Thursday, January 31, 2013

KATIKA UKURASA WA HABARI ZA KIMATAIFA>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>


KLABU ya Queens Park Rangers inakaribia kukamilisha uhamisho wa beki Christopher Samba kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala baada ya kufikia makubaliano na mchezaji huyo kufaulu vipimo. Beki huyo wa zamani wa Blackburn mwenye umri wa miaka 28 amesajili kwa ada ya paundi milioni 12.5 ambapo atakuwa akipokea kitita cha paundi 100,000 kwa wiki ikiwemo posho na mambo mengine. Nyota huyo alithibitisha kufanyiwa vipimo vya afya jijini London katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter jana. Mbali na Samba lakini pia meneja wa QPR Harry Redknapp yuko mbioni kumfukuzia mshambuliaji wa klabu ya Stoke City Peter Crouch.
KAGAWA AITWA TENA JAPAN.
KIUNGO nyota wa klabu ya Manchester United, Shinji Kagawa ameitwa tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Japan kitakachocheza mchezo wa kirafiki na Latvia Jumatano ijayo baada ya kupona na kurejea katika kiwango. Kagawa alikosa baadhi ya michezo ya nchi yake ukiwemo mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia ambao walipata ushindi mwembamba wa mabao 2-1 dhidi ya Oman Novemba mwaka jana kwasababu majeraha ya mguu aliyopata wakati anaichezea United. Kagawa alirejea katika kikosi cha United Desemba baada ya kupona na ameonyesha kurejea katika kiwango chake wakati timu yake hiyo ikiongoza Ligi Kuu nchini Uingereza kwa alama saba zaidi ya mahasimu wao Manchester City wanaoshika nafasi ya pili. Kocha wa Japan Alberto Zaccheroni amesema amekuwa akimfuatilia nyota huyo katika mechi alizocheza karibuni na ameshawishika kumuita tena kuimarisha kikosi chake baada ya kurejea katika kiwango chake.

ADEBAYOR AIPONDA CAF KUHUSU UWANJA WA MBOMBELA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor amewabwatukia Shirikisho la Soka la Barani Afrika na Kamati ya Maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon kwa hali mbaya ya Uwanja wa Mbombela uliopo jijini Nelspruit. Adebayor ambaye anacheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza aliulalamikia uwanja huo kuwa na mchanga na mabonde baada ya Togo kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Tunisia na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambapo watacheza na Burkina Faso Jumapili. Mbali na Adebayor, nahodha wa timu ya taifa ya Zambia Christopher Katongo naye alilalakia uwanja huo mapema wiki hii akidai kuwa inafanya timu yake ishinde kucheza mchezo wake wa kupasiana kama walivyozoea. Adebayor alidai michuano ya Afcon ni mikubwa barani Afrika na dunia nzima wanaangalia hivyo kuwa na viwanja vya aina hiyo ni jambo la kusikitisha. Nyota huyo amesema CAF lazima litafutie ufumbuzi suala hilo haraka ili wasiitie doa michuano hiyo ambayo mpaka sasa inaendelea vyema.

NFF YAWAJAZA MAPESA WACHEZAJI SUPER EAGLES.

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles wamepokea posho ya dola 30,000 kila mmoja kutoka kwa Shirikisho la Soka nchini humo-NFF baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon. Nigeria iliigaragaza Ethiopia kwa mabao 2-0 na kufanikiwa kusonga mbele pamoja na Burkina Faso katika Kundi na kuziacha Ethiopia pamoja na mabingwa watetezi wa michuano hiyo kuyaaga mashindano hayo. Nigeria imeshiriki Afcon mara 17 na kufanikiwa kuvuka hatua ya makundi mara 15 na sasa nchi hiyo itakwaana na Ivory Coast timu ambayo inapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji la michuano hiyo. Pamoja na Ivory Coast kupewa nafasi kubwa lakini kocha Nigeria Steven Keshi amesema ameandaa mbinu madhubuti ya kupambana na wapinzani wao ili kuhakikisha wanasonga mbele kwenye michuano hiyo.

