Saturday, December 29, 2012

TUSKER TATU, SIMBA TILA LILA TAIFA


Tusker wakishangilia mbele ya mashabiki wa Simba 
SIMBA SC imefungwa mabao 3-0 na Tusker ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa vema na refa Hashim Abdallah, hadi mapumziko, tayari Tusker walikuwa mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani na Jesse Were dakika ya 37 na 45.
Mabao yote yalitokana na udhaifu wa safu ya ulinzi ya Simba, ambayo hii leo iliongozwa na beki kutoka Mali, Komabil Keita kiasi cha kufikia mfungaji anafunga akiwa amebaki anatazamana na kipa.
Simba ilikuwa ikishambulia kutokea pembeni, lakini mipira mingi mirefu iliyokuwa inamiminwa langoni mwa Tusker ilikuwa inaokolewa na mabeki warefu wa klabu hiyo bingwa ya Kenya, wakiongozwa na beki wa zamani wa Yanga, Joseph Shikokoti.
Kipindi cha pili, Tusker walirudi kwa nguvu tena na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 54, mfungaji Frederick Onyango.
Simba pamoja na kufanya mabadiliko, ikiwatoa Haruna Shamte, Haruna Athumani, Paul Ngalema, Mussa Mudde, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhani Chombo na Kiggi Makassy na kuwaingiza Miraj Adam, Hassan Isihaka, Emily Ngeta, Jonas Mkude, Salim Kinje, Haruna Moshi, Ramadhani Singano, Nassor Masoud ‘Chollo’ na Edward Christopher, haikuweza kupata hata bao la kufutia machozi.
Nassor Masoud aliingia kuchukua nafasi ya Shamte, lakini naye akaumia na kutoka nafasi yake ikichukuliwa na kinda wa Simba, B, Masele Kaheza.
Simba SC; William Mweta, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Hassan Khatibu, Komabil Keita, Mussa Mude, Haroun Athumani, Abdallah Seseme, Abdallah Juma, Ramadhan Chombo na Kiggi Makassy.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Frederick Onyango, Ismail Dunga, Jesse Were, Robert Omonuk,

BAADHI YA MAGOLI BORA KATIKA HISTORIA YA SOKA DUNIANI

KWENYE MAFANIKIO MANENO MENGI HUTOKEA CHANGAMOTO HUWEPO TU======MESSI NI NOMA TU WE HATA KAMA HUMPENDI CHEKI VITU VYAKE HUMU VITU ADIMU

MWAKA HUU WA 2012 TANO JUMA IN SPORTS INAKULETEA TUKIO LA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI ALIYEUAWA KWA KULIPULIWA BOMU NA JESHI LA POLISI KULE IRINGA

GUADIOLA KUREJEA KUFUNDISHA SOKA MWAKANI 2013


 Pep Guardiola atarejea kufundisha soka mwakani 2013 baada ya muda mrefu nje ya soka kwa mujibu wa Rais wa zamani wa Barcelona Joan Laporta.

Guardiola aliondoka kuifundisha Barcelona baada ya kumalizika msimu uliopita akitaka kupumzika kwa muda baada ya misimu minne ya kuifundisha kwa mafanikio vijana wa Catalunya.

Kocha huyo raia wa Hispania alikuwa akihusishwa na kujiunga na moja ya vilabu vukubwa barani Ulaya tangu wakati ho alipoa achana na Barcelona, ikiwa ni pamoja na Paris Saint-Germain, ingawa Laporta anaamini kuwa klabu hiyo ya nchini Ufaransa haimfai Guardiola.

Akikaririwa amesema"nadhani Pep atarejea kufundisha mwakani. Ana mvuto mkubwa wa kufundisha, ana mawazo safi na ana akili"  Najisikia mwenye heshima kuwa karibu na Pep, kwangu mimi ndiye kocha bora dunia

ANZHI MAKHACHKALA WAPUUZA MADAI YA KWAMBA WANAMWITAJI LIONELL MESSI KWA EUO ML 250


 Anzhi Makhachkala imekanusha taarifa zilizowahusisha kuwa wametenga euro milioni 250 kwa ajili ya kumsajili nyota wa Barcelona Lionel Messi.

Taarifa zilizo ripotiwa na jarida la Mundo Deportivo ziliarifu kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina amekataa ofa ya euro milioni 30 kutoka katika klabu hiyo ya Russia.


