Wednesday, November 21, 2012

RATIBA YA CHAGUZI ZA TWFA MKOA WA TABORA ZATOKA-KUANZIA WILAYA ZOTE ZA TABORA[IGUNGA,NZENGA,URAMBO,SIKONGE,UYUI,TABORA MJINI, MPAKA MKOA


 Ratiba ya uchaguzi wa TWFA wilaya ya Igunga mkoa wa tabora imetoka na mchakato mzima umeanza tangu tarehe 19-11-2012 pale kamati ya uchaguzi ya TWFA wilaya ya igunga kutangaza uchaguzi wa TWFA na nafasi za wagombea.

Tarehe 21-25-11-2012 hii leo mchakato wa   uchukuaji wa fomu za kugombea za TWFA [w] umeanza.Na tarehe 26/11/2012 kamati ya uchaguzi itapitia fomu za waombaji wa TWFA na itatangaza matokeo ya upitiaji wa fomu hizo na kuweka katika mbao za matangazo majina ya waombaji uongozi wa TWFA.

TAREHE 27-29/11/2012 kamati ya uchaguzi itatoa pingamizi kwa waombaji uongozi wa TWFA[W] mwisho wa kupokea pingamizi ni tarehe 29.11.2012  saa 10;00 alasiri.pingamizi ziwasilishwe kwa katibu wa kamati ya uchaguzi bw.ramadhani khamis maghembe,hakuna ada ya kuweka pingamizi ni bure lakini pingamizi hizo zizingatie matakwa ya ibara ya 11[2]ya kanuni za uchaguzi.

30-01/12/2012 ni kujadili pingamizi na kufanya maamuzi na tarehe 2 /12/2012itakuw ani siku ya usaili na kutangaza matokeo/kuwajulisha kwa maandishi wagombea matokeo ya usaili.

Na tarehe 03-06/12/2012 itakuwa ni siku ya kutoa fursa ya kukata rufaa,kwenye kamati ya uchaguzi ya TWFA na mwisho wa kupokeo rufaa ni tarehe 06/12/2012 saa 10;00 alasiri.

Kuanzia tarehe 07-10/12/2012 kamati ya uchaguzi ya TWFA itasikiliza rufaa kama zipo na kutangaza matokeo ya rufaa.kama hakuna rufaa kamati ya uchaguzi ya TWFA itatangaza majina ya wagombea na nafasi zao na kuanza kampeni.

11/12/2012 baada ya uamuzi wa kamati ya uchaguzi ya TFF ,kamati ya uchaguzi ya TWFA itatangaza majina na kuanza kampeni mara moja na tarehe 15/12/2012 ndo uchaguzi rasmi kamili utafanyika kuwasaka viongozi wa TWFA wa wilaya zote za mkoa wa tabora.

Baada ya kumalizika kwa chaguzi za wilaya ya urambo,sikonge,nzega,uyui,igunga,tabora mjini na terehe 18/12/2012 watatafutwa viongozi watakaowakilisha mkoa wa tabora katika uongozi wa TWFA kwani siku hiyo itakuwa ndiyo  siku uchaguzi wa TWFA mkoa wa tabora .

 

 

 

SUNZU AMALIZA MKATABA SIMBA SC, KASHESHE KUMUONGEZEA

Felix Sunzu Jr. kushoto alipokuwa akisaini mkataba wa awali na Simba, ambao unamalizika mwezi ujao. Kulia ni Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zambia, Felix Mumba Sunzu Jr. anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwezi ujao katika klabu ya Simba SC na hadi sasa mustakabali wake haueleweki kama ataongezewa mkataba au la.
Kumekuwa na mawazo tofauti ndani ya Simba SC kuhusu Sunzu, ambaye kwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Tanzania, Sh Milioni 5, kwamba hachezi kwa kiwango cha fedha anazolipwa.
Lakini wengine wanaamini Sunzu anawajibika vizuri na anastahili kwa fedha anayolipwa. Pamoja na hayo, hali ya kiuchumi ndani ya klabu hiyo kwa sasa, inatia shaka kama itaweza kuurudia mkataba ule ule wa Sunzu.
Kwa kawaida, baada ya kumaliza mkataba, Simba ili kuendelea kuishi na Sunzu, italazimika kumpa fedha ya dau la usajili, ambalo kwa mwaka haliwezi kuwa chini ya dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. Milioni 20 za Tanzania) na kukubaliana kuhusu mshahara uwe ule ule au mpya.
Kulingana zengwe lililotawala juu ya dola za Kimarekani 3,500 anazolipwa Sunzu kuna uwezekano Simba ikataka kuuteremsha mshahara huo, hasa ikizingatiwa kuwa, kwa sasa hakuna taarifa zozote za Mzambia huyo kutakiwa na timu, iwe ndani ua nje ya nchi. 
Kumalizika kwa mkataba wa Sunzu ni mtihani mwingine kwa Simba, ambayo kwa sasa inakabiliwa na kasheshe la kuingia mkataba mpya na mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi ambaye yuko vizuri kisoka na anatolewa macho na Azam na Yanga.
Na suala la usajili linazidi kuwa zito kwa sababu Kamati ya Utendaji ya Simba SC wiki hii imevunja Kamati zote ndogondogo, ikiwemo Kamati ya Usajili, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Zacharia Hans Poppe.   

