Sunday, January 6, 2013

FA CUP LIVER POOL YAPETA 2-1 KWA BAO LA UTATA KWA MZEE WA KUSHIKA MPIRA LUIS SUAREZ LAKINI ARSENAL HALI TETE YATOA DROO SASA KURUDIANA KAMA ILIVYO KWA MASHETANI WEKUNDU

FA_CUP-NEW_LOGO++++++++++++++++++++++
FA CUP
MATOKEO:
Jumapili Januari 6
Swansea 2 Arsenal 2
Mansfield 1 Liverpool 2
++++++++++++++++++++++
MANSFIELD 1 LIVERPOOL 2
Luis Suarez aliifungia Liverpool Bao la pili la utata kwa kuudhibiti mpira kwa mkono na kufunga walipoipiga Mansfield Bao 2-1 na kutinga Raundi ya 4 ya FA CUP.
Mansfield, Timu ambayo haipo kwenye Mfumo ‘rasmi’’ wa Ligi huko England, walikuwa nyuma kwa Bao moja mfungaji akiwa Mchezaji mpya wa Liverpool Daniel Sturridge, lakini walikuwa wakitawala, kuleta presha kubwa na kosakosa nyingi, ndipo Suarez akapiga Bao la pili kwa Liverpool ambalo lilikuwa na walakini mkubwa.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Mansfield 1
-Green Dakika ya 79
Liverpool 2
-Sturridge Dakika ya 7
-Suarez 59
+++++++++++++++++
Matt Green aliifungia Mansfield Bao moja lakini walishindwa kupata Bao la kusawazisha licha ya kuiletea Liverpool kashikashi kubwa.
VIKOSI:
Mansfield: Marriott, Thompson, Dempster, Geohaghon, Beevers, Meikle, Clements, Murray, Howell, Briscoe, Green. Subs: Sutton, Speight, Wright, Rhead, Hutchinson, Stevenson, Daniel.
Liverpool: Jones, Wisdom, Coates, Carragher, Robinson, Lucas, Allen, Shelvey, Suso, Sturridge, Downing. Subs: Gulacsi, Suarez, Henderson, Sterling, Coady, Skrtel, Flanagan.
Refa: Andre Marriner
SWANSEA 2 ARSENAL 2
Swansea na Arsenal itabidi warudiane baada ya kutoka sare ya Bao 2-2 kwenye Uwanja wa Liberty katika Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP.
+++++++++++++++++
MAGOLI:
Swansea 2
-Michu Dakika ya 58
-Graham 87
Arsenal 2
-Podolski Dakika ya 81
-Gibbs 83
+++++++++++++++++
Michu alitoka Benchi na kuipa Swansea Bao la kuongoza lakini, ndani ya Dakika mbili, Arsenal walisawazisha kwa Bao la Lukas Podolski na kupiga la pili kupitia Kieran Gibbs.
Swansea walisawazisha Dakika 3 kabla Mechi kwisha kwa Bao la Danny Graham.
Timu hizi zitarudiana Januari 15 au 16 Uwanjani Emirates.
VIKOSI:
Swansea: Vaum, Tiendalli, Chico, Bartley, Davies, Dyer, Britton, de Guzman, Ki, Routledge, Graham
Akiba: Tremmel, Michu, Hernandez, Monk, Shechter, Rangel, Agustien.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Wilshere, Ramsey, Walcott, Giroud, Cazaula
Akiba: Martinez, Vermaelen, Rosicky, Podolski, Andre Santos, Oxlade-Chamberlain, Coquelin.
Refa: Howard Webb
++++++++++++++++++++++
FA CUP
RATIBA:
Jumatatu Januari 7
Cheltenham v Everton [SAA 4 Dak 45 Usiku]
++++++++++++++++++++++
MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
**FAHAMU: Kwa Timu zilizoenda sare kwenye Raundi ya 3 Mechi zake zitachezwa Januari 15 na 16.
Marudiano ya Swansea na Arsenal yatapangwa katika Tarehe hizo.
Jumanne Januari 15
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Leeds
Bournemouth v Wigan
Brentfaud v Southend
Leyton Auient v Hull
Wimbledon v Sheffield Wed
Stoke v Crystal Palace
Sunderland v Bolton
[SAA 5 Usiku]
Blackpool v Fulham
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham
West Brom v QPR
RAUNDI YA 4
[KUCHEZWA WIKIENDI YA JANUARI 26]
Nauwich City v Luton Town
Oldham Athletic v Liverpool 
Macclesfield Town v Wigan Athletic au Bournemouth
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City au Leyton Auient v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Millwall v Aston Villa
Leeds United au Birmingham City v Tottenham Hotspur
Brighton & Hove Albion v Swansea City au Arsenal
Crystal Palace au Stoke City v Manchester City
West Ham United au Manchester United v Fulham au Blackpool
Southend United au Brentfaud v Chelsea
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR au West Brom v Sheffield Wednesday au MK Dons
Bolton au Sunderland v Cheltenham au Everton

