Wednesday, January 23, 2013

SIMBA WAWASILI DAR, WACHEZAJI WAMEFUNGASHA HAO!


Nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili wakitokea Oman walipoweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili wakitokea Oman walipoweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja akizungumza na shabiki wa timu hiyo, Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jioni hii baada ya kuwasili wakitokea Oman walipoweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Wachezaji wakmiwa kwenye basi lililowapakia kuwapeleka kambini

Mwanachama wa Simba, Makoye akimlaki Kocha Mfaransa Patrick Liewig

Kipa wa Simba SC, Abbel Dhaira akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili wakitokea Oman walipoweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kiungo wa Simba SC, Mussa Mudde akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili wakitokea Oman walipoweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mshambuliaji wa Simba SC, Felix Sunzu akitoka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, baada ya kuwasili wakitokea Oman walipoweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mudde bila shaka anakuja kufungua duka....

Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' akimlaki Mrisho Ngassa

Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo akitoka kwa furaha, hapa alisema; "Tumerudi sasa maangamizi tu".

Kaburu akimlaki Komabil Keita

Nahodha Msaidizi wa Simba, Shomary Kapombe akiwasili

Kipa wa zamani wa Simba, Iddi Pazi 'Father' kulia akiwa na Julio Uwanja wa Ndege

WATUNISIA WAANZA VYEMA KWA WENZAO MIAMBA YA ALGERIA JANA

TEMBO WA AFRIKA WAWAKANYAGA WATOGO 2-1 KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA AFCON JANA..

HATIMAYE WENGER AKUBALI KUONGEZA WATATU KLABUNI

Arsene Wenger: Is planning to bring fresh faces into the Emirates

Mfaransa  Arsene Wenger  anafuraha zaidi hasa kwa  mwenendo wa sasa kwa klabu ambayo  inataraji kuongeza watu katika kikosi chake ambacho kimejaa wachezaji wenye kiwango kikubwa na wa kimataifa.
Wenger , kwa sasa , anajua kuwa majeruhi na na adhabu vitaigharimu timu yake hasa katika kipindi hiki cha pili cha ligi ya premier ya uingereza .

Akiwa ana piga Maheseabu ya  kina, Anatarajia kufanya manunuzi ya haja katika wakati huu wa majira ya baridi .

Kiungo wa West Ham United Mohamed Diame ni moja kati ya wachezaji ambao wamepewa nafasi kubwa ya kujiunga na vijana hao wa  Emirates,Na  Wenger ameshindwa kukataa kuwa hamhitaji mchezaji huyo .
Akimuelezea mchezaji huyo amesema kuwa kama hatutatukuwa na majeruhi itakuwa sawa lakini kwa sasa kama tutakuwa na majeruhi itakuwa hasara kwetu 
."
Aliongeza ,katika tetesi za sasa kati yetu na Diame  : " Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa kiwanjani na anao uwezo wa kuchezesha vizuri sehemu ya kiungo na nilimuona siku walio cheza na chelsea alionyesha uwezo mkubwa sana kiwanjani.


MCHEZAJI BORA WA ZAMANI WA DUNIA RONALDINHO GAUCHO AITWA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL TAYARI KUWAVAAA WAINGEREZA WEMBLEY FEB 6


Remember me? Ronaldinho has won a recall after shining for Atletico Mineiro
Ronaldinho amerejeshwa baada ya kutakata vilivyo katika klabu yake ya Atletico Mineiro.
Ronaldinho ametajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil chenye jumla ya wachezaji 20 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya England utakao pigwa katika dimba la Wembley.
 
Mchezo huo maalum utakao pigwa februari 6 utakuwa ni kwa ajili ya kuadhimisha miaka 150 ya chama cha soka cha England ambapo pamoja na Ronaldinho pia amejumuishwa katika kikosi hicho mlinzi wa Chelsea David Luiz.
 
Mchezo huo utakuwa unamrudisha Ronadilnho ambaye aliwahi kuwa mchezajo bora wa dunia mara mbili, baada ya kukosekana kwa muda mrefu.

David Luiz tweeted a picture of Brazil's squad for the friendly against England
Hii ni orodha ya majina yaliyoidhinishwa na kuwasilishwa katika shirikisho la soka la Brazil.
Ronaldinho
Wito wake katika kikosi hicho umefuatia pia kutajwa Ronaldihno nyota wa zamani wa Barcelona na AC Milan kutangazwa kuwa ni miongoni mwa nyota 11 wa timu ya Brazil baada ya kuonyesha uwezo katika klabu yake ya Atletico Mineiro.
Si tu Ronaldinho wengine walioitwa na bosi mpya wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari, ni pamoja na mlinda mlando wa QPR Julio Cesar ambaye naye alipotea kwa kwa muda pamoja na nyota wa Chelsea Ramires na Oscar.
In fine form: QPR goalkeeper Julio Cesar is also back in the Brazil squad
Akiwa katika fomu mlinda mlango wa QPR Julio Cesar sasa arejeshwa na Luis Felipe Scolari.
Taarifa za kutangazwa kikosi cha Brazil zimepokelewa kwa furaha na mashabiki wa soka nchini England kwani wanatarajia kuona vionjo vya wachezaji wanaotajwa kuwa ni bora kwa sasa kama mshambuliaji wa Santos Neymar na wengine wa zamani kama mlinzi wa Barcelona Daniel Alves na Adriano.

Scolari, ambaye aliiongoza Brazil katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2002 amemuacha Ricaldo Kaka na kumpa nafasi mshambuliaji Luis Fabiano kwa kuelekea mchezo huo wa mwezi ujao.
 
Brazil itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yao kuelekea katika michuano ya Confederations Cup na kombe la dunia 2014 World Cup. 
Kwasasa Scolari ana miezi chini ya 18 kujenga kikosi cha ushindi kitakacho chukua taji la sita katika ardhi ya nyumbani Brazil.

Kikosi kamili ..

