Wednesday, December 12, 2012

MWINYI KAZIMOTO KUCHUKUA NAFASI YA MRISHO NGASSA EL MERREIKH

Baada ya mchezaji Mrisho Ngassa kuingia mitini huku taarifa za kuaminika kutoka kwa vyanzo vilivyo karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga vikisema - Mrisho amekubali kimsingi kujiunga na mabingwa wa Afrika mashariki na kati baada ya mkopo wake utakapoisha katika klabu ya Simba, hivyo dili lake la kujiunga na El Merreikh kuota mbawa - leo hii kuna taarifa kutoka klabu ya Simba kwamba El Merreikh wameonesha nia ya kumtaka nyota Mwinyi Kazimoto kama mbadala wa Haruna Niyonzima ambaye walikuwa wakimtaka lakini ameamua kubaki kwenye klabu yake.

Akizungumza na mtandao chanzo cha habari kutoka Simba kinasema kwamba, kumefanyika mazungumzo ya mwanzo tu na El Merreikh wameonekana kuvutiwa na Mwinyi kwa kuwa walikuwa wanatafuta kiungo baada ya Niyonzima kukubali kuendelea kuichezea Yanga.

"Simba tupo tayari kumuuza Mwinyi Kazimoto kwa sababu klabu yetu inaamini katika kutoa nafasi kwa wachezaji kujiendeleza zaidi. Mazungumzo yanaendelea na kama kila kitu kikiwa sawa basi hivi karibuni Mwinyi atakuwa mchezaji mpya wa El Merreikh."

ATUDO AANGUKA MIWILI AZAM FC

Atudo
BEKI wa kimataifa wa Kenya, Joackins Atudo amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam FC ya Dar es Salaam.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrissa amesema mida hii kwamba, beki huyo kutoka Tusker ya Kenya, amekwishamalizana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kutua leo Dar esw Salaam.
Tayari Azam imekwishafikia makubaliano na mshambuliaji wa Uganda, Brian Umony kusaini mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
Awali, Umony alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
Umony alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu. Azam pia ina mpango wa kusajili Wakenya wengine wawili, Jockins Atudo na Humphrey Mieno. 

UGANDA ONE ANAMWAGA WINO LEO SIMBA SC

Dhaira anajitia kitanzi leo Msimbazi
KIPA namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira leo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia Simba baada ya kutua jana jioni mjini Dar es Salaam akitokea kwao Uganda.
Akizungumza  jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba, baada ya kusaini leo, Dhaira atarejea kwao mara moja kwa ajili ya kwenda kujiandaa kuja kuanza kazi rasmi Msimbazi.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) aliyepigana vita dhidi ya Uganda, alisema kwamba Dhaira hatachelewa kurejea kuanza kumtumikia mwajiri wake mpya, bali atakuja mapema.
Dhaira amekwishasema atafurahi kujiunga na Simba kwa kuwa ni klabu kubwa Afrika na inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na angependa kuungana na Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi huko.
Tayari Simba SC imefikia makubaliano na kipa huyo namba moja wa Uganda, aliyemaliza mkataba wake na klabu ya I.B.V FC ya Iceland na amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau ambalo halijafahamika.
Dhaira alisema kwamba amefikia makubaliano na Simba kusaini mkataba wa miaka miwili kuja kuanza maisha mapya Dear es Salaam.
Dhaira aliyeibukia Express ya Uganda mwaka 2006, mwaka 2008 alihamia U.R.A. pia ya Uganda, ambayo aliichezea hadi mwaka 2010 alipohamia Ulaya.
Ikimpata Dhaira, Simba SC itakuwa imepata kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisotoshwa peke yake bila kupumzika. Na hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema hataki tena kuchezea Simba.
Lakini pamoja na matatizo hayo, Kaseja aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli.  

BEKI LA NGUVU LA KENYA LATUA KUSAINI AZAM LEO

Humphrey Mieno yupo kwenye rada za Azam pia

BEKI mmoja matata wa Tusker ya Kenya, anatarajiwa kutua leo Dar es Salaam kwa ajili hya kusaini mkataba wa kuichezea Azam FC ya Dar es Salaam.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa alisema jana kwamba, beki huyo mzuri atafichuliwa leo  baada ya kusaini mkataba, ila kwa sasa wanaendelea kuweka kapuni jina lake.

YANGA YAANZA KAZI UHAI CUP LEO

MICHUANO ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom, inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi Kundi C kupigwa.
Kagera Sugar itacheza na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni. (Ratiba nzima imeambatanishwa)
Timu zinazoshiriki michuano hiyo iliyoanza jana na itamalizika Desemba 23, mwaka huu., zimegawanywa katika makundi matatu, Kundi A likiwa na timu za Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans, Kundi B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.
Katika mechi za jana, Azam FC ilianza vema baada ya kuilaza Mgambo Shooting mabao 2-0 jioni ya leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, shukrani kwao, Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ na Reyna Mgugingila, wafungaji wa mabao hayo leo katika mchezo huo wa Kundi B.
Katika mechi za asubuhi jana, Coastal Union ya Tanga nayo ilianza vizuri baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1, mchezo wa Kundi A uliopigwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma na African Lyon iliichapa mabao 4-0 Polisi Moro.

Al-Ahly YAKUNG'UTWA 1 NA Corinthians YATUPWA NJE UBINGWA WA DUNIA

Pichani ni Mshabuliaji wa Corinthians  Paolo Guerrero akishangilia mara baada ya kufunga bao la Ushindi katika michuano ya vilabu bingwa ya dunia inayofanyika huko Tokyo japan  Dhidi ya wawakilishi wa afrika Al-Ahly ya Masir alifunga goli hilo kwa kichwa .

Mabingwa wa  America Kusini   Corinthians wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali  ya michuano ya kombe la dunia kwa vilabu  mara baada ya kuifunga Timu ya  Al-Ahly    1-0 mchana wa leo huko   Toyota, Japan.

Kipigo hichi kinaifanya  Al-Ahly's kutupwa nje ya michuano hiyo pasipo wao kutarajia kwani mabingwa hao wa Msiri walikuwa wakicheza bila ya mashabiki kwa kipindi kirefu katika ligi yao ya nyumbani baada ya kutokea vifo vya watu sabini mwezi february huko Port Said .

Goli pekee katika mchezo huo lilifungwa na kijana kutoka Peru   Jose Paolo Guerrero katika dakika ya 29 baada ya kufunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya   Douglas' nje kidogo ya kisanduku cha penati .

Ushindi huu unaama kuwa timu hii kutoka  Sao Paulo itacheza na Na mabingwa ulaya Chelsea kutoka uingereza au Mabingwa wa Amerika ya kati Monterrey ya mexico siku ya jumapili Huko Yokohama .

Corinthians, ni washindi wa kombe la   Copa Libertadores kwa Mara ya kwanza Tangu mwaka 2000 katika historia yao ya hivi karibuni  wakishangiliwa na maelfu ya mashabiki  walisafiri kutoka   Brazil.

