Thursday, December 20, 2012

RONALDO DE LIMA XI vs ZIDANE ZIZOU XI 3-2 TIMU YA ZIDANE YAFUNGWA NA TIMU YA AKINA RONALDO RICHA YA ZIDANE KUIFUNGIA TIMU YAKE GOLI KATIKA MECHI DHIDI ya UMASIKIN


 

  RHINO RANGERS WAZIDI KUJIIMARISHA LIGI DARAJA LA KWANZA

 

Timu ya maafande wa jeshi la wananchi ya mkoani tabora RHINO RANGERS imeendelea kujiimarisha katika ligi daraja la kwanza kwa kucheza michezo kadhaa na timu za mkoani tabora ili kujiimarisha katika mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza FDL.

Timu hiyo leo imecheza mchezo wa kirafiki na timu ya LEEDS UNITED katika dimba la ALLY HASSAN MWINYI na imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 ,mabao ya rhino rangers hii leo yamefungwa na shija mongo dk ya 17 ,maganda machembe mchezaji mpya iliyemsajili alifunga dk ya 32,na bao la ushindi lilifungwa mnamo dk ya 52 ya kipindi cha pili na msafiri maiko.

Pia timu hiyo ya rhino rangers inatarajia kucheza mchezo mmoja w akirafiki na timu ya simba B kutoka dar es salaam ili iwape mazoezi ya kutosha kuelekea mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza FDL.

Kuelekea mzunguko w apili wa ligi daraja la kwanza rhino rangers imeendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji watano ili kuongeza nguvu katika kikosi,wachezaji iliowasajili ni ayoub iddy ,na josephy mapunda nafasi ya beki,doi mobby,mganda mchembe washambuliaji,na emanuely noely nafasi ya kiungo.

wachezaji wa zamani ni abdukarim mtumwa,iddy kihulya,charles mpinuki,james mwambembe,julius masunga,abass mohamedy,stanslaus mwakitosi,steven madhanda,shija sanju,shija mongo,salum mamro,salum majid,usi makame,na frank koe.

wengine ni josephy salaganda,victor hangaya,bakary mahadhi,said kipanga,issa mohamedy,stanley mlai,samwely mwamasangula,omary magesa,msafiri maiko,ramadhani shabyeji na ally rumba na kuhitimisha idadi ya wachezaji 30 katika klabu hiyo inayonolewa na kocha wa zaman wa mafunzo ya zanzibar akisaidiwa na kocha mongo.

 

 

UCHAGUZI W AMKOA W ATABORA TAREFA KUFANYIKA KESHO KATIKA UKUMBI WA TUWASA KUANZIA SAA NNE ASUBUHI .


 MWENYEKITI wa kamati ya uchaguzi mkoa wa tabora TAREFA bw.MKAMA BWIRE leo ametibitisha    kuwa uchaguzi w amkoa w atabora utafanyika kesho december 22 ya mwaka huu katika ukumbi  wa idara ya maji mkoani tabora TUWASAkutafuta viongozi watakaochaguliwa kuwakilisha mkoa wa tabora TAREFA.


Majina yaliyopitishwa LEO  2112/2012  katika nafasi ya MWENYEKITI.

1.Musa Ntimizi

2.Yusuph kitumbo.

3.Laurent paul

-===NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI

1.A laija Mwiga

===NAFASI YA KATIBU

1.Albert sitta

2.Fatteh Dewj

===NAFASI YA KATIBU MSAIDIZI

,,,,,,HAKUNA MGOMBEA

====NAFASI YA MWEKA HAZINA=AMEJIONDOA KUTOKANA NA KUONGEZEWA MAJUKUMU KATIKA UTENDAJI WA KAZI W AUHASIBU MKOA W ATABORA BW.

