Thursday, October 25, 2012

BIN KLEB AWAWAKIA WACHEZAJI WACHOYO WA PASI YANGA, KIIZA AFICHUA MGAWANYIKO KATIKA TIMU

Kiiza 

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb jana ‘aliwawakia’ wachezaji wa mbele wa timu hiyo kwa uchoyo wa pasi na kukemea tabia inayoonekana kuanza kujitokeza, wachezaji wa timu hiyo kutopendana.
Bin Kleb aliingia ‘kwa hasira’ chumba cha kubadilishia nguo cha Yanga na kuanza kufoka juu ya tabia hiyo, akisema timu inatengeneza nafasi nyingi, lakini kwa uchoyo wa baadhi ya wachezaji kutoa pasi kwa wenzao walio kwenye nafasi nzuri zaidi, inaambulia mabao machache.
Bosi huyo alifanya hivyo baada ya mechi dhidi ya Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambayo Yanga ilishinda 3-0.
Lakini pia Bin Kleb alimuuliza kocha Mkuu, Mholanzi Ernie Brandts kwa nini timu haichezi vizuri pamoja na kushinda. Brandts alitumia hekima kukwepa kujibu swali mbele ya wachezaji, lakini baadaye alimvuta pembeni Bin Kleb wakazungumza.
Tayari kuna dalili za mgawanyiko ndani ya Yanga baina ya wachezaji na hilo lilijidhihirisha wakati Hamisi Kiiza alipofunga bao lake lililokuwa la tatu katika ushindi wa 3-0, hakwenda kushangilia na wachezaji wenzake, bali alimkimbilia kipa wa akiba, Mghana Yawe Berko kushangilia naye jana.
Ingawa hajawahi kulalamika, lakini ukiifuatailia Yanga tangu baada ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, Kiiza ndiye ambaye mara nyingi amekuwa hapewi pasi na wenzake anapokuwa kwenye nafasi nzuri, ingawa yeye amekuwa anawapa tu wenzake pasi za mabao.
Pamoja na hayo, hali hiyo inaonekana kidogo kuathiri uchezaji wa Kiiza, anayeonekana kuwa mnyonge na asiye na raha uwanjani na haikushangaza alipotolewa nje kipindi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Simba, Oktoba 3, mwaka huu.
Lakini Kiiza amekuwa akicheza kwa kiwango cha juu mno katika timu yake ya taifa, Uganda, The Cranes pamoja na ‘kusuasua’ Yanga.  

NYOSSO AKISANUA SIMBA SC, BOBAN AAMUA KUTULIA, NGASSA, KAZIMOTO WATAZAMWA KWA JICHI LA TATU

Juma Nyosso

SIMBA SC imekubali kuvunja mkataba na beki wake Juma Said Nyosso kulingana na maombi yake, na imemtaka afike kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe kujadili suala hilo.
Habari za ndani kutoka Simba SC, zimesema kwamba Nyosso amewasilisha maombi ya kuvunja mkataba na klabu hiyo, baada ya kushushwa kikosi cha pili, akidaiwa kiwango chake kimeshuka hivyo amepewa fursa ya kwenda kukiboresha.
Lakini Nyosso mwenyewe ameona kama hastahili kushushwa timu ya pili na ameomba asitishiwe mkataba wake aondoke, jambo ambalo uongozi wa klabu umelikubali.
Nyosso si kama anatuhumiwa kuhujumu timu, bali anaambiwa uwezo wake umeshuka mno na kwamba amekuwa akiigharimu timu katika siku za karibuni, hivyo amepewa fursa ya kwenda kupandisha kiwango chake.
Adhabu kama hii amewahi kupewa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Carlos Tevez katika klabu ya Manchester City ya England msimu uliopita na aliitumikia vizuri hadi aliporejeshwa tena kikosi cha kwanza, ambako aliisaidia timu kumalizia msimu vizuri kwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu.   
Mbali na Nyosso, kiungo Haruna Moshi Shaaban amesimamishwa kwa wiki tatu kwa tuhuma za utovu wa nidhamu na katika kipindi hicho atakuwa akipokea nusu mshahara.
Boban ameamua kurudi nyumbani kwake kupumzika na mkewe hadi adhabu hiyo iishe ajue mustakabali wake, ila amesema anaonewa kwa sababu hakupewa nafasi ya kujibu tuhuma zake kabla ya hatua kuchukuliwa, ingawa amechukulia poa tu.
Wakati huo huo, habari zaidi kutoka ndani ya Simba, zimesema kwamba Mwinyi Kazimoto Mwitula, Ramadhan Suleiman Chombo na Mrisho Khalfan Ngassa nao wanaangaliwa kwa ‘jicho la tatu’ juu ya mwenendo wao kwenye timu hiyo na kwa nyakati tofauti wote wamekwishaitwa kuhojiwa masuala mbalimbali.   