Al-Ahly sasa wanatakiwa kuweka nguvu zao siku ya jumapili kwani nafasi yao pekee kwa sasa niku tafuta angalau nafasi tatu katika mashindano hayo   mwaka 2006 mabingwa hawa mara saba wa afrika walishika nafasi ya tatu

Kwa upande mwinge  Corinthians  watakuwa na matumani ya kuwa klabu yao inaweza kurejea yale waliyofanya wakiwa na Mkomgwe wa soka Brazil Romario pale walipotwaa ubingwa huo  katika  ardhi ya  nyumbani

Katika mechi ya mapema  timu mwenyeji ya  Japan's Sanfrecce Hiroshima -- ambao walifungwa na  Al-Ahly katika hatua ya Robo ya  fainali ilikamata nafasi ya tano baada ya kufumua 3-2   Ulsan Hyundai ya  South Korea.

GOALNE TECH:NI KUPOTEZA PESA PLATINI

Rais wa UEFA  Michel Platini amepinga vikali na amesema hata unga mkono matumizi ya utumiaji wa teknoloia ya ugunduzi wa goli Barani ulaya ,na ameelezea kuwa  juhudi hizo za fifa ni za kupoteza fedha pasipo na sababu ya msingi  ”. 

Platini ambaye amepewa jina la mlopkaji amekuwa akipinga juhudi hizo za fifa kutaka kuleta teknolojia ya ugunduiz wa goli kuvuka mstari  na amesema ni kheri wangejikita katika kuongeza waamuzi kuwa watano. 

Amesema hayo Katika ufunguzi wa kombe la dunia la vilabu huko japana vile vile kunafanyika majaribio ya mifumo mifumo aina ya ugunduzi wa goli wa  kwanza ni – GoalRef,  ambao hutumia sumaku kugundua kama goli limeingia au halijaingia na ya pili ni  jicho la samaki ambayo yenyewe hutumia vinasa picha mwendo sita mpaka nane (Moving Camera ) kutoka Engo tafauti  . 

 Platini, ambaye yupo asia kutia  saini makubaliano ya kupinga  matumizi ya mifumo hiyo na  (AFC) shirikisho la soka bara la Asia katika makao makuu yake huko   Bukit Jalil, ili kundelea na kusisitiza kuwa na msimamo mmoja wa kupinga kile wanaachookitaa ni upotevu wa fedha  

Platin  --- “itagharimu yuro   50mil katika kulipgia upatu wazo hilo katika mashindano ya vilabu bingwa barani la ulaya na ya kimataifa na itachukua miaka mitano anasema  Platini. 

'' Ni kheri nichukua mil yuro  mil 50 na kuwekeza katika maendeleo ya  soka la vijana  … Huo utakuwa utumiaji Mzuri wa pesa lakini sio kutumia fedha nyingi kiasi hicho  kwa tukio linalotokea kwa mwaka mara mbili au mara moja . 

“Nina amini  bora kutetea waamuzi wawe watano badala ya kuja na mfumo huo 

“Kama mwamuzi atasimama mita moja kutoka kwenye goli  atakuwa na uwezo wa kuona kama goli limeingia au halijaingia .” 

lakini wakati  UEFA hawataki mchakato hu rais wa shirikisho la asia ambaye anashikiria madaraka kwa  muda Zhang Jilong anaonekana kukubaliana na wazo la fifa . 

“Tutazama mafanikio katika michuano hii ya Tokyo na tutapata jibu kama tutumie mfumo huu  au tuachanane nao ,” aliongeza  Jilong.

Gomez: kutwaa taji la Bundesliga ndio kila kitu si yeye kucheza na Pazzini awataka AC Milan wasibweteke na ushindi mfululizo.

Mshambuliaji wa Mario Gomez amesema kwake yeye kusugua benchi sio tatizo,  fahari yake ni kuona Bayern Munich inatwaa taji la Bundesliga mwisho wa msimu.

Mshambuliaji huyo amekuwa akisugua benchi baada ya kupata majeraha tangu siku za mwanzo za kuanza msimu msimu wa 2012-13 lakini amesisistiza hilo si tatizo kikubwa ni kutwaa taji kuliko kurejea katika kikosi cha kwanza.

Amenukuliwa na gazeti la Bild akisema

"ki ukweli lengo langu kubwa ni kushinda taji la Bundesliga. Mambo mengine si muhimu kuliko taji".

Gomez ameshinda mataji mawili mpaka sasa akianza kupata taji msimu wa 2006-07 akiwa na Stuttgart na baadaye akiwa na Bayern msimu wa 2009-10.

Pazzini: AC Milan inabidi ikaze buti

Giampaolo Pazzini amesisitiza kuwa AC Milan inabidi kuongeza uwezo wake wa kiuchezaji katika wiki za hivi karibuni ili kupunguzo kupoteza michezo kama ilivyokuwa katika miezi ya mapema ya kuanza ligi msimu huu wa 2012-13.

Milani imekuwa ikifanya vizuri katika mfulilizo wake wa michezo saba ya ligi kuu ya Italia ‘Serie A’ katika siku za hivi karibuni, lakini Pazzini ameonya hiyo isiwe kigezo cha kubweteka na matokeo hayo katika sehemu iliyosalia ya msimu

Amenukuliwa na Sky Sport Italia akisema

"tulianza vibaya na morali ilikuwa chini na matokeo hayakuwa mazuri"

Milan watarejea katika mfululizo wa michezo ya Serie A nyumbani dhidi ya Pescara jumapili.

SANTOS YAMTANGAZIA DAU ROBINHO.

RAIS wa klabu ya Santos ya Brazil Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro amesema kuwa klabu yake hiyo imetangaza dau kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya AC Milan ya Italia Robinho na kumrejesha nyumbani katika klabu ambayo ndio alianza kucheza soka. Ribeiro amekiri kuwa dau hilo walilotoa limeonekana ni dogo kwa mahitaji ya mchezaji huyo mwenye miaka 28 pamoja na Milan lakini hiyo ni hatua ya kwanza katika mbio za kutaka kumrejesha nyumbani Robinho ambaye ameshinda mataji mawili ya ligi akiwa na timu hiyo mwaka 2002 na 2004. Rais huyo amesema kuwa tayari wameshatuma barua rasmi kwa Milan na anaamini kuwa watafikia makubaliano mwishoni kwani Robinho ameonyesha nia ya kutaka kurejea nyumbani baada ya kucheza Ulaya kwa kipindi kirefu. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil pia aliwahi kucheza katika vilabu vya Real Madrid ya Hispania kuanzia mwaka 2005 mpaka 2008 na kutimkia Uingereza katika klabu ya Manchester City ambayo aliondoka mwaka 2010 na kwenda Milan. 

FERGUSON AMNYATIA WALCOTT.

