Sunday, December 23, 2012

MABINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI YANGA YA DAR ES SLAAM KWENDA UTURUKI


Baadhi ya wachezaji wa Yanga wataachwa hapa nyumbani wakati timu hiyo itakapokwenda Uturuki kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Bara wiki ijayo.

  Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, amesema baadhi ya wachezaji wataachwa katika safari hiyo; ambayo imekosolewa kutokana na nchi za Ulaya kuwa katika kipindi cha majira ya Baridi kali  kwa sasa.

 Kocha ndiye mwenye maamuzi ya mwisho ya kujua ni wachezaji gani ataondoka nao kwenda kwenye kambi hiyo, amesema Sanga ambaye alisisitiza kikosi cha timu hiyo kitaondoka Ijumaa licha ya nchi hiyo kuwa katika kipindi cha baridi.

Kiwango cha chini cha joto katika jiji la Ankara, Uturuki kwa siku nne kuanzia leo ni kati ya nyuzi 4-6 sentigredi, ikiwa ni baridi zaidi kwa alama 27 kulinganisha na hali ya hewa ya Dar es Salaam.

Sanga hakutaja majina wala idadi ya wachezaji watakaochwa miongoni mwa 28 waliopo sasa kwa maelezo kuwa ni jukumu la mwalimu.

 Mipango ya kuipeleka timu hiyo imekamilika na Yanga inasubiri siku ya safari tu,  na kueleza zaidi kuwa:

Kocha Ernest Brandts amekubaliana na uongozi kuipeleka timu hiyo nchini Uturuki kwa ajili ya kambi hiyo.

"Hakuna tatizo na safari hii, tulikuwa kwenye vikao kujadili jambo hili na tumeamua timu iondoke kama ilivyopangwa awali lengo likiwa ni maandalizi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara."

Aidha, Sanga alisema wachezaji waliotemwa kwenye usajili kwa ajili ya mzunguko wa pili wameachwa kwa mapendekezo ya kocha huyo.



"Uongozi umepokea mapendekezo ya kocha kwa ajili ya wachezaji wa kuachwa na sisi tunamsikiliza yeye hivyo kocha ndiye anayejua nani wa kuachwa," .

Mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Bara unatarajiwa kuanza Januari 19 mwakani.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 29 ikifuatiwa na Azam yenye pointi 26 huku Simba ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 23.

RAGGE ABWAGWA KATIKA UONGOZI TAREFA,KITUMBO BOSSI MPYA WA TAREFA




SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeupongeza uongozi mpya wa Chama cha Soka Tabora (TAREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Desemba 22 mwaka huu).
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba, ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TAREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Tabora.
Amesema TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TAREFA chini ya uenyekiti wa Yusuf Kitumbo aliyeshinda kwa kura 16 dhidi ya nane za Musa Ntimizi, na Paul Werema ambaye hakupata kura.
“Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Tabora kwa kuzingatia katiba ya TAREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake,”.
“Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TAREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF,”alisema Wambura.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Yusuf Kitumbo (Mwenyekiti), Fate Remtulla (Katibu), Dick Mlimuka (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Razak Irumba (Mwakilishi wa Klabu TFF) na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao ni Eric Kabepele na Mwalimu Sizya.

SPECIAL ONE MOURINHO,HALI TETE JANA ALITANDIKWA NA MALAGA 3-2 NA ASEMA HAJIUZULU NGO!!!


MENEJA wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho amesisitiza kuwa hatajiuzulu wadhfa huo pamoja na timu yake kufungwa mabao 3-2 na Malaga ambao umewafanya kuachwa alama 16 na vinara wa La Liga Barcelona. Kufungwa kwa Madrid kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na Mourinho kufuatia uamuzi wake wa kumuacha golikipa ambaye ndiye nahodha wa timu hiyo Iker Casillas katika kikosi cha kwanza. Akihojiwa kama anahofu kibarua chake kitakuwa kimefikia ukingoni mara baada ya mchezo Mourinho amesema hahofii chochote na hawezi kuachia ngazi kwani kupoteza mechi ni sehemu ya mchezo la msingi ni kujipanga na kuangalia wapi walikosea. Hiyo ni mara ya kwanza kwa Casillas katika kipindi cha miaka 10 kupumzishwa benchi na kumpisha golikipa namba mbili Antonio Adan mwenye umri wa miaka 25.