TAIFA CUP KIKAPU OKTOBA 29 TANGA, WAMAREKANI WAJA KUFUNDISHA TIMU ZA TAIFA

Magesa

MASHINDANO ya mpira wa Kikapu ya kombe la Taifa, yanatarajiwa kufanyika mjini Tanga kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 4, mwaka huu.
Makamu wa rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa  amesema  leo kwamba, mashindano haya ya Kombe la Taifa kwa kawaida ndio hutumika kuchagua timu zetu za Taifa, hvyo ni muhimu kwa mikoa yote kushiriki ili kuwapa nafasi wanamichezo kutoka mikoa yao kuonekana katika ngazi ya Taifa.
Ameitaja mikoa iliyothibitisha hadi sasa ni Iringa, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Singida, Mara, Dodoma, Pemba, Unguja, Tanga, Mtwara, Lindi na Dar Es Salaam.
“Bado nafasi ya kuthibitisha kushiriki ipo kwa wanaopenda kushiriki katika mashindano haya na ratiba ya mashindano itapangwa tarehe 28/10/2012 katika kikao ambacho wawakilishi wa mikoa yote lazima wawepo na ndo itakuwa mwisho wa kuthibitisha kushiriki,”alisema.
Akizungumzia makocha wa timu yaifa kutoka Marekani, Magesa alisema Kocha Mkuu atakuwa Albert Sokaitis mwenye uzoefu wa miaka 24, ambaye kwa sasa anafundisha timu ya Chuo Kikuu cha Post, Marekani katika jimbo la Connecticut, ambaye pia amewahi kufundisha timu na kuendesha mafunzo nchi za Uchina, Lebanon, Ugiriki na Japan.
Amesema Sokaitis atasaidiwa na Jocquis L. Sconiers mwenye uzoefu wa miaka mingi, ambaye kwa sasa ni Kocha Msaidizi wa timu ya Chuo Kikuu cha Post huko Marekani katika jimbo la Connecticut.
“Walimu wote hawa wana shahada za juu kutoka vyuo vikuu  mbali mbali vya Marekani na katika utekelezaji wa mpango huo katika awamu ya kwanza Kocha Sconiers anatarajiwa kuwasili nchini  Oktoba 30 na ataelekea Tanga siku inayofuata katika Kombe la Taifa ili kuchagua wachezaji wa timu za taifa (wanawake na wanaume) na baada ya hapo ataanza kazi rasmi kwa timu zote Novemba 5,”alisema.
Alisema awamu hii ya kwanza ya mpango wa mafunzo unadhaminiwa na watu wa Marekani kupitia ubalozi wao hapa Tanzania na kwamba wanawashukuru kwa msaada huo.
Aidha, Magesa alisema kama mipango yote ikienda vizuri, wanatarajia kuwa wenyeji wa mashindano ya kanda ya Tano ya FIBA, yanayotarajiwa kufanyika mjini Dar es Salaam kuanzia Desemba 15 hadi 22, mwaka huu.
“Hivyo basi Kocha huyo atatumia nafasi hii kuanza maandalizi ya timu zetu za Taifa kuziandaa kwa mashindano haya yanayotarajiwa kushirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Misri Sudan na Sudani ya kusini,”alisema.
Kuhusu Mkutano Mkuu wa TBF, alisema wanatarajia utafanyika Novemba 1 hadi 2, mwaka huu na amewataka viongozi wote wa Mikoa na wawakilishi wachezaji, vyama shiriki kushiriki bila kukosa katika mkutano huu utakaofanyika Tanga.