KIPRE TCHETCHE AAGA MAPEMA KOMBE LA MAPINDUZI 2013


Kipre Herman Tchetche akiwa jukwaani jana. Mguu wa kushoto amefunga bandeji, hiyo ndiyo sehemu iliyomtoa mapema kwenye Kombe la Mapinduzi mwaka huu

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche hatacheza tena michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani hapa baada ya kuumia katika mchezo wa kwanza dhidi ya Coastal Union ya Tanga juzi.
Akizungumza  jana Uwanja wa Amaan, Tchetche alisema kwamba maumivu aliyoyapata ni makubwa chini ya kikanyagio kwa nyuma na atatakiwa kuwa nje kwa muda usiopungua wiki mbili akipata tiba.
“Sitacheza tena haya mashindano, maumivu yataniweka nje muda wote, ndio mambo ya soka, lakini namuomba Mungu nipone haraka nirudi kuitumikia klabu yangu,”alisema nyota huyo kutoka Ivory Coast.
Tchetche alikosa mchezo wa kwanza wa Azam jana, ilipoichapa Miembeni ya hapa mabao 3-1 na kufufua matumaini ya kutetea Kombe la Mapinduzi.
Matokeo hayo, yanaifanya Azam ifikisha pointi nne na kupanda kileleni mwa Kundi B, ikifuatiwa na Miembeni yenye pointi tatu, Coastal Union ya Tanga pointi mbili na Mtibwa Sugar yenye pointi moja inashika mkia.
Hadi mapumziko, Azam walikuwa mbele kwa mabao 2-1. Azam walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya pili lililofungwa na beki Mkenya, Joackins Atudo akiunganisha kwa kichwa kona ya kiungo Mkenya, Humphrey Mieno.
Miembeni walisawazisha bao hilo dakika mbili tu baadaye, baada ya kona iliyochongwa na Adeyoum Saleh kuingia moja kwa moja nyavuni, kutokana na jitihada za mshambuliaji mkongwe, Monja Liseki kumbana kipa Mwadini Ally asiufikie mpira.
Baada ya bao hilo, Azam walicharuka na kuzidisha kasi ya mashambulizi langoni mwa Miembeni, jambo ambalo liliwasaidia kupata bao la pili dakika ya 34 baada ya mshambuliaji Gaudence Mwaikimba kuinasa pasi maridadi ya Mieno na kusogea nayo mbele kidogo kabla ya kumchambua kipa Suleiman Hamad.
Baada ya refa Ally Omar Kisaka kupuliza kipyenga cha kuashiria kutimu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza, makocha wa timu zote, Muingereza Stewaert Hall wa Azam na Salum Bausi walimfuata mwamuzi huyo kumzonga kwa madai ya kuchezeha ovyo.
Kipindi cha pili, refa huyo aliporejea kabla ya kuanzisha mchezo, aliwapa kadi nyekundu makocha wote.
Ikiongozwa na Kocha Msaidizi, Muingereza Kali Ongala, Azam ilipata bao lake la tatu dakika ya 87, mfungaji Uhuru Suleiman aliyeuwahi mpira uliorudishwa na beki kufuatia Gaudence Mwaikimba kutaka kufunga kwa kichwa.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre Balou, Salum Abubakar/Jabir Aziz dk 82, Humphrey Mieno/Ibrahim Mwaipopo dk 83, Gaudence Mwaikimba, Brian Umony/Abdallah Seif dk60 na Hamisi Mcha ‘Vialli’/Uhuru Seleman dk 65.
Miembeni FC; Suleiman Hamad, Mfaume Odello, Adeyoum Saleh, Salum Hajji, Salum Juma, Sabri Ally/Adam Hamisi dk 70, Laurent Mugiya, Suleiman Hajji, Monja Liseki/Mohamed Hamdan dk45, Rashid Roshwa/Peter Ilunda dk62 na Issa Othman.   
Katika mchezo wa kwanza, Coastal Union ya Tanga ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro, katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi, jioni hii kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa.
Hadi mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Coastal Union ndio walitakiwa kujilaumu kwa kushindwa kutumia mwanya wa Mtibwa Sugar kucheza pungufu kutokana na beki wake, Salum Swedi kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 43.
Timu zilishambuliana kwa zamu katika kipindi hicho, upande wa Coastal ukiongozwa na Danny Lyanga na Mtibwa Hussein Javu.
Baada ya Swedi kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kocha Mecky Mexime alimuinua beki Rajab Mohamed kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji, Hassan Seif.
Kipindi cha pili, Mtibwa walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 58, mfungaji Ally Mohamed ‘Gaucho’ aliyepiga shuti la umbali wa mita 19 na kumtungua Juma Mpongo.
Coastal Union ilisawazisha bao hilo dakika ya 81, mfungaji Jerry Santo aliyefumua shuti la chini la umbali wa mita 24 na kumtungua kipa Hussein Sharrif.
Katika mchezo huo, kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Hussein Sharrif, Hamisi Issa, Yussuf Nguya, Salvatory Ntebe, Salum Swedi, Babu Ally Seif, Ally Mohamed ‘Gaucho’, Rashid Gumbo, Hussein Javu, Hassan Seif/Rajab Mohamed dk43 na Vincent Barnabas.
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jerry Santo, Mohamed Miraj, Mohamed Soud Othman na Danny Lyanga.