BWALYA ASIKITISHWA NA KUTOLEWA KWA ZAMBIA.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Zambia, Kalusha Bwalya amesema amesikitishwa na matokeo ya timu ya taifa ya nchi hiyo yaliyopelekea kuvuliwa ubingwa wao katika hatua ya makundi ya michuano ya Mataifa ya Afrika inayoendelea. Zambia walilazimishwa sare ya bila ya kufungana na Burkina Faso katika mchezo wao wa mwisho wa kundi C uliochezwa katika Uwanja wa Mbombela na matokeo hayo yalishindwa kuwavusha kwenda robo fainali baada ya Nigeria kuifunga Ethiopia kwa mabao 2-0 kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo uliochezwa katika Uwanja wa Royal Bafokeng, Rustenburg. Kalusha aliuambia mtandao wa shirikisho hilo kuwa wachezaji wa timu hiyo inabidi wajilaumu wenyewe kwa kutolewa mapema kwasababu hakuna timu yoyote kwenye mashindano hayo iliyopata maandalizi mazuri kama wao. Kalusha ambaye aliwahi kuwa mchezaji nyota wan chi hiyo amesema waliiandaa timu kwa muda wa kutosha na mategemeo yao ilikuwa ni kufika mbali zaidi ikiwezekana kutetea taji hilo lakini imeshindikana. Kwasasa Kalusha amesema inabidi wasahau michuano hiyo na kuhakikisha wanajiandaa vyema zaidi ili waweze kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014.

AFCON 2013: TOGO YAUNGANA NA IVORY COAST ROBO FAINALI!

