Tuesday, December 18, 2012

EXCLUSIVE: UONGOZI WA SIMBA WAITELEKEZA TIMU B, WATUMIA FEDHA ZAO ZA MAANDALIZI KULIPA GYM YA SIMBA A - WACHEZAJI KUGOMA KUINGIA UWANJANI KESHO

 

Baada ya kuvumilia kwa muda mrefu vitendo vya uongozi wa klabu ya Simba kutowapa huduma muhimu katika kuendesha timu ya B ya klabu hiyo, leo hii wachezaji na makocha wa timu Selemani Matola na Patrick Rweyemamu inasemekana wameamua kutoingiza timu hiyo uwanjani katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Uhai linaloendelea katika viwanja vya Karume na Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kilicho karibu na timu hiyo ya Simba B kimesema uongozi wa klabu hiyo umekuwa ukiwatelekeza wachezaji wa timu hiyo kwa muda mrefu katika kuwapa mahitaji yao ya kimsingi - "Kiukweli uongozi hauna habari hata kidogo na hii timu B, wamewaachia Matola na Rweyemamu kila kitu. Wachezaji wanadai mishahara ya miezi mitatu sasa, fedha zao za ushindi wa Kombe la BancABC hawakuambulia kitu chochote. Na juzi zile fedha za maandalizi walizotoa wadhamini wa Uhai Cup, wamechukua na kwenda kulipia gym kwa ajili ya timu A huku wakishindwa kutoa hata senti tano kwa ajili ya timu husika yenye kushiriki kombe la Uhai Cup ambayo ni timu B.

"Hii ni makusudi wanayofanya uongozi sio kwamba timu haina fedha, mfano angalia jzui wametoa $40,000 na mshahara wa $2000 kwa kipa Dhaira, pia wamempa Okwi mapesa kibao lakini wanashindwa kuangalia msingi wa maendeleo ya Simba SC ambao ni timu ya pili. Rweyemamu amekuwa akijitoa sana katika kuisadia hii timu ya pili lakini sasa anashindwa kuendelea kwa sababu uongozi hauonyeshi kuwa na mapenzi ya dhati na Simba B. Timu jana ilipata aibu kubwa wakati ikitoka Chamazi - basi walilokuwa wakitembelea liliishiwa na mafuta na kupaki barabarani, hivi kweli jambo kama hilo la kuitokea timu kubwa kama ya Simba kweli? Sasa kutokana na mambo yote hayo leo hii wachezaji wanataka kugoma kwenda uwanjani kesho ili kuushinikiza uongozi kutimiza mahitaji yao." - kilimaliza chanzo cha habari.

**Kwa mtindo huu soka la Bongo litaendelea kudumaa mpaka tutakapopata viongozi wenye mapenzi na nia ya dhati ya kutaka maendeleo ya soka Tanzania****   

ABDALLAH JUMA WA SIMBA AWANIWA NA TIMU TANO


PAMOJA na kutong’ara kwenye timu yake katika mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom, mshambuliaji wa Simba Abdallah Juma ameonekana lulu kwa timu nyingine baada ya kuwaniwa na timu zaidi ya tano. 
Nyota huyo ambaye alisajiliwa na Simba mawaka jana akitokea kwa maafande wa JKT Ruvu, aliweza kung’ara zaidi na timu hiyo kwenye mechi za kirafiki wakati wa maandalizi wa ligi hiyo. 
Habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba zinaekleza kwamba tayari vilabu vya Pamba ya Mwanza, Coastal Union ya Tanga, Tanzania Prisons ya Mbeya, African Lyon na Ruvu Shooting. 
Kiongozi mmoja wa Simba alisema hivi karibuni kwamba, timu hizo zimetuma maombi ya kutaka kumsajili kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo pamoja na ligi daraja la kwanza, lakini mpka sasa bado hawajaamua juu ya suala hilo. 
“Ndiyo hivyo bado hajuaamua juu ya suala la Abdallah kwanmi hata sisi pia ni mchezaji muhimu kwetu…tunasubiri majadiliano ya kamati ya ufundi kwanza ndipo tutakapotoa maamuzi na pia dau nono litazingatiwa,”alisema. 
Aidha, kiongozi huyo aliongeza kuwa nyota wao Haruna Shamte pia ameomba na klabu ya African Lyon  ambapo viongozi wa pande zote wapo kwenye mazungumzo.
WAKATI HUO HUO
Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom, Simba Sc wameanza mazoezi ya ufukweni chini ya kocha, Jamhuri Kihwelo 'Julio'
Ofisa habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba, Julio atakinoa kikosi hicho kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa ligi hiyo, huku wakisubiri ujio wa kocha wao mpya, Mfaransa,Patrick Liewang anayetarajiwa kutua nchini Desemba 27.
Amsema wachezaji walioanza mazoezi ni wale wasio kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kipo kambini kujiandaa na mchezo wake wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zambia 'Chipolopolo' utakaopigwa Desemba 22 kwenye dimba la Taifa.
"Pia wachezaji ambao hawapo ni wale wa kigeni ambao wapo makwao,"alisema.

