Saturday, January 5, 2013

JUMA KASEJA NA MRISHO NGASSA WAONDOLEWA MAPINDUZI CUP





Uongozi wa klabu ya Simba umewaondoa kwenye kikosi cha timu hiyo kinachoshiriki mashindano ya kombe la mapinduzi, Juma Kaseja aliyeomba kupumzika na Mrisho Ngasa kutokana na kuwa majeruhi.
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, amesema kuwa wamewatoa wachezaji hao kwenye mashindano haya kutokana na kuwa majeruhi.

"Kaseja na Ngasa hawatakuwepo kabisa kwenye mashindano ya Mapinduzi kwa sababu ni majeruhi na pia Kaseja aliomba kupumzika na uongozi umeliangalia hilo na kuamua kuwaondoa kikosini," .


Aidha, amesema kuwa benchi la ufundi limekubaliana na maamuzi hayo ya kuwaondoa kwenye kikosi kinachoshiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi yaliyoanza wiki hii mjini Zanzibar.


Awali, Kaseja aliuandikia barua uongozi wa timu hiyo kuomba kupewa miezi mitatu ya kupumzika kutokana na kucheza michezo mingi mfululizo akiwa na klabu yake hiyo pamoja na kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars'.


Simba kwa sasa inashiriki mashindano ya Mapinduzi ambapo Meneja wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo alisema kuwa mashindano yataisaidia timu yake kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara.


Alisema kuwa Simba ina wachezaji wengi chipukizi hivyo michuano hiyo ya kombe la mapinduzi itawapa nafasi kuonyesha uwezo wao.


Awali kulikuwa na taarifa kuwa kikosi cha timu hiyo kitaenda kuweka kambi nchini Oman kujiandaa na mzunguko wa pili lakini ushiriki wao katika michuano hiyo ya kombe la Mapinduzi ni wazi huenda safari hiyo isiwepo kwa kuwa mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara umepangwa kuanza Januari 19 mwaka huu.


Wakati Simba wakishiriki katika michuano hiyo, watani wao, Yanga wenyewe wapo nchini Uturuki walipokwenda kuweka kambi kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu.

COASTAL YASHINDWA KUIFUNGA MTIBWA PUNGUFU


Ally Mohamed ‘Gaucho’ akipambana na wachezaji wa Coastal Union, Othman Tamim na Suleiman Kassim ‘Selembe’ katika mchezo wa leo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 

COASTAL Union ya Tanga imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Morogoro, katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi, jioni hii kwenye Uwanja wa Amaan visiwani hapa.
Hadi mapumziko, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Coastal Union ndio walitakiwa kujilaumu kwa kushindwa kutumia mwanya wa Mtibwa Sugar kucheza pungufu kutokana na beki wake, Salum Swedi kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 43.
Timu zilishambuliana kwa zamu katika kipindi hicho, upande wa Coastal ukiongozwa na Danny Lyanga na Mtibwa Hussein Javu.
Baada ya Swedi kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kocha Mecky Mexime alimuinua beki Rajab Mohamed kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji, Hassan Seif.
Kipindi cha pili, Mtibwa walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 58, mfungaji Ally Mohamed ‘Gaucho’ aliyepiga shuti la umbali wa mita 19 na kumtungua Juma Mpongo.
Coastal Union ilisawazisha bao hilo dakika ya 81, mfungaji Jerry Santo aliyefumua shuti la chini la umbali wa mita 24 na kumtungua kipa Hussein Sharrif.
Katika mchezo huo, kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Hussein Sharrif, Hamisi Issa, Yussuf Nguya, Salvatory Ntebe, Salum Swedi, Babu Ally Seif, Ally Mohamed ‘Gaucho’, Rashid Gumbo, Hussein Javu, Hassan Seif/Rajab Mohamed dk43 na Vincent Barnabas.
Coastal Union; Juma Mpongo, Ismail Khamis, Othman Tamim, Philip Metusela, Mbwana Khamis ‘Kibacha’, Hamisi Shengo, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Jerry Santo, Mohamed Miraj, Mohamed Soud Othman na Danny Lyanga. 
MSIMAMO WA KUNDI B:
                          P    W  D   L    GF GA GDPts
Miembeni           1    1    0    0    4    1    3    3
Coastal Union    2    0    2    0    1    1    0    2   
Mtibwa Sugar     2    0    1    1    2    5    -3  1   
Azam FC           1    0    1    0    0    0    0    1   

KATIBU MKUU WA TAREFA FATTY REMTULA AKABIDHI VYETI KWA MAKOCHA 30 MKOANI TABORA LEO



Chama cha soka mkoa wa tabora TAREFA chini ya uenyekiti wa Yusuph Kitumbo  na katibu mkuu FATTY DEWJ REMTULA leo  kimetoa  vyeti vya wahitimu ngazi ya preliminary ya ukocha ambao bado hawajapatiwa vyeti vyao,ambao walimaliza mafunzo miaka ya nyuma na a mbao wamemaliza mafunzo hivi majuzi chini ya ukufuzi wa SLIVESTER MARSH kocha msaidizi w atimu ya Taifa ya Tanzania.

