UWANJA: Wembley
TAREHE : Jumapili Februari 24
SAA: 1 Usiku
Bradford City, Timu ya Daraja la
chini, Ligi 2, Madaraja matatu chini ya wapinzani wao Swansea City,
inawania kutwaa CAPITAL ONE CUP na hivyo kucheza EUROPA LIGI Msimu ujao.
ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU ZA FAINALI HIYO:
+++++++++++++++++++++++++++
HALI za TIMU:
Bradford City watamcheki Beki wao Rory
McArdle kama yuko fiti baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kuumia
enka lakini hawataweza kumchezesha Straika Andy Gray kwa vile
alishaichezea Leeds United kwenye Mashindano haya.
Swansea itamkosa Beki wao Chico Flores ambae ana tatizo la enka.
Meneja wa Swansea, Michael Laudrup, ameshatangaza kuwa Kipa wa Akiba Gerhard Tremmel ndia atakeacheza Fainali hii.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
WAMEFIKAJE FAINALI
SWANSEA CITY:
-RAUNDI ya 2: SWANSEA 3 BARNSLEY 1
-RAUNDI ya 3: CRAWLEY 2 SWANSEA 3
-RAUNDI ya 4: LIVERPOOL 1 SWANSEA 3
-ROBO FAINALI: SWANSEA 1 MIDDLESBROUGH 0
-NUSU FAINALI 1: CHELSEA 0 SWANSEA 2
-NUSU FAINALI 2 : SWANSEA 0 CHELSEA 0
BRADFORD CITY:
-RAUNDI ya 1: NOTTS COUNTY 0 BRADFORD 1 (Dakika 120)
-RAUNDI ya 2: WATFORD 1 BRADFORD 2
-RAUNDI ya 3: BRADFORD 3 BURTON ALBION 2 (Dakika 120)
-RAUNDI ya 4: WIGAN 0 BRADFORD 0 (Dakika 120, Penati 4-2)
-ROBO FAINALI: BRADFORD 1 ARSENAL 1 (Dakika 120, Penati 3-2)
-NUSU FAINALI 1: BRADFORD 3 ASTON VILLA 1
-NUSU FAINALI 2: ASTON VILLA 2 BRADFORD 1 (Bradford wapita 4-3]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
TATHMINI
Ni Fainali inayokutanisha Timu ya Daraja
la chini, Bardford City, ambayo iko Ligi 2, ikiwa ni Madara matatu toka
walipo wapinzani wao Swansea City, ambao wako BPL, Barclays Premier
League.
Bradford City, chini ya Kocha Phil
Parkinson, wametinga Fainali hii kwa kushinda Mechi 4 kati ya 7 kwenye
Mashindano haya kwa Mechi kuchezwa Dakika 120 na mbili kati ya hizo kwa
Mikwaju ya Penati 5 walipozibwaga Timu kubwa toka BPL, Wigan na Arsenal.
Pia,
Bradford wana historia ambayo bila shaka itaitetemesha Swansea ikiwa
Mechi itafikia hatua ya kuamuliwa Mshindi kwa Mikwaju ya Penati 5 kwani
wao wameshinda hatua hiyo mara 9 mfululizo.
Msimu huu Swansea, chini ya Meneja
Michal Laudrup na wakiwa na Straika hatari kutoka Spain Michu, wamekuwa
wakicheza Kandanda safi na kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu England wakiwa
nafasi ya 7.
USO kwa USO:
-Hii itakuwa Mechi ya kwanza kwa Bradford na Swansea kukutana katika Kikombe kikubwa.
-Swansea hawajafungwa katika Mechi 4 za
Ligi walizokutana mwisho na Bradford, zote zikiwa ni za Ligi 1, lakini
tatu kati ya hizo zilikuwa ni sare.
-Mara ya mwisho Bradford kuifunga Swansea ilikuwa ni Bao 5-1 Uwanjani Valley Parade kwenye Ligi 1 hapo Machi 30 Mwaka 1996.
REKODI:
Bradford City
Bradford ni Timu ya pili kutoka Darala chini, Ligi 2, kufika Fainali ya Kombe la Ligi.
Timu nyingine ilikuwa ni Rochdale Mwaka 1962 ambayo ilifungwa na Norwich iliyokuwa Daraja la Pili.
Ikiwa Bradford itanyakua Kombe, itakuwa
ni Timu ya 6 kufanya hivyo bila kuwa Ligi ya juu kabisa nyingine zikiwa
ni Norwich (Daraja la 2, 1962), QPR (Daraja la 3, 1967), Swindon (Daraja
la 3, 1969), Aston Villa (Daraja la 2, 1975) na Sheffield Wednesday
(Daraja la 2, 1991).
