Monday, November 19, 2012

HIVI NDIVYO SIMBA NA AZAM WALIVYOFANYA BIASHARA YA OWINO


Joseph Owino anarudi nyumbani Msimbazi
AZAM FC wanataka Sh. Milioni 10 pamoja na kiungo Uhuru Suleiman kutoka Simba, ili wawape beki Mganda Joseph Owino.
Habari za ndani, ambazo  tumezipata  kutoka Azam, zinasema kwamba tayari makubaliano yamefikiwa lakini, Simba inaonekana kusuasua kutekeleza makubaliano hayo.
Azam wanadai wamekubaliana na Simba walipe fedha hizo Sh Milioni 10 na kumuidhinisha Uhuru kuhamia Chamazi, lakini suala la fedha bado halijatekelezwa.
“Tena hapo bado kuna kesi ya fedha nyingine, Sh. Milioni 5, ambazo Simba wanadaiwa na Uhuru, sisi tumekubali kumpa fedha hizo Uhuru, halafu wao tutawakata kwenye mapato ya mlangoni katika mechi yetu na wao ya marudiano,”kilisema chanzo kutoka Azam.
Lakini upande wa Simba nao wanasema fedha zote, Sh Milioni 15 walikubaliana zikatwe katika mapato ya milangoni.
Simba imeamua kumrejesha Owino, ili kuimarisha safu yake ya ulinzi, ambayo imeonekana kuyumba katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Lakini pia hiyo ni nafuu kwa beki huyo Mganda, ambaye ameshindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Azam chini ya makocha wote, kuanzia Mserbia Boris Bunjak aliyefukuzwa na huyu wa sasa Muingereza, Stewart Hall aliyerejeshwa kazini.

NYAMLANI AULA CAF

Athumani Nyamlani
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani ameteuliwa kuwemo kwenye Ujumbe rasmi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) utakaosimamia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Januari mwakani nchini Afrika Kusini.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, uteuzi huo umefanywa na Rais wa CAF, Issa Hayatou na Kamati yake ya Utendaji. Ujumbe huo wa CAF kwa ajili ya fainali hizo zitakazoanza Januari 19 na kumalizika Februari 10 mwaka huu una jumla ya watu 148.
Wambura amesema Nyamlani atakuwa miongoni mwa wajumbe watatu, watakaoshughulikia masuala ya rufaa kwenye mashindano hayo. Wajumbe wengine ni Prosper Abega kutoka Cameroon na Pierre-Alain Monguengui wa Gabon. Nyamlani ni mjumbe wa Bodi ya Rufani ya CAF yenye watu 12.

CHAGUZI ZA TFF...


MCHAKATO wa uchaguzi wa Chama cha Soka Katavi (KAREFA), umefutwa kutokana na wagombea watano kati ya nane vyeti vyao vya elimu ya sekondari kuwa na utata. Mchakato wa uchaguzi huo utaanza upya Novemba 21 mwaka huu.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema leo kwamba, mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) utaanza upya Novemba 26 mwaka huu baada ya mchakto wa sasa kupata wagombea kwenye nafasi mbili tu za Kamati ya Utendaji ya chama hicho.
Mchakato wa uchaguzi wa RUREFA utaanza Novemba 26 mwaka huu na Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA itapewa maelekezo ya usimamiaji wa uchaguzi huo baada ya mchakato wa awali kuwa umefutwa kutokana na kufanyika bila kuzingatia kanuni za uchaguzi.
Wakati huo huo TFF, itakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika keshokutwa, saa 6:00 mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo.

 UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA KATAVI (KAREFA)  

 Mchakato wa uchaguzi wa KAREFA umefutwa kutokana na wagombea watano kati ya nane vyeti vyao vya elimu ya sekondari kuwa na utata. Mchakato wa uchaguzi huo utaanza upya Novemba 21 mwaka huu.

 
UCHAGUZI WA TASMA  
Mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wataalamu wa Tiba ya Michezo Tanzania (TASMA) utaanza upya Novemba 26 mwaka huu baada ya mchakto wa sasa kupata wagombea kwenye nafasi mbili tu za Kamati ya Utendaji ya chama hicho.

UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA RUKWA (RUREFA)  
Mchakato wa uchaguzi wa RUREFA utaanza Novemba 26 mwaka huu na Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA itapewa maelekezo ya usimamiaji wa uchaguzi huo baada ya mchakato wa awali kuwa umefutwa kutokana na kufanyika bila kuzingatia kanuni za uchaguzi.

 

NYINGINEZO:
++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za Juu:
1 Yanga Mechi 13 Pointi 29
2 Azam FC Mechi 13 Pointi 24
3 Simba Mechi 13 Pointi 23
4 Coastal Mechi 13 Pointi 22
++++++++++++++++++++++++++
Kwa sasa VPL imemesimama baada ya kumalizika kwa Mzunguko wa Kwanza na itarudi tena kilingeni Januari 26.
++++++++++++++++++++++++++
RAUNDI YA PILI
26TH JAN. 2013 - 18TH MAY, 2013.
Januari 26
African Lyon v Simba [National Stadium, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Polisi Morogoro [Manungu, Morogoro]
Coastal Union v Mgambo JKT [Mkwakwani, Tanga]
Ruvu Shootings v JKT Ruvu [Mabatini, Pwani]
Azam v Kagera Sugar [Azam Complex, Dar es Salaam]
JKT Oljoro v Toto Africans [Sheikh Amri Abeid, Arusha]
Januari 27
Yanga v Tanzania Prisons [National Stadium, Dar es Salaam]

SERENGETI BOYS WAINGIZA MILIONI 23 TU

Farid Mussa Shah wa Serengeto kulia akichuana na beki wa Kongo Brazzaville Tmouele Ngampio katika mechi hiyo

MECHI ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania, Serengeti Boys na Kongo Brazzaville iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza Sh. 23,021,000.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema  leo kwamba, mapato hayo yametokana na washabiki 18,022 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 10,000, sh. 5,000, sh. 2,000 na sh. 1,000. Washabiki 15,850 walikata tiketi za sh. 1,000.
Amesema asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 3,511,677.97 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 5,956,635), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000), umeme (sh. 300,000) na ulinzi wa mechi (sh. 3,500,000).
Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 1,000,537, asilimia 10 ya uwanja sh. 500,269, asilimia 5 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) sh. 250,134, asilimia 45 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,251,209, asilimia 20 ya TFF (sh. 1,000,537) na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) sh. 50,027.

MWANASOKA BORA TANZANIA KUPATIKANA DESEMBA 30

Athimani Iddi 'Chuji' wa Yanga kulia akiwa katika moja ya mechi za Ligi Kuu dhidi ya Mgambo JKT. Je, ataingia kwenye orodha ya wachezaji wa kuwanai tuzo ya Mwanasoka Bora Tanzania?

FAINALI ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka Tanzania, zinazotolewa na Kampuni ya Wazalendo Bright Media zinatarajiwa kufanyika Desemba 30 mwaka huu mjini Dar es Salaam katika sehemu, ambayo itatangazwa baadaye.
Mratibu wa mchakato huo, Ahadi Kakore amesema leo kwamba, mchakato wake ulianza tangu Agosti mosi mwaka huu kwa wanamichezo kupigiwa kura na mashabiki kupitia mitandao mbalimbali ikiwemo ile ya kijamii (face book, Twitter na Blogs) na wengine kwa njia ya simu za mikononi kwa kupitia namba maalum.
Amesema kwa sasa kamati ipo kwenye mchakato ya kuchuja majina ambayo yamependekezwa na  mashabiki wa soka kupitia kura zao ambapo zaidi ya wachezaji 93 wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara majina yao yameweza kuonekana ambapo kati ya majina hayo yataopunguzwa na kufikia 30.
Amesema kabla ya kufanyika kwa fainali hiyo wale wachezaji ambao wataingia kwenye fainali watapatiwa semina ya uwezekezaji na ujasiriamali ili kujiandaa na maisha ya baadaye baada ya kustaafu.
Amesema sababu za kufanya semina hii ni kuhakikisha kuwa wachezaji wetu wanapata elimu ya uwezekaji na ujasiriamali ili kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kwa ajili ya siku zijazo hasa ikizingatiwa kwamba wachezaji wengi wa Tanzania bado ni masikini.
Kakore amesema kwenye semina hiyo watakuwepo wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi na fedha ambao watatoa elimu ya uwekezaji, kwa kufanya hivi itawapa nafasi wachezaji hawa kuelewa na kutambua umuhimu wa uwekezaji.
Amesema semina hiyo inatarajiwa kufanyika Desemba 19 na  20 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam. Pamoja semina ambayo itakwenda sambamba na  utoaji wa elimu ya afya kwa washiriki wa semina hiyo ambao watakuwa wachezaji pekee. Amesema mshindi wa tunzo hiyo anatarajiwa kupata tuzo, fedha taslim, medali na cheti.

KILIMANJARO STARS WAKIJIFUA KWA TUSKER CHALLENGE 2012

Beki wa timu ya taifa ya Bara, Kilimanajro Stars, Kevin Yondan (kushoto) akiwa mazoezini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayotarajiwa kufanyika mjini Kampala, Uganda kuanzia Jumamosi wiki hii. Timu hii inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Bara, Kilimanajro Stars wakiwa mazoezini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, kujiandaa na mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yanayotarajiwa kufanyika mjini Kampala, Uganda kuanzia Jumamosi wiki hii. Timu hii inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

 

NIYONZIMA, KAVUMBANGU KWAHERI YANGA

Haruna Niyonzima anakwenda El Merreikh

KLABU ya Yanga imepokea ofa kutoka klabu mbili tofauti, moja ya Asia na moja ya hapa hapa Afrika zikiwahitaji wachezaji wao mahiri wa kigeni, kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda na mshambuliaji Didier Kavumbangu kutoka Burundi.
Habari za ndani kutoka Yanga, zimesema kwamba, Niyonzima anatakiwa na klabu ya El Merreikh ya Sudan, wakati Kavumbangu anatakiwa na klabu moja ya Qatar.   
Tayari barua rasmi za kuwahitaji wachezaji hao zimekwishawasilishwa Yanga na hivi sasa klabu inaingia kwenye majadiliano ya bei na klabu hizo.
Klabu ya Qatar, ilitangaza ofa ya dola za Kimarekani 100,000 (zaidi ya Sh. Milioni 150), lakini Yanga imekataa dau hilo na inataka dola 300,000 (zaidi ya Sh. Milioni 450) kwa ajili ya Kavumbangu.
Kuhusu Niyonzima, Merreikh imeomba itajiwe bei ya mchezaji huyo na Yanga. “Merreikh wana fedha, hatuna wasiwasi nao, sisi tutaanzia dola 300,000 na hata tukishuka, si chini ya 200,000, hawa wachezaji ni lulu”kilisema chanzo kutoka Yanga.
Didier Kavumbangu anakwenda Qatar
Haruna alisajiliwa msimu uliopita Yanga kutoka APR ya Rwanda, wakati Kavumbangu amesajiliwa msimu huu kutoka Atletico Olympic ya Burundi.
Kavumbangu kwa sasa ndiye anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara akiwa ametikisa nyavu mara nane, sawa na Kipre Tcheche wa Azam FC.
Wataalamu wa usajili wa Yanga, Seif Ahmad ‘Magari’ na Abdallah Ahmad ‘Bin Kleb’ tayari wanajiandaa kwenda Kampala, Uganda itakapofanyika michuano ya Kombe la Challenge kutafuta wachezaji wa kuziba nafasi za Kavumbangu na Niyonzima.
Lakini habari zaidi zinasema nafasi ya Niyonzima itazibwa na Kabange Twite kutoka APR ya Rwanda, ndugu wa mchezaji mwingine wa Yanga, Mbuyu Twite.  

 

 

 

 

 

 

 

FRIENDS OF SIMBA WAKUTANA KUJADILI MAMBO KLABUNI

Hans Poppe
KUNDI la Friends of Simba (F.O.S.) linatarajiwa kukutana kesho jioni kujadili mustakabali wa klabu kwa ujumla na kutoa msimamo wao mbele ya wanachama na wapenzi wa klabu hiyo.
Hamkani si shwari Simba kwa sasa baada ya timu kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikitoka kuongoza kwa wastani wa pointi saba.
Mwenyekiti wa F.O.S., Zacharia Hans Poppe alisema jana kwamba, watakuwa na Mkutano kesho kujadili hali ya mambo klabuni kwao.
“Sisi kazi yetu ni kusapoti uongozi uliopo madarakani, kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri, sasa hali inayoendelea sasa inatutia shaka kuelekea mwakani, ambako tutakuwa na mtihani wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na pia Ligi ya Mabingwa.
Kwa hivyo tutakutana, tutazungumza kwa mapana marefu sana, ili tujue undani na ukweli wa matatizo yaliyopo klabuni na baada ya hapo na sisi tutatoa mtazamo wetu,”alisema kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Kamati ya Utendaji ya Simba, chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage ilikutana na kufikia maamuzi ya kuvunja Kamati zote ndogondogo za klabu pamoja na kulifuta tawi la wanachama wakorofi, Mpira Pesa la Magomeni, waliomtukana kipa Juma Kaseja na kuendesha harakati za mapinduzi.  
Lakini pia wasiwasi umeingia kutokana na kuvunjwa pia kwa Kamati ya Usajili, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Hans Poppe katika kipindi hiki kigumu ambacho klabu inatakiwa kurekebisha usajili kuelekea mzunguko wa pili na Ligi ya Mabingwa.
Mbali na hivyo, kuna suala la mchezaji Emanuel Okwi ambaye amemaliza mkataba wake kwenye klabu hiyo na alikuwa kwenye majadiliano na Kamati ya Usajili, ambayo yalifikia pazuri, lakini kwa kuvunjwa kwa Kamati hizo, maana yake mazungumzo hayo hayawezi kuendelea.  