Julio Cesar (QPR), Diego Alves (Valencia); Daniel Alves, Adriano (both Barcelona), David Luiz (Chelsea), Dante (Bayern Munich), Leandro Castan (Roma), Miranda, Filipe Luis (both Atletico Madrid); Ramires (Chelsea), Arouca (Santos), Paulinho (Corinthians), Hernanes (Lazio), Oscar (Chelsea), Ronaldinho (Atletico Mineiro), Lucas Moura (Paris St Germain); Hulk (Zenit St Petersburg), Neymar (Santos), Fred (Fluminense), Luis Fabiano (Sao Paulo).

BIN KLEB AIGAWA TUZO YAKE KWA WAPIGANAJI WENZAKE YANGA


Bin Kleb

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Ahmed Bin Kleb amesema kwamba tuzo aliyopewa kwenye Mkutano wa Jumapili ni kwa ajili ya watu wote ambao amekuwa akifanya nao kazi bega kwa bega katika kuijenga klabu hiyo.
Bin Kleb alipewa tuzo ya kiongozi mwenye mchango mkubwa ndani ya Yanga katika mkutano wa Jumapili, Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam kutokana na mchango wake wenye kuonekana katika klabu hiyo.
Hata hivyo, Mtanzania huyo mwenye asili ya Kiarabu alisema kwamba ingawa yeye anaonekana anafanya kazi kubwa Yanga, lakini wapo watu ambao amekuwa akishirikiana nao na pengine wakifanya makubwa zaidi kuliko yeye, lakini ama hawaonekani au hawapendi kuonekana.
Bin Kleb alisema kwamba hadi kufikia hapa Yanga imerejesha heshma yake kuna watu ambao wamefanya kazi kubwa pamoja na Kamati ya Utendaji kwa ujumla, Baraza la Wadhamini na Kamati zote zilizoundwa.
“Kwenye Kamati yangu pekee kuna watu kama Beda Tindwa, Isaac Chanji, Mussa Katabaro na wengineo, lakini kuna watu ambao pia wamefanya kazi kubwa sana, tena sana pengine kuliko hata mimi, watu kama Seif Ahmad, Davis Mosha na wengineo ambao hawapendi kutajwa, hakika wana mchango mkubwa sana Yanga,”alisema Bin Kleb.
Aidha, Bin Kleb ameomba ushirikiano kwa wana Yanga ili kuhakikisha timu inaendelea kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaoanza Jumamosi.
“Kuongoza Ligi si maana yake tumechukua ubingwa, tunatakiwa kuendeleza mshikamano ambao ulileta mafanikiko haya, ili tufanikishe azma ya kutwaa ubingwa na pia kulipa kisasi cha 6-0 kwa watani wetu, Simba SC,”alisema Kleb.
Yanga ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 29, baada ya kucheza mechi 13, ikifuatiwa na Azam iliyomaliza na pointi zake 24 na mabingwa watetezi, Simba SC waliomaliza na pointi 23. 

KIPORO CHA BPL NI LEO KATI YA ARSENAL NA WAGONGA NYUNDO WEST HAM,PIA ANGALIA NA WANAOONGOZA KWA MABAO ENGLAND+++++++++++++++++++


>>WIKIENDI HII BPL HAMNA, KUPISHA FA CUP!!
JUMATANO, Januari 23, SAA 4 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu, Arsenal watatinga Uwanja wao wa Emirates Jijini London kucheza na West Ham katika Mechi pekee ya BPL, Barclays Premier League, ikiwa ni kiporo baada ya Mechi hii kuahirishwa kuchezwa Desemba 26 kufuatia mgomo wa Wafanyakazi wa Reli, London Underground.

BPL:
MSIMAMO-Timu zaJuu:
1 Man United Mechi 23 Pointi 56
2 Man City  Mechi 23 Pointi 51
3 Chelsea  Mechi 23 Pointi 45
4 Tottenham  Mechi 23 Pointi 41
5 Everton  Mechi 23 Pointi 38
6 Arsenal  Mechi 22 [Tofauti ya Magoli 15] Pointi 34
7 Liverpool  Mechi 23 [Tofauti ya Magoli 12] Pointi 34
8 West Brom Mechi 23 [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 34
9 Swansea  Mechi 23 Pointi 33
10 Stoke Mechi 23 Pointi 29
11 Sunderland Mechi 23 Pointi 28
12 West Ham Mechi 22 Pointi 27

