Friday, November 16, 2012

Goli zuri la mwaka ambalo lilifunwa?????????????????????


 

WACHIMBA ALMASI WA SHINYANGA TIMU YA MWADUI FC WAISHINDILIA KIKAPU CHA MAGOLI TIMU YA  WAPIGA KWATA YA POLISI DODOMA 4-0


Timu ya mwadui FC ya mkoani shinyanga jana  iliwacharaza  maafande wa polisi dodoma kwa mabao 4-0 mchezo uliochezwa katika dimba la kambarage shinyanga mchezo wa kiporo ambao ungechezwa juzi lakini ukaahirishwa kutokana na timu ya taifa ya tanzania taifa stars kuwa na mchezo wa kirafiki ulioko katika kalenda ya FIFA .

Mabao ya timu ya mwadui fc yalifungwa na CHIKA CHUKU aliyefunga 2,la tatu likifungwa na MWANDENGE SADICK na bao la nne lilifungwa na EYE SALIM na kuhitimisha idadi ya mabao 4-0 dhidi ya wapiga kwata wa polisi dodoma .

Nao maafande wa polisi tabora walishindwa kutamba mbele ya watoto wa mjini timu ya pamba katika dimba la CCM KIRUMBA mwanza baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 na kuhitimisha raundi ya kwanza wakiwa wanashika nafasi ya saba na pointi zao 3 baada ya kucheza michezo saba.

Na kule katika dimba la lake tanganyika kigoma timu ya wnajeshi la wananchi JKT kanembwa waliibamiza timu ya maafande wa polisi mara bao 1-0 na kuhitimisha raundi ya kwanza ya ligi daraja la kwanza katika KUNDI C

Na juzi  Timu ya maafande wa jeshi la wananchi  ya mkoani tabora  RHINO RANGERS jana waliendelea  kuwapa raha wakazi wa tabora baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya moran fc ya kiteto manyara kule.

Mabao ya rhino rangers hiyo jana yalifungwa  na SHIJA MONGO na ABDALAH SIMBA mshambuliaji ambaye ananguvu ,kasi,mashuti na mtaalaamu wa kumiliki mpira .
  MSIMAMO KUNDI C
1.RHINO RANGERS MECHI 7 POINTI 17
2.KANEMBWA JKT MECHI 7 POINTI 16
3.MWADUI FC MECHI7 POINTI 13
 4.PAMBA MECHI 7 POINTI 11
5.POLISI DODOMA MECHI 7 POINTI 8
6.POLISI MARA MECHI 7 POINTI 5
7.POLISI TABORA MECHI 7 POINTI 3
8.MORAN FC MECHI 7 POINTI 2

FAHAMU;Kila kundi litatoa timu moja ambayo itapanda ligi kuu ya vodacom tanzania bara VPL msimu ujao na tayari timu ya maafande ya polisi moro imeonyeshwa mlango wa kutokea kwani imemaliza mzunguko wa kwanza wa  VPL ikiwa imecheza mechi 13 na ina pointi 4 inashika mkia.timu zitakazo panda ni kutoka kundi A,B,na C

 MATOKEO TOKA LIGI IANZE oktoba 24
===Kanembwa vspolisi dodoma 3-0
===pamba vs polisi mara 3-2
===rhino rangers vs polisi tabora 2-1
===mwadui vs moran 3-0

oktoba 27
====polisi tabora vs polisi dodoma 0-1
====mwadui vs polisi mara 3-0
====kanembwa JKT vs moran 2-0
====pamba vs rhino rangers 1-1

oktoba 31
====polisi mara vs rhino rangers 0-0
====moran vs polisi tabora 1-1
====polisi dodoma vs pamba2-0
====kanembwa vs mwadui 3-2

novemba 4
===polisi mara vs polisi tabora 1-1
===moran vs polisi dodoma1-1
===rhino rangers vs kanembwa JKT 3-1
===mwadui vs pamba...2-0......

novemba 7
====polisi tabora vs kanembwa  JKT 1-4
====polisi dodoma vs polisi mara 0-0
====pamba vs moran ya manyara 2-0
novemba 8
====rhino rangers vs mwadui FC 2-0

novemba 11
====kanembwa vs pamba 0-0
====polisi tabora vs mwadui 0-0
====polisi dodoma vs rhino rangers 0-2
====polisi mara vs moran 3-1

  Novemba 14

===rhino rangers vs moran fc 2-1

novemba 15

===JKT kanembwa vs polisi mara 1-0

===mwadui fc vs polisi dodoma 4-0

===pamba vs polisi tabora 2-1

 

SMALL KIDS YAJISHUSHA DARAJA YENYEWE NI BAADA YA KUKACHA MICHEZO MIWILI YA LIGI DARAJA LA KWANZA

 

TIMU ya Small Kids ya Rukwa inayoshiriki daraja la kwanza  imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja baada ya kushindwa kufika kwenye viwanja kwa michezo miwili.

Small kids ambayo ilikuwa kama msindikizaji kutokana na kufungwa michezo yote ni sawa na imejishusha kwani haikufika kwenye mchezo mjini Mafinga dhidi ya Kurugenzi na juzi nyumbani kwao Rukwa dhidi ya Polisi Iringa.

Kulingana na kanuni za ligi ya Tanzania, timu isipofika uwanjani itakuwa imejishusha daraja yenyewe ikifuatiwa na kupigwa faini na kufutwa kwa pointi zote za michezo ambayo ilikuwa imecheza.

Wachezaji wa Small Kids ambao ni wenyeji wa Dar es Salaam walirejea jijini baada ya mchezo wao na Burkina Faso uliochezwa mjini Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri ambapo pia walifungwa bao 2-0.

Wenyeji wa Rukwa wamesikitishwa na kitendo cha mmiliki wa Small kids kushindwa kusimamia timu na kusambaratika kabla ya ligi hata kuamaliza mzunguko wa kwanza.