YAW BERKO BADO YUPO YUPO SANA YANGA SC


Yaw Berko
KIPA Mghana, Yaw Berko hataachwa katika klabu ya Yanga kama ambavyo magazeti mengi nchini yamekuwa yakiandika.
Habari  kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba Berko ambaye mkataba wake unamalizika Mei mwakani, ataendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba huo.
Kipa huyo anayelipwa mshahara wa Sh. Milioni 1.5 kwa mwezi, amerudishwa benchi siku za karibuni baada ya kufululiza kufungwa mabao rahisi, jambo ambalo lilimkera kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
Kwa sababu hiyo, vyombo vya habari vikaanza kubashiri kwamba ataachwa mwezi ujao kwa sababu pia, tayari klabu hiyo imesajili mchezaji mwingine wa kigeni, Kabange Twite kutoka APR ya Rwanda.
Kanuni za Usajili za Ligi Kuu zinataka wachezaji watano tu wa kigeni kwa kila klabu, na Yanga tayari inao Yaw Berko, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Hamisi Kiiza kutoka Uganda na Didier Kavumbangu kutoka Burundi.
Lakini habari zaidi zinasema Kabange atachukua nafasi moja kati ya mbili zinazotarajiwa kuachwa na wachezaji wawili wa klabu hiyo, ambao watauzwa hivi karibuni, Niyonzima na Kavumbangu. 


JUVENTUS YAMUWINDA DROGBA.

KLABU ya Juventus ya Italia inapanga kumsajili mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Didier Drogba anayecheza kwenye klabu ya Shanghai Shenhua ya China katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Mabingwa hao wa Serie A wamekuwa sokoni kwa kipindi kirefu wakitafuta mshambuliaji ambapo katika kipindi cha karibuni wamekuwa wakihusishwa na Fernando Llorente na Pablo Asvaldo na hivi sasa wamehamishia nguvu zao kumsajili Drogba mwenye umri wa miaka 34. Drogba alijunga na kabu hiyo inayoshiriki Ligi kuu nchini China kutoka Chelsea katika kipindi cha usajili cha majira ya kiangazi lakini anaonekana hana furaha na ana nia ya kurejea Ulaya tena. Sababu ya Drogba ambaye analipwa euro milioni 12 kwa mwaka ni kutofurahishwa na mazingira ya klabu hiyo kumcheleweshea mshahara wake zaidi ya mara moja toka alipohamia huko. Hatahivyo Juventus wanakabiliwa na wakati mgumu wa kumsajili mchezaji huyo kwa kuwa wamepanga kupunguza mshahara wake kama akikubalia kujiunga nao na kumlipa euro milioni 4.5 kwa mwaka pamoja na posho nyingine.

HUGHES KUBAKIA QPR.

MENEJA wa Queens Park Rangers, Mark Hughes atabakia kuinoa klabu hiyo ambayo inasuasua katika mstari wa kushuka daraja kufuatia mkutano aliofanya na Ofisa Mkuu wa klabu hiyo Philip Beard. Kuna taarifa zilizosambaa kuwa Hughes ambaye amewahi kuwa kocha wa Wales alifukuzwa baada ya wawili kukutana katika uwanja wa mazoezi jana lakini mwakilishi wa kocha huyo Kia Joobchian alikanusha tetesi hizo na kudai sio za kweli. Hughes amekuwa na matokeo mabaya toka mwanzoni mwa msimu huu akiwa ameambulia alama nne pekee katika michezo 12 ambayo timu hiyo imecheza msimu huu hivyo kushika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 ambaye amewahi kuzifundisha klabu za Blackburn Rovers, Manchester City na Fulham amesisitiza kuwa hawezi kujiuzulu kibarua hicho kufuatia kufungwa nyumbani mabao 3-1 na Southampton ambao wote wanapigania kutoshuka daraja.

KAGAWA KUKAA NJE WIKI NNE ZAIDI.

KIUNGO nyota wa klabu ya Manchester United, Shinji Kagawa ameongezewa wiki zingine nne kukaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi yanayomsumbua. Kiungo huyo wa kimataifa wa Japan mwenye umri wa miaka 23 aliumia mguu wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao timu yake ilishinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Braga Oktoba 23 mwaka huu. Meneja wa United Sir Alex Ferguson alimtegemea mchezaji huyo kupona katika kipindi cha wiki nne mpaka tano lakini nyota huyo ameonekana kupona taratibu hivyo kuna uwezekano wa kukaa nje ya uwanja kwa nyingine nne nyingine. Pamoja na habari mbaya kuhusu Kagawa lakini Ferguson amefarijika baada ya beki wake nyota Phil Jones kurejea katika kikosi chake baada ya kuumia mgongo wakati maandalizi ya msimu mpya wa ligi hiyo. Beki huyo mwenye umri wa miaka 20 anatarajiwa kuwepo katika mchezo wa kundi H leo ambapo United watakuwa wageni wa Galatasaray ya Uturuki.

BECKHAM KUIKACHA GALAXY MWISHONI MWA MSIMU.

Nahodha wa zamani wa Uingereza, DAVID BECKHAM anatarajiwa kuondoka katika klabu ya Los Angeles Galaxy mwezi ujao baada miaka sita kucheza katika Ligi Kuu nchini Marekani maarufu kama Major League. Nyota huyo amepanga kuikacha klabu hiyo baada ya msimu wa ligi hiyo kumalizika Desemba 1 mwaka huu. Katika taarifa yake BECKHAM mwenye umri wa miaka 37 amesema kuwa anahitaji changamoto nyingine kabla ya kuamua rasmi kustaafu soka. Klabu ya Melbourne Heart ya Australia imedai kuwa ipo katika mazungumzo na nyota huyo ili wamsajili kwa ajili ya mechi 10 nyota huyo pamoja na mwenyewe kudai kuwa hana mpango wa kucheza soka katika Ligi Kuu ya nchini humo maarufu kama A League. BECKHAM alianza kucheza soka katika klabu ya Manchester United ambapo akiwa hapo alifanikiwa kushinda taji la Ligi Kuu nchini Uingereza mara sita pamoja na taji moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kutua Real Madrid mwaka 2003 na baadae Marekani mwaka 2007.

KESI YA PARK KUSIKILIZWA LEO.

Kesi ya mchezaji soka wa kimataifa wa Korea Kusini ambaye aliyeleta msuguano wa kidiplomasia na Japan baada ya kupeperusha bango lenye maandishi ya kisiasa katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika London, Uingereza inatarajiwa kusikilizwa tena na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Kamati hiyo ambayo itaamua kama mchezaji huyo aitwaye PARK JONG-WOO atakabiliwa na adhabu ya kufungiwa kutokana na kitendo chake hicho alichokifanya mwishoni mwa mchezo wa kugombea nafasi ya tatu dhidi ya Japan, imekuwa ikishindwa kutoa uamuzi wakati ilipokutana Octoba kusikiliza kesi hiyo. Msemaji wa FIFA amesema kuwa hata kama uamuzi utafikiwa hii leo hautatangazwa kwa siku kadhaa mpaka ripoti kamili iweze kuandikwa na kutafsiriwa kabla ya kutolewa kwa wandishi wa habari. Kiungo huyo alishika bango lenye ujumbe ambao unaokumbushia tofauti za mipaka kati Korea Kusini na Japan wakati akishangilia ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya mahasimu wao hao. PARK alizuiwa kuhudhuria sherehe za kukabidhiwa medali ya shaba waliyopata lakini Chama cha Soka cha Korea-KFA mwezi uliopita kilitoa taarifa kuwa wametumiwa ujumbe kupitia kamati ya nchi iliyoandaa michuano ya olimpiki ikithibitisha kuwa mchezaji huyo atapokea medali yake. 

FIFPro na FIFA zatangaza Makipa 5 kugombea kuwemo Kikosi Bora Duniani 2012

FERGUSON_KUBADILI_KIPA_KILA_MECHIChama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa Duniani, FIFPro, pamoja na FIFA leo wametangaza Majina ya Makipa watano ambao watakuwemo ndani ya Listi ya mwisho ya Wachezaji 55 watakaotangazwa huko Mjini Sao Paulo, Brazil hapo Novemba 29 kugombea kuwemo kwenye ile Timu Bora Duniani, rasmi kama FIFA/FIFPro World XI 2012.
Listi hiyo ya Wachezaji 55, ambayo leo imeanza kwa Makipa, itaongezwa Mabeki, Viungo na Mafowadi ambao watatangazwa kwa awamu kwa kuanzia Mabeki, watakaotajwa Novemba 22, Viungo hapo Novemba 26 na Mafowadi Novemba 29 na kukamilisha Wagombea 55 ambao watapigiwa Kura kupata Kikosi Bora cha Wachezaji 11 kikiundwa na Kipa, Mabeki wanne, Viungo watatu na Mafowadi watatu.
+++++++++++++++++++++++
MAKIPA 5 WALIOTEULIWA:
-Gianluigi Buffon (Italy, Juventus)
-Iker Casillas (Spain, Real Madrid)
-Petr Cech (Czech Republic, Chelsea)
-Joe Hart (England, Manchester City)
-Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich).
+++++++++++++++++++++++
Wachezaji 50,000, ambao ni Wanachama wa FIFPro, wamesambaziwa Fomu za kupigia Kura hicho Kikosi Bora.
Washindi watatangazwa Januari 7, 2013 kwenye Tafrija maalum ya kumpata Mchezaji Bora Duniani, Mshindi wa Tuzo ya the FIFA Ballon d’Or, itakayofanyika huko Zurich, Uswisi.
 

UEFA CHAMPIONS LIGI: NI patashika Juventus v Chelsea!

>>USHINDI MUHIMU kwa kila Timu, au BALAA!
>>MECHI: Novemba 20 UWANJA: Juventus Arena, Turin, Italy
Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, wanaikwaa Juventus, Mabingwa wa Italy, na kila mmoja anataka ushindi ili ajihakikishie anatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini hii ni Mechi isiyotabirika ukizingatia Mwezi Septemba, ndani ya Stamford Bridge, Chelsea waliongoza Bao 2-0, kwa Bao za Oscar, lakini Juve wakazinduka na kusawazisha kwa Mabao ya Arturo Vidal na Fabio Quagliarella na kutoka 2-2.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI E
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Shakhtar Donetsk Pointi 7
2 Chelsea 7
3 Juventus 6
4 Nordsjaelland 1 [NJE]
FAHAMU: Timu mbili za juu toka kila Kundi zinaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Timu itakayomaliza nafasi ya 3 itaingizwa EUROPA LIGI.
++++++++++++++++++++++++++
JUVENTUS-Claudio_MarchisioIkiwa Chelsea hawatafungwa na Juventus ni wazi watafuzu kwani Mechi yao ya mwisho ni nyumbani Stamford Bridge dhidi ya Nordsjaelland ambayo imeshatupwa nje ya Mashindano na ambayo Chelsea waliibonda Bao 4-0 huko kwao Denmark.
Chelsea wataingia kwenye Mechi hii bila ya nguzo yao kubwa, Nahodha wao John Terry, ambae ni majeruhi lakini Mabingwa hawa wa Ulaya nguzo yao kubwa zaidi ni Mashambulizi wakitegemea kasi na ushirikiano wa kina Ramires, Eden Hazard, Oscar, Juan Mata kumlisha Straika wao Fernando Torres.
Juve, wakiongozwa na Mkongwe Andrei Pirlo kwenye Kiungo na ambao walitoka sare Mechi zao zote 3 za kwanza za Kundi hili na kuzinduka tu katika Mechi ya 4 walipowaponda vibonde Nordsjaelland Bao 4-0, wana Wachezaji wengine hatari kama vile Kiungo Claudio Marchisio [Pichani], Mirko Vucinic, Arturo Vidal na Fabio Quagliarella.
Hawa wanatisha hasa ukizingatia Chelsea, chini ya Kocha Roberto Mancini, ina Difensi  ‘nyanya’ ambayo imevujisha Mabao 17 katika Mechi zao 8 zilizopita.
Katika Mechi za Ligi zao za Wikiendi hii iliyopita, Chelsea walichapwa 2-1 na WBA na Juventus kuambua sare ya 0-0 walipocheza na Lazio bila ya kuwa na nguzo yao kubwa Andrei Pirlo ambae alikuwa kifungoni.
Juve, ambao wapo chini ya Kocha Angelo Alessio kwa vile Kocha wao Antonio Conte yuko kifungoni, wameshatamka hii ni ‘Mechi yao ya Mwaka.’
Hakika ni patashika.
++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille [SAA 2 Usiku]
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona [SAA 2 Usiku]
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++++++++

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Man United bila Mastaa kibao yaenda Uturuki!

>>KUIVAA Galatasaray bila Rooney, RVP, Rio, Evra, De Gea, Giggs, Scholes!!
>>MECHI: Novemba 20 UWANJA: Turk Telecom Arena, Istanbul, Turkey
Manchester United, ambao wameshafuzu toka Kundi H la UEFA CHAMPIONZ LIGI wakiwa Nambari Wani huku wana Mechi mbili mkononi, leo wamesafiri kwenda Uturuki kucheza na Galatasaray bila Mastaa wao wengi.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI H
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Man United Pointi 12 [IMEFUZU]
2 Galatasaray 4
3 CFR Cluj-Napoca 4
4 Braga 3
FAHAMU: Timu mbili za juu toka kila Kundi zinaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Timu itakayomaliza nafasi ya 3 itaingizwa EUROPA LIGI.
++++++++++++++++++++++++++
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRAMastaa ambao hawakuwemo kwenye msafara ni Wayne Rooney, Robin van Persie, Rio Ferdinand, Ryan Giggs, Paul Scholes, Patrice Evra, Valencia na David de Gea pamoja na majeruhi Nani (Musuli ya Paja), Shinji Kagawa (Goti) na Jonny Evans (Nyonga).
Kikosi ambacho kimeenda Uturuki kinao Chipukizi 7 ambao hawajacheza Mechi za Ulaya ambao ni pamoja na Nick Powell, Larnell Cole, Davide Petrucci, Joshua King, Marnick Vermijl,  na Ryan Tunnicliffe na wawili ambao hawajacheza hata Mechi moja ya Kikosi cha Kwanza ni Kiungo Tom Thorpe na Kipa Sam Johnstone.
Rooney na De Gea hawakucheza Mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England ambayo Man United walifungwa 1-0 na Norwich City  na wote waliripotiwa ni Wagonjwa lakini leo walifanya mazoezi kama kawaida Kituo cha Carrington huko Jijini Manchester.
Inasadikiwa Bosi wa Man United Sir Alex Ferguson, akijua Timu yake imeshafuzu, ameamua kuwapumzisha Mastaa wake.
KIKOSI KAMILI KILICHOSAFIRI: Sam Johnstone, Anders Lindegaard; Rafael, Alexander Buttner, Phil Jones, Tom Thorpe, Marnick Vermijl, Scott Wootton, Michael Carrick, Davide Petrucci, Larnell Cole, Tom Cleverley, Darren Fletcher, Anderson, Nick Powell, Ashley Young, Ryan Tunnicliffe, Javier Hernandez, Joshua King, Danny Welbeck, Federico Macheda.
++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille [SAA 2 Usiku]
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona [SAA 2 Usiku]
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++++++++


BPL: Inaelekea patamu!!

