiri kutoka mkoani Rukwa

HATUHUSIKI NA SELEMANI SAIDI VS CALED AMAEINDA


organaizesheni ya ngumi za kulipwa tanzania TPBO , Inapenda kuwaarifu kwamba haihusiki na pambano la ngumi za kulipwa kati ya mabondia waliotajwa hapo juu.

TPBO inalazimika kutowa taarifa hii kutokana na masharti iliyompatia muandaaji wa pambano hilo ndg yusuph montanga [GACHA] kushindwa kuyatekeleza.

pia izingatiwe kwamba TPBO ilitowa kibali kwa ndg muandaaji GACHA kwa ajili ya pambano kati ya bondia THOMAS MASHALI VS SELEMANI SAIDI ambalo lilitakiwa kuchezwa katika uwanja wa KINESI ulioko ktk jimbo la ubungo ,tarehe 10 -11-2012.

 lakini kokana na kuumia kwa bondia THOMAS MASHALI katika pambano lake la kugombea ubingwa wa AFRIKA MASHARIKI NA KATI dhidi ya bondia kutoka uganda MEDI SEBYALA ,tpbo ililazimika kumsaidia muandaaji huyo ndg GACHA ili aweze kumpata bondia kutoka kenya ili awe mbqdala wa THOMAS MASHALI.
 Na tpbo ilianza mara moja mawsiliano na kocha juliusn odhiambo kutoka kenya ili atupatie bondia wake .
 Lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele TPBO ilipata wasiwasi na uwezo wa muandaaji huyo kuweza kuandaa pambano hilo hasa alipofikia kutopokea simu ya RAIS wa TPBO kuhusu maendeleo ya maandalizi ya pamnao hilo.
 siku ya jumatatu tarehe 05 -11-2012 nilimuagiza ndg GACHA alete pesa za kuwasafirisha bondia na kocha wake kutoka kenya ili wawasili nchini siku ya alhamisi usiku kwa ajili ya zoezi la upimaji wa uzito siku ya ijumaa kwa ajili ya pambano las jumamosi tarehe 10- 11- 2012 kama kanuni ya ngumi za kulipwa zinavyoamuru ,upimaji wa uzito kwa mabondia siku moja kabla ya pambano.
 Na ikafikia hata mimi kumpatia ndg GACHA namba za simu za ndg bakari ambaye ni mfanyakazi wa SPIDER BUS SERVISES ili awasiliane naye kuhusu ujio huo wa bondia kutoka kenya. lkn mpaka hivi sasa ninapoandika taarifa hii kwenu sijapata taarifa yoyote inayohusu kuwasili kwa mabondia hao kutoka kenya ,na hivyo TPBO haiwezi kuvnja kanun i za mchezo wa ngumi za kulipwa , kwa kumfurahisha tu MUANDAAJI.
 TPBO pia ilimpa masharti ndg GACHA awsilishe OFISI ZA TPBO pesa za kuwarudisha wakenya baada ya mchezo badala ya kutegemea makusanyo ya mlangoni ,pia awasilishe DOLA 100 ambayo ilikuwa ni malipo ya bondia huyo kutoka kenya kabla ya pambano ,lakini alikataa.
 Kwa taarifa hii TPBO inatamka rasmi kwamba isihusishwe na lolote litakalotokea endapo bondia huyo kutoka kenya atakuwa amewasili kwa njia zingine ambazo NDG GACHA atakuwa ameamuwa kuzitumia.
 TPBO inalazimika kutowa taarifa hii kwenu ili kulinda heshima yake na uaminifu ambayo imejijengea katika nchi nzima ya tanzania na haiko tayari kufanya kazi na waandaaji ambao uwezo wao ni wa kujaribu jaribu mambo na siyo wazoefu kwani hatimaye huwa ni kuuvunjia heshima mchezo wa ngumi za kulipwa na kusababisha udharauliwe.
  imeletwa kwenu nami
yassin abdallah mwaipaya -USTAADH.
RAIS -TPBO
kwenda Morogoro.


