Tuesday, October 2, 2012

KASEJA NA MECHI 24 ZA WATANI, NANI KAMA YEYE?

Kaseja kinara wa mechi za watani


KAMA kesho atasimama kwenye milingoti mitatu, Juma Kaseja atatimiza mechi 25 za wapinzani wa jadi katika soka ya Tanzania kucheza, tangu ajiunge na Simba mwaka 2003, kati ya hizo moja tu, akiidakia Yanga mwaka 2009.
Kama itakumbukwa Kaseja, alisajiliwa Simba mwishoni mwa mwaka 2002, akitokea Moro United na moja kwa moja akaachiwa mikoba na aliyekuwa Simba One, Mwameja Mohamed.
 
 
Kwa kuwa Mwameja alikuwa Tanzania One pia, haikuchukua muda, Kaseja naye akawa Tanzania One, akirithi mikoba ya Manyika Peter, aliyekuwa kipa wa Yanga. Makipa wote hawa watatu, Mwameja, Manyika na Kaseja walikuwa mahiri wa kuokoa mikwaju ya penalti.
 
 
Mechi ya kwanza ya watani Kaseja kucheza ilikuwa Aprili 20, mwaka 2003 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, ambayo Yanga ilishinda 3-0, mabao yake yakifungwa na Kudra Omary dakika ya 30, Heri Morris dakika ya 32 na Salum Athumani dakika ya 47.
 
 
Hii ilikuwa mechi maalum ya kirafiki, iliyoandaliwa na promota Dika Sharp kwa kushirikiana na Prime Time Promotions, ambayo ilipewa jina ‘Big Match’
Mechi ya pili ikafuatia Septemba 28, mwaka 2003, katika Ligi Kuu ambayo iliisha kwa sare ya 2-2, mabao ya Simba yakifungwa na Emmanuel Gabriel dakika ya 27 na 36, wakati ya Yanga yalifungwa na Kudra Omary dakika ya 42 na Heri Morris dakika ya 55.
 
 
Mechi ya tatu ilikuja Novemba 2, mwaka 2003 ya Ligi Kuu, marudiano ambayo iliisha kwa sare ya bila kufungana.
 
Mechi ya nne iliikuja Agosti 7, mwaka 2004, ilikuwa ya Ligi Kuu pia, Simba ikashinda 2-1, mabao ya Shaaban Kisiga ‘Malone’ dakika ya 64 na Ulimboka Mwakingwe dakika ya 76, wakati la Yanga lilifungwa na Pitchou Kongo dakika ya 48.
 
Mechi ya tano ilikuja Septemba 18, mwaka 2004 ya Ligi Kuu pia, bao pekee la Athumani Machuppa dakika ya 82, likiipa ushindi Simba.
 
Mechi ya sita ilikuja Aprili 17, 2005 na Simba ikashinda tena 2-1, Ligi Kuu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, mabao yake yakifungwa na Nurdin Msiga dakika ya 44 na Athumani Machupa dakika ya 64, baada ya Aaron Nyanda kutangulia kuifungia Yanga dakika ya 39.
 
Mechi ya saba, ilikuja Julai 2, mwaka 2005 ya fainali ya Kombe la Tusker, ilichezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na Yanga ikalala 2-0, mabao ya Emmanuel Gabriel dakika ya 60 na Mussa Hassan Mgosi dakika ya 72.
 
Mechi ya nane ilikuja Agosti 21, mwaka 2005 ya Ligi Kuu, ambayo Simba ilishinda 2-0, mabao yote yakitiwa kimiani na Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Nico Nyagawa katika dakika za 22 na 56 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
 
Mechi ya tisa ilikuja Machi 26, mwaka 2006 ya Ligi Kuu, lakini hiyo iliisha kwa sare ya bila kufungana na mechi ya 10, ilikuja Agosti 15, mwaka 2006, Nusu Fainali ya Kombe la Tusker, ambayo iliisha kwa sare ya 1-1, Emanuel Gabriel akitangulia kuifungia Simba dakika ya 69 na Credo Mwaipopo akaisawazishia Yanga dakika ya 90. Simba ikashinda kwa penalti 7-6.
 