MBEYA CITY, KANEMBWA ZAMALIZA MZUNGUKO VEMA


TIMU ya Mbeya City jana ilimaliza mzunguko wa kwanza vema kwa kuifunga Majimaji bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya

Bao la Mbeya City lilifungwa na Deus Kaseke dakika ya 10 na lilidumu hadi dakika 90 ya mchezo.

Michezo mingine kwenye kundi A ilikuwa ni kati ya Mlale na Burkina Faso ambao walitoka sare ya 2-2 kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea na kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Mkamba walifungwa bao 1-0 na Kurugenzi ya Mafinga.

Kundi C ambalo limemaliza mzunguko wa kwanza lilikuwa na michezo minne kwenye viwanja vinne tofauti.

Kwenye uwanja CCM Kirumba, jijini Mwanza Pamba waliutumia vema uwanja wa nyumbani baada ya kuifunga Polisi Tabora mabao 2-1.

Uwanja wa Lake Tanganyika Kanembwa FC waliwachezesha kwata Polisi Mara kwa kuifunga bao 1-0 na Rhino ya Tabora ikaifunga Moran ya Kiteto nyumbani mabao 2-1.

Mkoani Shinyanga kwenye uwanja wa Kambarage wenyeji Mwadui waliifunga Polisi Dodoma mabao 4-0.

Kundi A na kundi c wamemaliza mzunguko wa kwanza juzi na kuacha kundi B likiendelea hadi Novemba 22, mwaka kutokana na michezo yao kusogezwa mbele kutokana na uhaba wa viwanja.

 

NKONGO, JESE NA ALI KUCHEZESHA CECAFA

MWAMUZI wa Kimataifa wa Tanzania Israel Mujuni Nkongo ameteuliwa kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha mashindano ya CECAFA maarufu kama Tusker Challenge yatakayofanyika nchini Uganda kuanzia Novemba 26 hadi Desemba 6 mwaka huu.

Nkongo ambaye ataambatana na waamuzi wasaidizi wawili wa kimataifa,Jese Erasmo toka Morogoro na Kinduli Ali toka Zanzibar.


Waamuzi wa kati wengine watakaochezesha mashindano hayo ni Thierry Nkurunzinza toka Burundi, Maeruf Mensur toka Eritrea.

Wengine ni Antony Ogwayo toka Kenya, Hakizimana Louis toka Rwanda, Ali Kalyango toka  Uganda, Mohamed Hussein El Fadhil toka Sudan na Denis Bate wa Uganda

Waamuzi wasaidizi ni Mark Ssonko wa Uganda, Mussie Kinde wa Ethiopia, Peter Sabatia wa Kenya, Idam Mohammed wa Sudan,
Hakizimana Ambroise wa Rwanda
na Omar Abukar wa Somalia.

Makundi ya timu zitakazoshiriki mashindano haya yameshapangwa ambapo Tanzania ipo kundi B na nchi za Sudan Kaskazini, Burundi na Somalia.

Kundi A lina nchi za Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudani Kusini na Kundi C lina nchi za Rwanda, Zanzibar, Eritrea na Malawi

SHEIN RANGERS YAIFUNGA DAYSA

TIMU ya Shein Rangers inayoshiriki ligi ya vijana waliochini ya miaka 17 ya mkoa wa Dar es Salaam jana iliifunga DAYSA bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa juzi mchana kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao wachezaji walionekana wanavipaji vya soka iliwachukua Shein Rangers dakika 7 na sekunde 12 kupata bao kupitia kwa Abdul Said.

Timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Shein Ranger waliwatoa Hamza Mwalimu, Lukinga Abdul na Yassin Wito na wakaingia Athuman Mohamed, Hassan Idd na Edward Thomas.

DAYSA waliwatoa John Wiliam na Godfrey Andrea na waliingia Jimmy Michael na Steven Daniel.

Akizungumza  baada ya mchezo kumalizika Katibu mkuu wa Chama cha Kuendelea vipaji (DAYOSA), Mwinyimad Tambaza alisema kuwa ligi inaendelea vizuri na timu zinaonyesha ushindani.

"Nashukuru ligi ya YOSO inaendelea vizuri na timu zinaonyesha ushindani wa kweli", alisema Tambaza.

UONGOZI SIMBA WAMUOMBA RADHI KASEJA, KIKOSI KWENDA HOLIDAY ULAYA


KATIKA kuhakikisha  ari ya wachezaji inarudi kama ilivyokuwa mwanzo, uongozi wa klabu ya Simba una mpango wa kuipeleka timu nje ya nchi ili kuwapa muda wachezaji wa kusahau yaliyopita na kujipanga vema kwa mzunguko wa pili. 
Aidha, uongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, umemuomba radhi kipa na nahodha wake, Juma Kaseja kutokana na kudhalilishwa na baadhi ya watu baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo usioridhisha katika michezo yake ya mwishoni mwa mzunguko wa kwanza. 
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema leo kwamba  kudhalilishwa kwa Kaseja si sahihi kwani anaweza kukofanya makosa ya kiufundi kama binadamu mwingine, hivyo anahitaji ushauri wa kimawazo. 
“Tuache kudhalilisha wachezaji kwani kufanya hivyo si uungwana wa michezo hata kidogo…kila mtu anafahamu kuna kushinda, kufungwa na kutoka sare, kama hatutaki kufungwa tujiondoe wenye ligi,”alisema Rage

AZAM FC, SIMBA SC WABADILISHANA WACHEZAJI




WAKATI uongozi wa klabu ya Simba ukisikitishwa na mwenendo mbaya wa timu hiyo katika mzunguko wa ligi, umejipanga kusajili wachezaji wataokaoingezea makali timu hiyo, huku pia wakitaraji kuopunguza wachezaji kadhaa.
 Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema leo kwamba,katika harakati za usajili wa usajili wa dirisha dogo wanampango wa kumrejesha beki wake wa zamani wa kimtaifa Mkenya, George Owino kutoka Azam Fc na kumpeleka huko kiungo wao, Uhuru Suleiman. 
“Tupo katika mazungumzo na uongozi wa Azam Fc ambayo yapo katika hatua nzuri na muda si mrefu tutasaini mkataba rasmi kuhusiana na hatua hiyo,”alisema

MSIGWA CUP KUANZA NOV.26


Mch.Peter Msigwa



TIMU 28 za soka kutoka sehemu mbalimbali za Iringa mjini zimethibitisha kushiriki mashindano ya Kombe la Msigwa linalotarajia kuanza Novemba 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Mratibu wa Kombe hilo, Abu Changawa Majeki alisema mashindano hayo yamegawanywa katika makundi matatu.