WANAOONGOZA KWA UFUNGAJI MABAO


1. Robin VAN PERSIEManchester United18

2. Luis SUAREZLiverpool16

3. Demba BAChelsea14

4. MichuSwansea City13

5. Edin DZEKOManchester City10

6. Steven FLETCHERSunderland10

7. Jermain DEFOETottenham Hotspur10

8. Rickie LambertSouthampton10

9. Theo WALCOTTArsenal9

10. Gareth BALETottenham Hotspur9

11. Romelu LUKAKUWest Bromwich Albion9

12. Javier HERNANDEZManchester United8

13. Frank LAMPARDChelsea8

14. Marouane FELLAINIEverton8

15. Sergio AGUEROManchester City8

BPL_LOGOSambamba na Mechi hiyo ya BPL, pia Jumatano kutakuwa na Mechi ya Marudiano ya CAPITAL ONE CUP kati ya Swansea City na Chelsea itakayochezwa Uwanja wa Liberty na katika Mechi hiyo Swansea wanaingia wakiwa kifua mbele wakiwa wameshinda 2-0 katika Mechi ya kwanza walipocheza Stamford Bridge.
Wikiendi hii inayokuja BPL itakuwa haina Mechi kwa kupisha Mechi za Raundi ya 4 ya FA CUP na Mechi za Ligi hiyo zitachezwa katikati ya Wiki hapo Jumanne Januari 29 na Jumatano Januari 30.
TATHMINI: Arsenal v West Ham
Huku akiwa amekiri Timu yake haina mwelekeo mzuri wa ushindi mfululizo, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, amekuwa akihofia kuikosa nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao wakati sasa wapo nafasi ya 6 wakiwa Pointi 7 nyuma ya Timu ya 4 Tottenham ambayo ndio nafasi ya mwisho kucheza Ulaya.
Msimu huu, Arsenal, ambao wana Pointi 34 kwa Mechi 22 zikiwa ni Pointi chache kabisa kuwa nazo hatua kama hii katika himaya ya Wenger, wameifunga Timu moja tu iliyo juu yao na ni muhimu kuzifunga Timu zilizo chini yao kama vile West Ham ambao wako nafasi ya 12 na wana Pointi 27.
Mara ya mwisho kwa Arsenal kucheza na West Ham ilikuwa ni Oktoba ambapo West Ham walitangulia kufunga Bao lakini Arsenal waliibuka washindi kwa Bao 3-1 na kuendeleza wimbi la kutofungwa na West Ham katika Mechi 10 walizocheza mwisho.
HALI za WACHEZAJI
Baada ya kuugua, Arsenal inawakaribisha tena Lukas Podolski na Alex Oxlade-Chamberlain baada ya kukosa Mechi ya Jumapili iliyopita waliyofungwa na Chelsea.
Lakini Arsenal wana upungufu kwenye Kiungo kufuatia kuumia kwa Mikel Arteta, Abou Diaby na Francis Coquelin.
West Ham itawakosa Marouane Chamakh, ambae juzi amehamia hapo kwa Mkopo akitokea Arsenal na hivyo haruhusiwi kucheza, na pia Sentahafu James Collins ambae ni majeruhi.
USO kwa USO
-Arsenal hawajafungwa katika Mechi 10 za mwisho walizocheza na West Ham na wameshinda Mechi 8 kati ya hizo.
-Katika Mechi zao 5 za mwisho za Ligi walizokutana, Penati 5 zilipigwa katika Mechi hizo.
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumatano Januari 23
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal v West Ham
Jumanne Januari 29
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Aston Villa v Newcastle
QPR v Man City
Stoke v Wigan
Sunderland v Swansea
Jumatano Januari 30
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Arsenal v Liverpool
Everton v West Brom
Norwich v Tottenham
[SAA 5 Usiku]
Fulham v West Ham
Man United v Southampton
Reading v Chelsea
Jumamosi Februari 2
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
QPR v Norwich
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Stoke
Everton v Aston Villa
Newcastle v Chelsea
Reading v Sunderland
West Ham v Swansea
Wigan v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Fulham v Man United
Jumapili Februari 3
[SAA 10 na Nusu Jioni]
West Brom v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
Man City v Liverpool

COPA del REY: BARCA HATARINI UGENINI NA MALAGA! NA ITALIAN CUP JUVE NA LAZIO NGOMA NZITO DROO 1-1


>>BARCA KUIKOSA EL CLASICO NUSU FAINALI??
>>COPPA ITALIA: NI NUSU FAINALI!!
MABINGWA watetezi wa COPA del REY Barcelona Ijumaa wanatinga La Rosaleda kurudiana na Malaga kwenye Robo Fainali ya Kombe hili la Mfalme huku wakiwa wametoka sare 2-2 na Malaga katika Mechi ya kwanza na huku wakiwa wametoka katika kipigo chao cha kwanza kwenye La Liga walipofungwa 3-2 na Real Sociedad Jumamosi iliyopita wakijua fika wakiteleza wanaweza kuikosa EL CLASICO kwa kukutana na Real Madrid kwenye Nusu Fainali.

COPA del REY
ROBO FAINALI-MARUDIANO
[Matokeo Mechi za Kwanza katika Mabano]
Jumatano Januari 23
[SAA 3 NA Nusu Usiku]
Sevilla FC v Real Zaragoza [0-0]
[SAA 5 na Nusu Usiku]
Valencia v Real Madrid CF [0-2]
Alhamisi Januari 24
[SAA 4 Usiku]
Real Betis v Atletico Madrid [0-2]
Ijumaa Januari 25
[SAA 6 Usiku]
Malaga v Barcelona [2-2]

LIONEL_MESSI-HUZUNIMahasimu wa Barcelina, Real Madrid, wao wanatinga ugenini Mestalla kurudiana na Valencia Timu ambayo waliipiga 2-0 katika Mechi ya kwanza ya  COPA del REY Uwanjani Santiago Bernabeu na Jumapili iliyopita waliitwanga 5-0 kwenye La Liga Uwanjani Mestalla.
Atletico Madrod nao wanarudiana na Real Betis huku nao wakiwa mbele kwa Bao 2-0 walizopta katika Mechi ya kwanza lakini wataingia kwenye Mechi hii bila ya Straika wao Nyota Radamel Falcao ambae ni majeruhi.
Robo Fainali nyingine ni kati ya Sevilla na Real Zaragoza na zinarudiana Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan, nyumbani kwa Sevilla, wakiwa walitoka sare 0-0 katika Mechi ya kwanza.
Huko Italy, Kombe la Nchi hiyo, COPPA ITALIA, linaingia hatua ya Nusu Fainali.

COPPA ITALIA
NUSU FAINALI:
Jumanne Januari 22
Juventus 1 v SS Lazio 1
Jumatano Januari 23
AS Roma v Inter Milan
Jumanne Januari 29
SS Lazio v Juventus
Jumatano Aprili 17
Inter Milan v AS Roma

MAPOU YANGA MBIWA YUPO NEWCASTLE,CARLOS PUYOL NI BARCA MWISHO,SNEIJDER ATUA GALATASARAY WALIPOKUWA YANGA,NA BENITEZ ASEMA MARCO MATERAZZI NI MUONGO

NEWCASTLE UNITED imemnasa Beki wa France Mapou Yanga-Mbiwa kutoka Montpellier, nae Wesley Sneijder amekamilisha Uhamisho kutoka Inter Milan kwenda kwa Vigogo wa Uturuki Galatasaray huku Nahodha wa Barcelona Carles Puyol akiendeleza Ndoa yake kwa Barca hadi 2016 lakini Meneja wa Chelsea, Rafael Benitez, amefunguka na kudai Beki wa Italy Marco Materazzi ni mwongo wa kutupwa.

Mapou Yanga-Mbiwa yupo Newcastle United toka Montpellier

Newcastle United imemsaini Beki Mapou Yanga-Mbiwa kutoka Klabu ya France Montpellier kwa Ada ambayo haikutajwa lakini inasadikiwa kuwa £6.7m.
Beki huyo wa France mwenye Miaka 23 amesaini Mkataba wa Miaka 5 na nusu.
Na wakati huo huo, Yoan Gouffran, Fowadi wa Klabu nyingine ya France, Bordeaux, ametoboa kuwa yuko njiani kujiunga na Newcastle.