 

MSONDO, SIKINDE USO KWA USO EQUATOR GRILL, SIKU YA KRISMAS


                                              Msondo Ngoma wakiwa kazini
                                               Sikinde Ngoma ya Ukae wakishoo love kwa wadau

Na Mwandishi Wetu
Baada ya kila mmoja kupewa vyombo vipya na Konyagi, bendi pizani za Msondo Ngoma na  Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae)  zitapambana siku ya Krismasi katika ukumbi wa Equator Grill, Temeke.
Mpambano huo umeandaliwa na kampuni za Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la kusherekea sikukuu ya Krismasi na kufunga mwaka 2012.
Kapinga alisema kuwa pia pambano hilo litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka 2012.
Mratibu huyo alisema bendi hizo zitapiga jukuwaa moja lakini kila moja atatumia vyombo vyake ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa. Kila bendi itatumia muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani.
“Litakuwa pambano la aina yake ukizingatia kuwa hii itakuwa ni mara ya pili kwa bendi hizo kupambana siku ya Krismasi tangu zianzishwe. Mwaka jana zilipambana katika TCC Club Chang’ombe,” alisema Kapinga.
Alisema mchuano huo itaanza saa tisa alasiri hadi liamba.

AZAM YALALA 2-0, NI KAMA IMETOLEWA KOMBE LA HISANI

Kiungo wa Azam FC ya Dar es Salaam, Humphrey Mieno akimtesa beki wa Shark FC ya Kinshasa katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Hisani jioni ya leo kwenye Uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa, DRC. Shark ilishinda 2-0. 

AZAM FC ya Dar es Salaam, imefungwa mabao 2-0 na Shark FC ya hapa, katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi B, Kombe la Hisani, kwenye Uwanja wa Martyrs jioni hii.
Mabao ya washindi, timu inayomilikiwa na mdogo wake rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Joseph Kabila yalifungwa na Ndibu Kalala dakika ya 23 na Kalala Kabongo dakika ya 34.
Hata hivyo, kipigo hicho kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na uchezeshaji mbovu wa marefa, ambao tangu mwanzo walionekana kuwapendelea wenyeji.
Azam leo imenyimwa penalti mbili za halali, moja kila kipindi, ya kwanza baada ya shuti la mshambuliaji Gaudence Mwaikimba kuzuiwa kwa mkono na beki wa Shark na ya pili kiungo Humphrey Mieno aliangushwa kwenye eneo la hatari, tena ndani ya sita akiwa amekwishamtoka kipa, lakini zote refa akapeta.
Washika vibendera nao walizima mashambulizi kadhaa ya Azam kwa kudai wachezaji walikuwa wameotea.
Mabao yote Azam walifungwa wakitoka kushambulia na hayakuwa na mushkeli, makosa ambayo walirekebisha na hawakuyarudia kipindi cha pili. Kipindi cha kwanza, timu zilishambuliana kwa zamu, lakini kipindi cha pili Azam walitawala zaidi mchezo na kama si ‘madudu’ ya refa, matokeo yangeweza kubadilika.
Kwa matokeo haya, Shark inaongoza Kundi B kwa pointi zake tatu, ikifuatiwa na Dragons iliyotoka 1-1 na Azam katika mchezo wa kwanza.
Azam sasa itaomba Shark iifunge zaidi ya mabao 2-0 Dragons katika mechi ya mwisho ya kundi hilo Desemba 23, ili ifuzu kuingia Nusu Fainali.
Azam imecheza mechi zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivory Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Nusu Fainali zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.  Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa. 
Kocha wa makipa, Iddi Abubakar aliyeiongoza timu hiyo katika mechi hizo mbili alilalamikia uchezeshaji wa marefa, ambao walisindikizwa na Polisi kutoka uwanjani baada ya mechi, kutokana na kuwakera hata mashabiki wa timu za hapa waliotaka kuwafanyia fujo.
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Malika Ndeule/Uhuru Suleiman dk 85, Samih Hajji Nuhu, Luckson Kakolaki/Omar Mtaki dk 65, David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo/Himid Mao dk80, Humphrey Mieno, Seif Abdallah, Gaudence Mwaikimba na Waziri Salum/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk 65.