Hata hivyo mshauri wao wa mambo ya masoko, German Tkachenko ameponda taarifa hiyo na kusema ilikuwa ni uongo mtupu na kusisitiza kwamba klabu yake haifanyi shughuli za uhamisho kwa namna hiyo.

Akiongea na gazeti la Russia la Sports-Express amesema

"hakuna hata chembe ya ukweli katika hilo"

Gazeti hilo la nchini Russia pia limearifu kuwa Messi si tu amekataa ofa hiyo, lakini pia kama mpango huyo ungefanikiwa basi mkataba wake ungemuweka katika klabu hiyo mpaka 2018.

Mshambuliaji mwenzake wa zamani wa Camp Nou Samuel Eto’o, ambaye alicheza pamoja na Messi  Barca, aliondoka Russia na kuelekea katika klabu hiyo kwa mshahara mnono akiwa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa duniani na alihama kwa uhamisho wa euro milioni 20 kwa mwaka.

DIEGO ALMANDO MARADONA ANAAMINI KUWA MOURINHO NI MIONGONI MWA MAKOCHA BORA DUNIANI

Diego Maradona anaamini kuwa kocha wa Real Madrid ni miongoni mwa makocha bora duniani.Mreno huyo aliiongoza Blancos mpaka kutwaa taji la ligi kuu nchini Hispania La Liga msimu uliopita na pia akiwa na rekodi ya kutwaa mataji katika nchi zenye ligi ngumu kama vile Ureno, England na Italia pamoja na kutwaa mataji mawili ya vilabu bingwa Ulaya.

Maradona, ambaye katika fani ya ufundishaji hakung’ara sana kama ilivyokuwa katika kipindi cha uchezaji wake, anaamini kuwa bosi huyo wa zamani wa Inter katika kipindi chote amefanikiwa kuwa juu.

Akinukuliwa nchini Dubai hapo jana Maradona amesema,

"matokeo aliyoyapata Mourinho yanaongeza nguvu ya sauti ya uwezo wake”

Ameendelea kwa kusema nimekuwa nikimuona akifundisha katika kiwango cha juu, amekuwa makini na kila mchezaji katika kikosi chake kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

"nilikuwa ni mchezaji niliyekuwa nataka kujulikana, lakini ni jambo jema kuona kocha hakujali peke yako lakini timu nzima kwasababu wao ndio wanao kusaidia uwanjani"

Maradona kwasasa hana timu ya kufundisha baada ya kuondoshwa katika klabu ya Al Wasl mapema mwaka huu wa 2012.

Nafasi kubwa aliyopata katika ufundishaji wake ni timu yake ya taifa ya Argentina mwaka 2010 katika fainali ya kombe la dunia, ambapo timu hiyo ya taifa kutoka Amerika ya kusini ilitolewa na Ujerumani katika robo fainali.

BARCA: KOCHA VILANOVA KURUDI JANUARI

>>BAADA KUFANYIWA OPERESHENI KUTIBU KANSA!
BARCA_v_REALRAIS wa FC Barcelona, Sandro Rosell, amesema kuwa Kocha wao Mkuu, Tito Vilanova, atarejea kazini baada ya Siku 15 hadi 20 kufuatia upasuaji ili kutibu Kansa iliyomrudia tena.
Vilanova, Miaka 44, alifanyiwa operesheni hiyo Desemba 20 kujaribu kuganga Kansa ya Tezi ambayo mara ya kwanza aliipata Mwaka 2011 na kutibiwa na hivi karibuni ikarudi tena.
Rosell amesema: “Atarudi baada ya Siku 15 au 20 lakini Siku nyingine itabidi awe Hospitalini kwa matibabu. Atachanganya kazi na matibabu.”
Chini ya Vilanova, ambae alitwaa himaya mwishoni mwa Msimu uliopita baada ya Kocha Pep Guardiola kung’atuka, Barcelona imeweka Rekodi ya kuanza vyema La Liga kwa kupoteza Pointi mbili tu katika Mechi 17 za Ligi hiyo ambayo wanaoongoza kwa Pointi 9.
Kwa sasa Barcelona wanasimamiwa na Msaidizi wa Vilanova, Jordi Roura, lakini Msimu wa Soka huko Spain upo kwenye Vakesheni ya Krismasi na Mwaka mpya na Mechi inayofuata kwa Barcelona ni Dabi ya Jiji la Barcelona dhidi ya Espanyol hapo Januari 6.
LA LIGA:
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 6
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 17]
1 Barcelona Pointi 49
2 Atletico Madrid 40
3 Real Madrid 33
4 Malaga 31
5 Real Betis 28
6 Levante 27
7 Real Sociedad 25
RATIBA:
Jumapili Januari 6
3:00 FC Barcelona v RCD Espanyol
3:00 Celta de Vigo v Real Valladolid
3:00 Deportivo La Coruna v Malaga CF
3:00 Real Mallorca v Atletico de Madrid
3:00 Real Madrid CF v Real Sociedad
3:00 Rayo Vallecano v Getafe CF
3:00 Sevilla FC v Osasuna
3:00 Real Zaragoza v Real Betis
3:00 Levante v Athletic de Bilbao
3:00 Granada CF v Valencia