BPL_LOGO>>MTANANGE WIKIENDI IJAYO STAMFORD BRIDGE: Chelsea v Man City!
Mabingwa watetezi, Manchester City, wametwaa uongozi wa BPL, Barclays Premier League, Ligi Kuu England, baada ya Wikiendi hii iliopita kuitwanga Aston Villa Bao 5-0 huku waliokuwa vinara Manchester United wakichapwa 1-0 na Norwich City na Chelsea wakipigwa bao 2-1 na WBA lakini Ligi hii sasa ndio kumekucha na Mechi mfululizo zitaziandama Klabu zikiwemo zile za UEFA CHAMPIONZ LIGI, EUROPA LIGI na CAPITAL ONE CUP kwa baadhi ya Klabu huku Chelsea, ambaio ndio Mabingwa wa Ulaya, wakiwa na safari ya kwenda Japan Mwezi Desemba kucheza Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani.
Wikiendi ijayo, Jumapili Novemba 25, Uwanja wa Stamford Bridge utawaka moto kwa mtanange mkali kati ya Chelsea na Man City.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man City Mechi 12 Pointi 28
2 Man United Mechi 12 Pointi 27
3 Chelsea Mechi 12 Pointi 24
4 WBA Mechi 12 Pointi 23
5 Everton Mechi 12 Pointi 20
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 11 Pointi 18
8 Tottenham Mechi 12 Pointi 17
9 Fulham Mechi 12 Pointi 16
10 Swansea Mechi 12 Pointi 16
11 Liverpool Mechi 12 Pointi 15
+++++++++++++++++++++++
Wakati Stamford Bridge ikiwaka, Jumamosi Novemba 24, Old Trafford itashuhudia Man United  wakitaka kutwaa tena uongozi watakapocheza na Timu ya mkiani QPR.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA ZA BPL kwa VIGOGO:
MAN CITY
MAN UNITED
CHELSEA
Nov 25 Chelsea v Man City
Nov 28 Wigan v Man City
Des 1 Man City v Everton
Des 9 Man City v Man Utd
Des 15 Newcastle v Man City
Des 22 Man City v Reading
Des 26 Sunderland v Man City
Des 29 Norwich v Man City
Jan 1 Man City v Stoke
Nov 24 Man Utd v QPR
Nov 28 Man Utd v West Ham
Des 1 Reading v Man Utd
Des 9 Man City v Man Utd
Des 15 Man Utd v Sunderland
Des 23 Swansea v Man Utd
Des 26 Man Utd v Newcasctle
Des 29 Man Utd v WBA
Jan 1 Wigan v Man Utd
Nov 25 Chelsea v Man City
Nov 28 Chelsea v Fulham
Des 1 West Ham v Chelsea
Des 8 Sunderland v Chelsea
Des 23 Chelsea v Aston Villa
Des 26 Norwich v Chelsea
Des 30 Everton v Chelsea
Jan 2 Chelsea v QPR
RIPOTI mechi ya Jumapili Novemba 18
Fulham 1 Sunderland 3
Jumapili Novemba 18, Uwanjani Craven Cottage, wenyeji Fulham walicheza Mtu 10 kwa Saa nzima baada ya Beki wao wa kutumainiwa Brede Hangeland kupewa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya na hilo liliwafanya wakubali kichapo cha Bao 3-1 toka kwa Sunderland huo ukiwa ushindi wa pili wa Sunderand katika Mechi 18 za BPL, Ligi Kuu England.
MAGOLI:
Fulham 1
-Petric 62′
Sunderland 3
-Fletcher 50′ Cuellar 65′ Sessegnon 70′
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumatatu Novemba 19
[SAA 5 Usiku]
West Ham V Stoke
Jumamosi Novemba 24
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland V West Brom
[SAA 12 Jioni]
Everton V Norwich
Man Utd V QPR
Stoke V Fulham
Wigan V Reading
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Aston Villa V Arsenal
Jumapili Novemba 25
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea V Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Southampton V Newcastle
[SAA 1 Usiku]
Chelsea V Man City
Tottenham V West Ham
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland V QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa V Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea V Fulham
Everton V Arsenal
Southampton V Norwich
Stoke V Newcastle
Swansea V West Brom
Tottenham V Liverpool
Man Utd V West Ham
[SAA 5 Usiku]
Wigan V Man City

OSCAR SORES A WONDER GOAL AGAINST KIBIBI KIZEE----EBU YAANGALIE MAGOLI YA DOGO OSCAR HAFU KESHO CHELSEA IPO UGENINI KUCHEZA NA JUVENTUS UNATABIRI ITAKUWAJE??????????



 

 

 

FIFPro na FIFA zatangaza Makipa 5 kugombea kuwemo Kikosi Bora Duniani 2012

FERGUSON_KUBADILI_KIPA_KILA_MECHIChama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa Duniani, FIFPro, pamoja na FIFA leo wametangaza Majina ya Makipa watano ambao watakuwemo ndani ya Listi ya mwisho ya Wachezaji 55 watakaotangazwa huko Mjini Sao Paulo, Brazil hapo Novemba 29 kugombea kuwemo kwenye ile Timu Bora Duniani, rasmi kama FIFA/FIFPro World XI 2012.
Listi hiyo ya Wachezaji 55, ambayo leo imeanza kwa Makipa, itaongezwa Mabeki, Viungo na Mafowadi ambao watatangazwa kwa awamu kwa kuanzia Mabeki, watakaotajwa Novemba 22, Viungo hapo Novemba 26 na Mafowadi Novemba 29 na kukamilisha Wagombea 55 ambao watapigiwa Kura kupata Kikosi Bora cha Wachezaji 11 kikiundwa na Kipa, Mabeki wanne, Viungo watatu na Mafowadi watatu.
+++++++++++++++++++++++
MAKIPA 5 WALIOTEULIWA:
-Gianluigi Buffon (Italy, Juventus)
-Iker Casillas (Spain, Real Madrid)
-Petr Cech (Czech Republic, Chelsea)
-Joe Hart (England, Manchester City)
-Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich).
+++++++++++++++++++++++

Wachezaji 50,000, ambao ni Wanachama wa FIFPro, wamesambaziwa Fomu za kupigia Kura hicho Kikosi Bora.
Washindi watatangazwa Januari 7, 2013 kwenye Tafrija maalum ya kumpata Mchezaji Bora Duniani, Mshindi wa Tuzo ya the FIFA Ballon d’Or, itakayofanyika huko Zurich, Uswisi.
 

UEFA CHAMPIONS LIGI: NI patashika Juventus v Chelsea!


>>USHINDI MUHIMU kwa kila Timu, au BALAA!
>>MECHI: Novemba 20 UWANJA: Juventus Arena, Turin, Italy
Mabingwa wa Ulaya, Chelsea, wanaikwaa Juventus, Mabingwa wa Italy, na kila mmoja anataka ushindi ili ajihakikishie anatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini hii ni Mechi isiyotabirika ukizingatia Mwezi Septemba, ndani ya Stamford Bridge, Chelsea waliongoza Bao 2-0, kwa Bao za Oscar, lakini Juve wakazinduka na kusawazisha kwa Mabao ya Arturo Vidal na Fabio Quagliarella na kutoka 2-2.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI E
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Shakhtar Donetsk Pointi 7
2 Chelsea 7
3 Juventus 6
4 Nordsjaelland 1 [NJE]
FAHAMU: Timu mbili za juu toka kila Kundi zinaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Timu itakayomaliza nafasi ya 3 itaingizwa EUROPA LIGI.

JUVENTUS-Claudio_MarchisioIkiwa Chelsea hawatafungwa na Juventus ni wazi watafuzu kwani Mechi yao ya mwisho ni nyumbani Stamford Bridge dhidi ya Nordsjaelland ambayo imeshatupwa nje ya Mashindano na ambayo Chelsea waliibonda Bao 4-0 huko kwao Denmark.
Chelsea wataingia kwenye Mechi hii bila ya nguzo yao kubwa, Nahodha wao John Terry, ambae ni majeruhi lakini Mabingwa hawa wa Ulaya nguzo yao kubwa zaidi ni Mashambulizi wakitegemea kasi na ushirikiano wa kina Ramires, Eden Hazard, Oscar, Juan Mata kumlisha Straika wao Fernando Torres.
Juve, wakiongozwa na Mkongwe Andrei Pirlo kwenye Kiungo na ambao walitoka sare Mechi zao zote 3 za kwanza za Kundi hili na kuzinduka tu katika Mechi ya 4 walipowaponda vibonde Nordsjaelland Bao 4-0, wana Wachezaji wengine hatari kama vile Kiungo Claudio Marchisio [Pichani], Mirko Vucinic, Arturo Vidal na Fabio Quagliarella.
Hawa wanatisha hasa ukizingatia Chelsea, chini ya Kocha Roberto Mancini, ina Difensi  ‘nyanya’ ambayo imevujisha Mabao 17 katika Mechi zao 8 zilizopita.
Katika Mechi za Ligi zao za Wikiendi hii iliyopita, Chelsea walichapwa 2-1 na WBA na Juventus kuambua sare ya 0-0 walipocheza na Lazio bila ya kuwa na nguzo yao kubwa Andrei Pirlo ambae alikuwa kifungoni.
Juve, ambao wapo chini ya Kocha Angelo Alessio kwa vile Kocha wao Antonio Conte yuko kifungoni, wameshatamka hii ni ‘Mechi yao ya Mwaka.’
Hakika ni patashika.

RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille [SAA 2 Usiku]
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona [SAA 2 Usiku]
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF

UEFA CHAMPIONZ LIGI: Man United bila Mastaa kibao yaenda Uturuki!

>>KUIVAA Galatasaray bila Rooney, RVP, Rio, Evra, De Gea, Giggs, Scholes!!
>>MECHI: Novemba 20 UWANJA: Turk Telecom Arena, Istanbul, Turkey
Manchester United, ambao wameshafuzu toka Kundi H la UEFA CHAMPIONZ LIGI wakiwa Nambari Wani huku wana Mechi mbili mkononi, leo wamesafiri kwenda Uturuki kucheza na Galatasaray bila Mastaa wao wengi.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI H
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Man United Pointi 12 [IMEFUZU]
2 Galatasaray 4
3 CFR Cluj-Napoca 4
4 Braga 3
FAHAMU: Timu mbili za juu toka kila Kundi zinaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Timu itakayomaliza nafasi ya 3 itaingizwa EUROPA LIGI.
++++++++++++++++++++++++++
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRAMastaa ambao hawakuwemo kwenye msafara ni Wayne Rooney, Robin van Persie, Rio Ferdinand, Ryan Giggs, Paul Scholes, Patrice Evra, Valencia na David de Gea pamoja na majeruhi Nani (Musuli ya Paja), Shinji Kagawa (Goti) na Jonny Evans (Nyonga).
Kikosi ambacho kimeenda Uturuki kinao Chipukizi 7 ambao hawajacheza Mechi za Ulaya ambao ni pamoja na Nick Powell, Larnell Cole, Davide Petrucci, Joshua King, Marnick Vermijl,  na Ryan Tunnicliffe na wawili ambao hawajacheza hata Mechi moja ya Kikosi cha Kwanza ni Kiungo Tom Thorpe na Kipa Sam Johnstone.
Rooney na De Gea hawakucheza Mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu England ambayo Man United walifungwa 1-0 na Norwich City  na wote waliripotiwa ni Wagonjwa lakini leo walifanya mazoezi kama kawaida Kituo cha Carrington huko Jijini Manchester.
Inasadikiwa Bosi wa Man United Sir Alex Ferguson, akijua Timu yake imeshafuzu, ameamua kuwapumzisha Mastaa wake.
KIKOSI KAMILI KILICHOSAFIRI: Sam Johnstone, Anders Lindegaard; Rafael, Alexander Buttner, Phil Jones, Tom Thorpe, Marnick Vermijl, Scott Wootton, Michael Carrick, Davide Petrucci, Larnell Cole, Tom Cleverley, Darren Fletcher, Anderson, Nick Powell, Ashley Young, Ryan Tunnicliffe, Javier Hernandez, Joshua King, Danny Welbeck, Federico Macheda.
++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille [SAA 2 Usiku]
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona [SAA 2 Usiku]
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF

 

 

  MCHAKATO WA UCHAGUZI MKOA WA TABORA WAENDELEA KUPAMBA MOTO.LEOWAPITISHA MAJINA  WAGOMBEA WANAOWANIA NAFASI MBALI MBALI

 

Mchakato wa uchaguzi mkoa wa tabora TAREFA umeendelea kupamba moto na leo terehe 19/11/2012  kamati ya uchaguzi imepitia fomu za waombaji na kutangaza matokeo ya upitiaji wa fomu hizo na fomu zimeshatumwa TFF jijini dare es salaam na kamati nzima ya TAREFA chini ya uenyekiti wa mkama bwire akisaidiwa na katibu wake mwene ufunguo pamoja na mjumbe mzee Adam fundikira.