Lionel Messi KUKAA MPAKA 2018 Barcelona

Lionel Messi amekubali kandarasi mpya katika klabu ya  Barcelona,ambao utamfanya kukaa klabuni hapo hadi  2018.

kijana huyu wa kimataifa  kutoka  Argentina mwenye miaka , 25,amepata mafanikio makubwa ikiwemo ya kuvunja takwimu ya mwaka  kwa kufunga magoli tisini kwa  Nchi yake kwa mwaka  2012. 

Aidha Mlinzi  Carles Puyol, 34, na Kiungo   Xavi Hernandez, 32, pia wamekubali kandarsi mpya na klabu hiyo ambapo watahudumu   Barcelona hadi  2016. 

"Majuma kadhaa yajayo , Puyol, Xavi na Messi watasaini kandarasi mpya aidha mchezaji huyo alivunja takwimu ya miaka Arobaini ya magoli 85 ya Gerd Mueller's katika ushindi wa mabao mawili kwa moja  2-1 Dhidi ya Real  Betis siku ya  9 December. 

 Messi aliongeza mabao mengine mawili katika ushindi wa Atletico Madrid 4-1.na kufikisha mbao 90 msimu  

 Vile vile ni moja ya kati ya wachezaji watatu ambao wamechaguliwa kuwania tuzo ya uchezaji bora wa dunia pamoja na  Cristiano Ronaldo na Andres Iniesta.

TWFA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA MOROGORO





Uchaguzi wa viongozi wapya wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) unafanyika kesho (Desemba 19 mwaka huu) kwenye hoteli ya Midlands mjini Morogoro.

Kamati ya Uchaguzi ya TWFA ikiongozwa na Mama Ombeni Zavala ndiyo itakayoendesha uchaguzi huo chini ya usimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Wagombea katika uchaguzi huo ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy wanaowania uenyekiti, Rose Kissiwa (mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (wanawania ukatibu mkuu).

Wengine ni Zena Chande (mgombea pekee wa nafasi ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya TWFA.



ROBO FAINALI KOMBE LA UHAI KUPIGWA KESHO




Robo Fainali za michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zitachezwa kesho (Desemba 19 mwaka huu) kwenye viwanja vya Karume na Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mtibwa Sugar itaumana na African Lyon kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume katika mechi itakayoanza saa 2 kamili asubuhi. Nazo Azam na JKT Ruvu zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 2 kamili asubuhi.
Mechi nyingine ya robo fainali itakuwa kati ya JKT Oljoro na Simba ambayo itachezwa kuanzia saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Coastal Union na Ruvu Shooting zitacheza kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni.
Nusu fainali ya michuano hiyo itachezwa Ijumaa ya Desemba 21 mwaka huu Uwanja wa Chamazi, wakati fainali na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu zitapigwa Jumapili ya Desemba 23 mwaka huu Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

Chipolopolo KUTUA KESHO, UKITAKA KUIONA 5000


Mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) wakiwa na msafara wa watu 32 wanatarajia kuwasili nchini kesho (Desemba 19 mwaka huu). Timu hiyo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11 kamili jioni kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Lusaka.

Mbali ya wachezaji 24, msafara wa Zambia ambayo inakuja nchini kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars utakuwa na maofisa wengine wanane wakiwemo wa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Herve Renard aliyeipa timu hiyo ubingwa wa Afrika mwaka jana nchini Gabon.
Wachezaji kwenye msafara huo ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
Mechi dhidi ya Taifa Stars itafanyika Jumamosi (Desemba 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Dar es Salaam tangu Desemba 12 mwaka huu chini ya Kocha Kim Poulsen kujiandaa kwa mechi hiyo.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tiketi zinatarajiwa kuanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Uhuru, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio na Samora, Sokoni Kariakoo, kituo cha mafuta cha Ubungo OilCom na Dar Live Mbagala.
Pia tiketi zitauzwa Ijumaa (Desemba 21 mwaka huu) kwenye tamasha la Kilimanjaro Premium Lager kuhamasisha washabiki wa Taifa Stars litakalofanyika kwenye viwanja vya Sigara, Chang’ombe.