TIMU YA RELI TABORA LEO IMENYAKUA KOMBE LA MAYOR CUP KW AKUWAFUNGA LEEDS UNITED MABAO 10-9 NA KUKABIDHIWA KOMBE NA SH 75,000


TIMU ZA LEEDS UNITED NA RELI TABORA TAYARI KWA MASHINDANO YA MAYOR CUP AMBAPO LEO ILIKUWA NDO FAINALI KATIKA UWANJA WA VITA

 
MAREFAREEE WAKIKAGUA TIMU TAYARI KWA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA MAYOR CUP HII LEO KATIKA UWANJA WA VITA

MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TABORA YUSUPH KHAMIS KITUMBO AKIWA ANAFUATILIA MPAMBANO KW AUMAKINI NA KATIBU WAKE WA TAREFA BW.FATTY DEWJ REMTULA
 
WACHEZAJI WAKO TAYARI KKWA MPAMBANO.....WA PILI KUTOKA KULIA NI MCHEZAJI WA RHINO RANGERS YA LIGI DARAJA LA KWANZA YA HAPA MKOANI TABORA ,,,,ABDALAH ,SIMBA


YUSUPH KITUMBO MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOA WA TABORA AKIKAGUA TIMU KABLA YA MCHEZO KUANZA..NYUMA YAKE NI KATIBU WA  TUFA MKOA W ATABORA MZEE MAPUNDA ALIYEKAA MGUU SAWA


SEHEMU YA MASHABIKI WAKIFUATILIA MCHEZO KW AUMAKINI HII LEO

 
BENCHI LA MAKOCHA WA TIMU YA RELI TABORA LEO KATIKA DIMBA LA VITA STADIUM





MAKOCHA WA  TIMU YA LEEDS UNITED WAKITOA MAELEKEZO KWA WACHEZAJI WAO BAADA YA HALT TIME KUTOKA UWANJANI WAKIWA NYUMA KWA BAO 1-0