RIDHIWANI KIKWETE APONDA MFUMO WA UENDESHAJI YANGA ASEMA AFADHALI WA SIMBA


Ridhiwani akihutubia Waandishi asubuhi ya leo Kiromo Hotel
MWENYEKITI wa Kamati ya Kusaidia timu za soka za vijana za taifa, Ridhiwani Kikwete, amesema mfumo wa uendeshwaji wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam ni mbovu kwa sababu unategemea mfuko wa mtu mmoja.
Akizungumza wakati anatoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani, Kikwete alisema kwamba Yanga inahitaji kubadilika kutoka mfumo huo.
Kikwete alisema ni afadhali mfumo wa uendeshwaji wa Simba SC, ambao desturi yao ni kuchangishana.
“Nilijaribu kufanya uchunguzi wa mfumo wa uendeshwaji wa klabu ya Yanga, nikashangazwa ni mfumo mbaya, kwa sababu unategemea mfuko wa mtu mmoja, afadhali Simba wao huwa wanachangishana,”alisema.
Ingawa hakumtaja mtu ambaye mfuko wake unategemewa Yanga, lakini wazi ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Yussuf Mehboob Manji.
Kwa ujumla katika hotuba yake, Kikwete alisema haridhishwi na mfumo wa uendeshwaji wa soka ya Tanzania na kwamba unahitaji mabadiliko.
Kikwete aliushauri uongozi wa TASWA upiganie nafasi ya uwakilishi ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kusisitiza juu ya umuhimu wa waandishi nchini kutambua haki zao.
Lakini pia Kikwete aliwaasa waandishi kuepuka uandishi wa kinazi wa Simba na Yanga na badala yake kuzama ndani zaidi katika kuripoti, sambamba na kuripoti michezo yote, badala ya kuegemea kwenye soka pekee.
“Vyombo vya habari lazima viwe na wataalamu tofauti wa kuripoti michezo tofauti, huyu akiegemea kwenye soka, mwingine aegemee kwenye mchezo mwingine, ili kuhakikisha tunafikisha ujumbe vema kwa jamii,” alisema mtoto huyo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.
Ridhiwani ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, NEC akiiwakilisha Wilaya ya Bagamoyo alisema kwamba ipo haja ya TASWA kuendesha semina kadhaa za kuelimisha Waandishi wa Habari kuweza kuripoti michezo mbalimbali nchini.  
Aidha, katika mkutano huo, wanachama walielimishwa kuhusu uanzishwaji wa Saccos na kuridhia kuanza kwa mchakato wa kuundwa kwa chama cha ushirika wa akiba na mikopo kwa Taswa. Walipendekezwa wajumbe waunde timu ya mpito.














WENGER AMKANA BA, NEYMAR BARCA BAADA 2014, ANCELOTTI na RONALDO!

DEMBA_BARIPOTI zimebainisha kuwa Arsene Wenger ameua ile minong’ono kuwa wako njiani kumsajili Straika wa Newcastle, Demba Ba, huku Meneja wa Paris St Germain Carlo Ancelotti akisisitiza kuwa hamna nafasi ya wao kumchukua Cristiano Ronaldo na huko Brazil, Baba Mzazi wa Neymar, amedokeza kuwa Mwanawe atajiunga na Barcelona mara baada ya kumalizika Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zitakazochezwa huko Brazil.

WENGER na BA
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amefuta ile dhana ya kuwa wana nia ya kumsajili Straika kutoka Senegal, Demba Ba, ambae hata Newcastle wenyewe wamenawa mikono kuwa huenda akauzwa.
Lakini Wenger amesema: “Nampenda Ba, lakini hatuwezi kumsaini!”
Demba Ba alijiunga na Newcastle akitokea West Ham Juni Mwaka 2011.