FRANSIS CHEKA VS Chiotra Chimwemwe


Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) tayari imemtafutia bondia Francis Cheka mpambano wa marudiano kati yake na bondia Chiotra Chimwemwe wa Malawi katika jiji la Addis Ababa, Ehtiopia.

Mpambano huo utafayika January 26, siku ya ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa nchi za Africa (AU Summit) katika jiji hilo la Wafalme la Abesinia!

Cheka na Chimwemwe watakutana jijini Arusha Desemba 26 (Boxing Day) katika mpambano wa kutafuta nani mbabe wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG). Katika mpambano huo mafahali hawa wawili wataumana kiume kwa raundi 12 za dakika tatu kila mmoja!

Mpambano wa Cheka na Chimwemwe jijini Arusha umeandaliwa na kampuni ya Screen Hills (T) Investment ya jijini Dar-Es-Salaam inayomilikiwa na promota maarufu aliyewahi kuwa bingwa wa taifa katika ngumi za ridhaa na kulipwa Andrew George aka Chagga Boy!

Umaarufu wa wawili hawa umewafanya mapromota wanaoandaa tamasha la kuchangisha pesa kwa ajili ya kulisha watu wenye njaa katika bara la Africa kuwaingiza Cheka 26(15)-6(3)-1 na Chiotra 26(15)-4(2)-1 katika mpambano hwa marudiano utakaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 26 Januaru 2012!

Katika tamasha hilo, pambano kuu litakuwa kati ya bondia Oliver McCall 56(37)-12(1)-0 kutoka Marekani ambaye aliwahi kuwa bingwa wa uzito wa juu duniani akipambana na bondia Sammy Retta - 18(17)-3(2)-0 kutoka Ethiopia kugombea ubingwa wa IBF Africa, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa juu (Heavyweight)

Mapambano mengine yatawakutanisha mabondia Daniel Wanyonyi 14(12)-5(2)-2 wa Kenya atakayechuana na bondia Issac Hlatswayo 30(10)-5(3)-1 kutoka Afrika ya Kusini katika kugombea ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Welterweight

Naye Manzur Ali 7(4)-8(3)-0 bingwa wa uzito wa juu kutoka nchi ya Misri atachuana vikali na bondia Harry Simon 27(20)-0-0 kutoka Namibia ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Light heavyweight.

Mpambano huu umeidhinishwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na Cheka kupewa kibali na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC)

Mohamed Bin Hammam JELA MAISHA


Mohamed Bin Hammam, Moja kati  ya wagombea Urais katika chama cha soka kinachosimamia mpira ulimwengu FIFA ambaye alihusika katika tuhuma za Rushwa na kujiuzulu katika nafasi zote alizokuwa akishilia amepigwa marafuku kabisa kuto kujihusisha na mchezo wa soka katika maisha yote ya ulimwengu  

Hammam ambaye ana miaka 63- alikuwa mkuu wa  chama cha soka cha asia alituhumiwa kutumia rushwa kumuondoa madarakani  Rais wa sasa wa fifa Sep  BLATTER katika uchaguzi mkuu  uliofanyika mwaka jana.
Adhabu ilifutwa na mahakama ya usuluhishi wa mchezo july mwaka jana lakini Fifa  imetoa adhabu nyingine ya Kumfungia maisha na hatoruhisiwa tena kuongoza shuguhuri za soka Duniani 


EUROPA LIGI: DROO RAUNDI YA TIMU 32 ALHAMISI!

EUROPA_LIGI_CUP
>>MABINGWA wa ULAYA Chelsea kujua Mpinzani wao wa EUROPA LIGI!!
Droo ya kupanga Mechi za Mtoano za Raundi ya Timu 32 za EUROPA LIGI itafanyika Alhamisi Desemba 20 mara tu baada ya kukamilika kwa Droo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na zitakuwemo Timu 24 zilizotoka Makundi ya EUROPA LIGI na kujumuishwa na Timu 8 toka UEFA CHAMPIONZ LIGI ambazo zilimaliza nafasi ya 3 toka Makundi yao na moja ya hizo ni Mabingwa wa Ulaya, Chelsea.