WANA LAMBA LAMBA NAO WALIKUWEPO KAMA KAWAIDA WATU WALICHEZESHA MIDOMO YAO HUKU WAKIFUATILIA MECHI YA LEEDS UNITED NA RELI=====UTAMU  ULIPO BALAAA SANA KWA WANALAMBA LAMBA HAWA WA AZAM,



 
WACHEZAJI WA LEEDS UNITED WAKISHANGILIA BAO LILILOFUNGWA NA MSHAMBULIAJI WAO HATARI KHAMIS BINGWA WA MWISHI NYUMA


PATASHIKA ILIKUWA KAMA SIMBA NA YANGA WANACHEZA WATU WALIVYOKUWA NYOMIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
 
KITUMBO ANAKABIDHI PESA ZA WASHINDI WA PILI LEEDS UNITED SHILINGI ELFU HAMSINI
 
MABINGWA WA KOMBE LA MAYOR CUP RELI TABORA

KITUMBO MWENYEKITI WA TAREFA MKOA WA TABORA AKIKABIDHI SH.50000 KWA WASHINDI WA KWANZA RELI KWA NAHODHA WA RELI PAMOJA NA KIKOMBE KILICHOTOLEWA NA MAYOR MKOA WA TABORA
 
NAHODHA WA RELI AKIKABIDHIWA KOMBE LAO HII LEO KATIKA UWNAJA W A VITA

 
ILIKUWA NI FULL SHANNGWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE


SERIE A & LA LIGA ZARUDI TENA KILINGENI! VIGOGO UWANJANI LEO!

>>LEO MIAMBA REAL, BARCA, JUVE, INTER MILAN, AC MILAN, DIMBANI!
BARCA_v_REALBAADA KUWA VAKESHENI, Ligi kali za Ulaya, Serie A huko Italy na La Liga huko Spain, zimeanza tena na hapo jana huko Italy, Lazio, ambayo ipo nafasi ya Pili, iliifunga Cagliari 2-0 na kuinyemelea Juventus iliyo kileleni na sasa kuwa Pointi 5 nyuma yao.
Huko Spain, La Liga ilianza tena juzi Ijumaa kwa Real Zaragoza kuchapwa nyumbani na Real Betis Bao 2-1 na kuendelea tena jana huku leo Vinara wake, Barcelona, watakuwa nyumbani kucheza Mechi yao ya kwanza ya Mwaka 2013 na Espanyol hii ikiwa Dabi ya Jiji la Barcelona.
Mabingwa watetezi, Real Madrid, walio nafasi ya 3, pia wapo nyumbani kucheza na Real Sociedad.
Huko Italy, Serie A itaendelea kunguruma leo kwa Mabingwa, ambao pia ni vinara, Juventus, kucheza na Sampdoria pamoja na kuwepo Mechi nyingine za Timu Vigogo kama vile AC Milan, Inter Milan huku Mechi ya mvuto ni kati ya Napoli na AS Roma.
SERIE A
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Januari 5
Catania 0 Torino 0
Lazio 2 Cagliari 0
Jumapili Januari 6
AC Milan v Siena
Chievo Verona v Atalanta
Juventus v Sampdoria
Parma v Palermo
Udinese v Inter Milan
Napoli v AS Roma
Genoa v Bologna
Fiorentina v Pescara
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Januari 4
Real Zaragoza 1 Real Betis 2
Jumamosi Januari 5
Sevilla FC 1 Osasuna 0
Levante 3 Athletic de Bilbao 1
Granada CF 1 Valencia 2
Deportivo La Coruna 1 Malaga CF 0
Jumapili Januari 6
FC Barcelona v RCD Espanyol
Celta de Vigo v Real Valladolid
Real Mallorca v Atletico de Madrid
Real Madrid CF v Real Sociedad
Jumatatu Januari 7
Rayo Vallecano v Getafe CF

BORA kwa DUNIA 2012: FIFA Ballon d’Or ni JUMATATU!