 

 

BARTHEZ ALIVYOMNUSURU YAW BERKO KUTUPIWA VIRAGO YANGA

Ally Mustafa 'Barthez'
WASIWASI kwamba Ally Mustafa ‘Barthez’ akibaki bila kipa mshindani ndani ya Yanga atabweteka, ndio umemnusuru kipa Mghana, Yaw Berko kutemwa Yanga.
Habari ambazo nimezipata kutoka ndani ya Yanga, zimesema kwamba, Yanga ilifikiria kumtema Berko, lakini kwa uzoefu wao juu ya tabia za wachezaji wa Kitanzania, wameamua kuachana na wazo hilo.
“Unaweza kusema umuache Berko, halafu yule Barthez akijiona yuko peke yake, akaanza kutuzingua, Berko mwenyewe amebadilika mno hivi sasa na yuko tayari kucheza wakati wowote,”alisema kiongozi mmoja ‘mzito’ wa Yanga.
Berko ambaye mkataba wake unamalizika Mei mwakani, ataendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba huo na akifanya vizuri ataongezewa mkataba mwishoni mwa msimu.
Kipa huyo anayelipwa mshahara wa Sh. Milioni 1.5 kwa mwezi, amerudishwa benchi siku za karibuni baada ya kufululiza kufungwa mabao rahisi, jambo ambalo lilimkera kocha Mholanzi, Ernie Brandts.
Kwa sababu hiyo, vyombo vya habari vikaanza kubashiri kwamba ataachwa mwezi ujao kwa sababu pia, tayari klabu hiyo imesajili mchezaji mwingine wa kigeni, Kabange Twite kutoka APR ya Rwanda.
Kanuni za Usajili za Ligi Kuu zinataka wachezaji watano tu wa kigeni kwa kila klabu, na Yanga tayari inao Yaw Berko, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Hamisi Kiiza kutoka Uganda na Didier Kavumbangu kutoka Burundi.
Lakini habari zaidi zinasema Kabange atachukua nafasi moja kati ya mbili zinazotarajiwa kuachwa na wachezaji wawili wa klabu hiyo, ambao watauzwa hivi karibuni, Niyonzima na Kavumbangu. 

 

 

F.O.S. WASAKA MAJIBU LEO SIMBA SC

Mwenyekiti wa F.O.S., Zacharia Hans Poppe 
KUNDI la Friends of Simba (F.O.S.) linatarajiwa kukutana leo jioni kujadili mustakabali wa klabu kwa ujumla na kutoa msimamo wao mbele ya wanachama na wapenzi wa klabu hiyo.
Hamkani si shwari Simba kwa sasa baada ya timu kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ikitoka kuongoza kwa wastani wa pointi saba.
Mwenyekiti wa F.O.S., Zacharia Hans Poppe alisema juzi kwamba, watakuwa na Mkutano kesho kujadili hali ya mambo klabuni kwao.
“Sisi kazi yetu ni kusapoti uongozi uliopo madarakani, kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri, sasa hali inayoendelea sasa inatutia shaka kuelekea mwakani, ambako tutakuwa na mtihani wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na pia Ligi ya Mabingwa.
Kwa hivyo tutakutana, tutazungumza kwa mapana marefu sana, ili tujue undani na ukweli wa matatizo yaliyopo klabuni na baada ya hapo na sisi tutatoa mtazamo wetu,”alisema kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Kamati ya Utendaji ya Simba, chini ya Mwenyekiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage ilikutana na kufikia maamuzi ya kuvunja Kamati zote ndogondogo za klabu pamoja na kulifuta tawi la wanachama wakorofi, Mpira Pesa la Magomeni, waliomtukana kipa Juma Kaseja na kuendesha harakati za mapinduzi. 
Lakini pia wasiwasi umeingia kutokana na kuvunjwa pia kwa Kamati ya Usajili, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Hans Poppe katika kipindi hiki kigumu ambacho klabu inatakiwa kurekebisha usajili kuelekea mzunguko wa pili na Ligi ya Mabingwa.
Mbali na hivyo, kuna suala la mchezaji Emanuel Okwi ambaye amemaliza mkataba wake kwenye klabu hiyo na alikuwa kwenye majadiliano na Kamati ya Usajili, ambayo yalifikia pazuri, lakini kwa kuvunjwa kwa Kamati hizo, maana yake mazungumzo hayo hayawezi kuendelea.   Mshambuliaji Mzambia, Felix Sunzu Jr. pia naye anamaliza mkataba wake mwezi ujao.


