Sunday, December 9, 2012

WAGOMBEA WAANZA KUNADI SERA ZAO MKOA WA TABORA KUWANIA UONGOZI MBALIMBALI WA MPIRA WA MIGUU TAREFA

 UCHAGUZI  WA WANAWAKE TWFA MKOA WA TABORA KUFANYIKA KESHO TAREHE 17/12/2012

 

Uchaguzi wa wanawake mkoa wa tabora TWFA unatarajia kufanyika kesho tarehe 17/12/2012 kuanzia saa tatu asubuhi  katika ukumbi wa shule ya taasisi mkoani tabora kusaka viongozi watakaowakilisha mkoa wa tabora ngazi ya wanawake.

Viongozi hao waliopitishwa katika usaili ni wagombea wanane nao ni ANNA MWINGIRA nafasi ya mwenyekiti,REHEMA ADAM RAJABU nafasi ya katibu mkuu,CHRISTINA WILLIAM FUNGAMEZA nafasi ya katibu msaidizi,CATHERINE BUNDALA nafasi ya mkutano mkuu TWFA tanzania.

Pia wamo ELEONORA BRUNO LUZIGA ,FATUMA JORAM PELEZI,ZENA MWAKASANGA na MWANAIDI OMARY katika nafasi ya mjumbe  wa TWFA mkoa wa tabora.

Haya ameyabainisha mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi mkoa wa tabora bw. MUSSA NTIMIZI na kubainisha pia  majina ambayo hayajapitishwa katika usaili kuwa ni ANNA ANTONY,STELLA ENOS, na THABIT ELIAS kw akutokidhi vigezo vya TWFA.

WAKATI HUO HUO amebainisha kuhusu Mikoa sita ambayo ni wanachama wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) ambayo haitashiriki katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya TWFA, ya wanachama hao hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo. Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora kwa taarifa iliyotolewa jana na ofisa habari wa shirikisho la soka tanzania TFF.
Uchaguzi huo utafanyika kwenye hoteli ya Midland, na wagombea ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (Katibu Mkuu), Zena Chande (Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

 

 

YANGA KUPAA DESEMBA 28, KULA MWAKA MPYA ULAYA


SIMBA SC YASISTIZA MUDDE NI MCHEZAJI WAKE HALALI

Mussa Mudde
SIMBA SC imesema kwamba Mussa Mudde ni miongoni mwa wachezaji wake wa kigeni wanne ilionao kwa sasa na imeshangazwa sana na habari zilizoandikwa katika tovuti ya supersport.com ya Afrika Kusini zikisema kwamba anarejea Sofapaka.
Akizungumza  jana kutoka Uingereza, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba Mudde ana mkataba wa miaka miwili na Wekundu hao wa Msimbazi.
“Nashangaa hizo habari wamezitoa wapi, huyu ni mchezaji wetu na mimi nilipoondoka Dar es Salaam nilimuacha pale, ni vema wakati mwingine wakawa wanawasiliana na sisi pia kutuuliza,”alisema Hans Poppe.
Wiki hii, supersport.com imeandika kwamba Mudde anarejea Sofapaka baada ya kuona mambo hayamuendei vizuri Simba SC.
Tovuti hiyo ilimnukuu na rais wa Sofapaka, Elly Kalekwa ambaye alisema kwamba ameingia mkataba wa miaka miwili na kiungo huyo mkabaji wa Mganda arejee Nairobi.
Mbali na Mudde, wachezaji wengine wa kigeni ambao hadi sasa wana uhakika wa kuvaa jezi za Simba SC ni kipa Abbel Dhaira, mshambuliaji Emmanuel Okwi wote kutoka Uganda pia na beki Komalbil Keita kutoka Mali.
Kutoka kikosi cha Simba kilichocheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, wachezaji Felix Sunzu kutoka Zambia, Daniel Akuffo kutoka Ghana na beki Paschal Ochieng kutoka Kenya, wametupiwa virago.
Mudde alisajiliwa tangu mwanzo wa msimu, lakini akaenguliwa kutokana na kuwa majeruhi na hakucheza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, wakati Dhaira pia amesajiliwa wiki iliyopita ili kuanza kazi Januari.      