 

>>FIFA Ballon d’Or: NANI MKALI-INIESTA, RONALDO au MESSI??
>>KOCHA BORA: NANI ZAIDI-GUARDIOLA, DEL BOSQUE au MOURINHO??
>>GOLI BORA: LIPI-FALCAO, NEYMAR au STOCH??
FIFA_LOGO_BESTKESHO Jumatatu huko Kongresshaus, Zurich, Switzerland, Dunia itashuhudia Tafrija maalum, FIFA World Player Gala, ambayo ni mahsusi kwa kutangaza Washindi wa Tuzo za walio Bora katika Soka kwa Mwaka 2012 kuanzia kwa Wachezaji, Makocha, Goli Bora, Kikosi Bora na Tuzo maalum za Uchezaji wa Haki na ile ya Tuzo ya Rais.
++++++++++++++++++++++++++++++++++
TUZO ZITAKAZOTOLEWA: 
FIFA Ballon d’Or [MCHEZAJI BORA DUNIANI 2012] 
FIFA MCHEZAJI BORA DUNIANI-WANAWAKE 2012
FIFA KOCHA BORA DUNIANI-WANAUME 2012
FIFA KOCHA BORA DUNIANI-WANAWAKE 2012
FIFA TUZO YA RAIS 2012
FIFA TUZO YA UCHEZAJI WA HAKI 2012 
FIFA TUZO YA PUSKAS [GOLI BORA] 2012
FIFA/FIFPro KIKOSI BORA DUNIANI 2012
++++++++++++++++++++++++++++++++++
WAGOMBEA MBALI MBALI KWA BAADHI ya TUZO hizo ni:
FIFA Ballon d’Or [MCHEZAJI BORA DUNIANI 2012]:
-Cristiano RONALDO, Portugal,
-Andres INIESTA, Spain
-Lionel MESSI, Argentina.
MESSI_n_RONALDO
FIFA MCHEZAJI BORA DUNIANI-WANAWAKE 2012:
-MARTA, Brazil,
-Alex MORGAN, USA
-Abby WAMBACH, USA.
LADIES_BEST
KOCHA BORA KWA WANAUME:
-Vicente DEL BOSQUE, Spain (Spain)
-Pep GUARDIOLA, Spain (FC Barcelona)
-Jose MOURINHO, Portugal (Real Madrid)
KOCHA BORA KWA WANAWAKE:
-Bruno BINI, France (France)
-Norio SASAKI, Japan (Japan)
-Pia SUNDHAGE, Sweden (USA)
***Wagombea hao wa Tuzo hizo walipatikana kwa Kura za Manahodha na Makocha wa Timu za Taifa za Wanaume na Wanawake pamoja na Wawakilishi wa Wanahabari walioteuliwa na Gazeti la France Football ambao ni Washirika wa FIFA katika Tuzo hizi.
TUZO YA FIFA PUSKÁS [GOLI BORA]:
- FALCAO (América de Cali-Atletico Madrid, 19 Mei 2012)
-NEYMAR (Santos-Internacional, 7 Machi 2012) –
-Miroslav STOCH (Fenerbahçe-Gençlerbirliği, 3 Machi 2012).
Pia, yalitangazwa Majina ya Fowadi 15 ambao wanaungana na Makipa watano, Mabeki 20, na Viungo 15, waliotangazwa kabla, kufanya jumla ya Wachezaji 55 watakaowania nafasi 11 za kuwemo kwenye Listi ya Wachezaji 11 watakauonda Timu Bora Duniani, FIFA/FIFPro World XI 2012, yenye Kipa mmoja, Mabeki wanne, Viungo watatu na Mafowadi watatu.
LISTI HIYO ya Wachezaji 55:
MAKIPA 5 WALIOTEULIWA:
-Gianluigi Buffon (Italy, Juventus)
-Iker Casillas (Spain, Real Madrid)
-Petr Cech (Czech Republic, Chelsea)
-Joe Hart (England, Manchester City)
-Manuel Neuer (Germany, Bayern Munich).
MABEKI 20:
-Jordi Alba (Spain, Barcelona)
-Gareth Bale (Wales, Tottenham Hotspur)
-Giorgio Chiellini (Italy, Juventus)
-Ashley Cole (England, Chelsea)-
-Dani Alves (Brazil, Barcelona)
-David Luiz (Brazil, Chelsea)
-Patrice Evra (France, Manchester United)
-Rio Ferdinand (England, Manchester United)
-Mats Hummels (Germany, Borussia Dortmund)
-Branislav Ivanovic (Serbia, Chelsea)
-Vincent Kompany (Belgium, Manchester City)
-Philipp Lahm (Germany, Bayern Munich)
-Marcelo (Brazil, Real Madrid)
-Javier Mascherano (Argentina, Barcelona)