Alisema kundi la kwanza litacheza katika uwanja wa Ruaha, Kundi la pili litakuwa uwanja wa Mlandege na wengine watapambana uwanja wa Kihesa.

Mratibu huyo alisema mshindi wa kwanza atapata sh. mil. 1, mshindi wa pili sh.700,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa sh. 500,000.

Alizitaja timu shiriki kuwa ni Bodaboda FC, Tax FC, maselemara FC, Isakalilo FC, Galilaya FC, Mivinjeni,Itamba,Lugalo,Magereza S.C, Mawelewela FC,Kwakilosa SC,Mwandege SC, Sengo FC,Jamaika FC.

Nyingine ni Nduli FC, Usalama (Polisi) FC,Mtivila SC, Doni FC, Kigonzile FC, Ngongo SC, Mwangata SC, Ruaha Shooting SC, Uronge SC, Magari Mabovu SC, Magorofani FC,Mshindo SC, Ilala SC na Kihesa Kilolo FC.

Mratibu huyo alisema mashindano hayo yatakayodhaminiwa na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA, yatagharimu sh. mil. 18.5 kwa ajili ya kununua jezi kwa timu zote shiriki, zawadi na gharama nyingine.

SIMBA SC WATIMUA WANACHAMA, WAVUNJA KAMATI ZOTE

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage akizungumza leo


KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba imewafuta uanachama viongozi na tawi maarufu la Mpira Pesa, sambamba na kuzivunja kamati zake ndogondogo. 
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage, amesema kamati ya utendaji ya Simba iliyokutana juzi ilifikia maamuzi hayo baada ya kutokea kwa chokochoko katika siku za hivi karibuni. 
Alisema mwenyekiti wa tawi hilo, Masoud Awadh na Katibu wake Ali Bane walikiuka katiba ya Simba kwa kuongea hovyo na vyombo vya habari sambamba na kuitisha mkutano wa wanachama bila ya kupata ruhusa ya uongozi. 
Rage aliongeza kuwa Awadhi si mwanachama hai wa klabu hiyo kutokana na kutolipa ada ya uanachama kwa zaidi ya miaka miwili, huku barua yake aliyouandikia uongozi  kwa niaba ya Simba nayo ni kinyume na katiba kwani hana mamlaka ya kufanya hivyo. 
Tawi la Mpira Pesa chini ya Awadhi lilifanya kikao cha kushinikiza Rage na viongozi wenzake kuachia ngazi baada ya timu kufanya vibaya katika mechi za mwisho za mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom na kuishia nafasi ya tatu. 
Kama hiyo haitoshi, wanachama wa tawi hilo waliorodhesha majina zaidi ya 600 ili kutimiza akidi inayoruhusu kufanyika kwa mkutano wa dharula wa Simba. 
Hata hivyo, Rage alisema uongozi umebaini kuwa zaidi ya asilimia 90 ya wanachama waliojiorodhesha ni wafu, huku pia saini zilizowekwa ni za kughushi. 
Kuhusiana na kamati ndogondogo, Rage alisema uongozi umeona hazina msaada wowote kwa timu hivyo hivi karibuni ataunda kamati nyingine zitakazosaidia timu kupata ushindi.

 

 

JAMHURI KIHWELU JULIO; TUTACHEZA NA CONGO TUKIWA NA RUFAA YETU MKONONI WACHEZAJI WALIOKUJA SIO WALIOPIMWA UMRI. TANOJUMAINSPORTS YABAINI 8 NI VIJEBA.

Kikosi cha timu ya vijana ya Congo Brazzaville wakifanya mazoezi uwanja wa Karume.
Kuelekea mchezo wa jumapili baina ya timu ya soka ya vijana ya Tanzania bara Serengeti Boys dhidi ya timu ya vijana ya Congo Brazzaville utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,  kocha msaidizi wa Serengeti Boys Jamhuri Kihwelu 'Julio' amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na rufaa mkononi kutokana na kile alichokieleza kuwa wachezaji wengi wa Congo wanaonekana kama wana umri mkubwa.
Julio amesema amepata nafasi ya kuwaona wachezaji hao asubuhi ya leo wakati wakifanya mazoezi na ushahidi wa machoni unaonyesha wazi kuwa wachezaji hao wengiwao si chini ya umri wa miaka 17.
Julio amesema anaimani kuwa wachezaji waliopimwa vipimo vya umri na shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa siyo hao walikokuja nchini. 
Jana Rockersports ilikuwa ikiongea na kocha Jacob Michelsen kuhusiana na wasiwasi wa kucheza na wachezaji vijeba ambao wengine walishiriki kombe la dunia mwaka jana na kutolewa katika hatua ya 16 bora na Uruguay, kimsingi amesema hilo analiacha kwa shirikisho la soka TFF.
Sasa Rockersports imejaribu kuperuzi mtandao wa shirikisho la soka duniani fifa ambapo imebaini wachezaji ambao ni zaidi ya umri wa miaka 17. 