KLABU ya Manchester United imeingia katika kinyang’anyiro cha kumgombea winga wa Arsenal Theo Walcott kama walivyofanya wakati walipomchukua Robin van Persie Agosti mwaka huu. Meneja wa United Sir Alex Ferguson amenuia kumchukua winga huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye mkataba wake unaishia mwishoni mwa msimu huu. Walcott akama ilivyokuwa kwa Van Persie amekataa kusaini mkataba mpya mpya ambao utamuwezesha kulipwa kiasi cha paundi 75,000 kwa wiki na kudai kuwa kama klabu hiyo inamuhitaji basi haina budi kumlipa paundi 100,000 kwa wiki. Liverpool, Manchester City na Chelsea zote zimeonyesha nia ya kumsajili winga huyo lakini United ndio wanaonekana wana nafasi kubwa ya kumnyakuwa baada ya Walcott mwenyewe kuonyesha kuvutiwa na klabu hiyo.

WENGER AKATAA KUWALAUMU WACHEZAJI WAKE BAADA YA KUTOLEWA BRADFORD.

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amewatetea wachezaji wake baada ya kutolewa na Bradford City kwa changamoto ya mikwaju ya penati katika mchezo war obo fainali ya Kombe la Ligi lakini amekiri kuwa tatizo la umaliziaji nalo lilichangia kupoteza mchezo huo. Arsenal ilitolewa kwa kufungwa matuta 3-2 baada ya wachezaji watatu wa timu hiyo kukosa penati na kocha huyo raia raia wa Ufaransa analaumu uwezo wa wachezaji wake kutumia nafasi walizopata kuwa ndio chanzo kikubwa cha kufungwa. Akiohijiwa mara baada ya mchezo huo Wenger huo Wenger amewasifu wapinzani wao  Bradford kwa kuanza mchezo vyema na kupata bao la mapema halafu kwa kuwadhibiti vyema washambuliaji wake ili wasilete madhara langoni kwao. Wenger alikataa kuwalaumu wachezaji wake kwa kucheza chini ya kiwango kwani walipata wakati mgumu kutokana na Bradford kuzuia karibu muda wote wa mchezo huo hivy kuwapa wakati mgumu wapinzani wao kuwafunga. Kombe la Ligi ndio pekee Arsenal ilikuwa ikipewa nafasi ya kulinyakuwa ili kukata kiu ya miaka saba ya kukosa taji lolote lakini bado wana nafasi nyingine katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambayo wameingia katika hatua ya timu 16 bora.

FUPI za LEO: Wright, Wenger, Fergie na Kiboko kwa Wabaguzi!!

WENGER_AHIMIZA12WRIGHT ATAKA BODI ARSENAL KUJIUZULU!
Aliekuwa Mchezaji wa Arsenal, Ian Wright, ametaka Bodi ya Arsenal kujiuzulu kutokana na aibu ya kutolewa kwenye CAPITAL ONE CUP na Timu ya Ligi, Daraja la 4, Bradford, hapo jana.
Wright, ambae ndie Mchezaji wa Pili katika historia ya Arsenal ya kufunga Bao nyingi, amesema ili kufuta ukame wa Miaka 8 bila Kombe lazima iondoke na arudishwe aliekuwa Makamu Mwenyekiti David Dean.
Pia, Wright amedokeza sasa upo uwezekano mkubwa wa Arsene Wenger kuiongoza Arsenal na kumaliza Ligi ikiwa chini kwenye Msimamo na hasa amemponda kwa kukataa kumchukua Dennis Bergkamp kama mmoja wa Makocha Klabu hiyo.
Wright amelalamika: “Wenger amemkataa Bergkamp!”

WENGER: HASIKII AIBU KUTOLEWA NA BRADFORD!!
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amedai Timu yake haina haja ya kusikia aibu kwa kutolewa na Timu ya Daraja la Chini Bradford kwenye CAPITAL ONE CUP.
Hapo jana, kwenye Robo Fainali, Arsenal ilitoka sare Bao 1-1 na Bradford katika Dakika 120 na kutupwa nje kwa Mikwaju ya Penati 3-2.
Lakini Wenger amedai: “Tulifanya kila jitihada katika Dakika 120 na Bradford wanastahili pongezi. Unasikia fedheha ikiwa hukujaribu.”

FERGIE KUIVAMIA TENA ARSENAL??
FERGIE_na_SIMU
Zipo tetesi nzito kuwa Sir Alex Ferguson yupo mbioni kumnasa Winga hatari wa Arsenal, Theo Walcott, Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho litapofunguliwa ili afuate nyayo za aliekuwa Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie, ambae alitua Manchester United, bila kutarajiwa, Mwezi Agosti.
Hadi sasa, Walcott, ambae Mkataba wake na Arsenal unamalizika Mwezi Juni Mwakani, yupo kwenye mvutano mkubwa na Klabu hiyo kuhusu kusaini Mkataba mpya huku ikidaiwa anataka alipwe Mshahara mkubwa kinyume na msimamo wa Arsenal kuhusu Mishahara ya Wachezaji.
Walcott, Miaka 23, Kisheria atakuwa huru kuanzia Mwezi Januari kuongea na kufikia makubaliano na Klabu yeyote inayomtaka na Mkataba wake na Arsenal ukimalizika yu huru kuondoka bila Arsenal kupata Senti hata moja.
Ukweli huu unaweza ukailazimishe Arsenal imuuze Mwezi Januari ili iambue chochote kuliko kumuona akiondoka bure Mkataba wake ukimalizika.

WABAGUZI KULA 5!!
KUFUATIA majadiliano kati ya Chama cha Soka England, FA, na kile Chama cha Soka cha Wachezaji wa Kulipwa, PFA, sasa Wachezaji wakosaji wanaohusishwa na makosa ya Ubaguzi watafungiwa si chini ya Mechi 5 ikiwa mapendekezo hayo yatapitishwa rasmi.
Pia, Kikao hicho kilijadili uwezekano wa kuwapiga msasa Makocha na Wachezaji wanaotoka nje ya England ili kuwaweka sawa kuhusu Utamaduni wa Kiingereza na pia kuwekwa Vipengele kwenye Mikataba ya Wachezaji wakitakiwa kutokuwa Wabaguzi na wakipatikana na hatia kwa makosa ya Ubaguzi wanaweza kutimuliwa.
+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:  
Jumamosi 15 Desemba 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Newcastle v Man City
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Aston Villa
Man United v Sunderland
Norwich v Wigan
QPR v Fulham
Stoke v Everton
Jumapili 16 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Tottenham v  Swansea
[SAA 1 Usiku]
West Brom v West Ham
Jumatatu 17 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Reading v Arsenal
+++++++++++++++++++++++
RATIBA BPL kwa VINARA:
MAN CITY MAN UNITED CHELSEA
Des 15 Newcastle v City
Des 22 Man City v Reading
Des 26 Sunderland v City
Des 29 Norwich v Man City
Jan 1 Man City v Stoke
Des 15 Man v Sunderland
Des 23 Swansea v Man U
Des 26 Man v Newcasctle
Des 29 Man Utd v WBA
Jan 1 Wigan v Man Utd
Des 23 Chelsea v Villa
Des 26 Norwich v Chelsea
Des 30 Everton v Chelsea
Jan 2 Chelsea v QPR

ZAMBIA FA: REKODI ya MESSI ni ya CHITALU!!