VILANOVA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI.


MENEJA wa Barcelona, Tito Vilanova ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kufanyiwa upauji kuondoa uvimbe wa kansa uliokuwa umeota kwenye koo. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alifanyiwa upasuaji huo Alhamisi iliyopita na kwasasa anakabiliwa na matibabu ya mionzi kwa kipindi cha wiki sita ili kudhibiti kabisa tatizo hilo linalomkabili. Huo ni upasuaji wa pili kufanyiwa baada ya ule aliofanyiwa mwaka 2011 kipindi hicho akiwa msaidizi wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Pep Guardiola. Barcelona ilifanikiwa kuifunga Valladolid mabao 3-1 jana usiku na baada ya hapo Xavi Hernandez ambaye alifunga bao la kwanza amesema wanamzawadia ushindi huo kocha wao huo ambaye anapitia kipindi kigumu hivi sasa katika maisha yake. Kwasasa kocha msaidizi Jordi Roura ambaye amekuwa benchi la ufundi la klabu hiyo toka mwaka 2009 ndiye aliyekabidhiwa timu wakati wa kipindi hiki ambacho Vilanova hayupo.

STURRIDGE KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA LIVERPOOL.


MSHAMBULIAJI wa Chelsea Daniel Sturridge anatarajiwa kwenye Merseyside baadae leo kwa ajili ya vipimo vya afya ikiwa ni sehemu ya hatua ya kutaka kuhamia katika klabu ya Liverpool. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anatarajiwa kufanyiwa vipimo katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Melwood lakini inaaminika kuwa tayari wameshafikia makubaliano juu ya masuala ya mkataba. Liverpool wanatarajiwa kulipa kiasi cha euro milioni 14 kwa ajili ya mshambuaji huyo mwenye umri wa miaka 23. Klabu hiyo ilikuwa ikihitaji mshambuliaji mapema katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani baada ya kucheza nusu ya msimu wakimtegemea mshambuliaji mmoja Luis Suarez.

ARSENAL KUPOTEZA PAUNDI MILIONI 30 WAKISHINDWA KUSHIRIKI CHAMPIONS LEAGUE MWAKANI.


KLABU ya Arsenal inaweza kupoteza kiasi cha paundi milioni 30 kwa mwaka wanazopata kutoka kwa wadhamini wao Emirates kama klabu hiyo ikishindwa kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Meneja wa klabu hiyo Arsenal Wenger ameiongoza kushiriki michuano hiyo kila msimu toka amechukua mikoba ya kuinoa ya kuinoa timu hiyo. Lakini hivi sasa Arsenal inakabiliwa na msimu mgumu chini ya kocha huyo Mfaransa na wako katika hatari ya kukosa taji lolote katika kipindi cha miaka nane mfululizo huku wakiwa bado wanapigania nafasi nne za juu ili washiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Emirates wadhamini wa klabu hiyo ambao wako katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mpaka msimu wa mwaka 2014-2015 wameamua kuionya klabu hiyo kwa kuchukua tahadhari kama ikishindwa kushiriki michuano ya klabu bingwa. Kwasasa Arsenal wako katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza lakini kuna uwezekano mkubwa wa kutoka katika nafasi hiyo kama Chelsea ambao walikuwa katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia iliyofanyika Japan wakishinda mechi zao mbili za viporo walizonazo.

