Friday, January 18, 2013

ARMSTRONG AKIRI MBELE YA OPRAH WINFREY KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU.


HATIMAYE mwendesha baiskeli Lance Armstrong amekiri hadharani kutumia dawa za kuongeza nguvu na kumuwezesha kupata mataji yote saba ya mashindano ya baiskeli ya Toure de France. Armstrong mwenye umri wa miaka 41 alikiri kufanya hayo katika mahojiano na mtangazaji maarufu nchini Marekani Oprah Winfrey mbele ya watazamaji zaidi ya milioni 10 waliokuwa wakitazama kipindi hicho. Nyota huyo alikiri kuwa alikuwa akitumia dawa hizo mara nyingi lakini amejitokeza hadharani kuomba radhi kwa mashabiki wake waliokuwa wakimuamini. Armstrong ambaye ni raia wa Marekani amesema wakati akitumia dawa hizo alijua madhara yake baadae lakini aliamua kuendelea kufanya hivyo pamoja na hatari zilizopo. Mahojiano ya Armstrong na Winfrey mwenye umri wa miaka 58 yalirushwa katika kipindi chake OWN network kinachorushwa hewani na luninga ya Prime Time ya nchini Marekani wakati watu sehemu nyingine duniani kote waliangalia kupitia tovuti yake.

No comments:

Post a Comment