Majina yaliyopitishwa katika usaili huo ni majina 19 katika nafasi zinazongombewa,mwenyekiti,katibu,katibu msaidizi,makamu mwenyekiti,wajumbe wa mkutano mkuu TFF ,mweka hazina ,mweka hazina msaidizi,katibu msaidizi,wawakilishi wa vilabu,mwakilishi wanawke TFF pamoja na ujumbe wa kamati ya utendaji.

Katika nafasi ya mwenyekiti kuna wagombea watatu [3] nao ni MUSA NTIMIZI,YUSUPH KITUMBO,LAURENT PAUL,katika nafasi ya makamu mwenyekiti kuna mgombea mmoja naye ni ALAIJA MWIGA,na katika nafasi ya katibu mkuu kuna wagombea wawili[2]nao ni FATTY REMTULA,na ALBERT SITTA.

Katika nafasi ya katibu msaidizi haikuwa na mgombea ipo wazi,pia nafasi ya mweka hazina ina mgombea mmoja naye ni MUSSA MSANANGA,na nafasi ya mweka hazina msaidizi haina mtu ipo wazi.

Nafasi ya wajumbe wa mkutano mkuu TFF ina wagombea wanne [4] nao ni DICK MLIMKA,MILAMBO KAMILI,RAMADHANI MAGHEMBE,na CHARLES MWAKAMBAYA.

Wawakilishi wa vilabu TFF ina wagombea watatu[3] nao ni ACHERY MANJORI AMOSSI,RAZACK JUMA IRUMBA,na LUAMBA YUSSA,vile vile katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ina wagombea watatu[3] nao ni STANSLAUS N.SIZYA,ABDUL MOHAMMEDY AMAN,na JAMES ERICK KABEPELE.

Na katika nafasi ya mwakilishi wa mpira wa miguu kwa wanawake ina mgombea mmoja naye ni JANETH MAICHAEL ambaye amejitosa pekee yake kugombea nafasi hii.

Na tarehe 20-24/11/2012 itakuwa ni kutoa fursa ya pingamizi kwa waombaji uongozi .Mwisho wa kupokea pingamizi ni tarehe 24/11/2012 saa 10;00 alasiri katika ofisi za TUWASA mkoa wa tabora.hakuna ada ya kuweka pingamizi ni bure ila mbali tu pingamizi zizingatie matakwa ya ibara ya 11[2]ya kanuni za uchaguzi.

Na tarehe 25/11/2012 kamati ya uchaguzi ya mkoa wa tabora TAREFA itajadili pingamizi na kufanya maamuzi na tarehe inayofuata ya 26-27/11/2012 itakuwa ni usaili na kutangaza matokeo/kuwajulisha kwa maandishi wagombea matokeo ya usaili.

Tarehe 28-30/11/2012 itakuwa ni kutoa fursa ya kukata Rufaa,kwenye kamati ya uchaguzi TFF mwisho wa kupokea rufaa ni tarehe 30/11/2012 saa 10;00 alasiri.

Vile vile kamati ya uchaguzi ya TFF itasikiliza rufaa toka tarehe 01-05/12/2012 kama zitakuwa zipo na kutangaza matokeo ya rufaa,kama hakuna rufaa kamati ya uchaguzi ya TAREFA itatangaza majina ya wagombea na nafasi zao na tayari kwa kuanza kampeni.

06/12/2012 baada ya maamuzi ya uamuzi wa kamati ya TFF kamati ya uchaguzi ya TAREFA itatangaza majina na nafasi zao na waanze kampeni tayari na tarehe 22/12/2012 uchaguzi utafanyika kutafuta wawakilishi watakaopitishwa katika uchaguzi ule yaani kuwapigia kura wagombea.

 

BONANZA LA WACHEZAJI WA ZAMANI LILIKUWA ZAIDI YA BURUDANI BWANA

TIMU ya maveterani ya Simba imeshindwa kuwatambia maveterani wenzao wa Kariakoo ya Lindi baada ya kukubali kutoka sare ya 0-0 kwenye bonanza lililofanyika jana kwenye viwanja vya TTC sigara, jijini Dar es salaam.

Bonanza hili lilihusisha timu zilizocheza ligi zamani na jumala ya timu saba zimeshiriki.

Simba ilisheheni wachezaji wake mahiri wa zamani akina Bita John, Husein Balo, Majuto Comu, Quresh Ufunguo, Damian Kimti, Barnabas Sekelo, Gabriel Emanuel, Said Msasu, Abubakar Kombo, Abdul Mashine na wengine wengi.

Mchezo huo ambao ulikuwa burudani kwa mashabiki ulishuhudia Dua Said wa Simba wakikosa penalti waliyopata dakika ya 60 baada ya mshambuliaji wao Husein Balo kufanyiwa faulo na golikipa wa Kariakoo Lindi Jumanne Ally.

Mchezo mwingine ulizikutanisha Pilsener na Reli ya Morogoro, Reli walishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Salhina Mjengwa baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Mwanamtwa Kiwelu.

Bandari iliifunga Mirambo ya Tabora mabao 3-2, na magoli ya bandari yalifungwa Kingsley Malwilo aliyefunga mabao mawili na Mohamed Hussein na wafungaji wa Mirambo ni Paul Muhonda na Athuman Tippo

Kikosi cha Reli ya Morogoro na viongozi wake

Kikosi cha Simba

Mgeni Rasmi Jamal Rwambo akifungua bonanza

Jamali Rwambo akisalimiana na wachezaji wa Mirambo ya Tabora


Beki wa Kariakoo Lindi Mwamedi Pwani akimdhibiti mshambuliaji wa Simba Bita John kwenye bonanza la wachezaji wa zamani lililofanyika juzi viwanja vya TTC Sigara, mchezo ulimalizika 0-0.

Kocha Mshindo Msolwa ambaye jana alikuwa anaifundisha Mirambo ya Tabora

 Kenedy Mwaisabula akifurahia mchezo uwanjani


Kikosi cha Kariakoo ya Lindi

Kikosi cha Pilsner

Kikosi cha Reli "Kiboko ya vigogog"


Hapa mchezo umenoga, mgeni rasmi anatazama kwa makini
Huyu ni mchezaji wa Reli alicheza dakika kumi akatoka kupumzika kwenye hema baadae akarudi, ndio mpira wa kikubwa/kiutuzima huo

Mirambo Tabora hiyo wanasakata kabumbu na Bandari ya Mtwara


Mbwiga ndani ya jezi kuivaa Ushirika ya Kilimanjaro lakini alitoka mapema. Sikiliza maneno yake baada ya kutoka "Mkifungwa ni nyie maana mimi ninetoka timu ipo salama" lakini walitoka suluhu

Mirambo na Bandari (blue)

Bwiga akiwapa mashabiki udambwiudambwi

Mwamuzi wa zamani mzee Makwega

BPL: Inaelekea patamu!!


BPL_LOGO>>MTANANGE WIKIENDI IJAYO STAMFORD BRIDGE: Chelsea v Man City!
Mabingwa watetezi, Manchester City, wametwaa uongozi wa BPL, Barclays Premier League, Ligi Kuu England, baada ya Wikiendi hii iliopita kuitwanga Aston Villa Bao 5-0 huku waliokuwa vinara Manchester United wakichapwa 1-0 na Norwich City na Chelsea wakipigwa bao 2-1 na WBA lakini Ligi hii sasa ndio kumekucha na Mechi mfululizo zitaziandama Klabu zikiwemo zile za UEFA CHAMPIONZ LIGI, EUROPA LIGI na CAPITAL ONE CUP kwa baadhi ya Klabu huku Chelsea, ambaio ndio Mabingwa wa Ulaya, wakiwa na safari ya kwenda Japan Mwezi Desemba kucheza Mashindano ya FIFA kusaka Klabu Bingwa Duniani.
Wikiendi ijayo, Jumapili Novemba 25, Uwanja wa Stamford Bridge utawaka moto kwa mtanange mkali kati ya Chelsea na Man City.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man City Mechi 12 Pointi 28
2 Man United Mechi 12 Pointi 27
3 Chelsea Mechi 12 Pointi 24
4 WBA Mechi 12 Pointi 23
5 Everton Mechi 12 Pointi 20
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 11 Pointi 18
8 Tottenham Mechi 12 Pointi 17
9 Fulham Mechi 12 Pointi 16
10 Swansea Mechi 12 Pointi 16
11 Liverpool Mechi 12 Pointi 15
+++++++++++++++++++++++
Wakati Stamford Bridge ikiwaka, Jumamosi Novemba 24, Old Trafford itashuhudia Man United  wakitaka kutwaa tena uongozi watakapocheza na Timu ya mkiani QPR.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA ZA BPL kwa VIGOGO:
MAN CITY MAN UNITED CHELSEA
Nov 25 Chelsea v Man City
Nov 28 Wigan v Man City
Des 1 Man City v Everton
Des 9 Man City v Man Utd
Des 15 Newcastle v Man City
Des 22 Man City v Reading
Des 26 Sunderland v Man City
Des 29 Norwich v Man City
Jan 1 Man City v Stoke
Nov 24 Man Utd v QPR
Nov 28 Man Utd v West Ham
Des 1 Reading v Man Utd
Des 9 Man City v Man Utd
Des 15 Man Utd v Sunderland
Des 23 Swansea v Man Utd
Des 26 Man Utd v Newcasctle
Des 29 Man Utd v WBA
Jan 1 Wigan v Man Utd
Nov 25 Chelsea v Man City
Nov 28 Chelsea v Fulham
Des 1 West Ham v Chelsea
Des 8 Sunderland v Chelsea
Des 23 Chelsea v Aston Villa
Des 26 Norwich v Chelsea
Des 30 Everton v Chelsea
Jan 2 Chelsea v QPR
RIPOTI mechi ya Jumapili Novemba 18
Fulham 1 Sunderland 3
Jumapili Novemba 18, Uwanjani Craven Cottage, wenyeji Fulham walicheza Mtu 10 kwa Saa nzima baada ya Beki wao wa kutumainiwa Brede Hangeland kupewa Kadi Nyekundu kwa rafu mbaya na hilo liliwafanya wakubali kichapo cha Bao 3-1 toka kwa Sunderland huo ukiwa ushindi wa pili wa Sunderand katika Mechi 18 za BPL, Ligi Kuu England.
MAGOLI:
Fulham 1
-Petric 62′
Sunderland 3
-Fletcher 50′ Cuellar 65′ Sessegnon 70′
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumatatu Novemba 19
[SAA 5 Usiku]
West Ham V Stoke
Jumamosi Novemba 24
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland V West Brom
[SAA 12 Jioni]
Everton V Norwich
Man Utd V QPR
Stoke V Fulham
Wigan V Reading
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Aston Villa V Arsenal
Jumapili Novemba 25
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea V Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Southampton V Newcastle
[SAA 1 Usiku]
Chelsea V Man City
Tottenham V West Ham
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland V QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa V Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea V Fulham
Everton V Arsenal
Southampton V Norwich
Stoke V Newcastle
Swansea V West Brom
Tottenham V Liverpool
Man Utd V West Ham
[SAA 5 Usiku]
Wigan V Man City

WENGER: ‘Walcott haondoki Arsenal Januari!’

>>KAMA HASAINI MKATABA MPYA, KUONDOKA BURE BILA MALIPO MWAKANI!!
>>AMESHAGOMEA MKATABA MPYA wa MSHAHARA PAUNI 75,000 kwa Wiki!
WALCOTT_WILSHERE_OXArsene Wenger amesisitiza kuwa Arsenal haitamuuza Theo Walcott, ambae sasa ndie anaongoza kwa kuwafungia Bao nyingi, Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguka na msimamo huo unaihatarisha Klabu hiyo kutopata Senti hata moja ifikapo mwisho wa Msimu ambapo Mkataba wa Mchezaji huyo utakapomalizika na yeye kuwa huru kuhamia popote.
Ikifika Mwezi Januari, Sheria zinamruhusu Walcott, Miaka 23, kusaini Makubaliano ya Awali na Klabu yeyote inayotaka kumnunua ikiwa Arsenal na upande wa Walcott hautaafikiana ili kumfanya Mchezaji huyo kusaini Mkataba mpya na Arsenal.
Hadi sasa mazungumzo kati ya Arsenal na Walcott kuhusu Mkataba mpya yamekwama lakini Wenger bado anasisitiza Mchezaji huyo hauzwi.
Mwezi Agosti, Walcott aliukataa Mkataba mpya wa Arsenal wa Miaka mitano ambao ungemlipa Mshahara wa Pauni 75,000 kwa Wiki na ameshadokezea kuwa huenda maisha yake ya baadae yapo Klabu nyingine.
+++++++++++++++++++++++++++++
WAFUNGAJI BORA wa Arsenal Msimu huu:
-Theo Walcott Magoli 9
-Olivier Giroud 7
-Lukas Podolski 6
-Gervinho 5
-Santi Cazorla 4
+++++++++++++++++++++++++++++
Mbali ya Walcott kutaka Mshahara wa juu zaidi, Winga huyo, ambae alijiunga na Arsenal Mwaka 2006 kutoka Southampton, amekuwa akitaka achezeshwe kama Straika na si Winga hoja ambayo pengine ina msingi kwa vile Msimu huu ndie anaeongoza kwa kufunga Bao nyingi hapo Arsenal.
Klabu ya Arsenal imekuwa ikikumbwa na sakata kama hili la Walcott ambapo Nyota wao, wakikaribia kumaliza Mikataba yao, hugomea Mkataba mpya na kuilazimisha Klabu iwauze badala ya kungoja wamalize Mikataba na kuhama bila Klabu kulipwa hata Senti moja.
Hivi karibuni baadhi ya Wachezaji waliohama, wengine kwa mtindo huo, ni pamoja na Robin van Persie, Alex Song na Cesc Fabregas.