Carles Puyol

Nahodha wa Barcelona Carles Puyol amesaini nyongeza ya Mkataba ambayo itamweka Barcelona hadi Mwaka 2016.
Puyol, ambae ni Sentahafu, anaungana na Mastaa wengine wa Barca, Xavi na Lionel Messi, kwa kusaini Mikataba mipya.
Puyola, Miaka 34, alikuwa na Mkataba ambao ulikuwa umalizike Mwaka 2014.

Sneijder atua Galatasaray

Internazionale's Wesley Sneijder
Wesley Sneijder amesaini kuichezea Klabu ya Uturuki Galatasaray kwa Mkataba wa Miaka Mitatu na Nusu na kwa Dau la Pauni Milioni 8.4.
Sneijder alihamia Inter Milan Mwaka 2009 na kufanikiwa kutwaa Trebo Mwaka 2010, yaani Ubingwa wa Ulaya, Coppa Italia na Ubingwa wa Serie A.
Kutokana na mvutano na Inter Milan hasa kutaka kulazimishwa apunguzwe Mshahara, Sneijder hajaichezea Inter Milan tangu Septemba Mwaka jana.

Benitez v Materazzi
  rafa benitez
Meneja wa Liverpool Rafael Benitez amemwita Beki wa Italy Marco Materazzi kuwa ni mwongo baada ya Mchezaji huyo kudai himaya ya Benitez wakati akiwa Inter Milan ni kama kurudi Shule.
Benitez, aliekaa Inter Milan Miezi 6 tu baada ya kumrithi Jose Mourinho na kushinda Mechi 12 tu kati ya 25, amedaiwa na Materazzi kuwa alirubuniwa kuchukuliwa na Inter wakati hata Mourinho hajaondolewa na pia alimuamrisha kuondoa Picha zote za Mourinho kwenye Kabati lake binafsi Klabuni hapo.
Benitez amewaambia Wanahabari: “Anaongopa. Marco Materazzi anadanganya. Ni uongo, anadanganya tu. Akiongelea kuhusu Mourinho ni uongo, hakuna Mtu aliejua ntaenda Inter hata mie mwenyewe. Ni uongo”

TIMU NDOGO YA DARAJA LA KWANZA ILIYOIFUNGA ARSENAL,WIGAN YATIGA FAINAL CAPITAL ONE CUP BAADA YA KUIONDOSHA ASTON VILLA KATIKA DIMBA LA VILLA PARK JANA SASA KUWASUBIRI SWANSEA CITY AU CHELSEA

>>KUIVAA WEMBLEY SWANSEA AU CHELSEA!!
CAPITAL_ONE_CUP-BEST>>WAMEZIFUNGA TIMU 3 ZA LIGI KUU KUTINGA FAINALI!!
Bradford City imekuwa Timu ya kwanza ya Daraja la 4, Ligi 2, kwa zaidi ya Miaka 50 kutinga Fainali ya Kombe la Ligi, sasa linaitwa CAPITAL ONE CUP, baada ya kuibwaga Timu ya Ligi Kuu England Aston Villa kwa Jumla ya Bao 4-3 katika Mechi mbili za Nusu Fainali.

MAGOLI:
Aston Villa 2
-Benteke Dakika ya 24
-Weimann 89
Bradford 1
-Hanson Dakika ya 55

Bradford City walishinda Mechi ya Kwanza 3-1 na jana kufungwa 2-1 na Aston Villa Uwanjani Villa Park na sasa wapo Wembley kucheza Fainali na Mshindi kati ya Swansea City na Chelsea wanaorudiana leo Usiku huku Swansea wakiwa na ushindi wa 2-0 katika Mechi ya Kwanza.

BRADORD WAMEZIFUNGA TIMU 3 ZA LIGI KUU KUTINGA FAINALI:
-Wigan
-Arsenal
-Aston Villa
**FAINALI NI WEMBLEY FEBRUARI 24: Bradford City v Swansea au Chelsea

Licha ya Aston Villa kutawala Kipindi cha Kwanza na kufunga Bao kupitia Christian Benteke Bradford walisawazisha kwa Bao la kichwa la James Hanson.
Andreas Weimann aliifungia Aston Villa Bao la pili Dakika ya 89 lakini walishindwa kupata Bao nyingi ambalo lingelazimisha Muda wa Nyongeza wa Dakika 30.
VIKOSI:
Aston Villa: Given, Lowton, Vlaar, Clark, Bennett, Ireland, Delph, Bannan, N'Zogbia, Benteke, Agbonlahor
Akiba: Guzan, Bent, Holman, Weimann, Stevens, Lichaj, Carruthers.
Bradford: Duke, Darby, McHugh, McArdle, Good, Hines, Gary Jones, Doyle, Atkinson, Hanson, Wells
Akiba: McLaughlin, Ravenhill, Reid, Thompson, Connell, Nelson, Turgott.
Refa: Phil Dowd 
RATIBA/MATOKEO:
NUSU FAINALI
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Jumla ya Magoli kwa Mechi mbili]
Jumanne Januari 22
Aston Villa 2 Bradford 1 [3-4]
Jumatano Januari 23
[Mechi kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku]
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
Swansea City v Chelsea [2-0]
FAINALI
Jumapili Februari 24
Uwanja wa Wembley, London
Bradford City v Swansea/Chelsea

DONDOO MUHIMU za CAPITAL ONE CUP:
-KABLA LILIKUWA ni Carling Cup na Bingwa Mtetezi alikuwa ni Liverpool.
-Linaitwa CAPITAL ONE CUP kwa sababu Mdhamini wake ni Kampuni ya masuala ya Fedha, Capital One.
-Linashirikisha Timu za Ligi za juu England 92 kwa mtindo wa Mtoano [Timu 20 toka Ligi Kuu na 24 kila moja kutoka Madaraja ya Npower, Ligi 1 na 2.
-FAINALI itafanyika Uwanja wa Wembley Tarehe 24 Februari 2013
-Bingwa wa michuano hii hucheza EUROPA LIGI Msimu unaofuata kuanzia Raundi ya Tatu ya Mtoano.