TFF YATEUA WADAU 10 KWA AJILI YAKUSAIDIA TIMU YA TAIFA

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania limeteua wadau 10 kwa ajili ya kusaidia timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys itakayopambana na Congo (Brazaville) katika mechi ya raundi ya tatu ya michuano ya awali ya Mataifa ya Afrika.
Uteuzi huo umefanywa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga baada ya Kamati ya Vijana ya TFF kufanya kikao chake kujadili kwa umakini ushiriki wa timu hiyo na kupeleka mapendekezo yake kwa rais huyo wa shirikisho.
Kutokana na umuhimu wa mechi hiyo itakayoamua timu itakayofuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, TFF imeona umuhimu wa kuwa na kamati ambayo itakuwa na majukumu mawili makubwa ambayo ni:
1.       Kuhamasisha vijana waone umuhimu na kuwa na ari ya kushinda mechi hiyo
2.       Kuhamasisha umma uone umuhimu wa mechi hiyo na hivyo kuisaidia iweze kufuzu.
Walioteuliwa kuunda kamati hiyo ni:
1.       Ridhiwani Kikwete                                           Mwenyekiti
2.       Ahmed Seif (Magari)                                      Mjumbe
3.       Nassoro Bin Slum                                             Mjumbe
4.       Henry Tandau                                                    Katibu
5.       Ahmed Mgoyi                                                   Mjumbe
6.       Aboubakar Bakhresa                                      Mjumbe
7.       Angetile Osiah                                                   Mjumbe
8.       Kassim Dewji                                                     Mjumbe
9.       Abdallah Bin Kleb                                             Mjumbe
10.   Salim Said                                                            Mjumbe
Baada ya kuvuka raundi mbili za kwanza bila ya kucheza mechi kutokana na wapinzani wake kujitoa, timu ya Serengeti Boys inahitaji kufanya kila iwezalo kuweza kuiondoa Congo kwenye mashindano hayo na kuweka rekodi ya kufuzu kucheza fainali hizo za Afrika ambazo pia zitatoa wawakilishi wa Afrika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia. Mechi za kwanza za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Novemba 16 na 18, 2012 na mechi za marudiano zitachezwa kuanzia Novemba 30, 2012 hadi Desemba 2, 2012
 
*Kuhusu suala la Azam FC kuwasimamisha wachezaji watatu kwa tuhuma za kuhusika kuhujumu timu, tayari TFF imepokea barua hiyo ya Novemba 8, 2012 na inalishughulikia na kulifuatilia kwa makini.
*TFF inapenda kukipongeza Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Mwanza kwa kufanya uchaguzi wake kwa amani na kufanikiwa kupata viongozi wapya watakaokuwa chini ya uenyekiti wa Jackson Songora. Rais wa TFF amewapongeza viongozi waliorekjea madarakani na viongozi wapya akieleza magtumaini yake kuwa kamati mpya ya Utendaji ya MRFA itaelekeza nguvu zake katika kuendeleza mikakati iliyokuwepo ya kuinua kiwango cha mpira wa miguu na kubuni mikakati mingine kwenye mkoa huo na Tanzania kwa ujumla ikishirikiana na TFF.
*Ligi Kuu ya Vodacom inatazamiwa kuendelea kesho kwenye viwanja tofauti
1. Simba                               v Toto Africans                                  Uwanja wa Taifa
2. T. Prisons                        v JKT Ruvu                                           Sokoine
3. Kagera Sugar                 v Polisi Moro                                      Kaitaba
4. African Lyon                  v Mtibwa Sugar                                 Azam Complex
5. Oljoro JKT                       v Ruvu Shooting                               Sheikh Amri Abeid
6. Mgambo JKT                 v Azam FC                                           Mkwakwani
Jumapili
1.       Coastal Union    v Young Africans                               Mkwakwani

 