Mechi ya 11 ilikuja Oktoba 29, mwaka 2006, Ligi Kuu ambayo iliisha kwa sare tasa, yaani 0-0 na mechi ya 12 ilikuja Julai 8, mwaka 2007, Fainali ya Ligi Ndogo, ambayo matokeo yalikuwa 1-1 ndani ya dakika 120, Moses Odhiambo akitangulia kuifungia Simba penalti dakika ya pili, kabla ya Said Maulid ‘SMG’ kusawazisha dakika ya 55 na Simba ikashinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
 
Mechi ya 13, ilikuja Oktoba 24, mwaka 2007, Ligi Kuu na ilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na bao pekee la Ulimboka Mwakingwe, dakika ya 14, lilipa Simba ushindi. Mechi ya 14 ilikuja Aprili 27, ya Ligi Kuu pia, mwaka 2008, ambayo iliisha kwa sare ya bila kufungana, wakati mechi ya 15, ilikuja Aprili 19, mwaka 2009, Juma Kaseja akiwa katika mkataba wa mwaka na Yanga.
 
Aliidakia Yanga siku hiyo na mechi hiyo ya Ligi Kuu ikaisha kwa sare ya 2-2, mabao ya Simba yakifungwa na Ramadhan Chombo ‘Redondo’ dakika ya 23 na Haruna Moshi ‘Boban’ dakika ya 62, wakati ya Yanga yalifungwa na Ben Mwalala dakika ya 48 na Jerry Tegete dakika ya 90.
 
Mechi ya 16 ilikuja Oktoba 31, mwaka 2009, Kaseja akiwa tayari amerejea Simba SC na akaiongoza timu yake kipenzi kuilaza Yanga 1-0, bao pekee la Mussa Hassan Mgosi dakika ya 26 katika Ligi Kuu.
 
Mechi ya 17, ilikuja Desemba 25, mwaka 2009, Nusu Fainali ya Kombe la Tusker na Yanga ilishinda 2-1, mabao ya Jerry Tegete dakika ya 67 na Shamte Ally dakika ya 120, wakati la Simba lilifungwa na Hillary ‘Ford’ Echesa dakika ya 78 kwa penalti.
 
Mechi ya 18, ilikuja Aprili 18, mwaka 2010 na Yanga ilichapwa mabao 4-3, Ligi Kuu pia, mabao ya Simba yakifungwa na Uhuru Suleiman dakika ya tatu, Mussa Mgosi dakika ya 53 na 74 na Hillary Echesa dakika ya 90 na ushei, wakati ya wana Jangwani, yalifungwa na Athumani Iddi ‘Chuji’ dakika ya 30, Jerry Tegete dakika ya 69 na 89.
 
Mechi ya 19 ilikuja Oktoba 16, mwaka 2010, Ligi Kuu pia, Yanga ikishinda 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, bao pekee la Jerry Tegete dakika ya 70, wakati ya mechi ya 20 iliyokuja Machi 5, mwaka 2011, timu hizo zilitoka sare ya 1-1, Stefano Mwasyika akitangulia kuifungia Yanga kwa penalti dakika ya 59, kabla ya Mussa Mgosi kuisawazishia Simba dakika ya 73, ilikuwa ya Ligi Kuu pia.
 
Mechi ya 21 ilikuja Julai 10, mwaka 2011, Yanga ilishinda 1-0, Fainali Kombe la Kagame, mfungaji Mghana Kenneth Asamoah dakika ya 108, wakati mechi ya 22 ilikuja Agosti 17, mwaka 2011, Simba ikishinda 2-0, mabao ya Haruna Moshi ‘Boban’ dakika ya 15 na Felix Sunzu dakika ya 38 kwa penalti, kuwania Ngao Jamii.
 
Mechi ya 23 ilikuja Oktoba 29, mwaka 2011 na Yanga ikashinda 1-0, bao pekee la Davies Mwape dakika ya 75, Ligi Kuu pia na mechi ya 24 na ya mwisho Kaseja kudaka hadi sasa katika mapambano ya watani ni ile ya 5-0.
 

Mei 6, mwaka 2012, Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mabao ya Emmanuel Okwi dakika ya pili na 62, Felix Sunzu kwa penalti dakika ya 56, Juma Kaseja kwa penalti dakika ya 67 na Patrick Mafisango (marehemu) kwa penalti pia dakika ya 72. Kesho akidaka, itakuwa mechi ya 25, nani kama Kaseja?

BASI LA RS KUTOKA DAR-ES-SALAAM KWENDA BUKOBA LAPATA AJALI NA KUUWA WATU 3 NA KUJERUHI 24.