WASHIRIKI WA MISS UTALII WATEMBELEA KAMPUNI YA UHURU PUBLICATION



WAREMBO 31 watakaoshiriki katika shindano la kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2013, jana walitembelea katika ofisi za Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), inayochapisha magazeti ya Uhuru, Burudani na Mzalendo. Katika ziara hiyo, warembo hao walijionea kazi mbalimbali za za utayarishaji wa magazeti hayo, zinavyofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kabla ya kuwafikia wasomaji. Wakizungumza baada ya ziara hiyo ya mafunzo, warembo hao walisema wamefurahi kutembelea ofisi za UPL kwa vile ndiyo kampuni pekee kongwe ya habari nchini. Wakati wa ziara hiyo, Msanifu wa Habari wa gazeti la Uhuru, Lilian Timbuka aliwaeleza warembo hao kuwa, gazeti la Uhuru lilianzishwa Desemba 9, 1961. Lilian pia aliwaeleza warembo hao kuwa, maktaba ya UPL ndiyo kongwe kuliko zote nchini na imekuwa ikihifadhi magazeti ya kampuni hiyo tangu mwaka 1961. "Hata kwa kuzalisha waandishi wa habari nchini, UPL ndio chimbuko na wanahabari wengi waliopo kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini," Lilian aliwaeleza warembo hao. Warembo hao ni Rose Edwin, Beatrice Idd, Sophia Yusufu, Ivony Steven, Irene Thomas, Erica Elibariki, Hamisa Jabir, Debora Jacob, Jania Abdul, Mulky Huda, Asha Ramadhan, Zena Alkly, Rosemary Emmanuel. Wengine ni Ana Posialy, Idan John, Doreen Bukoli, Diana Joachim, Hadija Said, Jesica Peter, Mary Lutta, Halima Hamis, Pauline Mgeni, Anganile Rodgers, Furaha Kinyunyu, Neema Julius, Chrisina Daudi, Lightness Kitua, Flora Msangi, Saraphina Jackson, Magreth Michael na Irene Richard. Shindano la Miss Utalii limepangwa kufanyika Februari 16 mwaka huu kwenye hoteli ya
Lamada mjini Dar es Salaam.


IVORY COAST YAIBANJUA TOGO 2-1,GERVINHO AITAKATIISHA IVORY


Ivory Coast imeanza kampeini yake ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa kuilaza Togo kwa magoli mawili kwa moja katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi D.
Ivory Coast ilipata bao lake la kwanza kunako dakika ya nane kupitia kwa mchezaji Yaya Toure na kwa mara nyingine, wachezaji hao wa Ivory Coast wanatafuta fursa ya kutwaa kombe hilo ambalo liliwaponyoka mwaka uliopita.Nahodha wa Ivory Coast, Didier Drogba, analiongoza tena timu hiyo, kwa fainali hizo ambazo ndizo za mwisho atakazoshiriki. Licha ya wengi kuipa timu hiyo ya Ivory Coast nafasi kubwa ya kushinda mashindano ya mwaka huu, The Elephants hawakucheza mechi ya kusisimua katika kipindi cha kwanza.
Mara ya Mwisho Ivory Coast, ilishinda kombe hilo ni mwaka wa 1992.



Togo nayo inaongozwa na mshambulizi wa Tottenham, Emmanuel Adebayor.
Dakika ya 44, Yahya Toure, nusura afunge bao la pili, lakini mkwaju wake uligonga mlingoti.
Ushirikiano kati ya Didier Drogba, Yahya Toure and Gervinho umeonekana kuwa nguzo ya timu hiyo ya Ivory Coast.
Dakika moja baadaye Togo ikasawazisha baada ya walinda lango wa Ivory Coast kufanya masihara, kwenye eneo la hatari.
Kufikia wakati wa mapumziko timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana na nguvu ya kufungana bao moja kwa moja.
Lakini katika kipindi cha pili, Ivory Coast iliimarisha mashambulizi yake na kunako dakika ya 87, ivory coast ikapata bao lake la pili kupitia kwa mchezaji Gervinho.
Ivory Coast sasa inaongoza kundi hilo la alama tatu huku Togo ikiwa bila alama yoyote.
Kinyume na ilivyotarajiwa, mechi hiyo iligeuka na kuwa maonyesho ya nguvu, baina ya wachezaji kadhaa wanaoshiriki katika ligi mbali mbali za kulipwa na mara nyingi ilikuwa kati ya Kolo Toure na Adebayor na Vincent Bossou na Didier Drogba ambao walifanya makosa mengi na hivyo kuhujumu mtiririko wa mechi hiyo.
Mechi ya pili ya kundi hilo kati ya Tunisia na Algeria itaanza mwendo wa saa tatu za usiku majira ya Afrika Mashariki.

Gervinho akishangilia kivyake baada ya kuiokoa Ivory Coast usiku huu.
Vinara wa EPL Kolo Toure (kushoto), Cheick Tiote (kulia) na Emmanuel Adebayor (kati) wakigombea mpira usiku huu kwenye AFCON 2013

Yaya Toure (katikati) akipongezwa na wenzake

Gervinho akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la ushindi na hapa anabusu uzi

Shabiki wa Togo kushoto na kulia ni shabiki wa Ivory Coast akipuliza "vuvuzela"

MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 1]
KUNDI A
-South Africa Pointi 1
-Cape Verde 1
-Morocco 1
-Angola 1
KUNDI B
-Mali Pointi 3
-Congo DR 1
-Ghana 1
-Niger 0
KUNDI C
-Burkina Faso Pointi 1
-Ethiopia 1
-Nigeria 1
-Zambia 1
KUNDI D
-Ivory Coast Pointi 3
-Tunisia 3
-Togo 0
-Algeria 0
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
[SAA za BONGO]
Jumamosi Januari 19
South Africa 0 Cape Verde Islands 0
Angola 0 Morocco 0
Jumapili Januari 20
Ghana 2 Congo DR 2
Mali 1 Niger 0
Jumatatu Januari 21
Zambia 1 Ethiopia 1
Nigeria 1 Burkina Faso 1
Jumanne Januari 22
Ivory Coast 2 Togo 1
Tunisia 1 Algeria 0
Jumatano Januari 23
South Africa v Angola [Moses Mabhida Stadium Saa 12 Jioni]
Morocco v Cape Verde Islands [Moses Mabhida Stadium Saa 3 Usiku]
Alhamisi Januari 24
Ghana v Mali [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Niger v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast v Tunisia [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Algeria v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumapili Januari 27
Morocco v South Africa [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Cape Verde Islands v Angola [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatatu Januari 28
Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumanne Januari 29
Ethiopia v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Burkina Faso v Zambia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatano Januari 30
Algeria v Ivory Coast [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Togo v Tunisia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]

KAGERA SUGAR ASHINDWA KUTAMBA MBELE YA MAAFANDE WA TABORA POLISI TABORA ALLY HASSAN MWINYI.


Timu ya kagera sugar kutoka katika mashamba ya miwa bukoba kule leo imeshindwa kutamba mbele ya wapiga kwata wa mkoani tabora polisi tabora baada ya kufungana bao 1-1 mchezo wa mwisho wa ziara wa kagera sugar ambayo ilikuwa tabora ikitoka burundi ilikokuwa imeenda kucheza mechi za kirafiki.

Kama kawaida timu ya wakatamiwa kagera sugar walikuwa wa kwanza kujipatia bao lao kupitia kwa mshambuliaji wao kutoka nigeria Wilfredy Emme aliyewachambua mabeki wa polisi tabora na kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa polisi tabora Abdul Aziz.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza timu ya kagera sugar walienda mbele kwa bao lao 1-0 kama jana ilivyokuwa kwa rhino rangers na kipindi cha pili timu ya maafande wa polisi tabora walirudi wakiwa wamerekebisha makosa yao.

Na mnamo dakika ya 57 daniel msengi aliunganisha krosi vizuri iliyochongwa na mshambuliaji w atimu hiyo iddy kibwana na kufanya matokeo kuwa 1-1.Hadi dakika 90 za mchezo mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho timu zote zilitoka hakuna mbabe baada ya kutoshana nguvu ya bao moja kwa moja 1-1.

Na kesho katika dimba hilo hilo la ALLY HASSAN MWINYI kutakuwa na mpambano mwingine wa kirafiki kati ya wanakisha mapanda wa mwanza toto african dhidi ya wanajeshi wa hapa mkoani tabora rhino rangers mchezo wa kujipima nguvu kuelekea katika duru la pili la ligi kuu tanzania VPL na ligi daraja la kwanza tanzania FDL ammbapo michuano hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi jan 26.1.2013 katika viwanja tofauti hapa tanzania.

Mchezo wa leo umeingiza shilingi laki nane na elfu hamsini na nane 858,000 kutokana na mashabiki mia nane na hamsini na nane 858 waliokata tiketi kuangalia mchezo huu kwa shilingi 1000 ikumbukwe jana waliingia watazamaji 1630 na kupata shilingi mil.1630000 kuangalia mechi ya rhino rangers na kagera sugar.
Leo wachezaji wa

KAGERA SUGAR+Andrew ntala,luhende kanyata,martin muganyizi,lamban kambole,malegesi mwangwa,zubery dabi,mecky maiko,shamte odiro,shija mkina,paul ngwai,
walioingia kipindi cha pili ni adam oseja,juma nade,benjamin asukile,george kavilla,daudi jumanne,rashid madawa,paul kabange na kamana salum.
POLISI TABORA+Abdul aziz,kaizar kilowoko,josephy manyira,jeremia ng'ambi,jamali jumanne,benard adam,mussa boaz,hussein abdalah,ramadhan semwa,daniel msengi na iddy kibwana.
BECHI+husein abdalah,david joseph,ibrahim mussa,baraka adim,ernest nkadi,na john matuli.

YANGA INATARAJIA KUWATWANGA TENA VIBONDE WA LIGI KUU SOUTH AFRICA BLACK LEOPARD CMM KIRUMBA MWANZA


Yanga SC
YANGA SC inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza leo kumenyana na Black Leopard ya Afrika Kusini, huo ukiwa mchezo wa pili kuzikutanisha timu hizo ndani ya siku nne.
Awalil, timu hizo zilimenyana Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga ikashinda mabao 3-2.
Huo utakuwa mchezo wa mwisho wa kujipima nguvu kwa Yanga, kabla ya kuingia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu hya Vodacom Tanzania Bara unaoanza mwishoni mwa wiki.
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, katika kujiandaa na mzunguko huo wa pili wa Ligi Kuu, waliweka kambi ya wiki mbili Jijini Antalya, Uturuki kuanzia Desemba 30 mwaka jana hadi Januari 12 mwaka huu.
Katika kambi hiyo, pamoja na kufanya mazoezi ya nguvu ya ufukweni, uwanjani na gym, Yanga ilipata mechi tatu za kujipima nguvu dhidi ya Ariminia Bielefed ya Daraja la Nne Ujerumani waliyotoka nayo sare ya 1-1, kabla ya kufungwa 2-1 na Denizlispor FC ya Daraja la Kwanza Uturuki na 2-0 na Emmen FC ya Daraja la Kwanza Uholanzi.
Yanga ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi zake 29, baada ya kucheza mechi 13, ikifuatiwa na Azam iliyomaliza na pointi zake 24 na mabingwa watetezi, Simba SC waliomaliza na pointi 23.  
Katika mchezo wa kwanza na Leopard Dar es Salaam, hadi mapumziko, Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na mshambuliaji wake aliyefufua makali, Jerry John Tegete dakika ya 33.
Tegete, alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti, baada ya kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Niyonzima kuangushwa kwenye eneo la hatari na beki Nkosiyaba Xakane na refa Hashim Abdallah wa Dar es Salaam akatoa adhabu hiyo.
Kipindi cha pili, kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts alifanya mabadiliko, akiwatoa pacha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wenye uraia wa Rwanda, Mbuyu Twite na Kabange Twite na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ na kuwaingiza Simon Msuva, Juma Abdul na kipa Said Mohamed.
Mabadiliko hayo, hayakuisaidia Yanga, kwani Leopard walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya kwanza tu tangu kuanza kipindi cha pili, lililofungwa kwa kichwa na Humphrey Khoza aliyetumia udhaifu wa mabeki wa timu hiyo ya Jangwani na kumtungua kipa Said Mohamed Kasarama.     
Baada ya kufungwa bao hilo, Yanga walicharuka na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 63, lililofungwa na Frank Domayo aliyeunganisha krosi maridadi ya Niyonzima.
Jerry Tegete aliifungia Yanga bao la tatu dakika ya 72 akiunganisha pasi ya beki Juma Abdul na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo waruke kwa shangwe za ‘Uturuki, Uturuki’, kuashiria hayo ni matunda ya ziara ya timu hiyo nchini Uturuki.
Beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alimuangusha kwenye eneo la hatari Humphrey Khoza dakika ya 88 na refa akawapa penalti Leopard ambayo ilikwamishwa kimiani na Rodney Romagalela na kufanya matokeo yawe 3-2.
Katika mchezo wa leo, vikosi vinatarajiwa kuwa, Yanga; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Stefano Mwasyika, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Kabange Twite, Frank Domayo, Jerry Tegete, Didier Kavumbangu na Haruna Niyonzima.
Black Leopard; Ayunda Mtshati, Ernort Zaga, Nkosiyaba Xakane, Harry Nyirenda, Humphrey Khoza, Muganga Dyange Jean, Mongezi Bobe, Thomas Madiba, Abbas Amidu, Edgar Manake na Rodney Romagalela. 