GODFREY_CHITALU>>WADAI CHITALU NDIE MFUNGAJI BAO NYINGI, 107 MWAKA 1972!
Chama cha Soka cha Zambia, ZFA, kimedai kuwa Straika wao Godfrey Chitalu  ndie anaeshikilia Rekodi ya kufunga Bao nyingi ndani ya Mwaka mmoja wa Kalenda na si Lionel Messi kama inavyoshabikiwa.
Wikiendi iliyopita, Messi alifunga Bao lake la 86 kwa Mwaka 2012 na kuipiku Rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Mjerumani Gerd Muller alipofunga Mabao 85 Mwaka 1972 lakini sasa Zambia wameibuka na kudai Rekodi hiyo ya Goli nyingi bado inashikiliwa na Godfrey Chitalu aliyoiweka Mwaka 1972 kwa kufunga Bao 107 wakati akiichezea Kabwe Warriors na Timu ya Taifa ya Zambia.
Msemaji wa ZFA amedai: “Tunayo Rekodi hii, imerekodiwa Zambia lakini, bahati mbaya, haikurekodiwa Dunia nzima!”
ZFA imesema kuwa sasa wameunda Tume huru kuihakiki Rekodi ya Chitalu kuonyesha kila Mechi aliyofunga Goli na matokeo ya Tume hiyo yatatumwa CAF na FIFA ili wadhihirishe ukweli wa madai yao.
Godfrey Chitalu alifariki Mwaka 1993 kwenye Ajali ya Ndege iliyowaua pia Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zambia huko Nchini Gabon.

FIFA KLABU BINGWA DUNIANI: Corinthians kucheza Fainali!

>>WABRAZIL waifunga Al Ahly 1-0!!
>>ALHAMISI: Chelsea v Monterrey!!
FIFA_CLUB_WORLD_CUPKatika Nusu Fainali ya Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani iliyochezwa leo Uwanja wa Toyota, Japan, Klabu ya Brazil, Corinthians, iliwafunga Mabingwa wa Afrika, Al Ahly, kwa Bao 1-0 na sasa wanangojea Mshindi wa Nusu Fainali nyingine itakayochezwa Alhamisi kati ya Chelsea na Monterrey ya Mexico.
Bao la ushindi la Corinthians lilifungwa na Straika kutoka Peru Paolo Guerrero kwa kichwa katika Dakika ya 30 na kuibua furaha kubwa mbele ya Mashabiki 20,000 wa Corinthians waliokuwemo Uwanjani.
+++++++++++++++++++++
RATIBA:
[SAA za BONGO]
Jumatano Desemba 12
MSHINDI wa 5:
Usain Hyundai 2 Sanfrecce Hiroshima 3
NUSU FAINALI
Al Ahly 0 Corinthians 1
Alhamisi, Desemba 13
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey v Chelsea
MSHINDI wa 3
Desemba 16
[Uwanja wa Yokohama]
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Al Ahly v Chelsea/Monterrey
FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Corinthians v Chelsea/Monterrey
+++++++++++++++++++++
Katika Mechi nyingine iliyochezwa awali leo, Usain Hyundai ya Korea ya Kusini ilifungwa Bao 3-2 na Sanfrecce Hiroshima ambao sasa wamenyakua nafasi ya 5.
Kwa kufungwa leo kwenye Nusu Fainali, Al Ahly watacheza Mechi ya kutafuta Mshindi wa 3 hapo Jumapili.
+++++++++++++++++++++
MABINGWA WALIOPITA:
-2000 - Corinthians
-2005 - Sao Paulo
-2006 - Internacional
-2007 - AC Milan
-2008 - Manchester United
-2009 - Barcelona
-2010 - Inter Milan
-2011 – Barcelona
++++++++++++++++++
KLABU BINGWA DUNIANI 2012
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI:
Chelsea-BINGWA ULAYA
Corinthians-BINGWA MAREKANI ya KUSINI
Monterrey-BINGWA MAREKANI ya KATI NA KASKAZINI
Auckland City-BINGWA KANDA ya OCEANIA
Usain Hyundai-BINGWA-Barani Asia
Al Ahly-BINGWA-Barani Afrika
Sanfrecce Hiroshima-BINGWA-Japan J-LIGI
RATIBA/MATOKEO:
Raundi ya Mchujo - Desemba 6, Yokohama
Sanfrecce Hiroshima 1 Auckland City 0
ROBO FAINALI - Desembar 9, Toyota
Usain Hyundai 1 Monterrey 3
Sanfrecce Hiroshima 1 Al Ahly 2
MSHINDI wa 5- Desemba 12, Toyota
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai 2 Sanfrecce Hiroshima 3
NUSU FAINALI
Desemba 12, Toyota
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly 0 Corinthians 1
Desemba 13, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey v Chelsea
MSHINDI wa 3 - Desemba 16, Yokohama
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
FAINALI - Desemba 16, Yokohama
[Saa 7 na Nusu Mchana]
 
CAPITAL ONE CUP: Ukame Makombe Arsenal kuendelea!