KLABU 24 ZILIZOFUZU TOKA EUROPA LIGI:
Olympique Lyonnais
FC Rubin Kazan
FC Internazionale Milano
Hannover 96
Bayer 04 Leverkusen
FC Metalist Kharkiv
FC Anji Makhachkala
Fenerbahçe SK
VfL Borussia Mönchengladbach
AC Sparta Praha
S.S. Lazio
Club Atlético de Madrid
FC Viktoria Plzeň
Levante UD
KRC Genk
FC Dnipro Dnipropetrovsk
SSC Napoli
Newcastle United FC
FC Girondins de Bordeaux
Steaua Bucharest
Stuttgart
Liverpool
Tottenham
FC Basel

8 TOKA UEFA CHAMPIONZ LIGI:
[Timu zilizomaliza Nafasi ya 3 kwenye Makundi]
-Dynamo Kiev
-Olympiacos
-Zenit St Petersburg
-Ajax Amsterdam
-Chelsea
-BATE Borisov
-Benfica
-CFR Cluj-Napoca

Klabu 12 zilizomaliza EUROPA LIGI zikiwa Vinara wa Makundi yao pamoja na 4 toka UEFA CHAMPIONZ LIGI ambazo zipo juu kwenye Listi ya Ubora zitakuwa Chungu Namba 1 na 12 zilizomaliza nafasi ya Makundi ya EUROPA LIGI zikiwa Nafasi ya Pili pamoja na 4 zilizobaki kati ya 8 toka UEFA CHAMPIONZ LIGI zitawekwa Chungu Namba 2.

RAUNDI YA MTOANO TIMU 32:
CHUNGU NAMBA 1
-Liverpool FC
-FC Viktoria Plzeň
-Fenerbahçe SK
-FC Girondins de Bordeaux-
-FC Steaua Bucureşti
-FC Dnipro Dnipropetrovsk
-KRC Genk, FC Rubin Kazan
-Olympique Lyonnais
-S.S. Lazio
-FC Metalist Kharkiv
-Hannover 96
-Chelsea FC [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
-CFR 1907 Cluj [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
-Olympiacos FC [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
SL Benfica [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
CHUNGU NAMBA 2
-FC Anji Makhachkala
-Club Atlético de Madrid
-VfL Borussia Mönchengladbach
-Newcastle United FC
-VfB Stuttgart
-SSC Napoli
-FC Basel 1893
-FC Internazionale Milano
-AC Sparta Praha
-Tottenham Hotspur FC
-Bayer 04 Leverkusen
-Levante UD
-FC Dynamo Kyiv [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
-FC Zenit St Petersburg [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
-AFC Ajax [UEFA CHAMPIONZ LIGI]
-FC BATE Borisov [UEFA CHAMPIONZ LIGI]

Mechi zitapangwa kwa kutoa Jina moja toka Chungu Namba 1 na jingine toka Chungu Namba mbili ila Timu zilizokuwa Kundi moja ama zinazotoka Nchi moja haziwezi kukutanishwa.
Mara baada ya Droo ya Timu 32, Siku hiyo hiyo Alhamisi, itafuata Droo ya ile ya Raundi inayofuata, Raundi ya Timu 16, ambayo itakuwa haina ubaguzi na Timu yeyote inaweza kukutana na mwingine yeyote bila kujali hata Nchi.
RATIBA HATUA YA MTOANO
RAUNDI YA TIMU 32:
Mechi ya 1=14 Februari 2013 
Mechi ya 1=21 Februari 2013
RAUNDI YA TIMU 16:
Mechi ya 1=7 Machi 2013
Mechi ya 2=14 Machi 2013
ROBO FAINALI:
Mechi ya 1=4 Aprili 2013
Mechi ya 2=11 Aprili 2013
NUSU FAINALI
Mechi ya 1=25 Aprili 2013
Mechi ya 2=2 Mei 2013
FAINALI
15 Mei 2013
UWANJA wa AMSTERDAM ARENA
 

BPL: WASHIKA MITUTU WA JIJI LA EMIRATES ARSENAL JANA WALIWAADHIBU READING BAO 5 CAZORLA ATUPIA TATU PEKEE!