UCHOVU ULITUNYIMA USHINDI JANA, ASEMA KOCHA AZAM

Iddi Abubakar
KOCHA wa makipa wa Azam, Iddi Abubakar Mwinchumu amesema kwamba, jana walilazimishwa sare ya 1-1 na Dragons ya hapa katika mchezo wa Kundi B kuwania Kombe la Hisani kwenye Martyrs mjini hapa kutokana na uchovu wa safari na pia timu kucheza bila makocha wake.
Akizungumza baada ya mechi ya jana mjini hapa, Iddi alisema kwamba timu ilifika usiku sana wa juzi na jana ikaingia uwanjani, hivyo wachezaji walikuwa wana uchovu, lakini anaamini mechi ijayo kesho watashinda.
Aidha, Iddi alisema pia timu kucheza bila makocha wake, ambao wamebaki Kenya nako kwa namna moja au nyingine kulichangia matokeo hayo. “Ilikuwa ghafla tu, nikaambiwa Iddi utaongoza timu katika mechi hii, nashukuru tumepata sare na tumecheza mpira mzuri sana kila mtu ameona, ila kama makocha wangekuwapo tungecheza vizuri zaidi na tungeshinda,”alisma Iddi ambaye ni kocha wa makipa Azam na kipa wa zamani wa timu hiyo.
Azam ilicheza mechi hiyo bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao wamebaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Katika mechi ya jana, hadi mapumziko, wenyeji walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji wao hatari, Nkate Jason dakika ya 24.
Nkate alifunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Azam, ambao walichanganyana na kipa wao, Mwadini Ally. Pamoja na kufungwa, Azam walicheza vizuri katika dakika 45 za kwanza na zaidi walikosa mipango tu ya kumalizia.
Hata hivyo, mashambulizi ya pembeni ya wapinzani wao yalilitia misukosuko ya kutosha lango la Azam katika ngwe hiyo.
Kipindi cha pili Azam walirudi na kikosi kile kile, lakini walibadilika kiuchezaji na iliwachukua dakika nne tu kukomboa bao, kupitia kwa Nahodha mpya, Jabir Aziz aliyeunganisha pasi ya Abdi Kassim ‘Babbi’.
Baada ya bao hilo, Azam waliendelea kushambulia lango la wapinzani wao, lakini safu ya ulinzi ya Dragons ilisimama imara kudhibiti mashmbulizi hayo.
Katika dakika ya 76, kipa Mwadini alipangua kwa uhodari mkubwa mkwaju wa penalti wa Mukinzi Mawesi, baaada ya mchezaji huyo huyo kuangushwa kwenye eneo la hatari na Ibrahim Mwaipopo.
Baada ya hapo Azam walihamia langoni mwa Dragons, ambao safu yao imara ya ulinzi iliwanusuru adhabu hii leo.
Azam ambao ni washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na Ligi Kuu, wamepangwa katika Kundi B pamoja na Dragons na Shark FC, ambayo watacheza nayo Desemba 17.
Ikifuzu kwenye kundi lake, Azam itaingia Nusu Fainali moja kwa moja, ambazo zitachezwa Desemba 25 na Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu. 
Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa. 
Kikosi cha Azam jana kilikuwa; Mwadini Ally, Himidi Mao, Waziri Salum, Luckson Kakolaki, David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim, Gaudence Mwaikimba, Abdallah Seif/Humphrey Mieno na Uhuru Suleiman/Zahor Pazi.    
Azam wakiingia na wapinzani jana