Akikabidhi vyeti hivyo katibu mkuu wa TAREFA mkoa wa tabora FATTY REMTULA ametoa vyeti hivyo kwa  Makocha 30 ambao walihitimu ngazi hiyo  wa awali ni hawa wafuatao,Stephen Paulo Luziga,Hassan Omary Morrocco,Balunda K. Njeno,Emmanuel M,Kahuka,Gidion P.K Masunga,Kopa Rashid,Kopa,Bastidi G Protas,Seif Salim Omary,Joseph R Kitwenya,Maganga J Brighton ,Selemani Ally Malenge,na Fredrick D Jairos.

Wengine wanaotarajia kukabidhiwa vyeti hivyo ni Mashaka S Kalunga,Mohamedy J Mkoko,Emmanuely P Kinandikwa,Gift E Mwinuka,Milambo Camil Yusuph,Eliah John Lusinde,Hamady Hamis Simba,Osborn Mathew Msaka,Reuben Maige Lishim ,Donard S Mlawa,Fedinand S Machunde,Goerge Marriot Kazi,Revocatus M Fundi,Peter Seif Sizya,Joel Mathayo Rukutsa,Charles K Kidifu,Bora Frank Nduguru na Yahaya Masimba Mntangi.

WAKATI HUO HUO Chama cha makocha mkoa wa Tabora TAFCA  kimeamua kuufuta uchaguzi ambao ulikuwa unatarajia kufanyika mkoa Tabora tarehe 10/1/2013 hapa mkoani tabora umefutwa kutokana na wanachama wa TAFCA kuridhia kuwa ni bora kwanza chama kikafufuliwa ili kiwe hai kwani kuna baadhi ya wanachama wanalipa pesa zao za uanachama lakini hawatambuliwi kuwa ni wanachama kutokana na ubazilifu wa pesa kwa baadhi ya viongozi wa TAFCA kuziminya pesa za wajumbe hao.

BA RASMI CHELSEA, COLE RASMI WEST HAM, BALOTELLI ‘NAFASI 100!’

>>CHAMAKH NAE ATU WEST HAM KWA MKOPO!!
>>LIVERPOOL YAMLIPA COLE PAUNI MILIONI 3 KUNG’OKA!
DEMBA_BA-AENDA_CHELSEAUHAMISHO umepamba moto huku Demba Ba akithibitishwa kuihama Newcastle na kutua Chelsea, West Ham ikiwapata Joe Cole kutoka Liverpool na kumchukua Straika wa Arsenal Marouane Chamakh kwa mkopo lakini Mario Balotelli atabaki Manchester City baada ya Meneja Roberto Mancini kutamka atampa ‘nafasi 100’ ili ajirekebisha baada ya jana kutaka kutwangana nae mazoezini.
DEMBA BA
Chelsea imemsaini Demba Ba, Miaka 27, kutoka Newcastle kwa Mkataba wa Miaka mitatu na nusu na kwa Dau ambalo halikutajwa.


REKODI YA DEMBA BA:
-Alizaliwa Paris, France ikiwa ni mmoja wa Watoto wanane
-Klabu alizowahi kuchezea: Rouen, Mouscron, Hoffenheim, West Ham, Newcastle
-Aliifungua West Ham Bao 7 katika Mechi 12 alizocheza za Ligi Kuu England
-Alifunga Bao 17 katika Msimu wake wa kwanza na Newcastle
-Msimu huu ameshapachika Mabao 13 kwa Newcastle

Ba, ambae alihamia Newcastle kutoka West Ham Mwezi Juni 2011, anambadili Daniel Sturridge alieihama Chelsea kwenda Liverpool hivi juzi.
Demba Ba anaruhusiwa kuichezea Chelsea kwenye Mechi yao ya Jumamosi ya FA CUP dhidi ya Southampton na ile Nusu Fainali ya CAPITAL ONE CUP ambayo watacheza na Swansea lakini haruhusiwi kucheza UEFA EUROPA LIGI kwa vile alishawahi kuichezea Newcastle kwenye Mashindano hayo.