 RHINO RANGERS WAANZA VYEMA MASHINDANO  YA LIGI DARAJA LA KWANZA  KWA KUMTANDIKA MPINZANI WAKE BAO 2-1 HIYO JANA

 Michuano ya daraja la kwanza ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu hapa nchini ilifunguliwa rasmi hiyo jna na katika matokeo ya mechi ya rhino rangers na polisi tabora zote za tabora na timu ya  rhino rangers ilionyesha imejipanga vyema katika mashindano hayo baada ya kuifunga polisi tabora mabao mawili kwa moja 2-1 katika dimba la ally hassan mwinyi.

Na katika mchezo huo mabao ya rhino rangers yalifungwa na victor hangaya dakika ya 17 ya kimchezo na bao la pili lilifungwa na Abdalah simba dakika ya 68 ya kimchezo na bao la kufutia machozi kwa upande wa polisi lilifungwa na Iddy kibwana dk ya 90 ya kimchezo.

Na mashindano hayo yataendelea tena hapa mkoani tabora siku ya tarehe 27 ,10,mwaka huu kwa mchezo kati ya polisi tabora na polisi dodoma katika dimba la ally hassan mwinyi na pamba dhidi ya mwanza dhidi ya rhino rangers ya hapa mkoani tabora.

Mechi hiyo ilichezeshwa na refa kutoka kigoma richard kienze akisaidiwa na martin walaje na shabani masanda wa hapa mkoani tabora na refaree wa akiba alikuwa maulid mwikalo na fourthofficial alikuwa ni ramadhani jingi.

Na katika kundi c la michuano hiyo timu zinazoshiriki ni 1.kanembwe fc

2.polisi dodoma,3.mwadui fc,4.moran fc,5.polisi tabora,6.polisi mara,7.rhino rangers,8.pamba fc

MKUTANO MKUU TASWA MWEZI UJAO

Amir Mhando
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA),k imefikia hatua ya mwisho ya mazungumzo na mdhamini wa Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao katika tarehe ambayo itatangazwa rasmi.
Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando  amesema  leo kwamba, Kamati ya Utendaji ya TASWA ilikubaliana katika kikao chake mwezi uliopita kuwa Mkutano Mkuu wa TASWA mwaka huu uwe wa aina yake kwa kuwawezesha wanachama kukaa pamoja na kubadilishana mawazo na ikashauri ikiwezekana ufanyike nje ya Dar es Salaam kama hali itaruhusu.
Amesema kutokana na hali hiyo, kikao kiliiagiza sekretarieti ya TASWA itafute mdhamini wa kufanikisha suala hilo na kwamba kama ikishindikana mkoani ifanyike Dar es Salaam lakini kuwe na mdhamini.
Amesema tayari hilo limefanyika na mdhamini amepatikana, ambapo hatua ya mwisho ya mazungumzo na mdhamini itakuwa mapema wiki ijayo  na baada ya hapo itatangazwa tarehe rasmi.
“Nichukue nafasi hii kuwaomba wanachama ambao hawajalipa ada zao wafanye hivyo kwa kuwasiliana na Mhazini wa chama au Mhazini Msaidizi ili waepuke usumbufu wa kushindwa kuhudhuria mkutano huo,”alisema Mhando.
Wakati huo huo: TASWA imempongeza mwanachama wake, Boniface Wambura kwa kuteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (CAF) kuwa mmoja wa maofisa watakaoshughulikia masuala ya habari wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea.
Mhando amesema TASWA imepokea kwa furaha uteuzi huo wa Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na inaamini ataendelea kufanya vizuri kama anavyotekeleza majukumu yake ya kazi ndani ya TFF.
“Tangu Wambura aanze kazi ya Ofisa Habari wa TFF kumekuwa na mapinduzi makubwa yanayohusiana na mambo ya habari na katika hili waandishi wa habari za michezo nchini ni mashahidi wa hilo kwani amekuwa mtu sahihi kwao na amekuwa na ushirikiano mkubwa usio na kifani kwa wanahabari wenzake,”alisema.
Mhando amesema kwa kuwa Wambura ni mwanachama hai wa TASWA, kwa kuteuliwa kwake huko ni faraja kwa chama na tunamtakia kila la heri ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake kwani hiyo ni ishara tosha kwamba kazi yake inaonekana na inathamanika.
Wambura ameteuliwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa fainali hizo za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zilizopangwa kuanza Oktoba 28, 2012 na kumalizika Novemba 11, 2012, ambapo atakuwa mmoja wa maofisa watatu watakaoshughulikia habari kwenye fainali hizo. Wengine ni ofisa kutoka makao makuu ya CAF, Mahmoud Garga na Arlindo Macedo kutoka Angola.