PSG na RONALDO

Kocha wa Paris St Germain Carlo Ancelotti amesisitiza Supastaa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hajiungi na na Timu yake.
Hivi karibuni kumekuwa na uvumi kuwa Ronaldo ataondoka Real na Klabu za Man United na PSG ndizo zinazotajwa kumchukua.
Ancelotti ametamka: “Hamna ukweli kuhusu Ronaldo kuja kwetu. Si tatizo la Pesa lakini je Klabu yake itakubali kuuzwa?”
Vile vile, Ancelotti aligusia kuwa pamoja na Lucas Moura kwenda PSG Mwezi Januari atakuwa na Wachezaji 30 Klabuni hapo.


NEYMAR na BARCA
Kwa mujibu wa Baba Mzazi wa Staa wa Brazil na Klabu ya Santos Neymar, Mchezaji huyo atajiunga na FC Barcelona mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa Nchini Brazil Mwaka 2014.
Baba huyo amesema mipango hiyo ipo lakini bado haijakamilika na kufafanua: “Anataka kucheza Ulaya. Tumebadili kikomo cha Mkataba wake kutoka 2015 na kuwa 2014. Kwa sasa atabaki Brazil hadi Kombe la Dunia kwisha! Na kwa sasa ni bora kila Mtu akae kimya!”

YANGA SAFARINI KESHO SAA KUMI ALFAJIRI KWENDA UTURUKI NA WACHEZAJI 27

YANGA_MJENGO
>> WACHEZAJI 27 KUPIGA KAMBI MJINI ANTALYA
MABINGWA wa AFRIKA MASHARIKI na KATI, Yanga, kesho Asubuhi wanatarajiwa kuondoka Jijini Dar es Salaam kwa Ndege ya Turkish Airlines kwenda Nchini Uturuki kupiga Kambi ya Mazoezi ya Wiki mbili ikiwa na Wachezaji 27 na Viongozi 7.
Msafara huo mara baada ya kutua Mjini Instanbul utasafiri hadi Mji wa Antalya ulio Kusini Magharibi mwa Uturuki na kufikia Hoteli ya Sueno iliyo ufukweni mwa Bahari ya Mediterranean.
Msafara huo utaongozwa na Mohammed Nyenge, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, na Viongozi wengine ni Kocha Mkuu, Ernest Brandts, Kocha Msaidizi, Fred Felix Minziro, Kocha wa Makipa, Razaki Siwa, Daktari wa Timu, Suphian Juma, Meneja wa Timu, Hafiz Saleh na Afisa Habari, Baraka Kizuguto.
YANGA_UTURUKI
Wachezaji watakaoandaman na Timu hiyo ni:
MAKIPA: Ally Mustafa ‘Barthez’, Said Mohammed na Yusuph Abdul
MABEKI: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na Oscar Joshua.
VIUNGO WAKABAJI: Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Ladislaus Mbogo na Kelvin Yondani.
VIUNGO WASHAMBULIAJI: Athumani Iddi, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega Seme, Saimon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfan na David Luhende.
MASTRAIKA: Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza.