>>SANTI CAZORLA HETITRIKI!
>>FELLAINI JELA, KUZIKOSA WEST HAM, WIGAN & CHELSEA
BPL_LOGOSanti Cazorla amepiga hetitriki na kuisaidia Arsenal kukamata nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England walipowatandika Timu ya Mkiani Reading 5-2 wakiwa kwao Uwanja wa Madejski Jumatatu Usiku.
Arsenal walitangulia 4-0 mbele baada ya Lukas Podolski kufungua magoli na Santi Cazorla kupiga 3 lakini Reading wakapata Bao mbili kupitia Adam Le Fondre na Jimmy Kebe na kuifanya gemu iwe 4-2.
Hata hivyo, Theo Walcott, aliekuwa akicheza kama Sentafowadi kama mwenyewe anavyong'ang'ania awekwe nafasi hiyo akapiga Bao la 5 kwa Arsenal na kuwadidimiza Reading mkiani ambako wapo Pointi 6 toka kwenye nafasi ya usalama.
Hii ilikuwa ni Mechi muhimu mno kwa Arsenal kushinda hasa baada ya Wiki iliyopita kubwagwa nje ya CAPITAL ONE CUP na Timu ya Daraja la chini Bradford na kuleta mfarakano kwa Wadau wao.

MAGOLI:
Reading 2
-Le Fondre Dakika ya 66
-Kebe 71
Arsenal 5
-Podolski Dakika ya 14
-Cazorla 32, 34 & 60
-Walcott 80

Mara ya mwisho Timu hizi kucheza ilikuwa Uwanja huu huu wa Madejski na Arsenal kushinda Bao 7-5 kwenye Mechi ya CAPITAL ONE CUP.
VIKOSI:
Reading: Federici, Cummings, Gorkss, Mariappa, Shorey, McAnuff, Leigertwood, Tabb, Kebe, Hunt, Pogrebnyak
Akiba: Taylor, Gunter, Pearce, Le Fondre, McCleary, Robson-Kanu, Harte.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs, Arteta, Wilshere, Cazorla, Oxlade-Chamberlain, Walcott, Podolski
Akiba: Mannone, Koscielny, Rosicky, Giroud, Ramsey, Coquelin, Gervinho.
Refa: Anthony Taylor
>>FELLAINI KUZIKOSA West Ham United, Wigan Athletic & Chelsea
Mchezaji wa Everton, Marouane Fellaini, amefungiwa Mechi 3 baada ya kukiri kosa la kumtwanga kichwa Beki wa Stoke City Ryan Shawcross wakati Timu zao zilipocheza Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Brittania Jumamosi iliyopita.
Tukio hili halikuonwa na Refa Mark Halsey lakini lilinaswa kwenye Kamera na FA, Chama cha Soka England, kiliamua kumfungulia Mashitaka.
Lakini, mara baada ya Mechi hiyo Fellaini aliomba radhi kuhusu kosa lake.
Fellaini atazikosa Mechi za Everton za Ligi dhidi ya West Ham United, Wigan Athletic na Chelsea, na atarejea tena Uwanjani Januari 2 wakati Everton watakaposafiri kwenda St James Park kucheza na Newcastle.

MSIMAMO:
[Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi]
1 Man United Mechi 17 Pointi 42
2 Man City Mechi 17 Pointi 36
3 Chelsea Mechi 16 Pointi 29 [Tofauti ya Magoli 11]
4 Tottenham Mechi 17 Pointi 29 [Tofauti ya Magoli 5]

5 Arsenal Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 13]
6 Everton Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 7]
7 WBA Mechi 17 Pointi 27 [Tofauti ya Magoli 3]
8 Norwich Mechi 17 Pointi 25

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 22 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Wigan v Arsenal
[SAA 12 Jioni]
Man City v Reading
Newcastle v QPR
Southampton v Sunderland
Tottenham v Stoke
West Brom v Norwich
West Ham v Everton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Liverpool v Fulham
Jumapili 23 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea v Man United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Aston Villa