Katika kikosi kilichoshiriki kombe la dunia kwa vijana nchini Mexico kuna wachezaji 8ambao wana umri zaidi ya miaka 17 ambao wamezaliwa si zaidi mwezi oktoba mwaka 1994 ambao kimsingi wamezidi umri wa miaka 17 ambao ni hao wafuatao
1        Chill NGAKOSSO                   26/07/1994         GK          191
  2             Stevy SAMBA                     03/06/1994         DF           177
  3              Melvan LEKANDZA           02/04/1994         DF           186
4              Ange SITOU                        24/05/1994         MF         176
 5              Elvia IPAMY                        27/09/1994         FW         175
6            Gildas MPASSI                     10/01/1994           FW         175
 7             Gloire MAYANITH               13/10/1994         DF           181
8             Christ NKOUNKOU            27/07/1994         FW         180

Kikosi cha Congo Brazzaville kilicho shiriki kombe la dunia mwaka jana hiki hapa 

Nr.NameDate of BirthPositionHeight
1Chill NGAKOSSO26/07/1994GK191
2Cisse BASSOUMBA13/05/1996DF183
3Stevy SAMBA03/06/1994DF177
4Charvely MABIALA31/03/1996MF179
5Melvan LEKANDZA02/04/1994DF186
6Tierry KOUYIKOU17/01/1995MF177
7Ange SITOU24/05/1994MF176
8Hardy BINGUILA17/07/1996MF178
9Elvia IPAMY27/09/1994FW175
10Justalain KOUNKOU02/08/1996FW169
11Ramaric ETOU25/01/1995DF173
12Gildas MPASSI10/01/1994FW175
13Gloire MAYANITH13/10/1994DF181
14Christ NKOUNKOU27/07/1994FW180
17Bel EPAKO17/04/1995FW173
18Kader BIDIMBOU20/02/1996FW176
19Amour LOUSSOUKOU05/12/1996MF178
20Mavis TCHIBOTA07/05/1996FW177
21Pavelh NDZILA12/01/1995GK185

JOSEPH OWINO NJIANI KURUDI NYUMBANI MSIMBAZI

Zoezi la klabu bingwa ya Tanzania bara Simba kupata mbadala wa beki wake aliyetimkia Yanga, Kelvin Yondani linaendelea, baada ya Lino Musombo kutemwa na kusajiliwa kwa Keita na Ocheing ambao wameonekana kuhangaika kuziba pengo la Yondani, sasa klabu hiyo ya Simba inasemekana wapo katika harakati za kumrudisha moja wa mabeki wao bora katika kipindi cha miaka 10 iliyopita mganda Joseph Owino.

Simba ambao walianza ligi vizuri na kuongoza ligi kwa muda mrefu kabla ya kupoteza muelekeo mwishoni mwa mwa raundi ya kwanza ya msimu wa VPL. Sasa katika kujaribu kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo imeonekana kuyumba sana msimu huu, uongozi wa Simba umeona bora ufanye mpango wa kumrudisha kundini Owino ambaye amesajiliwa Azam lakini amekuwa akikosa namba ya kudumu baada ya kurudi kutoka kwenye majeruhi yaliyomuweka nje kwa muda mrefu.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Simba tayari wapo kwenye mazungumzo na Azam ili kuweza kuona uwezekano wa kumsaini Owino.

Owino ambaye aliondoka Simba baada ya kupata majeraha ya goti ambayo yalimuweka nje kwa muda mrefu, na Azam wakamsajili akiwa mgonjwa wakamtibu lakini baada ya kupona amekuwa na urafiki mzuri na benchi la Chamazi.

 

NSA KWENDA INDIA JUMATATU BAADA YA KUFUNGUA HOGO

Mshambuliaji wa Coastal Union ya Tanga, Nsa Job Mahenya (Jumatatu) ataondoka Jumatatu nchini kwenda India kwa matibabu zaidi ya goti. Mkurugenzi wa Ufundi wa Coastal, Nassor Bin Slum amesema Nsa amefungua plasta gumu (PoP) leo na sasa anajiandaa kwa safari hiyo ya India, kwa matibabu zaidi. Nsa aliumia goti hilo Oktoba 28, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

PETER MANYIKA, MTOTO WA NYOKA ANAYETARAJIWA KUIBEBA TANZANIA LANGONI JUMAPILI TAIFA

Huyu anaitwa Peter Manyika Peter, ni kipa namba wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, ambaye anatarajiwa kudaka keshokutwa katika mechi dhidi ya Kongo Brazzaville, kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco. Ni mtoto wa kipa wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Manyika Peter aliyewika klabu ya Yanga, ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa Serengeti Boys. Dogo anadaka vizuri sana na bila shaka ataibeba Tanzania katika mtihani huu. anayetaka kuthibitisha uwezo wake, asikose Jumapili Taifa.





Baba wa Peter Manyika, Manyika Peter 

AZAM FC WAMTAKA UHURU ROBINHO WA MSIMBAZI

KIIZA AONDOKA LEO YANGA

Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Friday Kiiza 'Diego' (pchani), anatarajiwa kuondoka leo saa 11:00 jioni mjini Dar es Salaam kwenda Kampala, Uganda kujiunga na timu yake ya taifa, The Cranes kwa ajili ya kambi ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, Tusker Challenge itakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu hadi mwanzoni mwa mwezi ujao mjini Kampala. Kiiza aliyewezesha Yanga kuongoza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacoim Tanzania Bara, anaondoka akiwa katika kiwango kizuri kwenda kuisaidia Uganda kutetea taji lake ililotwaa mwaka jana Dar es Salaam wakiifunga Rwanda katika fainali.

MICHELSEN AHOFIA WAKONGO KULETA VIJEBA

Michelsen wa tatu kutoka kulia waliosimama akizungumza na wachezaji wa Serengeti. Kulia kwake ni wasaidizi wake, Jamhuri KIhwelo na Manyika Peter, wakati kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Serengeti, Kassim Dewji, Katibu wa Kamati, Henry Tandau, Suleiman na Nyambui na Katibu wa TFF, Angetile Osiah.