 

TAARIFA YA BFT YA KUSOGEZA MBELE MASHINDIANO YA NGUMI YA TAIFA



Mashindano ya klabu bingwa ya taifa 2012 yaliyokuwa yaanze Kufanyika kuanzia tarehe 26-30/11/2012 yamesogezwa mbele hadi 29/01-03/02/2013 kutokana na sababu mbalimbali.
Sababu zilizopelekea mashindano hayo kusogezwa mbele kubwa ni  hadi tunapotoa taarifa hii katika vyombo vya habari hakuna timu iliyokamilisha taratibu tulizoziweka za kuweza kusaidia kukamilisha mashindano hayo kwa ufanisi.
 Kwani katika barua ya taarifa ya mwaliko wa kushiriki katika mashindano BFT iliagiza kufikia tarehe 15/11/2012 timu zote ziwe zimethibitisha ushiriki wao ikiwa pamoja na kuwasilisha majina na picha za mabondia na viongozi watakaoshiriki  katika mashindano hayo na kulipa ada ya ushiriki ya Tsh. 200,000/=.
Hadi leo hakuna hata timu moja iliyokamilisha utaratibu huo kwa nia ya kupanga mashindano vizuri ili yawe na hadhi ya taifa kwa kuzingatia sheria za chama cha ngumi cha dunia (AIBA)
Sababu kama hizi mara nyingi zimesababisha mashindano mengi kuyaendesha katika kiwango cha chini na lawama nyingi kuelekezwa kwa BFT bila ya kufahamu sababu za msingi za kusababisha kutokea hivyo.kitu ambacho tungeweza kuepukana nacho kama tutafata taratibu tulizojiwekea. 
Kwani kwa kufanya hivyo tungejua mapema   idadi ya washiriki ili kupanga mipango halisi ya Kufanyika kwa mashindano.
Aidha kozi ya waamuzi iliyokuwa ianze tatehe 11-30/11/2012 imeshindwa Kufanyika kutokana na wanafunzi walikuwa wameomba kujiunga na kozi hiyo kushindwa kufika kwa wakati na kushindwa kukamilisha malipo ya kujiunga na kozi kwa wakati.
Kutokana na majukumu mengine  iliyonayo BFT kozi hiyo sasa itafanyika kuanzia tarehe 15/01-04/02/2013 na mazoezi ya vitendo yatafanyika katika mashindano ya klabu bingwa.
Kwa sasa BFT nguvu kubwa inaweka katika usajiri kwa makocha .waamuzi ,mabondia, madaktari katika data base za chama cha ngumi cha dunia (AIBA) ili wengi watambulike kwa ajili ya kujiunga na mashirikisho ya ngumi za kulipwa ndani ya ngumi za  ridhaa (AIBA PRO BOXING).

Makore Mashaga
KATIBU MKUU (BFT)

 

CHIPOLOPOLO yaisaka Taifa Star

Kuna ripoti kuwa Chama cha Soka cha Zambia, FAZ, kinaandaa Mechi ya kujipima nguvu na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ikiwa ni moja ya matayarisho ya Timu yao ya Taifa, Chipolopolo, kwa ajili ya utetezi wa Ubingwa wao wa Afrika huko Afrika Kusini kwenye Fainali za AFCON 2013 ambapo wataanza Mechi yao ya Kundi C dhidi ya Ethiopia Januari 21 ndani ya Mbombela Stadium Mjini Nelspruit.
Pamoja na Mechi ya Taifa Stars, ambayo inatarajiwa kuchezwa Desemba 23, Zambia wameaandaa Mechi 4 za kujipima nguvu ikiwa pamoja na ile itakayochezwa na Norway hapo Januari 12 Uwanja wa Levy Mwanawasa Mjini Ndola.
Hadi sasa Mechi na Taifa Stars bado ipo kwenye maandalizi na hata Uwanja upi itachezwa bado haijajulikana.
Wiki iliyopita, Chipolopolo iliifunga Bafana Bafana Bao 1-0 kwenye Mechi maalum iliyoitwa Nelson Mandela Chalenji na bao la ushindi kufungwa na Collins Mbesuma.
Zambia bado wapo chini ya Kocha Herve Renard ambae ndie aliwaongoza kutwaa Ubingwa wa Afrika mapema Mwaka huu kwenye Fainali za AFCON 2012 zilizochezwa Nchini Gabon na Equatorial Guinea.
Kwenye AFCON 2013, Zambia wapo Kundi C pamoja na Nigeria, Burkina Faso na Ethiopia.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
KUNDI A: South Africa, Cape Verde, Morocco, Angola
KUNDI B: Ghana, DR Congo, Niger, Mali
KUNDI C: Zambia, Ethiopia, Nigeria, Burkina Faso
KUNDI D: Ivory Coast, Togo, Tunisia, Algeria
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
VIWANJA:
-Soccer City, Johannesburg [Mashabiki 94,700]
-Moses Mabhida Stadium, Durban [Mashabiki 54,000]
-Nelson Mandela Bay Stadium, Port Elizabeth [Mashabiki 48,000]
-Mbombela Stadium, Nelspruit [Mashabiki 41,000]
-Royal Bafokeng Stadium, Rustenburg [Mashabiki 42,000]
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Jumamosi Januari 19
South Africa v Cape Verde Islands [Soccer City Saa 1 Usiku]
Angola v Morocco [Soccer City Saa 4 Usiku]
Jumapili Januari 20
Ghana v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mali v Niger Nelson Mandela Bay Stadium 20:00
Jumatatu Januari 21
Zambia v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Nigeria v Burkina Faso [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumanne Januari 22
Ivory Coast v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Tunisia v Algeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumatano Januari 23
South Africa v Angola [Moses Mabhida Stadium Saa 12 Jioni]
Morocco v Cape Verde Islands [Moses Mabhida Stadium Saa 3 Usiku]
Alhamisi Januari 24
Ghana v Mali [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Niger v Congo DR [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
Ijumaa Januari 25
Zambia v Nigeria [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Burkina Faso v Ethiopia [Mbombela Stadium Saa 3 Usiku]
Jumamosi Januari 26
Ivory Coast v Tunisia [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Algeria v Togo [Royal Bafokeng Stadium Saa 3 Usiku]
Jumapili Januari 27
Morocco v South Africa [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Cape Verde Islands v Angola [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatatu Januari 28
Congo DR v Mali [Moses Mabhida Stadium Saa 2 Usiku]
Niger v Ghana [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 2 Usiku]
Jumanne Januari 29
Ethiopia v Nigeria [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Burkina Faso v Zambia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
Jumatano Januari 30
Algeria v Ivory Coast [Royal Bafokeng Stadium Saa 2 Usiku]
Togo v Tunisia [Mbombela Stadium Saa 2 Usiku]
ROBO FAINALI
Jumamosi Februari 2
Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [Nelson Mandela Bay Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
Jumapili Februari 3
Mshindi Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C [Royal Bafokeng Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D [Mbombela Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
NUSU FAINALI
Jumatano Februari 6
Mshindi RF 3 v Mshindi RF 2 [Mbombela Stadium Saa 12 Jioni]
Mshindi RF 1 v Mshindi RF 4 [Moses Mabhida Stadium Saa 3 na Nusu Usiku]
MSHINDI wa TATU
Jumamosi Februari 9
[Nelson Mandela Bay Stadium Saa 3 Usiku]
FAINALI
Jumapili Februari 10
[Soccer City Saa 3 Usiku]