1.Mussa Msananga

===NAFASI YA MWEKA HAZINA MSAIDIZI

,,,,HAKUNA MGOMBEA

===NAFASI YA MJUMBE MKUTANO MKUU TFF

1.Dick Mlimuka

2.Milambo Kamili

3.Ramadhani Maghembe

4.Charles Mwakambaya

===NAFASI YA MWAKILISHI WA VILABU

1.Achery manjori

2.Razack j.Kumba

3. Lwamba yussa

===NAFASI YA UJUMBE KAMATI YA UTENDAJI

1.Stanslaus Sizya

2.Abdul mohamed Aman

3.James Erick Kabepele

===NAFASI YA MWAKILISHI WA MPIRA WA MIGUU KWA UPANDE WA WANAWAKE NI-janeth michael


 

LULU AACHIWA KWA DHAMANA

Lulu katika siku za mwanzo za kesi yake, akifikishwa Mahakama ya Kisutu
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo asubuhi imemuachia kwa dhamana msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayetuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba ‘The Great’ baada ya kupitia vifungu vya sheria.
Hatua hiyo inakuja baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kubadilisha mashitaka ya mwanadada huyo kutoka kesi ya mauaji hadi kuua bila kukusudia.
Kutokana na mabadiliko hayo, hata kama atashindwa kesi, Lulu hatapewa hukumu ya kunyongwa kwa kuwa anatuhumiwa kwa kesi ya kuua bila kukusudia na kwa mujibu wa kifungu cha sheria, anaweza kufungwa maisha au miaka kadhaa.
Lulu anakabiliwa na tuhuma za kumuua The Great Kanumba aliyefariki dunia, Aprili 7, mwaka huu nyumbani kwake Vatican, Sinza Dar es Salaam.
Lulu aliyecheza filamu kadhaa na marehemu Kanumba waliyeibuka naye katika kundi la Kaole, Magomeni, anadaiwa alimsukuma Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican, ambaye pia inadaiwa alikuwa mpenzi wake.
Inaelezwa baada ya tukio hilo, Lulu alikimbia nyumbani kwa Kanumba na mdogo wa The Great, Sethi Bosco akaenda kuchukua gari kumpeleka kaka yake hospitali ya Muhimbili, ambako alipofika iligundulika amekwishafariki dunia.
Sethi alikaririwa akisema kwamba siku ya tukio, Lulu alikwenda kwao usiku wa manane na alipofika yeye (Sethi) alimuacha aongee na kaka yake. Sethi alidai aliwaacha sebuleni akaingia chumbani kwake na baadaye akasikia wameingia chumbani (kwa Kanumba).
Sethi alisema baada ya muda alisikia kelele za dalili ya ugomvi na baada ya muda Lulu alitoka kumwambia (Sethi) juu ya hali ya Kanumba kubadilika na kuwa mbaya.
Sethi alidai aliposikia hivyo akashituka na kwenda chumbani ambako alimkuta kaka yake katika hali mbaya, povu likimtoka mdomoni hivyo kuchukua hatua ya kumuita daktari wake, kabla ya kumkimbiza Muhimbili.
Lulu alikamatwa asubuhi ya kuamkia siku ya tukio hilo, linalodaiwa kutokea usiku wa manane na kuwekwa kizuizini katika kituo cha Polisi Oysterbay, Kinondoni, Dar es Salaam, kabla ya kufikishwa mahakamani.
Uchunguzi wa madaktari katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ulisema pombe kali aina ya Jackie Daniels ilisababisha kifo cha mwigizaji huyo. 
Kifo cha Kanumba kiliwaumiza wengi, kwani msanii huyo alikuwa mahiri na kipenzi cha wapenzi wa filamu nchini.
Wapembuzi wa mambo wanasema huu ni msiba wa kwanza kuteka hisia za watu wengi zaidi, tangu kifo cha baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Oktoba mwaka 1999.

RAUL: AFUNGIWA MECHI KUMI NA MOJA

Mchezaji wa zamani na  kiungo wa  klabu ya Liverpool na  Chelsea  Raul Meireles amefungiwa mechi kumi na moja baada kutuhumiwa kumtemea mate mwamuzi  .