>>SAFU ROBO FAINALI YAKAMILIKA, KUANZA JUMAMOSI!!
AFCON_2013-NA_KABUMBU_LIANZESAFU YA ROBO FAINALI ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, leo imekamilika baada ya Togo kuungana na Ivory Coast ambao tayari walikuwa wamefuzu kabla ya Mechi za mwisho za leo za KUNDI D ambazo zote mbili zilimalizika kwa sare.
Ivory Coast ndie Mshindi wa KUNDI D na Togo kutwaa nafasi ya Pili kwa kumzidi Tunisia kwa tofauti ya Magoli baada ya kufungana kwa Pointi.
Kwenye Robo Fainali, ambazo zinaanza Jumamosi Februari 2, Ivory Coast watacheza na Nigeria na Togo kuikwaa Burkina Faso.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Ghana v Cape Verde [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Afrika Kusini v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Ivory Coast v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Togo [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
TOGO 1 TUNISIA 1
Togo leo wamefanikiwa kuingia Robo Fainali yao ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutoka sare 1-1 na Tunisia na hivyo kuungana na Vinara Ivory Coast kwenye Robo Fainali.
+++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Togo 1
-Gakpe Dakika ya 13
Tunisia 1
-Mouelhi Dakika ya 30 (Penati)
+++++++++++++++++++++++
Emmanuel Adebayor alimtengezea Floyd Ayite alieipa Togo bao lao katika Dakika ya 13 na Tunisia kusawazisha kwa Penati ya Khaled Mouelhi ambae baadae alikosa Penati nyingine waliyopewa Tunisia.
Togo nao walinyimwa Penati ya wazi baada ya Adebayor kuangushwa.
VIKOSI:
Togo: Atsu, Nibombe, Akakpo, Bossou, Mamah, Salifou, Amewou, Wome, Floyd Ayite, Adebayor, Jonathan Ayite
Akiba: Agassa, Mani, Ouro-Akoriko, Segbefia, Romao, Gakpe, Placca, Ametepe, Donou, Djene, Damessi, Tchagouni.
Tunisia: Ben Cherifia, Hichri, Abdennour, Chammam, Khazri, Mouelhi, Traoui, Hammami, Darragi, M'Sakni, Khelifa
Akiba: Ben Mustapha, Ifa, Baratli, Dhaouadi, Gharbi, Harbaoui, Ben Youssef, Ben Yahia, Dhaouadi, Jemaa, Boussaidi, Mathlouthi.
Refa: Daniel Bennet (South Africa)
ALGERIA 2 IVORY COAST 2
Ivory Coast, ambao ndio Washindi wa KUNDI D, leo wametoka nyuma kwa Bao 2-0 na kutoka sare ya Bao 2-2 na Algeria hivyo kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa AFCON 2013.
+++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
Algeria 2
-Feghouli Dakika ya 64 (Penati)
-Soudani 70
Ivory Coast 2
-Drogba Dakika ya77
-Wilfred 81
+++++++++++++++++++++++
Algeria, ambao walikuwa wameshaaga Mashindano haya hata kabla ya Mechi ya leo, walikosa Penati iliyopigwa na Ryad Boudebouz katika Kipindi cha Kwanza lakini Sofiane Feghouli alifunga Bao lao la kwanza kwa Penati ya Kipindi cha Pili.
Hilal Soudani aliipatia Algeria Bao la pili na kufanya gemu iwe 2-0 lakini Didier Drogba aliipigia Ivory Coast Bao la kwanza na Wilfried Bony kuisawazishia Ivory Coast.
VIKOSI:
Algeria: M'Bolhi, Halliche, Mesbah, Belkalem, Mostefa, Boudebouz, Lemmouchia, Guedioura, Lacen, Soudani, Slimani
Akiba: Doukha, Cadamuro, Feghouli, Bouazza, Medjani, Aoudia, Kadir, Bezzaz, Tedjar, Ghoulam, Rial, Si Mohamed.
Ivory Coast: Yeboah, Boka, Ismael Traore, Toure, Lolo, Romaric, Razak, Kalou, Bony, Kone, Drogba
Akiba: Barry, Zokora, Tiote, Gervinho, Konan, Gradel, Tiene, Lacina Traore, Toure, Eboue, Bamba, Ali Sangare.
Refa: Eric Otogo-Castane (Gabon)
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
KUNDI A
1 South Africa Mechi 3 Pointi 5
2 Cape Verde Mechi 3 Pointi 5
3 Morocco Mechi 3 Pointi 3
4 Angola Mechi 3 Pointi 1
KUNDI B
1 Ghana Mechi 3 Pointi 7
2 Mali Mechi 3 Pointi 4
3 Congo DR Mechi 3 Pointi 3
4 Niger Mechi 3 Pointi 1
KUNDI C
1 Burkina Faso Mechi 3 [Tofauti ya Magoli 4] Pointi 5
2 Nigeria Mechi 3 [Tofauti ya Magoli 2] Pointi 5
3 Zambia Mechi 3 Pointi 3
4 Ethiopia Mechi 3 Pointi 1
KUNDI D
1 Ivory Coast Mechi 3 Pointi 7
2 Togo Mechi 3 [Tofauti ya Magoli 1] Pointi 4
3 Tunisia Mechi 3 [Tofauti ya Magoli -2]  Pointi 4
4 Algeria Mechi 3 Pointi 1
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA/MATOKEO:
[SAA za BONGO]
Jumamosi Januari 19
South Africa 0 Cape Verde Islands 0
Angola 0 Morocco 0
Jumapili Januari 20
Ghana 2 Congo DR 2
Mali 1 Niger 0
Jumatatu Januari 21
Zambia 1 Ethiopia 1
Nigeria 1 Burkina Faso 1
Jumanne Januari 22
Ivory Coast 2 Togo 1
Tunisia 1 Algeria 0
Jumatano Januari 23
South Africa 2 Angola 0
Morocco 1 Cape Verde Islands 1
Alhamisi Januari 24
Ghana 1 Mali 0
Niger 0 Congo DR 0
Ijumaa Januari 25
Zambia 1 Nigeria 1
Burkina Faso 4 Ethiopia 0
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast 3 Tunisia 0
Algeria 0 Togo 2
Jumapili Januari 27
Morocco 2 South Africa 2
Cape Verde Islands 2 Angola 1
Jumatatu Januari 28
Congo DR 1 Mali 1
Niger 0 Ghana 3
Jumanne Januari 29
Ethiopia 0 Nigeria 2
Burkina Faso 0 Zambia 0
Jumatano Januari 30
Algeria 2 Ivory Coast 2
Togo 1 Tunisia 1
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Ghana v Cape Verde [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Afrika Kusini v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Ivory Coast v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Togo [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]