Swansea City
Hii ni mara ya kwanza kwa Swansea City
kutinga Fainali ya Kombe hili na kabla walikuwa hawajawahi kuvuka Raundi
ya 4 ya Mashindano haya.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Bradford (Mfumo: 4-4-2): Duke; Darby, Nelson, McArdle, McHugh; Hines, G Jones, Doyle, Reid; Wells, Hanson.
Swansea (Mfumo: 4-5-1): Tremmel; Rangel, Monk, Williams, Davies; Dyer, Hernandez, Ki, De Guzman, Routledge; Michu.
Refa: Kevin Friend [Mechi: 23 Kadi Nyekundu: 1 Kadi Njano: 74]
WASHINDI WA LIGI CUP WALIOPITA:
1961 Aston Villa 0–2
1963 Birmingham City
1964 Leicester City
1965 Chelsea
1966 West Bromwich Albion
1967 Queens Park Rangers
1968 Leeds United
1969 Swindon Town
1970 Manchester City
1971 Tottenham Hotspur
1972 Stoke City
1973 Tottenham Hotspur
1974 Wolverhampton Wanderers
1975 Aston Villa
1976 Manchester City
1977 Aston Villa
1978 Nottingham Forest
1979 Nottingham Forest
1980 Wolverhampton Wanderers
1981 Liverpool
1982 Liverpool
1983 Liverpool
1984 Liverpool
1985 Norwich City
1986 Oxford United
1987 Arsenal
1988 Luton Town
1989 Nottingham Forest
1990 Nottingham Forest
1991 Sheffield Wednesday
1992 Manchester United
1993 Arsenal
1994 Aston Villa
1995 Liverpool
1996 Aston Villa
1997 Leicester City
1998 Chelsea
1999 Tottenham Hotspur
2000 Leicester City
2001 Liverpool
2002 Blackburn Rovers
2003 Liverpool
2004 Middlesbrough
2005 Chelsea
2006 Manchester United
2007 Chelsea
2008 Tottenham Hotspur
2009 Manchester United
2010 Manchester United
2011 Birmingham City
2012 Liverpool
VINARA
wa La Liga, Barcelona, wamezidi kujongelea Ubingwa, baada ya kuichapa
Sevilla kwa Bao 2-1 hii ikiwa ni Mechi yao ya kwanza toka wapokee
kichapo kule San Siri mikononi mwa AC Milan katika UEFA CHAMPIONZ LIGI.
AL
AHLY ya Misri jana ilitwaa CAF SUPER CUP kwa kuifunga AC Leopards ya
Congo Brazzaville Bao 2-1 katika Mechi ilitochezwa Uwanja wa Borg El
Arab uliopo Ukanda wa Kitalii kando kando mwa Bahari ya Mediterranean.
MABINGWA
watetezi wa BPL, Barclays Premier League, Manchester City, wakicheza
kwao Uwanja wa Etihad, leo wameichapa Chelsea Bao 2-0 na kujichimbia
nafasi ya pili na kuwasogelea Vinara wa Ligi Man United kwa kuwa Pointi
12 nyuma yao Mechi zikiwa zimebaki 11 lakini Chelsea sasa wapo hatarini
kwenye 4 bora kwani wako nafasi ya 3 na nyuma yao kwa Pointi 1 tu ni
Tottenham walio na Mechi 1 mkononi na wanafuatia Arsenal walio nafasi ya
5 Pointi 2 nyuma ya Tottenham.
Newcastle
walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuishinda Southampton, iliyo nafasi za
hatari za kushushwa Daraja, Bao 4-2 katika Mechi iliyochezwa St James
Park.
walipata
Penati katika Dakika 52 baada ya Kipa Joe Hart kumwangusha Demba Ba
lakini Frank Lampard alishindwa kufunga kwa Kipa Joe Hart kuokoa.
BAO
la Dakika ya 16 la Salvatory Ntebe leo limewapa ushindi Mtibwa Sugar wa
Bao 1-0 walipocheza na Mabingwa Simba kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu
Vodacom, iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na wao kupanda
nafasi mbili hadi ya 5 kwenye Msimamo wa Ligi na kuiacha Simba nafasi ya
3 wakiwa hatarini kung’olewa na Coastal Union walio Pointi 1 nyuma na
Mechi moja mkononi.