BASI LA YANGA LAPASULIWA KIOO KIBUKU NA SHABIKI WA SIMBA

Basi la Yanga

BASI la Yanga limefanyiwa fujo na watu wasiojulikana, wanaosadikiwa kuwa ni mashabiki wa Simba, eneo la Kabuku, wakiwa njiani kuelekea Tanga.
Baraka Kizuguto, Ofisa tovuti wa Yanga aliye katika msafara wa timu  amesema  mida hii kwamba, jamaa aliyerushwa jiwe alikuwa juu ya mti na limepasua kioo, ila halijajeruhi mtu.
Amesema wametoa ripoti Polisi, ingawa hawakufanikiwa kumkamata mtu kwa sababu wahusika walikuwa wamekwishakimbia baada ya tukio.
Yanga iliyoondoka leo alfajiri Dar es Salaam tayari ipo Tanga , imefikia katika hoteli ya Central City, barabara ya Nane na jioni itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
Yanga iko Tanga kwa ajili mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumapili.
Yanga imepania kushinda mechi hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri katika msimamo wa Ligi Kuu, ambayo mzunguko wake wa pili utarejea Januari mwakani.
Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam jana na wachezaji wake wote wapo vizuri, chini ya kocha wake Mholanzi, Ernie Brandts.
Wchezaji wa Yanga wamepania kuvunja rekodi ya Coastal Union kutofungwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani, Mkwakwani, Tanga katika mechi hiyo.
Akizungumza  kwa niaba ya wenzake mapema wiki hii, Nahodha Msaidizi wa Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ alisema kwamba wanataka kustawisha uongozi wao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwafunga Coastal Jumamosi.
Alisema wanajua Coastal ni timu nzuri na wanatarajiwa upinzani katika mechi hiyo, ila ameonya Yanga ya sasa ni tishio na wachezaji wako vizuri ‘ile mbaya’.
“Kwa kweli mimi na wachezaji wenzangu tunamshukuru mwalimu mpya (Ernie Brandts) kwa kutupa vitu vipya na muhimu. Timu yetu imebadilika na kila mtu anaona sasa. Wale Coastal si hawafungwi kwao wale, sasa sisi tutaenda kuwafunga pale pale, tena kipigo kikali,”alisema.
Lakini pia habari za ndani kutoka Yanga zinasema kwamba tayari wachezaji wameahidiwa donge nono iwapo watashinda mechi hiyo.
Wachezaji hao, walizawadiwa Sh. Milioni 15 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC mwishoni mwa wiki katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, uliifanya Yanga iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi moja ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi 23, ambayo juzi imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.  

YANGA WAIFUATA COASTAL ALFAJIRI

Yanga SC
YANGA SC inaondoka leo alfajiri Dar es Salaam kwenda Tanga, tayari kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa mzunguko wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Jumapili.
Yanga imepania kushinda mechi hiyo ili kujiweka katika mazingira mazuri katika msimamo wa Ligi Kuu, ambayo mzunguko wake wa pili utarejea Januari mwakani.
Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam jana na wachezaji wake wote wapo vizuri, chini ya kocha wake Mholanzi, Ernie Brandts.
Wchezaji wa Yanga wamepania kuvunja rekodi ya Coastal Union kutofungwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani, Mkwakwani, Tanga katika mechi hiyo.
Akizungumza  kwa niaba ya wenzake mapema wiki hii, Nahodha Msaidizi wa Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ alisema kwamba wanataka kustawisha uongozi wao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwafunga Coastal Jumamosi.
Alisema wanajua Coastal ni timu nzuri na wanatarajiwa upinzani katika mechi hiyo, ila ameonya Yanga ya sasa ni tishio na wachezaji wako vizuri ‘ile mbaya’.
“Kwa kweli mimi na wachezaji wenzangu tunamshukuru mwalimu mpya (Ernie Brandts) kwa kutupa vitu vipya na muhimu. Timu yetu imebadilika na kila mtu anaona sasa. Wale Coastal si hawafungwi kwao wale, sasa sisi tutaenda kuwafunga pale pale, tena kipigo kikali,”alisema.
Lakini pia habari za ndani kutoka Yanga zinasema kwamba tayari wachezaji wameahidiwa donge nono iwapo watashinda mechi hiyo.
Wachezaji hao, walizawadiwa Sh. Milioni 15 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC mwishoni mwa wiki katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, uliifanya Yanga iongoze Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 26, ikiwa imebakiza mechi moja ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Caostal Union mjini Tanga, ikifuatiwa na Simba SC yenye pointi 23, ambayo juzi imefungwa 2-0 na Mtibwa Sugar mjini Morogoro.  