 

MISHAHARA ZA WACHEZAJI WAKUBWA BARANI ULAYAAAAAAAAAA

Lionel Messi - Mpira wa miguu FC Barcelona - Kuzaliwa: 1987 Argentina
Lionel Messi
Lionel Messi
Mwaka: ? 39.000.000,00
Kwa Mwezi: ? 3.250.000,00
Kwa Wiki: ? 780.000,00
Kwa Siku: ? 156.000,00

Didier Drogba - Mchezaji wa soka ya Shanghai Shenhua - Kuzaliwa: 1978 Ivory Coast - Oa/Olewa - Watoto: 3
 
Didier Drogba
Didier Drogba
Mwaka: ? 10.400.000,00
Kwa Mwezi: ? 866.666,00
Kwa Wiki: ? 208.000,00
Kwa Siku: ? 41.600,00

Michael Essien - Soka mchezaji Chelsea - Kuzaliwa: Ghana 1982 - Oa/Olewa - Watoto: 1
 
Michael Essien
Michael Essien
Mwaka: ? 6.600.000,00
Kwa Mwezi: ? 550.000,00
Kwa Wiki: ? 132.000,00
Kwa Siku: ? 26.400,00

Emmanuel Adebayor - Soka mchezaji wa Manchester City - Kuzaliwa: 1984 Togo
 

Emmanuel Adebayor
Emannuel Adebayor
Mwaka: ? 14.000.000,00
Kwa Mwezi: ? 1.166.666,00
Kwa Wiki: ? 280.000,00
Kwa Siku: ? 56.000,00

Samuel Eto'o - Soka mchezaji Anzhi Makhachkala - Kuzaliwa: 1981 Cameroon - Oa/Olewa - Watoto: 3
 
Samuel Eto'o
Samuel Eto'o
Mwaka: ? 28.500.000,00
Kwa Mwezi: ? 2.375.000,00
Kwa Wiki: ? 570.000,00
Kwa Siku: ? 114.000,00

 
David Beckham - Soka mchezaji Los Angeles Galaxy / AC Milan - Kuzaliwa: 1975 Uingereza - Oa/Olewa - Watoto: 4
 
David Beckham
David Beckham
 
Mwaka: ? 46.000.000,00
Kwa Mwezi: ? 3.833.333,00
Kwa Wiki: ? 920.000,00
Kwa Siku: ? 184.000,00

Wayne Rooney - Soka mchezaji wa Manchester United - Kuzaliwa: 1985 Uingereza - Rafiki wa Kike
Wayne Rooney
 
Wayne Rooney
Mwaka: ? 24.300.000,00
Kwa Mwezi: ? 2.025.000,00
Kwa Wiki: ? 486.000,00
Kwa Siku: ? 97.200,00

Andrés Iniesta - Soka mchezaji FC Barcelona - Kuzaliwa: 1984 Hispania
 

Andrés Iniesta
Andrés Iniesta
Mwaka: ? 5.000.000,00
Kwa Mwezi: ? 416.666,00
Kwa Wiki: ? 100.000,00
Kwa Siku: ? 20.000,00

Luis Alberto Suárez - Soka Player FC Liverpool - Kuzaliwa: 1987, Urugay - Oa/Olewa - Watoto: 1
 
Luis Alberto Suárez
Luis Alberto Suárez
Mwaka: ? 4.200.000,00
Kwa Mwezi: ? 350.000,00
Kwa Wiki: ? 84.000,00
Kwa Siku: ? 16.800,00

Thierry Henry - Soka mchezaji New York Red Bulls - Kuzaliwa: 1977 Ufaransa - Oa/Olewa - Watoto: 1
 
Thierry Henry
Thierry Henry
Mwaka: ? 5.600.000,00
Kwa Mwezi: ? 466.666,00
Kwa Wiki: ? 112.000,00
Kwa Siku: ? 22.400,00

Michael Owen - Soka mchezaji Newcastle United - Kuzaliwa: 1979 Uingereza - Oa/Olewa - Watoto: 3
 
Michael Owen
Michael Owen
Mwaka: ? 2.000.000,00
Kwa Mwezi: ? 166.666,00
Kwa Wiki: ? 40.000,00
Kwa Siku: ? 8.000,00

Gregory van der Wiel - Hajaoa/Hajaolewa
 
Gregory van der Wiel
Gregory van der Wiel
Mwaka: ? 1.450.000,00
Kwa Mwezi: ? 120.833,00
Kwa Wiki: ? 29.000,00
Kwa Siku: ? 5.800,00

Clint Dempsey - Oa/Olewa - Watoto: 2
Clint Dempsey
 
Clint Dempsey
Mwaka: ? 7.500.000,00
Kwa Mwezi: ? 625.000,00
Kwa Wiki: ? 150.000,00
Kwa Siku: ? 30.000,00
Dirk Kuijt - Oa/Olewa - Watoto: 4
Dirk Kuijt
Dirk Kuijt
Mwaka: ? 5.100.000,00
Kwa Mwezi: ? 425.000,00
Kwa Wiki: ? 102.000,00
Kwa Siku: ? 20.400,00

Cuauhtémoc Blanco - Hajaoa/Hajaolewa - Watoto: 0
 
Cuauhtémoc Blanco
Cuauhtémoc Blanco
Mwaka: ? 7.200.000,00
Kwa Mwezi: ? 600.000,00
Kwa Wiki: ? 144.000,00
Kwa Siku: ? 28.800,00

Giovanni van Bronckhorst - Mstaafu - Oa/Olewa - Watoto: 2
 
Giovanni van Bronckhorst
Giovanni van Bronckhorst
Mwaka: ? 1.700.000,00
Kwa Mwezi: ? 141.666,00
Kwa Wiki: ? 34.000,00
Kwa Siku: ? 6.800,00

Rafael van der Vaart - Oa/Olewa - Watoto: 1
 
Rafael van der Vaart
Rafael van der Vaart
Mwaka: ? 3.620.000,00
Kwa Mwezi: ? 301.666,00
Kwa Wiki: ? 72.400,00
Kwa Siku: ? 14.480,00

John Heitinga - Oa/Olewa - Watoto: 1
 
John Heitinga
John Heitinga
Mwaka: ? 4.500.000,00
Kwa Mwezi: ? 375.000,00
Kwa Wiki: ? 90.000,00
Kwa Siku: ? 18.000,00

Mark van Bommel - Oa/Olewa - Watoto: 3
 
Mark van Bommel
Mark van Bommel
Mwaka: ? 9.620.000,00
Kwa Mwezi: ? 801.666,00
Kwa Wiki: ? 192.400,00
Kwa Siku: ? 38.480,00

Klaas Jan Huntelaar - Rafiki wa Kike - Watoto: 1
 
Klaas Jan Huntelaar
Klaas Jan Huntelaar
Mwaka: ? 4.450.000,00
Kwa Mwezi: ? 370.833,00
Kwa Wiki: ? 89.000,00
Kwa Siku: ? 17.800,00

Javier Hernandez - "Chicharito"
 
Javier Hernandez - "Chicharito"
Javier Hernandez - "Chicharito"
Mwaka: ? 4.000.000,00
Kwa Mwezi: ? 333.333,00
Kwa Wiki: ? 80.000,00
Kwa Siku: ? 16.000,00

Zlatan Ibrahimovic - Soka mchezaji Paris St-Germain - Kuzaliwa: 1981 Sweden - Oa/Olewa - Watoto: 2
Zlatan Ibrahimović
 Zlatan Ibrahimović
Mwaka: ? 20.000.000,00
Kwa Mwezi: ? 1.666.666,00
Kwa Wiki: ? 400.000,00
Kwa Siku: ? 80.000,00

Franck Ribéry - Oa/Olewa - Watoto: 2
 
Franck Ribéry
Franck Ribéry
Mwaka: ? 11.600.000,00
Kwa Mwezi: ? 966.666,00
Kwa Wiki: ? 232.000,00
Kwa Siku: ? 46.400,00

Carles Puyol - Soka mchezaji Barcelona - Kuzaliwa: 1978 Spain - Rafiki wa Kike
 
Carles Puyol
Carles Puyol
Mwaka: ? 11.400.000,00
Kwa Mwezi: ? 950.000,00
Kwa Wiki: ? 228.000,00
Kwa Siku: ? 45.600,00

WATANO WALIOACHA HISTORIA ISIYOFUTIKA CHALLENGE

Bwalya

KALUSHA BWALYA:
SAHAU kuhusu Zambia iliyochukua Kombe a Challenge mwaka 2006, wakati huo imekwishajitoa katika nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na kuingia nchi za Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Zambia iliyotikisa katika soka ya Afrika Mashariki na kati ni ile iliyokuwa ikiitwa KK Eleven kuanzia miaka ya 1970 hadi 1990 mwanzoni, kabla ya ajali ya ndege iliyoua nyota wa kikosi hicho pwani ya Gabon mwaka 1993.
Kalusha Bwalya alikuwa katika orodha ya wachezaji waliotakiwa kuingia kwenye ndege iliyopata ajali, lakini bahati nzuri kwake alisema atatokea kwenye klabu yake moja kwa moja Ulaya kwenda Tunisia, hivyo akanusurika.
Katika historia yake ya ushiriki wa Challenge, KK Eleven ilibeba taji hilo mwaka 1984 na 1991 ambao, Kalusha Bwalya aliungana na Majid Musisi katika ufungaji bora, kila mmoja akifunga mabao yake matatu.
Challenge ya mwisho kwa Bwalya ilikuwa mwaka 1992 mjini Mwanza, alipoiongoza Zambia hadi Nusu Fainali ilipotolewa na Uganda kwa penalti 4-2, Uwanja wa CCM Kirumba kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.
Huwezi kuizungumzia historia ya Challenge bila ya kumtaja Bwalya, aliyezaliwa Agosti 16, mwaka 1963 mjini Mufulira, kwani enzi zake alikuwa mkali haswa.
Huyo ni mchezaji aliyeichezea Zambia mechi nyingi zaidi na kuifungia mabao mengi zaidi pia kuliko mchezaji yoyote hadi sasa. Ndiye mchezaji babu kubwa zaidi kuwahi kutokea katika ardhi ya Zambia. Unamzungumzia Mwanasoka Bora wa Afrika mwaka 1988, ambaye mwaka 1996 aliingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, ambayo ilichukuliwa na Mwafrika mwenzake, George Weah.
Omondi Philip
PHILIP OMONDI:
UGANDA ndio mabingwa wa kihistoria wa michuano ya Challenge, wakiwa wamebeba Kombe hilo mara 12 (1973, 1976, 1977, 1989, 1990, 1992, 1996, 2000, 2003, 2008, 2009 na 2011).
Wapo wachezaji wawili ambao huwezi kuwatenganisha na mafanikio ya The Cranes katika Challenge. Akina nani hao?
Wote hawa wamekwishatangulia mbale ya haki hivi sasa, Philip Omondi na Majjid Musisi.
Phillip Omondi aliyezaliwa mwaka 1957 na kufariki dunia Aprili 21, mwaka 1999 huyu alikuwa mtu hatari sana enzi zake na waliobahatika kumuona wanaweza kukiri juu ya hilo.
Omondi aliyechezea klabu ya Kampala City Council FC kuanzia mwaka 1973 hadi 1979, alipotimkia Sharjah ya Falme za Kiarabu (UAE) alikuwa shukaa wa Uganda hadi kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Omondi aliichezea The Cranes katika fainali za Afrika miaka ya 1974, 1976 na za 1978, ambazo pamoja na kuifikisha Cranes fainali, pia aliibuka mfungaji bora.
Kwenye Challenge, Omondi aliisaidia mno Uganda kutwaa mataji ya mwaka 1973 na 1977.
Katika fainali za mwaka 1978, mkali wa mabao wa zamani wa Uganda, Phillip Omondi aliungana na Opoku Afriyie na Segun Odegbami katika ufungaji bora, kila mmoja akipachika nyavuni mabao matatu. Leo Omondi hayupo duniani, lakini huwezi kuzungumzia historia ya Challenge bila kumtaja yeye.
Musisi
MAJID MUSISI:
NI kweli, Philipo Omondi alikuwa noma enzi zake, lakini unaweza kusema nini kuhusu Majid Musisi Mukiibi?
Mshambuliaji huyo aliyezaliwa Septemba 15, mwaka 1967 kabla ya kufariki dunia Decemba 13, mwaka 2005 vyombo vya habari Uganda vimechekecha vikaamua kuweka bayana, huyo ndiye mchezaji bora zaidi kihistoria kuwahi kutokea nchini humo.
Musisi, ambaye ni mchezaji wa kwanza wa Uganda kucheza soka ya kulipwa Ulaya, alikuwa ana majina mawili maarufu ya utani enzi zake, ambayo ni Tyson na Magic. Tyson kwa sababu alikuwa mkorofi na Magic ni kwamba soka yake iliitwa ya miujiza.
Huyo aliisaidia The Cranes kutwaa Kombe la Challenge katika miaka ya 1989 na 1990. Mfumo wa maisha ya kuendekeza pombe, ulimfanya afananishwe na magwiji wa soka duniani akina George Best, Eric Cantona au Paul Gascoigne ‘Gazza’.
Musisi alikuwa ana utajiri miguuni mwake na mabeki kwa pamoja na makipa walikuwa wanamheshimu sana mtu huyo. Alikuwa hashindwi kufanya jambo anapoamua kufanya kwa juhudi zake zote.
Umaarufu wake uliwavutia vijana wengi kucheza soka Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla. Jamaa alikuwa anaijua soka.
Nteze John
NTEZE JOHN:
WENGINE wanaweza kujiuliza kwa nini siyo Sunday Manara ama Zamoyoni Mogella, Peter Tino au Edibily Lunyamila, lakini jibu ni kwamba, wote hao hawafui dafu mbele ya Nteze John Lungu kwa kufanya vitu vikubwa kwenye Kombe la Challenge.
Haimaanishi Nteze alikuwa anawazidi kisoka akina Abdallah Kibadeni, Mogella, Lunyamila, Said Mwamba Kizota na wengine waliowahi kuwika katika soka ya Tanzania, la hasha- ila Nteze aling’ara zaidi yao kwenye michuano hiyo.
Huyo ndiye aliyekuwa shujaa wetu wakati tunachukua taji la pili la michuano hiyo, mwaka 1994 mjini Nairobi, Kenya.
Mabao yake manne aliyofunga katika Kundi A, kwenye michuano hiyo yaliifanya Tanzania Bara iongoze kundi hilo kwa pointi tisa ilizokusanya kutoka na kushinda mechi zote za kundi lake, Nteze akifunga katika kila mechi.
Novemba 29, Tanzania ikiitandika Somalia mabao 4-0, Nteze alifunga mabao mawili katika dakika za 11 na 84, mengine yakifungwa na George Masatu dakika ya 67 na Madaraka Suleiman dakika ya 74.
Siku mbili baadaye Nteze alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 57, Bara ikiwafunga wenyeji Kenya 1-0, wakati Desemba 3, Bara ikiichapa Djibouti 3-0, Nteze alifunga la tatu dakika ya 75, baada ya Edward Chumila (sasa marehemu) kufunga dakika ya pili na Clement Kahabuka dakika ya 30.
Nteze hakufunga katika mechi mbili zilizofuata, Nusu Fainali dhidi ya Eritrea, bao pekee la Said Mwamba ‘Kizota’ dakika ya saba likiipa Bara ushindi wa 1-0 na fainali, ambayo baada ya sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 dhidi ya Uganda, Bara ilifanikiwa kutwaa Kombe kwa mikwaju ya penalti 4-3.
Ilikuwa ni Desemba 10, wakati mabao ya Stars yalipotiwa kimiani na Juma Amir Maftah dakika ya 14 na Kizota dakika ya 40 wakati Iddi Batambuze aliifungia Uganda dakika ya 47 kabla ya George Ssemogerere dakika ya 88 kusawazisha.
Nteze aliibuka pia mfungaji bora wa michuano hiyo kwa mabao yake manne na kutwaa Kiatu cha Dhahabu.
Oliech
DENNIS OLIECH:
WAMETOKEA wanasoka wengi Kenya ambao waling’ara kwenye Challenge, lakini kama ilivyo kwa wachezaji wa Tanzania unahitajika utulivu wa hali ya juu, ili kumtaja mmoja ambaye daima anastahili kukumbukwa katika historia ya michuano hiyo. 
Mfungaji wa bao la tatu na la ushindi katika dakika ya 72 ya fainali ya Kombe la Challenge Desemba 14, mwaka 2002 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Tanzania Bara ikilala 3-2 na kupoteza matumaini ya kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu.
Nani zaidi ya Dennis Oliech. Na kwa nini asahaulike mtu huyo siyo tu kwa kuwakomoa wenyeji na kuwapokonya tonge mdomoni, bali soka yake iliyomuuza Ulaya baadaye.
Siku hiyo, Emmanuel Gabriel alitangulia kuifungia Bara dakika ya 28, kabla ya Paul Oyuga kusawazisha dakika ya 30 na Mecky Mexime kufunga la pili kwa penalti dakika ya 59 na John Barasa kuisawazishia Harambee Stars dakika ya 70 na Oliech kupiga la ushindi dakika ya 72.
Oliech alikuwa mfungaji bora katika fainali hizo kutokana na mabao yake matano, akiwa ana umri wa miaka 17 tu wakati huo.
Oliech alizaliwa Februari 2, mwaka 1985, baada ya kung’ara kwenye fainali hizo, mwaka 2003 alinunuliwa na Al-Arabi ya Qatar hadi mwaka 2005, aliposaini mkataba wa miaka minne na  FC Nantes ya Ufaransa na kuanza safari yake kuogelea kwenye bwala la fedha Ulaya na sasa anachezea Auxerre.
Aliiwezesha Kenya kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2004 na alicheza vizuri kwenye fainali hizo nchini Tunisia na mwaka huo huo akatabiriwa kuwa miongoni mwa washambuliaji hatari baadaye duniani, akiwekwa katika orodha moja na Wayne Rooney wa Manchester United. Oliech kwa sasa ameipa kisogo michuano ya Challenge, ingawa bado anaichezea Harambee Stars katika michuano mikubwa, ila Challenge ndio iliyomtoa.