WEST HAM
West Ham imewanasa Joe Cole kutoka Liverpool kwa Uhamisho wa bure bila kulipa chochote na pia Marouane Chamakh ambae atakuwa hapo kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu.
Cole, mwenye Miaka 31 ambae alihamia Liverpool kutoka Chelsea Mwaka 2010 pia kwa Uhamisho wa bure, amekuwa hana namba Liverpool na Msimu uliopita alipelekwa kuchezea Klabu ya France Lille kwa Mkopo.
Cole amepewa Mkataba wa Miezi 18 na West Ham, Klabu ambayo alianzia Soka lake, na yupo huru kucheza dhidi ya Manchester United Jumamosi kwenye Mechi ya FA CUP itakayochezwa Upton Park.
+++++++++++++++++++++++++++++++
REKODI ya JOE COLE:
-West Ham: Mechi 150 Magoli (1999-2003)
-Chelsea: Mechi 282 Magoli (2003-2010)
-Liverpool: Mechi 42 Magoli 5 (2010-2013)
-Lille: Mechi 38 Magoli 4 (Mkopo 2011-2012)
-England: Mechi 56 Magoli 10 (2001-2010)
+++++++++++++++++++++++++++++++
Inaaminika Liverpool imekubali kumlipa Joe Cole Pauni Milioni 3 ili ahame ili wao waokoe Pauni Milioni 4 ambazo angelipwa kama angeendelea kubakia Klabuni hapo hadi Mkataba wake unakwisha baada ya Miezi 18 huku akipokea Mshahara wa Pauni 92,000 kwa Wiki.
Huko West Ham atalipwa Pauni 50,000 kwa Wiki.
Wakati huo huo, West Ham imemchukua Straika wa Arsenal Marouane Chamakh kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu.
Ingawa Straika huyo amekuwa hana namba ya kudumu huko Arsenal tangu atue hapo kutoka Bordeaux Mwaka 2010, Meneja wa West Ham, Sam Allardyce, amesema amelazimika kupata Straika mwingine kwa vile Andy Carroll ni majeruhi, Modibo Keita atakuwa hayupo kwa vile anaenda kucheza AFCON 2013 na wamebakiwa na Straika mmoja tu, Carlton Cole.
Hata hivyo, Marouane Chamakh, haruhisiwi kucheza dhidi ya Manchester United Jumamosi kwenye Mechi ya FA CUP itakayochezwa Upton Park kwa vile amechelewa kusajiliwa.


BALOTELLI KUPEWA ‘NAFASI 100!’
Bosi wa Manchester City Roberto Mancini amesema atampa Mario Balotelli "nafasi 100 zaidi" ili ajirekebishe baada ya kuvaana na nusura kutwangana jana mazoezini.MANCINI_n_BALOTELLI-MSHIKEMSHIKE
Hata hivyo Mancini amekana kuhusu kupigana na ametamka: "Hamna kupigana, si kweli. Picha zinaonyesha vibaya!”
Akaongeza: “Nitampa nafasi 100 zaidi ikiwa upo uwezekano wa yeye kubadilika. Nampa nafasi nyingine kwa vile ana Miaka 22 na anaweza kufanya makosa!”
Akisisitiza kuwa Picha zilizochapishwa kwenye Vyombo vya Habari zimepotosha ukweli, Mancini alisema: “Haikuwa mbaya kiasi kile! Tulikuwa tunacheza gemu na Mario akampiga teke Mchezaji mwingine! Nikwambia aondoke Uwanjani, aende ndani na yeye akasema hapana, nikamkunja Jezi na kumsukuma! Haikuwa kitu kikubwa!”

FA CUP LEO INAENDELEA KULE ENGLAND VIGOGO DIMBANI!

>>MECHI 4 TU KUKUTANISHA TIMU ZA LIGI KUU!!
FA_CUP-NEW_LOGOYALE MASHINDANO YA KALE kupita yeyote Duniani, FA CUP ya England, yanaingia Raundi ya 3 Wikiendi hii na hii ni nafasi kubwa kwa Timu ‘ndogo’ kuzibwaga Timu ‘kubwa’ kwani Timu za Ligi Kuu England ndipo zinapoanza kushindana na Mabingwa watetezi, Chelsea, wataanza utetezi wao kwa kucheza ugenini na Southampton Jumamosi Januari 5 na hiyo ni Mechi mojawapo kati ya 4 itakayozikutanisha Timu za Ligi Kuu England pekee.
Mechi nyingine ambazo zitakutanisha Timu za Ligi Kuu England pekee ni zile za Manchester United kutua Upton Park kucheza na West Ham United, QPR kuikaribisha West Brom na Arsenal kusafiri kucheza na Swansea.
++++++++++++++++++++++
RATIBA:
RAUNDI ya TATU:
Jumamosi Januari 5
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Brighton v Newcastle
[SAA 12 Jioni]
Crystal Palace v Stoke
Tottenham v Coventry City
Wigan v Bournemouth
Fulham v Blackpool
Aston Villa v Ipswich
Charlton v Huddersfield
Barrow au Macclesfield v Cardiff
Barnsley v Burnley
Manchester City v Watford
Leicester v Burton
Millwall v Preston
Derby v Tranmere
Crawley v Reading
Aldershot v Rotherham
Middlesbrough v Hastings
Oxford v Sheffield United
Southampton v Chelsea
QPR v West Brom
Peterborough v Norwich
Bolton v Sunderland
Nottingham Forest v Oldham
Hull v Alfreton or Leyton Orient
Blackburn v Bristol City
Leeds v Birmingham
Southend v Brentford
Luton v Wolves
Sheffield Wednesday v MK Dons
[SAA 2 na Dak 15 Usiku]
West Ham v Manchester United
Jumapili Januari 6
Swansea v Arsenal [SAA 10 na Nusu Jioni]
Mansfield v Liverpool [SAA 1 Usiku]
Jumatatu Januari 7
Cheltenham v Everton [SAA 4 Dak 45 Usiku]