Gari la Rs katika muonekano baada ya ajali.
 WATU Watatu wamekufa papo hapo na wengine 24 wameruhiwa vibaya baada ya  Basi la Kampuni ya RS Bus Express linalofanya safari zake kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Bukoba  kugongana na Lori la Mizingo la Kampuni ya Dhaudho (Faw) katika kata ya Ngongwa Wilayani Kahama.

Ajali hiyo iliyotokea Katika eneo hilo ilihusisha Basi hilo lenye namba za usajili T 495 ATG pamoja na Lori lenye namba T 513 BNP ambalo likuwa likitokea Ushirombo Wilayani Bukombe mkoani Geita kwenda jijini Dar es Salaam majira ya saa 12.20 Asubuhi

Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Emanueli Endrew alisema kuwa mapaka kufikia majira ya saa nne za Asubuhi tayari alikuwa amepokea jumla ya maiti tatu pamoja na majeruhi 24.

Alisema kuwa baadhi ya majiruhi wamevunjika miguu huku Wanne wakiwa mahututi na kulazisha kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza kwa matibabu baada ya hali zao kuwa mbaya zaidi.

Kaimu Mganga Mkuu huyo aliwataja waliofariki duni katika ajali hiyo kuwa ni Edwin Stephano, Hamidu Yusuph ambaye alikuwa Dereva wa Lori la Mizigo pamoja na Zuraia Tuli (50) na kuongeza kuwa waliopelekwa katika Hospitali ya Bugando ni  Chabukana Raia wa Uganda, Makame Suliman ambaye ni Mwanajeshi, Fred Peter na Shafii Abdala.

Kwa mujibu wa Mashuhuda wa ajali walisema kuwa kiini cha ajali hiyo kuwa Dereva wa lorri la mizigo alikuwa akimkwepa mwendesha Baiskeli hali ambayo ilisababisha lori hilo kwenda upande ambao basi ilikuwapo.

Hata hivyo mmoja wa Majeruhi wa Ajali hiyo Johanes Ndyamukamu alisema kuwa kabla ya ajali hiyo Basi hilo likuwa lifukuzana na jingine la Sumry ambapo baada ya kulipita walikutana na Lori jingine ambalo lilikuwa limemkwepa mwendesha Baiskeli huyo na kuingia katika upande wao.

Hata hivyo Kaimu Maganga huyo wa Haspitali ya Wilaya ya Kahama Emanuel Endrew alisema kuwa taarifa zingine atazitoa baadaye ili kujua kama kuna majeruhi wengine ambao watapatiwa ruhusa baada ya kupatiwa matibabu.
MATUKIO KATIKA PICHA
                                 Baiskeli iliyosababisha ajali ikiwa imeachwa na mwenye nayo.

                                            Basi la RS katika muonekano wa ubavuni baada ya ajali.

                                  Kidole gumba na kikanyagio cha abiria mmoja baada ya kukatika.

Mmoja wa mashuhuda akiwasaidia askari polisi kupima ajali.
 
                                    Askari polisi akionyesha mguu uliokatika ukiwa ndani ya kiatu.

                     Miguu ya abilia iliyokatika  ikikusanywa na kuweka kwenye mfuko na askari polisi.

 Askari Polisi wakilinda amani na kuhakikisha vibaka hawaibi mizigo ya abiria,Mkono wa kulia ni askari wa kike akiwa amebeba mfuko uliojaa miguu na viungo vingine vya abiria vilivyokatika.

 Ubongo wa mmoja wa marehemu wa ajali hiyo ukiwa umemwagika ndani ya gari baada ya kichwa kupasuka.
 Wauguzi wakiwa katika harakati ya kuokoa maisha ya majeruhi waliofikishwa katika hospitali ya wilaya ya kahama.
                                                  Majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu.

         Mmoja wa majeruhi ambaye amekatika mguu akipata huduma kabla ya kupelekwa bugando.

Majeruhi aliyevunjika mguu akipata huduma ya kwanza.
 
 Kijana kutoka kampuni ya Kahama yote ya mjini kahama akimfariji jamaa yake ambaye amepata ajali.

 Mwonekano wa Roli ambalo limegongana uso kwa uso na basi la RS.
 Hii ndiyo hali halisi ya mwonekano wa roli la kampuni ya Dhaudho baada ya ajali hiyo.
 Wauguzi wa hospitali ya wilaya ya kahama wakiwa katika harakati ya kuokoa abiria ba kuwapa huduma ya kwanza.
Wananchi wakishudia ajali hiyo.