WANALAMBA LAMBA WA AZAM ,AZAM FC WANATARAJIA KUREJEA LEO TANZANIA WAKITOKEA JIJINI NAIROBI KENYA WALIKOKUWA WAPO WANAJIKUSANYIA SUMU ZA VPL


Azam FC
MABINGWA wa Kombe la Mapinduzi, Azam Fc wanatarajiwa kurejea leo usiku Dar es Salaam, wakitokea Nairobi, Kenya walipokwenda kwa ziara ya wiki moja hya michezo ya kujipima nguvu kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
AZAM FC yenye maskani yake Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ilihitimisha vema ziara yake hiyo jana, baada ya kuifunga timu ya Benki ya Biashara Kenya, KCB bao 1-0 kwenye Uwanja wa City, Nairobi jioni hii.
Bao pekee la ushindi la Azam jioni ya jana lilifungwa na kiungo Ibrahim Mwaipopo kwa shuti la mpira wa adhabu katika dakika ya pili ya muda wa nyongeza, baada ya kutimu kwa dakika 45 za kawaida za kipindi cha kwanza.
Hata hivyo, Azam ingeweza kuondoka na ushindi mnene zaidi jana, kama si kiungo wake mwingine Abdulhalim Humud ‘Gaucho’ kukosa penalti dakika ya 83 baada ya shuti lake la kudakwa na kipa wa KCB.
Huo unakuwa ushindi wa pili katika mechi zake tatu za kujipima nguvu nchini humo, kwani awali bao pekee la Gaudence Exavery Mwaikimba kwa penalti dakika ya 58 liliipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Sofapaka ya Kenya kwenye Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Katika mchezo wake wa kwanza, mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi walifungwa mabao 2-1 na AFC Leopard kwenye Uwanja huo huo wa Nyayo.
Pamoja na kufungwa na Leopard, Azam watajilaumu wenyewe, kwani walipoteza penalti mbili kupitia kwa Joackins Atudo na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Mabao ya Leopard katika mchezo huo, yalifungwa na Paul Were na Mike Barasa, wakati la Azam lilifungwa na Sammih Hajji Nuhu kwa penalti.
Azam ilimaliza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ikiwa katika nafasi ya pili kwa pointi zake 24, nyuma ya vinara Yanga waliomaliza na pointi 29, wakati Simba walimaliza nafasi ya tatu kwa pointi zao 23.
Pamoja na Ligi Kuu, Azam pia itacheza Kombe la Shirikisho la Soka Afrika na itaanza na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini mjini Dar es Salaam kati ya Februari 15 na 17 mwaka huu.
Mechi hiyo itachezeshwa na marefa wa Kenya, katikati Davies Omweno na atakayesaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Peter Keireini, mwamuzi msaidizi namba mbili Gilbert Cheruiyot wakati mwamuzi wa mezani Anthony Ogwayo.
Kamisaa wa mechi hiyo atakuwa Hassan Mohamed Mohamud kutoka Somalia, wakati marefa wa mechi ya marudiano itakayochezwa mjini Juba wiki mbili baada ya mechi ya kwanza watatoka Rwanda, wakiongozwa na Gervais Munyanziza.