 

DI MATTEO ATUPIWA VIRAGO CHELSEA

Di Matteo amebaki historia Chelsea

BILIONEA Mrusi Roman Abramovich amemfukuza kazi Kocha Mtaliano, Roberto Di Matteo asubuhi ya leo baada ya matokeo mabaya mfululizo.
Mmiliki huyo wa Chelsea, amekasirishwa na matokeo mabaya ya timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kumfukuza kazi Mtaliano huyo baada ya timu kuzabwa mabao 3-0 na Juventus jana, ikiwa ni miezi sita tu tangu aipe timu hiyo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Sasa mtu wa kwanza kabisa ambaye Abramovich anamtaka akarithi mikoba ya Mtaliano huyo ni kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola, na kama akikwama kwa Mspanyola huyo ambaye amesema hataki ukocha tena kwa sasa, basi atahamishia ndoana zake kwa Rafa Benitez.
MAKOCHA WALIODUMU MUDA MFUPI CHESLEA:
Guus Hiddink         Siku 105
Felipe Scolari         Siku 223
Avram Grand          Siku 247
Andre Villas-Boas   Siku 256
Roberto Di Matteo   Siku 262
MATOKEO YALIYOMFUKUZISHA KAZI DI MATTEO:
Oktoba 23: Shakhtar 2 Chelsea 1        (Ligi ya Mabingwa)
Oktoba 28: Chelsea 2 Man United 3    (Ligi Kuu)
Oktoba 31: Chelsea 5 Man United 4    (Kombe la Ligi)
Novemba 3: Swansea 1 Chelsea 1      (Ligi Kuu)
Novemba 7: Chelsea 3 Shakhtar 2      (Ligi ya Mabingwa)
Novemba 11: Chelsea 1 Liverpool 1     (Ligi Kuu)
Novemba 17: West Brom 2 Chelsea 1  (Ligi Kuu)
Novemba 20: Juventus 3 Chelsea 0     (Ligi ya Mabingwa)

 

 

Chelsea yamtimua Roberto Di Matteo!!