MAREKEBISHO YA KATIBA TFF YAPITA KWA KISHINDO

Rais wa TFF, Tenga
WARAKA wa marekebisho ya Katiba ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umepita baada ya kuungwa mkono na theluthi mbili ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu waliopiga kura.
Jumla ya Wajumbe waliopiga kura kwa njia hiyo ya waraka ni 103 ambapo 70 wameunga mkono wakati waliokataa ni 33. Idadi hiyo ni asilimia 68 ya kura zote zilizopigwa, hivyo kupatikana theluthi mbili ya kura zilizopigwa ili kufanya marekebisho kikatiba.
Kura zilizosema ndiyo kutoka kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa vyama vya mikoa ni 46, wajumbe kutoka vyama shiriki ni 13 wakati klabu za Ligi Kuu zilizounga mkono ni 11.
Kamati ya Utendaji ya TFF inawashukuru wajumbe wote wa Mkutano Mkuu- kwa waliounga mkono na waliokataa kwa vile walikuwa wanatekeleza wajibu wao wa kikatiba.
Vipengele vilivyoingizwa ni ‘club licencing’ kama ilivyoagizwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF kama ilivyoshauriwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na kuondoa nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Vilevile Kamati ya Utendaji itakutana Desemba 23 mwaka huu kufanya marekebisho ya Kanuni za Uchaguzi, kutokana na kupitishwa kwa marekebisho hayo ambayo yanaunda Kamati ya Rufani ya Uchaguzi wa TFF. Pia itachagua wajumbe wa Kamati ya Rufani ya TFF.
Mkutano Mkuu wa TFF ambapo pia utakuwa na ajenda ya uchaguzi utafanyika Februari 23 na 24 mwakani. Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wanatakiwa kupewa taarifa ya Mkutano Mkuu siku 60 kabla.
Wakati huo huo: Mikoa sita ambayo ni wanachama wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) haitashiriki katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa ya TWFA, wanachama hao hawatashiriki kwa vile hadi sasa haijapokea taarifa za uchaguzi kwenye vyama hivyo. Vyama hivyo ni vya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa, Shinyanga na Tabora.
Uchaguzi huo utafanyika kwenye hoteli ya Midland, na wagombea ni Isabela Kapera, Joan Minja na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma na Cecilia Mkafum (Katibu Mkuu), Zena Chande (Mjumbe Mkutano Mkuu wa TFF) na Sophia Charles na Triphonia Temba wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji. (Mwandishi wa Habari hizi ni Ofisa Habari wa TFF)

 

MAZOEZI YA TIMU YA TAIFA "TAIFA STARS" KATIKA KUJIANDAA NA MCHEZO WA KIRAFIKI DHIDI YA ZAMBIA DESEMBA 22 MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA PICHA






 

VIJANA JAZZ WAIBUKA UPYA, WAIPUA MBILI KALI *Wamshukuru Rais Kikwete kwa kuwapatia vyombo vipya *Zilipendwa zao zakonga mashabiki Masae Bar, Kawe




Picha tofauti za wanamuziki wa Vijana Jazz wakiwajibika jukwaani katika ujio mpya wa bendi hiyo


DAR ES SALAAM, Tanzania
BAADA ya kuwa 'juu ya mawe' kwa muda mrefu, bendi ya muziki wa dansi ya  Vijana Jazz,  'Wana Air Pambamoto' imeibuka upya kuanza kupiga muziki kwenye kumbi za starehe, huku ikiwa imepua vibao viwili vipya kusuuza nyoyo za mashaki wake.

Ikipiga kwa mara ya kwanza kwenye ukumbi wa Masae Bar, Kawe wilaya ya Kinodoni jijini Dar es salaam, usiku wa kuamkia leo, bendi hiyo imedhihirisha kwamba mashabiki wake wengi bado wapo.

Kwenye ukumbi huo unaotazamana na kilichokuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packes, Vijana Jazz ilithihirisha kuwa 'bado wamo', kwa kupiga nyimbo zake za zamani zikiwemo 'Mary Maria', 'Mwsiho wa mwezi', 'Ngapulila' na 'mawifi', zilizopigwa enzi za muasisi wa bendi hiyo,  marehemu Ahmed Maneti katika miaka ya 1980.

Nyimbo hizo ziliwafanya mashabiki wa bendi hiyo, kucheza kwa hamasa kubwa huku baadhi yao wakifuatisha kuimba samba mba na wanamuziki waliovuokuwa wakiimba jukwaani na wengine kwenda jukwaani kutuza waimbaji.

Licha ya kuonyesha kuwa bendi hiyo bado ni mahiri,  wanamuziki wa zamani iliobaki nao ni Roshi Mselela, Nuru Mhina (Baby White) na viongozi wa bendi Abdallah Mgonahazelu (Katibu) na Saburi Athuman ambaye ni kiongozi wa bendi.

Vibao vibya ambavyo bendi hiyo imeipua ni  'Utanieleza nini', utunzi wake kiongozi huyo na Kina mama wanaweza  uliotungwa na Mgonahazelu.
Athumani alisema, nyumbo hizo zimesharekodiwa na hivi karibuni zitaanza kuingizwa sokoni, lakini akasema bendi yake itafanya hivyo baada ya kuzipiga mara nyingi majukwaani na kuzoeleka masikioni kwa mashabiki wao.