YANGA WAENDA ARUSHA ALFAJIRI YA LEO

Tegete akishangilia na Kavumbangu

YANGA SC imeondoka leo alfajiri Dar es Salaam na kikosi cha wachezaji 20 kwenda Arusha kwa ajili ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya wenyeji JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Wachezaji waliokwenda Arusha leo ni makipa Yaw Berko, Ally Mustafa ‘Barhez’, mabeki, Oscar Joshua, Juma Abdul, David Luhende, Stefano Mwasyika, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Nahodha), Mbuyu Twite na Kelvin Yonda.
Viungo ni Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Nurdin Bakari, Nizar Khalfan, Juma Seif ‘Kijiko’ na washambuliaji Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Didier Kavumbangu.
Yanga inakimbilia Arusha mapema ili kuwahia kuzoea hali ya hewa ya huko, wasije kupata tabu katika mchezo wa Jumamosi.
Mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu, wanakwenda Arusha wakitoka kuendeleza wimbi la ushindi jana katika Ligi Kuu, baada ya kuichapa Polisi Morogoro mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Yanga itimize pointi 17, baada ya kucheza mechi tisa na kuendelea kusimama katika nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye pointi 18, baada ya sare ya 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.  
Hadi mapumziko jana, Yanga walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na washambuliaji Simon Msuva na Didier Kavumbangu.
Msuva alikuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wa Yanga dakika ya tano kabla ya dakika moja baadaye, Mrundi Kavumbangu naye kuwapa raha mashabiki wa timu hiyo.
Yanga ingekwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0 kama mkwaju wa penalti wa Haruna Niyonzima usingegonga mwamba na kurudi uwanjani kabla ya mabeki wa Polisi kuondosha kwenye hatari.
Refa Alex Mahagi kutoka Mwanza alitoa penalti hiyo, baada ya Msuva kuangushwa na beki John Bosco kwenye eneo la hatari wakati anakwenda kufunga.    
Kipindi cha pili Yanga walirudi kwa kasi tena na kuendelea kulishambulia lango la Polisi, ingawa walipoteza nafasi nyingi na kutumia moja tu, dakika ya 58, mfungaji Hamisi Kiiza aliyeingia kuchukua nafasi ya Jerry Tegete.
Matokeo ya jana yanaziweka karibu mno, Simba inayoongoza kwa pointi zake 19 baada ya kucheza mechi tisa, Azam na Yanga pale juu, kiasi kwamba ushindani na uhondo wa ligi hiyo unaongezeka.