>>ABRAMOVITCH ANASAKA MENEJA WA 9 TANGU AJE CHELSEA 2003!!
CHELSEA-MANCINI_n_TORRESChelsea imetangaza kumfukuza kazi Meneja wake Roberto Di Matteo mara baada ya jana kuchapwa Bao 3-0 na Juventus kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo imewaweka katika hali ngumu kusonga mbele Raundi inayofuata na hivyo kuwa hatarini kulitetea Taji lao la Ubingwa wa Ulaya.
Msimu uliopita Di Matteo alitwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI na FA CUP akiwa Meneja wa muda na Mwezi Juni alisaini Mkataba mpya wa Miaka miwili uliomsimika kama Meneja wa kudumu.
Chelsea, ikitoa taarifa ya kufukuzwa Di Matteo, pia imesema watatangaza hivi karibuni nani atashika wadhifa wa Meneja.
++++++++++++++++++++++++++++++
HIMAYA ya ROMAN ABRAMOVICH=MAMENEJA:
-Claudio Ranieri: Septemba 2000-Mei 2004
-Jose Mourinho: Juni 2004-Septemba 2007
-Avram Grant: Septemba 2007-Mei 2008
-Luiz Felipe Scolari: Julai 2008-Februari 2009
-Guus Hiddink: Februari 2009-Mei 2009
-Carlo Ancelotti: Juni 2009-Mei 2011
-Andre Villas-Boas: Juni 2011-Machi 2012
-Roberto di Matteo: Machi 2012-Novemba 2012
++++++++++++++++++++++++++++++
Inaaminika Mmiliki wa Chelsea, Tajiri Roman Abramovich, ameshafanya mazungumzo na Meneja wa zamani wa Liverpool Rafael Benítez ili ashike wadhifa wa Meneja.
Chelsea walianza vyema Msimu huu kwa kushinda Mechi 7 kati ya 8 za kwanza kwenye Ligi na kutwaa uongozi lakini tangu wachapwe 3-2 na Manchester United Uwanjani kwao Stamford Bridge wamezidi kudidimia na wameshinda Mechi mbili tu kati ya 8 za mwisho.
Kwa sasa wapo nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 4 nyuma ya vinara Manchester City ambao Jumapili ijayo watapambana nao Uwanjani Stamford Bridge kwenye Mechi ya Ligi.
Ikiwa Chelsea watashindwa kuvuka hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, kitu ambacho ni kigumu hasa kwa vile kwenye Kundi lao Shakhtar Donetsk washafuzu na Juventus wanahitaji sare watakapocheza na Shakhtar katika Mechi ya mwisho ili wafuzu, itawafanya Chelsea waweke historia ya kuwa Mabingwa wa kwanza watetezi kushindwa kuvuka hatua ya Makundi.
Hivi sasa, Abramovich anasaka Meneja wake wa 9 tangu yeye mwenyewe atue Stamford Bridge Mwaka 2003.
 

 

 

UEFA CHAMPIONZ LIGI: NI KIMBEMBE MAN CITY KUFUZU!!

AGUERO_n_TEVEZ>>KIMAHESABU, INAWEZEKANA LAKINI……..!!!
>>MANCINI AKIRI RONALDO HAKABIKI LABDA AITE POLISI!!
Wana Pointi 2 tu kwa Mechi 4 za Kundi D, ‘Kundi la Kifo’ na uwezo wao Manchester City kufuzu ni finyu, na pengine ni ‘’Ndoto za Alinacha’, lakini uwezekano upo ikiwa tu watashinda Mechi zao mbili zilizobaki, nyumbani Etihad dhidi ya Real Madrid na ugenini na Borussia Dortmund, na vile vile wakiomba sana Mungu matokeo mengine yawabebe, hali ambayo imemfanya Meneja wao, Roberto Mancini, aibuke na imani kuwa ikiwa watapita Kundi hili kimiujiza basi Ubingwa wa Ulaya ni wao tu.
YAFUATAYO NI MAHESABU MAKALI JINSI MAN CITY ANAVYOWEZA KUFUZU:
-KWANZA ni LAZIMA MAN CITY ASHINDE MECHI ZAKE MBILI.
-Ajax lazima waifunge Borussia Dortmund huko Amsterdam kwani sare inaweza kuwamaliza Man City.
-Ikiwa Ajax na Dortmund watatoka sare, Man City watahitaji Real Madrid na Ajax pia zitoke sare huko Santiago Bernabeu. Lakini hata hiyo sare itawafanya Man City wawe wameifunga Real kwa zaidi ya Goli 2 au kwa zaidi ya Goli 1 ikiwa Mabao ni 4 kwenda juu.
-Ikiwa Dortmund wataifunga Ajax, Man City watafuzu ikiwa Ajax wataifunga Real lakini Ajax wakifungwa na Real, City wako nje. Lakini Ajax na Real zikitoka sare itawafanya Man City wawe wameifunga Real kwa zaidi ya Goli 2 au kwa zaidi ya Goli 1 ikiwa Mabao ni 4 kwenda juu.
-MATOKEO MEMA kabisa kwa Man City ni ushindi wa Ajax kwa Borussia Dortmund na kule Santiago Bernabeu Mechi ya Real na Ajax imalizike kwa mmoja kufungwa. Lakini Mechi hiyo ikiwa sare, Timu zote 4 zitamaliza zikiwa sawa kwa Pointi 8 kila mmoja na Mshindi ataamuliwa kwa Tofauti ya Mabao ya Kufunga na Kufungwa.
FAHAMU: MAHESABU HAYA YOTE YANAANZA TU IKIWA MAN CITY ATASHINDA MECHI ZAKE MBILI ZILIZOBAKI.
+++++++++++++++++++
MATOKEO:
06/11 Real Madrid 2 Borussia Dortmund 2
06/11 Manchester City 2 Ajax 2
24/10 Borussia Dortmund 2 Real Madrid 1
24/10 Ajax 3 Manchester City 1
03/10 Manchester City 1 Borussia Dortmund 1
03/10 Ajax 1 Real Madrid 4
18/09 Real Madrid 3 Manchester City 2
18/09 Borussia Dortmund 1 Ajax 0
RATIBA:
21/11 19:45 Ajax – Borussia Dortmund
21/11 19:45 Manchester City – Real Madrid
04/12 19:45 Real Madrid – Ajax
04/12 19:45 Borussia Dortmund – Manchester City
MSIMAMO:

P W D L F A GD PTS
Borussia Dortmund 4 2 2 0 6 4 2 8
Real Madrid 4 2 1 1 10 7 3 7
Ajax 4 1 1 2 6 8 -2 4
Manchester City 4 0 2 2 6 9 -3 2
KANUNI ZILIZOPO:
Ikiwa Timu zimefungana kwa Pointi Mshindi ataamuliwa kama ifuatavywo kwa kufuata kipengele kimoja hadi kingine hadi Mshindi apatikane:
1) Matokeo ya Mechi kati ya Timu zilizofungana na ikiwa bado wamefungana, Mshindi atapatikana kwa kuzingatia Tofauti ya Magoli ya Kufunga na Kufungwa na ikiwa ni sawa basi Magoli ya ugenini yatahesabiwa mara 2.
2) Tofauti ya Magoli ya Kufunga na Kufungwa katika Mechi zote za Kundi.
3) Magoli ya Kufunga katika Mechi zote za Kundi.
4) Yule ambae yuko juu kwenye Listi ya Ubora ya UEFA kwa Miaka mitano iliyopita.
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF

 

 

EUROPA LEAGUE ACTION.

Michuano ya Ligi ya Ulaya maarufu kama Europa League inatarajiwa kutimua vumbi tena leo huku kila timu ikijaribu kuhakikisha inatinga katika hatua ya timu 32 bora za michuano hiyo. Timu za Anzhi mkhachkala ya Urusi, Udinese ya Italia, Liverpool ya Uingereza na Young Boys ya Switzerland zote zitajitupa uwanjani kusaka ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika michuano hiyo. Katika michezo mingine ya leo mabingwa watetezi wa michuano hiyo Atletico Madrid ya Hispania itaikaribisha Hapoel Tel Aviv ya Israel, Rubin Kazan ya Urusi nao watakuwa wenyeji wa Inter Milan ya Italia wakati Basel ya Swtzerland itaikaribisha Sporting Lisbon ya Ureno. Katika viwanja vingine Tottenham Hotspurs watakuwa na kibarua kigumu cha kusaka ushindi ugenini mbele ya Lazio ya Italia wakati waingereza wenzao Newcastle United wenyewe watakuwa nyumbani kuikabili Maritimor ya Ureno.

 

 

REKODI BINAFSI HAINA UMUHIMU KWANGU - MESSI.

Mshambuliaji wa Barcelona, LIONEL MESSI amesisitiza kuwa mawazo yake yapo katika kuisaidia timu yake kuliko kufikia rekodi ya kufunga mabao 85 katika kipindi cha mwaka mmoja aliyoweka GERD MULLER wa Ujerumani. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina aliifungia Barcelona mabao mawili na kuisadia timu yake hiyo kuifunga Spartak Moscow mabao 3-0 na kumfanya kufikisha mabao 80 kwa mwaka huu lakini Messi amesema mataji kwa timu yake ndio muhimu zaidi kuliko rekodi binafsi. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo kuhusiana na suala ya yeye kuikaribia rekodi ya MULLER, MESSI amesema kuwa kitu muhimu kwake ni timu yake kupata matokeo mazuri ndio maana amekuwa akifanya juhudi pamoja na wachezaji wenzake kuhakikisha hilo linawezekana. Naye kocha wa Barcelona TITO VILANOVA aliungana na MESSI akidai kuwa nyota huyo hachezi ili aweze kuvunja rekodi bali kuisaidia timu ili iweze kufanya vizuri.

 

 

BOLT KUHAMIA KATIKA KRIKETI AU SOKA BAADA YA 2016.

Mwanariadha nyota wa mbio fupi USAIN BOLT anatarajiwa kutoshiriki mashindano ya riadha ambayo ni ya mwisho kwa mwaka huu ya Twenty20 League lakini ataweza kuhamia katika mchezo wa kriketi au soka baada ya michuano ya Olimpiki 2016. Wakala wa mwanariadha huyo RICKY SIMMS amesema kuwa kwasasa nyota huyo ni mwanariadha alielekeza nguvu zake katika maandalizi ya mashindano ya Dunia ya riadha yatakayofanyika jijini Moscow 2013. SIMMS alikiri kuwa nyota huyo ana ndoto za kucheza kriketi au soka wakati ambapo atastaafu mchezo wa riadha lakini itakuwa baada ya olimpiki ya 2016 itakayofanyika jijini Reo de Janeiro, Brazil. BOLT ni mwanariadha anayepewa heshima kubwa kwasasa baada ya kufanikiwa kutetea mataji yake yam bio za mita 100, 200 na mita 400 za kupokezana vijiti katika michuano ya olimpiki iliyofanyika iliyopita.

 

 

MESSI AENDELEA KUVUNJA REKODI MBALIMBALI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi ameendeleza rekodi yake ya kufunga mabao baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao timu yake ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Spartak Moscow. Mabao hayo ya nyota huyo aliyofunga jana yamemwezesha kufikisha mabao 56 katika michuano hiyo ya Ulaya na kumuweka sawa katika nafasi ya pili ya wafungaji bora wa bara hilo akiwa sambamba na Ruud van Nisterlrooy wakizidiwa na Raul ambaye yeye amefunga mabao 71. Messi pia amefikia rekodi ya Raul ya kufunga bao katika nchi 19 tofauti katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na kumpita nyota huyo huyo wa zamani kwa kufunga mabao zaidi ya mawili katika mechi 14 za michuano hiyo. Nyota huyo amebakisha mabao matano pekee kufikia rekodi ya Gerd Muelller aliyefunga mabao 85 ndani ya mwaka mmoja katika mashindano yote rekodi ambayo aliiweka mwaka 1972. Messi amekuwa akiongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka minne iliyopita huku msimu uliopita akifikisha mabao 14 ambayo ndio mengi zaidi kwa msimu.