SIMBA WAPEWA BASI NA CHAKULA KIBOVU LAKINI BASSENA ASEMA TUTASHINDA


KOCHA HUYU WA ZAMANI WA SIMBA MOSES BASENA AMBAYE ALIIONGOZA SIMBA MWAKA JUZI KUSHIRIKO  MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO PALE ILIPOENDA KISHANSA MWAKA 2011-06-12 NA KUTOLEWA LAKINI KITU AMBACHO WALIKIZUNGUMZA NI KUHUSU EEEEEEEEH SIJUI TUMEISHWA CHAKULA KIBOVU TUMEPEWA MAJI MACHAFU UKIANGALIA PICHA HII KWA UNDANI UTAWAONA WACHEZAJI WA TIMU HII WAKIWA WAMESHIKILIA MATUMBO AKIWEMO OKWII,.JE HILI LINAWEZA LIKAISHA LINI KWANI TUMEONA HATA JUZI KOCHA WA YANGA MBELIGIJI BRANDTS KUSINGIZIA WAMELALA MZUNGU WA NNE KULE MBEYA SIJUI MSOSI LINASABABISHWA NA KINA NANII? KWA UPANDE WA MAKOCHA KUWA WANASINGIZIA VITU AMBAVYO HAVINA MSINGI WOWOTE EBU CHEKI HATA KWA WENZETU MAJUU BAADA YA KUPOKEA KIPIGO JUZI FERGI NAYE ASEMA MANENO.:FERGIE ataka Refa asiwe Msimamizi wa Muda kwenye Mechi!!
MECHI ILIPIGWA DAKIKA 94 SEKUNDE 28!!

JUMA JABU, BANKA NA WACHEZAJI WENGINE WAKIPASHA KWENYE UWANJA WA SHARK KINSHASA - CONGO

GOLIKIPA JUMA KASEJA AKIWA MAZOEZINI

KOCHA MOSES BASENA AKIWAONGOZA WACHEZAJI KATIKA MAZOEZI

VIONGOZI WA SIMBA WAKIPATA CHAKULA KATIKA HOTEL WALIYPFIKIA HAPA KINSHASA
EMMANUEL OKWI, KELVIN YONDAN NA JUMA NYOSSO WAKIPASHA