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Mdenmark Jacob Michelsen amesema kwamba kuelekea mechi ya keshokutwa ana wasiwasi wapinzani wake, Kongo Brazzaville wana wachezaji waliozidi umri.
Akizungumza  jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mazoezi ya jioni, Michelsen alisema kwamba ameichunguza vizuri Kongo na sasa anaifahahamu vema.
Serengeti itamenyana na Kongo keshokutwa Uwanja wa Taifa, katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Tatu na ya mwisho ya kuwania kucheza Fainali za Vijana Afrika zitakazofanyika nchini Morocco mwakani.
Michelsen alisema kwamba alikwenda kushuhudia mchezo wa kwanza wa raundi iliyopita, baina ya Kongo na Zimbabwe waliotolewa na wapinzani wao hao na kujionea makali ya wapinzani wao.
Pamoja na kukiri kwamba Kongo ni timu bora na ilicheza Fainali zilizopita za Kombe la Dunia nchini Mexico mwaka jana na kutolewa raundi ya pili, Michelsen alisema bado ana wasiwasi timu hiyo ina ‘vijeba’.
“Nilipokwenda kuwaangalia wakicheza na Zimbabwe, nilikuta kikosini mwao kuna wachezaji sita wa kikosi kilichokwenda Mexico kwenye Kombe la Dunia, inanitia shaka kwa sababu hakuna mchezaji anayeweza kucheza michuano mikubwa kama ile akiwa ana umri wa miaka 15.
Mimi ni kocha wa vijana na ninajua, haiwezekani. Ucheze fainali za Kombe la Dunia za U17 una miaka 15, hakuna,”alisema Michelsen, ambaye aliwataja baadhi ya wachezaji anaowatilia shaka wamezidi umri ni Hady Binguila na Charvely Mabiat.
Pamoja na hayo, Michelsen amesema ana matumaini ya kuwatoa Kongo kutokana na maandalizi yao ya muda mrefu na pia sapoti anayoipata kutoka kwa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kamati maalum iliyoundwa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.
Amesema wamecheza mechi za kujipima nguvu 15 zikiwemo dhidi ya timu za Ligi Kuu na hawajafungwa hata moja, kitu ambacho anaamini ni kipimo cha ubora wa timu yake.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Serengeti Ishinde, Kassim Dewji alisema kwamba wanapambana kwa uwezo wao wote kuhakikisha timu hiyo inakwenda kwenye fainali za Morocco, mwakani.
Dewji aliwataka wachezaji wa timu hiyo kucheza kwa nidhamu, kujituma na kufuata maelekezo ya makocha wao, ili wapate ushindi katika mchezo wa Jumapili.
Serengeti imefanikiwa kufuzu hadi Raundi ya Tatu bila jasho, baada ya wapinzani wake wa awali katika Raundi ya Kwanza na ya Pili, Kenya na Misri kujitoa. Iwapo timu hii itafuzu, hii itakuwa mara ya pili kwa Serengeti kukata tiketi ya kucheza fainali hizo, baada ya mwaka 2005.
Hata hivyo, pamoja na kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe, Serengeti haikwenda Gambia mwaka huo kutokana na kuondolewa kwenye michuano hiyo na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya kubainika walitumia kijana aliyezidi umri, Nurdin Bakari.

 

PELE ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI.

MWANASOKA nguli wa zamani wa Brazil, Pele amewashukuru mashabiki wake ambao walionyesha kuguswa na kuugua kwake baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali jana. Pele mwenye umri wa miaka 72 alifanyiwa upasuaji wa nyonga katika hospitali ya Albert Einstein iliyopo jijini Sao Paulo na kuruhusiwa nyumbani baada ya matibabu kumalika kwa mafanikio. Mara baada ya kuruhisiwa kutoka hospitali Pele alitumia muda huo kuwashukuru mashabiki wake kwa kuonyesha upendo mkubwa kwake toka alipolazwa. Nguli aliondoka hospitalini akiwa katika baiskeli ya magurudumu na atahitaji kutumia magongo kwa ajili ya kumsaidia kutembea wakati kidonda chake kikipona na pia ameshauriwa kupumzika kwa miezi kadhaa.

SIJUTII KUIHAMA MACLAREN - HAMILTON.

DEREVA nyota wa Langalanga, Lewis Hamilton amekanusha taarifa za kiongozi wa timu ya MacLaren Martin Whitmarsh kuwa anajutia kitendo chake cha kuhamia timu ya Marcedes msimu ujao. Hamilton amesema kuwa ameshangazwa kidogo na kauli ya Whitmarsh aliyotoa wiki iliyopita kuhusiana na kuhama kwake na kusisitiza kuwa ulikuwa umuzi mgumu kuihama McLaren lakini kamwe hajajutia uamuzi huo. Marcedes walishinda mbio za Chinese Grand Prix April mwaka huu na kuonyesha kiwango kizuri mwanzoni mwa msimu baada ya kushindwa kutamba katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011 lakini wameonyesha kuporomoka tena katika kipindi hiki cha mwishoni mwa msimu. Hamilton ambaye alikuwa katika mbio za ubingwa wa dunia mwishoni mwa msimu huu ameshindwa kufanya hivyo baada ya gari lake kuharibika katika mashindano ya Abu Dhabi Grand Prix. Kushindwa kutamba katika mashindano hayo kumewapa nafasi wapinzani wake Sebastian Vettel wa Red Bull na Fernando Alonso wa Ferrari kubakia peke yao katika kugombea taji la dunia huku yakiwa yamebakia mashindano mawili kabla ya msimu kumalizika.

HATUNA FEDHA ZA KUMSAJILI ROBINHO - RAMALHO.