 Mchezaji huyo wa mwenye miaka 29-anayechezea  Fenerbahce , alitolewa nje kwa kadi Nyekundu siku ya mechi dhidi ya  Galatasaray,
ambayo mechi hiyo walipoteza kwa mabao mawili kwa moja aidha Raul Amekataa tuhuma hizo. 

Japokuwa shirikisho la soka la uturuki limeshutumu mwamuzi huyo  Halis Ozkahya's kwa kukiri na kuidhinisha adhabu hiyo . 

 Meireles amesema : "Nitachukua hatua za kisheria dhidi yake  kuonyesha kuwa nimechukizwa na siku fanya kitendo hicho." pia alikata kuwa alifamnyia ishara za kumdharau mwamuzi huyo ,

"Sijui ishara yoyote  ya kituruki kuwa nilimuonyesha mwamuzi kuwa yeye ni shoga huyu mwamuzi ni kigeugeu na anasikiliza sana kelele za mashabiki  ,"Aliongeza mreno huyo    

 "Tazam mtindo wangu wa Nywele 'Nilichovaa mimi sio mtu wa aina hiyo ishara ya mkono wangu haiku ya maana hiyo au kitendo mnaachokiita cha kishoga  
Mwamuzi huyu anatoa tuhuma za kudharirishana na ni kashfa hii mimi nina mtoto wa miaka nane sasa itakuwaje watooto wakisema kuwa baba yenu kamtemea mate mwamuzi au kamtukana 
 
Meireles alichezea misimu mwili klabu ya za ligi ya uingereza akitokea porto akijiunga na  Liverpool na badae kwenda  Chelsea 2011. 

 Alijiunga  mwezi kenda na Fenerbahce kwa ada ya pauni  £8m . 


HATUTADHARAU MECHI "KATONGO "

Christopher Katongo nahodha wa timu ya Taifa ya Zambia akieleza mikakati ya ushindi hapo kesho dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars mchezo utakaopigwa kesho katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Christopher Katongo (30), ambaye pia ni Mwanasoka Bora wa Afrika wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) mwaka huu, amesema kuwa mipango endelevu ya kulea wachezaji vijana na nidhamu ya wachezaji ndiyo chanzo cha mafanikio yao.

 Amesema kwamba hata katika mechi ya timu yake dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi, wachezaji wenye umri mdogo ndiwo watakaopewa kipaumbele katika kikosi cha Chipolopolo.

 “Nidhamu, kujituma na kufuata taratibu ndiyo siri ya mafanikio yetu. Nadhani umeona mazoezi yetu, tunafanya kazi kwa umoja na kila mchezaji ana ari ya kufanya kile anachoelekezwa na mwalimu,” .

Kocha wa kikosi wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars Kim Poulsen alikielezea namna atakavyotumia nafasi ya kesho ya kucheza na timu bora ya Afrika Zambi hapo kesho, ambapo ameeleza kuwa anamatumaini ya kushinda katika mchezo huo licha ya kuwakosa wachezaji wake wawili muhimu Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.
 “
KIBIRA AFUNGIWA CHANETA
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limemuondolea adhabu ya kifungo cha muda usiojulikana katibu mkuu wa zamani wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Kibira kufuatia baraza hilo kubaini kuwa hana hatia yoyote.

Taarifa kutoka ndani ya BMT zimeeleza kuwa sasa, Kibira yuko huru na kwamba, akitaka anaweza kujitosa katika kuwania uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa Chaneta utakaofanyika hivi karibuni.

  Mwenyekiti wa BMT, Dioniz Malinzi, amesema Kibira yuko huru na kwamba kuanzia sasa anaweza kugombea nafasi yoyote anayoitaka kutokana na ukweli kwamba hana hatia inayomzuia kugombea katika uchaguzi mkuu wa chama hicho.

 Amesema kuanzia sasa, Kibira na wanamichezo wengine wenye nia ya kugombea wanapaswa kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho.