CHALLENGE: BABA WA MICHUANO YA KIMATAIFA AFRIKA

Uganda, mabingwa wa kihistoria wa Challenge 

NA MAHMOUD ZUBEIRY
MICHUANO ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama CECAFA Challenge Cup, mwaka huu itafanyika mjini Kampala, Uganda kuanzia Novemba 24 hadi Desemba 8.
Kampuni ya Bia Afrika Mashariki (EABL), kupitia bia yake ya Tusker Lager, ndio wadhamini michuano hiyo kwa dau lao la dola za Kimarekani 450,000 walizitoa kwa ajili ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la CECAFA –Tusker Challenge Cup.
Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye alisema mapema tu wakati wa maandalizi ya awali ya michuano hiyo, kwamba lengo la michuano hiyo ni kuzisaidia maandalizi timu za Afrika Mashariki na Kati katika kuwania tiekti ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Udhamini wa mwaka huu huo ni ongezeko la aslimia 5, kutoka michuano ya mwaka jana mjini Dar es Salaam, ambayo Uganda waliibuka mabingwa.
Ni udhamini ambao utahusu usafiri, malazi na huduma nyingine, wakati jumla ya dola za Kimarekani 60.000 zitakuwa kwa ajili ya zawadi, bingwa akipewa dola 30.000, mshindi wa pili dola 20.000 na dola 10.000 mshindi wa tatu.   Kama ilivyo ada, mechi zote za michuano hiyo zitaonyeshwa na Televisheni ya Super Sport ya Afrika Kusini.
Michuano hiyo huandaliwa na CECAFA, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, ambalo lina wanachama 12.
Japokuwa ukanda wa CECAFA ndiyo eneo linalojikongoja kwa sasa katika soka ya kimataifa, lakini ukweli ni kwamba, mpira wa miguu barani Afrika, ulianzia ukanda wa Afrika Mashariki.
Michuano ya kwanza kabisa mikubwa barani Afrika, ilihusisha mataifa manne, Kenya, Uganda, Tanganyika (sasa Tanzania Bara) na Zanzibar, ikijulikana kwa jina la Kombe la Gossage.
Michuano hiyo ya Gossage ambayo sasa imekuwa Kombe la Challenge, ilifanyika mara 37 kuanzia mwaka 1926 hadi 1966, ilipobadilishwa jana na kuwa michuano ya wakubwa ya soka kwa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, ilifanyika mara saba kati ya mwaka 1965 na 1971, ilipozaliwa rasmi CECAFA Challenge.
Tanganyika ilianza kushiriki michuano hiyo tangu mwaka 1945, wakati Zanzibar ilijitosa miaka minne baadaye, 1949.
Michuano hiyo ilikuwa ikidhaminiwa na bepari aliyekuwa akimiliki kiwanda cha sabuni, William Gossage, aliyezaliwa Mei 12 mwaka 1799 na kufariki dunia Aprili 9, mwaka 1877.
Michuano hiyo mikongwe zaidi barani, imekuwa ikiandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), ikihusisha timu za taifa za ukanda huo.
Hadi inafikia tamati michuano ya Gossage, Uganda ilikuwa inaongoza kwa kutwaa taji hilo, mara 22, ikifuatiwa na Kenya iliyotwaa mara 12 na Tanzania mara tano.
Mwaka 2005, michuano hiyo ilifanyika chini ya udhamini wa bilionea wa Ethiopia mwenye asili ya Saudi Arabia, Sheikh Mohammed Al Amoudi na kupewa jina la Al Amoudi Senior Challenge Cup, lakini sasa Tusker ndiyo mambo yote.
MABINGWA CHALLENGE;
Mwaka Bingwa         
1973    Uganda     
1974    Tanzania   
1975    Kenya      
1976    Uganda     
1977    Uganda     
1978    Malawi     
1979    Malawi     
1980    Sudan      
1981    Kenya      
1982    Kenya      
1983    Kenya      
1984    Zambia     
1985    Zimbabwe   
1986   Haikufanyika
1987    Ethiopia   
1988    Malawi     
1989    Uganda     
1990    Uganda     
1991    Zambia     
1992    Uganda     
1993   Haikufanyika
1994    Tanzania   
1995    Zanzibar   
1996    Uganda     
1997   Haikufanyika
1998   Haikufanyika    
1999    Rwanda B   
2000    Uganda     
2001    Ethiopia   
2002    Kenya      
2003    Uganda     
2004    Ethiopia   
2005    Ethiopia   
2006    Zambia     
2007    Sudan      
2009    Uganda     
2009    Uganda 
2010    Tanzania Bara
2011    Uganda
KUNDI A: Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini
KUNDI B: Tanzania, Sudan, Burundi na Somalia
KUNDI C: Malawi, Eritrea, Rwanda na Zanzibar
RATIB KUNDI A:
Novemba 24, 2012:
Ethiopia v Sudan               (Saa 9:00 Alasiri)
Uganda v Kenya                (Saa 12:00 jioni)
Novemba 27, 2012:
Sudan Kusini v Kenya       (Saa 9:00 Alasiri)
Uganda v Ethiopia             (Saa 12:00 jioni)
Novemba 30, 2012:
Kenya v Ethiopia               (Saa 9:00 Alasiri)
Sudan Kusini v Uganda     (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI B:
Novemba 25, 2012:
Burundi v Somalia             (Saa 9:00 Alasiri)
Tanzania v Sudan              (Saa 12:00 jioni)
Novemba 28, 2012:
Somalia v Sudan                (Saa 9:00 Alasiri)
Tanzania v Burundi           (Saa 12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Sudan v Burundi                (Saa 9:00 Alasiri)
Somalia v Tanzania           (Saa 12:00 jioni)
RATIBA KUNDI C:
Novemba 26, 2012:
Zanzibar v Eritrea             (Saa 9:00 Alasiri)
Rwanda v Malawi             (Saa 12:00 jioni)
Novemba 29, 2012:
Malawi v Eritrea               (Saa 9:00 Alasiri)
Rwanda v Zanzibar           (Saa 12:00 jioni)
Desemba 1, 2012:
Malawi v Zanzibar            (Saa 9:00 Alasiri)
Eritrea v Rwanda              (Saa 12:00 jioni)
ROBO FAINALI:
Desemba 3, 2012
Mshindi Kundi C vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:00 jioni)
Mshindi Kundi A vs Mshindi wa Tatu Bora wa pili (Saa 1:00 usiku)
Desemba 4, 2012 (16:00):
Mshindi Kundi B vs Mshindi wa Tatu Bora wa kwanza (Saa 10:00 jioni)
Mshindi wa Pili Kundi A vs Mshindi wa Pili Kundi C       (Saa 1:00 usiku)
NUSU FAINALI:
Desemba 6, 2012
Nusu Fainali ya Kwanza    (Saa 10:00 jioni)
Nusu Fainali ya Pili           (Saa 1:00 usiku)
MSHINDI WA TATU:
Desemba 8, 2012
Waliofungwa Nusu Fanali (Saa 10:00 jioni)
FAINALI:
Desemba 8, 2012
Walioshinda Nusu Fainali  (Saa 1:00 usiku)