CAPITAL_ONE_CUP-BEST>>BRADFORD 1 ARSENAL 1, MATUTA ARSENAL HOI 3-2!!
>>BRADFORD, VILLA ZATINGA NUSU FAINALI!!
>>LEO ni Swansea v Middlesbrough
>> BPL KIPORO: Sunderland 3 Reading 0
Bradford, Timu inayocheza Ligi 1 ikiwa ni nafasi 65 chini ya Arsenal iliyo Ligi Kuu England, jana iliitupa Arsenal nje ya CAPITAL ONE CUP kwa kuishinda kwa Mikwaju ya Penati 3-2 kufuatia sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo na kuhakikisha ukame wa Arsenal wa kutotwaa Kombe lolote kubwa wa tangu Mwaka 2005 kuendelea.
++++++++++++++
MAGOLI:
Bradford 1
-Thompson Dakika ya16
Arsenal 1
-Vermaelen Dakika ya  88
++++++++++++++
Katika Mechi hiyo iliyochezwa, Coral Windows Stadium, Nahodha wa Arsenal Thomas Vermaelen ndie aliekosa Penati muhimu na kuifanya Arsenal imeshinda Mechi moja tu katika Mechi zake 6 za mwisho na pia kuifanya Bradford kuwa Timu ya kwanza toka Madaraja ya chini kutinga Nusu Fainali ya Mashindano haya tangu Wycombe ilipofanya hivyo Mwaka 2006/7.
Norwich 1 Aston Villa 4
Aston Villa wametinga Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP baada ya kuichapa Norwich City Bao 4-1.
++++++++++++++
MAGOLI:
Norwich 1
-Morison Dakika ya 19
Aston Villa 4
-Holman Dakika ya 21
-Weimann 79 na 85
-Benteke 90
++++++++++++++
Hii ni mara ya pili katika Minne kwa Aston Villa kutinga Nusu Fainali ya Mashindano haya.
CAPITAL ONE CUP-Robo Fainali:
RATIBA/MATOKEO:
Jumanne Desemba 11
Norwich 1 Aston Villa 4
Bradford 1 Arsenal 1 [Bradford yasonga Penati 3-2]
[Mechi zote kuchezwa Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumatano Desemba 12
Swansea v Middlesbrough
Jumatano Desemba 19
Leeds United v Chelsea
+++++++++++++++++++++++++
Mechi pekee ambayo inazikutanisha Klabu za Ligi Kuu England ni ile kati ya Norwich City na Aston Villa.
+++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU za CAPITAL ONE CUP:
-KABLA LILIKUWA ni Carling Cup na Bingwa Mtetezi alikuwa ni Liverpool.
-Linaitwa CAPITAL ONE CUP kwa sababu Mdhamini wake ni Kampuni ya masuala ya Fedha, Capital One.
-Linashirikisha Timu za Ligi za juu England 92 kwa mtindo wa Mtoano [Timu 20 toka Ligi Kuu na 24 kila moja kutoka Madaraja ya Npower, Ligi 1 na 2.
-Bingwa wa michuano hii hucheza EUROPA LIGI Msimu unaofuata kuanzia Raundi ya Tatu ya Mtoano.
+++++++++++++++++++++++++
BPL KIPORO: Sunderland 3 Reading 0
Meneja wa Sunderland, Martin O'Neill, amesherehekea Mwaka mmoja wa kuwepo Klabuni hapo kwa ushindi mtamu wa Mechi yao ya kiporo ya Ligi Kuu England ambayo ilikuwa ichezwe Agosti 25 lakini ikaahirishwa baada ya Uwanja wa Stadium of Light kufurika kufuatia Mvua kubwa.
Ushindi huu wa Bao 3-0 dhidi ya Reading umewang’oa kutoka kwenye zile Timu 3 za mwisho mkiani.
++++++++++++++
MAGOLI:
-McClean 3′
-Fletcher 28′
-Sessegnon 90′
++++++++++++++

BAADA YA KUPORA FEDHA ZA ZAWADI KWA KATIBU MTENDAJI WA ZFA, NADIR KANAVARO NA AGGREY MORIS KUHOJIWA LEO.

Kamati ya utendaji ya chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kimeamua kuwaweka kiti moto nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes, Nadir Haroub Cannavaro na msaidizi wake, Aggrey Morris.
Uamuzi huo wa ZFA umefikiwa jana  katika kikao cha dharula cha kamati ya utendaji ya chama hicho kilichoitishwa kwa ajili ya kujadili kitendo cha manahodha hao kupokonya dola 10,000 za ushindi wa tatu wa michuano ya Kombe la Chalenji na kuzigawa kwa wachezaji.
Cannavaro na Morris wanadaiwa kupora fedha hizo kwa Katibu Mtendaji wa ZFA, Kassim Ali wakati timu hiyo ilipokuwa ikirejea kutoka Kampala, Uganda, ambako ilishiriki michuano ya Kombe la Chalenji na kutwaa nafasi ya tatu.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya ZFA, Mussa Soraga amesema leo kuwa, wachezaji hao wameitwa kesho kwa ajili ya kuhojiwa na kamati ya utendaji  kuhusu kuongoza kitendo hicho.
Tayari ZFA imeshatangaza kuwafungia kwa muda usiojulikana wachezaji wote wa Zanzibar Heroes, wakiwemo walioteuliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachojiandaa kumenyana na Ethiopia na Zambia katika mechi za kirafiki za kimataifa.
Kwa mujibu wa Soraga, fedha hizo ni zile zilizotolewa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kutokana na Zanzibar kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji.
Soraga alisema baada ya Cannavaro kumnyang'anya Kassim fedha hizo, aliamua kuzigawa kwa wachezaji kwa madai kuwa ni mali yao na si ya ZFA.
Mjumbe huyo wa ZFA alisema kutokana na kitendo cha wachezaji kukubali kugawana fedha hizo, chama hicho kimewaona wote kuwa wana hatia ya kushiriki kula njama ya kupora fedha hizo na kugawana.
"Kitendo kilichofanywa na wachezaji wetu ni cha aibu na kimeifedhehesha mno serikali ndio sababu ZFA iliamua kukutana kwa dharula leo na kuamua kuchukua uamuzi huu mzito,"amesema Soraga alipozungumza na liwazozito muda mfupi uliopita.
Kutokana na uamuzi huo, Soraga alisema chama chake kimeamua kuandika barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulifahamisha kwamba, wachezaji hao, waliopo kwenye timu ya taifa, Taifa Stars na klabu za Yanga, Azam na Simba hawaruhusiwi kuzichezea kwenye michuano yoyote.
Wachezaji waliopo Tanzania Bara waliokumbwa na adhabu hiyo ni Cannavaro wa Yanga, Mwadin Ally, Aggrey Morris, Mcha Khamis na Samir Nuhu wa Azam, Selemani Selembe wa Coastal Union,Masoud Nassoro Cholo wa Simba, Amir Hamad wa JKT Oljoro na Twaha wa Mtibwa Sugar.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa ZFA, Amani Makungu ameamua kulizawadiwa benchi la ufundi la Zanzibar Heroes, dola 10,000 kutokana na timu hiyo kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji.
Soraga amesema leo kuwa, Makungu alikuwa ameahidi kuwaongezea wachezaji wa Zanzibar Heroes kitita hicho cha fedha kutokana na kushika nafasi hiyo, lakini kutokana na kitendo chao cha kupora fedha kutoka kwa kiongozi wa ZFA, ameamua kufuta ahadi hiyo.
Makungu amekabidhi fedha hizo kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Seif Bausi na msaidizi wake, Kassim Muhidin.
Kikosi cha Zanzibar Heroes kilichokwenda Uganda kushiriki michuano ya Chalenji ni makipa; Mwadini Ali (Azam), Suleiman Hamad (Black Sella), Abdalla Juma (Kipanga).
Mabeki ni Nassor Masoud 'Chollo' (Simba), Samir Haji Nuhu (Azam), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub Ali 'Canavaro' (Yanga), Aziz Said Ali (Kmkm), Mohammed Juma Azan (JKU) na Ali Mohammed Seif (Mtende Rangers).
Viungo ni Hamad Mshamata (Chuoni), Ali Bakar (Mtende Rangers), Is-haka Mohammed (JKU), Twaha Mohammed(Mtibwa Sugar), Suleiman Kassim 'Selembe' (Coastal Union), Saad Ali Makame (Zanzibar All Stars), Makame Gozi (Zimamoto), Issa Othman Ali (Miembeni), Aleyuu Saleh (Black Sella), Khamis Mcha Khamis 'Viali' (Azam).
Washambuliaji ni Amir Hamad (JKT Oljoro), Jaku Juma Jaku (Mafunzo), Abdallah Othman (Jamhuri), Nassor Juma (JKU) na Faki Mwalim (Chipukizi). 