TOTO WAPO KAMA HAWAPO, WAMEJICHIMBIA TANDIKA TAYARI KUUA MNYAMA KESHO

Toto African

TIMU ya Toto African imejichimbia eneo la Tandika mjini Dar es Salaam kwa takriban wiki nzima, ikijifua vikali tayari kwa mchezo wao dhidi ya Simba kesho.
Kocha wa Toto, John Tegete alisema  jana kwamba, yeye hatakuja Dar es Salaam kuungana na timu yake kwa ajili ya mechi hiyo kwa sababu ya majukumu ya kitaifa, lakini kikosi kipo vizuri.
“Mimi nina majukumu ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Taifa Stars na Kenya huku Mwanza, ila kila kitu kipo sawa, timu iko huko, imeweka kambi Tandika na Jumamosi Mnyama anachinjwa Uwanja wa Taifa,”alisema Tegete.
Tegete alisema Toto wafufuliwe kwa kaburini, kwa Simba watacheza mechi na kushinda kwa sababu wanaamini hao ni vibonde wao tu.
“Na ndiyo maana sina wasiwasi nimebaki Mwanza najua tu vijana wangu watachinja Mnyama,”alisema.  
Toto imekuwa na rekodi ya kuisumbua Simba katika Ligi Kuu hata ikiwa vibaya na hilo ndilo linatarajiwa kwenye mchezo wa kesho Uwanja wa Taifa.
Awali, Simba ilitishia kugoma kucheza mechi hiyo kesho, siku tofauti na wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mapema wiki hii limetangaza kuzirudisha nyuma kwa siku moja mechi zote za mwisho za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, kutoka Jumapili wiki hii hadi Jumamosi, kasoro mechi ya Yanga na Coastal Union pekee, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Na sababu za kutorudishwa nyuma kwa mechi ya Yanga ni kwa kuwa Jumamosi kutakuwa na mchezo mwingine wa ligi hiyo, Uwanja wa Mkwakwani, kati ya Mgambo JKT na Azam FC.
Lakini Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga alisema  juzi kwamba hawako tayari kucheza siku tofauti na Yanga kwa sababu ya upinzani uliopo baina yao katika mbio za ubingwa, kwani wanahofia mchezo mchafu.
“Unajua bwana ligi hii ilipofikia ni pabaya, haiwezekani uzichezeshe Simba na Yanga siku tofauti, hivyo sisi tunawaandikia barua TFF kuwataarifu kwamba hatuko tayari kwa mabadiliko hayo,”alisema Kamwaga.
Lakini inavyoonekana Wekundu hao wa Msimbazi wamefyata mkia na kesho wataingiza timu Taifa.
Mechi nyingine za Jumamosi ni Mgambo JKT na Azam FC Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, African Lyon na Mtibwa Sugar Chamazi, Dar es Salaam, Prisons na JKT Ruvu Sokoine, Mbeya, Kagera Sugar na Polisi Morogoro, Kaitaba, Bukoba na JKT Oljoro na Ruvu Shooting Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