WACHEZAJI WA SIMBA WAKIPATA CHAI BAADA YA MAZOEZI YA LEO ASUBUHI

JUMA NYOSSO, SALUM KANONI NA JERRY SANTO WAKIPIGA TIZI

WADAU WA KLABU YA SIMBA WAKIWA KINSHASA WA PILI KUTOKA KULIA NI MAKAMU MWENYEKITI WA KLABU HIYO KABURU

KUELEKEA PAMBANO LA WATANI; MAMBO YALIVYOKUWA MEI 6, 2012 NA VIPIGO VINGINE VYA MBWA MWIZI ALIVYOPEWA YANGA

Okwi alikuwa mwiba kwa Yanga Mei 6


SIMBA na Yanga zinamenyana kesho katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambao utarushwa moja kwa moja na Televisheni ya Super Sport ya Afrika Kusini kuanzia saa 11:00 jioni. Kabla ya mchezo wa leo, timu hizo zilimenyana Mei 6, mwaka huu katika mchezo wa kufunga msimu, je unakumbuka mambo yalikuwaje siku hiyo? Bin Zubeiry anakukumbusha…
Kikosi cha Simba msimu uliopita kilichoipiga yanga bao 5-0..kutoka kushoto waliosimama ni felix sunzu,victor costa nyumba,,boban,,mafisango,,santo,,,na walioinama toka kushoto,,nyoso,,machaku,,kaseja,,cholo,maftah,na okwii
Mambo yalivyokuwa Mei 6, Taifa hadi 5-0...
ILIKUWA ni Mei 6, mwaka 2012 wakati Wekundu wa Msimbazi, Simba SC walipokabidhiwa Kombe lao la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa shangwe nzito, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kuwabwaga wapinzani wao wa jadi, Yanga mabao 5-0.
Mabao ya Simba yalifungwa na Emmanuel Okwi mawili, Juma Kaseja, Felix Sunzu na Patrick Mutesa Mafisango.
Hicho kilikuwa kipigo cha pili kikali kihistoria Simba wanaifunga Yanga, baada ya zile 6-0 za mwaka 1977.
Ilikuwa ni hoi hoi, nderemo na vifijo kuanzia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi kona mbalimbali za Jiji, rangi nyekundu na nyeupe zikiwa zimetawala na shangwe za Simba.
Hadi mapumziko, Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi dakika ya pili tu ya mchezo huo.
Okwi alimtungua kipa Mghana, Yaw Berko baada ya kutumia mwanya wa kuzubaa kwa mabeki wa Yanga mwanzoni mwa mchezo huo.
Katika kipindi hicho, Okwi alikuwa akimpita kwa urahisi beki mkongwe wa Yanga, Nsajigwa Shadrack Joel Mwandemele ambaye aliishia kumkwatua mara kwa mara, jambo ambalo lilimponza kwenda chumba cha kupumzikia akiwa ana kadi moja ya njano aliyopewa dakika ya 39.
Pamoja na kufungwa bao hilo, Yanga waliendelea kucheza kwa utulivu, wakigongeana pasi vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa, ingawa kikwazo kilikuwa Tanzania One, Juma kaseja.
Nafasi pekee nzuri katika kipindi hicho na ambayo Yanga wataijutia waliipata dakika ya 35, baada ya Mwanasoka Bora wa Uganda, Hamisi Kiiza kuwatoka vizuri mabeki wa Simba, lakini akiwa amebaki yeye na kipa, hesabu zake ziliendana na Kaseja.
Kiiza aliupelekea mpira upande wa kushoto wa kipa huyo bora Tanzania, ambaye naye akachupa upande huo huo na kuokoa.
Kipindi cha pili, Yanga walianza kwa mabadiliko, wakimtoa kipa Yaw Berko na kumuingiza Said Mohamed Kasarama, wakati Simba walimpumzisha Mwinyi Kazimoto na nafasi yake kuchukuliwa na Jonas Mkude.
Simba waliingia tena kwa kasi na kufanikiwa kupata mabao matatu ya haraka haraka, mawili yakipitia kwa Nsajigwa.
Bao la pili la Simba lilitokana na penalti, baada ya Nsajigwa Shadrack kumkwatua Okwi kwenye eneo la hatari na Felix Sunzu akaenda kufunga kwa penalti dakika ya 56.
Okwi alifunga bao la tatu dakika ya 62, baada ya kumtoka Nsajigwa Fusso na kumchambua kipa Said Mohamed Kasarama.
Baada ya bao hilo, kocha Fred Felix Minziro alipumzishwa Nsajigwa na kumuingiza Godfrey Taita Magina. 
Dakika ya 67 Uhuru Suleiman aliangushwa na Taita kwenye eneo la hatari na Juma Kaseja akaenda kufunga bao la nne kwa penalti. Patrick Mafisango (sasa marehemu) alifunga bao la tano kwa penalti pia dakika ya 72.
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Kelvin Yondan, Patrick Mafisango/Obadia Mungusa, Uhuru Suleiman, Mwinyi Kazimoto/Jonas Mkude, Felix Sunzu/Edward Christopher, Haruna Moshi ‘Boban’ na Emmanuel Okwi.
Yanga: Yaw Berko/Said Mohamed, Nsajigwa Shadrack/Godfrey Taita, Oscar Joshua, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Seif ‘Kijiko’, Nurdin Bakari, Haruna Niyonzima, Davies Mwape/Kenneth Asamoah, Rashid Gumbo na Hamisi Kiiza.
Naam, hivi ndivyo mambo yalivyokuwa Mei 6, 2012 na baada ya hapo Yanga wakafanya mabadiliko makubwa ya uongozi, wakimtoa Mwenyekiti wao wa wakati huo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga na kuweka safu mpya ya uongozi, chini ya Mwenyekiti Yussuf Manji.
Je, kesho tutarajie nini Uwanja wa Taifa, miamba hiyo ikikutana tena? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.
Okwi na Fusso siku hiyo...palikuwa patamu shandrack nsajigwa alikuwaga njia mpaka sasa hawamwamini katika kikosi kile pale aliposababisha bao za penalti
VIPIGO VINGINE VYA ‘MBWA MWIZI’ SIMBA WALIVYOICHAPA YANGA:
LIGI KUU BARA:
JULAI 19, 1977
Simba v Yanga
6-0
WAFUNGAJI:
Abdallah Kibadeni dk. 10, 42 na 89, Jumanne Hassan 'Masimenti' dk. 60 na 73, Selemani Sanga alijifunga dk. 20.
JULAI 2, 1994
Simba v Yanga
4-1
WAFUNGAJI:
Simba: George Masatu, Athumani China, Madaraka Selemani, Dua Saidi Yanga; Constantine Kimanda.
MACHI 31, 2002.
Simba Vs Yanga 4-1 (Kombe la Tusker)
WAFUNGAJI:
SIMBA: Mark Sirengo dk. 3 na 76, Madaraka Selemani dk. 32 na Emanuel Gabriel dk. 83.
YANGA: Sekilojo Chambua dk 16.
(Mechi hii ya fainali iliyohudhuriwa na rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, chupuchupu ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Mwamuzi wa mchezo huo, Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. Baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania, FAT).
MEI 6, 2012
Samba 5-0 Yanga SC
WAFUNGAJI:
Emmanuel Okwi (dk 2 na 62), Felix Sunzu (penalti 56), Juma Kaseja (penalti dk 67) na Patrick Mafisango (penalti dk 72)