 

 

HENRY KUREJEA TENA ARSENAL JANUARI.

MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry anaweza kurejea tena katika klabu hiyo yenye maskani yake kaskazini mwa jiji la London kwa mkopo kutokea katika klabu ya New York Red Bull ya Marekani Januari mwaka huu. Meneja wa Arsenal, Arsenal Wenger alibainisha hayo katika wavuti wa klabu hiyo kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kumsajili nyota huyo katika kipindi cha dirisha dogo la usajili kwasababu amekuwa akifanya nao mazoezi nab ado anaonekana ana uwezo ya kukabiliana na mikiki ya ligi. Henry ambaye ana rekodi ya kufunga mabao 228 alirejea katika klabu hiyo Januari mwaka jana na kufunga bao katika mchezo dhidi ya Leeds United katika Kombe la FA na kufunga bao la ushindi katika dakika za mwisho katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza dhidi ya Sunderland. Wenger ameonyesha nia ya kumrejesha tena shujaa wake huyo na anaamini kuwa anaweza kuwa msaada mkubwa haswa ikizingatiwa kuwa anaweza kuwapoteza washambuliaji wake wawili Gervinho kutoka Ivory Coast na Marouane Chamakh ambao kuna uwezekano mkubwa wa kuitwa kuzitumikia timu zao za taifa katika Kombe la Mataifa ya Afrika Januari mwakani. 

 

MABINGWA ULAYA Chelsea wanyukwa 3-0 na Juve, TAJI hatarini !!

JUVENTUS-Claudio_Marchisio>>BARCA, SHAKHTAR, BAYERN, VALENCIA ZAFUZU!
Mabingwa watetezi wa Ulaya, Chelsea, wapo hatarini kulibwaga chini Taji lao baada ya kunyukwa Bao 3-0 na Juventus huko Mjini Turin kwenye Mechi ya Kundi E la UEFA CHAMPIONZ LIGI na sasa hatima yao haipo tena mikononi mwao maana katika Mechi za mwisho za Kundi lao ikiwa Mechi kati ya Shakhtar Donetsk, ambao tayari wamefuzu, na Juventus itakuwa sare tu basi wao hata wawafunge Nordsjaelland Bao Milioni moja wako nje.
Katika Mechi nyingine zilizochezwa Jumanne Barcelona, Shakhtar Donetsk, Bayern Munich na Valencia zimefanikiwa kufuzu na kuungana na Manchester United, Malaga na FC Porto ambao walikuwa tayari wamefuzu kabla MECHI DEI 5 kuanza.
Mitanange mingine ya Makundi A hadi D inaendelea Jumatano Usiku.
++++++++++++++++++++++++++++++++
[MISIMAMO=Kila Timu imecheza Mechi 5]
KUNDI E
FC Nordsjælland 2 FC Shakhtar Donetsk 5
Juventus 3 Chelsea FC 0
MSIMAMO:
1 Shakhtar Donetsk Pointi 10 [IMEFUZU]
2 Juventus 9
3 Chelsea 7
4 Nordsjaelland 1 [NJE]
KUNDI F
BATE Borisov 0 Lille 2
Valencia CF 1 FC Bayern München 1
MSIMAMO:
1 Bayern Munich Pointi 10 [IMEFUZU]
2 Valencia 10 [IMEFUZU]
3 BATE Borisov 6 [NJE]
4 Lille 3 [NJE]
KUNDI G
Spartak Moscow 0 Barcelona 3
SL Benfica 2 Celtic FC 1
MSIMAMO:
1 Barcelona   Pointi 12 [IMEFUZU]
2 Celtic 7
3 Benfica 7
4 Spartak Moscow 3 [NJE]
KUNDI H
Galatasaray 1 Manchester United 0
CFR 1907 Cluj 3 SC Braga 1
MSIMAMO:
1 Man United Pointi 12 [IMEFUZU]
2 Galatasaray 7
3 CFR Cluj-Napoca 7
4 Braga 3 [NJE]
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Mechi zote kuanza SAA 4 DAK 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]
Jumatano Novemba 21
FC Porto v GNK Dinamo
FC Dynamo Kyiv v Paris SaintvGermain FC
Arsenal FC v Montpellier Hérault SC
FC Schalke 04 v Olympiacos FC
FC Zenit St. Petersburg v Málaga CF [SAA 2 Usiku]
RSC Anderlecht v AC Milan
AFC Ajax v Borussia Dortmund
Manchester City FC v Real Madrid CF
++++++++++++++++++++++++++++++++
 

Raymond Domenech aiponda Ufaransa ya 2010, awaita ‘MAZUZU!