WASIFU WA TIMU ZINAZOSHIRIKI TUSKER CHALLENGE 2012


Kenya
NYOTA WA HARAMBEE:
Kenya ambayo timu yake ya taifa inaitwa Harambee Stars, imeshiriki mara tano fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, ingawa haijawahi kuingia raundi ya pili zaidi ya kunusa na kutolewa. Ilishiriki michuano ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa mara yakwanza mwaka 1974 na imeendelea hadi fainali za mwaka huu zilizofanyika Afrika Kusini, lakini haijafanikiwa kufuzu. Mwaka 2004, FIFA iliisimamisha Kenya kushiriki michuano yote ya kimataifa kwamiezi mitatu, kufuatia serikali ya nchi hiyo kuingiliwa masuala ya soka, lakini kifungo hicho kilisitishwa baada ya nchi hiyo kukubalia kufuata masharti ya shirikisho hilo la kimataifa la soka. Oktoba 25, mwaka 2006, Kenya ilisimamishwa tena katika soka ya kimataifa kwa kushindwa kutekeleza makubaoliano yaliyofikiwa Januari mwaka huo ya kutatua matatizo yaliyokuwa yametawala kwenye shirikisho lao la soka, hata hivyo walipomaliza matatizo yao adhabu yao ilifutwa. Kenya waliosyhiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mara nne, katikamiaka ya 1988, 1990, 1992 na 2004 na mara zote wakitolewa raundi ya kwanza, ni mabingwa mara tano wa Kombe la Challenge la CECAFA katika miaka ya 1975, 1981, 1982, 1983 na 2002, wakati pia imeshika nafasi ya pili mara nne.
Sudan
MWEWE WA JANGWANI;
TIMU ya taifa ya Sudan inajulikana kwa jina la utani kama Sokoor Al-Jediane Kiarabu, Kiingereza Desert Hawks, yaani Mwewe wa Jangwani. Hii ilikuwa moja ya nchi tatu tu nyingine zikiwa ni Misri na Ethiopia zilizoasisi Kombe la Mataifa Huru ya Afrika mwaka 1957 na ilifanikiwa kushinda taji hilo mwaka 1970, wakiwa wenyeji, baada ya kuwafunga Ghana 1-0 kwenye fainali, wakitoka kuifunga Misri 2-1 katika Nusu Fainali. Sudan ni miongoni mwa timu kongwe barani Afrika na ilikuwa ina historia ya utajiri miaka ya 1950 na 1970. Sudan pia ilishika nafasi ya pili kwenye michuano hiyo katika fainali za mwaka 1959 zilizofanyika mjini Cairo, Misri zikishirikisha nchi tatu, yani mbali na wenyeji, pia walikuwapo Ethiopia. Ilishika tena nafasi ya pili katika fainali za mwaka 1963 baada ya kufungwa na Ghana 3-0 kwenye fainali, wakati 1957 ilikuwa ya tatu. Sudan pia wametwaa mara tatu Kombe la Challenge katika miaka ya 1980, 2006 na 2007 na wamekuwa wa pili mara mbili 1990 na 1996 na washindi wa tatu mara mbili pia, 1996 na 2004.
Uganda
KORONGO WA KAMPALA;
Uganda ambayo timu yake ya taifa inaitwa The Cranes, yaani Korongo hawajawahi kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia, na kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika matokeo yao mazuri kabisa ni kushika nafasi ya pili mwaka 1978, baada ya kufungwa na wenyeji Ghana 2-0 mjini Accra. Lakini Korongo wa Uganda wanajivunia kuwa timu iliyotwaa mara nyingi zaidi taji (mara 12) Kombe la Challenge, katika miaka ya 1973, 1976, 1977, 1989, 1990, 1992, 1996, 2000, 2003, 2008, 2009 na 2011 na pia imeshika nafasi ya pili mara nne.
Rwanda
NYIGU WA KIGALI;
Rwanda ambayo timu yake ya taifa inaitwa Amavubi Kinyarwanda, yaani (The Wasps),  yaani Nyigu, pamoja na kwamba walichelewa kuingia kwenye soka ya kimataifa kutoka muda mrefu wa kutokuwa na amani nchini mwao, lakini tangu wamefunguliwa milango wanaonekana kuwa tishio. Walikuwapo kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2004 nchini Tunisia na wana taji moja la Challenge walilotwaa mwaka 1998, wakati wamekwishakuwa washindi wa pili mara tano katika miaka ya 2003, 2005, 2007, 2009 na 2011 na wameshika nafasi ya tatu mara tatu katika miaka ya  2001, 2002 na 2006.
Burundi
MBAYUWAYU WA BUJUMBURA;
Burundi ambayo timu yake ya taifa inaitwa Int’hamba Murugamba Kirundi, Les Hirondelles Kifaransa au The Swallows Kiingereza yaani Kiswahili Mbayuwayu, hii kwa pamoja na Eritrea na Djibouti ndio zinaweza kuwa zenye mafanikio duni kabisa katika ukanda wa CECAFA, kwani hazijawahi kushinda hata taji moja la Challenge wala hata kunusa kwenye fainali za Matafa ya Afrika.
Lakini ni nchi ambayo imebarikiwa wachezaji wenye vipaji, ingawa wengi baadaye huikana nchi hiyo na kuchukua uraia wa nchi jirani, kwa mfano Nonda Shabani aliyehamia DRC na Hamadi Ndikumana aliyejivika Unyarwanda.
Somalia
MABAHARIA WA MOGADISHU;
Somalia ambayo timu yake ya taifa inafahamika kama The Ocean Stars, yaani Nyotan wa Bahari ni nchi mwanachama wa mashirikisho ya mawili ya soka; kwanza Afrika (CAF) na pili Urabuni (UAFA). Haijawahi kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia wala Mataifa ya Afrika na kwa sasa imezuiwa kucheza mechi nyumbani kwake, Somalia kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea. Lakini Somalia inapendewa soka yake maridadi, japokuwa haizalishi matokeo mazuri.
Zanzibar
MASHUJAA WA VISIWANI;
Zanzibar ambayo timu yake ya taifa inajulikana kama Zanzibar Heroes, au Mashujaa wa Visiwa vya Karafuu, kwenye soka ya kimataifa bado ni sehemu ya Tanzania, ingawa inapigania uanachama wake FIFA, ili iwe taifa kamili katika dunia ya soka. Lakini kwa CECAFA, Zanzibar inaingia kama nchi na imewahi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka 1995, ikiwafunga wenyeji Uganda 1-0.
Zanzibar pia imewahi kuingia Nusu Fainali mara sita na mbili ikishika nafasi ya tatu, wakati michuano ya mwaka huu, inaeonekana kuwa na kikosi imara zaidi.
Ethiopia
SWALA DUME;
Ethiopia ambayo timu yake ya taifa inajulikana kama The Walya Antelopes, mchanganyiko wa maneno mawili, la Kiingereza na Kihabeshi, lenye maana ya ‘Swala dume’ ni miongoni mwa nchi tatu pamoja na Misri na Sudan zilizoasisi michuano ya Mataifa Huru ya Afrika mwaka 1957 na wakafanikiwa kutwaa taji hilo mwaka 1962 walipokuwa wenyeji, ingawa baada ya muongo huo, ilipoteza makali yake.
Baada ya kuzisakosa kidogo fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2004, kwa kuzidiwa pointi tatu tu, baada ya kufungwa na Guinea, Ethiopia mwakani itashiriki tena fainali hizo nchini Afrika Kusini, baada ya miaka 31. Inajivunia pia kutwaa mataji ya Challenge katika miaka ya 1987, 2001, 2004 na 2005.
Tanzania Bara
NYOTA WA KILIMANJARO;
Tanzania, ambayo kabla ilikuwa ikijulikana kama Tanganyika, timu yake ya taifa inaitwa Kilimanjaro Stars- ingawa nje ya michuano ya CECAFA inatambulika kama Taifa Stars, kwa sababu inaungana na Zanzibar kuunda timu moja.
Haijawahi kushiriki fainali hata moja za Kombe la Dunia, lakini inajivunia kucheza fainali moja za mwaka 1980 za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Nigeria, sambamba na kutwaa mara tatu Kombe la Challenge katika miaka ya 1974, 1994 na 2010 na kushika nafasi ya pili mara tano.
   
Malawi
MWALE WA NYASA;
Malawi iliyokuwa ikijulikana kama Nyasaland kabla ya mwaka 1966, ambayo timu yake ya taifa inaitwa The Flames, yaani Mwale (mwako wa moto) hawajawahi kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia, lakini wameshiriki fainali mbili za Kombe la Mataifa ya Afrika katika miaka ya 1984 na 2010, mara zote wakiishia raundi ya kwanza.
Mafanikio yao makubwa katika soka ya kimataifa ni kushika nafasi ya tatu katika Michezo ya Afrika mwaka 1987. timu hiyo ambayo kwa sasa iko chini ya kocha mzalendo Kinnah Phiri, imewahi kushika nafasi ya pili mara mbili katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA), wakati kabla ya kuhami huko, ikiwa bado mwanachama wa CECAFA, ilitwaa Kombe la Challenge mara tatu katika miaka ya 1978, 1979 na 1988 na pia kushina nafasi ya pili mara tatu. Imekuja tena kushiriki Challenge mwaka huu kama mgeni mualikwa. 
Sudan Kusini
NYOTA ANGAVU WA SUDAN KUSINI;
Sudan Kusini, au Bright Star, yaani Nyota Angavu kwa jina la utani, huyu ni mwanachama mpya kabisa wa CECAFA, nchi iliyojigawa kutoka Sudan ambayo sasa inatambulika katika familia ya soka kama taifa kamili. Kwao hizi zitakuwa fainali za kwanza kabisa za Challenge. Sudan Kusini rasmi ilicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa Julai 10, mwaka huu na kutoka sare ya 2-2 na Uganda nyumbani. Hii ni kuashiria kwamba, pamoja na upya wao si timu ya kubeza kwa kitendo cha kutoka nguvu sawa na mabingwa watetezi wa michuano hii.
Eritrea
WAVUVI WA BAHARI NYEKUNDU ERITREA;
Imekosekana katika fainali mbili zilizopita za Challenge kutokana na tabia ya wachezaji wake kuzamia nchi za watu wanapokwenda kucheza mechi. Wachezaji wanne wa klabu ya Red Sea FC walizamia Nairobi baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa na wengine 12 wa timu ya taifa wakazamia Tanzania mwaka 2007 baada ya Challenge. Wachezaji wengine sita walizamia Angola Machi mwaka 2007 baada ya mechi ya kufuzu ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Wachezaji wengine watatu zaidi walizamia Sudan, hivyo Eritrea ikajitoa kwenye soka ya kimataifa kwa ujumla ili kutafuta dawa ya kukabiliana na tatizo hilo na sasa serikali ya nchi hiyo inamtaka kila mchezjai kuweka nakfa 100,000 (fedha za kwao) kabla ya kusafiri nje. Timu yao ya taifa inaitwa Red Sea Boys, yaani vijana wa Bahari Nyekundu na haina cha kujivunia kwenye mashindano haya, ikiwa ilicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa Juni 26, mwaka 1992 na kutoka 1-1 na Sudan.
VIWANGO VYA UBORA FIFA
NCHI              NAFASI
Uganda            86
Malawi            101
Ethiopia           102
Sudan              102
Rwanda           122
Burundi           128
Kenya              130
Tanzania          134
Zanzibar          134
Somalia           193
Eritrea             192
Sudan Kusini   200
(Viwango hivi vimetoka mwezi huu)

TOURE AONGOZA KWA KULIPWA FEDHA NYINGI AFRIKA.

KIUNGO wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure ametajwa kama mwanamichezo kutoka Afrika anayelipwa fedha nyingi zaidi katika orodha ya wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani iliyotolewa na gazeti la Forbes hivi karibuni. Toure mwenye umri wa miaka 29 anashika namba 73 katika orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi duniani akiwa sambamba na mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka Marekani Tim Duncan ambao wote kwa pamoja wanakusanya kiasi cha dola milioni 19.1 kwa mwaka. Kiungo huyo ambaye anacheza katika klabu ya Manchester City na mcheza gofu Ernie Els kutoka Afrika Kusini ndio waafrika pekee katika orodha hiyo ya wanamichezo 100 wanaolipwa zaidi iliyotolewa na gazeti hilo. Toure ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2011 ana mkataba wa miaka mitano na City unaomuwezesha kukusanya kiasi cha dola milioni 16.6 ukijumlisha na dola milioni 2.5 kwa ajili ya matangazo unapata dola milioni 19.1 anazokusanya kwa mwaka. Katika orodha hizo inaongozwa na bondia kutoka Marekani Floyd Mayweather akikusanya kiasi cha dola milioni 85 akifuatiwa na bondia mwingine kutoka Philippines Manny Pacquiao anayekusanya kiasi cha dola milioni 62. Wanamichezo wengine na kiasi wanachokusanya ni pamoja na Tiger Woods dola milioni 54.9, LeBron James dola milioni 53, Roger Federer dola milioni 52.7, Kobe Bryant dola milioni 52.3, Phil Mickelson dola milioni 47.8. Wengine ni David Beckham dola milioni 46, Cristiano Ronaldo dola milioni 42.5 na Peyton Manning dola milioni 42.4 anayefunga orodha ya wanamichezo 10 bora wanaolipwa zaidi duniani.

DJOLIBA, LEOPARDS ZATOKA SARE YA MABAO 2-2 KATIKA FAINALI YA KWANZA YA KOMBE LA SHIRIKISHO.

TIMU ya Djoliba ya Mali imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na timu ya AC Leopards ya Congo katika fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho iliyopigwa jijini Bamako jana usiku. Wageni Leopards ndio walikuwa wa kwanza kuona lango la wenyeji wao dakika ya 21 kupitia kwa mchezaji Rochel Fernand kabla ya Alou Bagayoko kuisawazishia Djoliba kwa penati dakika 10 baadae na kunyanyua matuamaini ya mashabiki wengi waliojitkeza kuishangilia timu yao katika Uwanja wa 26 Mars. Kipindi cha pili wenyeji walionyesha juhudi za kutafuta ushindi kwa kushambulia lango la wapinzani kasi na juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 73 baada ya beki wa Djoliba kuifungia bao la kuongoza na kuwafanya mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo kulipuka kwa furaha. Zikiwa zimebakia dakika tano kabla ya mpira kumalizika Heritier Ngouelou wa Leopards aliwanyamazisha mashabiki waliokuwa wakijua wameshinda mchezo huo kwa kufunga bao la kusawazisha. Matokeo hayo yatakuwa sio mazuri kwa Djoliba ambao wiki ijayo watasafiri kuelekea jijini Dolisie kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Leopards, mchezo ambao utaamua bingwa wa Kombe la Shirikisho kwa mwaka huu

HAMILTON ASHINDA MBIO ZA GRAND PRIX ZA MAREKANI.

DEREVA nyoya wa Langalanga, Lewis Hamilton wa timu ya McLaren amefanikiwa kushinda mbio za Marekani za Grand Prix baada ya kufanikiwa kumpita katika dakika mwisho Sebastian Vettel wa timu ya Red Bull. Katika mashindano hayo Hamilton alionekana kumfukuza kwa karibu Vettel toka mwanzo na baadae kufanikiwa kumpita ikiwa imebakia mizunguko 14. Nafasi ya tatu katika mashindano hayo ilishikwa na Fernando Alonso wa timu ya Ferrari hivyo kufanya mbio za ubingwa mwaka huu kuwa wazi kwa kubakisha alama 13 nyuma ya kinara Vettel. Mashindano ya mwisho yatakayofanyika nchini Brazil mwishoni mwa wiki ijayo ndio yatakayoamua bingwa wa dunia kwa msimu huu.

NYOTA WA ZAMANI WA UNITED AFARIKI DUNIA.

NYOTA wa zamani wa klabu ya Manchester United ambaye ni mmoja wa wachezaji waliopona katika ajali ya ndege iliyotokea jijini Munich, Ujerumani mwaka 1958, Kenny Morgans amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73. Katika taarifa iliyotumwa katika tovuti ya United imebainisha kuwa Morgans alikimbizwa hospitali Jumamosi baada ya kuugua ghafla na baadae kufariki dunia katika hospitalini. Nyota huyo ambaye alikuwa winga alianza rasmi kucheza katika kikosi cha kwanza cha United katika mchezo dhidi ya Leicester City Desemba mwaka 1957 akiwa na umri wa miaka 18. Morgans aliumia wakati ndege iliyokuwa imepakia wachezaji wa United wakitokea jijini Belgrade kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Ulaya wakati walipopata ajali hiyo baada ya kujaza mafuta jijini Munich na kuua watu 23 kati ya 44 waliokuwepo katika ndege hiyo. Katika ajali hiyo Morgans alipatikana baadaye joni akiwa amebanwa kwenye viti vya ndege hiyo na waandishi wawili wa Ujerumani na baadae alifanikiwa kupona na kurejea tena uwanjani kabla ya kuhama Old Traford mwaka 1961 kwenda Swansea City.