YUSSUF BAKHRESA WA AZAM AENDA HIJJA

Yussuf Bakhresa

WAKALA wa wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Yussuf Said Salim Bakhresa yupo, Makka, Saudi Arabia kwa ajili ya kufanya ibada ya Hijja kesho.
Yussuf ambaye ni mtoto wa bilionea, Said Salim Bakhresa, mmiliki wa Azam FC, moja ya timu tishio katika Ligi Kuu nchini, anakuwa miongoni mwa vijana wachache wa Kitanzania waliothubutu kutekeleza nguzo hiyo ya tano ya Uislamu katika umri wa ujana.
Alhaj huyo mtarajiwa anakuwa kiongozi wa pili kijana katika msafara wa Watanzania waliokwenda mwaka huu Hijja, baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Mehboob Manji.
Yussuf Bakhresa pamoja na kuwa mtu muhimu katika ustawi wa Azam, lakini pia amekuwa mfano wa mawakala wa wachezaji hapa Tanzania waliofanya juhudi za makusudi kujaribu kuwatafutia timu Ulaya wachezaji nchini.
Amewahi kumpeleka Mrisho Ngassa katika klabu ya West Ham United ya England ambako pamoja na kufuzu majaribio, akarudishwa Afrika ‘kuongeza lishe’. Amewahi kumpeleka John Bocco ‘Adebayor’ Israel ambako pia alikubalika mno.
Yussuf pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bakhresa Food Products Limited ingawa pia ni Mkurugenzi wa makampuni mengine yote ya Bakhresa, chini ya Mwenyekiti, baba yao, Said Salim Awadh Bakhresa.
Wakurugenzi wengine wa Bakhresa Group Of Companies ni Mohamed, Abubakar na Omar. Mohamed ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bakhresa Grain Milling (Uganda) na Mkurugenzi Mkuu wa Said Salim Bakhresa & Company Limited, wakati Omar ni Mkurugenzi Mtendaji Said Salim Bakhresa & Co Ltd na Abubakar Mkurugenzi Mkuu wa  Bakhresa Grain Milling (Malawi) na Bakhresa Grain Milling (Msumbiji) Limitad.
Lakini pia Abubakar ni Mkurugenzi Mtendaji wa Said Salim Bakhresa & Co. Ltd na wote ni Wakurugenzi wa bodi ya Azam FC chini ya Mwenyekiti, mzee Said Salim Awadh Bakhresa.

AFCON 2013: MAKUNDI tayari, UFUNGUZI: Bafana v Cape Verde!

WALE WABABE wa Cameroun, Kisiwa kidogo cha Cape Verde, ambao wanacheza Fainali yao ya kwanza kabisa ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, wamepangwa Kundi moja na Wenyeji Afrika Kusini katika Droo iliyofanyika jana na wao ndio watafungua dimba Mashindano hayo kwa Mechi rasmi ya ufunguzi dhidi ya Afrika Kusini hapo Januari 19, 2013, ndani ya Soccer City, Soweto, Johannesburg.
Mabingwa watetezi Zambia wamepangwa Kundi moja na Timu ngumu Nigeria katika Kundi C pamoja na Ethiopia na Burkina Faso.
Vigogo wengine Ghana wamepangwa pamoja na Congo DR, Niger na Mali katika Kundi B.
++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
++++++++++++++++++
MABINGWA AFRIKA:
-2012: Zambia
-2010: Egypt
-2008: Egypt
-2006: Egypt
-2004: Tunisia
-2002: Cameroon
-2000: Cameroon
++++++++++++++++++
AFCON 2013 itachezwa Afrika Kusini kuanzia Januari 19 hadi Februari 10 kwenye Viwanja ambavyo vilitumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 zilizochezwa Nchini humo.
Viwanja hivyo ni pamoja na FNB cha Mjini Johannesburg, Moses Mabhida huko Durban, Mbombela ya Nelspruit, Nelson Mandela Bay ya Port Elizabeth naRoyal Bafokeng ya Rustenburg.

 UEFA CHAMPIONZ LIGI: Man City, Arsenal, Real ZALIZWA!!

UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZMATOKEO:
Jumatano Oktoba 24
FC Porto 3 FC Dynamo Kyiv 2
GNK Dinamo 0 Paris SaintvGermain 2
Arsenal FC 0 FC Schalke 2
Montpellier 1 Olympiacos 2
FC Zenit St. Petersburg 1 RSC Anderlecht 0
Málaga 1 AC Milan 0
AFC Ajax 3 Manchester City FC 1
Borussia Dortmund 2 Real Madrid 1
++++++++++++++++++++++++++
Katika MECHI DEI 3 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Mabingwa wa England, Manchester City walipata kipondo cha 3-1 toka kwa Ajax Amsterdam Mjini Amsterdam na vile vile hali hiyo kuwakuta wenzao Arsenal, wakiwa nyumbani, walichapwa 2-0 na Schalke ya Germany wakati huko Germany Mabingwa wa Nchi hiyo Borussia Dortmund waliwakung’uta Real Madrid bao 2-1.