KOCHA wa klabu ya Santos, Muricy Ramalho amesema kuwa kumsajili Robinho kutahitaji uwekezaji mkubwa kitu ambacho klabu hiyo ya Brazil haiko katika nafasi ya kufanya hivyo. Robinho ambaye amewahi kucheza katika klabu za Real Madrid na Manchester City amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kurejea Santos ambayo ni klabu yake ya zamani akitokea AC Milan ya Italia lakini vikwazo vya kifedha linaonkana wazi kukwamisha suala hilo. Ramalho amesema kuwa kuna wachezaji wengi ambao walikuwa waawahitaji kuongeza nguvu katika kikosi chake lakini watakuwa mzigo mkubwa kiuchumi na Robinho ni mmoja wapo. Robinho mwenye umri wa miaka 28 ameshindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Milan msimu huu akiwa ameonekana mara sita pekee katika mashindano yote ikiwa ni matokeo ya majeruhi ya mara kwa mara yanayomsumbua.

WILSHERE ATOA TAHADHARI.

Kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere amevionya vilabu vingine vya Ligi Kuu nchini Uingereza kwa kusisitiza kuwa bado hajapona kwa asilimia mia majeraha ambayo yalikuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Baada ya kukaa nje ya uwanja kwa miezi 17 kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu Wilshere alirejea tena katika kikosi cha Arsenal mwezi uliopita pamoja na kuitwa tena katika kikosi cha Uingereza katika mchezo dhidi ya Sweden ulochezwa Jumatano. Lakini pamoja na hayo Wilshere anaamini kuwa bado hajafikia kiwango chake kwa asilimia mia na bado hajafahamu ni lini atakuwa amepona kabisa kifundo chake cha mguu. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger na kocha wa Uingereza Roy Hodgson walijikuta katika mzozo juu ya afya ya Wilshere baada ya Hodgson kumjumuisha kiungo huyo katika kikosi chake kilichopambana na Sweden Jumatano.

Cisse kuzuiwa na Senegal kuichezea Newcastle?? Suarez kung’oka Anfield??


SUAREZ_V_EVRA12Kukiwa kumezuka mzozo kati ya Senegal na Newcastle kuhusu Straika Papiss Cisse baada ya juzi kutojiunga na Timu ya Taifa ambao unaweza ukaifanya Senagal itumie Sheria ya FIFA na kumfungia Siku 5 ambapo kutamfanya aikose Mechi kati ya Newcastle na Swansea, huko Anfield Liverpool wanahaha kuzima stori zilizoibuka kuwa Straika wao Luis Suarez yuko mbioni kuhamia Manchester City Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguka.
Papiss Cisse could kuikosa Newcastle v Swansea??
Bosi wa Newcastle Alan Pardew ametoboa kuwa Papiss Cisse huenda asicheze Mechi ya Ligi Kuu Jumamosi dhidi ya Swansea kwa sababu ya mgogoro na Senegal kufuatia Straika huyo kutojiunga na Timu ya Taifa ya Senegal ambayo Jumatano, Siku ya Kalenda ya FIFA, ilicheza Mechi ya Kirafiki na Niger.
Inadaiwa sasa Senegal wametishia kuitumia Sheria ya FIFA ya kumfungia Papiss Cisse kwa Siku 5 kwa sababu hawakujulishwa kuhusu Mchezaji huyo kutojiunga na Timu ya Taifa.
Pardew amedai Cisse alikuwa na maumivu ya mgongo aliyoyapata kwenye Mechi ya Jumapili iliyopita waliyofungwa 1-0 na West Ham ambayo yalimlazimu Mchezaji huyo kutolewa nje kwenye Mechi hiyo.
Newcastle imedai ilituma Ripoti ya Madaktari kuhusu Cisse kwa Barua Pepe kwa Chama cha Soka cha Senegal lakini Pardew amesema inaelekea haikupokelewa.
Ikiwa Cisse, Miaka 27, ataikosa Mechi na Swansea hilo litakuwa pigo kwa Newcastle ambao wanahitaji ushindi kwa vile wameshinda Mechi moja tu kati ya sita zilizopita za kwenye Ligi.
Pardew amesema kuwa wanawasiliana na FA ya England na Viongozi wa Senegal ili kupata uhakika kama wanaweza kumtumia Mchezaji huyo Jumamosi.
Luis Suarez ni furaha kubakia Liverpool Miaka mingi!!
Straika wa Liverpool Luis Suarez amesema anafurahia kubakia Liverpool na anataka awe hapo kwa Miaka mingi ingawa sasa kuna tetesi kubwa Manchester City wanataka kumsaini Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguliwa.
Mwanzoni mwa Msimu huu, Suarez alisaini Mkataba mpya na Liverpool na Msimu huu amekuwa kwenye fomu nzuri kwa kufunga Mabao 11 katika Mechi 16 alizochezea Liverpool.
++++++++++++++++++++++++++
Luis Suarez akiwa Liverpool
-ALISAINIWA: Januari 2011 (£22.7m)
-MECHI: 68
-MAGOLI: 32
++++++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, amesema Mchezaji huyo hauzwi.
Rodgers ametamka: “Tukimpoteza Suarez hatuna Straika, hivyo hatuwezi kumuuza.”
Tangu atue England Suarez, licha ya kufanya vizuri akiwa na Liverpool, amekuwa akikumbwa na migogoro ya mara kwa mara.
Alifungiwa Mechi 8 baada ya kumkashifu Kibaguzi Beki wa Manchester United Patrice Evra na baada ya hapo akazua mzozo mpya baada ya kukataa kumpa mkono Evra Timu za Liverpool na Man United zilipokutana Old Trafford.
Hata hivyo, Msimu huu, Wachezaji hao walipeana mikono Timu zao zilipokutana.
Hivi karibuni aliandamwa kwa madai kuwa hujiangusha makusudi kwenye Eneo la Penati ili kuwahadaa Marefa apewe Penati tabia ambayo wakati mwingine imemdhuru mwenyewe kwa kunyimwa Penati za wazi huku Marefa wakidhani anawadaa.