LIGI za ULAYA: Atletico Madrid yashinda, iko 3 nyuma ya Barca!! Inter Milan sare!!


MESSI_n_RONALDOBaadhi ya Ligi kubwa za Ulaya ziliendelea Jumapili na huko Spain, kwenye La Liga, Atletico Madrid waliifunga Granada Bao 1-0 na kuendelea kukamata nafasi ya Pili wakiwa Pointi 3 nyuma ya vinara Barcelona wakati huko Italy, katika Serie A, Timu inayoshika nafasi ya Pili, Inter Milan, ilihitaji goli la kujifunga wenyewe ili kutoka sare ya 2-2 na Cagliari na kuwafanya wawe Pointi 4 nyuma ya vinara Juventus.
Matokeo na Misimamo ni kama ifuatavywo:
BUNDESLIGA:
MATOKEO:
Jumapili Novemba 18
Werder Bremen 2 Fortuna Dusseldorf 1
Hoffenheim 1 Wolfsburg 3
MSIMAMO-Timu za juu
[Kila Timu imecheza Mechi 12]
1 Bayern Munich Pointi 31
2 Schalke 23
3 Eitracht Frankfurt 23
4 Borussia Dortmund 21
SERIE A
MATOKEO:
Jumapili Novemba 18
Inter Milan 2 Cagliari 2
Udinese 2 Parma 2
Catania 2 Chievo Verona 1
Siena 1 Pescara 0
Fiorentina 4 Atalanta 1
Bologna 3 Palermo 0
Sampdoria 3 Genoa 1
MSIMAMO-Timu za juu
[Kila Timu imecheza Mechi 13]
1 Juventus Pointi 32
2 Inter Milan 28
3 Fiorentina 27
4 Napoli 27
5 Lazio 23
6 Catania 19
LA LIGA
MATOKEO:
Jumapili Novemba 18
Deportivo La Coruna 0 Levante 2
Celta Vigo 1 Real Mallorca 1
Getafe 2 Real Valladolid 1
Granada 0 Atletico Madrid 1
Sevilla 5 Real Betis 1
MSIMAMO-Timu za juu
[Kila Timu imecheza Mechi 12]
1 Barcelona Pointi 34
2 Atletico Madrid 31
3 Real Madrid 26
4 Levante 20
5 Malaga 19
6 Real Betis 19

Jamie Carragher: “Liverpool itamaliza Ligi 4 Bora!”

>>AMSIFIA Brenda Rodgers kwa kuegemea Makinda kina RAHEEM!!
>>PATA RATIBA Mechi zijazo BPL!!
RAHEEM_STERLINGBeki Mkongwe wa Liverpool Jamie Carragher anaamini kuwa Klabu yake Msimu ujao wanaweza kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa vile wana uwezo wa kumaliza ndani ya 4 Bora kwenye BPL, Ligi Kuu England, na imani hiyo imekuja mara baada ya kuitwanga Wigan 3-0 Jumamosi na kuwafanya wawe hawajafungwa katika Mechi 7 za Ligi.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man City Mechi 12 Pointi 28
2 Man United Mechi 12 Pointi 27
3 Chelsea Mechi 12 Pointi 24
4 WBA Mechi 12 Pointi 23
5 Everton Mechi 12 Pointi 20
6 Arsenal Mechi 12 Pointi 19
7 West Ham Mechi 11 Pointi 18
8 Tottenham Mechi 12 Pointi 17
9 Fulham Mechi 12 Pointi 16
10 Swansea Mechi 12 Pointi 16
11 Liverpool Mechi 12 Pointi 15
+++++++++++++++++++++++
Baada ya kusuasua mwanzoni mwa Ligi, ushindi huu wa Liverpool dhidi ya Wigan umewafanya wakamate nafasi ya 11 wakiwa na Pointi 15 lakini hilo halikumteteresha Jamie Carragher ambae amesema: “Hatukuanza vizuri lakini ushindi huu wa Wigan umetufanya tuzikaribie Timu 4 za juu. Lolote linaweza kutokea!”
Ukiondoa vinara na ambao ndio Mabingwa watetezi, Manchester City, ambao wana Pointi 28, wakifuatiwa na Man United na Chelsea, Timu iliyoshika nafasi ya 4 ni West Bromwich Albion, isiyotegemewa, ambayo ina Pointi 23, ikifuatiwa na Everton na Arsenal ambao wana Pointi 19, Pointi 4 mbele ya Liverpool.
Msimamo huu umempa matumaini makubwa Jamie Carragher ambae anaamini Liverpool itarejea tena kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo walicheza mara ya mwisho Msimu wa Mwaka 2009/10.
Carragher ametamka: “Kila Timu inapoteza Pointi. Hili linatupa nafasi sisi kukaza buti, tutafika tu!”
Msimu uliopita Liverpool ilimaliza ikiwa Pointi 17 nyuma ya Timu ya 4 Tottenham na hilo lilimfukuzisha kazi Meneja Kenny Dalglish na akabadilishwa na Brendan Rodgers.
Hata hivyo hilo halikusaidia kwani Liverpool walianza Msimu huu wakiambulia Pointi 3 tu katika Mechi zao 5 za kwanza lakini mabadiliko na matokeo mazuri ya sasa yanawapa matumaini makubwa huku wakiwategemea Chipukizi kama kina Raheem Sterling kitu ambacho Carragher amemsifia Meneja Brendan Rodgers kwa kuamua njia hiyo.
BPL: RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili Novemba 18
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Fulham v Sunderland
Jumatatu Novemba 19
[SAA 5 Usiku]
West Ham v Stoke
Jumamosi Novemba 24
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Sunderland v West Brom
[SAA 12 Jioni]
Everton v Norwich
Man United v QPR
Stoke V Fulham
Wigan v Reading
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Aston Villa v Arsenal
Jumapili Novemba 25
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea v Liverpool
[SAA 12 Jioni]
Southampton v Newcastle
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Man City
Tottenham v West Ham
Jumanne Novemba 27
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Sunderland v QPR
[SAA 5 Usiku]
Aston Villa v Reading
Jumatano Novemba 28
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Fulham
Everton v Arsenal
Southampton v Norwich
Stoke v Newcastle
Swansea v West Brom
Tottenham v Liverpool
Man United v West Ham
[SAA 5 Usiku]
Wigan v Man City
Jumamosi Desemba 1
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
West Ham v Chelsea
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Swansea
Fulham v Tottenham
Liverpool v Southampton
Man City v Everton
QPR v Aston Villa
West Brom v Stoke
[SAA 2 Dak 30 Usiku]
Reading v Man United
Jumapili Desemba 2
[SAA 1 Usiku]
Norwich v Sunderland
Jumatatu Desemba 3
[SAA 5 Usiku]
Newcastle v Wigan
 

UEFA CHAMPIONZ LIGI ni Jumanne & Jumatano: Mahesabu makali nani atasonga!


>>NI PEKEE Man United, Malaga & Porto zipo RAUNDI ijayo!
UEFA_CHAMPIONZ_LIGI_LOGO-BOMBAZHatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Ulaya, UEFA CHAMPIONZ LIGI, imebakisha Mechi mbili tu kufikia tamati na hadi sasa ni Timu 3 tu ndizo zimefuzu kusonga mbele na ambazo ni Manchester United, ambao pia wameshanyakua Nambari Wani toka Kundi H, Malaga na FC Porto, wakiwaacha Mabingwa wa England, Manchester City, wakiweweseka kwa kutojua hatima yao lakini wenzao Chelsea na Arsenal hatima zao zipo mikononi mwao wenyewe ikiwa pamoja na Vigogo wengine kama vile Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich.
Kila Kundi litatoa Timu mbili kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Timu zitakazoshika nafasi ya 3 toka kila Kundi zitatupwa kwenye EUROPA LIGI.
++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumanne Novemba 20
FC Nordsjælland v FC Shakhtar Donetsk
Juventus v Chelsea FC
FC BATE Borisov v LOSC Lille
Valencia CF v FC Bayern München
FC Spartak Moskva v FC Barcelona [SAA 2 Usiku]
SL Benfica v Celtic FC
Galatasaray A.S. v Manchester United FC
CFR 1907 Cluj v SC Braga
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++++++++
ZIFUATAZO ni DONDOO MUHIMU KUHUSU KILA KUNDI:
KUNDI A
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 FC Porto Pointi 10 [IMEFUZU]
2 Paris SG  9
3 Dynamo Kiev 4
4 Dinamo Zagreb  0 [NJE]
FC Porto tayari wamefuzu na PSG wanaweza kuungana nao ingawa Dynamo Kiev bado wana matumaini lakini Dinamo Zagreb tayari wameshaaga Mashindano.
KUNDI B
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Schalke Pointi 8
2 Arsenal 7
3 Olympiakos  6
4 Montpellier 1
Arsenal, ambao waliumwaga uongozi wa Bao 2-0 walipocheza ugenini na Schalke katika Mechi iliyopita na kutoka 2-2, bado wapo kwenye kinyang’anyiro lakini wakifungwa katika moja ya Mechi zao mbili zilizobaki watakuwa hatarini.
Arsenal Jumatano wapo nyumbani kucheza na Montpellier.
Olympiakos, wako Pointi 1 nyuma ya Arsenal, na Jumatano wako ugenini kucheza na Schalke kisha kumaliza nyumbani kwao na Arsenal.
Hizo ni Mechi muhimu mno katika kuamua nani anafuzu toka Kundi hili.
KUNDI C
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Malaga Pointi 10
2 AC Milan 5
3 Anderlecht 4
4 Zenit St P'sbg 3
Malaga, ambao wameshangaza wengi, wametinga Raundi inayofuata wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili AC Milan na kuziacha Timu 3 nyingine zigombee nafasi moja iliyobaki.
KUNDI D
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Borussia Dortmund Pointi 8
2 Real Madrid 7
3 Ajax 4
4 Man City 2
Manchester City wapo mkiani na hali ilivyo inaonyesha vinara Borussia Dortmund na Real Madrid ndio watatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Ili kufuzu, Man City wanaombea miujiza ambayo ni pamoja na kuifunga Real Madrid Uwanjani Etihad Siku ya Jumatano, pia kushinda Mechi yao ya mwisho ugenini na Borussia Dortmund na pia kusali sana ili matokeo mengine yawe mazuri kwao.
Ni hesabu kali sana!
KUNDI E
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Shakhtar Donetsk Pointi          7
2 Chelsea 7
3 Juventus 6
4 Nordsjaelland 1 [NJE]
Hapa ni mtanange mkali maana Timu zote 3 zilizo juu, Shakhtar Donetsk, Chelsea na Juventus, mbili kati ya hizo zinaweza kufuzu.
KUNDI F
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Bayern Munich Pointi 9
2 Valencia 9
3 BATE Borisov 6
4 Lille 0 [NJE]
Bayern Munich na Valencia zimejongelea kuingia Raundi inayofuata na kila Timu inahitaji sare tu watakapokutana huko Spain Siku ya Jumanne.
KUNDI G
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Barcelona Pointi 9
2 Celtic 7
3 Benfica 4
4 Spartak Moscow 3
Celtic wanatambua ili kufuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa Mwaka 2007/08 ni lazima wawafunge Benfica kwao ndani ya Estadio da Luz.
Ikiwa Celtic watashinda na Barcelona kutoka sare au kuifunga Spartak Moscow huko Moscow Urusi hapo Jumanne Usiku basi Benfica na Spartak zitatupwa nje huku zikiwa na Mechi moja mkononi.
Barcelona bado wanahitaji Pointi 1 kufuzu na Benfica ni lazima waifunge Celtic ili kuweka hai matumaini yao.
KUNDI H
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
1 Man United Pointi 12 [IMEFUZU]
2 Galatasaray 4
3 CFR Cluj-Napoca 4
4 Braga 3
Manchester United tayari wamefuzu na tena wameshajihakikishia nafasi ya kwanza ya Kundi H.
Kwa Timu nyingine zote 3 zilizobaki, moja kati yao inaweza kuungana na Man United lakini hili halitaweza kujulikana hadi baada ya Mechi za mwisho hapo Desemba 5.
+++++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumanne Novemba 6
FC Dynamo Kyiv 0 FC Porto 0
Paris SaintvGermain FC 4 GNK Dinamo 0
FC Schalke 2 Arsenal 2
Olympiacos FC 3 Montpellier Hérault 1
RSC Anderlecht 1 FC Zenit St. Petersburg 0
AC Milan 1 Málaga 1
Manchester City 2 AFC Ajax 2
Real Madrid 2 Borussia Dortmund 2
+++++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumatano Novemba 7
Juventus 4 FC Nordsjælland 0
Chelsea FC 3 FC Shakhtar Donetsk 2
Valencia CF 4 FC BATE Borisov 2
FC Bayern München 6 LOSC Lille 1
SL Benfica 2 FC Spartak Moskva 0
Celtic 2 Barcelona 1
CFR 1907 Cluj 1 Galatasaray 3
SC Braga 1 Manchester United 3
+++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZA MWISHO ZA MAKUNDI:
Jumanne Desemba 4
GNK Dinamo v FC Dynamo Kyiv
Paris SaintvGermain FC v FC Porto
Montpellier Hérault SC v FC Schalke 04
Olympiacos FC v Arsenal FC
Málaga CF v RSC Anderlecht
AC Milan v FC Zenit St. Petersburg
Borussia Dortmund v Manchester City FC
Real Madrid CF v AFC Ajax
Jumatano Desemba 5
FC Shakhtar Donetsk v Juventus
Chelsea FC v FC Nordsjælland
LOSC Lille v Valencia CF
FC Bayern München v FC BATE Borisov
FC Barcelona v SL Benfica
Celtic FC v FC Spartak Moskva
Manchester United FC v CFR 1907 Cluj
SC Braga v Galatasaray A.S.