AJAX 3 MAN CITY 1
Roberto M... Yale mategemeo ya Manchester City kusonga mbele kuingia Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI yamepata pigo kubwa baada ya kucharazwa Bao 3-1 na Ajax ndani ya Amsterdam ArenA katika Mechi ya Kundi F.
Huku Ajax wakitawala, Samir Nasri aliipa Man City bao la kuongoza lakini Siem de Jong akaisawazishia Ajax kabla haftaimu na baadae Kipindi cha Pili Niklas Moisander akapiga bao la pili kwa Ajax na Christian Eriksen kuipigia bao la 3.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI D-MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Borussia Dortmund Pointi 7
2 Real Madrid 6
3 Ajax 3
4 Manchester City 1

++++++++++++++++++++++++++
Matokeo haya yamewaacha Man City wakiwa mkiani mwa Kundi lao wakiwa na Pointi 1 tu kwa Mechi 3 na Mechi inayofuata ni ya wao kuwa Wenyeji wa Ajax hapo Novemba 6 na pia kuwa mwenyeji wa Real Madrid Novemba 21 na kumalizia ugenini na Borussia Dortmund.
VIKOSI:
Ajax: Vermeer, Van Rhijn, Alderweireld, Moisander, Blind, Schone, Poulsen, Eriksen, Sana, De Jong, Babel
Akiba: Cillessen, Enoh, Sulejmani, Boerrigter, Veltman, Dijks, Fischer.
Man City: Hart, Richards, Kompany, Lescott, Clichy, Toure, Barry, Milner, Aguero, Nasri, Dzeko
Akiba: Pantilimon, Sinclair, Kolarov, Tevez, Nastasic, Balotelli, Evans.
Refa: Svein Oddvar Moen (Norway)

ARSENAL 0 SCHALKE 2
Wenger on Arsenal's Champions League match against Schalke - video Schalke wamewastua Arsenal wakiwa kwao Emirates kwa kuwachapa bao 2-0 huku bao zote zikija katika Dakika 15 za mwisho kupitia Klaas Jan-Huntelaar na Ibrahim Afellay na kuifanya Klabu hiyo ya Bundesliga Germany itwae uongozi wa Kundi B.
Huku Arsene Wenger akikaa kwenye Jukwaa la Watazamaji akitumikia Kifungo cha Mechi ya mwisho alichoshushiwa na UEFA, benchi la Arsenal liliongozwa na Msaidizi wake Steve Bould lakini Timu yao ilonyesha udhaifu kwenye Difensi hasa upande wa kushoto ambako Andre Santos alionekana ni uchochoro.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI B-MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Schalke Pointi 7
2 Arsenal 6
3 Olympiacos 3
4 Montpellier 1
++++++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, Arsenal wana nafasi kubwa ya kufuzu kuingia Raundi ya Mtoano baada ya kushinda Mechi zao mbili za kwanza dhidi ya Montpellier na Olympiakos.
VIKOSI:
Arsenal: Mannone, Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Andre Santos, Ramsey, Coquelin, Arteta, Podolski, Cazorla, Gervinho
Akiba: Shea, Koscielny, Giroud, Djourou, Arshavin, Chamakh, Gnabry.
Schalke 04: Unnerstall, Uchida, Howedes, Matip, Fuchs, Hoger, Neustadter, Holtby, Afellay, Farfan, Huntelaar
Akiba: Hildebrand, Marica, Jones, Barnetta, Moritz, Draxler, Kolasinac.
Refa: Jonas Eriksson (Sweden)

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Novemba 6
FC Dynamo Kyiv v FC Porto
Paris SaintvGermain FC v GNK Dinamo
FC Schalke 04 v Arsenal FC
Olympiacos FC v Montpellier Hérault SC
RSC Anderlecht v FC Zenit St. Petersburg
AC Milan v Málaga CF
Manchester City FC v AFC Ajax
Real Madrid CF v Borussia Dortmund
Jumatano Novemba 7
Juventus v FC Nordsjælland
Chelsea FC v FC Shakhtar Donetsk
Valencia CF v FC BATE Borisov
FC Bayern München v LOSC Lille
SL Benfica v FC Spartak Moskva
Celtic FC v FC Barcelona
CFR 1907 Cluj v Galatasaray A.S.
SC Braga v Manchester United FC

MABINGWA Chelsea CHALI, Man United yatoka nyuma 2-0 na kushinda!!

UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZ>>BARCA yapewa ushindi na ALBA Dakika za Majeruhi!
Mabingwa watetezi wa Ulaya, Chelsea, wamepigwa bao 2-1 ugenini na Shakhtar Donetsk na wenzao wa England, Manchester United, wakiwa kwao Old Trafford, walipindua uongozi wa Braga wa Bao 2-0 ndani ya Dakika 20 na kushinda 3-2 huku huko Nou Camp Celtic ilivunjwa moyo Dakika za majeruhi baada ya Jordi Alba kuifungia Barca bao la pili na kuwapa ushindi wa Bao 2-1.
MATOKEO:
Jumanne Oktoba 23
FC Nordsjælland 1 Juventus 1
FC Shakhtar Donetsk 2 Chelsea 1
FC BATE Borisov 0 Valencia 3
LOSC Lille 0 Bayern Munich 1
FC Spartak Moskva 2 SL Benfica 1
FC Barcelona 2 Celtic 1
Galatasaray 1 CFR 1907 Cluj 1
Manchester United 3 Braga 2
++++++++++++++++++++++++++++++

BARCELONA 2 CELTIC 1
Jordi Alb... Bao la Dakika za majeruhi la Jordi Alba limewapa ushindi Barcelona Uwanjani kwao Nou Camp baada ya Celtic ya Scotland kutangulia kwa bao moja ambalo alifunga Samaras na Iniesta kusawazisha kabla ya haftaimu.
VIKOSI:
Barcelona: Valdes, Adriano, Bartra, Mascherano, Jordi Alba, Xavi, Song, Iniesta, Sanchez, Messi, Pedro
Akiba: Pinto, Fabregas, Villa, Jonathan, Montoya, Sergi Roberto, Tello.
Celtic: Forster, Lustig, Wilson, Ambrose, Izaguirre, Samaras, Brown, Wanyama, Ledley, Mulgrew, Hooper
Akiba: Zaluska, Matthews, Miku, Commons, Rogne, Kayal, Forrest.
Refa: Gianluca Rocchi (Italy)
++++++++++++++++++++++++++++++

MAN UNITED 3 BRAGA 2
Chicharit... Javier Hernandez, ‘Chicharito’, alipiga bao mbili na Jonny Evans bao moja baada ya Man United kutoka nyuma kwa bao 2-0 za Braga ya Ureno zote zikifungwa na Alan ndani ya Dakika 20 na kupata ushindi wa bao 3-2 wakiwa kwao Old Trafford huo ukiwa ushindi wao wa 3 mfululizo kwenye Kundi lao.
VIKOSI:
Man United: De Gea, Da Silva, Carrick, Evans, Buttner, Kagawa, Fletcher, Cleverley, Rooney, Hernandez, van Persie
Akiba: Johnstone, Ferdinand, Anderson, Giggs, Nani, Young, Welbeck.
Braga: Beto, Leandro Salino, Nuno Andre, Paulo Vinicius, Elderson, Custodio, Hugo Viana, Ruben Amorim, Alan, Ruben Micael, Eder
Akiba: Quim, Mossoro, Helder Barbosa, da Solva, Baiano, Ze Luis, Anibal.
Refa: Milorad Mazic (Serbia)
++++++++++++++++++++++++++++++

