Saturday, January 12, 2013

LIGI ULAYA: SERIE A & LA LIGA WIKIENDI!


JUVENTUS-Claudio_Marchisio>>REAL, BARCA ZOTE UGENINI!
>>MABINGWA JUVE UGENINI na PARMA!!
LIGI za Nchini Spain na Italy zinaendelea Wikiendi hii na huko Spain kwenye La Liga, Mabingwa watetezi, Real Madrid, ambao wako Pointi 16 nyuma ya Vinara Barcelona, Jumamosi watakuwa ugenini kucheza na Osasuna wakati Barca watacheza ugenini na Malaga Siku ya Jumapili wakati huko Italy, Mabingwa watetezi ambao pia ni vinara, Juventus, watacheza ugenini Siku ya Jumapili na Parma.
ZIFUATAZO NI RATIBA ZA WIKIENDI:
RATIBA:
LA LIGA
Jumamosi Januari 12
Real Valladolid v Real Mallorca
RCD Espanyol v Celta de Vigo
Osasuna v Real Madrid CF
Valencia v Sevilla FC
Jumapili Januari 13
Real Betis v Levante
Real Sociedad v Deportivo La Coruna
Atletico de Madrid v Real Zaragoza
Malaga CF v FC Barcelona
Jumatatu Januari 14
Getafe CF v Granada CF
SERIE A
Jumamosi Januari 12
Bologna v Chievo Verona
Inter Milan v Pescara
Jumapili Januari 13
Torino FC v Siena
SS Lazio v Atalanta
Parma v Juventus
Udinese v Fiorentina
Napoli v Palermo
Cagliari v Genoa
Catania v AS Roma
Sampdoria v AC Milan

AFCON 2013: WIKI MOJA IMEBAKI!!


AFCON_2013_LOGOIKIWA imebaki Wiki moja tu kwa Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, kuanza huko Afrika Kusini kwa Mechi ya ufunguzi ya Kundi A kati ya Wenyeji Afrika Kusini na Cape Verde itayochezwa Januari 19 huko Johannesburg, Kamati ya Maandalizi imesema Mauzo ya Tiketi imefikia 320,000 kati ya Tiketi 500,000 zilizotolewa kuuzwa.
Kamati ya Maandalizi imesema kudorora kwa Mauzo ya Tiketi hizo kunatokana na upungufu katika mikakati ya mauzo.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Wakati huo huo, Marefa 18 na Marefa Wasaidizi 21 ndio wameteuliwa kuchezesha Mechi za AFCON 2013 na kati yao Marefa wawili na Wasaidizi 8 ndio wapya kutoka wale waliochezesha AFCON 2012 huko Equatorial Guinea na Gabon Mwezi Januari 2012.
Huku Nigeria ikiwa haikutoa hata Mwamuzi mmoja, Marefa wapya ni Sylvester Kirwa wa Kenya na kutoka Seychelles  ni Bernard Camille na Wenyeji Afrika Kusini wametoa Marefa wawili, Daniel Bennett na Zakhele Siwela.
Algeria na Senegal ndio zenye Waamuzi wengi huku kila mmoja ikitoa Marefa watatu.
Marefa hao wanatarajiwa kujumuika Januari 15 Mjini Johannesburg kwa kufanyiwa Vipimo na Majaribio ya mwisho.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFCON 2013==AFRIKA KUSINI
VIWANJA:
-Soccer City, Johannesburg [Mashabiki 94,700]
-Moses Mabhida Stadium, Durban [Mashabiki 54,000]
-Nelson Mandela Bay Stadium, Port Elizabeth [Mashabiki 48,000]
-Mbombela Stadium, Nelspruit [Mashabiki 41,000]
-Royal Bafokeng Stadium, Rustenburg [Mashabiki 42,000]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi Januari 19
South Africa v Cape Verde Islands [Soccer City Saa 1 Usiku]
Angola v Morocco [Soccer City Saa 4 Usiku]

WENGER BADO ALIA NA RVP, COLOCCINI AIPIGA CHINI NEWCASTLE!!

>>TEVEZ-CITY YATAFAKARI MKATABA MPYA!!
Wenger aumia na RVP
WENGER_AHIMIZA12Arsene Wenger amekiri kuwa inamsononesha sana kumwona Nyota wake wa zamani wa Arsenal Robin van Persie akiipaisha Manchester United kuelekea kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England.
Man United walimsaini Robin van Persie Mwezi Agosti 2012 kutoka Arsenal kwa Dau la Pauni Milioni 24 na Magoli yake 20  yameisaidia Man United kuwa kileleni mwa BPL, Barclays Premier League, wakiwa Pointi 7 mbele ya Timu ya Pili Man City na Pointi 18 mbele ya Arsenal na hilo limemfanya Wenger akubali Mchezaji huyo ndie atakaepeleka Ubingwa Old Trafford.
Amesema: “Inaumiza sana kuiona Manchester United wako mbali mbele yetu. Unajua ukiwauzia Robin van Persie Manchester United basi wataongoza Ligi.”
Wenger aliongeza: “Robin ni mmoja wa Mastraika Bora Duniani na inajulikana atawafungia Magoli. Yupo kwenye kilele cha Gemu yake! ”
Coloccini
Nahodha wa Newcastle United Fabricio Coloccini ameiambia Klabu hiyo kuwa anataka kuhama Mwezi huu Januari kwa sababu binafsi.
Coloccini, Miaka 30, ambae anatoka Cordoba, Argentina, alisainiwa na Newcastle Mwaka 2008 na kwa Dau la Pauni Milioni 10.3.
Kwenye Dirisha la Uhamisho la Januari, Newcastle tayari ishamuuza Straika wao Demba Ba kwa Chelsea.
Tevez
Manchester City inatafakari uwezekano wa kumuongezea Mkataba Mchezaji wao Carlos Tevez ili kumzuia asiondoke bure bila malipo Mkataba wake wa sasa utakapomalizika Miezi 18 ijayo.
Tevez, ambae alisaini Mkataba wa Miaka mitano na Man City Mwaka 2009, hajaamua chochote kuhusu hatima yake lakini inaaminika anataka kurudi kwao Argentina kuichezea Boca Juniors, Klabu ambayo alianza kucheza Soka.
Akiongelea kuhusu Tevez, Mancini alisema: “Sijui Carlos anafikiria nini. Bado tuna Miezi 18 na muda upo wa kuongea nae.”
+++++++++++++++++++++++
BPL, BARCLAYS PREMIER LEAGUE
RATIBA:
Jumamosi 12 Januari 2013
[SAA 12 Jioni]
Aston Villa v Southampton
Everton v Swansea
Fulham v Wigan
Norwich v Newcastle
Reading v West Brom
Stoke v Chelsea
Sunderland v West Ham
Jumapili 13 Januari 2013
[SAA 10 na Nusu Jioni]
Man United v Liverpool
[SAA 1 Usiku]
Arsenal v Man City
Jumatatu 14 Januari 2013
[SAA 5 Usiku]
QPR v Tottenham