LA LIGA & SERIE A KUANZA KURINDIMA WIKIENDI HII BAADA YA KUWA LIKIZONI KWA SIKUKUU YA XMASS NA NEW YEAR 2013!!

BARCA_v_REALBAADA ya kutoka Vakesheni ya Krismasi na Mwaka mpya, Ligi za Nchini Spain na Italy, LA LIGA na SERIE A, zinaingia kilingeni Wikiendi hii.
La Liga itaanza Mechi zake leo Ijumaa kwa Mechi moja ya Real Zaragoza v Real Betis na nyingine kuchezwa Jumamosi ambapo vinara FC Barcelona watakuwa nyumbani kucheza Dabi ya Jiji la Barcelona dhidi ya Espanyol, Mabingwa watetezi, walio nafasi ya 3 Real Madrid, kucheza pia nyumbani na Real Sociedad.
Huko Italy, Serie A itaanza kunguruma Jumamosi kwa Mechi mbili na Mabingwa, ambao pia ni vinara, Juventus, watacheza Jumapili na Sampdoria.
LA LIGA
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 17]
1 Barcelona Pointi 49
2 Atletico Madrid 40
3 Real Madrid 33
4 Malaga 31
5 Real Betis 28
6 Levante 27
7 Real Sociedad 25
RATIBA:
Ijumaa Januari 5
Real Zaragoza v Real Betis
Jumapili Januari 6
FC Barcelona v RCD Espanyol
Celta de Vigo v Real Valladolid
Deportivo La Coruna v Malaga CF
Real Mallorca v Atletico de Madrid
Real Madrid CF v Real Sociedad
Sevilla FC v Osasuna
Levante v Athletic de Bilbao
Granada CF v Valencia
Jumatatu Januari 7
Rayo Vallecano v Getafe CF
SERIE A
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 18]
1 Juventus Pointi 44
2 Lazio 36
3 Fiorentina 35
4 Inter Milan 35
5 Napoli 34
6 AS Roma 32
7 AC Milan 27
8 Parma 26
RATIBA:
Jumamosi Januari 5
Catania v Torino
Lazio v Cagliari
Jumapili Januari 6
AC Milan v Siena
Chievo Verona v Atalanta
Juventus v Sampdoria
Parma v Palermo
Udinese v Inter Milan
Napoli v AS Roma
Genoa v Bologna
Fiorentina v Pescara

KIBIBI KIZEE CHA TURIN JUVENTUS WAKANA KUMTAKA DROGBA.



 Antonio Conte amekanusha kuwa Juventus iko kwenye mpango wa kumchukua Didier Drogba kuelekea Turin lakini amesema Fernando Llorente yuko katika mipango ya mapendekezo.
Didier Drogba kwasasa anasaka klabu ya kuelekea kutoka katika klabu yake ya sasa Shanghai Shenhua ya dirisha dogo la usajili.
Juve maarufu kama Bianconeri tangu kufunguliwa kwa  dirisha la usajili wa majira ya baridi, imekamilisha usajili wa mchezaji mmoja tu mlinzi Federico Peluso aliyetokea Atalanta lakini pia wakiwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
Drogba, amekuwa akihusishwa na Juve katika kipindi cha hivi karibu wakati ambapo Athletic Bilbao ikiweka wazi kuwa mshambuliaji wao Llorente ameanza mazungumzo ya kujiunga na Juventus mara baadya mkataba wake kumalizika.
MANCINI ASEMA KLABU ILIGUSWA NA NA MZOZO WAKE NA BAOTELLI