KASEJA AIBUKA KAMA MTAZAMAJI MAZOEZINI SIMBA

Kaseja akiomba dua katika moja ya mechi za timu hiyo

NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja kwa siku ya tatu mfululizo jana ameendelea na mgomo wake wa mazoezi ya timu yake inayojiandaa na mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, utakaopigwa kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku kukiwa kuna habari ameamua kuachana na timu hiyo.
Lakini tofauti na siku mbili za awali, Kaseja jana alifika kwenye Uwanja wa Kinesi, ila mtazamaji kama watazamaji wengine.
Hakufanya mazoezi, ingawa alipoulizwa alisema yeye bado bado mchezaji wa Simba na ana mkataba na timu hiyo.
Mwanzoni mwa wiki ilielezwa kwamba Kaseja amewaaga wachezaji wenzake na kuwaambia yeye na klabu hiyo basi.
Hatua hiyo ilifuatia Kaseja kutukanwa na kutishiwa maisha na mashabiki wa Simba baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakimtuhumu kufungwa mabao ya kizembe.
Lakini tayari uongozi wa Simba umelaani vikali vurugu na vitisho alivyotolewa kipa wao huyo namba moja,  na kusema wanafikiria kuwachukulia hatua kali watu waliomfanyia hivyo Nahodha wao huyo. 


INTER, PARTIZAN, LYON, LEVERKUSEN, KAZAN, METALIST NA HANOVER 96 ZATINGA 32 BORA EUROPA LEAGUE.

MABAO mawili yaliyofungwa na Rodrigo Palacio yaliiiwezesha Inter Milan kutinga katika hatua ya mtoano wa Europa League wakati Atletico Madrid walijikuta wakifungwa kwa mara ya kwanza katika mechi 16 walizocheza nchini Ureno. 
 Milan ambao waliwafunga Partizan Belgrade ya Serbia kwa mabao 3-1 wameungana na timu za Bayer Leverkusen, Rubin Kazan, Metalist Kharkiv, Hanover 96 na Olympique Lyon katika hatua hiyo ya mtoano ambayo itashirikisha timu 32.
 Rubin Kazan ya Urusi ilifanikiwa kuongoza katika kundi H wakiwa na alama 10 sawa na Inter baada ya kuifunga Neftchi Baku ya Azerbaijan kwa bao 1-0 wakati Leverkusen na Metalist nazo pia zikikabana koo kwa alama 10 katika kundi K baada ya kushinda michezo yao ya jana usiku.
 Lyon waliendeleza rekodi yao nzuri kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mshindi wa pili wa michuano hiyo msimu uliopita Athletic Bilbaona kushika usukani wa kundi I wakifuatiwa na Sparta Prague katika nafasi ya pili.

MUAMBA AWASHUKURU MASHABIKI WA WHITE HART LANE.

MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Bolton Wanderers, Fabrice Muamba ambaye alikumbwa na tatizo la moyo wake kusimama wakati wa mchezo baina ya timu yake na Totenham Hotspurs Machi mwaka huu amerejea kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa White Hart Lane mahali ambao ndipo alipoanguka.
 Muamba ambaye moyo wake ulisimama kwa dakika 78 baada ya kuanguka wakati wa mchezo huo wa Kombe la FA baadae alipona kabisa kutokana na tatizo hilo lakini alilazimika kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 24 kutokana na ushauri wa madaktari.
 Akitembea uwanjani wakati wa kipindi cha mapumziko katika mchezo wa Europa League kati ya Spurs na Maribor ya Slovenia, Muamba alionyesha mahali ambapo alianguka na baade kuzungumza na mashabiki waliokuwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo. 
 Muamba aliwashukuru mashabiki wa Spurs ambao walikuwepo na kumuombea wakati alipopata tatizo hilo na kusema kwamba hatawasahau kamwe katika maisha yake.
 Timu ya madaktari wa Spurs na Bolton walijaribu kuokoa maisha ya Muamba kwa muda wa dakika 20 baada ya kuanguka kabla ya kuondolewa na ukimbizwa hospitali ambapo alilazwa kwa kipindi cha wiki nne.