FA CUP: RAUNDI YA 5, RATIBA YATHIBITISHWA! WAZEE WA KURUHUSU DAKIKA 3 MPIRA KUMALIZIKA WANARUDIANA NA BRENTFORD


>>MARUDIANO CHELSEA v BRENTFORD FEB 17!
FA_CUP-NEW_LOGORATIBA za Mechi za FA CUP zimethibitishwa na Raundi ya 5 itachezwa Jumamosi Februari 16, Jumapili Februari 17 na Jumatatu Februari 18 wakati ile Mechi ya Marudiano ya Raundi ya 4 kati ya Chelsea na Brentford itakuwepo Jumapili Februari 17.
Mshindi wa Mechi kati ya Chelsea na Brentford atacheza Raundi ya 5 ugenini dhidi ya Middlesbrough katika Tarehe itakayothibitishwa baadae ingawa inategemewa kuwa ni Mwezi Februari.
Wakati Jumamosi Februari 16 zipo Mechi 4 za Raundi ya 5, Jumapili zitachezwa Mechi mbili na Jumatatu Februari 18 ni moja tu na ni ile ya Old Trafford kati ya Manchester United na Reading.
FA CUP
RAUNDI YA 5
RATIBA
Jumamosi Februari 16
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
Luton v Millwall
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Blackburn Rovers
Wimbledon v Barnsley
[SAA 3 Usiku]
Oldham v Everton
Jumapili Februari 17
[SAA 9 Mchana]
Chelsea v Brentford [MARUDIANO RAUNDI ya 4]
[SAA 11 Jioni]
Man City v Leeds
[SAA 3 Dak 55 Usiku]
Huddersfield au Leicester v Wigan
Jumatatu Februari 18
[SAA 5 Usiku]
Man United v Reading
[*** Middlesbrough v Brentford/Chelsea==TAREHE KUTHIBITISHWA]

MFUMO FA CUP:
MSIMU WA 2012/13
RAUNDI YA 5: Jumamosi Februari 16
RAUNDI YA 6: Jumamosi Machi 9
NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 13 na Jumapili Aprili 14
FAINALI: Jumamosi Mei 11

CHEKI CHELSEA ALIVYOPOKONYWA TONGE MDOMONI JANA JAN 30-1-2013 DHIDI YA READING

BPL MASHETANI WEKUNDU MAN U WAENDELEA KUFUMANIA NYAVU ,ROONEY AIWEZESHA MAN U KUWA MBELE KWA POINTI 7 DHIDI YA MAN CITY,CHELSEA MDEBWEDOOOOOO......WARUHUSU BAO 2 NDANI YA DAKIKA 3


>>ARSENAL YATOKA 2-0 NYUMA, SARE 2-2 NA LIVERPOOL!!
>>READING YAPIGA 2 DAKIKA 3 ZA MWISHO, SARE 2-2 NA CHELSEA!
BPL_LOGOMATOKEO:
Jumatano Januari 30
Arsenal 2 Liverpool 2
Everton 2 West Brom 1
Norwich 1 Tottenham 1
Fulham 3 West Ham 1
Man United 2 Southampton 1
Reading 2 Chelsea 2

VINARA Manchester United wameishinda 2-1 Southampton Uwanjani Old Trafford na kukwea Pointi 7 mbele kileleni mwa BPL, Barclays Premier League, wakati Uwanjani Emirates Arsenal walitoka Bao 2-0 nyuma na kutoka droo ya 2-2 na Liverpool huku Reading ikitoka 2-0 nyuma walipocheza na Chelsea waliweza kupiga Bao 2 Dakika 3 za mwisho na kupata sare ya 2-2.

BPL:
MSIMAMO-Timu zaJuu:
1 Man United Mechi 24 Pointi 59
2 Man City  Mechi 24 Pointi 52
3 Chelsea  Mechi 24 Pointi 46
4 Tottenham  Mechi 24 Pointi 42
5 Everton  Mechi 24 Pointi 41
6 Arsenal  Mechi 24 Pointi 38
7 Liverpool Mechi 24 Pointi 35

MAN UTD 2 SOUTHAMPTON 1

MAGOLI:
Man United
-Rooney Dakika ya 8 & 27
Southampton
-Rodriguez Dakika ya 3

VIKOSI:
Man United: De Gea, Jones, Smalling, Vidic, Evra, Welbeck, Carrick, Anderson, Kagawa, Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Da Silva, Ferdinand, Valencia, Nani, Cleverley, Buttner.
Southampton: Boruc, Clyne, Yoshida, Hooiveld, Fox, Schneiderlin, Cork, Puncheon, Rodriguez, Ramirez, Lambert
Akiba: Kelvin Davis, Steven Davis, Lee, Lallana, Richardson, Shaw, Chaplow.
Refa: Lee Mason
ARSENAL 2 LIVERPOOL 2