DABI ya LONDON Jumamosi: AVB adai Spurs ni lazima wawe juu ya Arsenal!! 
>>AVB akata tamaa Ubingwa, ataka nafasi ya 4 tu!!
>>AKIRI BINGWA Ni Man United, City au Chelsea, walobaki kugombea 4!
AVB_ACHUCHUMAAIli kuishika nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England ili wapate fursa ya kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, Andre Villas-Boas anaamini Tottenham ni lazima wamalize Ligi wakiwa juu ya Arsenal Msimu huu.
Lakini mara ya mwisho kwa Tottenham kumaliza Ligi wakiwa mbele ya Arsenal ni Mwaka 1995 wakati hata Arsene Wenger, Meneja wa sasa wa Arsenal, hajaanza kibarua.
Msimamo huo wa Villas-Boas umetolewa kwenye mahojiano na Wanahabari kuhusu Dabi yao na Arsenal itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Emirates.
Villas-Boas alijibu swali kuhusu nini lengo lao Msimu huu kwa kusema: “Ninachoona ni dhahiri Man United, Man City na Chelsea wapo kwenye mbio kubwa za Ubingwa. Ingawa ngumu kumaliza nafasi ya 4 lakini ni lazima tumalize juu ya Arsenal ili kuipata.”
++++++++++++++++++++++++
DONDO za DABI: Arsenal v Tottenham
-Tottenham wamepoteza Mechi moja tu kati ya 5 walizocheza mwisho na Arsenal.
-Magoli 100 yamefungwa katika Dabi 32 tangu Arsene Wenger atue Arsenal
++++++++++++++++++++++++
Kimsimamo, kwa sasa, Tottenham wapo nafasi ya 7 wakiwa Pointi 1 mbele ya Arsenal walio nafasi ya 8.
Tottenham wapo Pointi 7 nyuma ya Timu ya 3 Chelsea na Pointi 10 nyuma ya vinara Manchester United.
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
Msimu uliopita Arsenal walimaliza wakiwa nafasi ya 3 na Tottenham nafasi ya 4 lakini Tottenham hawakupewa nafasi ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kama ilivyotakiwa kwa vile Chelsea walitwaa Ubingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI na hivyo kupewa nafasi ya kutetea Taji lao na Tottenham kutupwa kwenye EUROPA LIGI.
Wakati huo huo, Villas Boas amethibitisha Kiungo wa Belgium Mousa Dembele hatacheza Dabi hiyo na Arsenal kwa vila bado ana tatizo la nyonga.
Baada ya kuumia nyonga, Dembele amezikosa Mechi 8 za Tottenham.
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City
MAREFA-Ratiba ya Mechi zao:
Jumamosi Novemba 17
Arsenal v Tottenham
Refa: H Webb
Refa Wasaidizi: M Mullarkey,  D Cann
Refa wa Akiba: C Foy
Reading v Everton
Refa: M Atkinson
Refa Wasaidizi: P Kirkup, J Flynn
Refa wa Akiba: A Marriner
West Bromwich Albion v Chelsea
Refa: M Oliver
Refa Wasaidizi: S Child, D England
Refa wa Akiba: S Attwell
Manchester City v Aston Villa
Refa: J Moss
Refa Wasaidizi: S Beck, A Holmes
Refa wa Akiba: L Probert
Newcastle United v Swansea City
Refa: P Dowd
Refa Wasaidizi: A Garratt, S Ledger
Refa wa Akiba: A Bates
Queens Park Rangers v Southampton
Refa: M Dean
Refa Wasaidizi: J Collin, J Brooks
Refa wa Akiba: L Mason
Liverpool v Wigan Athletic
Refa: K Friend
Refa Wasaidizi: R Ganfield, A Halliday
Refa wa Akiba: J Adcock
Norwich City v Manchester United
Refa: A Taylor
Refa Wasaidizi: R West, P Bankes
Refa wa Akiba: N Swarbrick
Jumapili Novemba 18
Fulham v Sunderland
Refa: L Probert
Refa Wasaidizi: D Bryan, L Betts
Refa wa Akiba: A Marriner
Jumatatu Novemba 19
West Ham United v Stoke City
Refa: C Foy
Refa Wasaidizi: H Lennard, M McDonough
Refa wa Akiba: H Webb

BPL: Baada Robo Msimu, Msimamo kufuata Historia, kubaki hivi hivi??