 
Roberto Mancini amesisitiza kuwa mmiliki wa klabu na mwenyekiti wa klabu ya Manchester United wameonekana kuridhishwa na hatua yake ya kutaka kumrekebisha kumpa nafasi zaidi Mario Balotelli.
Mancini amesema hapingani na hali ya sintofahamu iliyojitokeza wakati wa mzozo wake na Balotelli katika uwanja wa mazoezi ambapo meneja huyo wa City alionekana kwenye picha akimkunja mshambuliaji wake kijezi cha juu cha mazoezi(bips).
Mtaliano huyo amesema mmiliki wa klabu Sheikh Mansour na mwenyekiti wa klabu Khaldoon al Mubarak wamekubaliana na mawazo yake ya kutaka kumpa muda zaidi wa kujirekebisha sambamba kumpa fursa nyingine.
Amenukuliwa Mancini akisema,
"kwakweli wananipa sapoti mimi na timu kwa ujumla na nadhani wananipenda na wana matumaini kuwa Mario anaweza kubadilika na tufikirie zaidi juu ya kazi yake na mpira"
Boateng huenda akaondoka Italia.
 Kiungo wa AC Milan Kevin-Prince Boateng anatarajiwa kutoa maamuzi yake magumu katika siku zijazo kama ataendelea kucheza soka katika ligi kuu ya nchini Italia Serie A au kuondoka, kufuatia kitendo cha kibaguzi alicho fanyiwa wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Pro Patria mwishoni mwa juma.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ghana Boateng pamoja na wachezaji wenzake wa Milan waliamua kuondoka uwanjani kufuatia kitendo hicho kilichofanywa na mashabiki.
Shirikisho la soka la Italia (FIGC) limesema litaendesha uchunguzi, wakati ambapo kitendo cha kususia kuendelea na mchezo huo kuonekana kuwavutia watu wengi mashuhuri akiwemo kocha wa timu ya taifa ya Italia Cesare Prandelli.
Boateng ambaye ana mkataba mpaka 2014, anafikiria kuondoka nchini Italia.
Amenukuliwa na gazeti la Bild la nchini Italia Bouteng mchezaji huyo mzaliwa wa Ujerumani akisema
"hili si jambo la mzaha, nipe siku tatu nilale niamke na nikutane na wakala wangu Roger Wittmann wiki ijayo tuone kama kama kuna haja ya kuendelea kucheza Italia"

ANDY MURRAY KUTWAA UBINGWA BRISBANE INTERNATIONAL KESHO?



BRISBANE, Australia
NYOTA wa tenisi raia wa Uingereza, Andy Murray, 25, kesho Jumapili anakutana uso kwa uso na Grigor Dimitrov wa Ubelgiji katika fainali ya michuano ya Brisbane International, huku akipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.
Murray alitinga kirahisi fainali ya michuano hiyo baada ya mpinzani wake katika mechi ya nusu fainali, Kei Nishikori kujitoa mchezoni kutokana na kuumia goti.
Murray anayeshikilia nafasi ya tatu kidunia kwa ubora wa tenisi na namba moja kwa Uingereza, alirudi vema kutoka mapumziko na kutoka nyuma na kushinda 6-4 katika mechi za seti tatno mfululizo.
Mkali huyo alikuwa mbele kwa seti 2-0 katika nusu ya pili ya pambano lao, wakati Nishikori wa Japan alipoamua kujitoa rasmi na kumruhusu Mskochi huyo kutinga fainali.
Kesho Murray ataoneshana ubabe na mkali wa mchezo huo Dimitrov raia wa Ubelgiji, ambaye alimshinda Marcos Baghdatis wa Cyprus kwa 6-3 5-7 7-6 (7-5) katika nusu fainali nyingine ya michuano hiyo.
Brisbane International ni michuano inayochukuliwa kama sehemu ya maandalizi ya Murray, anayejiweka tayari kwa mashindano ya Australian Open, yatakayofanyika kwa wiki mbili kuanzia Januri 14 hadi 27, jijini Melbourne.

PRINCE-BOATENG ALIFANYA MAKOSA - SEEDORF.


MCHEZAJI nguli wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya AC Milan Clerence Seedorf amesema Kevin-Prince Boateng ambaye alikuwa mchezaji mwenzake katika klabu alifanya vibaya kuwaongoza wenzake kuondoka uwanjani kwasababu ya kufanyiwa vitendo vya kibaguzi. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ghana alikamata mpira kisha kuupiga kwa mashabiki ambao walikuwa wakishangilia kwa kutoa kelele za nyani kwa wachezaji weusi wa Milan na kusababisha mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Pro Patria uliochezwa Alhamisi kuvunjika dakika ya 25. Pamoja na Seedorf kuponda tukio hilo lakini Patrick Vieira, Rio Ferdinand na Vincent Kompany waliunga mkono kwa nyakati tofauti kitendo kilichofanywa na Prince Boateng. Seedorf ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya Botafogo ya Brazil alitegemea tukio tofauti na hilo ili kupambana na mashabiki hao wabaguzi badala kuondoka uwanjani na kususia mchezo. Nyota huyo amesema ingekuwa vizuri zaidi kama Boateng angewatambua mashabiki hao wabaguzi na kisha kuamriwa kutoka nje ya uwanja na mchezo uweze kuendelea na sio kususia mchezo kwani unawanyima burudani mashabiki wengi wastaarabu ambao walikuja uwanja kutizama mechi. Seedorf amecheza Milan kuanzia mwaka 2002 mpaka 2012 na kufanikiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya m waka 2003 na 2007.