SIMBA WANATARAJIA KUREJEA LEO DSM WAKITOKEA UGHAIBUNI WALIKOKUWA WAMEFUATA SUMU ZA LIGI KUU JUMAMOSI


Wachezaji wa Simba SC
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC wanatarajiwa kurejea leo Dar es Salaam, baada ya ziara ya wiki mbili nchini Oman ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Baada ya kuwasili mchana wa leo, Simba wataingia moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Black Leopard ya Afrika Kusini, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Katika ziara yake ya Oman, Simba ilipata mechi tatu za kujipima nguvu na kushinda moja na kufungwa mbili.
Katika mchezo wake wa mwisho Jumamosi, Simba SC ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Ahly Sidab kwenye Uwanja wa Sidab mjini Muscat.
Katika mchezo huo, shujaa wa Simba, alikuwa ni kiungo aliyerudi juu kisoka hivi sasa, Amri Ramadhan Kiemba aliyeifungia timu hiyo bao la ushindi.
Katika mechi hiyo nzuri na ya kusisimua, wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kipindi cha kwanza, lililofungwa na kiungo Mbrazil, aitwaye Lopez, kabla ya kiungo wa Simba, Kiggi Makassy kusawazisha kipindi hicho hicho cha kwanza.
Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na leo Simba walicheza soka nzuri mno, huku wachezaji vijana, Miraj Adam, Abdallah Seseme, Haroun Chanongo na Shomari Kapombe waking’ara zaidi. 
Kipindi cha pili, kocha Mfaransa, Patrick Liewig alifanya mabadiliko, akiwaingiza Rashid Ismail, Marcel Kaheza wote waliopandishwa kutoka timu B na Kiemba ambao waliongeza makali ya Mnyama na hatimaye kupata ushindi huo.
Alikuwa ni kiungo wa zamani wa Kagera Sugar, Yanga SC, Miembeni na Moro United aliyeipatia Simba ushindi wa kwanza katika ziara yake ya Oman kwa kufunga bao safi la ushindi dakika za mwishoni.
Katika mechi nyingine, Simba ilifungwa 1-0 na U23 ya Oman na 3-1 na timu ya Jeshi la nchi hiyo, Qaboos, bao la Wekundu hao wa Msimbazi, likifungwa na Haruna Moshi ‘Boban’.  

JUMAMOSI KINDUMBWE NDUMBWE CHA VPL KINAANZA TANZANIA ANGALIA RATIBA NZIMA YA KOMBE LA LIGI KUU TANZANIA MPAKA MEI 18


RATIBA MZUNGUKO WA PILI LIGI KUU BARA:
Januari 26, 2013
African Lyon Vs Simba SC
Mtibwa Sugar Vs Polisi Morogoro
Coastal Union Vs Mgambo JKT
Ruvu Shooting Vs JKT RUVU
Azam FC Vs Kagera Sugar
JKT Oljoro Vs Toto Africans
Januari 27, 2013
Yanga SC Vs TZ Prisons
Januari 30, 2013
Azam FC  Vs Toto Africans
Februari 2, 2013
Yanga SC Vs Mtibwa Sugar
Polisi Moro Vs African Lyon
Mgambo JKT Vs Ruvu Shooting
Februari 3, 2013
Simba SC Vs JKT Ruvu
Coastal Union Vs TZ Prisons
JKT Oljoro Vs Kagera Sugar
Polisi Moro Vs JKT Oljoro
Februari 9, 2013
Mtibwa Sugar Vs Azam FC
Toto Africans Vs Coastal Union
Kagera Sugar Vs Mgambo JKT
TZ Prisons Vs African Lyon
JKT Oljoro Vs Simba SC
Februari 13, 2013
Kagera Sugar Vs Coastal Union
Toto Africans Vs Polisi Moro
Mgambo JKT Vs  JKT Oljoro
Mtibwa Sugar Vs Ruvu Shooting
African Lyon Vs Yanga SC
Februari 20, 2013
JKT Ruvu Vs Azam FC
TZ Prisons Vs Simba SC
Coastal Union Vs JKT Oljoro
Toto Africans Vs Africans
Februari 23, 2013
Yanga SC Vs Azam FC
Mgambo JKT Vs  JKT Ruvu
TZ Prisons Vs Polisi Moro
Februari 24,  2013
Simba SC Vs Mtibwa Sugar
Februari 27, 2013
Coastal Union Vs Ruvu Shooting
Yanga SC Vs Kagera Sugar
Polisi Moro Vs Mgambo JKT
JKT Ruvu Vs Totot Africans
Mtibwa Sugar Vs TZ Prisons
Machi 6, 2013
African Lyon Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs  Mtibwa Sugar
JKT Oljoro Vs TZ Prisons
Machi 7, 2013
JKT Ruvu Vs Kagera Sugar
Machi 9, 2013
Yanga SC VS Toto Africans
Azam FC Vs Polisi Moro
Machi 10, 2013
Simba SC Vs Coastal Union
Machi  16, 2013
Toto Africans Vs Mgambo JKT
Ruvu Shooting vs Yanga SC
Mtibwa Sugar Vs Coastal Union
Machi 17, 2013
JKT Ruvu Vs Polisi Moro
Machi 18, 2013
African Lyon Vs   JKT Oljoro
Machi 27, 2013
Azam FC  Vs TZ Prisons
Kagera Sugar Vs Simba SC
Machi 30, 2013
JKT Oljoro Vs JKT Ruvu
Ruvu Shooting Vs Azam FC
African Lyon Vs Coastal Union
Polisi Moro Vs Yanga SC
Kagera Sugar Vs Mtibwa Sugar
Toto Africans Vs Simba SC
Aprili 3, 2013
Toto Africans Vs TZ Prisons
Aprili 10, 2013
Yanga SC Vs JKT Oljoro
Azam FC Vs African Lyon
TZ Prisons Vs  Mgambo JKT
Polisi Moro Vs Ruvu Shooting
Coastal Union Vs JKT Ruvu
Mtibwa Sugar Vs Toto Africans
Aprili 13, 2013
Azam FC  Vs Simba SC
Mgambo JKT Vs Yanga SC
Mtibwa Sugar Vs JKT Oljoro
TZ Prisons Vs Ruvu Shooting
Aprili 17, 2013
Kagera Sugar Vs Toto Africans
African Lyon Vs JKT Ruvu
Aprili 21, 2013
JKT Ruvu Vs Yanga SC
Aprili 23, 2013
KAGERA SUGAR AFRICAN LYON FC   Kaitaba       KAGERA
Aprili 25, 2013
Ruvu Shooting Vs Simba SC
Aprili 27, 2013
Coastal Union Vs Azam FC
Aprili 28, 2013
Simba SC Vs Polisi Moro
Mei 1, 2013
Mtibwa Sugar Vs African Lyon
Yanga SC Vs Coastal Union
JKT Ruvu Vs TZ Prisons
Polisi Moro Vs Kagera Sugar
Ruvu Shooting Vs JKT Oljoro
Mei 8, 2013
Simba SC Vs Mgambo JKT
Mei 11, 2013
Azam FC  Vs Mgambo JKT
Kagera Sugar Vs Ruvu Shooting
Mei 18, 2013
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union
(Endapo Simba SC na Azam FC hazitafanikiwa kusonga mbele michuano ya Afrika, ratiba itafanyiwa marekebisho)