Alisema wakati kazi ya kuzirekodi nyimbo hizo kwa ajili ya kiusikilizwa, imeshakamilika, sasa bendi imo katika jitihada za kuzirekodi katika video ili ziweze kurushwa kwenye vipindi vya Televisheni na pia kuuzwa kwa mashabiki.

"Tunamshukuru Rais Jakaya Kikwete ametutoa juu ya mawe, hivi vyombo mnavyoona ametuwezesha mheshimiwa Kikweye. Kwa kweli tunamshukuru sana", alisema Mgoma Hazeru wakati kabla ya bendi hiyo kuanza kuiba wimbo wao mpya wa 'Utanieleza nini'.

Vijana Jazz ni moja ya bendi ambazo Mratibu wa Budurano zote kwenye ukumbi huo wa Masae, Juma Mbizo, amesema atakuwa anazitumia kutoa burudani kwa mashabiki. Nyingine ni kama Msondo Band na FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma'.

AZAM YAANZA NA SARE KWA DRAGONS IKICHEZA BILA KOCHA

Mshambuliaji wa Azam, Gaudence Mwaikimba akiwatoka mabeki wa Dragons katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Hisani leo Uwanja wa Martyrs mjini Kinshasa, DRC. Timu hizo zilitoka 1-1. 

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, (CAF), Azam FC wameanza na sare ya 1-1 dhidi ya Dragons ya hapa katika mchezo wa Kundi B kuwania Kombe la Hisani kwenye Martyrs mjini hapa.
Hadi mapumziko, wenyeji walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililotiwa kimiani na mshambuliaji wao hatari, Nkate Jason dakika ya 24.
Nkate alifunga bao hilo baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Azam, ambao walichanganyana na kipa wao, Mwadini Ally. Pamoja na kufungwa, Azam walicheza vizuri katika dakika 45 za kwanza na zaidi walikosa mipango tu ya kumalizia.
Hata hivyo, mashambulizi ya pembeni ya wapinzani wao yalilitia misukosuko ya kutosha lango la Azam katika ngwe hiyo.
Kipindi cha pili Azam walirudi na kikosi kile kile, lakini walibadilika kiuchezaji na iliwachukua dakika nne tu kukomboa bao, kupitia kwa Nahodha mpya, Jabir Aziz aliyeunganisha pasi ya Abdi Kassim ‘Babbi’.
Baada ya bao hilo, Azam waliendelea kushambulia lango la wapinzani wao, lakini safu ya ulinzi ya Dragons ilisimama imara kudhibiti mashmbulizi hayo.
Katika dakika ya 76, kipa Mwadini alipangua kwa uhodari mkubwa mkwaju wa penalti wa Mukinzi Mawesi, baaada ya mchezaji huyo huyo kuangushwa kwenye eneo la hatari na Ibrahim Mwaipopo.
Baada ya hapo Azam walihamia langoni mwa Dragons, ambao safu yao imara ya ulinzi iliwanusuru adhabu hii leo.
Azam ilicheza mechi ya leo bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao wamebaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Azam ambao ni washindi wa pili wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na Ligi Kuu, wamepangwa katika Kundi B pamoja na Dragons na Shark FC, ambayo watacheza nayo Desemba 17.
Ikifuzu kwenye kundi lake, Azam itaingia Nusu Fainali moja kwa moja, ambazo zitachezwa Desemba 25 na Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu. 
Kundi B, lina timu za DC Motema Pembe, Diables Noirs, FC MK na Real De Kinshasa. 
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himidi Mao, Waziri Salum, Luckson Kakolaki, David Mwantika, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Abdi Kassim, Gaudence Mwaikimba, Abdallah Seif/Humphrey Mieno na Uhuru Suleiman/Zahor Pazi.    

Kikosi cha Dragons

Azam wakishangilia bao la kusawazisha 

Sefi Abdallah wa Azam akchuana na beki wa Dragons

Abdi Kassim ''Babbi' amemuacha mtu chini, anataka kuanza safari

Uhuru Suleiman kulia anatafuta mbinu za kumtoka  beki wa Dragons

Mwaikimba anatafuta njia...