>>FRANCK RIBÉRY, NICOLAS ANELKA & THIERRY HENRY WAMO!!
>>ADAI: ‘’Anelka alinitukana Haftaimu….aliua Timu!’
>>AMSIFIA EVRA kwa kujaribu kuunganisha Timu!
Aliekuwa Kocha wa France iliyocheza Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwaka 2010 na kutokea mgomo wa Wachezaji, Raymond Domenech, amechapisha Kitabu na kudai Wachezaji walimkera kiasi cha kulipuka na kuwaita ‘Kundi la Mazuzu!’
Mwaka huo 2010, huko Afrika Kusini, France ilishangaza Dunia baada ya Wachezaji kufanya mgomo mara baada ya mwenzao, Nicolas Anelka, kufungashwa virago kwa kumkashifu Kocha Domenech wakati wa Haftaimu ya Mechi ya Makundi dhidi ya Mexico.
+++++++++++++++++++++++++++++
FAINALI KOMBE LA DUNIA [Afrika Kusini]:
KUNDI A:
11 Juni 2010: Uruguay 0 France 0
17 Juni 2010: France 0 Mexico 2
22 Juni 2010: France 1 South Africa 2
**Uruguay na Mexico ndio walifuzu, France walimaliza mkiani.
+++++++++++++++++++++++++++++
DOMENECH_N_ANELKAMara baada ya Fainali hizo za Kombe la Dunia, Domenech aliondolewa kama Kocha wa France cheo ambacho alidumu nacho kwa Miaka 6 na pia kutimuliwa toka kwenye Shirikisho la Soka la France, FFF.
Katika Kitabu chake, kiitwacho ‘Tout Seul‘. Kiingereza ni All Alone, ikimaanisha Ni Peke Yako, Domenech amewashambulia vibaya Wachezaji Franck Ribéry, Anelka na Thierry Henry.
Alisema: “Nilishindwa kustahamili kila Mtu akizungumza kuhusu kila kitu. Ilinifanya nijisikie mgonjwa, nataka kulia, kuondoka!”
Siku ambayo Wachezaji wa France waligoma huko Afrika Kusini, wakiwa Mji wa Knysna, Wachezaji, wakielekea mazoezini, walipofika Uwanjani walipokewa kwa shangwe na Mashabiki na wao kushuka kwenye Basi lao na kwenda kupeana nao mikono, kusaini Vitabu vyao na wakarudi ndani ya Basi, wakigomea mazoezi.
Domenech ameeleza: “Timu ya Ufaransa imejisulubu yenyewe, mbele ya kadamnasi, Televisheni.”
Ingawa wakati huo France ilibakisha Mechi moja kwenye Kundi lao, lakini Domenech alishakata tamaa.FRENCH_TEAM
Baada ya kuchapwa 2-0 na Mexico, Domenech aliandika Kitabuni kuwa Anelka alimtukana wakati wa Haftaimu na hakuna Mchezaji yeyote aliemuunga mkono yeye isipokuwa Nahodha wa Kikosi hicho, Patrice Evra, aliejaribu kupoza mambo.
Domenech anaeleza: “Alinitukana haftaimu…. Wakati mie ndie nlikuwa upande wake Siku zote! Baada ya Mechi ile, tumefungwa yeye na Gallas wakawa wanacheka. Hawana hisia hao! Wanafurahia kufungwa?”
Domenech amemwelezea Anelka kama msununu asiejaribu kusaidia wenzake.
Ingawa wakati huo Viongozi wa France walikanusha kuwepo na mgogoro ndani ya Timu kama ilivyokuwa ikidaiwa na Vyombo vya Habari vya France, Domenech amethibitisha hilo kwa kukiri kulikuwepo na bifu kubwa kati ya Ribery na Gourcuff, ambae alikuwa akisifiwa kama ndie Zinedine Zidane mpya.
Domenech ameandika: “Ribery hampendi Gourcuff. Katika Mechi kabla kucheza na Uruguay nlikuwa nikimwambia Gourcuff kuwa anao ufunguo wa Mechi na nilipomtazama Ribery niliona sura ya chuki kubwa.”
Aliongeza: “Ribery ni sawa na Anelka na Henry, kila kitu kimo tumboni mwao. Vitu vikienda kombo wao wa kwanza kuulaza. Kuna Mchezaji mkongwe aliwahi kunitonya kuhusu Ribery Mwaka 2008 lakini nilipuuza na huo ndio ujinga wangu!”
Kitabuni Domenech alimsifia Evra kwa kujaribu kuunganisha Kikosi lakini alisikitishwa na kushindwa kwake kuzima mgomo wa Wachezaji.
Ulipotokea mgomo, Domenech ameeleza: “Nilikwenda kulala baada ya Bia kadhaa. Hataa, ni Lita kadhaa!”
KUMBUKUMBU:
-Mara baada ya Fainali za Kombe la Dunia za 2010, FFF ilimfungia Nicolas Anelka Mechi 18 na Anelka akatangaza kustaafu kuichezea Timu ya Taifa.
-Patrice Evra alifungiwa Mechi 5
-Franck Ribery alifungiwa Mechi 3 
-Jeremy Toulalan Mechi 1.