ATUDO AANGUKA MIWILI AZAM FC

Atudo

BEKI wa kimataifa wa Kenya, Joackins Atudo amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam FC ya Dar es Salaam.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrissa amesema mida hii kwamba, beki huyo kutoka Tusker ya Kenya, amekwishamalizana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kutua leo Dar esw Salaam.
Tayari Azam imekwishafikia makubaliano na mshambuliaji wa Uganda, Brian Umony kusaini mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
Awali, Umony alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
Umony alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu. Azam pia ina mpango wa kusajili Wakenya wengine wawili, Jockins Atudo na Humphrey Mieno.

KOCHA MPYA WA SIMBA NI PATRICK LIEWIG AKIRITHI MIKOBA YA MILOVAN. NI KOCHA WA ZAMANI WA PARIS ST GERMAIN YA UFARANSA NA ASEC MEMOSAS YA IVORY COAST.

BAADA ya klabu ya Simba kuachana na kocha wake Milovan Circkovic ambaye ameikacha klabu hiyo bila sababu za kueleweka, taarifa za ndani za awali zinasema klabu hiyo imeamua kumuajiri kocha wa zamani wa Paris Saint-Germain na Asec Memosas ya Ivory coast ambaye ni raia wa Ufaransa.

Patrick Liewig aliyezaliwa mwaka 04/10/1950 kwasasa akiwa na umri wa miaka 62 ndiye kocha mtarajiwa wa wekundu hao wa Msimbazi na anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote kuanzia sasa kuanza kibarua hicho.
Uchunguzi wa Rockersports umebaini kuwa kocha huyo atakuwa ndiye kocha mwenye mshahara mkubwa kuliko makocha wote wa kigeni walioko nchini kwasasa wakifundisha vilabu mbalimbali vya ligi kuu. 
  Kwasasa atakuwa anatokea katika klabu ya El Gawafel Sportives de Gafsa(EGS) inayoshiriki ligi kuu ya Tusia ambako alimwajiri tarehe 20.10.2012 na kudumu nayo kwa kipindi cha mwezi mmoja.
 
Kabla ya hapo alitokea katika klabu ya MC Algier ya Algeria ambako aliajiriwa kama meneja 01/07/ 2012 ambako pia alidumu kwa mwezi mmoja kabla ya kuelekea EGS Gafsa).

Ni kocha mzoefu katika soka la Afrika licha ya kufundisha zaidi timu za Tunisia ambapo alifundisha pia Club Africain ya Tunis       kuanzia 19/04/2012 mpaka 30/06/2012 akiwa kama kocha wa muda pia amewahi kuifundisha Stade Tunisien ya Tunisia kuanzia 01/07/2009 mpaka 22/07/2011 kama meneja.

Kocha huyu amekuwa katika kipindi cha mafanikio zaidi katika kazi yake ya ufundishaji soka katika klabu ya ASEC Mimosas ya Ivory coast ambako alidumu kwa miaka zaidi ya saba baada ya kuajiriwa 01/09/2003 mpaka 2009 kabla ya kuelekea Stade Tunisien.

Kabla ya kuja barani Afrika alikuwepo Uarabuni kuanzia 01/07/2001 mpaka 29/08/2003.

Historia yake ilianzia kuifundisha Paris Saint-Germain kama kocha msaidizi kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia 01.07.1999 mpaka 30.06.2002 kabla ya hapo akiwa katika kipindi cha kujifunza zaidi akiwa kama meneja wa daraja la chini 01/07/1989 mpaka 30/06/1999.

Pia amewahi kuzifundisha USM Malakoff  ya Paris na Al Wahda Club ya Abu Dhabi.
Uchunguzi wa Rockersports umebaini kuwa kocha Patrick Liewig ambaye ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1  ni kocha mwenye wastani wa ushindi wa asilimia

30.77%  sare asilimia 38.46%  na kupoteza kwa asilimia

30.77%.
Katika kipindi chake cha kuifundisha Asec Memosas amefainikiwa kuingiza timu hiyo katika michuano ya vilabu bingwa Afrika mara saba na kufikia hatua ya nusu fainali moja mwaka 2006.

Katika miaka ya 2003, 2005, 2007 timu hiyo iliishia katika hatua ya makundi 2008 na miaka ya 2004 na 2009 aliisaidia kufikia hatua ya mzunguko wa pili.

MRISHO NGASSA ASAINI YANGA MIAKA MIWILI NA KUPEWA MILLIONI 10 - AHAIDIWA NYINGENE MWISHO WA MSIMU

Huku masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea muda ambao msemaji wa klabu ya El Merreikh alioutoa kwa mchezaji Mrisho Ngassa kujitokeza alikojificha na kufanya taratibu za uhamisho wake kwenda Sudan - mapema asubuhi ya leo, kuna taarifa za ndani kabisa kwamba mchezaji huyo ameamua rasmi kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya mitaa ya jangwani.

Chanzo cha habari kilicho karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga ni kwamba Mrisho Ngassa tayari amekubaliana kimsingi na Yanga kwamba atajiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo uliobakisha miezi isiyopungua sita  na klabu ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna Niyonzima.

"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na pre-contract na Yanga ya miaka miwili, kwa sasa hivi amepewa millioni 10 na fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu. Sasa hivi mchezaji amejificha ili kuepeuka usumbufu wa El Merreikh na Simba pamoja na Azam."

Mrisho Ngassa amekuwa katika vichwa vya habari kwa takribani wiki mbili sasa juu ya usajili wake wa kwenda kujiunga na El Merreikh ambao wamemuahidi mshahara wa $4000 kwa mwezi pamoja na $75000 kama ada ya usajili, huku vilabu vyake vya Simba na Azam FC vikilipwa $100,000. 