QPR yadidimizwa mkiani!

Jumanne, 02 Oktoba 2012 10:46
 
BPL_LOGO>>MECHI YAWEKA REKODI: KADI za NJANO 8 Mechi moja Timu moja!
West Ham wamezidi kumletetea mchecheto Meneja wa Queens Park Rangers Mark Hughes wakati jana walipotua nyumbani kwao Loftus Road na kuwatandika bao 2-1 na kuwaacha wakimaliza Mechi hiyo wako Mtu 10 na pia kuendelea kubaki mkiani mwa Msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuambulia Pointi mbili tu katika Mechi 6.
++++++++++++++++++++++++++
KADI za KIHISTORIA:
• West Ham ndio Timu ya kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kupata Kadi za Njano 8 katika Mechi moja.
• QPR wamezoa jumla ya Kadi Nyekundu 10 tangu mwanzo mwa Msimu wa 2011-12 ambazo ni Kadi 3 zaidi ya Timu nyingine yeyote.
++++++++++++++++++++++++++
West Ham walianza vyema na kupata bao katika Dakika ya 3 tu alilofunga Matt Jarvis na Ricardo Vaz Te akapiga bao la pili kabla ya mapumziko.
++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
QPR 1
-Taarabt 57′
WEST HAM 2
-Jarvis 3′
-Vaz Te 35′
++++++++++++++++++++++++++
Baada ya mapumziko, QPR wakazinduka na kukaza buti hasa baada ya kuwaingiza Adel Taarabt na Samba Diakite, na Taarabt ndie alieipa QPR bao lao moja kwa shuti kali na zuri.
Hata hivyo, QPR walipata dosari pale Samba Diakite alipobandikwa Kadi za Njano mfululizo na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Ushindi huu umewapaisha West Ham hadi nafasi ya 7 na kuleta faraja kwa Meneja Sam Allardyce ambae pia alifurahi kurudi Uwanjani kwa Straika wake mpya wa mkopo kutoka Liverpool, Andy Carroll, ambae alumia katika Mechi yake ya kwanza kuichezea West Ham na jana alimudu kucheza Dakika 20 za mwisho.


VIKOSI;
Queens Park Rangers: Julio Cesar, Hill, Onuoha (Hoilett - 84' ), Nelsen, Park Ji-sung (Diakite - 55' ), Wright-Phillips (Taarabt - 56' ), Granero, Faurlin, M'bia, Cisse, Zamora
Akiba: Green, Diakite, Taarabt, Ephraim, Ehmer, Mackie, Hoilett

West Ham United: Jaaskelainen, Reid (Tomkins - 23' ), O'Brien (McCartney - 35' ), Collins, Demel, Nolan, Jarvis, Noble, Diame, Cole, (Carroll - 72' ), Vaz Te
Akiba: Henderson, McCartney, Tomkins, Benayoun, O'Neil, Carroll, 11 Maiga
Refa: Clattenburg
Watazamaji: 17,363

Aguero: “Marefa wanabeba Wazawa”, Gerrard: “Ubingwa ni Miujiza!”