 Aliongeza kuwa Kibira anatarajiwa kufika kwenye ofisi za BMT kuanzia leo kupata maelekezo kutokana na adhabu aliyokuwa amepewa awali na kamati ya utendaji ya CHANETA, ambayo iliashiria kufungiwa kwake kwa muda usiojulikana.

 Aidha, Kibira amesema kuwa bado hajapata taarifa yoyote kuhusiana na kufungiwa kwake Chaneta, lakini amefurahishwa na uamuzi wa kuondolewa adhabu na kwamba atakuwa tayari kutangaza nia yake pale atakapopata uthibitisho rasmi kuwa yuko huru kugombea katika uchaguzi huo.

 "Nimefurahi kusikia hivyo. Lakini nasubiri taarifa rasmi kutoka kwa BMT ili nijihakikishie kama kweli ninaruhusiwa kugombea," amesema Kibira.

 Aliongeza kuwa, katika muda wote wa kusimamishwa kwake CHANETA, amekuwa akijishughulisha na michezo mingine kutokana na ukweli kuwa michezo iko damuni.

Licha ya kufungiwa kwa muda usiojulikana, Kibira alikuwa hajawahi kupewa barua yoyote hadi BMT ilipoeleza jana kuwa yuko huru na kwamba sasa anaweza kujishughulisha na CHANETA

REAL MADRID VS MAN UNITED: RONALDO "SITOSHANGILIA GOLI ENDAPO NITAFUNGA DHIDI YA UNITED"

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amesisitiza kwamba hatoweza kushangilia ikiwa atafunga katika hatua ya 16 ya UEFA Champions league dhidi ya Manchester United.

 Nahodha huyo wa Ureno ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa akiwa na United katika kipindi cha miaka 6 kabla ya kuondoka na kujiunga Los Blancos katika kipindi cha kiangazi mwaka 2009 kwa ada iliyovunja rekodi ya dunia ya £80 million.

"Sitoshangilia goli nikiweza kufunga dhidi ya Man United," Ronaldo alikaririwa akisema siku ya alhamisi na mtandao wa AS.


Ronaldo, 27, hivi karibuni alielezea hisia zake juu ya kocha wa Manchester United na kusema kocha huyo raia wa Scotland amecheza part kubwa katika kumfanya mchezaji ambaye alivyo sasa.

"Ferguson ni mtu mzuri sana. Mwanadamu mwema. Amenifundisha vitu vingi," Ronaldo aliiambia The Sun.


"Kama nilivyosema huko nyuma, Fergie ni kama baba yangu kwenye soka. Nammisi sana yeye na mahusiano tuliyokuwa nayo."


HIVI NDIVYO TUZO YA BALLON D'OR INAVYOTENGENEZWA - RONALDO, MESSI, AU INIESTA NANI KUIBUKA KIDEDEA WIKI 2 ZIJAZO????

RONALDO, INIESTA OR MESSSI

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Timu ya masonara sita ndio wanashughulikia utengenezwaji wa tuzo ya Ballon d'Or

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Utengenezaji wa Ballon d'Or ukiendelea

Golden balls: The world's oldest jewellers have a team of six working on the Ballon d'Or trophy
Ufaransa ndio imekuwa nchi inayotengeneza tuzo tangu mwaka 1956.



Piece by piece: The same family-run store in Paris have built the trophy every year since 1956
Mtengenezaji akiweka kipande kimojawapo kwenye tuzo hiyo

Craftsman: All the finishing touches are applied by hand... but who will get their hands on the trophy?
Craftsman: All the finishing touches are applied by hand... but who will get their hands on the trophy?

 

 

 

 

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: BAADA ya DROO, NINI WAMESEMA!!