MAGOLI:
Arsenal
-Goroud Dakika ya 64
-Walcott 67
Liverpool
-Suarez Dakika ya 5
-Henderson 60

VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs, Ramsey, Wilshere, Cazorla, Walcott, Podolski, Giroud
Akiba: Mannone, Koscielny, Jenkinson, Santos, Diaby, Oxlade-Chamberlain, Rosicky.
Liverpool: Reina, Johnson, Agger, Carragher, Wisdom, Lucas, Gerrard, Henderson, Downing, Suarez, Sturridge
Akiba: Jones, Enrique, Skrtel, Shelvey, Allen, Borini and Sterling.
Refa: Kevin Friend
READING 2 CHELSEA 2

MAGOLI:
Reading
-Le Fondre Dakika ya 87 & 90
Chelsea
-Juan Mata Dakika ya 45
-Lampard 66

VIKOSI:
Reading: Federici, Kelly, Pearce, Mariappa, Harte, Kebe, Karacan, Leigertwood, Guthrie, McAnuff, Pogrebnyak
Akiba: Stuart Taylor, Shorey, Le Fondre, McCleary, Morrison, Robson-Kanu, Akpan.
Chelsea: Turnbull, Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Cole, Mata, Ramires, Lampard, Oscar, Bertrand, Torres
Akiba: Hilario, Ferreira, Marin, Terry, Ba, Benayoun, Ake.
Refa: Mark Halsey
NORWICH 1 TOTTENHAM 1

MAGOLI:
Norwich
-Hoolahan Dakika ya 32
Tottenham
-Bale Dakika ya 80

VIKOSI:
Norwich: Bunn, Martin, Bassong, Turner, Garrido, Snodgrass, Johnson, Tettey, Pilkington, Hoolahan, Holt
Akiba: Camp, Whittaker, Howson, Jackson, Fox, Elliott Bennett, Ryan Bennett.
Tottenham: Lloris, Walker, Vertonghen, Dawson, Assou-Ekotto, Lennon, Parker, Dembele, Bale, Dempsey, Defoe
Akiba: Friedel, Gallas, Naughton, Sigurdsson, Holtby, Livermore, Caulker.
Refa: Neil Swarbrick
EVERTON 2 WEST BROM 1

MAGOLI:
Everton
-Baines Dakika ya 29 & 45 [Penati]
West Brom
-Long Dakika ya 65

VIKOSI:
Everton: Howard, Jagielka, Heitinga, Distin, Baines, Mirallas, Neville, Osman, Pienaar, Fellaini, Anichebe
Akiba: Mucha, Gibson, Jelavic, Oviedo, Naismith, Hitzlsperger, Gueye.
West Brom: Foster, Jones, McAuley, Olsson, Popov, Morrison, Dorrans, Thorne, Brunt, Thomas, Lukaku
Akiba: Myhill, Yacob, Ridgewell, Rosenberg, Long, Tamas, Fortune.
Refa: Michael Oliver
FULHAM 3 WEST HAM 1

MAGOLI:
Fulham
-Berbatov Dakika ya 10
-Rodallega 49
-Petric 90
West Ham
-Nolan 48

VIKOSI:
Fulham: Schwarzer, Riether, Hangeland, Senderos, Riise, Duff, Karagounis, Sidwell, Rodallega, Ruiz, Berbatov
Akiba: Etheridge, Baird, Petric, Frimpong, Hughes, Dejagah, Davies.
West Ham: Jaaskelainen, Demel, Reid, Tomkins, O'Brien, Diame, Noble, Nolan, Jarvis, Joe Cole, Chamakh
Akiba: Henderson, Carroll, Carlton Cole, Vaz Te, Taylor, Pogatetz, O'Neil.
Refa: Chris Foy
RATIBA MECHI ZA WIKIENDI:
Jumamosi Februari 2
[SAA 9 Dak 45 Mchana]
QPR v Norwich
[SAA 12 Jioni]
Arsenal v Stoke
Everton v Aston Villa
Newcastle v Chelsea
Reading v Sunderland
West Ham v Swansea
Wigan v Southampton
[SAA 2 na Nusu Usiku]
Fulham v Man United
Jumapili Februari 3
[SAA 10 na Nusu Jioni]
West Brom v Tottenham
[SAA 1 Usiku]
Man City v Liverpool

COPA CLASICO: NGOMA NGUMU, SARE 1-1, SI CR7 WALA MESSI WAFUNGAJI!