-Pepe (Portugal, Real Madrid)
-Gerard Piqué (Spain, Barcelona)-
-Carles Puyol (Spain, Barcelona)
-Sergio Ramos (Spain, Real Madrid)
-John Terry (England, Chelsea)
-Thiago Silva (Brazil, Paris St-Germain).
VIUNGO 15:
-Xabi Alonso (Spain / Real Madrid),
-Sergio Busquets (Spain / FC Barcelona),
-Cesc Fabregas (Spain / FC Barcelona),-
-Steven Gerrard (England / Liverpool)
-Eden Hazard (Belgium / Chelsea)
-Andres Iniesta (Spain / FC Barcelona)
-Frank Lampard (England / Chelsea)
-Luka Modric (Croatia / Real Madrid)
-Mesut Özil (Germany / Real Madrid)
-Andrea Pirlo (Italy / Juventus)
-Franck Ribery (France / Bayern Munich)
-David Silva (Spain / Manchester City)
-Bastian Schweinsteiger (Germany / Bayern Munich)
-Yaya Touré (Ivory Coast / Manchester City)
-Xavi Hernandez (Spain / FC Barcelona)
MAFOWADI 15:
-Sergio Agüero (Argentina, Manchester City)
-Mario Balotelli (Italy, Manchester City)
-Karim Benzema (France, Real Madrid)
-Edinson Cavani (Uruguay, AS Napoli)
-Didier Drogba (Ivory Coast, Shanghai Shenhua)
-Samuel Eto’o (Cameroon, Anzhi Makhachkala)
-Radamel Falcao (Colombia, Atletico Madrid)
-Mario Gomez (Germany, Bayern Munich)
-Zlatan Ibrahimovic (Sweden, Paris Saint-Germain)
-Lionel Messi (Argentina, Barcelona)
-Neymar (Brazil, Santos)
-Robin van Persie (The Netherlands, Manchester United)
-Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid)
-Wayne Rooney (England, Manchester United)
-Luis Suarez (Uruguay, Liverpool)
WASHINDI 2011:
MCHEZAJI BORA: Lionel MESSI (ARG)
MCHEZAJI BORA-WANAWAKE: Homare SAWA (JPN)
KOCHA BORA: Pep GUARDIOLA (ESP)
KOCHA BORA-WANAWAKE: Norio SASAKI (JPN)
FIFA TUZO YA RAIS: Sir Alex Ferguson
FIFA TUZO YA UCHEZAJI WA HAKI: Japanese Football Association
WASHINDI WALIOPITA wa FIFA Ballon d'Or:
2011 - Lionel Messi
2010 - Lionel Messi
**FAHAMU: Tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA na ile ya France Football Ballon d'Or ziliunganishwa Mwaka 2010 na kuitwa FIFA Ballon d'Or.
WASHINDI WALIOPITA wa France Football Ballon d'Or:
2009 - Lionel Messi
2008 - C. Ronaldo
2007 - Kaka
2006 - F.Cannavaro
2005 - Ronaldinho
2004 - A. Shevchenko
2003 - P. Nedved
2002 - Ronaldo
2001 - M.Owen
2000 - L. Figo
1999 - Rivaldo
1998 - Z. Zidane
1997 - Ronaldo
1996 - M. Sammer
1995 - G. Weah
1994 - H. Stoitchkov
1993 - R. Baggio
1992 - M. Van Basten
1991 - J-P. Papin
1990 - L. Matthaeus
1989 - M. Van Basten
1988 - M. Van Basten
1987 - R. Gullit
1986 - I. Belanov
1985 - M. Platini
1984 - M. Platini
1983 - M. Platini
1982 - P. Rossi
1981 - K-H. Rummenigge
1980 - K-H. Rummenigge
1979 - K. Keegan
1978 - K. Keegan
1977 - A. Simonsen
1976 - F. Beckenbauer
1975 - O. Blokhin
1974 - J. Cruyff
1973 - J. Cruyff
1972 - F. Beckenbauer
1971 - J. Cruyff
1970 - G. Müller
1969 - G. Rivera
1968 - G. Best
1967 - F. Albert
1966 - B.Charlton
1965 - Eusebio
1964 - D. Law
1963 - L. Yashin
1962 - J. Masopust
1961 - O. Sivori
1960 - L. Suarez
1959 - A. Di Stefano
1958 - R. Kopa
1957 - A. Di Stefano
1956 - S. Matthews