KOCHA MPYA SIMBA AWASILI LEO, KUISHUHUDIA TIMU TAIFA IKIMENYANA NA TUSKER


Liewig
KOCHA mpya wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba SC, Mfaransa Patrick Liewig anatarajiwa kuwasili leo nchini na atakuwapo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuishuhudia timu hiyo ikimenyana na mabingwa wa Kenya, Tusker FC.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema kwamba, awali kocha huyo alitarajiwa kuawasili nchini juzi, lakini ilishindikana baada ya kukosa nafasi kwenye ndege na sasa mashabiki wa timu hiyo wamtarajie leo.
Alisema kocha huyo ambaye anakuja kurithi mikoba ya Mserbia Profesa Milovan Cirkovick, atakishuhudia kikosi cha Simba kikicheza mechi hiyo kabla ya kuendelea na taratibu nyingine ikiwemo kusaini mkataba wa kazi na baadaye kuanza kutumikia kibarua chake kipya.
Liewig ni kocha wa zamani wa Akademi ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa, ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Club Africain ya Tunisia, Patrick Liewig na ana Stashahada ya Juu ya ukocha na Shahada ya tatu ya ualimu wa soka ya vijana aliyotunukiwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufaransa, Gerard Houiller na amehudhuria pia kozi za ufundishaji mazoezi ya viungo Juni mwaka 1999 katika Chuo Kikuu cha Dijon.
Kwa upande wa uzoefu, Liewig alifanya kazi PSG kuanzia mwaka 1989 hadi 1999 kama Kocha Mkuu wa akademi na kuna wakati alikuwa akishirikishwa pia katika programu za timu A, ingawa majukumu yake zaidi yalikuwa ni kwa Under 20, Under 18 aliowawezesha kutwaa Kombe la French Junior Gambardella na Under 16.
Kuanzia mwaka 1989 hadi 1990:  alikuwa Meneja Mkuu wa Tomislav IVIC, 1990 hadi 1991 alikuwa Msaidizi wa Henri Michel, 1991 hadi 1994 alikuwa Msaidizi wa Artur Jorge, 1994 hadi 1996 alikuwa Msaidizi wa Luis Fernandez, 1996 hadi 1998: alikuwa Msaidizi wa Ricardo Gomez, 1998 hadi 1999 alikuwa Msaidizi wa Alain Giresse.
Liewig pia alifundisha Al Wahda FC ya Abu Dhabi kuanzia 1999 hadi 2001, ambayo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu ya nchi hiyo na Kombe la Ligi.
Januari mwaka 2003 alikuwa Msimamizi wa Chama cha Soka UAE katika fainali za Afrika za U20 nchini Burkina Faso.
Kuanzia mwaka 2004 hadi 2009 alikuwa Kocha wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyoipa mataji matatu ya Ligi Kuu ya nchini humo mfululizo, 2004, 2005 na 2006, Super Cup ya nchini humo 2005, 2007, 2008 na 2009 na akaiwezesha kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa mara tatu, mara moja akiifikisha Nusu Fainali.
Amekuwa Kocha bora wa Ivory Coast miaka mitatu mfululizo, 2004, 2005 na 2006 na tangu Septemba mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alikuwa kocha wa Club Africain ya Tunisia
Kuelekea mchezo wa leo, Simba itamenyana na Tusker FC ambayo ilianza vema ziara yake nchini, baada ya kuichapa Yanga 1-0 katika mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa Jumatano.
Simba SC na Tusker zinatarajiwa kukutana pia kwenye Kundi la Mapinduzi visiwani Zanziabr hivi karibuni, kwani zimepangwa kundi moja, A pamoja na Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba.
Aidha, katika Kundi B, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara, Azam FC ya Dar e Salaam pia, imepangwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union  ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Kamati Maalum ya Kusimamaia michuano hiyo, inaonesha kuwa katika mchezo wa kwanza utakaochezwa siku ya ufunguzi itakuwa ni kati ya Bandari kutoka Unguja ambayo itacheza na Jamhuri kutoka kisiwani Pemba ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika, pamabanolitakalochezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja, huku usiku wa siku hiyo hiyo katika Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja pambano la ufunguzi rasmi katika mashindano hayo likiwakutanisha mabingwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC ambao watapambana na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo jumla ya timu nane zitashiriki katika mashindano hayo ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa visiwani hapa, timu hizo zimegawanya katika makundi mawili ambayo ni kama ifuatavyo:
Awali michuano hiyo ilitarajiwa kuanza kisiwani Pemba tarehe 1 Januari, lakini kutokana na kujitoa katika mashindano kwa klabu ya Al-Ahly ya Misri kutokana na klie kilichoelezwa sababu za kiusalama, mechi zote sasa zitachezwa kisiwani Unguja na ufunguzi ukipangwa kuanza tarehe 2 badala ya tarehe 1 januari.
Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na zawadi ya kombe na fedha taslim Tsh.Milioni kumi (10,000,000), mshindi wa pili Milioni tano (5,000,000), pamoja na zawadi nyengine ambazo zimegawanywa katika makundi tofauti ikiwemo zawadi ya mfungaji bora, mchezaji bora, mwamuzi bora, kipa bora, mwandishi wa habari bora, timu bora na zawadi nyinginezo.