MCHEZAJI COASTAL UNION AFARIKI DUNIA, KUZIKWA LEO TANGA

 


Boniface Wambura,
Ofisa Habari TFF
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Coastal Union, Mussa Rico kilichotokea jana (Desemba  22 mwaka huu) jijini Tanga.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba, msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti akiwa mchezaji Rico, na baadaye kocha alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na kufundisha ikiwemo Coastal Union, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Amesema TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Rico, Chama cha Soka Tanga (TRFA) na klabu ya Coastal Union na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Amesema mazishi yanatarajiwa kufanyika leo (Desemba 23 mwaka huu) mkoani Tanga. Mungu aiweke roho ya marehemu Rico mahali

 

MWAIKIMBA BADO ANATISHA ABEBA KIATU CHA DHAHABU DRC

Gaudence Mwaikimba; Mfungaji bora Kombe la Hisani DRC
MSHAMBULIAJI Gaudence Mwaikimba wa Azam amekuwa mfungaji wa mashindano ya Kombe la Hisani yaliyoandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kumaliza na mabao matatu, akifuatiwa na Kipre Herman Tchetche na Ngulubi Kilua wa Shark FC waliofunga mawili kila mmoja.
Jumla pamoja na penalti za baada ya dakika 90 za mechi, Mwaikimba amefunga mabao matano, Kilua matatu na Kipre matatu.
Hata hivyo, kwa kuwa mashindano haya ni ya hisani, hakutakuwa na zawadi mwa bingwa wala wachezaji bora, hivyo Mwaikimba anaondoka DRC na hadhi tu ya ufungaji bora.  
Azam jana iliwafunga wenyeji Dragons FC kwa penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs mjini hapa na kutwaa Kombe. Azam walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha dakika ya 75.
Katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na Samih Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
Hata hivyo, Azam jana hawakukabidhiwa Kombe uwanjani hapo baada ya waandaji kusema wanakwenda kulipamba kwanza, hivyo sherehe za makabidhiano ya Kombe zinaweza kufanyika leo.
Azam iliingia fainali, baada ya juzi kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs. Azam inatarajiwa kuondoka hapa kesho mchana kurejea Dar es Salaam.

AZAM BINGWA KOMBE LA HISANI DRC 2012/2013


AZAM FC ya Dar es Salaam, jana imetwaa ubingwa wa Kombe la Hisani, linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kuwafunga wenyeji Dragons FC kwa penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs mjini hapa.
Azam walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha dakika ya 75.
Katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na Samih Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
Hata hivyo, Azam jana hawakukabidhiwa Kombe uwanjani hapo baada ya waandaji kusema wanakwenda kulipamba kwanza, hivyo sherehe za makabidhiano ya Kombe zinaweza kufanyika leo.
Azam jana ilicheza bila kocha wake Mkuu, Muingereza Stewart Hall ambaye aliondoka juzi usiku mjini hapa kwenda kwao Uingereza kwa ajili ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.
Akizungumza kabla ya kuondoka mjini kinshansa a, Stewart alisema kwamba anamuachia timu hiyo msaidizi wake, Kali Ongala na anaamini atafanya kazi.
Stewart alisema Kali ni mtu ambaye siku zote amekuwa akimuandaa kuwa kocha wa baadaye wa Azam na hii si mara ya kwanza kumuachia timu, kwani aliwahi kufanya hivyo mara kadhaa ikiwemo kwenye Kombe la Urafiki, ambalo aliiongoza timu kufika Fainali.
“Siku moja nitaondoka Azam na kumuacha Kali awe kocha Mkuu, siku zote namtayarisha, namjengea kujiamini, naamini atakuwa kocha bora sana wa Azam, sina wasiwasi naye, namuachia timu na anaweza kurudisha Kombe Dar es Salaam,”alisema Stewart ambaye atarejea mwakani.
Azam iliingia fainali, baada ya juzi kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs. Azam inatarajiwa kuondoka hapa kesho mchana kurejea Dar es Salaam.
Katika mchezo wa jana, kikosi cha Azam kinatarajiwa kuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samih Hajji Nuhu, Joackins Atudo, David Mwantika, Jabir Aziz, Kipre Balou, Seif Abdallah/Uhuru Suleiman, Kipre Tchetche/Zahor Pazi, Humphrey Mieno na Gaudence Mwaikimba.  