RAIS WA PSG NASSER AL KHELAIFI ASEMA HAWEZI KUONGEA NA RONALDO KWA MLANGO WA NYUMA - AL KHELAIFI.


RAIS wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG, Nasser Al Khelaifi amesisitiza kuwa klabu yake haitaanza mbio za kumfukuzia Cristiano Ronaldo bila kwanza kuzungumza na Real Madrid. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno anaonekana kutokuwa na furaha katika klabu hiyo yenye maskani yake katika Uwanja wa Santiago Bernabeu ambapo PSG wameonyesha kwamba wapo tayari kumsajili nyota huyo katika Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Al Khelaifi amesema anatambua Ronaldo ni mchezaji wa Real Madrid na anaheshimiana sana na rais wa klabu hiyo hivyo hawezi kufanya jambo bila kumtaarifu. Mbali na Ronaldo kuripotiwa kutakiwa na PSG lakini pia kocha wa Madrid Jose Mourinho naye amehusishwa na tetesi za kutimkia katika klabu hiyo tajiri nchini Ufaransa lakini Khelaifi amesisitiza bado wana imani kubwa na kocha wa sasa Carlo Ancelotti.

RAIS TOGO KUM'BEMBELEZA ADEBAYOR.


RAIS wa Togo, Faure Gnassingbe amepanga kukutana na nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Emmanuel Adebayor kufuatia mgomo wa mchezaji kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ili kudai posho zao kwa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-TFF. Wizara ya Michezo ilitoa taarifa hizo juzi kwamba Adebayor ambaye anacheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza alitegemewa kutua wakati wowote katika mji mkuu wan chi hiyo Lome kuzungumza na mkuu wa nchi, kitendo ambacho wachambuzi wa soka nchini humo wamesema kinaweza kubadilisha msimamo wa nyota huyo. Togo inapambana na Niger jijini Niemey leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano hiyo ya Afrika ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 19 mwaka huu nchini Afrika Kusini. Kiungo mkabaji Alaixys Romao anayecheza katika klabu ya Lorient ya Ufaransa amerejea katika kikosi cha nchi hiyo wakati golikipa chaguo la kwanza katika kikosi cha kocha Didier Six bado amekataa kujiunga na wenzake mpaka tatizo la Adebayor litakapotatuliwa. Togo itaanza kampeni zake katika michuano hiyo kwa kupambana na Ivory Coast ambao wote wanatoka magharibi mwa Afrika katika kundi D jijini Rustenburg.

BLATTER AGUSWA NA VIFO VILIVYOTOKEA NCHINI IVORY COAST.


RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter ametuma barua ya salamu rambirambi kwa Shirikisho la Soka nchini Ivory Coast na nchi nzima kwa ujumla kufuatia vifo vya watu 61 vilivyotokea katika mkesha wa mwaka mpya jijini Abidjan. Katika barua hiyo Blatter ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa hizo za kuhuzunisha za vifo hivyo ambavyo vilitokea baada ya kukanyagana wakati watu wakikimbia kuangalia mafataki kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya 2013. Amesema kwa niaba ya FIFA nay eye mwenyewe anapenda kutuma salamu zake za rambirambi kwa shirikisho hilo, familia za wahanga wa tukio hilo pamoja na watu wote wa Ivory Coast. Wahanga wengi katika tukio hilo walikuwa ni watu wenye umri kati ya miaka 8 mpaka 18 ambapo rais wan chi hiyo alitangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Jumatano iliyopita.

YANGA KUCHEZA MECHI YA KWANZA ULAYA LEO


Yanga wakiwa Antalya
KLABU ya Yanga ya Dar es Salaam, leo inashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na Arminia Bielefeld ya Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya, Uturuki.
Yanga ambayo imeweka kambi ya mafunzo mjini Antalya, itatumia mchezo huo kama fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani ambayo pia imekuja kuweka kambi ya mafunzo kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Pili Ujerumani.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo ina wachezaji wa kiwango cha kimataifa, hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
“Unajua tuna siku sita tangu tufike hapa (Antalya Uturuki) na tumeshafanya mazoezi kwa siku nne, hivyo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu,” alisema Brandts.
Arminia Bielefeld  imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na timu ya Yanga ambao ni mabingwa mara 23 Tanzania Bara.
Yanga imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna majeruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.