VIWANJA SITA KUWA TAYARI KWA AJILI YA CONFEDERATION CUP JUNE MWAKANI.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limesema kuwa viwanja sita kama vitakuwa tayari kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho kama ilivyopangwa mwanzoni.
 Katika taarifa yake iliyotolewa jana imeelezea kuwa miji iliyopo Kaskazini-Mashariki ya Salvador na Racife itakuwa miji mojawapo itakayoandaa michuano hiyo ambayo itafanyika mwakani huku mingine ikiwa ni miji ya Rio de Janeiro, Brasilia, Salvadr na Fortaleza.
 Pamoja na kutangaza miji hiyo sita ambayo itakuwa wenyeji wa michuano hiyo lakini Recife na Salvador itathibitishwa rasmi kama wakionyesha jitihada na kulishawishi shirikisho hilo kwamba maandalizi yao yatakamilika kwa wakati.
 Kombe la Shirikisho litaanza kutimua vumbi June 15 hadi 30 mwakani ambapo itazikutanisha nchi sita ambazo ni mabingwa wa mabara, mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2010 na nchi wenyeji wa michuano hiyo.

WACHEZAJI WATANO WAFUNGIWA NCHINI UFARANSA.

KIKUNDI cha wachezaji wa kimataifa wa Ufaransa chini ya miaka 21 wamefungiwa kushiriki michezo ya kimataifa kwasababu ya kutoroka kambini wakati wa mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya mwezi uliopita. 
 Wachezaji waliopata adhabu hiyo ni pamoja na Yann Mvila na Chris Mavinga wanaocheza katika klabu ya Rennes, Wissam Ben Yedder anayecheza timu ya Toulouse, Antoine Griezmann wa Real Sociedad na Mbaye Niang anayekipiga AC Milan. 
 Wachezaji wote hao wamefungiwa kucheza michezo ya kimataifa mpaka Desemba 31 mwakani kasoro Mvila ambaye amepata adhabu kubwa zaidi ya kufungiwa mpaka Juni 30 mwaka 2014 adhabu ambayo imetolewa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini Ufaransa.
 Wachezaji hao walitoroka katika kambi yao iliyopo katika mji uliopo Kaskazini mwa mji wa Le Havre na kwenda jijini Paris kujirusha na kupelekea timu yao kufungwa na Norway bao 1-0.
 Mvila amekuwa akioywa na FFF mara kwa mara kwa kukataa kushikana mikono na aliyekuwa na kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Laurent Blanc wakati alipotolewa wakati wa robo fainali ya michuano ya Ulaya iliyofanyika mwaka huu katika mchezo baina ya timu hiyo na Hispania.

TUNISIA KUWEKA KAMBI QATAR.

SHIRIKISHO la Soka nchini Tunisia limetangaza kuwa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kitafanya maandalizi yake nchini Qatar kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwakani Afrika Kusini. 

 Tunisia inatarajiwa kuweka kambi ya siku 12 jijini Doha kwa ajili ya maandalizi hayo ambapo wanatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mali na Burkina Faso.

 Msafara wan chi hiyo unatarajiwa kutua katika mji wa Rustenburg, Afrika Kusini Januari 15 ambapo kundi D ambalo litakuwa na timu za Ivory Coast, Algeria na Togo ndio zitacheza michezo ya hatua ya makundi katika michuano hiyo.

 Kabla ya kuelekea Qatar chi hiyo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Switzerland Novemba 14 mwaka huu na kocha wa Sami Trabeslsi tayari ametangaza kikosi cha wachezaji 22 tayari kwa ajili ya mchezo huo.

SANTI CAZORLA, JUAN MATA NA MICHU WANUNUA HISA ZA UMILIKI WA TIMU NCHINI HISPANIA

Tumekuwa tukisikia namna wanamichezo wanavyotumia vibaya utajiri wao wanaopata katika fani zao, hasa wanasoka - huku wakiacha majukumu yao ya kurudisha kwa jamii katika kusaidia soka lizidi kupiga mbele zaidi, lakini jambo ambalo nimelisikia sasa limenifurahisha kiasi kujua kwamba kundi la wachezaji wa zamani wa Real Oviedo wamejiunga pamoja kuisadia timu yao inayokabiliwa na ukata mkubwa.