Jumatatu, 01 Oktoba 2012 18:00
   
Wakati Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard akikiri Liverpool kutwaa Ubingwa itakuwa ni miujiza, Straika wa Mabingwa Manchester City STEVEN_GERRARD_SHOUTINGanaetoka Argentina, Sergio Aguero, ameungama Marefa huko England wanawapendelea Wachezaji wa Kiingereza.
Gerrard na Ubingwa Liverpool
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amesema itakuwa ni miujiza ikiwa Klabu hiyo itatwaa Ubingwa kabla hajastaafu.
Liverpool, ambao mara ya mwisho kutwaa Ubingwa wa England ilikuwa Mwaka 1990, wameuanza Msimu huu kwa kusuasua na wapo nafasi ya 14 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu.
Gerrard, Miaka 32, ametamka: “Itakuwa ni miujiza tukichukua Ubingwa kabla sijastaafu.”
Gerrard amekiri kuibuka kwa Timu kama Manchester City na kutwaa Ubingwa ndiko kumezidisha zaidi ugumu wa Liverpool kutwaa Taji hilo.
++++++++++++++++++++++++++++
Gerrard na Liverpool:
>>Aligunduliwa akichezea Timu ya Whiston Juniors akiwa na Miaka 9.
>>Alisaini Mkataba wa kuwa Mchezaji wa Kulipwa wa Liverpool Mwaka 1997.
>>Novemba 1998 alichezea Liverpool mara ya kwanza Mechi na Blackburn. >>Mwaka 2001 alishinga ‘TREBO’ Kombe la Ligi, FA Cup na UEFA Cup.
>>Octoba 2003 ralimbadili Sami Hyypia na kuwa Nahodha wa Liverpool.
>>Alipiga Bao na kuisaidia Liverpool kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2005
>>Alipiga Bao mbili Liverpool ilipotwaa FA Cup Fainali na West Ham Mwaka 2006.
>>Octoba 2008 alipiga Bao lake la 100 kwa Liverpool Mechi na PSV Eindhoven.
>>Asaini Mkataba mpya utakaombakisha Liverpool kama Balozi akistaafu.
++++++++++++++++++++++++++++
Amesema: “Si Manchester United na Arsenal pekee, sasa wapo Man City, Chelsea na Tottenham. Newcastle nao wamekuja.”
Aliongeza: “Tulikuwa wa 8 Msimu uliopita. Kama Msimu huu ukienda vyema, tukiwa na bahati pia na kupanda kidogo, tunaweza kufikia 4 bora. Lakini hata kama tukifika 4 bora nitakuwa na Miaka 33 mwishoni mwa Msimu na hiyo ndio maana tunahitaji miujiza kuwa Mabingwa kabla sijastaafu. Lakini nitaendelea kupigana na tutaona nini kitatokea!”


Sergio Aguero na Marefa
Sergio Aguero, Straika wa Manchester City anaetoka Argentina, anaamini Wachezaji wa Kiingereza wanapendelewa na Marefa ukilinganisha na wale kutoka nje.
Aguero ametamka: “Huwa sipendi kujihusisha na matatizo ya Marefa. Lakini hapa Marefa wanapendelea Wachezaji wa England. Lakini hatuna la kufanya ila kuendelea kucheza tu!”
Tuhuma hizi za Aguero zinafuatia matukio kwenye Mechi ya Ligi Kuu kati ya Fulham na Man City ambayo Wachezaji wenzake kutoka Argentina, Pablo Zabaleta na Carlos Tevez, walidai Penati baada ya kufanyiwa madhambi lakini Refa hakutoa.
Lakini alipohojiwa kama hadhani kuwa Wachezaji wa nje ya England huwa wanajidondosha kuhadaa Marefa, Aguero alijibu: “Pengine ndio. Inatokea lakini hapa si sawa wengine hupendelewa!”
Madai haya ya Aguero yamekuja Wiki tu baada ya Wachezaji wa England wanaochezea Liverpool, Steven Gerrard na Glen Johnson, kutamka kuwa Mchezaji mwenzao wa Liverpool anaetoka Uruguay, Luis Suarez, ni mhanga wa sifa yake mwenyewe na ndio maana Marefa hawamsapoti na kumpa Penati kutokana na sifa yake ya kuhadaa Marefa kwa kujiangusha ovyo.
Mara ya mwisho kwa Aguero kupewa Penati ni Mwezi Machi walipocheza na Arsenal na tangu wakati huo Marefa wamekuwa hawampi na wakati mwingine kumtwanga Kadi ya Njano kwa kujidondosha.