AZAM NA MIEMBENI ILIYOIPIGA MTIBWA NNE MAPINDUZI LEO, COASTAL NA WAKATA MIWA WA MANUNGU LEO


Kikosi cha Azam
MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuendelea leo visiwani hapa kwa mechi mbili za Kundi B kupigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Mtibwa Sugar kutoka Morogoro wataanza kushuka dimbani kumenyana na Coastal Union ya Tanga saa 10:30 jioni kwenye Uwanja huo, kabla ya mabingwa watetezi, Azam kumenyana na Miembeni SC saa 2:30 usiku.
Mechi zote zinatarajiwa kuwa kali na za kusisimua, kutokana na matokeo ya awali ya timu zote.
Mtibwa walifungwa 4-1 na Miembeni katika mchezo wa kwanza na ili kufufua matumaini ya kubaki katika michuano hii watatakiwa kushinda leo. Coastal walilazimishwa sare ya bila kufungana na Azam FC katika mchezo wa kwanza, hivyo nao watahitaji ushindi kuweka hai matumaini ya kuendelea na Kombe la Mapinduzi.
Azam na Miembeni, hiyo ni mechi inayotarajiwa kuteka hisia za wengi zaidi leo visiwani hapa, kwani timu zote ziko madhubuti.
Miembeni imeimarishwa upya kwa usajili kamambe chini ya kocha Salim Bausi, aliyeiwezesha Zanzibar kushika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Challenge mjini Kampala, Uganda mwezi uliopita wakati Azam pamoja na kuwa mabingwa watetezi wa Kombe hilo, ndiyo yenye kuvutia hisia za wengi Bara baada ya Simba na Yanga.
Kikosi cha Coastal

JAMBO MOJA TU LAMKERA MFARANSA SIMBA SC, KUTAKA MABAO RAHISI


Liewig akiwa na wasaidizi wake katika mchezo wa jana wakijadiliana kabla ya mechi
KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig amekubali yote kutokana na mechi ya timu yake jana dhidi ya Tusker ya Kenya, lakini amekerwa na jambo moja tu, timu yake kutaka kufunga mabao mepesi.
Akizungumza  baada ya mechi ya jana, Liewig alisema timu inabadilika taratibu na anaamini watafanikiwa kuwa na timu bora, lakini jambo moja tu amesema wachezaji wake lazima wabadilike haraka wanapofika kwenye eneo la hatari la wapinzani kwa kuonyesha uchu.
“Wanapofika kwenye eneo la hatari la wapinzani, wanakuwa wanataka kufunga bao la rahisi sana, hapana, wakati mwingine lazima ujifunze kufunga bao katika mazingira magumu. Hili lazima tulifanyie kazi haraka na wachezaji wabadilike,”alisema Liewig.
Simba SC jana ilitoka sare ya kufunga bao 1-1  na Tusker ya Kenya katika mchezo wa Kundi A, Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Kwa matokeo hayo, Tusker inaendelea kuongoza Kundi A, kwa piointi zake tatu sawa na Simba, lakini mabingwa hao wa Kenya wana wastani mzuri zaidi wa mabao.
Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimekwishafungana bao 1-1, Simba wakitangulia kupata bao dakika ya 18 mfungaji Haruna Moshi Shaaban, maarufu kama Boban au Balotelli wa Bongo kabla ya Tusker kusawazisha dakika ya 39, mfungaji Khalid Aucho.
Boban alifunga bao tamu sana kwa ufundi wa hali juu akiwa amedhibitiwa na beki ngongoti wa Tusker, Joseph Shikokoti na kuirukia pasi ya Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kuitumbukiza nyavuni.
Baada ya kufunga bao hilo, Boban aliangukia mkono na kuumia, hivyo hakushangilia bao lake na moja kwa moja alianza kutibiwa na Daktari Cossmas Kapinga wa Simba.
Baada ya bao hilo, Simba iliongeza mashambulizi langoni mwa Tusker na Boban alikaribia kufunga tena dakika ya 30 kama si shuti lake kutoka nje sentimita chache.
Aucho alifunga bao lake akiunganisha krosi ya Jeremiah Bright kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
Baada ya hapo, timu zilianza kushambuliana kwa zamu hadi refa Ramadhani Kibo alipopuliza kipyenga cha kuhitimisha ngwe ya kwanza.
Kipindi cha pili timu zote zilirudi vizuri na kucheza kwa umakini wa hali ya juu, jambo ambalo lilisababisha dakika 90 zimalizike zikiwa zimefungana 1-1.
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba kilikuwa; William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Shomary Kapombe, Komabil Keita, Jonas Mkude, Haroun Athumani/MKussa Mudde75, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Haruna Moshi na Ramadhan Chombo ‘Redondo’/Edward Christopher dk 52.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright/Humphrey Okoth, Mark Odhiambo, Joseph Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono/Benson Amanda, Justin Monda, Ismail Dunga/Michael Olunga, Jesse Were na Robert Omonuk.
Katika mchezo uliotangulia, Jamhuri ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Bandari kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung. Mabao ya Jamhuri yalifungwa na Fahad Abdallah Athumani dakika ya 25 na Ally Bilal dakika ya 67, wakati la Bandari lilifungwa na Faudhi Ally dakika ya tano.