Santi Cazorla, Juan Mata na Michu wote ni wachezaji wa zamani wa Oviedo wakiwa wamekulia na kujifunza soka katika klabu hiyo na tunaambiwa kwamba watatu hao wamenunua hisa katika klabu hiyo ili kuikoa klabu hiyo kukaa vizuri kibiashara. 

Klabu hiyo ya Hispania, ambao kwa sasa wapo katika nafasi ya tano katika daraja la tatu la soka la Spain, ndio klabu ambayo Mata, Michu, na Cazorla wote walianzia maisha yao ya soka la kisasa katika klabu hiyo, Michu kwa kipekee zaidi alitumia muda mrefu zaidi katika klabu hiyo kabla ya kwenda Celta Vigo B.

Mie, Mata na Cazorla wote tumenunua hisa, lakini haitakuwa sawa kwangu mimi kusema ni hisa kiasi gani. Tumejaribu kuisadia klabu yetu ambayo wote tumeichezea," alithibitisha Michu.

Uchumi wa Hispania upo katika hali mbaya sana na klabu inahitaji kiasi kinachokaribia €2m ili kuweza kuendelea. Watu wengi wamenunua hisa  na tumaini letu sasa hali ya uchumi itaimarika kiasi mpaka kufikia mwisho wa ununuzi wa hisa tarehe 17 mwezi huu. 
"Hii ni klabu yangu ya nyumbani, klabu niipendayo, hivyo naamini mchang wetu na watu wengine utatosha kuisadia."
  

EUROPA LIGI: Liverpool hoi, Newcastle sare, Spurs yashinda!!