Harry Redknapp: 'Wachezaji wengi QPR wanalipwa Fedha nyingi bure! '

Harry Redknapp: 'Wachezaji wengi QPR wanalipwe Fedha nyingi bure! '
>>AMTWANGA FAINI BOSINGWA £130,000!!
Bosi wa Queens Park Rangers Harry Redknapp ameponda msimamo wa Klabu hiyo wa kununua Wachezaji wanaolipwa Mishahara minono kuliko uwezo wao na kauli hiyo imekuja mara tu baada ya kupokea kipigo chake cha kwanza Klabuni hapo baada ya kutoka sare 3 na kushinda Mechi moja na kuwaacha wakamate nafasi ya 19.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO-Timu za chini:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 17 Pointi 18
17 Southampton 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++
HARRY_REDKNAPP12Redknapp ametamka: “Wapo Wachezaji wengi Klabuni wanalipwa Fedha nyingi kupita uwezo wao na nini wanaipa Klabu!”
Aliongeza kuwa hataki kuwaona Wamiliki wa QPR waliwe Pesa zao bure na alishtuka alipompiga Faini Mchezaji mmoja na kugundua Mchezaji huyo analipwa Fedha za juu kuliko hata Wachezaji wa Tottenham ambako alikuwa akifanya kazi kable.
Kitu kilichomshangaza sana ni kuona Uwanja wa QPR unachukua Watu 18,000 tu wakati Newcastle wana Uwanja wa Watu 52,000 lakini huko hawafikii Mishahara ya Wachezaji wa QPR.
Harry Redknapp amechukua wadhifa wa Umeneja hapo QPR baada ya kufukuzwa Mark Hughes ambae alisajili Wachezaji wengi lakini Timu haikupata ushindi hata mmoja hadi Redknapp alipotua.
+++++++++++++++++++++++
WACHEZAJI WALIOSAJILIWA na Meneja Mark Hughes:
-Nedum Onuoha
-Djibril Cisse
-Bobby Zamora
-Federico Macheda (Mkopo)
-Taye Taiwo (Mkopo)
-Samba Diakite
-Ryan Nelsen
-Andy Johnson
-Robert Green
-Park Ji-Sung
-Junior Hoilett
-Jose Bosingwa
-Julio Cesar
-Esteban Granero
-Sam Magri
-Stephane Mbia
+++++++++++++++++++++++
Mchezaji aliepigwa Faini na Redknapp ni Jose Bosingwa ambae amepigwa Faini ya Mshahara wa Wiki mbili baada kukataa kukaa Benchi katika Mechi ambayo QPR walipata ushindi wao wa kwanza walipoifunga Fulham Bao 2-1.
Bosingwa, ambae alikuwa Chelsea Msimu uliopita, amecheza Mechi 12 za Ligi za QPR na sasa anaelekea kutemwa na Klabu hiyo.
Redknapp ameleza: “Hakutaka kukaa Benchi, alitaka acheze na akaenda nyumbani bila kuaga! Amepigwa Faini £130,000! Na ataona nini kipo Januari!”
Redknapp amedokeza kuwa Januari atatafuna kuimarisha Kikosi na pia kuuza Wachezaji.

ULAYA: Real yaaga Mwaka kwa kichapo, Barca yapaa, Inter yanasa!