Himid Mao aliyecheza beki ya kulia leo, akiupitia mpira miguuni mwa winga matata wa Dragons
Soka tamu iliwafurahisha viongozi wa Azam, kulia Katibu, Nassor Idrisa na kushoto Mapwisa
Kikosi cha Azam leo 

 

BPL: United, City ushindi, Liverpool kwao Anfield kipondo!!

>>QPR YASHINDA KWA MARA YA KWANZA MSIMU HUU!!
BPL_LOGO+++++++++++++++++++++++
MATOKEO:  
Jumamosi 15 Desemba 2012
Newcastle 1 Man City 3
Liverpool 1 Aston Villa 3
Man United 1 Sunderland 3
Norwich 2 Wigan 1
QPR 2 Fulham 1
Stoke 1 Everton 1
+++++++++++++++++++++++
KATIKA mfululizo wa Mechi za Barclays Premier League, BPL, Vinara Manchester United wameendelea kuwa Pointi 6 mbele kileleni baada ya kupata ushindi lakini Timu Kigogo, Liverpool, ilitandikwa Bao 3-1 nyumbani kwao Anfield walipocheza na Aston Villa huku QPR, ambao walikuwa hawajashinda hata Mechi moja Msimu huu, leo kupata ushindi wao wa kwanza.
TAARIFA KAMILI:
MAN UNITED 1 SUNDERLAND 3
Vinara wa Ligi Kuu England, Manchester United, wakiwa kwao Old Trafford wameifunga Sunderland Bao 3-1 na kuendelea kukaa kileleni wakiwa Pointi 6 mbele ya Man City.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Man United 3
-Robin van Persie Dakika ya 16
-Tom Cleverley 19
-Wayne Rooney 59
Sunderland 1
-Fraizer Campbell Dakika ya 72
+++++++++++++++++
Robin van Persie ndie aliefunga Bao la kwanza baada ya kutengenezewa na Ashley Young hilo likiwa Bao lake la 12 na kumfanya aongoze kwenye Ligi kwa Magoli 12.
Kazi nzuri ya Michael Carrick ilimfungulia Tom Cleverley kufunga Bao zuri na kuiweka Man United iwe Bao 2-0 mbele.
Kipindi cha Pili ushirikiano mzuri wa Man United ulimalizika kwa Robin van Persie kumlisha Wayne Rooney aliepachika Bao la 3.
Lakini ule udhaifu wa Man United wa kuokoa kona ulijirudia baada ya Mchezaji wa zamani wa Man United Fraizer Campbell kufunga kilaini Bao pekee la Sunderland kwa kichwa.
VIKOSI:
Man United: De Gea; Jones, Smalling, Ferdinand, Evra; Valencia, Carrick, Cleverley, Young; Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Giggs, Chicharito, Vidic, Welbeck, Scholes, Fletcher.
Sunderland: Mignolet, Larsson, Gardner, Colback, O'Shea (c), Bramble, Johnson, McClean, Cuellar, Fletcher, Sessegnon
Akiba: Campbell, Wickham, McFadden, Kilgallon, Vaughan, Westwood, Saha.
Refa: Chris Foy
LIVERPOOL 1 ASTON VILLA 3
Wakiwa kwao Anfield, Liverpool leo wamechapwa Bao 3-1 na Aston Villa huku Christian Benteke akiibuka Shujaa wa Aston Villa kwa kufunga Bao mbili na kutengeneza moja.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Liverpool 1
-Steven Gerrard Dakika ya 87
Aston Villa 3
-Christian Bentekel Dakika ya 29 & 51
-Andreas Weimann 40
+++++++++++++++++
Benteke alikuwa mwiba kwa Liverpool kwa kupachika Bao bila kutarajiwa wakati Liverpool walikuwa wakitawala na kumtengenezea Andreas Weimann kufunga Bao la pili.
Kipindi cha Pili Benteke akafunga Bao lake la Pili na kuifanya Villa iwe 3-0 mbele kabla Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard kufunga Bao pekee.
Kipigo hiki kimekuwa pigo kwa Liverpool wanaoota kumaliza 4 Bora kwa kuteremshwa hadi nafasi ya 12.
VIKOSI:
Liverpool: Reina, Johnson, Skrtel, Agger, Downing, Gerrard, Lucas, Allen, Shelvey, Suarez, Sterling. Subs: Jones, Cole, Henderson, Coates, Carragher, Fernandez Saez, Wisdom.
Aston Villa: Guzan, Lowton, Baker, Clark, Lichaj, Westwood, Herd, Holman, Bannan, Benteke, Weimann. Subs: Given, El Ahmadi, N'Zogbia, Albrighton, Delph, Bowery, Bennett.
Refa: Neil Swarbrick
STOKE 1 EVERTON 1
Kenwyne Jones leo amefunga Bao lake la kwanza baada ya Mechi 28 za Ligi na kuipa Timu yake Stoke sare ya 1-1 kufuatia Nahodha Ryan Shawcross kujifunga kwa kichwa mwenyewe akijaribu kuokoa krosi ya Steven Pienaar na kuipa Everton uongozi wa Bao moja.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Wilkinson, Shawcross, Huth, Cameron, Walters, Whelan, Nzonzi, Etherington, Adam, Jones. Subs: Sorensen, Palacios, Whitehead, Upson, Kightly, Crouch, Jerome.
Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, Naismith, Osman, Gibson, Pienaar, Fellaini, Jelavic. Subs: Mucha, Heitinga, Oviedo, Hitzlsperger, Barkley, Vellios, Duffy.
Refa: Mark Halsey
NORWICH 2 WIGAN 1
Wes Hoolahan leo ameipa ushindi Norwich wa Bao 2-1 dhidi ya Wigan baada ya kufunga Bao la Pili na kutengeneza Bao moja la kwanza lililofungwa na Anthony Pilkington
Bao la Wigan lilifungwa na Shaun Maloney.
VIKOSI:
Norwich: Bunn, Whittaker, Turner, Bassong, Garrido, Snodgrass, Tettey, Johnson, Pilkington, Hoolahan, Holt. Subs: Rudd, Martin, Howson, Jackson, Morison, Elliott Bennett, Barnett.
Wigan: Al Habsi, Boyce, Lopez, Figueroa, Stam, McArthur, McCarthy, Beausejour, Kone, Gomez, Boselli. Subs: Pollitt, Jones, Di Santo, Maloney, McManaman, Fyvie, Golobart.
Refa: Lee Probert
QPR 2 FULHAM 1
Mchezaji wa Morocco, Adel Taarabt, leo amepiga Bao mbili tamu na kuipa QPR ushindi wake wa kwanza kwenye Ligi Msimu huu.
Wakiwa wanaongoza 2-0, Mladen Petric aliipatia Fulham Bao moja na kuleta wasiwasi mkubwa kwa Timu ya QPR lakini walimaliza kwa ushindi wa 2-1 na hii ni Mechi ya 4 kwa Meneja mpya Harry Redknapp ambae ametoka sare 3 na kushinda moja.
VIKOSI:
QPR: Green, Traore, Hill, Nelsen, Onuoha, Faurlin, Mbia, Wright-Phillips, Taarabt, Cisse, Mackie
Akiba: Julio Cesar, Diakite, Derry, Ferdinand, Granero, Da Silva, Hoilett. 
Fulham: Schwarzer, Riether, Hangeland, Hughes, Riise, Duff, Sidwell, Baird, Richardson, Berbatov, Rodallega
Akiba: Etheridge, Kelly, Senderos, Petric, Karagounis, Dejagah, Kacaniklic.
Refa: Martin Atkinson
NEWCASTLE 1 MAN CITY 3
Manchester City kutoka huzuni ya kuchapwa Bao 3-2 na Mahasimu wao Manchester United na kuifunga Newcastle United Uwanjani St James' Park.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Newcastle 1
-Ba Dakika ya 51
Man City 3
-Aguero Dakika ya 10
-Garcia 39
-Yaya Toure 78
+++++++++++++++++
Sergio Aguero ndie aliepata Bao la kwanza kwa City baada ya kazi njema ya Yaya Toure na Samir.
Javi Garcia akaifanya City iwe mbele 2-baada ya kona ya David Silva lakini Demba Ba akafunga Bao kichwa na kuifanya gemu iwe 2-1.
Hata hivyo Bao la 3 la Yaya Toure, baada ya pasi ya Pablo Zabaleta, liliwamaliza Newcastle ambao sasa wamefungwa Mechi 6 za Ligi katika 7 walizocheza mwishoni.
VIKOSI:
Newcastle United: Krul, Simpson, Williamson, Coloccini, Santon, Perch, Tiote, Anita, Cisse, Ba, Gutierrez.
Akiba: Elliot, Bigirimana, Marveaux, Shola Ameobi, Sammy Ameobi, Ferguson, Tavernier.
Manchester City: Hart, Zabaleta, Nastasic, Toure, Clichy, Javi Garcia, Toure, Nasri, Aguero, Silva, Tevez.
Akiba: Pantilimon, Lescott, Dzeko, Sinclair, Kolarov, Rekik, Razak.
Refa: Andre Marriner
+++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumapili 16 Desemba 2012
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Tottenham v  Swansea
[SAA 1 Usiku]
West Brom v West Ham
Jumatatu 17 Desemba 2012
[SAA 5 Usiku]
Reading v Arsenal
+++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
[Kila Timu Mechi 16 isipokuwa inapotajwa]
1 Man United Mechi 17 Pointi 42
2 Man City Mechi 17 Pointi 36
3 Chelsea 29
4 Everton Mechi 17 Pointi 27
===============
5 Tottenham 26
6 WBA 26
7 Norwich Mechi 17 Pointi 25
8 Arsenal 24
9 Stoke Mechi 17 Pointi 24
10 Swansea 23
11 West Ham 22
12 Liverpool Mechi 17 Pointi 22
13 Fulham Mechi 17 Pointi 20
14 Aston Villa Mechi 17 Pointi 18
15 Newcastle Mechi 17 Pointi 17
16 Sunderland Mechi 17 Pointi  16
17 Southampton 15
===============
18 Wigan Mechi 17 Pointi 15
19 QPR Mechi 17 Pointi 10
20 Readind 9