 
AKINA DIDIER,ANDREW AYEW ,YAYA TOURE WAPOKONYWA TUZO YA MCHAZAJI BORA AFRIKA NA  KATONGO NI MCHEZAJI BORA AFRIKA kwa BBC!!
KATONGO>>NI MARA YA KWANZA MCHEZAJI TOKA KUSINI MWA AFRIKA KUTWAA!!
Christopher Katongo, Nahodha wa Zambia anaecheza Soka lake huko China na Klabu ya Henan Construction, ndie ameshinda Tuzo ya BBC, Shirika la Utangazaji Uingereza, ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2012 baada ya kuwabwaga Demba Ba, Didier Drogba, Younes Belhanda na Yaya Toure.
Katongo, ambae Mwezi Februari aliiongoza Zambia kutwaa Ubingwa wa Afrika huko Nchini Gabon walipoitoa Ivory Coast kwenye Fainali, amepata Kura Asilimia 40 ya Kura zote.
+++++++++++++++++++++++++++++++++
WASHINDI WALIOPITA:
2011 - Andre 'Dede' Ayew (Marseille & Ghana)
2010 - Asamoah Gyan (Sunderland & Ghana)
2009 - Didier Drogba (Chelsea & Ivory Coast)
2008 - Mohamed Aboutrika (Al Ahly & Egypt)
2007 - Emmanuel Adebayor (Arsenal & Togo)
2006 - Michael Essien (Chelsea & Ghana)
2005 - Mohamed Barakat (Al Ahly & Egypt)
2004 - Jay Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2003 - Jay Jay Okocha (Bolton & Nigeria)
2002 - El Hadji Diouf (Liverpool & Senegal)
2001 - Sammy Kuffour (Bayern Munich & Ghana)
2000 - Patrick Mboma (Parma & Cameroon)
 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: DROO RAUNDI YA MTOANO TIMU 16 ALHAMISI!!

UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZ>>TATHMINI: KILA TIMU MPINZANI ANAWEZA KUWA NANI!!!
DROO YA KUPANGA MECHI ZA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16 itafanyika huko Nyon, Uswisi Alhamisi, Desemba 20, kuanzia Saa 7 na Nusu Mchana, Bongo Taimu, na Timu 16, zikijumuisha Timu 9 ambazo zishawahi kutwaa Ubingwa wa michuano hii, na moja, Malaga FC, wakiwa ni wapya kabisa, lakini pia, kwa mara ya kwanza kabisa aliekuwa Bingwa mtetezi hatakuwemo baada ya Chelsea kushindwa kwenye Makundi.
+++++++++++++++++++
TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA Raundi ya Mtoano ya Timu 16:
WASHINDI wa MAKUNDI:
Paris St Germain
Schalke 04
Malaga
Borussia Dortmund
Juventus
Bayern Munich
Barcelona
Manchester United
WASHINDI wa PILI wa MAKUNDI:
Porto
Arsenal
AC Milan
Real Madrid
Valencia
Shakhtar Donetsk
Galatasaray
Celtic

Kwa mujibu wa Kanuni za UEFA za Droo ya upangaji Ratiba ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16, zile Timu ambazo zimekuwa Washindi wa Makundi watawekwa Kapu Namba 1 na wale waliomaliza Nafasi ya Pili kwenye Makundi wapo Kapu Namba 2.
Droo itafanywa kwa kutoa Jina moja toka Kapu Namba 2 na kufuatia Jina jingine toka Kapu Namba 1 na Timu hizo ndizo zitakazokutana isipokuwa Timu zinazotoka Nchi moja na zile zilizokuwa Kundi moja haziwezi kupambanishwa.
Pia, Mechi za kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 zitachezwa nyumbani kwa Timu itakayotoka Kapu Namba 2, Timu zilizomaliza Nafasi ya Pili, na marudiano ni nyumbani kwa Washindi wa Makundi.
IFUATAYO NDIO TATHMINI YA KILA TIMU na TIMU ZIPI ZINAWEZA KUWA WAPINZANI:
WASHINDI wa MAKUNDI
A: PARIS SAINT-GERMAIN FC (FRANCE)
MPINZANI ANAWEZA KUWA: Arsenal, Milan, Madrid, Shakhtar, Valencia, Celtic, Galatasaray
B: FC SCHALKE 04 (GERMANY)
MPINZANI: Porto, Milan, Madrid, Shakhtar, Valencia, Celtic, Galatasaray
C: MÁLAGA CF (SPAIN)
MPINZANI: Porto, Arsenal, Shakhtar, Celtic, Galatasaray
D: BORUSSIA DORTMUND (GERMANY)
MPINZANI: Porto, Arsenal, Milan, Shakhtar, Valencia, Celtic, Galatasaray
E: JUVENTUS (ITA)
MPINZANI: Porto, Arsenal, Madrid, Valencia, Celtic, Galatasaray
F: FC BAYERN MÜNCHEN (GERMANY)
MPINZANI: Porto, Arsenal, Milan, Madrid, Shakhtar, Celtic, Galatasaray
G: FC BARCELONA (SPAIN)
MPINZANI: Porto, Arsenal, Milan, Shakhtar, Galatasaray
H: MANCHESTER UNITED FC (ENG)
MPINZANI: Porto, Milan, Madrid, Shakhtar, Valencia, Celtic