FA CUP: MAN UNITED KURUDIANA NA WEST HAM JANUARI 16!

>>NI OLD TRAFFORD, SAA 5 USIKU!
MAN_UNITED-ANDO_RVP_SHINJI_EVRABAADA ya kunusurika kutolewa nje ya FA CUP hapo jana kwa Robin van Persie kusawazisha Bao Dakika ya 90 na kuifanya Manchester United itoke sare 2-2 na West Ham Uwanjani Upton Park, Mechi hii ya Raundi ya 3 itarudiwa Uwanjani Old Trafford Jumatano Januari 16 kuanzia Saa 5 Usiku.FA_CUP-NEW_LOGO
Mechi nyingine za Raundi ya 3 zilizotoka sare hapo jana zimepangwa kurudiwa Jumanne Januari 15 na moja ipo Jumatano Januari 16 kama ya Man United.
Leo, Raundi ya 3 inaenedelea kwa Mechi mbili, Swansea v Arsenal [SAA 10 na Nusu Jioni] na Mansfield v Liverpool [SAA 1 Usiku] na Mechi ya mwisho ya Raundi ya 3 ni kesho ya Cheltenham v Everton [SAA 4 Dak 45 Usiku]
Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya 4 zitakazochezwa Wikiendi ya Januari 26 itafanyika baadae leo.
MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
Jumanne Januari 15
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Leeds
Bournemouth v Wigan
Brentford v Southend
Leyton Orient v Hull
Wimbledon v Sheffield Wed
Stoke v Crystal Palace
Sunderland v Bolton
[SAA 5 Usiku]
Blackpool v Fulham
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham
West Brom v QPR

FA CUP: DROO YA RAUNDI YA 4 YAFANYIKA!

>>VIGOGO WAKWEPANA!
FA_CUP-NEW_LOGODroo ya kupanga Mechi za Raundi ya 4 ya FA CUP imefanyika leo lakini hamna ‘Bigi Mechi’ kwa vile Vigogo wametenganishwa.
DROO KAMILI:
[MECHI KUCHEZWA WIKIENDI YA JANUARI 26]
Norwich City v Luton Town
Oldham Athletic v Mansfield Town au Liverpool (Raundi ya 3)
Macclesfield Town v Wigan Athletic au Bournemouth
Derby County v Blackburn Rovers
Hull City au Leyton Orient v Barnsley
Middlesbrough v Aldershot Town
Millwall v Aston Villa
Leeds United au Birmingham City v Tottenham Hotspur
Brighton & Hove Albion v Swansea City au Arsenal
Crystal Palace au Stoke City v Manchester City
West Ham United au Manchester United v Fulham or Blackpool
Southend United au Brentford v Chelsea
Reading v Sheffield United
Huddersfield Town v Leicester
QPR au West Brom v Sheffield Wednesday au MK Dons
Bolton au Sunderland v Cheltenham au Everton
**FAHAMU: Kwa Timu zilizoenda sare kwenye Raundi ya 3 Mechi zake za marudiano zitachezwa Januari 15 na 16.
Marudiano ya Swansea na Arsenal yatapangwa katika Tarehe hizo.
MECHI ZA MARUDIANO- FA CUP-Raundi ya 3
Jumanne Januari 15
[SAA 4 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Leeds
Bournemouth v Wigan
Brentford v Southend
Leyton Orient v Hull
Wimbledon v Sheffield Wed
Stoke v Crystal Palace
Sunderland v Bolton
[SAA 5 Usiku]
Blackpool v Fulham
Jumatano Januari 16
[SAA 5 Usiku]
Man Utd v West Ham
West Brom v QPR