>>NDUGU Ameobi wacheza pamoja Newcastle!!
EUROPA_LIGI_CUP+++++++++++++++++++
MATOKEO-KLABU za ENGLAND:
FC Anzhi Makhachkala 1 Liverpool 0
Club Brugge KV 2 Newcastle United 2
Tottenham Hotspur 3 NK Maribor 1
+++++++++++++++++++
FC Anzhi Makhachkala 1 Liverpool 0
Nafasi ya Liverpool kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 32 imepata pigo kubwa baada ya kufungwa Bao 1-0 na Timu inayofundishwa na Guus Hiddink, Anzhi Makhachkala.
+++++++++++++++++++
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 4]
KUNDI A
1 FC Anzhi  Pointi 7
2 Liverpool 6
3 Young Boys 6
4 Udinese 4
+++++++++++++++++++
Kikosi cha Liverpool kilichoteuliwa na Meneja Brendan Rodgers kilikuwa na Wachezaji wengi Chipukizi wasiokuwa na uzoefu na wakajikuta wakipigwa na Bao la Lacina Traore kabla ya Haftaimu.
VIKOSI:
Anzhi Makhachkala: Georgi Gabulov, Logashov, Samba,Joao Carlos, Tagirbekov, Ahmedov, Jucilei, Zhirkov, Eto'o, Boussoufa, Traore. 
Akiba: Pomazan, Gadzhibekov, Agalarov, Lakhiyalov, Carcela-Gonzalez, Smolov, Burmistrov.
Liverpool: Jones, Wisdom, Carragher, Coates, Flanagan, Henderson, Coady, Cole, Shelvey, Downing, Morgan. 
Akiba: Gulacsi, Assaidi, Pacheco, Wilson, Fernandez Saez, Sama, Robinson.
Refa: David Fernandez Borbalan (Spain)
Club Brugge 2 Newcastle United 2
Newcastle walitoka nyuma kwa bao 2-0 na kufanikiwa kusawazisha na kutoka sare ya 2-2 walipocheza na Club Brugge.
Matokeo hayo yamewafanya Newcastle waendelee kushikilia uongozi wa Kundi D.
Ivan Trickovski na Jesper Jorgensen ndio waliofunga Bao za Club Brugge lakini Newcastle wakacharuka na kusawazisha kupitia Vurnon Anita na Shola Ameobi
+++++++++++++++++++
KUNDI D
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Newcastle Pointi  8
2 Bordeaux 7
3 Brugge 4
4 Maritimo 2
+++++++++++++++++++
Kwa mara ya kwanza katika Miaka 60, Ndugu wawili walikuwa kwenye Kikosi cha Newcastle ambapo leo Shola na Sammy Ameobi walianza Mechi hiyo wakiwaiga Ndugu George na Ted Robledo walivyofanya Mwaka 1952.
VIKOSI:
Club Brugge: Bojan Jorgacevic, Carl Hoefkens, Jordi Figueras, Tom Høgli, Michael Almebäck, Ryan Donk, Vadis Odjidja-Ofoe, Ivan Trickovski (Mohammed Tchité, 45),
Jesper Jørgensen, Maxime Lestienne, Carlos Bacca
Newcastle United: Tim Krul, Fabricio Coloccini, James Tavernier, Michael Williamson,
Gael Bigirimana, Vurnon Anita, Gabriel Obertan, Sylvain Marveaux, Cheik Tioté, Sammy Ameobi, Shola Ameobi
Refa: Luca Banti
Tottenham 3 Maribor 1
Jermain Defoe amepiga hetitriki na kuipa Tottenham ushindi wa Bao 3-1 dhidi ya NK Maribor na kufufua matumaini yao ya kufuzu baada ya kutoka sare Mechi zao zote 3 kwanza.
+++++++++++++++++++
KUNDI J
1 Lazio Pointi 8
2 Tottenham 6
3 Maribor 4
4 Panathinaikos 2
+++++++++++++++++++
VIKOSI:
Tottenham: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton, Lennon, Huddlestone, Carroll, Bale, Defoe, Adebayor
Akiba: Cudicini, Dempsey, Gallas, Sigurdsson, Falque, Livermore, Mason.
Maribor: Handanovic, Milec, Rajcevic, Arghus, Mejac, Cvijanovic, Mertelj, Filipovic, Ibraimi, Tavares, Beric
Akiba: Pridigar, Vidovic, Mezga, Komazec, Potokar, Viler, Dodlek.
Refa: Antti Munukka (Finland)
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Alhamisi Novemba 8
FC Anzhi Makhachkala 1 Liverpool FC 0
Udinese Calcio 2 BSC Young Boys 3
A. Académica de Coimbra 2 Club Atlético de Madrid 0
FC Viktoria Plzen 4 Hapoel TelvAviv 0
Olympique de Marseille 2 VfL Borussia Mönchengladbach 2
Fenerbahçe SK 2 AEL Limassol FC 0
Club Brugge KV 2 Newcastle United 2
FC Girondins de Bordeaux 1 CS Marítimo 0
Molde FK 1 FC Steaua Bucuresti 2
FC København 0 VfB Stuttgart 2
AIK 1 PSV Eindhoven 0
SSC Napoli 4 FC Dnipro Dnipropetrovsk 2
FC Basel 1893 1 Videoton FC 0
Sporting Clube de Portugal 1 KRC Genk 1
Neftçi PFK 0 FC Rubin Kazan 1
FK Partizan 1 FC Internazionale Milano 3
Hapoel Kiryat Shmona FC 1 AC Sparta Praha 1
Athletic Club 2 Olympique Lyonnais 3
S.S. Lazio 3 Panathinaikos FC 0
Tottenham Hotspur FC 3 NK Maribor 1
FC Metalist Kharkiv 3 Rosenborg BK 1
Bayer 04 Leverkusen 3 SK Rapid Wien 0
Hannover 3 Helsingborgs IF 2
FC Twente 0 Levante UD 0