BARCA_v_REALLIGI za Spain na Italy hapo jana ziliaga Mwaka 2012 kwa Mechi zao za mwisho na kwenda Vakesheni hadi Januari 6 huku Mabingwa wa Spain, Real Madrid, wakitandikwa kwenye La Liga na kutupwa Pointi 17 nyuma ya vinara Barcelona wakati huko Serie A Inter Milan walijikuta wakishushwa hadi nafasi ya 4 na Mabingwa Juventus kubaki kileleni Pointi 8 mbele.
Wakati Barcelona ikishinda ugenini kwa kuichapa Real Valladolidi Bao 3-1 kwa Bao za Xavi, Lionel Messi na Tello, Real Madrid walichapwa 3-2 ugenini na Malaga ambao walifunga Bao zao kupitia Isco na Santa, bao mbili, na Real kufunga kwa Bao za Sanchez, kujifunga mwenyewe, na Karim Benzema.
Barcelona wamefunga Mwaka wakiwa kileleni na wana Pointi 40, wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye Pointi 40, Real Madrid 33 na Malaga 31.
Huko Italy kwenye Serie A, Inter Milan walikosa nafasi ya kupunguza pengo lao na Mabingwa Juventus walio kileleni wakiwa na Pointi 44 baada ya kutoka sare 1-1 na Genoa na kujikuta wakiporomoka hadi nafasi ya 4.
Nafasi ya 2 imekamatwa na Lazio ambao waliwafunga Sampdoria 1-0 na Fiorentina kushika nafasi ya 3 baada ya kuifunga Palermo 3-0.
MATOKEO:
LA LIGA
Alhamisi Desemba 20
RCD Espanyol 2 Deportivo La Coruna 0
Real Sociedad 2 Sevilla 1
Rayo Vallecano 3 Levante 0
Ijumaa Desemba 21
Valencia 4 Getafe 2
Atletico Madrid 1 Celta Vigo 0
Jumamosi Desemba 22
Real Betis 1 Real Mallorca 2
Real Valladolid 1 FC Barcelona 3
Malaga 3 Real Madrid 2
Osasuna 1 Granada 2
Jumapili Desemba 23
Athletic Bilbao 0 Real Zaragoza 2 [IMECHEZWA JANA USIKU BAADA SAA 6]
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 6

MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 17]
1 Barcelona Pointi 49
2 Atletico Madrid 40
3 Real Madrid 33
4 Malaga 31
5 Real Betis 28
6 Levante 27
7 Real Sociedad 25


SERIE A
Ijumaa Desemba 21
Pescara 2 Catania 1
Cagliari 1 Juventus 3
Jumamosi Desemba 22
Inter Milan 1 Genoa 1
Atalanta 1 Udinese 1
Bologna 1 Parma 2
Torino FC 2 Chievo Verona 0
Sampdoria 0 SS Lazio 1
Siena 0 Napoli 2
Palermo 0 Fiorentina 3
AS Roma 4 AC Milan 2
**LIGI MAPUMZIKONI HADI JANUARI 6

MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 18]
1 Juventus Pointi 44
2 Lazio 36
3 Fiorentina 35
4 Inter Milan 35
5 Napoli 34
6 AS Roma 32
7 AC Milan 27
8 Parma 26

BPL: City yaikaribia United Pointi 3, Arsenal ni ya 3, Liverpool ipo 8!!

BPL_LOGO>>CHELSEA YASHUKA HADI 7, USHINDI JUMAPILI KUWARUDISHA 3!
MATOKEO:
Jumamosi 22 Desemba 2012
Wigan 0 Arsenal 1
Man City 1 Reading 0
Newcastle 1 QPR 0
Southampton 0 Sunderland 1
Tottenham 0 Stoke 0
West Brom 2 Norwich 1
West Ham 1 Everton 2
Liverpool 4 Fulham 0
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
=Tofauti ya Magoli inatajwa kwa Timu zilizofungana Pointi
1 Man United Mechi 17 Pointi 42
2 Man City Mechi 18 Pointi 39
3 Arsenal Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 14]
4 Everton Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 8]
5 Tottenham Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 5]
6 WBA Mechi 18 Pointi 30 [Tofauti ya Magoli 4]
7 Chelsea Mechi 16 Pointi 29 [Tofauti ya Magoli 11]
8 Liverpool Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 4]
9 Stoke Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli 2]
10 Norwich Mechi 18 Pointi 25 [Tofauti ya Magoli -7]
11 Swansea Mechi 17 Pointi 23 [Tofauti ya Magoli 4]
12 West Ham Mechi 18 Pointi 23 [Tofauti ya Magoli 0]
13 Fulham Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -5]
14 Newcastle Mechi 18 Pointi 20 [Tofauti ya Magoli -6]
15 Sunderland Mechi 18 Pointi 19
16 Aston Villa Mechi 17 Pointi 18
17 Southampton 15 [Tofauti ya Magoli -10]
===============
18 Wigan Mechi 18 Pointi 15 [Tofauti ya Magoli -15]
19 QPR Mechi 18 Pointi 10
20 Reading Mechi 18 Pointi 9
+++++++++++++++++++++++
LIVERPOOL 4 FULHAM 0
Bao za Skrtel, Gerrard, Downing na Suarez, zimewapaisha Liverpool wakiwa kwao Anfield hadi nafasi ya 8 baada ya kuichapa Fulham Bao 4-0.