MOROCCO YAMTAKA TAARABT KUOMBA RADHI.


SHIRIKISHO la Soka nchini Morocco limemtaka kiungo wa kimataifa wa nchi hiyo Adel Taarabt kuomba radhi kufuatia kumkashifu kocha wa timu ya taifa Rachid Taoussi ambaye alimuacha katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon. Kiungo huyo anayecheza katika klabu ya Queens Park Rangers ya Uingereza anatuhumiwa kumtumia ujumbe wa kumdhalilisha Taoussi na vyombo vya habari vya nchi hiyo kufuatia kuenguliwa katika michuano hiyo inayotarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini. Katika taarifa yake iliyotolewa katika vyombo vya habari, shirikisho linamtaka mchezaji huyo kuomba radhi kwa maandishi kufuatia maneno yake ya kashfa aliyotoa. Taoussi alimuacha Taarabt mwezi uliopita akidai kuwa nyota huyo alikataa kuonana naye wakati akifanya ziara barani Ulaya Octoba mwaka jana kwa ajili ya kuangalia wachezaji atakaowatumia katika Afcon.

WAHABESHI ETHIO[PIA WAIHENYESHA STARS 2-1 ADIS ABABA

TAIFA_STARS-FRAMEDTanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia uliochezwa leo (Ijumaa Januari 11, 2013) kwenye Uwanja wa Addis Ababa hapa jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki mmoja wa Ethiopia.
Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.
Taifa Stars inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.
Boniface Wambura

KAMATI TENDAJI YA MPIRA WA MIGUU MKOA WA TABORA TAREFA YAKUTANA KWA MARA YA KWANZA TOKA ICHAGULIWE DEC 22 MWAKA JANA KATIKA UKUMBI WA FRANKMAN



Kamati tendajiya uongozi wa mpira wa miguu mkoa wa tabora TAREFA  leo imekutana kwa mara ya kwanza toka ichaguliwe tarehe 22 dec.2012 mwaka jana kujadili mambo mbali mbali ya soka la mkoa wa tabora kubwa zaidi ajenda zilizojadiliwa  ni pamoja na maandalizi ya timu za daraja la kwanza kuweza kupandisha timu mojawapo ya daraja la kwanza ipande ligi kuu tanzania bara kati ya timu hizo mbili za mkoani tabora Rhino Rangers ama Polisi Tabora.

Ajenda ya pili ni pamoja na kuandaa ligi za wilaya pamoja na mkoa wa tabora ili kupata timu ambazo zitakuwa na makali ya kurudisha taswira ya soka la mkoa wa tabora ni pamoja na kupata timu 2 ambazo zitapatikana wilayani kote za tabora wilaya ya uyui ,skonge,urambo,nzega,igunga na tabora mjini kila wilaya ipate timu 2 na mkoa timu moja.

Ajenda ya tatu ni pamoja na makabidhano ya  nyaraka za TAREFA ikiwemo na vifaa vya ofisi,kwani mpaka sasa ivi katibu wa zamani wa TAREFA bw. Albert Sitta hataki kukabidhisha nyaraka hizo kw auongozi mpya uliochaguliwa tarehe 22 dec.2012 chini ya uenyekiti wa Yussuph Kitumbo.

Ajenda nyingine ni pamoja na kujaza nafasi zilizowazi katika uongozi kama nafasi ya katibu msaidizi  kwani mwenyekiti aliridhia kumjaza katibu mkuu wa TUFA bw.Juma Mapunda kuwa kaimu katibu msaidizi na kamjaza bi Janethi Michael kuwa kaimu  mweka hazina wa TAREFA.

Ajenda nyingine iliyojadiliwa ni pamoja na maendeleo ya soka mawilayani mkoani tabora wamehakikisha kuwa soka la wilayani liwe na taswira ya kisoka siyo kama ilivyopotea kutokana na uongozi uliopita chini ya uenyekiti wa Ismail Aden Ragge pamoja na katibu mkuu wake Albert Sitta kuwa hawana organization nzuri juu ya uongozi wao pamoja na ajenda nyingine mengineyo kama kuandaa vitega uchumi,kuandaa ligi mbalimbali,kuandaa kozi za waamuzi,marefarii pamoja na kozi za makocha..