>>NUSU FAINALI NYINGINE ALHAMISI ATLETICO MADRID v SEVILLA

Barcelona's Cesc Fabregas (L) celebrates scoring
MECHI ya kwanza ya Nusu Fainali ya COPA del REY iliyochezwa Santiago Bernabeu kati ya Mahasimu wakubwa huko Spain, Real Madrid na Barcelona, ilikwisha kwa sare ya Bao 1-1 na wafungaji wa Bao hizo si wale tuliowazoea, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, na Timu itakayotinga Fainali itajulikana huko Nou Camp hapo Februari 27 katika marudiano.Level pegging: Raphael Varane (left) celebrates after scoring the equaliser

COPA del REY
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 30
Real Madrid 1 Barcelona 1
Alhamisi Januari 31
[SAA 6 Usiku]
Atletico Madrid v Sevilla
MARUDIANO
Jumatano Februari 27
Sevilla v Atletico Madrid
Barcelona v Real Madrid

Barcelona ndio walitangulia kupata Bao alilofunga Cesc Fabregas Dakika ya 50 baada ya pasi ya Messi.
Real Madrid walisawazisha kwa Bao la kichwa la Beki kutoka Ufaransa Raphael Varane katika Dakika ya 81.
VIKOSI:
Real Madrid (Mfumo 4-2-3-1): Diego López; Essien, Varane, Carvalho, Arbeloa; Khedira, Alonso; Callejón, Özil, Ronaldo; Benzema.
Akiba: Adán, Kaká, Marcelo, Albiol, Modric, Higuaín, Morata.
Barcelona (Mfumo 1-8-1): Pinto; Alves, Piqué, Puyol, Alba; Sergio; Xavi, Fàbregas; Pedro, Messi, Iniesta.
Akiba: Valdés, Villa, Alexis, Thiago, Mascherano, Adriano, Song.

KIM POULSEN AMFUNGIA VIOO TEGETE ALIYE HATARI KWENYE KIKOSI CHA STARS DHIDI YA CAMEROON


Kim Poulsen
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja kikosi cha wachezaji 21 kitakachoingia kambini Jumapili (Februari 3 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Cameroon (Indomitable Lions).
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo (Januari 31 mwaka huu), Kim amesema mechi dhidi ya Cameroon itakuwa kipimo kizuri kwake kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya kucheza mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayofanyika Machi mwaka huu.
“Itakuwa mechi ngumu na kipimo sahihi kwetu. Tuko tayari, tutacheza kwa staili yetu kwa sababu ni sehemu ya maandalizi kabla ya mechi dhidi ya Morocco. Ni mechi nzuri kwa sababu wachezaji wameonyesha wako tayari.
“Tumetoka kucheza dhidi ya Zambia na Ethiopia. Lengo ni Taifa Stars kucheza fainali za AFCON 2015, kwa hiyo mechi dhidi ya Cameroon ni sehemu ya mipango yetu kuhakikisha tunafika huko,” amesema Kim ambaye amerejea nchini juzi kutoka Afrika Kusini kuzifuatilia timu za Morocco na Ivory Coast zilizo kundi moja na Tanzania katika mechi za mchujo za Kombe la Dunia.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco, Machi 24 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Stars inashika nafasi ya pili katika kundi lake nyuma ya Ivory Coast inayoongoza. Timu nyingine katika kundi hilo ni Gambia.
Wachezaji aliowaita kwenye kikosi chake ni makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba) na Issa Rashid (Mtibwa Sugar).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Simon Msuva (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Khamis Mcha (Azam), Athuman Idd (Yanga) na Mwinyi Kazimoto (Simba). Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Simba), na Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Katika kikosi hiki, Poulsen hajamuita Jerry Tegete ambaye siku za karibuni amefufua makali yake wakati ameita washambuliaji halisi wawili tu, Ulimwengu na Samatta.