UGANDA ONE ANAMWAGA WINO LEO SIMBA SC

Dhaira anajitia kitanzi leo Msimbazi

KIPA namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira leo anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia Simba baada ya kutua jana jioni mjini Dar es Salaam akitokea kwao Uganda.
Akizungumza  jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba, baada ya kusaini leo, Dhaira atarejea kwao mara moja kwa ajili ya kwenda kujiandaa kuja kuanza kazi rasmi Msimbazi.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) aliyepigana vita dhidi ya Uganda, alisema kwamba Dhaira hatachelewa kurejea kuanza kumtumikia mwajiri wake mpya, bali atakuja mapema.
Dhaira amekwishasema atafurahi kujiunga na Simba kwa kuwa ni klabu kubwa Afrika na inacheza Ligi ya Mabingwa Afrika na angependa kuungana na Mganda mwenzake, Emmanuel Okwi huko.
Tayari Simba SC imefikia makubaliano na kipa huyo namba moja wa Uganda, aliyemaliza mkataba wake na klabu ya I.B.V FC ya Iceland na amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili kwa dau ambalo halijafahamika.
Dhaira alisema kwamba amefikia makubaliano na Simba kusaini mkataba wa miaka miwili kuja kuanza maisha mapya Dear es Salaam.
Dhaira aliyeibukia Express ya Uganda mwaka 2006, mwaka 2008 alihamia U.R.A. pia ya Uganda, ambayo aliichezea hadi mwaka 2010 alipohamia Ulaya.
Ikimpata Dhaira, Simba SC itakuwa imepata kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisotoshwa peke yake bila kupumzika. Na hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema hataki tena kuchezea Simba.
Lakini pamoja na matatizo hayo, Kaseja aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli.  

BEKI LA NGUVU LA KENYA LATUA KUSAINI AZAM LEO

Humphrey Mieno yupo kwenye rada za Azam pia
BEKI mmoja matata wa Tusker ya Kenya, anatarajiwa kutua leo Dar es Salaam kwa ajili hya kusaini mkataba wa kuichezea Azam FC ya Dar es Salaam.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa alisema jana kwamba, beki huyo mzuri atafichuliwa leo  baada ya kusaini mkataba, ila kwa sasa wanaendelea kuweka kapuni jina lake.
Tayari Azam imekwishafikia makubaliano na mshambuliaji wa Uganda, Brian Umony kusaini mkataba wa miaka miwili, akitokea KCC ya kwao, Uganda.
Awali, Umony alifanya mazungumzo na Simba SC ya Dar es Salaam pia na kufikia nao makubaliano, lakini Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kumalizamna naye, sasa ‘wanaishia kunawa’.
Umony alikuwa pia akiwaniwa na El Merreikh ya Sudan, ambayo nayo ilituma mwakilishi wake kwenda kuzungumze naye Uganda wiki iliyopita.
Brian amerejea nyumbani Uganda na kujiunga na KCC baada ya kumaliza mkataba wake, Becamex Binh Duong F.C. ya Vietnam.
Mwaka 2009, baada ya Simba kuzidiwa kete na SuperSport United ya Afrika Kusini, ikamsajili Emmanuel Okwi aliyekuwa SC Villa wakati huo.
Umony aliichezea Supersport United hadi 2010 alipohamia University of Pretoria ya Afrika Kusini pia hadi mwaka 2011 alipohamia Portland Timbers ya Marekani kwa mkopo na mwaka huu akatua Becamex Binh Duong F.C. Brian anang’ara katika Kombe la Challenge, hadi sasa ana mabao matatu. Azam pia ina mpango wa kusajili Wakenya wengine wawili, Jockins Atudo na Humphrey Mieno.  

YANGA YAANZA KAZI UHAI CUP LEO

MICHUANO ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom, inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi Kundi C kupigwa.
Kagera Sugar itacheza na Oljoro JKT saa 8 mchana- Karume wakati Yanga na Ruvu Shooting zitakuwa kwenye Uwanja wa Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni. (Ratiba nzima imeambatanishwa)
Timu zinazoshiriki michuano hiyo iliyoanza jana na itamalizika Desemba 23, mwaka huu., zimegawanywa katika makundi matatu, Kundi A likiwa na timu za Coastal Union, JKT Ruvu, Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Toto Africans, Kundi B ni African Lyon, Azam, Mgambo Shooting, Polisi Morogoro na Simba, wakati timu za Kagera Sugar, Oljoro JKT, Ruvu Shooting na Yanga zinaunda kundi C.
Katika mechi za jana, Azam FC ilianza vema baada ya kuilaza Mgambo Shooting mabao 2-0 jioni ya leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, shukrani kwao, Jamil Mchaulu ‘Balotelli’ na Reyna Mgugingila, wafungaji wa mabao hayo leo katika mchezo huo wa Kundi B.
Katika mechi za asubuhi jana, Coastal Union ya Tanga nayo ilianza vizuri baada ya kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1, mchezo wa Kundi A uliopigwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same na Yusuf Chuma na African Lyon iliichapa mabao 4-0 Polisi Moro.

SANTOS YAMTANGAZIA DAU ROBINHO.

RAIS wa klabu ya Santos ya Brazil Luis Alvaro de Oliveira Ribeiro amesema kuwa klabu yake hiyo imetangaza dau kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya AC Milan ya Italia Robinho na kumrejesha nyumbani katika klabu ambayo ndio alianza kucheza soka. Ribeiro amekiri kuwa dau hilo walilotoa limeonekana ni dogo kwa mahitaji ya mchezaji huyo mwenye miaka 28 pamoja na Milan lakini hiyo ni hatua ya kwanza katika mbio za kutaka kumrejesha nyumbani Robinho ambaye ameshinda mataji mawili ya ligi akiwa na timu hiyo mwaka 2002 na 2004. Rais huyo amesema kuwa tayari wameshatuma barua rasmi kwa Milan na anaamini kuwa watafikia makubaliano mwishoni kwani Robinho ameonyesha nia ya kutaka kurejea nyumbani baada ya kucheza Ulaya kwa kipindi kirefu. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil pia aliwahi kucheza katika vilabu vya Real Madrid ya Hispania kuanzia mwaka 2005 mpaka 2008 na kutimkia Uingereza katika klabu ya Manchester City ambayo aliondoka mwaka 2010 na kwenda Milan. 

FERGUSON AMNYATIA WALCOTT.

KLABU ya Manchester United imeingia katika kinyang’anyiro cha kumgombea winga wa Arsenal Theo Walcott kama walivyofanya wakati walipomchukua Robin van Persie Agosti mwaka huu. Meneja wa United Sir Alex Ferguson amenuia kumchukua winga huyo wa kimataifa wa Uingereza ambaye mkataba wake unaishia mwishoni mwa msimu huu. Walcott akama ilivyokuwa kwa Van Persie amekataa kusaini mkataba mpya mpya ambao utamuwezesha kulipwa kiasi cha paundi 75,000 kwa wiki na kudai kuwa kama klabu hiyo inamuhitaji basi haina budi kumlipa paundi 100,000 kwa wiki. Liverpool, Manchester City na Chelsea zote zimeonyesha nia ya kumsajili winga huyo lakini United ndio wanaonekana wana nafasi kubwa ya kumnyakuwa baada ya Walcott mwenyewe kuonyesha kuvutiwa na klabu hiyo.

CAPITAL ONE CUP: Ukame Makombe Arsenal kuendelea!