>>KWA MIAKA 20, BAADA Mechi 10, ni mara 3 tu Man United kileleni na mara zote 3 walimaliza Mabingwa!!!
>>FAHAMU MAREFA MECHI ZA WIKENDI HII!
+++++++++++++++++++++++
MSIMAMO Timu za juu:
1 Man United Mechi 11 Pointi 27
2 Man City  Mechi 11 Pointi 25
3 Chelsea Mechi 11 Pointi 24
4 Everton Mechi 11 Pointi 20
5 WBA Mechi 11 Pointi 20
6 West Ham Mechi 11 Pointi 18
7 Tottenham Mechi 11 17
8 Arsenal Mechi 11 Pointi 16
+++++++++++++++++++++++
FERGIE_MAZOEZINIAkijibu swali mara baada ya kuifunga Manchester United Bao 1-0 katika Wikiendi ya ufunguzi ya MsimuWENGER_AHIMIZA12 huu wa Ligi Kuu England, Meneja wa Everton David Moyes alisema ni mapema kuitathmini Timu yake labda baada ya Mechi 10, msimamo ambao ulichukuliwa pia na Mameneja wa Arsenal, Arsene Wenger, na wa Newcastle, Alan Pardew, na leo hii Timu zimeshacheza Mechi 11, Robo ya Ligi nzima, na Manchester United ndio wako kileleni, hii ikiwa mara yao ya 3 tu kuwa hapo baada ya Mechi 10 ingawa wametwaa Taji mara 12 lakini katika mara zote hizo 3 walizokuwa kileleni wao ndio waliibuka Mabingwa.
Akiongea, Meneja wa zamani wa England, Graham Taylor, alisema: “Msimamo wa Ligi wa Kipindi hiki huwa haubadiliki sana ifikapo Mwezi Mei. Pengine zitatokea Klabu moja au mbili ambazo zitaleta maajabu lakini si zaidi.”
Nae David Pleat, Meneja wa zamani wa Tottenham, amesema: “Baada ya Robo ya Msimu, unapata fununu nini kitaendelea. Klabu mbili za Manchester zipo juu pamoja na Chelsea. Inawezekana Masimu huu Timu ngeni ikakamata nafasi ya 4 ingawa Arsenal na Tottenham hawatakuwa mbali.”
Akiongeza, David Pleat, alisema wasiwasi mkubwa ni ule uwezekano wa Klabu mbili au tatu kufungua pengo kubwa kileleni na pia Klabu za mkiani kuachwa mbali nyuma.
Ingawa kwa wakati huu Msimamo hauleti dira ya kweli nini kitatokea mwishoni mwa Msimu lakini takwimu zinaonyesha katika Miaka 20 Man United, chini ya Sir Alex Ferguson, imetwaa Taji mara 12 na katika mara hizo walikuwa kileleni mara 3 tu baada ya Mechi 10 lakini katika mara zote hizo 3 walimaliza Msimu wakiwa Mabingwa na hilo limemfanya Graham Taylor atamke: “Hiyo ni dalili mbaya kwa Wapinzani wa Man United. Kawaida hawaanzi Ligi vizuri na ni baadae ndio wanakaza uzi lakini sasa wapo juu bila hata kuonekana wamegangamara.”
Mbali ya mbio za Ubingwa na kumaliza kuwa katika Timu 4 bora ili kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, pia ipo vita ya kujinusuru kutimuliwa kwa Mameneja wa Timu zinazofanya vibaya na pia ile vita ya kukwepa kuporomoka Daraja.
Wakiwa mkiani, Meneja wa Southampton, Nigel Adkins, amekiri yeye ndie anaeongoza kwa kuwa Meneja wa kwanza kutegemewa kumwaga unga hali ambayo pia inampa presha Mark Hughes, Meneja wa QPR, ambae Timu yake ipo juu tu ya Southampton.
Katika historia ya Ligi Kuu England, Klabu ambayo pia ilifungwa bao nyingi kufikia hatua hii ya Mechi 10 kama ambavyo Southampton imefungwa, Mabao 28, ni Barnsley katika Msimu wa 1997/8 na ikashushwa Daraja.
Graham Taylor amezitambua West Bromwich Albion chini ya Meneja Steve Clarke, ambao wapo nafasi ya 5, Fulham, nafasi ya 8 na Wigan, nafasi ya 13, kuwa ndizo Timu zinazostahili pongezi kwa mafanikio yao kufikia hatua hii ya Mechi 10.
Pamoja na hizo pia aliipa mkono Everton kwa wanzo mwema ambapo sasa wapo nafasi ya 4.
Akiizungumzia Wigan, ambayo katika hatua hii Msimu uliopita ilikuwa mkiani na hatimae kujikokota na kujinusuru na kumaliza ikiwa nafasi ya 15, David Pleat amesema: “Timu zinazosuasua hubadilisha Mameneja, hubadilisha Wachezaji kwenye Dirisha la Uhamisho, lakini Wigan hawakufanya hata moja kati ya hayo! Meneja Roberto Martinez alibadilisha Mfumo wa Uchezaji na hilo limeleta mafanikio makubwa! Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na wengine!”
+++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi, Novemba 17, 2012
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Arsenal v Tottenham Hotspur
[SAA 12 Jioni]
Liverpool v Wigan Athletic
Manchester City v Aston Villa
Newcastle United v Swansea City
Queens Park Rangers v Southampton
Reading v Everton
West Bromwich Albion v Chelsea
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Norwich City v Manchester United
Jumapili, Novemba 18, 2012
[SAA 1 Usiku]
Fulham v Sunderland
Jumatatu, Novemba 19, 2012
[SAA 5 Usiku]
WestHam v Stoke City
MAREFA-Ratiba ya Mechi zao:
Jumamosi Novemba 17
Arsenal v Tottenham
Refa: H Webb
Refa Wasaidizi: M Mullarkey,  D Cann
Refa wa Akiba: C Foy
Reading v Everton
Refa: M Atkinson
Refa Wasaidizi: P Kirkup, J Flynn
Refa wa Akiba: A Marriner
West Bromwich Albion v Chelsea
Refa: M Oliver
Refa Wasaidizi: S Child, D England
Refa wa Akiba: S Attwell
Manchester City v Aston Villa
Refa: J Moss
Refa Wasaidizi: S Beck, A Holmes
Refa wa Akiba: L Probert
Newcastle United v Swansea City
Refa: P Dowd
Refa Wasaidizi: A Garratt, S Ledger
Refa wa Akiba: A Bates
Queens Park Rangers v Southampton
Refa: M Dean
Refa Wasaidizi: J Collin, J Brooks
Refa wa Akiba: L Mason
Liverpool v Wigan Athletic
Refa: K Friend
Refa Wasaidizi: R Ganfield, A Halliday
Refa wa Akiba: J Adcock
Norwich City v Manchester United
Refa: A Taylor
Refa Wasaidizi: R West, P Bankes
Refa wa Akiba: N Swarbrick
Jumapili Novemba 18
Fulham v Sunderland
Refa: L Probert
Refa Wasaidizi: D Bryan, L Betts
Refa wa Akiba: A Marriner
Jumatatu Novemba 19
West Ham United v Stoke City
Refa: C Foy
Refa Wasaidizi: H Lennard, M McDonough
Refa wa Akiba: H Webb

No comments:

Post a Comment