SIMBA YATUPA KETE YA MWISHO MAPINDUZI LEO, JULIO AAHIDI KUJIUZULU TIMU IKIFUNGWA

Kikosi cha Simba

SIMBA SC inarudi dimbani leo katika Kombe la Mapinduzi, kumenyana na Bandari ya hapa katika mchezo wake wa mwisho wa Kundi A, kwenye Uwanja wa Amaan, visiwani hapa kuanzia saa 2:30 usiku.
Simba SC inahitaji ushindi katika mchezo wa leo ili kujihakikishia kutinga Nusu Fainali, kwani hadi sasa ina pointi nne sawa na vinara wa kundi hilo, Tusker FC ya Kenya wenye wastani mzuri wa mabao.
Kocha Msaidizi wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo ameahidi kujiuzulu leo iwapo timu hiyo itafungwa na Bandari leo.
Katika mchezo uliopita, Simba SC ilionyesha kuimarika kiuchezaji na kutoa sare dhidi ya timu ngumu, Tusker ya Kenya ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Kwenye mchezo huo, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Simba wakitangulia kupata bao dakika ya 18 mfungaji Haruna Moshi Shaaban, maarufu kama Boban au Balotelli wa Bongo kabla ya Tusker kusawazisha dakika ya 39, mfungaji Khalid Aucho.
Boban alifunga bao tamu sana kwa ufundi wa hali juu akiwa amedhibitiwa na beki ngongoti wa Tusker, Joseph Shikokoti na kuirukia pasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kuitumbukiza nyavuni.
Baada ya kufunga bao hilo, Boban aliangukia mkono na kuumia, hivyo hakushangilia bao lake na moja kwa moja alianza kutibiwa na Daktari Cossmas Kapinga wa Simba.
Baada ya bao hilo, Simba iliongeza mashambulizi langoni mwa Tusker na Boban alikaribia kufunga tena dakika ya 30 kama si shuti lake kutoka nje sentimita chache.
Aucho alifunga bao lake akiunganisha krosi ya Jeremiah Bright kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
Baada ya hapo, timu zilianza kushambuliana kwa zamu hadi refa Ramadhani Kibo alipopuliza kipyenga cha kuhitimisha ngwe ya kwanza.
Kipindi cha pili timu zote zilirudi vizuri na kucheza kwa umakini wa hali ya juu, jambo ambalo lilisababisha dakika 90 zimalizike zikiwa zimefungana 1-1.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuwa kile kile kilichotoa sare ya 1-1 na Tusker; William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Shomary Kapombe, Komabil Keita, Jonas Mkude, Haroun Athumani, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Ramadhan Chombo ‘Redondo’.
Julio kushoto akiwa na Kocha Mkuu, Patrick Liewig. Ameahidi kujiuzulu timu ikifungwa

TUSKER YAIBEBA SIMBA NUSU FAINALI MAPINDUZI CUP


Tusker ya Kenya, imekuwa timu ya kwanza kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya jioni hii kuilaza Jamhuri ya Pemba bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji wake hatari, Jesse Were dakika ya 23 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mabingwa hao wa Kenya, sasa wamefikisha pointi saba na kujiimarisha kileleni mwa Kundi A na kwa matokeo hayo, Simba SC pia tayari imefuzu Nusu Fainali, kwani mabingwa hao wa Bara tayari wana pointi nne hadi sasa, wakati Jamhuri imemaliza na tatu na Bandari haina pointi hata moja. Simba inacheza mechi ya mwisho na Bandari usiku Amaan.