CAPITAL_ONE_CUP-BEST>>BRADFORD 1 ARSENAL 1, MATUTA ARSENAL HOI 3-2!!
>>BRADFORD, VILLA ZATINGA NUSU FAINALI!!
>>LEO ni Swansea v Middlesbrough
>> BPL KIPORO: Sunderland 3 Reading 0
Bradford, Timu inayocheza Ligi 1 ikiwa ni nafasi 65 chini ya Arsenal iliyo Ligi Kuu England, jana iliitupa Arsenal nje ya CAPITAL ONE CUP kwa kuishinda kwa Mikwaju ya Penati 3-2 kufuatia sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za Mchezo na kuhakikisha ukame wa Arsenal wa kutotwaa Kombe lolote kubwa wa tangu Mwaka 2005 kuendelea.
++++++++++++++
MAGOLI:
Bradford 1
-Thompson Dakika ya16
Arsenal 1
-Vermaelen Dakika ya  88
++++++++++++++
Katika Mechi hiyo iliyochezwa, Coral Windows Stadium, Nahodha wa Arsenal Thomas Vermaelen ndie aliekosa Penati muhimu na kuifanya Arsenal imeshinda Mechi moja tu katika Mechi zake 6 za mwisho na pia kuifanya Bradford kuwa Timu ya kwanza toka Madaraja ya chini kutinga Nusu Fainali ya Mashindano haya tangu Wycombe ilipofanya hivyo Mwaka 2006/7.
Norwich 1 Aston Villa 4
Aston Villa wametinga Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP baada ya kuichapa Norwich City Bao 4-1.
++++++++++++++
MAGOLI:
Norwich 1
-Morison Dakika ya 19
Aston Villa 4
-Holman Dakika ya 21
-Weimann 79 na 85
-Benteke 90
++++++++++++++
Hii ni mara ya pili katika Minne kwa Aston Villa kutinga Nusu Fainali ya Mashindano haya.
CAPITAL ONE CUP-Robo Fainali:
RATIBA/MATOKEO:
Jumanne Desemba 11
Norwich 1 Aston Villa 4
Bradford 1 Arsenal 1 [Bradford yasonga Penati 3-2]
[Mechi zote kuchezwa Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumatano Desemba 12
Swansea v Middlesbrough
Jumatano Desemba 19
Leeds United v Chelsea
+++++++++++++++++++++++++
Mechi pekee ambayo inazikutanisha Klabu za Ligi Kuu England ni ile kati ya Norwich City na Aston Villa.
+++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU za CAPITAL ONE CUP:
-KABLA LILIKUWA ni Carling Cup na Bingwa Mtetezi alikuwa ni Liverpool.
-Linaitwa CAPITAL ONE CUP kwa sababu Mdhamini wake ni Kampuni ya masuala ya Fedha, Capital One.
-Linashirikisha Timu za Ligi za juu England 92 kwa mtindo wa Mtoano [Timu 20 toka Ligi Kuu na 24 kila moja kutoka Madaraja ya Npower, Ligi 1 na 2.
-Bingwa wa michuano hii hucheza EUROPA LIGI Msimu unaofuata kuanzia Raundi ya Tatu ya Mtoano.
+++++++++++++++++++++++++
BPL KIPORO: Sunderland 3 Reading 0
Meneja wa Sunderland, Martin O'Neill, amesherehekea Mwaka mmoja wa kuwepo Klabuni hapo kwa ushindi mtamu wa Mechi yao ya kiporo ya Ligi Kuu England ambayo ilikuwa ichezwe Agosti 25 lakini ikaahirishwa baada ya Uwanja wa Stadium of Light kufurika kufuatia Mvua kubwa.
Ushindi huu wa Bao 3-0 dhidi ya Reading umewang’oa kutoka kwenye zile Timu 3 za mwisho mkiani.
++++++++++++++
MAGOLI:
-McClean 3′
-Fletcher 28′
-Sessegnon 90′
++++++++++++++

KLABU BINGWA DUNIANI: NUSU FAINALI Jumatano & Alhamisi!

>>NGULI ABOUTRIKA kuiongoza Al Ahly dhidi ya Wabrazil Corinthians!!
>>ALHAMISI: Chelsea v Monterrey!!
FIFA_CLUB_WORLD_CUPMOHAMED ABOUTRIKA, wenyewe huko Misri, Siku zote humuita kwa upendo mkubwa, ‘Malaika’, ‘Nguli’ au ‘Mtu wa Amani’, baada ya kuifungia Al Ahly Bao la pili na la ushindi walipoichapa Sanfrecce Hiroshima ya Japan Bao 2-1 Jumapili, Siku ya Jumatano atawaongoza Mabingwa hao wa Afrika kucheza na Mabingwa wa Marekani ya Kusini, Corinthians ya Brazil, kwenye Nusu Fainali ya Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani Uwanja wa Toyota, Japan.
+++++++++++++++++++++
RATIBA:
[SAA za BONGO]
Jumatano Desemba 12
MSHINDI wa 5:
[Saa 4 na Nusu Asubuhi]
Usain Hyundai v Sanfrecce Hiroshima
NUSU FAINALI
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Al Ahly v Corinthians
Alhamisi, Desemba 13
[Saa 7 na Nusu Mchana]
Monterrey v Chelsea
+++++++++++++++++++++
Kabla ya Mechi hiyo ya Nusu Fainali hapo Jumatano, kutakuwepo Mechi ya kusaka Mshindi wa Tano kati ya Usain Hyundai ya Korea Kusini na Sanfrecce Hiroshima ya Japan.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Alhamisi kati ya Chelsea, Mabingwa wa Ulaya, na Monterrey ya Mexici, ambao ni Mabingwa wa Marekani ya Kati na Kaskazini.
VIKOSI:
CORINTHIANS:
MAKIPA: JULIO CESAR, CASSIO, DANILO FERNANDES
MABEKI: ALESSANDRO, CHICAO, WALLACE, FABIO SANTOS, PAULO ANDRE, ANDERSON POLGA, GUILHERME ANDRADE, FELIPE
VIUNGO: RALF, PAULINHO, DOUGLAS, WILLIAN ARAO, DANILO, EDENILSON
MAFOWADI: Juan MARTINEZ, Paolo GUERRERO, EMERSON, JORGE HENRIQUE, GIOVANNI, ROMARINHO
KOCHA: TITE
AL AHLY:
MAKIPA: Sherif EKRAMY, Ahmed ADEL, Mahmoud ABOU ELSEOUD
MABEKI: Saadeldin SAAD, Ramy RABIA, Sherif ABDELFADEEL, Wael GOMAA, Mohamed NAGUIB
VIUNGO: Shehab AHMED, Mohamed BARAKAT, Ahmed KENAWI, Hossam GHALY, Sayed MOAWAD, AHMED FATHI, Hossam ASHOUR, TREZEGUET
MAFOWADI: EMAD METEAB, Walid SOLIMAN, GEDO, ELSAYED HAMDI, Abdalla SAID, Mohamed ABOUTRIKA, Dominique DA SYLVA
KOCHA: EL BADRY Hossam