WASHINDI wa PILI:
A: FC Porto (PORTUGAL)
MPINZANI: Schalke, Málaga, Dortmund, Juventus, Bayern, Barcelona, Manchester United
B: Arsenal FC (ENGLAND)
MPINZANI: PSG, Málaga, Dortmund, Juventus, Bayern, Barcelona
C: AC Milan (ITALY)
MPINZANI: PSG, Schalke, Dortmund, Bayern, Barcelona, Manchester United
D: Real Madrid CF (SPAIN)
MPINZANI: PSG, Schalke, Juventus, Bayern, Manchester United
E: FC Shakhtar Donetsk (UKRAINE)
MPINZANI: PSG, Schalke, Málaga, Dortmund, Bayern, Barcelona, Manchester United
F: Valencia CF (SPAIN)
MPINZANI: PSG, Schalke, Dortmund, Juventus, Manchester United
G: Celtic FC (SCO)
MPINZANI: PSG, Schalke, Málaga, Dortmund, Juventus, Bayern, Manchester United
H: Galatasaray AŞ (TURKEY)
MPINZANI: PSG, Schalke, Málaga, Dortmund, Juventus, Bayern, Barcelona
 

UGIRIKI: KLABU MOJA MDHAMINI DANGURO LA MAKAHABA, NYINGINE ‘MWOSHA MAITI’!!

MDHAMINI-DANGURO_LA_MAKAHABAKlabu moja, Voukefalas FC, ina Jezi safi, zinazomeremeta za Pinki zenye maneno mgongoni "Villa Erotica", nyingine, Palaiopyrgos FC, ina Jezi Nyeusi bomba zenye alama ya Msalaba, zote hizo zikiwa ni Nembo za Wadhamini wao, "Villa Erotica" likiwa ni Danguro la Makahaba na ile yenye Msalaba Mdhamini ni Duka la ‘Kuosha Maiti’, watayarishaji Marehemu kabla hawajazikwa.
Klabu ya Voukefalas FC inatoka Mji wa Larissa huko Ugiriki na ilikuwa ikiyumba sana kwa kukosa udhamini lakini akajitokeza Madam Soula Alevridou ambae ni Mmiliki wa Danguro la Makahaba, ambako huko Ugiriki ni halali, kuidhamini na kuiokoa Voukefalas FC.
Madam Soula Alevridou amesema Biashara yake ni halali na hamna kosa kudhamini Timu kwa vile inahitaji msaada.
Hata hivyo, Jezi hizo zimezua upinzani mkubwa ikidaiwa mambo ya ngono yasihusishwe na michezo.MDHAMINI-MWOSHA_MAITI
Wakati huko Larissa mambo ni hayo, katika Mji jirani wake uitwao Trikala, Viongozi wa Soka wako kwenye mtihani mkubwa baada ya moja ya Timu ya Mji huo, Palaiopyrgos FC, ambayo hucheza Soka la Ridhaa, kujikwamua Kiuchumi baada ya kupata Udhamini wa Duka dogo linaloshughulika na utayarishaji wa Miili ya Marehemu kabla kuzikwa, kikwetu ‘Waosha Maiti’ [Undertakers] na Timu hiyo huvaa Jezi Nyeusi zenye Msalaba.
Mmiliki wa Duka hilo, Christos Panagiotou, amesema wazo la kuidhamini Timu hiyo ya Mjini kwake lilikuja wakati wakigida Pombe na Marafiki zake.
Christos Panagiotou amesema awali Watu walishtuka na Wapinzani Uwanjani kuiogopa Timu hiyo lakini sasa wameanza kuzoea.
Lakini kama ilivyokuwa huko Larissa, hata hapo Mjini Trikala kumezuka upinzani mkali kutaka Klabu ya Palaiopyrgos isidhaminiwe na hilo Duka la Maiti kwa misingi kuwa kitendo hicho ni udhalilishaji wa Binadamu na pia si kitendo cha busara kwa Michezo kuhusishwa na tendo kubwa la utu.
Hadi sasa hamna maamuzi yaliyotolewa dhidi ya Klabu hizo mbili.