MAJEMBE MAWILI AZAM NJE KOMBE LA MAPINDUZI

Waziri Salum
VIUNGO wa Zanzibar, Waziri Salum na Abdulhalim Humud hawatacheza michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayoanza wiki ijayo visiwani Zanzibar kutokana na kuwa bado majeruhi.
Meneja Msaidizi wa Azam, Jemadari Said Kazumari alisema jana kwamba, wawili hao hadi jana walikuwa hawajaripoti mazoezini, hivyo uwezekano wao wa kucheza michuano hiyo ni mdogo.
Azam ambao ndio mabingwa watetezi wa taji hilo na mabingwa wa Kombe la Hisani la DRC, walianza mazoezi jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya mapumziko mafupi ya sikukuu ya Krisimasi.
Katika maozezi hayo, wachezaji wengine watatu walikosekana, beki Joackins Atudo, kiungo Humphrey Mieno wote wa Wakenya na mshambuliaji Brian Umony wa Uganda kwa sababu bado wana udhuru hadi baada ya sikukuu ya Krisimasi.
Azam ilitua Dar es Salaam Jumatatu usiku wiki hii, ikitokea Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ilikotwaa Kombe la Hisani, linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la DRC.
Azam walitwaa taji hilo Jumamosi iliyopita, baada ya kuwachapa wenyeji, Dragons FC kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Azam iliingia fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya DRC Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
Kikosi cha Azam kilichoshiriki mashindano hayo ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki, Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey Mieno na Joackins Atudo.
Katika mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti. Mchezaji mwingine wa kigeni wa Azam, Brian Umony wa Uganda, atajiunga na timu hiyo baada ya sikukuu pia.
Azam wamepangwa Kundi B, katika Kombe la Mapinduzi pamoja na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union  ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
Kundi A lina timu za Simba SC, Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka ndani na nje ya Tanzania.

JUMA SEIF KIJIKO, SHAMTE ALLY, OBADIA MUNGUSA NA IBRAHIM JOB KUVAA JEZI YA AFRIKAN LYON MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU TANZANIA BARA.


Kutoka kushoto, Juma Seif Kijiko, Obadia Mungusa, Shamte Ally na Ibrahim Job.
Wachezaji kiungo wa pembeni Shamte Ally, kiungo stadi wa kati Juma Seif Kijiko wa Yanga, mlinzi wa kati Obadia Mungusa wa Simba na mlinzi wa pembeni wa zamani wa Yanga Ibrahim Job, wanatarajiwa kuvaa jezi ya timu ya African Lyon ya Temeke jijini Dar es Salaam katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Wachezaji hao tayari wamekamilisha taratibu zote za kuhamia klabu hiyo katika kipindi cha dirisha dogo kwa mkopo, na tayari wameanza mazoezi na klabu hiyo katika uwanja wa Sigara ulioko Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Akiongea na Rockersports katibu wa Afrikan Lyon Brown Elias amesema uongozi wa Lyon umefurahishwa na ujio wa wachezaji hao ambao licha ya kwamba walikuwa hawapewi nafasi katika vikosi vya kwanza katika vilabu vyao lakini anaamini ni wazuri.
Amesema ni ngumu kupata nafasi katika vilabu vikubwa vya Simba na Yanga hata kama mchezaji ni mzuri kutokana na ushindani mkubwa wa kugombea namba miongoni mwa wachezaji na hiyo haiondoi uzuri wa mchezaji na kwamba kama mchezaji anajua kucheza basi atakuwa anajua tu jambo la msingi ni mazoezi na kujituma uwanjan.

Hata hivyo Brown amesema uongozi wa Lyon chini ya mkurugenzi wake Rahimu Zamunda Kangezi "mmachinga" umesikitishwa na kumkosa mshambuliaji mrefu kuliko wote katika ligi kuu ya soka Tanzania Bara Gaudience Mwaikimba kufuatia ombi lao kutolewa nje na uongozi wa klabu hiyo.
Lyon tayari imenza maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara wakifanya mazoezi yao katika uwanja wa Sigara ulioko Changombe jijini Dar es Salaam. 
Kwasasa klabu hiyo haina kocha mkuu mara baada ya aliyekuwa kocha mkuu Pablo Ignacio Velez kutimka rasmi na sasa Afrikan Lyon inasaka kocha mrithi wake kabla ya kuanza kwa ligi kuu mzunguko wa pili.
Pichani Pablo Ignacio Velez kulia, alipokuwa akitambulishwa kwa waandishi wa habari mwezi Agosti. kushoto ni Rahim Kangezi na Charles Otieno katikati.