SHAKHTAR DONETSK 2 CHELSEA 1

Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, leo wamegalagazwa ugenini na Shakhtar Donetsk baada ya kupigwa bao 2-1.
Shakhtar walifunga bao zao kupitia Alex Teixeira, Dakika ya 3, na Fernandinho, Dakika ya 52, na Chelsea kupata bao lao pekee katika Dakika ya 88 mfungaji akiwa Oscar.
VIKOSI:
Shakhtar Donetsk: Pyatov, Srna, Kucher, Rakitskiy, Rat, Hubschman, Fernandinho, Alex Teixeira, Mkhitaryan, Willian, Luiz Adriano
Akiba: Kanibolotskiy, Stepanenko, Eduardo, Gai, Douglas Costa, Kryvtsov, Ilsinho.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Luiz, Cole, Oscar, Ramires, Mikel, Lampard, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Romeu, Hazard, Sturridge, Cahill, Azpilicueta, Bertrand.
Refa: Damir Skomina (Slovenia)
++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
[MECHI ZOTE Saa 3 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumatano Oktoba 24
FC Porto v FC Dynamo Kyiv
GNK Dinamo v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v FC Schalke 04
Montpellier Hérault SC v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v RSC Anderlecht [SAA 1 USIKU]
Málaga CF v AC Milan
AFC Ajax v Manchester City FC
Borussia Dortmund v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++

EUROPA LIGI: Ni Usiku wake Alhamisi!!

>>ANFIELD ni Liverpool v FC Anzhi, Newcastle v Club Brugge & Maribor v Spurs!
EUROPA_LIGI_CUPEUROPA LIGI, Alhamisi Oktoba 25, inaingia MECHI DEI 3, huku Wawakilishi wa England, Liverpool na Newcastle wakicheza nyumbani na Tottenham wakiwa ugenini na hizi zitakuwa ni Mechi zao za 3.
+++++++++++++++++++
TIMU za ENGLAND:
MSIMAMO:
]Kila Timu Mechi 2]
KUNDI A
1 FC Anzhi Pointi 4
2 Udinese 4
3 Liverpool 3
4 Young Boys 0
KUNDI D
1 Newcastle Pointi 4
2 Bordeaux 3
3 Brugge 3
4 Maritimo 1
KUNDI J
1 Lazio Pointi 4
2 Maribor 3
3 Tottenham 2
4 Panathinaikos 1
+++++++++++++++++++
Mara nyingi, hasa Timu za England, zimekuwa zikipanga Vikosi hafifu kwenye michuano hii hasa kwa vile Mechi zake zinachezwa Alhamisi na wao Wikiendi wana mitanange ya Ligi Kuu England.
Kwa Alhamisi hii, hali hiyo haiwezi kubadilika, hasa kwa Liverpool, ambao Jumapili wana kimbembe cha DABI ya Liverpool dhidi ya Mahasimu wao wakubwa Everton, kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo itachezwa Uwanjani Goodison Park.
RATIBA:
Alhamisi, Oktoba 25
[SAA, zikionyeshwa, ni za BONGO]
2205 Liverpool FC v FC Anzhi Makhachkala
BSC Young Boys v Udinese Calcio
Club Atlético de Madrid v A. Académica de Coimbra
Hapoel TelvAviv FC v FC Viktoria Plzen
VfL Borussia Mönchengladbach v Olympique de Marseille
AEL Limassol FC v Fenerbahçe SK
Newcastle United FC v Club Brugge KV
CS Marítimo v FC Girondins de Bordeaux
FC Steaua Bucuresti v Molde FK
VfB Stuttgart v FC København
PSV Eindhoven v AIK
FC Dnipro Dnipropetrovsk v SSC Napoli
Videoton FC v FC Basel 1893
KRC Genk v Sporting Clube de Portugal
FC Rubin Kazan v Neftçi PFK
FC Internazionale Milano v FK Partizan
AC Sparta Praha v Hapoel Kiryat Shmona FC
Olympique Lyonnais v Athletic Club
Panathinaikos FC v S.S. Lazio
NK Maribor v Tottenham Hotspur FC
Rosenborg BK v FC Metalist Kharkiv
SK Rapid Wien v Bayer 04 Leverkusen
Helsingborgs IF v Hannover 96
Levante UD v FC Twente
FC Anzhi Makhachkala

2205 Newcastle United FC v Club Brugge KV

2000 NK Maribor v Tottenham Hotspur FC
Rosenborg BK v FC Metalist Kharkiv
SK Rapid Wien v Bayer 04 Leverkusen
Helsingborgs IF v Hannover 96
Levante UD v FC Twente

MKUTANO MKUU TASWA MWEZI UJAO

Amir Mhando
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), imefikia hatua ya mwisho ya mazungumzo na mdhamini wa Mkutano Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao katika tarehe ambayo itatangazwa rasmi.