Refa: Mark Clattenburg

WEST BROM 2 NORWICH 1
West Brom walimaliza wimbi la Norwich la kutofungwa katika Mechi 10 na wao wenyewe kutofunga Bao katika Masaa 6 ya Soka baada ya kutoka nyuma kwa Bao la Robert Snodgrass na kusawazisha kwa frikiki ya Zoltan Gera na kisha Romelu Lukaku kuwapa Bao la ushindi.
Refa: Martin Atkinson

TOTTENHAM 0 STOKE 0
Tottenham wameipoteza nafasi ya kukamata nafasi ya 3 baada ya kubanwa na Stoke na kutoka sare 0-0 Uwanjani White Hart Lane.
Stoke sasa hawajafungwa katika Mechi 8.
Refa: Lee Mason

NEWCASTLE 1 QPR 0
Shola Ameobi leo katika Dakika ya 81 amefunga Bao lake la 3 Msimu huu na kuwapa ushindi Newcastle wa Bao 1-0 dhidi ya QPR na kumfanya Meneja wa QPR, Harry Redknapp, apate kipigo chake cha kwanza katika himaya yake ya Mechi 4 Klabuni hapo.
Refa: Kevin Friend

SOUTHAMPTON 0 SUNDERLAND 1
Bao la 8 la Steven Fletcher kwenye Ligi leo limewapa ushindi Sunderland wa Bao 1-0 ugenini walipocheza na Southampton.
Refa: Howard Webb

WEST HAM 1 EVERTON 2
Leo Everton walitoka nyuma kwa Bao 1-0 Uwanjani Upton Park na kuwafunga West Ham Bao 2-1 lakini shukrani ziende kwa Refa Mark Anthony ambapo alimpa Kadi Nyekundu Shola Ameobi, Mfungaji wa Bao la West Ham, kwa rafu ambayo haikustahili na kufungua njia kwa Everton kusawazsha kupitia Victor Anichebe na kupiga Bao la pili la ushindi kupitia Steven Pienaar.
Baada ya Bao hizo Darron Gibson wa Everton alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu na Refa Anthony Taylor baada ya kugongana na Mark Noble.
Refa: Anthony Taylor

MAN CITY 1 READING 0
Bao la faulo la Gareth Barry la Dakika ya 92 limeipa Manchester City ushindi Manchester City wa 1-0 dhidi ya Klabu ya mkiani Reading na kuwafanya wawe Pointi 3 tu nyuma ya vinara Manchester United.
Mbali ya Bao hilo la utata, Reading pia walipigia kelele Penati mbili walizonyimwa na Refa Mike Dean na matukio hayo yalimkera sana Meneja wa Reading Brian McDermott ambae alilalamika sana kuhusu Refa huyo na maamuzi yake..
Refa: Mike Dean

WIGAN 0 ARSENAL 1
Penati ya Dakika ya 60 ya Mikel Arteta leo imewapa Arsenal ushindi wao wa 3 mfululizo kwenye Ligi na kuwapaisha hadi nafasi ya 3.
Kipigo hiki kimewafanya Wigan wawe wamepoteza Mechi 6 kati ya 8 za Ligi walizocheza mwisho na pia kuwafanya kwa Misimu mitatu mfululizo wawe mkiani, nafasi 3 za chini, wakati wa Krismasi.
Refa: Jon Moss

+++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumapili 23 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Swansea v Man United
[SAA 1 Usiku]
Chelsea v Aston Villa
Jumatano 26 Desemba 2012
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v West Ham
Everton v Wigan
Fulham v Southampton
Man United v Newcastle
Norwich v Chelsea
QPR v West Brom
Reading v Swansea
Sunderland v Man City
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Aston Villa v Tottenham
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Stoke v Liverpool