MONJA 'ANELKA' AMALIZIA SOKA YAKE KISIWANI


Monja 'Anelka'
MSHAMBULIAJI wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Monja Privas Liseki amejiunga na Miembeni ya Daraja la Kwanza Zanzibar kwa mkataba wa miaka miwili.
Monja yupo kwenye kikosi cha Miembeni FC kinachoshiriki Kombe la Mapinduzi visiwani hapa, ambayo leo usiku itamenyana na Azam FC, ikitoka kuifunga 4-1 Mtibwa Sugar katika mchezo wake wa kwanza wa Kundi B.
“Nipo hapa Miembeni, nadhani nitastaafu nikiwa na timu hii. Huku nimekuja kumalizia soka yangu nafikiri,”alisema Monja leo .
Monja alizaliwa Agosti 8, mwaka 1975, Kinondoni Muslim mjini Dar es Salaam na alipata elimu yake pekee, ya Msingi katika shule ya Muhimbili, Upanga mjini Dar es Salaam. “Mimi nilikuwa napenda sana soka, nilipomaliza shule ya Msingi tu, nikaachana na shule kabisa nikaanza mitikasi ya soka hadi nikasajiliwa Sigara mwaka 1991 nikiwa bado mdogo sana nina miaka 16 tu,”alisema Monja.
Alicheza Sigara hadi mwaka 1996 iliposhushwa daraja, akahamia Simba SC ambako alidumu hadi mwaka 1998 alipotolewa kwa mkopo Yanga ili aichezee kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hata hivyo, Monja anasema baada ya kwisha kwa Ligi ya Mabingwa, Yanga walitaka kumsajili moja kwa moja, ila yeye akakataa na kwenda kujiunga na Mtibwa Sugar ambayo aliichezea hadi mwaka jana alipotua Miembeni.
“Nikiwa Mtibwa nilikuwa nikitoka mara moja moja kwenda kubadilisha upepo kwa kucheza Uarabuni na kurudi Mtibwa, kwa mfano mwaka juzi nilitolewa kwa mkopo niende kuisaidia Ocean View ya Zanzibar, niliichezea hadi ikachukua ubingwa wa Zanzibar,”alisema.  
Mbali na kujivunia kuwa mchezaji mkongwe zaidi katika soka ya Tanzania, lakini pia Monja anajivunia kucheza timu ya taifa, kucheza klabu kubwa Simba na Yanga na pia kucheza soka ya kulipwa Uarabuni.
Katika hayo amecheza michuano mikubwa kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Washindi, Kombe la CAF, Kombe la Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia katika hatua za awali za kuwania tiketi ya kushiriki fainali za michuano hiyo.
“Mimi ndiye mchezaji wa kwanza wa Tanzania kufunga bao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, kama utakumbuka Yanga ndio klabu ya kwanza ya Tanzania kucheza michuano hii. Sasa mimi nikiwa na Yanga mwaka 1998, wakati huo naitwa Andy Cole kwa jina la utani, niliifungia Yanga bao katika mechi na Manning Rangers ya Afriika Kusini huu Uwanja ambao siku hizi mnauita Uhuru, wakati huo unaitwa Taifa. Hiyo mechi tulitoka 1-1. Nikarudia kufunga tena kwenye mechi na hao jamaa jamaa kwao, siku wakitufunga 4-1,”alisema.
Monja alisema kwa sasa anataka aitwe Nicolas Anelka wa Tanzania kwa sababu huyo ndiye mchezaji mkongwe ambaye anaendelea kucheza soka ya ushindani.
WASIFU WAKE:
JINA: Monja Privas Liseki
KUZALIWA: Agosti 8, 1975
ALIKOZALIWA: Kinondoni
KLABU YA SASA: Miembeni FC
KUJIUNGA: 2012
KLABU ZA AWALI:
Mwaka          Klabu
1991- 1995   Sigara FC
1996- 1998   Simba SC
1998- 1999   Yanga SC
1999-2012    Mtibwa Sugar