>>RATIBA KAMILI YATOKA!!
>>REAL v MAN UNITED ni FEBRUARI 13
>> FERGIE: ‘NDIO BIGI MECHI RAUNDI YA TIMU 16!!’
+++++++++++++++++++
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku]
Jumanne 12  Februari 2013
Celtic v Juventus
Valencia v Paris St Germain
Jumatano 13  Februari 2013
Real Madrid v Manchester United
Shakhtar Donetsk v Borussia Dortmund
Jumanne 19  Februari 2013
Arsenal v Bayern Munich
FC Porto v Malaga
Jumatano 20  Februari 2013
Galatasaray v FC Schalke
AC Milan v Barcelona
Jumanne 5 Machi 2013
Borussia Dortmund v Shakhtar Donetsk
Man United v Real Madrid
Jumatano 6 Machi 2013
Juventus v Celtic
Paris St George v Valencia
Jumanne 12 Machi 2013
Barcelona v AC Milan
Schalke v Galatasaray
Jumatano 13 Machi 2013
Bayern Munich v Arsenal
Malaga v FC Porto
+++++++++++++++++++
FERGIE_n_MOURINHOMara baada ya kumalizika kwa Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI hapo jana huko Nyon, Uswisi, Wadau mbalimbali waliibuka kutoa maoni yao kuhusu Ratiba hiyo na Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, alisema pambano la Real Madrid na Manchester United ndio ‘mpambano’ wa Raundi hiyo.
Real Madrid na Manchester United hawajakutana kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI tangu Robo Fainali ya Mwaka 2003 ambayo Real walishinda kwa jumla ya Mabao 6-5 baada ya kushinda Mechi ya kwanza 3-1 huko Santiago Bernabeu na kufungwa 4-3 Uwanjani Old Trafford huku Ronaldo de Lima akipiga Hetitriki.
Mbali ya pambano kuwa zito, Mechi hii itakuwa na mvuto kwani Cristiano Ronaldo atarudi Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu aihame Man United na kwenda Real Madrid Juni 2009 kwa Dau la Pauni Milioni 80.
Mara ya mwisho kwa Sir Alex Ferguson kumvaa Jose Mourinho ilikuwa kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2009 wakati Man United ilipoibwaga Inter Milan kwenye Robo Fainali baada ya kutoka 0-0 na kuifunga 2-0 Old Trafford kwa Bao za Vidic na Ronaldo.
Ferguson amesema: “Ni nafasi nzuri kwa Mashabiki wetu kumuona Ronaldo tena na mimi kukutana na Jose-itabidi niagize Mvinyo safi!”
+++++++++++++++++++
Man United v Real Madrid
-1957: European Cup-Nusu Fainali: Real washinda 3-1Madrid, sare 2-2 na Real kushinda Jumla ya Bao 5-3
-1968: European Cup-Nusu Fainali: Man United washinda 1-0 Old Trafford, sare 3-3 ugenini na Man United washindi Jumla ya Bao 4-3
-2000: European Cup-Robo Fainali: Sare 0-0 huko Bernabeu, Man United wafungwa 3-2 nyumbani
-2003: European Cup-Robo Fainali: Real washinda 3-1 nyumbani, Man United washinda 4-3 nyumbani, Real wapita Jumla ya Mabao 6-5.
+++++++++++++++++++
YAFUATAYO ni NINI KILISEMWA KUTOKA KWA WADAU MBALIMBALI:
Real Madrid
Mkurugenzi wa Real Madrid, Emilio Butragueno, aliewahi kuwa Straika wao zamani:  "Tungependa kucheza na Man United baadae lakini hata wao hawakufurahia!"
Barcelona
Makamu wa Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu "AC Milan ni Klabu kubwa Ulaya, inaheshimika. Kwa sasa hawachezi vizuri lakini mpira hubadilika Siku hadi Siku."
Bayern Munich
Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge "Tunaijua Arsenal vizuril. Tunaridhika na Droo hii lakini hatuwadharau!"
Paris St Germain
Mkurugenzi wa Soka, Leonardo: "Siku zote ni ngumu kusema ni Droo nzuri au siyo!"
Valencia
Mkurgenzi wa Valencia, Fernando Giner: "Kama tumefika hapa basi sisi ni moja ya Timu Bora 16 Ulaya!"

No comments:

Post a Comment