ENGLAND: FELLAINI MATATANI, KOLAROV ‘UBAGUZI’ WAMPELEKA POLISI!!


>>KUMTWANGA KICHWA SHAWCROSS, FELLAINI ASUBIRI KIFUNGO TU!!
>>KOLAROV ATUA POLISI KWA KUKASHIFU KIBAGUZI UWANJANI!!
FELLAINIMechi za leo za Ligi Kuu England zimezua migogoro ambayo huenda ikawatia matatani Mchezaji wa Everton, Marouane Fellaini, kwa kumtwanga Kichwa Beki wa Stoke City, Ryan Shawcross, bila Refa kuona na pia Beki wa Manchester City, Aleksandar Kolarov, kwa kutumia lugha ya Kibaguzi dhidi ya Shabiki aliekuwepo Uwanjani St James Park.
Wakati Meneja wa Everton, David Moyes, akikiri kuwa Kiungo wake Marouane Fellaini anastahili adhabu kwa kumtandika kichwa Beki wa Stoke City, Ryan Shawcross, kwenye Mechi waliyotoka sare 1-1 Uwanjani Britannia, huku Refa Mark Halsey akilikosa tukio hilo ambalo lilinaswa waziwazi na TV, huko St James Park kumezuka mgogoro mpya wa Ubaguzi na Polisi kuhusishwa baada ya kupelekewa malalamiko kuwa Beki wa Manchester City, Aleksandar Kolarov, alimkashifu Kibaguzi Shabiki mmoja aliekuwa Uwanjani akipeperusha Bendera ya Albania.
Kolarov, ambae ni Raia wa Serbia, alikuwa Benchi kwenye Mechi kati ya Newcastle na Man City na tukio hilo lilitokea wakati yeye akipasha moto na kuanza kubishana na Mashabiki wawili waliokuwa na Bendera za Albania.
Inadaiwa Kolarov aliwatupia Matusi ya Kibaguzi Washabiki hao na mmoja wao akapeleka malalamiko kwa Walinzi wa Uwanja ambao waliwajulisha Polisi ambao walimhoji Kolarov wakati wa Haftaimu na kumtaka baadae Wiki hii aende Kituoni kuhojiwa zaidi.
Katika Mechi hiyo Kolarov aliingizwa kutoka Benchi lakini baadae alitolewa na kubalishwa Mchezaji mwingine